Bei ya mafuta vipi?

Makoye Matale

JF-Expert Member
May 2, 2011
6,491
2,104
Serikali ilitangaza kuwa ifikapo Julai mosi mafuta ya petroli na dizeli yatashuka bei, hadi leo Julai 2 mbona bei ziko palepale, serikali imelala?
 
Serikali ilitangaza kuwa ifikapo Julai mosi mafuta ya petroli na dizeli yatashuka bei, hadi leo Julai 2 mbona bei ziko palepale, serikali imelala?

Bei ya mafuta haitapingua kwa kodi zilizo ondolewa, lakini utakubaliana na mimi kuwa hiyo bei iliyokuwepo kabla ya kodi kuondolewa haikuwa realistic kwa sababu mafuta mengi yalikuwa yemechakachuliwa hiyo kuwafanya wenye vituo vya mafuta kupunguza bei ya disel wakijua kuwa tayari walikuwa na super profit( baada ya chua), so baada ya mafuta ya taa kuongezewa kodi hiii ina maana kuwa ile super profit haipo tena, ili kupata angalau kidogo mafuta lazima yatapanda
 
mkuu hii ni bongo huwa tupo sensitive kwenye kupandisha kuliko kushusha bei za vitu sukari yenyewe mpka maandamano..
 
Serikali ilitangaza kuwa ifikapo Julai mosi mafuta ya petroli na dizeli yatashuka bei, hadi leo Julai 2 mbona bei ziko palepale, serikali imelala?

Hahahahaaaaaaaaaaaaaa! Kama wew ni mkiristo naomba nikukumbushe kwenye biblia kuna mstari unaosema, je wewe ni mgeni hapa? Maana hujui yaliyotendeka humu uyahudi?

Kama siyo Mkristo basi naomba nikuulize ulikaa nje ya nchi miaka mingapi maana hujui yanayoendelea kwa muda unaofikia miaka sita sasa.

Ndugu yangu hujui kuwa serikali ya sasa ikitangaza bei ya kitu kupungua hicho kitu kinapanda bei? Kumbuka suala la sukari, Kumbuka tumeambiwa mara ngapi kuwa tatizo la mgawo wa umeme litakuwa historia halafu unaionaje hali?
 
Back
Top Bottom