Bei mpya ya umeme na siasa yetu

kidumu chama cha mapinduzi...kazi ipo kwenu..mi nipo kijijin hapa natumia kuni na kibatali changu,redio nishaanika mawe yangu juani,tv nitaangalia kwa jirani..usafiri nina baiskel yangu kuukuu..
 
Tunaanza kulipia gharama za ufisadi sasa.Tulirukaruka na kufurahia kanga,kofia na tshirts za kijani na kuwapa kura,hii ndo ari zaidi,kasi zaidi na nguvu zaidi.

Haya ilikuwa iwe kabla ya uchaguzi,wamesubiri uchaguzi upiteee.......safi zaidi , kasi zaidi, kwa ariii zaiddiii...Wabongo ujinga mpaka lini ?.....hawajui kukataaa... hata kama wanaumia......!!!!!!!!:angry:
 
Kimsingi wala siumii ni furaha tu ili watz tufumbuke akili na kuondoa ukungu kwenye ubongo wetu.

Alipokuja dr wa ukweli Slaa na mikakati ya kuboresha maisha ya mmbongo tukamwita vuvuzela mwenye ngonjera tukaamua kuwarudisha madarakani mafisadi.

Haya ndo tuloyataka, niko likizo home Biharamulo na nimekwenda filling station leo asubuhi bei ya lita ya petrol ni 1950 na nimeambiwa ndo kwanza bei imeshuka.

Kulikuwa na barabara inatengenezwa kwa kiwango cha lami toka Lusahunga to Muleba, hiki kipande cha Biharamulo wamesimamisha eti hawajalipwa, tunaelekea wapi?

Haya ndo maisha tuloyataka, tanesco wanapaswa kuwalipa dowans mabilioni, wakati huo huo ccm wanapaswa kurudisha gharama za kampeni.

ACHENI TANZANIA IZIDI KUANGAMIA HUKU TUKIJISIFU KUWA TUNA AMANI? NI AMANI KWELI HII AU CYNICISM?
 
Sasa mnasemaje?
Maana naona ninachokisoma humu naona ni manung'uniko na kunyoosheana vidole ambavyo havitatusaidia kitu!!

Hivi mnajua wenzetu Zambia down the road wakiongezewa hata senti moja kwenye kilo ya unga huko mtaani hapatoshi na nchi huwa haikaliki?
Why not here?
Can't we do something? Anything???
Damn it wasomi, anything!!!

Nakubaliana na wewe 110%....lets do something.....maprofesa wa vyuo vikuu wagome sijui kwa niaba ya wananchi...yaani kujimobilize kuandamana kwa wasomi na wanaharakati mbalimbali ni ngumu na sauti yao huwa inaishia hewani...
 
Hivi tunaitaji EWURA ya nini? tunailipa unaponunua umeme kwa kazi ipi? overhead kwa mtanzania. 18% kwa ufanisi upi unaotengemea?
Tunaanza kuchangia uchaguzi 2015 - kwa kulipa Downs. Machungu yote haya ikifika 2015 tutakuwa tumesahau- mbele ya T-shirt, Khanga, kofia na kubebwa kwenye malori. Vote aganist CCM
 
Sasa mnasemaje?
Maana naona ninachokisoma humu naona ni manung'uniko na kunyoosheana vidole ambavyo havitatusaidia kitu!!

Hivi mnajua wenzetu Zambia down the road wakiongezewa hata senti moja kwenye kilo ya unga huko mtaani hapatoshi na nchi huwa haikaliki?
Why not here?
Can't we do something? Anything???
Damn it wasomi, anything!!![/QUOTE]

Hivyo ndivyo tulivyo M-mbabe.

Nilipoanza kusoma nilidhani kuna utofauti kati ya walalamikaji wengine waliotangulia na mtuma ujumbe (yaani M-mbabe). Mwisho naye kaishia kulalamikia wasomi. Na hili tatizo tumetoka nalo kwenye jamii zetu. Unakuta mtoto anakufa kwa utapiamlo au malaria watu wanalalamikia wachawi. Muda sio mrefu utasikia watu humu wakiwalalamikia wazungu, world bank, IMF na utandawazi.
 
Nakubaliana na wewe 110%....lets do something.....maprofesa wa vyuo vikuu wagome sijui kwa niaba ya wananchi...yaani kujimobilize kuandamana kwa wasomi na wanaharakati mbalimbali ni ngumu na sauti yao huwa inaishia hewani...

Professor na Dr. wa chuo kikuu agome? weeeeeh aaah wapi!!!! Hivi haufahamu kuwa uhuru wa nchi hii uliletwa na watu wasioenda shule ndugu yangu? Wasomi walikuwa busy maofisini wakimtumikia kafiri wapate ujira wao.

Siku hawa wanaouza kura zao kwa kanga, Tshirt, vijipesa vidogo vidogo na kubebwa kwenye malori wakishtuka basi nchi hii itapata uhuru mwingine. Kwa sasa hivi wacha tupate kibano kwanza akili zije.
 
Jenerali Ulimwengu aliwahi kuandika wakati tunaelekea uchaguzi kuwa, tuna tabia ya kuchagua hovyo na baadaye tunalalamika nadhani uchaguzi wetu ndio umeleta matunda haya sasa hatuna budi kulalamika next time tuwe waangalifu kwenye uchaguzi ili kuepuka kulalamika.

Tusilaumiane sana kwani CCM ni balaa wanaindesha nchi wanavyopenda wao. Tusidanganyane hawakushinda ni wizi wa kura. Tutapiga porojo we halafu tutaizoea hali hiyo na kununua luku kama njugu kuwalipia CCM gharama za uchaguzi. tukiweza tuahamasishane kukataa upuuzi huu hivi wawakilishi wetu aka wazee wa mjengoni hawaruhusiwi kuliingilia kati hili na kulikemea je hao wapinzani nao wasemaje watuhamasishe kwa hili hata wale waliofaidi kanga na kofia na raba na suruali za njano tutakuwa nao kupinga hili. Shime Slaa japo uliibiwa ushindi ongoza nchi kwa remote control mkubwa, Mnyika, Mbowe, Kabwe twafwa mtusaidie huko msikubali kila kitu ovyo ovyo.
 
Siasa inapoingia katika masuala ya msingi, tunaelekea kuua taifa letu! leo tunaambiwa bei ya unit 1 ya umeme inapanda kwa asilimia 18, so kutoka ilipo karibu Shs. 129 tunaelekea Shs.160 kwa unit moja and then tuna matumaini ya kuvuka kutoka uchumi unaotegemea kilimo kuwa industrial led economy, Jamani acheni kuchakachua mambo ya msingi kama ikiwezaka EWURA si ife tu!

The Planner:

Kwa Mahesebu ya haraka haraka gharama ya unit itakuwa inakaribia Tshs 180.00 regardless upo segment 1 or 2 (domestic)! Kwahiyo kama ulikuwa unanunua umeme wa 30,000 kwa mwezi then ukijumlisha EWURA Fee, Service Charges, utapata umeme wa kutumia wiki mbili tu! Around 110 units! Kwa maana nyingine ili umentaini namba za units itabidi kwa mwezi ulipe Tshs 55,000 (assuming ulikuwa unalipa Tshs 30,000)..

Anyways DOWANS watatutesa saaaaaaaaaana hadi 2015!
 
Suala ni Taifa kujielekeza katika vyanzo mbadala, na huduma ya umeme iboreshwe kwanza halafu ndiyo bei ipande siyo zigzag namna hiyo. Hivi wahusika huwa hawasomi issues ziandikwazo na wapenda nchi.......
 
Hivi sisi lini tutakua angalau kama wazambia????... Kwa nini hatuoneshi reaction yoyote kwa huu upuuzi wanaotufanyia hawa MAFISADI hawa???!!! Wenzetu bei ya mkate ikipanda hata kidogo wanaingia mtaani kuonesha grievances zao!!!! Sisi tunanini lakini???? Kwa nini tunakubali kuburuzwsa tu bila hata kuonesha resistance kidogo????!!! It's better dying stand than living on your knees!!!....
 
>>> Umeme ulianzan kukatika katika bila wananchi kupewa taarifa wananchi walipoanza kulalama...
>>>Tukambiwa Mgao wa umeme unatokana na upungufu wa maji Kidatu na Mtera
>>>Meneja wa mtera akatuambia maji yapo tele na mgao haupasi kuwepo.
>>> Meneja wa Tanesco akashtuka kuwa viongozi akiwemo yeye wamechemsha na kauli zao
>>Akatokea hewani akasema hakutakuwa na mgao tena maana maji yapo na vyanzo vya umeme vipo vya kutosha..
>>>Tukashangaa baada ya kauli ya hizo Mgao unaendelea kuwepo kama kawa!
>>> Waziri akaja na nyingine Kali ...Hatukakuwa na Mgao maana kuna vyanzo vya kutosha vya umeme..akazidi kusema kama kutakuwa na mgao basi watu wajue ni Matatizo ya kiufundi au Transfoma!
>>> Baada ya hilo tukashangaa Mgao unbeep mara moja moja..Tukaendelea kujiuliza kunani
>>> Muda si muda punde si pende Tukaambiwa Tanseco itaongeza bei ya Umeme kwa asilimia zaidi ya 18..MAMBO HAYO!!!!
>>HII NDO TANZANIA YETU>>>Kasi zaidi Ari zaidi...Nia Zaidi..Nguvu zaidi
>>>
 
Bila kusaha mafuta ya magari yanelekea shs 2000/= kwa lita!

Ndio maana yake mkuu,

Hii nchi yani shangaza sana Dollar ikipanda wao nao wanapandisha bidhaaa ati wanakuambia twamalia stock iyo stock huwaga haiishagi khaaa, na cha ajabu zaidi dollar ikishuka wauzaji hawashushi bidhaaa zao chini watapiga piga chenga hapo na wataitafutia thamani tuu ili isiendane na dollar na wata kuambia stock tena au??

Hatuna mifumo mizuri ya kukuza uchumi na kufuatilai mapato ya taifa hata kidogo na ndio maana watu wanadai KATIBA mpya ili ikidhi maitaji ya sasa kwa wananchi na sio kutupotezea.

Sasa twachangia kulipa Bil 182 ile tunayo daiwa na DOWANS/RICHMOND nchi hii wale wote walio sign mikataba mibovu walipaswa kwanza wa jiuzuru hatuwezi lipa hiyo pesa anagli wao wako madarakani ni kuwa tuna haralisha upuuzi wao kuwa walikuwa wako sawa, ni kuwa watoke kwanza hata kama tutailipa basi na watako kuja nao ndio watakuwa makini

Wajua inashangaza sana nchi inaendeshwa kipuuzi sana mambo yako wazi kabisa yet viongozi wanafanya madudu kabisa sasa sijui wana wadanganyika wakina nani? Kuwa muwazi hali kama hii hufikisha hasira ya hao wadanganyika kubadilika na kuwa janga lisilo amulika na watakapo nyanyua siraha hawa wadanganyika hakuna wa kuwazuia sasa lililopo ni kuepusha hii hali kwa kufuata mikakati iliopo na kurekebisha maisha ya hawa wadanganyika
 
HIYO NI DANGANYA TOTO YA SERIKALI KUTOA MWELEKEO WA KUDAI KATIBA MPYA ILI WATU WA-CONCENTRATE NA UMEME NA EWURA.
AFTRA ALL,HAINA HAJA YA KULALAMIKA KWANI SI MLICHAGUA WENYEWE CCM?
uNAFIKI TU KUANDIKA HUMU ETI KUINGIA MTAANI...AKITOKEA SLAA KUSHAWISHI KUINGIA MTAANI WOTE KIMYAAAA!
WA-TZ WOTE WANAFIKI TU..WAOGA KAMA NGEDERE ALIYEKOSWA KUNASWA NA MTEGO WA JANGIRI!
 
Ukisikia utamu hasa sasa ndio tunaanza kuonjeshwa huo utamu. Tulifurahia T-shirt, Kofia, Muziki toka TOT, mapipa ya komoni nakadhalika. Utamu wa kuongezeka kwa bei ya umeme kwa 18% kwa kila unit, haiishii tu pale unaponunua umeme.Sheshe lake linaingia katika nyanja kibao za uchumi na uzalishaji mali. Kila bidhaa yenye kutengenezwa kwa mashine inayotumia umeme wa Tanesco, basi nayo itapanda kwa karibu ya asilimia kama hiyo. Anzia ugali kwa mama Lishe, gharama ya kushona suruali/gauni, Bei ya ndoo moja ya maji pale kwenye bomba la mpemba mtaani kwetu, gharama ya kilo moja ya samaki toka mwanza nk. Gharama itapanda kwa kila kitu. Huundio mwanzo wa ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI na KASI ZAIDI. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kidumu:embarrassed:; Chaguzi zijazo tutakuwa makini kujua scope ya kauli mbiu kama hizi "ARI ZAIDI, NGUVU ZAIDI na KASI ZAIDI" ili kujua kama haijabeba mizigo zaidi kwa wananchi kama inavyojionesha sasa hivi
 
Kwa choice ya kikwete 2010,Ili viherehere viwaishe ndugu zangu watanzania Tutegemee by 2015 hali iwe hivi.

UMEME:unit moja 800/=
PETROLI/DIZELI: lita moja 5000/=
SUKARI:kilo moja 5000/=
MCHELE:kilo moja 5000/=
mishahara ileile.
Huduma za afya,zilezile.
Kikwete atasafir jumla ya siku 400 katika kipindi chake cha uraisi
Zitatoke EPA nyingine kama 20
Mafisadi wataongezeka maradufu
Ujambazi utaongezeka maradufu

then october 2015 kitasimama kipimbi kingine kutoka CCM kitawaambia watanzania,MAISHA BORA KWA KILA MDANGANYIKA/MTANZANIA.

zitapigwa tarumbeta,utaliwa ubwabwa,zitanyweka pombe,zitagawika pombe,ZITAIBIWA KURA..,

TUTAIMBIWA WIMBO WA AMANI,tutaambiwa baba wa TAIFA hakuenzi ubishi/uvunjifu wa amani.

Tutaahidiwa meeengi..,

Watarudi tena..,CCM..,ujambazi utaendelea,umasikini utaendelea,Kelele za hapa na pale zitakuwepo..,NOTHING will change..,forever.

UNLESS we ACT NOW.
 
Back
Top Bottom