Bei mpya ya umeme kutangazwa leo

Kipis

JF-Expert Member
Jul 23, 2011
492
61
Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Bei mpya ya umeme inatangazwa rasmi tayari kwa kuanza kutumika hivyo wananchi tujiandae kwa hilo. Wana nchi tunaumizwa na viongozi wasiokuwa na huruma kwa wananchi wao ukilinganisha na hali mbaya ya maisha tulionao. Bidhaa zimepanda bei kipato bado kipo palepale..

ongezeko la 155% kutaongeza maradufu mfumuko wa bidhaa mbalimbali na kufanya maisha kuwa magumu zaidi. Hivi hii serikali haina njia nyingine mbadala badala ya kuendelea kumkamua mwananchi hali ya kuwa huduma zenyewe ni mbovu? Umeme wa uhakika hakuna huduma zitolewazo na shirika husika haziendani kabisa na wakati tulionao. Hivi,mnatumia vigezo gani hadi kufikia hatuwa hiyo! Sikumbuki vizuri ni lini kabla ya hii bei inayotangazwa leo tayari mlishapandisha. Je kuna mabadiriko gani katika kutoa huduma kwa wateja wenu kutokana na hiyo bei? Bado tunaona miundo mbinu ileile kukatika umeme bila mpangilio na mengine mengi kisha leo mnatutangazia bei nyingine. HAPANA!

Mheshimiwa Rais kwa mwenendo huu wa serikali yako,sina budi kusema itaendelea kubeba laana ya manung'uniko ya wapiga kura wako kwa kuendelea kuwatwisha mzigo usiopaswa kuwatwisha kwa uroho,ulafi na ukandamizaji usiokuwa na hata chembe ya ubinaadamu ndani yake na wewe mh. Rais kuwa kimya kwa hili.

Kumbuka maisha unayoishi wewe na watendaji wako si maisha wanayoishi wantanzania wote. Hakika serikali yako itakuwa ni yenye kulaaniwa mpaka mwisho wa utawala wako kutokana na mateso haya. Nawasilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom