Bei ya soda yamtoa jasho muuzaji

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
KATIKA hali ya kushangaza ambayo watu wengi hawakuweza kuamini macho yao ni pale kijana mmoja wa milima ya usambaa kumkunja shati muuza duka baada ya kurudishiwa chenji ambayo hakuitarajia.
Hayo yalitokea jana majira ya jioni, katika maeneo ya Kariakoo baada ya kijana huyo anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 22 kuhamaki baada ya kurudishiwa shilingi mia nne [400] baada ya ya mia tano [500] kama alivyotarajia.

Imedaiwa kuwa, kijana huyo ambaye inasemekana anajishughulisha na ubebaji mizigo sokoni Kariakoo na kuchukua tenda mbalimbali za ubebaji mizigo alifika dukani hapo na kuaigza soda aina “Mountain Dew’ na kuanzakupata kinywaji hicho bila ya kuuliza bei kwa kutambua bei ni ile ile ya awali.

Sheshe lilianza mara baada ya kumaliza kinywaji hicho na kumuamuru muuza duka hilo ampatie chenji yake ili aweze kuondoka na ndipo muuza alipotoa kiasi cha shilingi mia nne na kumpatia na kumambia chenji yake ni hii kwa kuwa alimpa noti ya shilingi elfu moja

Ilidaiwa kijana huyo alianza kucheka kwa kuashiria huenda muuzaji huyo anamtania na kuanza kumwambia “ bwana acha utani naomba mia yangu niondoke bwana” na muuza kumjibu kuwa hakuna mia kwani bei ya soda ni 600

Kijana huyo alimwambia kwa mara nyingine naomba mia yangu niondoke, ghafla kijana huyo alitaka kuingia dukani humo na muuzaji huyo kumwambia acha fujo ondoka soda zimepanda bei

“Kwanini hukunambia mapema mbona bei hiyo haijatangazwa wewe mwizi, baada ya kutoa kauli hiyo muuzaji kauli ya kuambiwa mwizi hakuipenda na kumtia kibao kijana huyo na ndipo varangati lilipoanza na kijana huyo kuonyehsa mabavu kumkunja muuzaji na wasamalia kumuamuru muuzaji huyo aachane na kijana huyo kwani anageweza kumletea kesi.

Wakati NIFAHAMISHE inapita mtaa huo ilishuhudia ugomvi huo na kubahatika kuongea na kijana huyo na kijana huyo kudai “ mimi nilishapanga bajeti yangu halafu huyu muuzaji ananiletea ujinga hiyo mia tano nilipaanga kesho nianzie kupata chai “ alilalama kijana huyo

Hata hivyo baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wlimsihi kijana huyo kuwa baadhi ya maduka ya walikuwa wakiuza soda kwa abei hiyo na wengine wakiuza bei ya awali shilingi 500.

Hata hivyo wazalishaji wa vinywaji hivyo walikana upandaji bei wa vinywaji hivyo na kukiri wauzaji wamekuwa wajipandisha bei hiyo kiholela.

Wazalishaji hao walidai kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakiongeza bei ya vinywaji hivyo ka manufaa ya kupata faida maaradufu na kwa kuwa hakuna tangazo linalonyesha kupanda kwa bidhaa hizo.

Hata hivyo badhi ya mabango ya vinywaji hivyo kutoka viwandani yameonyesha hakuna mabadiliko ya bei kama wanavyofanyan wauzaji wa rejareja mitaani.
 
Back
Top Bottom