Bei mpya za kuunganisha umeme!!

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
3,142
5,634
Wadau nimesikia baadhi ya Wabunge wakipongeza Wizara ya Nishati na Madini kwa kushusha viwango vya kuunganisha umeme. Naomba kwa yeyote mwenye viwango vipya anipatie tafadhali. Hii itatusaidia kwa wale ambao bei ya kuunga umeme ilikuwa inatusumbua tuweze kuunganisha faster. Pia viwango vipya vitaanza kutumika lini. Thanx JF.
 
Lol, ya kusitisha utoaji mafao Ilianza immediately, ya kushusha bei ndo inahitaji maandalizi?
 
Ila wamejitahidi kushusha bei za kuunganisha umeme na bei za nguzo!! Nguzo moja kwa mjini ni kama laki 5 hivi,imeshuka kutoka million moja na laki mbili........Kuunganisha umeme kwa mjini ni kama laki3 hv from 450,000/=
 
Lol, ya kusitisha utoaji mafao Ilianza immediately, ya kushusha bei ndo inahitaji maandalizi?

King'asti kuelewa uongozi wa Tanzania yahitaji moyo na uvumilivu mkubwa sana, otherwise unaweza ukajikuta unajifunga mabomu na kuwalipua wote
.
 
Ila wamejitahidi kushusha bei za kuunganisha umeme na bei za nguzo!! Nguzo moja kwa mjini ni kama laki 5 hivi,imeshuka kutoka million moja na laki mbili........Kuunganisha umeme kwa mjini ni kama laki3 hv from 450,000/=

Hivi kinachozuia hizi bei kuanza kutumika kwa sasa nini? Kwa nini wasubiri mpaka January?
 
Labda hakuna nguzo wala nyaya ndio maana bei haianzi immediatly!
Au wanamalizia stock ya zamani kwanza ya nguzo!
 
Hivi kwanini tunalipia Gharama za kuvuta Umeme...?? Mi nadhani ni kama vile kuweka kiingilio Dukani... Ukitaka kuja kununua nguo say kwenye duka fulani ulipe kiingilio mlangoni halaf ndio ukachague unachotaka na ukipata bidhaa Ulipie Tena...
Sisi ni wateja wa Tanesco, tunapochargiwa connection fee na nguzo fee, wakati hatuelezwi hizo fedha zinarudije kwa mteja ni utemi flani....Kwasababu siku ukitaka kuachana na Tanesco ukawaambia wakupe Nguzo zako ulizonunua, Ukachane hata mbao za kujengea banda la kuku, Je watakupa? Na kama sababu ni kwamba wengine watakuwa wanatumia nguzo hizo hizo kupata umeme, kwanini wasikurefund pesa zako basi, hata kwa depreciation...

Tunalipa Gharama kuubwa kwa umeme wa mashaka... Mara umekuja mwingi unaunguza vitu na nyumba za watu, mara umekuja mdogo hauwezi kuwasha pasi... Mara ohooo Mgao miezi sita kwa masaa 16 nchi nzima...
Wananchi tusikubali kuburuzwa namna hii..Kwakuwa system ni corrupt...Basi, Ni wakati Muafaka Kuanza kutumia Umeme Jua au njia nyingine za kuzalisha umeme kama upepo nk...halafu tuone na hizo wanatucharge connection fee, au solar panels ownership fee...

Kwa mtu anayehitajika kuvuta umeme kwa kutumia nguzo tatu au nne, anaweza kabisa kuafford kuwa na umeme wake mwenyewe unaotumia Solar, tena bila hata ya gharama za uendeshaji na matumizi kama vile Luku....
NI MTAZAMO TU.
 
Inaboa mkuu unalipishwa nguzo tatu peke yako unawaomba majirani msaidiane wanakataa ukimaliza tu wote wanaunganisha fasta kiulaini kama nguzo nalipia kwann waniunganishe na wengine bila kunichangia garama
 
Natamani sana yawepo mashirika zaidi ya kusambaza umeme ili ushindani uongezeke zaidi maana ukifanya biashara katika mfumo wa monopolism mara nyingi unaweza kufanya maamuzi ya kumuumiza consumer, na consumer anakuwa hana alternative nyingine zaidi ya kuendelea kutegeme huduma yako.
 
Bei za mkuonganisha umeme zimeleta nafuu kidogo ya maisha kwa wa tz! Ila sasa kod kubwa ya kwenye kununua unit zaluku
 
kwa bimkubwa walikata long tym wakachukua na nyaya{zetu za umeme} naweza kung'oa mita alafu nikaweka ruku mwakani. Msaada wakuu
 
kwa
wateja watakaojengewa njia moja (single phase)
kwenye umbali usiozidi mita 30 bila kuhitaji
nguzo, katika maeneo ya vijijini watalipa Shilingi
177,000 na wa mijini watalipa Shilingi 320,960 badala ya Shilingi 455,108 zinazolipwa na wateja
hao kwa sasa. Punguzo hili ni sawa na asilimia
61.11 kwa wateja waishio vijijini na asilimia 29.4
kwa wateja waishio mijini.
 
umeme bila nguzo mjini ni 320000.huu umbali usizid mita 30,kijijjini 177000.nguzo moja kijijini 337740=,mjini 515618, nguzo mbili kijijini 454,654=,mjini 696,670. bei hizi ni mpya
 
[asante kwa ufafanuzi mkuu, QUOTE=HUGO CHAVES;5332657]umeme bila nguzo mjini ni 320000.huu umbali usizid mita 30,kijijjini 177000.nguzo moja kijijini 337740=,mjini 515618, nguzo mbili kijijini 454,654=,mjini 696,670. bei hizi ni mpya[/QUOTE]
 
ofcoz watu wanaumia sana na bei ya kuingiza umeme ila kama ndo wameshusha kihvyo wamejitahidi na big up kwao. Hayo ni maendeleo pia.
 
Bei mpya ishaanza kutumika, lakini bado kuna bureacracy TANESCO kwenye utendaji. Wiki ya pili nishafanya na malipo lakini bado mpaka leo havajanifungia mita.
 
Back
Top Bottom