Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Wakati wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi, wenye akili waliitaka Serikali iachane na biashara ya kuingiza mafuta nchini na kuyasafisha. Mwinyi alikuwa rais, Yona Kilaghane DG wa TPDC (ni mkuu wa TPDC hadi sasa! Sikumbuki Waziri wa Nishati alikuwa nani kati ya Rais Kikwete au Alnoor Kassum. Kilichofuata ni kukifunga kiwanda cha TIPER, mamia ya wafanyakazi kukosa ajira na kuibuka Makampuni ya kuagiza mafuta. Kwa kugundua makosa yetu, Serikali mwaka juzi ikaiagiza TPDC ianze kuagiza mafuta tena.