Bei ya cement ya Dangote ilikuwa Propaganda?

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Nimeona matangazo ya Cementi ya Dangote....Je bei zao ni rahisi kama wanasiasa walivyokuwa wanajipamba? Hasa ukizingatia Mtwara na Lindi walitwanga mabomu ya kutosha suala la gesi

Bei ya Cementi Dangote ni Rahisi ulinganisha kwamba wanatumia Gesi

Gesi ni nishati gharama nafuu ya uzalishaji kuliko Umeme wa TANESCO

Katika kutengeneza Cementi, je ni malighafi gani zinatoka nje ya nchi na zipi zinatoka Tanzania hapa hapa?

Ni kwa % ngapi Malighafi za Tanzania zinatengeneza cementi?

Kwa nini Cementi ya kutoka Kenya au Pakistani iwe bei sawa au bei rahisi kuliko ya Tanzania?

Sasa wananchi amkeni, sasa ukweli ndio huu, bei ya cementi ndio hii...Mjipime wananchi, mlikuwa mnadanganywa au la,....
 
Wawekezaji wote waliokuja awamu zikizopita walikuwa na usanii sana. Sitegemei bei ya cement ya dangote kuwa ya chini.
 
Wawekezaji wote waliokuja awamu zikizopita walikuwa na usanii sana. Sitegemei bei ya cement ya dangote kuwa ya chini.
Hata halotel walikuja na gear hizo pia, mwisho wa siku bodi ya ushindani wa kibiasha ndo inakuwa muamuzi wa mwisho ...
 
Boss ata twiga cement wanatumia gas miaka mingi sana
 
Mkuu mfanyabiashara sio Imam wala Padri. Shida yake kubwa ni faida.

Mbaya zaidi wazalisha cement wakikaa chini wenyewe wakaamua bei iwe kiasi kadhaa hata ufanye nini bei yao ndiyo itatumika. Ama mje na kitengo cha kudhibiti bei kama EWURA ambapo ni vigumu.
 
Wanaofanya bei ipande ni wafanya biashara wakubwa a.k.a distributors...

hawa ndo wanachukua kiwandani na kuweka margin wanazotaka wao.

Pia hawa viwanda vya cement wana kama cartel yao ambayo hupanga bei ili wote wafaidike... badala ya kuwa na ushindani wanakuwa wanashirikiana kama ilivyo kwa mafuta.
 
Dangote wasikubali wahuni wachache kuwaharibia soko. Wao wasimamie na waweke mashariti ya bei zao kwa mlaji wa mwisho, nilikuwa mteja wa mwanzo kabisa kununua Cement ya dangote kwa ajili ya Ujenzi site kwangu. Nilibahatika kuinunua kwa bei ya jumla kwa mashariti ya kununua mifuko 50@11,500/= lakini cha ajabu leo bei ya rejareja kwa mlaji wa mwisho ni 13,000/=
 
unataka iwe shin'ngapi?
 
Back
Top Bottom