Bei ya Vyakula nchini: A Recipe for Political upheaval..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Ni kweli bei ya vyakula inapanda kwa kasi zaidi na watu wanaanza kufikiria vya kununua na kwa kiasi gani? Kwamba, wapo watu wameanza kubadilisha manunuzi yao ya vyakula kuakisi ongezeko la bei vya vyakula mbalimbali? Je hili litakuwa na matokeo gani katika uchumi hasa kwenye headline inflation? Je kuna namna yoyote kweli ya kuweza kuepusha the inevitable?
 
MM, kinachotokea na ongezeko la kasi ya ukuaji wa bei kutokana na kwamba wananchi wameshaweza kusoma alama za nyakati na wanapanga matumizi na bei (kwa wafganyabiashara) kuendana na makisio ya bei kuendelea kupanda. Matokeo yake ni kuendelea kupanda kwa bei. Njia pekee iliyobaki ya kutatua tatizo hili ni kuongeza uzalishaji wenye tija, kupunguza gharama za usafirishaji, kuomba mvua inyeshe na pia kuboresha mifumo ya uzalishaji katika nchi jirani ili kupunguza biashara ya chakula baina ya nchi na nchi hususani wakati huu ambao uzalishaji wetu ni wa kukidhi mahitaji yetu muhimu tu bila ya kuwa na ziada ya kutosha.

Jibu ni moja: Hali itaendelea kuwa mbaya zaidi kabla ya kurekebika
 
Dagaa ilikuwa ndiyo mboga ya watu wa kipato cha chini, sasa hivi kilo moja ya dagaa inaanzia shilingi 5,000/= na kuendelea
 
sio lazima ununue kilo nzima, waweza kununua kwa mafungu, ukawaunga dagaa wako vizuri na ukafurahi. Usisahau matembele kidogo
 
Ni kweli bei ya vyakula inapanda kwa kasi zaidi na watu wanaanza kufikiria vya kununua na kwa kiasi gani? Kwamba, wapo watu wameanza kubadilisha manunuzi yao ya vyakula kuakisi ongezeko la bei vya vyakula mbalimbali? Je hili litakuwa na matokeo gani katika uchumi hasa kwenye headline inflation? Je kuna namna yoyote kweli ya kuweza kuepusha the inevitable?

Iwapo unaongelea Tz, bei ziko juu siku nyingi na watu wengi wamejarimu coping mechanism kwa kubadili staili ya maisha katika kujaribu kufidia pengo. Sina uhakika watu wanawezaje kumudu hizi bei lakini naona foleni haziishi barabarani kwa maana wenye magari bado wana wana uwezo wa kuyamudu na msongamano sokoni uko palepale!
Nadhani wabongo wote sasa wamekuwa 'wachakachuaji!'
 
MM, kinachotokea na ongezeko la kasi ya ukuaji wa bei kutokana na kwamba wananchi wameshaweza kusoma alama za nyakati na wanapanga matumizi na bei (kwa wafganyabiashara) kuendana na makisio ya bei kuendelea kupanda. Matokeo yake ni kuendelea kupanda kwa bei. Njia pekee iliyobaki ya kutatua tatizo hili ni kuongeza uzalishaji wenye tija, kupunguza gharama za usafirishaji, kuomba mvua inyeshe na pia kuboresha mifumo ya uzalishaji katika nchi jirani ili kupunguza biashara ya chakula baina ya nchi na nchi hususani wakati huu ambao uzalishaji wetu ni wa kukidhi mahitaji yetu muhimu tu bila ya kuwa na ziada ya kutosha.

Jibu ni moja: Hali itaendelea kuwa mbaya zaidi kabla ya kurekebika

Sumu ni KILIMO KWANZA, Pembejeo zimepanda kutokana na kuwapo na RUZUKU kwani MAGUMUSH yote na DILI zimehamia huku kwenye KILIMO. Na huwezi hamini huuo uzalishaji haujaongezeka hata kidogo pamoja na kuwepo RUZUKU kwenye KILIMO.
 
Dagaa ilikuwa ndiyo mboga ya watu wa kipato cha chini, sasa hivi kilo moja ya dagaa inaanzia shilingi 5,000/= na kuendelea

Hiyo bei ya wapi? Mbona Kigoma tunanunua kg 1 kwa 15,000? Au ni dagaa wa mwanza?
 
Back
Top Bottom