Ben na bully

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Na Abu Halima Sa Changwa

BEN: Karibu Mshikaji, habari za huko?

BULLY: Poa, mshikaji. Vipi mambo? Unaitwaje vile?

BEN: Naitwa Ben Willy MacKapper. Jina la utani Netanyahu.

BULLY: Aisee! Mambo yanaendaje, Bob Mackapper.

BEN: Kama unavyojua tumo kwenye mpambano wa vyama vingi.

BULLY: Ah, mimi naondoka ulingoni, nawaachia wengine sasa. Lakini naona huna wasi wasi.

BEN: Ah, wapi mshirika. Kuna jamaa hao sijui wanajiita ngangali ngangali. Wananitia mcheche kishenzi. Tena afadhali umekuja. Mzee Nelly amekuita uje umsaidie kuwatuliza hawa jamaa, lakini kwetu kuna msemo unasema ukimuona jumbe hapo hapo ndipo pa kumsalimia.

BULLY: Sasa mimi nitakusaidiaje wakati ndio naondoka? Hata kuja huku nimekuja tu kutalii, maana nilikuwa nasikia tu huku kuna mlima mrefu kuliko yote Afrika, halafu kuna wanyama kibao. Pamoja na kuwatishia hawa wanaojidai wanajua kuuana, pia nilitaka na mimi niucheki tu ule mlima.

BEN: Fanya lolote uwezalo, mshikaji. Unajua mimi nakumaindi sana. Si unajua Hayati Mzee Jully alivyokuwa hawamaind mayakii, anawaita mabepari. Sasa hivi hayupo ndio maana sioni noma kupanga majamboz na wewe, sio! Wewe mwenzangu uko freshi, unaweza kunisaidia.

BULLY: Ah, mimi niko freshi. Si unacheki hata madogi yangu yaliyocheki gari yako yalivyo?

BEN: Oh, mshkaji una mijibwa balaa! Halafu unajua umenitoa nishai kwa raia wangu, sasa yale ndo yalikuwa yanacheki nini.

BULLY: Ah, unajua tena mshikaji, ulinzi ulinzi tu, na nini. Halafu si unajua mambo zangu, sasa maadui zangu wanaweza wakafanyiza kinoma noma, kwa hiyo yale madogi yakianza kuhakikisha usalama hayaelewi. Yanaingia tu kila mahali. Halafu mshikaji huku kwenu gari ya Rais huwezi kuijua upesi, iko sawa na ya meneja wa kiwanda kule kwetu. Kwa hiyo wale manjagu wangu hawakujua kama ile ndio gari ya Rais wa nchi.

BEN: Sasa unapakaza mshikaji. Hebu tuongee maswala muhimu. Kabla kikao hakijaanza, utanisaidiaje?

BULLY: Mimi ninachoweza kukusaidia ni ubabe tu. Zangu si unazijua? Mtu akijitia mbabe naingia tu nabonda halafu naondoka. Akiwa sugu kama Saddam nawaleta washirika wangu kibao tunasaidiana kumbonda. Sasa wewe hao sijui ndio nani, hao unaowaogopa, wanahitaji ubabe au pesa tu.

BEN: Pesa sio tatizo. Hao wao hawaangalii pesa. Unaweza kuwamwagia pesa na wakakuliza vile vile. Hao ubabe tu.

BULLY: Sasa nipe ruhusa ya kuingiza vifaa vyangu.

BEN: Vifaa gani mshikaji, madogi?

BULLY: Ah, anazungumzia madogi! Nipe ruhusa ya kuingiza zana zangu za angani. Mzee Jully ndio alikuwa mnoko sana, hakupenda mambo yetu, lakini wewe ukinipa ruhusa ya kuingia humu na ndege zangu hao jamaa zako wenyewe watafyata mikia. Sasa unasemaje?

BEN:Yap, yap. Gonga basi! Hamna noma. Hiyo tu. Wala sina haja ya kuitisha kikao chochote. Mimi ndo Netanyahu wa huku. Leo hiihii tuandikishane. Tuweke mkataba wa anga huru, ili noma likiibuka uingie kiulaiini kunisevu.

BULLY: Kwa nini tusipange siku nyingine.

BEN: Hapana, linalowezekana leo lisingoje kesho.

BULLY: Basi freshi, mimi nitasaini mkataba, halafu wakijidai wajuaji we unanitonya tu, naingia. Halafu uzuri wenyewe watu wako ni poa kishenzi, nasikia hawajui vita wala vagi, kwa hiyo mimi nitakusevu. Hata hivyo, mkataba huu utasaidia pia kudhibiti na wengine unaopakana nao, kama hapo Sudan, wanapojidai wana siasa kali. Si unakumbuka niliwaweka kwenye listi yangu ya magaidi? Wakijidai tu natua kwako halafu nawabonda kishenzi kutokea kwako. Au vipi!

BEN: Sasa tena, si unacheki, bonge la advanteji. Twende, naona Mzee Nelly anakuja, tuminye kwanza.

BULLY: Sawa, mshikaji.

MZEE NELLY: Vipi vijana, naona mmekutana mnateta. Mnapanga jinsi ya kumaliza huu mgogoro wa wenzetu?

BEN na BULLY: Ndio mzee!
 
Big up kamanda,

Hiyo imetulia sana kwa WATU WENYE KUTAFAKARI. wengi wetu watachukulia jokes tu. Natamani iwekwe ktk ulingo wa siasa!!!

safari ya ukombozi bado ndefu
 
Back
Top Bottom