Bei ya Umeme kupanda kwa asilimia 50 kuanzia January 2013

taarifa kutoka vyanzo vyangu vya kuaminika bei ya Umeme itaongezeka kwa asilimia 50 kuanzia mwezi wa kwanza.

Sababu inayotajwa ni gharama kubwa ya kuendesha shirika, kwa kiasi kikubwa bei hii huchangiwa na umeme ambao TANESCO inabidi inunue kutoka makampuni mengine.

My Take
Ingekua bora kama TANESCO wangejikita katika upunguza gharama zao za uendeshaji kwa kuzalisha wenyewe umeme wa bei nafuu kuliko kukimbilia tu kutupa mzigo kwa walaji

Pamoja na nchi kujisifia mmegundua gas na mafuta mengi bado umeme ni kimeo?
 
Umeme hautapanda wala hakutakuwa na bei mpya January 2013, hii ni kauli ya Waziri wa Nishati na Madini alipokuwa anahojiwa na ITV- Kipindi dakika 29/10/2012.

kwenye hicho hicho kipindi waziri alisema Tanzania inayo policy document ya gas, wewe unaamini?
 
Umeme bado tatizo ndugu yangu

Mkuu kazi nchi hii ipo! Hata hilo ziwa nyasa kama kinachogombewa ni wese, basi hakuna haja ya kutwangana na Malawi manake kuwa na ziwa na hayo mafuta hayatoisaidia Tanzania. Hiyo gas iliopo inatusaidia nini?
 
Jamaa wanataka kutengeneza policy ya gas (ingawa wameshachelewa tayari lakini sio mbaya), ila ona watu waliowaita kwenye hicho kikao cha kutengeneza draft ya policy

Ubalozi wa marekani, wa canada, wa india, wa norway, wa Uk, wa Sweden, wa Ufaransa nk

Sijui serikali yetu wanatumia nini kufikiri, hivi hawa watu wataenda kulinda maslahi ya mtanzania kweli? hata wangeniita mie ningeweza kuwa na mchango wa kusaidia taifa kuliko hizi embassies, sie ndio tunajua mazingira yetu.

kwa hali hii kwa nini yasijirudie yale yale ya madini, tutaibiwa tena, viongozi hawajajifunza bado
 
kwenye hicho hicho kipindi waziri alisema tanzania inayo policy document ya gas, wewe unaamini?

kwani gas yenyewe nasikia mkulu si kaiweka rehani kwa kumgomboa mwanae huko kwa gin tao?
 
kwani gas yenyewe nasikia mkulu si kaiweka rehani kwa kumgomboa mwanae huko kwa gin tao?

nimetafuta sana validity ya hiyo story naona kama imeanzia hapahapa TZ
 
Naaminibado tuna safari ndefu sana ambayo inabidi kila mmoja kwa pamoja kushirikiana katika kufika hii safari, kupata wawekezaji wa ndani zaidi kuliko wa nje, ni hakika nchi ina rasilimali watu wengi lakini wengi waliojazana katika fani moja hii ni changamoto kwa vyuo katika kuleta fani ya watu tofauti ndani ya nchi kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa mashirika ya serikali.

Naamini katika kujenga nchi ushirikiano wa pamoja ndani ya nchi unaitajika ila unapokuwa tegemezi sana ni mazara mengi katika nchi hutokea.......

Elimu ni jambo jema sana katika kujiletea maendeleo leo ata ukiambiwa mtambo uliopo unakula lita mia mbili kwa siku sababu una elimu ya utambuzi itakuwa ni jambo ambalo ni kazi.

Hii ni changamoto kwa wasomi wetu wa ndani na nje katika kuleta mpango madhuti kuinusuru nchi uko tuendeka, tukiendelea kutegemea msaada kwa kila jambo atima yake maisha yetu ni kuwa gharama kufanana na nchi za ulaya.

Nina imani na watanzania walio wengi wenye elimu na wenye nia ya kuleta maendeleo kwa nchi ya tanzania kwa ujumla..
 
I will be more than suprised wasipopandisha bei ya umeme comes 2013, wanavyopenda sifa na kuropoka, wangeshasema tu kama wana hata fununu ya mpango mbadala. Nadhani jambo la msingi ni kila mmoja wetu kuanza kufikiri how to get rid of tanesco, bei lazima wapandishe.
 
taarifa kutoka vyanzo vyangu vya kuaminika bei ya Umeme itaongezeka kwa asilimia 50 kuanzia mwezi wa kwanza.

Sababu inayotajwa ni gharama kubwa ya kuendesha shirika, kwa kiasi kikubwa bei hii huchangiwa na umeme ambao TANESCO inabidi inunue kutoka makampuni mengine.

My Take
Ingekua bora kama TANESCO wangejikita katika upunguza gharama zao za uendeshaji kwa kuzalisha wenyewe umeme wa bei nafuu kuliko kukimbilia tu kutupa mzigo kwa walaji
Na mashaka sana na hiki chanzo chako cha habari kwani tulishaaidiwa kuwa kuanzia Jan 2013 gharama za umeme zitashuka kama ifuatavyo:
-Mijini itakuwa laki 360.
-Vijijini itakuwa laki 170.
Na sisi huku vijijini tunasubiri sana Jan 2013.
 
unaongea kuhusu gharama za kuunganisha umeme na mie ninaongelea bei ya unit ya umeme, bila shaka vitakua vitu viwili tofauti
 
Kazi ya JK na mafisadi papa wenzake, si wanamlipa RA na JK then watu wanauliza Riz anapata wapi mpunga?
 
Hii niliibandika 17th October, Jumamosi nimesikia Haruna masebu anaitisha wananchi kujitokeza karimjee ili kutoa maoni yao kuhusu bei za umeme, watu wanatakia leo kuanzia saa 4 asubuhi.

hii inafanywa ili kutimiza tu matakwa ya kisheria lakini ki ukweli bei ya umeme ilishapanda siku nyingi, ndio maana tarehe 17 mimi nilikua najua kwamba umeme utapanda kwa asilimia 50% ifikapo January
.
 
Fafanua zaidi vyanzo vyako. Unatutakia presha na magonjwa mengine yatokanao na mshtuko

taarifa kutoka vyanzo vyangu vya kuaminika bei ya Umeme itaongezeka kwa asilimia 50 kuanzia mwezi wa kwanza.

Sababu inayotajwa ni gharama kubwa ya kuendesha shirika, kwa kiasi kikubwa bei hii huchangiwa na umeme ambao TANESCO inabidi inunue kutoka makampuni mengine.

My Take
Ingekua bora kama TANESCO wangejikita katika upunguza gharama zao za uendeshaji kwa kuzalisha wenyewe umeme wa bei nafuu kuliko kukimbilia tu kutupa mzigo kwa walaji
 
Labda kama hawajitaki. You don't just raise some bill by 50% in an already overtaxed system.

But then again this is bongo.

If at all this is credible, waacheni wabane sana tu, labda watu wataamka na kufanya mapinduzi.

Maana kula kwingine huku hata kipofu anastuka.

Misri watu wameanza "Arab Spring" kwa sababu bei ya mkate ilipanda. Syria kwa sababu Assad aliendekeza big landowners kulima thirsty cash crops baada ya ukame bila kujali watu wa hali ya chini.

Don't you know, they are talking about a revolution it sounds, like a whisper...
Only there is not even a welfare system or unemployment line.
 
Fafanua zaidi vyanzo vyako. Unatutakia presha na magonjwa mengine yatokanao na mshtuko

Vyanzo huwa haviwekwi wazi, siku ingine vitaogopa kutoa taarifa, lakini hii taarifa ni sahihi, si ulisikia jamaa waliitisha mkutano wa watu kwenda kutoa maoni tarehe 10 December 2012 na mimi niliweka hili bandiko tarehe 17 October 2012, nafikiri you can connect the dots.

huku kuitisha walaji eti kukusanya maoni yao pale karimjee ni sanaa tu, wanajua nini tayari wamekubaliana, wanatimiza tu matakwa ya kisheria.

Ikifika January watakuja na madai kwamba TANESCO waliomba asilimia 155 lakini kwa kuzingatia maoni na maslahi ya walaji tumewakatilia tukawaruhusu kuongeza kwa asilimia 50 tu
 
Back
Top Bottom