*Beijing Olympics 2008*

Hata nguo zao ziliniacha mnyonge! Angalau wenzetu wa magharibi wanaonyesha wametokea wapi. Hapa ni same old, same old. Tunategemea kuvuna bila kupalilia.
 
Kwa habari zaidi tembelea bandiko kama hili kwenye ukumbi wa michezo humuhumu jamii forums


kibunango nimekusoma ..ila naomba tupige siasa kidogo hapa hadi mashindano yaishe..si ajabu ukasikia ..TANZANIA KIDEDEA YAZOA MEDALI ZOTE MARATHON...hapo ndipo utamsikia rais wetu ambaye kwa sasa HAJUI ATOKE VIIPI[SI MNAJUA ALITAKA KUTOKA NA TAIFA STARS IKAMUANGUSHA]....Ataibuka NA kuagiza siku tatu za mapumziko na kuitisha kikao cha dharura cha bunge kuwapongeza vijana.............

unajuwa tabu ya serikali yetu ...wanajua kuvuna tu ....hawajui kupanda.....wakati hawa vijana wa olimpiki waanakosa hata nauli wao wako kimya.wakati yule bondia mmoja anashindwa hata kuwekwa kambini ...na hadi kufikia kubebeshwa unga wao wapoo wapo tu.......NA STILL WANATEGEMEA MIUJIZA YA MEDALI ZIDONDOKE KAMA MANA JANGWANI..............thats why i want this bandiko to be here for a while....

wenzetu kenya waliagwa na rais wao..na kuahidi kila medali ya dhahabu atatoa milioni 8 za kenya....na kushuka chini as per medali....utalii wa kenya au kujitangaza kunachangiwa sana na michezo........sisi tunaota miujiza kutegemea kujitangaza kama biskuti CNN........hatujuwi tukishinda olimpiki we will make even more headlines..........
 
........naona RAIS WA MAREKANI bush na mkewe laura wameingia uwanjani kuwapa tafu ..kwa kushabikia timu ya OLIMPIKI YA BASKETBALL YA MAREKANI ..inapambana na CHINA ....wachina ni wakali sana na warefu..marekani wanaongoza ...japo ushindani ni mkali................kobe bryant anapiga mabao tu....
 
Naam ushindani ni mkali US wanaongoza kwa 12 (49-37) na ni half time sasa, lakini China wanashoot 3 points kwa accuracy ya hali ya juu na si ajabu wakapunguza gap hiyo haraka baada ya mapumziko kwisha.
 
naam Ushindani Ni Mkali Us Wanaongoza Kwa 12 (49-37) Na Ni Half Time Sasa, Lakini China Wanashoot 3 Points Kwa Accuracy Ya Hali Ya Juu Na Si Ajabu Wakapunguza Gap Hiyo Haraka Baada Ya Mapumziko Kwisha.

..yeah Three Points Na Rebound Za Wachina Zinanifurahisha..inaonesha Namna Wachina Walivyo Determined Kujifunza Wanachotaka...miaka Ya Nyuma Sidhani Kama China Walikuwa Wanajua Basket Namna Hii..lakini Sasa Kwenye Nba Wapo Wengi Tu...na Hata China Wana Ligi...

Mwisho Wa Siku Najua Marekani Watashinda Lakini Kwa Taabu....
 
Serikali ya China ina kitu kinaitwa Project 119, ambayo ililenga kuhakikisha kuwa China inaweza kunyakua medali katika michezo 119 ambayo ilikuwa haina uwezo kutamba.

Nashangaa hatuna hata walenga shabaha, mabondia, wapanda baiskeli, mpira wa miguu, mieleka, kubeba vyuma (uzito), volleyball hata handball?

Narudia, tukibadilisha mawazo yetu finyu kupuuza michezo kama si vianzio vya kazi na mapato, tutaendelea kutegemea kufanya kazi ofisini, viwandani na mashambani.

Wenzetu kila kinachomtoa jasho Mwanadamu ni kazi, mpaka picha za ngono, sisi tunaona michezo, sanaa na utamaduni ni kupoteza muda!
 
Nukuu ya Project 119

China's Gold Strategy
Shortly after China was awarded these Games seven years ago, its sports leaders devised Project 119, an initiative to help boost their country to the top of the Beijing medal standings. One-one-nine refers to the number of golds given out at the 2000 Games in the medal-rich sports of track and field, swimming, rowing, sailing and canoe/kayak. In Sydney, China won only one medal, total, in those sports.
At this year's Games the home team could win more than a dozen medals in the Project 119 events—potentially enough to make a difference in a tight battle with the U.S. for the No. 1 spot. Given their traditional strength in table tennis, diving, badminton and gymnastics (in which Yang Wei, top right, is favored to win the men's all-around); their domination of shooting (in which they could win 10 of the 15 events); their depth in women's sports (with stars like weightlifter Liu Haixia, right, world champion in the 139-pound class); and the usual surge in victories by the host country, the Chinese should easily top their 2004 totals of 63 medals (third behind the U.S.'s 102 and Russia's 92) and 32 golds (second to the U.S.'s 36). An analysis in June by the accounting firm PricewaterhouseCoopers projected that China would edge the U.S. in total medals 88--87, and a British university study predicted a stunning 46 golds for the hosts. Bookmakers have made the Chinese the favorites to win both the overall and gold medal counts. What will actually happen in Beijing?
 
...uzuri wenyewe kila Raisi anatimiza majukumu yake wakati huu wa michezo ya Olimpiki, ...na pengine Raisi wetu kajichokea na 'u-bichwa wa mwendawazimu' wa wanamichezo wetu.

View attachment 1955
President George W. Bush is in Beijing, China for the Olympics. As the leader of the United States, he has lots of important things on his mind. One seeming to be the ladies volleyball team! George Bush hangs out with Misty-May Treanor and Kerri Walsh!

View attachment 1957
Rais Jakaya Kikwete akiangalia ng'ombe aliyezalishwa kwa chupa wakati alipotembelea baadhi ya mabanda katika viwanja vya Nzuguni Dodoma,jana mchana wakati wa kilele cha Sherehe za wakulima Nanenane

View attachment 1956
Russian Prime Minister Vladimir Putin poses with members of the Russian delegation during his visit to the Olympic Village in Beijing August 9 2008.
 
.......

mnakumbuka enzi za kina juma ikangaa,,...
Huyo Ikangaa ndie aliyefilisi mawazo ya watz wengi katika fani ya kufukuza upepo. Ikangaa hakuwahi kushinda medali yoyote katika olimpiki, lakini aliweza kuwa moja wa matajili katika histiria ya wanariadha wa tz. Marathon ilichukua sura mpya katika historia ya TZ baada ya Ikangaa kuzawadiwa Benz, kila mwanariadha alitaka kushiriki katika marathon.

Ni Ikangaa aliyeweza kubadili mawazo ya watimua upepo lukuki wa Kitz, Marathon ikaonekana ndio njia mbadala ya kuondokana na ulofa, mbio za mita 10,000, 5,000, 3,000 1,500 na mita 800 zikakosa wakimbiaji, kwani wote walihamia kwenye marathoni ili wawe sana na Ikangaa!

Kuna dada mmoja kwa jina la Taus Said ambae angeweza kuleta medali kwa TZ katika mbio za mita 800 na 1500 lakini nae alikubwa na zimwi la Ikangaa, Mikoa ya Singida, Arusha na Zenj wote hawa walikubwa na zimwi la Ikangaa. Riadha tz ikawa ni marathon tu.

Mwaka 1979 wakati Sebastin Coe akivunja rekodi ya F. Bayi na TZ ikiwa katika vita dhidi ya Uganda, maelfu ya watz walishikwa na huzuni. Ni marehemu Nyerere kidogo aliweza kututoa katika majonzi hayo. Na Bayi mwenyewe aliweza kutufariji mwaka mmoja baadae alipoweza kutwaa medali kule Moscow.

TAAA sijui kwa sasa inajulikana vipi, lakini kwa ufupi wamechangia kwa mapana kuua riadha hapa TZ, Ulofa wa Viongozi TAAA ndio matunda ambayo leo tunayaona. Tz sio tofauti na Kenya, asilimia kubwa ya Wakenya wanaofanya vizuri katika riadha wamehusu Bonde la Ufa, ambalo hata Tz lipo tokea nyanda za juu kusini hadi kaskazini. Kwa nini hatuwezi kuwa sawa na Kenya? tuna tatizo gani?
 
Last edited:
Mwaka 1976 hatukushiriki olimpiki, nina imani F. Bayi angeweza kutuletea medali ya dhahabu ya kwanza hapa TZ
 
Tanzania Highlight in Olympics Games

Well known for its distance runners, Tanzania has surprisingly only ever won two Olympic medals. Both came at the 1980 Moscow Olympic Games in the Soviet Union where Filbert Bayi came second in the men's 3000m steeplechase and Suleiman Nyambui finished a desperately close second to Ethiopia's Miruts Yifter in the men's 5000m event.

Bayi missed out on the chance to compete four years earlier in Montreal when Tanzania joined the African boycott of the 1976 Games. Bayi was the then world record-holder in the 1500m.
At the 1968 Olympic Games in Mexico City, Tanzanian marathon runner Stephen Akhwari badly injured his knee but limped on to finish over an hour behind the rest of the field. When asked by filmmaker Bud Greenspan after the finish why he had continued to run, Akhwari famously replied, "My country did not send me 7000 miles away to start the race. They sent me 7000 miles to finish it."


sasa uzalendo kama huu umeishia wapi yarabi!! au ndio tuliufukia kaburini pamoja na baba wa taifa?
 
Hata nguo zao ziliniacha mnyonge! Angalau wenzetu wa magharibi wanaonyesha wametokea wapi. Hapa ni same old, same old. Tunategemea kuvuna bila kupalilia.

tungekuwa tunategemea kuvuna bila kupalilia ingekuwa afadhali kidogo, manake tungevuna hata mabua machache tukawapa ng'ombe...yaani sisi ni kama mkulima anayelima mshamba wake, hapandi mbegu hata moja...halafu wenzie wakianza kuvuna, na yeye anabeba magunia yake eti anaenda kuvuna
 
...inawezekana Juma Ikangaa ndio wa kulaumiwa, lakini saa nyingine ni 'bora lawama, almuradi mkono uende kinywani'. Juma Ikangaa mwenyewe pamoja na heshima kubwa aloiletea taifa, alilisotea sana kulitoa hilo Benzi lake Bandarini kwa Serikali kudai kodi. Kitendo hicho kilikuwa motisha au kumvunja moyo, yeye na wengine? Tax Exemption kwa wanamicheo wetu ingesaidia kukuza ari ya kufanya vizuri zaidi.

... Mara ngapi ushasikia Vifaa vya michezo (i.e mats za Karate na Judo, majani bandia ya uwanja wa taifa, etc) vimekwama Bandarini miezi na miezi kwa kukosekana pesa ya kuvikomboa? Priority ya Serikali kuhusiana na suala la michezo sasa lipo kwa JK boys tu.

...Miaka ya Nyuma, pale Gymkhana Club vilizaliwa Vipaji vya Basketball, Railway Gerezani vipaji vya Netball vilionekana, Diamond Jubilee vipaji vya Hokey vilizaliwa, leo hii Gymkhana palipitishwa ujenzi wa Sheraton Hotel, Railway Gerezani ndio imekuwa Paradise sijui nini, Diamond Jubilee Jeshi wamezungushia ukuta ~MARUFUKU KUPITA HAPA! Hata Dojo ya sensei Bomani pale Zanaki kama ipo basi ni majaaliwa.

...nilitarajia wanariadha wetu maarufu wa enzi hizo Tanzania, mf; Bayi, Ikangaa, Nyambui, Nzael Kyomo, Mwinga Mwanjala, Mosi Alli etc angalau mmoja wao angekuwa mbunifu kufungua chuo (hata kwa udhamini wa NIKE, ADIDAS, PUMA) ili kukuza vipaji vya wanariadha wetu, lakini naona wengi wao wamejikita kufungua academy tu za elimu ya kawaida.

...Haya, tusubiri muujuza tu mwingine, labda toka kwa mfukuza ng'ombe mmoja, maana angalau hao waliomwona/msikia Ikangaa akikimbia na kutamani wawe marathon runners. Kufa kwa UMISETA na UMISHUMTA, etc imekifanya kizazi kipya wao na Bongo flava tu.
 
Tanzanians athletes to start Games campaign on Thursday

2008-08-11 08:37:27
By Steve William, Beijing

Tanzanian athletes will start their Olympic Games campaign on Thursday with Magdalena Alex Moshi will be competing in swimming.

Tanzania Chief of the Mission Charles Nyange said yesterday that Khalid Shaka would compete in the mens swimming competition on Friday.

...ehhh!.... Fingers Crossed, ....tusijebatizwa kina "the eagle" na the "fish"!....
 
...inawezekana Juma Ikangaa ndio wa kulaumiwa, lakini saa nyingine ni 'bora lawama, almuradi mkono uende kinywani'. Juma Ikangaa mwenyewe pamoja na heshima kubwa aloiletea taifa, alilisotea sana kulitoa hilo Benzi lake Bandarini kwa Serikali kudai kodi. Kitendo hicho kilikuwa motisha au kumvunja moyo, yeye na wengine? Tax Exemption kwa wanamicheo wetu ingesaidia kukuza ari ya kufanya vizuri zaidi.

... Mara ngapi ushasikia Vifaa vya michezo (i.e mats za Karate na Judo, majani bandia ya uwanja wa taifa, etc) vimekwama Bandarini miezi na miezi kwa kukosekana pesa ya kuvikomboa? Priority ya Serikali kuhusiana na suala la michezo sasa lipo kwa JK boys tu.

...Miaka ya Nyuma, pale Gymkhana Club vilizaliwa Vipaji vya Basketball, Railway Gerezani vipaji vya Netball vilionekana, Diamond Jubilee vipaji vya Hokey vilizaliwa, leo hii Gymkhana palipitishwa ujenzi wa Sheraton Hotel, Railway Gerezani ndio imekuwa Paradise sijui nini, Diamond Jubilee Jeshi wamezungushia ukuta ~MARUFUKU KUPITA HAPA! Hata Dojo ya sensei Bomani pale Zanaki kama ipo basi ni majaaliwa.

...nilitarajia wanariadha wetu maarufu wa enzi hizo Tanzania, mf; Bayi, Ikangaa, Nyambui, Nzael Kyomo, Mwinga Mwanjala, Mosi Alli etc angalau mmoja wao angekuwa mbunifu kufungua chuo (hata kwa udhamini wa NIKE, ADIDAS, PUMA) ili kukuza vipaji vya wanariadha wetu, lakini naona wengi wao wamejikita kufungua academy tu za elimu ya kawaida.

...Haya, tusubiri muujuza tu mwingine, labda toka kwa mfukuza ng'ombe mmoja, maana angalau hao waliomwona/msikia Ikangaa akikimbia na kutamani wawe marathon runners. Kufa kwa UMISETA na UMISHUMTA, etc imekifanya kizazi kipya wao na Bongo flava tu.

hawa kina ikangaa ,bayi,naali,mwangata..ets..waligunduliwa UMISETA ..na wakati huo JESHI lilikuwa na utaratibu wa kuwanyakuwa vijana wanaotamba umiseta na kuwalea ..ndio hawa !!!..mnakumbuka miaka ya kati ya 80..tulipata kushiriki HANDBALL..KITU KAMA OLIMPIKI AU ALL AFRICAN GAMES...ENZI HIZO JESHI WALIKUWA WAKICHEZA MICHEZO YOTE.....nakumbuka kipa wa handball maarufu wa upande wa wanawake enzi hizo aliitwa ..RABIA YASSIN......jina kama la kipa wa NATIONAL AL AHLY aliyedunguliwa na MOGELLA ZAMOYONI na mtemi RAMADHANI pale kirumba stadium mwanza....siku hiyo golini alikaa...MOSES MKANDAWILLE..,KULIA SAULO GEORGE ,BEKI KATI ni LILA SHOMARI,RAMANDANI LENY KATI ..WINGA SUNDAY JUMA....DAUD SALUM...MTEMI RAMADHANI,MALOTA SOMA"ball juggler",ZAMOYONI MOGELLA...MALIZIA
 
kenya Wametuma Wanamichezo Zaidi Ya 100 ..na Mkuu Wa Msafara Wao Ni Just Senior Officer Kwenye Wizara Ya Michezo....sisi Tuna Wachezaji 8 Tu..na Msafara Unaongozwa Na Waziri Wa Michezo Capt Mkuchika.........hiyo Si Aibu....au Ushamba Wa Safari Au Kutaka Posho Tu...siku Tukipeleka Wanamichezo 15 Nadhani Tuitathubutu Kumfanya Mkuu Wa Msafara Awe Rais Mtalii
 
Back
Top Bottom