Simulizi: Before I die

: BEFORE I DIE
SEHEMU YA 50
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Oh Mungu wangu ! Latoya si binadamu wa kawaida.Mambo yake ni mazito na yanaogopesha.” akawaza Innocent huku akihisi baridi mwilini
Latoya aliingia katika jumba lile ambalo lilikuwa na giza nene ndani.Akawasha taa ndogo nyekundu iliyomuwezesha kuona.Akafungua chumba kimoja akangia.Akavua mavazi yake na kuvaa gauni refu jeupe.Akatoka mle chumbani na kuelekea katika ukumbi mpana.Alikuwa akitembea taratibu hadi katika meza yenye mishumaa sita na kuiwasha halafu akapiga magoti akainama na kusujudu
“ Atha.Lut pakta du mokaja,akta pata ovakoja du mapakta” alitamka taratibu maneno haya .Akayarudia mara tatu na mara moshi ukaanza kutoka katika madhabahu ile .Latoya akaendelea kuongea maneno aliyoyafahamu yeye mwenyewe na kila alipoongea moshi mwingi ulizidi kutoka.Ulikuwa ni moshi wenye harufu nzuri ya uturi.Chumba chote kilijaa moshi na mara ghafla ukatokea mwanga mkali sana ambao ulimulika eneo lile lote.Baada ya mwanga ule mkali kutokea,Latoya akainuka na kusimama .Mbele yake toka ndani ya moshi ule wakatokea watu wawili wenye mavazi meupe na ndevu nyingi

ENDELEA………………………..

“Innocent.!! Innocent !!!..” Ilikuwa ni sauti ya Latoya iliyomstua .Akafumbua macho na kuangaza huku na huku.Alikuwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa.Latoya akamshika kichwani kwa mikono yake na mara fahamu zake zikamrejea
“ Latoya ..!!..” akasema Innocent
“ what happened?Nilisikia unalia nikataka kukufuata huko ndani lakini ghafla nika……” kabla hajamaliza sentensi yake Latoya akasema
“I know what happened.Twende tondoke”
Wakaingia garini na kuondoka
“Kwa masikio yangu nimesikia Latoya akipiga ukelele wa uchungu .Nilitaka kuingia mle ndani lakini kilichonitokea sintakisahau.I’m real scared” akawaza Innocent halafu akageuza shingo yake na kumtazama Latoya
“Huyu si binadamu wa kawaida.Kuna siri nzito katika maisha yake.Ouh Mungu wangu mambo yaliyoko hapa ni mazito .Natamani niondoke na kuachana na maisha haya lakini siwezi tena .I’m stuck in here and I cant leave this place anymore because I love Latoya.” Akawaza Innocent na kwa mbali macho yake yakatoa machozi
“ Latoya ni nani hasa? Natamani nimjue kiundani lakini naogopa.Maisha yake yametawaliwa na nguvu zisizo za kawaida.” akawaza halafu akageuka tena na kumtazama Latoya.Alikuwa ameinama analia
“ Latoya …..!!!!! akaita Innocent.Latoya hakuitika
“ Latoya ….!! akaita tena.Latoya akageuza shingo na kumtazama Innocent.
“ are you ok? Akauliza Inno
“ I’m ok Innocent.” Akajibu Latoya
“ You are crying.Whats your problem?
“ Never mind about me.I’m ok” akajibu Latoya Innocent hakumuuliza tena kitu chochote
“Naogopa kumuuliza tena kitu chochote.Anaonekana ana jambo zito, ngoja nimuache” akawaza Inno
“ Innocent” akaita Latoya
“ naam Latoya” akaitika Inno
“ Jiandae kesho kutwa tuanze ile safari yetu”
“ Usijali Latoya Mimi niko tayari muda wowote kuongozana nawe sehemu yoyote ile” akajibu Inno
“ ahsante sana Innocent.Thank you for being there for me” akasema Latoya halafu safari ikaendelea kimya kimya hadi wakafika nyumbani.Latoya hakuongea na mtu akapanda moja kwa moja ghorofani kwake.Innocent naye akapanda chumbani kwake.
“ Nimeogopa sana kwa kilichotokea leo.Kwa nini Latoya alikuwa analia.? Kuna mtu alikuwa anamuumiza?Kuna nini ndani ya jumba lile? Maswali haya yaliendelea kumuumiza kichwa Innocent lakini hakuweza kupata jawabu.
“ katika maisha yangu sijawahi kukutana na mauza uza kama haya.Inawezekana ni mipango yake nikutane na Latoya ili niweze kuufahamu upande wa pili wa mwanadamu ukoje.” akawaza Innocent akiwa kitandani.Alihisi joto sana akavua shati
“ Latoya anataka twende wapi kwa mapumziko?Niliwahi kumuuliza ni wapi tunakwenda lakini hakuwa tayari kuniambia.Kutokana na maisha haya anayoishi ananipa uoga hata mimi kuhusiana na safari hiyo ya sisi wawili pekee japokuwa ninatamani sana kuwa karibu naye nimueleze kilichomo moyoni mwangu.”
Innocent akastuliwa toka katika mawazo mengi na mlio wa simu
“hallo” akasema Innocent
‘ Innocent naomba tukutane bustanini” akasema Latoya
‘”Ok Latoya Nakuja sasa hivi” akajibu Innocent
“Wanasema kwamba Love is all about sacrifices.Because I love her I’ll sacrifice everything for her .I know its not going to be easy but even if it’s going to take my whole life I’ll die trying.” Akawaza Innocent halafu akavaa shati akatoka mle chumbani na kuelekea katika bustani ya Latoya iliyoko juu.Tayari Latoya alikwisha fika kule bustanini.
“ Unajisikiaje Innocent? akauliza Latoya
“ I’m ok Latoya.najisikia vizuri.Vipi kuhusu wewe? Unajisikiaje?
“ Najisikia vizuri Innocent” akajibu Latoya.
“Nikikuangalia machoni naona kama hauko sawa.Kitu gani kinakusumbua Latoya? Akauliza Innocent
“Ouh Innocent don’t mind about me.I’m ok.Ni uchovu ndio unaonisumbua .Hii ni sababu inayonipelekea kuamua kwenda mapumzikoni.Vile vile mambo mengi yametokea katika kipindi kifupi kwa hiyo ninahitaji kupumzika na kujaribu kuyasahau yote yaliyotokea. Nikiwa kisiwani husahau dunia kwa muda.No TV, no phone calls,no meetings,no any contact with the world.Its just me and the island.I talk to birds,animals and I go back to sleep.Hivyo ndivyo namna ninavyoishi nikiwa mapumzikoni” akasema Latoya
“Nimeipenda sana aina yako ya upumzikaji lakini kwa kuwa umezoea kuwa mwenyewe huoni kwamba nitakuwa mzigo kwako na kukuzuia usipumzike vile ulivyozoea? Akauliza Inno
“Innocent huwa ninakwenda mapumzikoni peke yangu kwa sababu sikuwa na mtu ninayemuamini ambaye ningeweza kwenda naye.Safari hii nimekupata wewe ambaye ninakuamini na kwa hiyo nitakuwa na mapumziko mazuri sana kuliko miaka yote ambayo nimekuwa nikipumzika peke yangu.Innocent wewe ni mtu wangu wa muhimu sana .Tumejuana katika kipindi kifupi lakini naomba ufahamu kwamba nilikujua kabla hata hatujakutana na ndiyo maana umetokea kuwa mtu muhimu mno kwangu.Duniani ninafahamika na mamilioni ya watu lakini sijawahi kupata rafiki kama wewe.Ninafurahi na kufarijika ninapokuwa nawe” akasema Latoya halafu akavua pete yake ya dhahabu na kumvalisha Innocent kidoleni
“ Innocent nakupatia pete hii, ambayo ni ya muhimu sana kwangu.Ninakuomba usiivue pete hii.Huu ni ukumbusho wangu kwako hata kama hatutakuwa pamoja kwa muda mrefu.Wakati mwingine inaweza ikawa na msaada mkubwa kwako “ akasema Latoya
“ahsante sana Latoya.Its a beautiful ring.I love it” akasema Innocent huku akifurahia pete ile nzuri
“ Utanikumbuka kila mara utakapoitazama pete hii” akasema Latoya huku akitabasamu
“Latoya bila hata ya pete hii,ninakukumbuka kila dakika ya maisha yangu.You are a wonderfull person I’ve ever met.Ninafurahi sana kuwa mmoja wa watu wako wa karibu”
“ Ouh Innocent,that’s so sweet.Ndiyo maana napenda kuwa nawe karibu muda wote.Ninapokuwa nawe ninasahau matatizo yangu.I forget death and everything..” akasema Latoya na ghafla akanyamaza na kumtazama Innocent ambaye alikuwa anatabasamu
“Innocent natamani watu wote duniani wangekuwa kama ulivyo wewe Dunia ingekuwa mahala pazuri sana pa kuishi lakini kwa bahati mbaya dunia hii imejazwa na watu makatili wasio na hata chembe ya huruma kwa wenzao” akasema Latoya
“ Kwa nini unasema hivyo Latoya? Akauliza Innocent
“Innocent bado hujajaliwa kuufahamu pande wa pili wa duna hii ukoje.Dunia hii ina sehemu mbili moja ni hii tunayoiona kwa macho ya kawaida nay a pili haionekani kwa macho ya kawaida.Siku ukijaliwa kuiona sehemu ya pili ya dunia hii utakubaliana na ninachokwambia kwamba binadamu ni kiumbe anayeweza kubadilik na kuwa mbaya sana kuliko hata mnyama wa mwitu” akasema Latoya
“nakubaliana nawe Latoya duniani humu kuna mambo mazito ambayo hatuwezi kuyaona,kuna watu makatili na ubinafsi umeitawala dunia siku hizi”
“ Thats my point.Mungu aliumba mwanadamu akamuweka duniani atawale kila kitu ,lakini mwanadamu huyo huyo amemgeuka hata muumba wake na kumpinga.Watu wanazivunja amri zake .Hawamuabudu tena.Wamewageukia miungu wengine.Wanaua wanadamu wenzao pamoja na kutenda dhambi nyingi zenye kuleta machukizo mbele za Mungu.Do you think its time now for God to put and end to this world? Akauliza Latoya
“ Latoya ni kweli dunia hii imejaa machukizo ya kila aina, makubwa na yasiyovumilika ,lakini pamoja na dhambi hizo za wanadamu Mwenyezi Mungu bado amezidi kutupa nafasi ya kubadilika na kumrudia yeye kutokana na sala na maombi ya wachamungu wachache wasiochoka kuomba.Nadhani Itakuwa Vyema kama Mungu ataendelea kutupa nafasi zaidi ya kujirekebisha.I don’t want to die” akasema Innocent halafu kimya kikatanda
“ Innocent you seem scared when you think of death..why? .Akauliza Latoya
“Latoya kifo kipo na kila mwanadamu atakufa lakini ninaogopa kufikiri kifo changu kwa sababu sipendi kufa.Kama ingetokea nikapewa nafasi ya kuchagua jambo moja tu na mwenyezi Mungu,basi ningeomba aniepushe na kifo..I don’t want to die.Naomba nife wakati nimekwisha zitimiza ndoto zangu kubwa” akasema Innocent
“ Me either.I don’t want to die especially this young. Lakini hata hivyo kama imeandikwa kwamba utakufa katika umri mdogo there is nothng you can do to change that.It hurt so much Innocent,kuiacha hii dunia na watu wake uliowapenda na kuwaozea.” Akasema Latoya
“ Inauma sana na ndiyo maana sitaki kufikiria kuhusu masuala ya kufa” akasema Innocent
‘ Ok Innocent lets not talk about death.Its so scary.Lets talk about something else like love” akasema Latoya na Innocent akatabasamu
“Innocent uliniambia kwamba hauna mpenzi.Je hakunamwanamke yeyote aliyewahi kukuvutia hadileo hii?
Swali lile likaonekana kuwa gumu kwa Innocent
“ Swali lako gumu Latoya lakini ukweli nikwamba wanawake wapo wengi wa kila aina na wenye kila sifa lakini kwa muda mrefu nilikuwa nikimtafuta yule ambaye nitamkabidhi moyo wangu bila mafanikio lakini nashukuru Mungu kwa kuniangazia na kwa sasa nina matumaini kwamba huenda siku za karibuni nikafanikiwa kumpata Yule ambaye anayafanya mapigo ya moyo wangu yaende kwa kasi ” akasema Innocent.Latoya akamuangalia halafu akatabasamu.
“Wow hongera kama tayari umekwisha pata mwangaza kuhusiana na mwnamke wa ndoto zako”akasema Latoya kwa sauti ya upole
“ Vipi kuhusu wewe? Akauliza Innocent
“ Innocent lets not talk about me.Lakini kuna jambo moja ambalo nataka kukushauri”
“ Jambo gani Latoya?
“Love don’t have a time to wait. Kama unafikiri kwamba tayari umekwisha mpata mtu ambaye unaamini ndiye unayempenda kwa moyo wako wote basi usipoteze muda,mueleze ukweli.Hakuna anayejua nini kitatokea katika dakika ijayo.Kwa maana hiyo tusisubiri na kujilaumu baadae kwa nini hatukuwaambia wale tuwapendao kwamba tunawapenda. Mariah carey na Boyz 2 men waliimba wimbo mmoja unaoitwa one sweet day.Do you know that song?
Innocent akaitika kwa kichwa ishara ya kwamba anaufahamu wimbo ule.taratibu Latoya akaanza kuimba
“Sorry, I've never told you, all I wanted to say
And now it's too late to hold you
'Cause you've flown away
So far away

Never had I imagined
Living without your smile
Feelin' and knowing you, hear me
It keeps me alive, alive
And I know you're shining down on me from Heaven
Like so many friends we've lost along the way
And I know eventually we'll be together
One sweet day…………………………………
“ wow sijawahi kukusikia ukiimba.Sauti yako tamu na laini kama ya malaika.Umebarikiwa mno Latoya kwa kila kitu.Laiti ungekuwa mwanamuziki nina hakika ungekuwa mmoja wa wanamuziki wakubwa mno duniani” akasema Innocent na kumfanya Latoya acheke kidogo
“ Innocent you real make me so happy.Sijawahi kuwa na furaha kama hii hapo kabla,ahsante kwa kuja katika maisha yangu” akasema Latoya
“Mimi pia.Ninajisikia furaha sana kuwapo mahala hapa,furaha ambayo siwezi kuielezea and that’s the reason I’ve sacrificed everything ,my job,my dreams,and everything just to be here only because I feel so connected to this place” akasema Innocent
“ Innocent be honnest with me.Are you happy with me as your friend? Akauliza Latoya
“Latoya naomba niwe muwazi kwako kwamba nina furaha tena kubwa sana na ndiyo maana nimeacha kila kitu kwa ajili ya kuwa na mtu kama wewe.You are a wonderfull friend,a friend that is worth to die for” akasema Innocent
Uso wa Latoya ukapambwa na tabasamu zito sana.Akamuangalia Innocent na kuuliza
“ Innocent unamaanisha hicho ulichokisema? Can you die for me?
“Ndiyo Latoya.Kama kuna mtu yeyote yule anayetaka kukudhuru mimi niko tayari kupambana hadi kufa kwa ajili yako”
“ Ouh Innocent you are like an angel to me.How can you die for a woman like me? Akasema Latoya huku machozi yakimlenga
“Latoya wewe ni mtu ambaye dunia inakuhitaji sana.Una moyo wa huruma na upendo usio na mfano.Wewe ni mkombozi na kimbilio la watu masikini kwa hiyo siko tayari kuona jambo lolote baya linakutokea na hii ndiyo sababu niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili ya kutafuta kitu ambacho kitakufanya uwe na furaha.Ninaumia kila niuonapo uso mzuri wa kimalaika kama huu ukiwa na machozi.Ninataka tabasamu hilo lililoko sasa hivi usoni pako liendelee kuwepo katika siku zote za maisha yako” akasema Innocent na uso wa Latoya ukazidi kuchanua kwa tabasamu
“ Ouh gosh ! Why I have to die?.Sitaki kumuacha Innocent. Ananipa furaha ambayo sijawahi kuipata katika maisha yangu.It hurt that I’ve found my happiness at my dying days.It hurt even more that I cant change anything now.It’s too late.Ninachotakiwa kufanya ni kutumia kila dakika iliyobaki vizuri.Nataka nife nikiwa na furaha na zaidi ya yote nikiwa msichana.sitaki kufa nikiwa bikira.Mwanaume pekee atakayenitoa bikira yangu ni Innocent” akawaza Latoya
Ulikuwa ni usiku wa aina yake kwao wote.Hakuna aliyetamani kwenda kulala.Waliongea mambo mengi sana usiku ule na hadi ilipofika usiku wa saa tisa ndipo walipoagana na kila mmoja akaenda kulala.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 51
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Ouh Innocent you are like an angel to me.How can you die for a woman like me? Akasema Latoya huku machozi yakimlenga
“Latoya wewe ni mtu ambaye dunia inakuhitaji sana.Una moyo wa huruma na upendo usio na mfano.Wewe ni mkombozi na kimbilio la watu masikini kwa hiyo siko tayari kuona jambo lolote baya linakutokea na hii ndiyo sababu niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili ya kutafuta kitu ambacho kitakufanya uwe na furaha.Ninaumia kila niuonapo uso mzuri wa kimalaika kama huu ukiwa na machozi.Ninataka tabasamu hilo lililoko sasa hivi usoni pako liendelee kuwepo katika siku zote za maisha yako” akasema Innocent na uso wa Latoya ukazidi kuchanua kwa tabasamu
“ Ouh gosh ! Why I have to die?.Sitaki kumuacha Innocent. Ananipa furaha ambayo sijawahi kuipata katika maisha yangu.It hurt that I’ve found my happiness at my dying days.It hurt even more that I cant change anything now.It’s too late.Ninachotakiwa kufanya ni kutumia kila dakika iliyobaki vizuri.Nataka nife nikiwa na furaha na zaidi ya yote nikiwa msichana.sitaki kufa nikiwa bikira.Mwanaume pekee atakayenitoa bikira yangu ni Innocent” akawaza Latoya
Ulikuwa ni usiku wa aina yake kwao wote.Hakuna aliyetamani kwenda kulala.Waliongea mambo mengi sana usiku ule na hadi ilipofika usiku wa saa tisa ndipo walipoagana na kila mmoja akaenda kulala.


ENDELEA………………………..

Saa mbili za asubuhi Innocent na Latoya walikwisha jiandaa tayari kwa ratiba ya siku hiyo.Latoya alimuomba Innocent aambatane naye katika mizunguko ya siku hiyo.Saa mbili na nusu waliingia garini na na msafara wa magari sita ukaondoka.
“ nataka nizungukie sehemu zote muhimu siku ya leo kabla ya kiza kuingia.This is my last day here.Ni siku yangu ya mwisho kuwepo hapa Tanzania kwa hiyo nataka nionane na wafanyakazi wangu pamoja na kufika sehemu zile zote ambazo nilipenda kuzitembelea .Sintaziona tena” akawaza Latoya ambaye siku hii alikuwa mkimya sana.
Kituo cha kwanza ilikuwa ni katika jengo lenye ofisi zake.Wafanyakazi wake walifurahi sana kumuona mkuu wao amefika kuwatembelea.Kwa siku kadhaa hawakuwa wamemuona kutokana na matatizo yaliyompata.Aliwaita wote katika ukumbi wa mikutano na kuwashukuru kwa namna waliyvomuunga mkono wakati wa matatizo.Aliwashukuru vile vile kwa kuendelea kuchapa kazi na kujituma hata pale ambapo yeye hayupo.Aliwataka waendelee na moyo huo wa kufanya kazi kwa kujituma hata kama hatakuwepo.Latoya aliongea maneno haya kwa uso wenye tabasamu lakini moyoni alikuwa na huzuni kubwa sana kwa kuwa alifahamu wazi hataonana nao tena wafanyakazi hawa wa ofisi yake kuu ya hapa Afrika.Kwa muda mrefu amekuwa akiishi nao kama ndugu.Baada ya kuongea nao alirejea ofisini kwake ,akaingalia ofisi yake kubwa na ya kupendeza machozi yakamtoka.Alizunguka sehemu mbali mbali za jengo lile kubwa la ghorofa nane kisha akaingia garini na msafara ukaelekea sehemu nyingine.Walizunguka sehemu mbali mbali ,na halafu wakafika katika hospitali kubwa ya magonjwa ya moyo ambayo ilikuwa imekamilika kwa asilimia tisini.Hospitali hii ambayo ilijengwa na Latoya mwenyewe ilikuwa ni kwa ajili ya kutoa tiba ya maradhi ya moyo bure kwa wagonjwa wote wenye maradhi ya moyo.Hapa alitoa machozi
“ nasikitika sintaweza kuifungua hospitali hii japokuwa nilitamani sana kushuhudia mgonjwa wa kwanza akipatiwa matibabu.Hii itabaki kumbu kumbu yangu kwa vizazi vingi vijavyo.”akawaza Latoya kisha wakaondoka.
Ratiba ilikuwa ndefu sana .Alitembelea miradi mingi anayoifadhili, mashule, zahanati,vikundi vya maendeleo vya akinamama na vijana, n.k Wengi walishangazwa na ziara ile ya ghafla aliyoifanya kwani siku zote anapotaka kutembelea mahala fulani huwa anatoa taarifa mapema.
“sehemu ya mwisho kutembelea siku hii ilikuwa ni katika kanisa moja kubwa sana alilokuwa analijenga ambalo nalo lilikuwa limekamilika.
“ katika mambo yote niliyowahi kuyafanya katika maisha yangu,hili ndilo kubwa sana.Nimemjengea Mungu wangu nyumba .Kupitia nyumba hii ataabudiwa na kutukuzwa na kupewa sifa kwani ni yeye pekee anayestahili sifa na utukufu.” Akawaza Latoya huku akitabasamu kutokana na uzuri wa kanisa lile
Toka kanisani walielekea nyumbani kwa akina Innocent ambako walipokelewa kwa furaha kubwa.Hawakukaa sana wakaaga kwa dhumuni la kuondoka.Kabla hawajaondoka baba yake Innocent akamuita mwanae pembeni na kumvisha msalaba mdogo.
“ Huu utakulinda na hatari zote.Be safe my son” akasema baba yake Innocent.
Siku ilikwisha namna hii wakarejea nyumbani kwao saa tatu za usiku
“ Innocent jiandae.Saa sita kamili juu ya alama na mwanzo wa siku mpya safari yetu itaanza” akasema Latoya nakuelekea chumbani kwake huku akionekana ni mwenye majonzi mengi.


* * * *

Saa sita kasoro dakika ishirini,mlango wa chumba cha Innocent ukagonjwa akaufungua na kukutana na Latoya
“ Its time Innocent.are you ready? Akauliza Latoya
“I’m ready” akajibu Innocent.Wakaanza kushuka ngazi taratibu halafu wakatembea katika ujia moja mrefu ulioelekea baharini bila kukutana na mtu yeyote Yule.Kitu kilichomshangaza Innocent siku hii hakukuwa na mtu yeyote kulizunguka jumba la Latoya hata walinzi wake ambao huwa wanalizunguka jumba hili kwa saa ishirini na nne hakuwaona.Hakushangaa sana kwani mambo kama haya alikwisha anza kuyazoea.
“ are you nervous? Akauliza Latoya
“ No ! I’m not” Innocent akajibu
“ Good”
Walitembea katika gati kuiendea meli moja ya kifahari iliyokuwa imeegeshwa ukingoni mwa gati lile..Ilikuwa ni meli ya kupendeza na kuvutia mno
‘ welcome aboard madam Latoya” kijana mmoja aliyekuwa amevalia mavazi meupe akamkaribisha Latoya melini.Waliingia na kusalimiana na wafanyakazi kumi na nane wa meli ile na kisha wakaelekea juu kabisa ambako ndiko Latoya hupenda kukaa.
“ Latoya nimeipenda sana hii meli yako.Meli kama hizi nimekuwa nikiziona katika filamu na sikutegemea kama siku moja ningeweza kupanda meli nzuri kama hii”akasema Innocent.Latoya akatabasamu
“wanaiita meli ya maajabu kutokana na uzuri wake”
“ I wish I could live in here for the rest of my life.Hii ni meli inayoongoza kwa uzuri duniani.Sina hakika kama kuna meli ya kifahari ya kulinganisha na hii” akasema Innocent na wote wakacheka kwa nguvu
Saa sita kamili juu ya alama meli iling’oa nanga na safari ikaanza.
“ Bye bye Tanzania.nakupenda nchi yangu na watu wake.I’ll never see u again” akawaza Latoya wakati meli ikiondoka.Kwa kuwa ilikuwa bado usiku Latoya akamuomba Innocent waende kupumzika kwani bado walikuwa na safari ndefu majini.Inno akaonyeshwa chumba chake na kuingia kulala


* * * *


Saa mbili za asubuhi,Innocent aliamshwa na wahudumu.Baada ya kuoga na kujiweka safi akaenda kujumuika na Latoya kwa ajili ya kifungua kinywa.Ilikuwa ni asubuhi nzuri sana.Anga lilikuwa la bluu na kulikuwa na mawingu madogo madogo .Hakuna kilichokuwa kinaonekana mbele yao zaidi ya maji. Bahari ilikuwa kila upande.
“ Umeamkaje Innocent? akauliza Latoya ambaye uso wake ulikuwa umepambwa na tabasamu
“ Nimeamka salama Latoya.Sijui wewe”
“ Hata mimi nimeamka salama kabisa.How was your night?
“My night was so wonderfull.Nimelala usingizi mzito sana ambao sijawahi kuupata.Pengine ni kutokana na uzuri wa meli hii”
Waliendelea kupata kifungua kinywa na walipomaliza wakaenda kukaa sehemu ya kupumzika juu kabisa ya meli.Hali ya hewa ilikuwa nzuri na ya kupendeza.waliongea mambo mengi na ilipofika mchana wakaenda kupata chakula cha mchana halafu kila mmoja akaenda chumbani kwake kupumzika.Latoya alionekana kuwa na mawazo mengi mno
“ Muda unazidi kuyoyoma na muda wangu wa kuishi unakwisha .Usiku wa leo ni usiku wangu wa kipekee kabisa.Nitamwambia Innocent ukweli wa moyo wangu na usiku wa leo nitafanya mapenzi kwa mara ya kwanza.I’m prepared for that.Huu unaweza kuwa ndio usiku wangu wa mwisho kuwa na Innocent kwa hiyo kila kitu lazima kifanyike usiku wa leo.Ile ndoto yangu lazima itimie usiku wa leo.Nimeisubiri kwa muda mrefu sana siku hii ya leo ” Akawaza Latoya na kujilaza kitandani.Picha mbalimbali za maisha yake zikaanza kumjia kichwani .Alikumbuka mambo mengi sana na machozi yakamtiririka
“ Why I have to die? Latoya akasema kwa uchungu
“Sitaki kufa.Nataka niendelee kuishi.Kwa nini nife hasa katika wakati huu ambao tayari nimempata mwanaume wa ndoto zangu ? Sitaki kumuacha Innocent”
kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Latoya kila alipofikiria kuhusiana na kifo chake.
“Nimekwisha chelewa.Siwezi tena kufanya kitu chochote kubadili ukweli huu kwamba nitakufa muda si mrefu.Ninachotakiwa kufanya ni kuutumia vizuri muda huu mchache niliobaki nao.”
Akafungua kabati lake na kuchagua nguo atakayoivaa usiku atakapokutana na Innocent kwa ajili ya chakula cha usiku
“Gauni hili nililiandaa miaka mingi kwa ajili ya kulivaa siku ya leo,usiku wangu wa kwanza na mwanaume ninayempenda.Nitalivaa kwa usiku wa leo ambao ni muhimu kwa mimi na Innocet.” Akatabasamu halafu akajilaza tena kitandani
Mlio wa saa ukiashiria ni saa kumi na mbili za jioni ulimstua Latoya toka usingizini.Akaelekea bafuni akaoga na kisha akaanza kujiandaa.Alijipaka mafuta mazuri yenye kunukia vizuri halafu akavaa gauni refu lile jekundu lililomkaa vyema.kama ilivyo kawaida yake hakuacha kuvaa koti jeusi
“ Nina hofu kubwa jinsi itakavyokuwa lakini sina namna nyingine .Usiku wa leo lazima nifanye mapenzi na Innocent.Akawaza Latoya akiwa bado amesimama anajiangalia katika kioo.Akavuta pumzi ndefu halafu akafungua mlango akatoka akaelekea katika chumba ambacho aliagiza kiandaliwe chakula maalum kwa ajili yake na Innocent usiku huo.Latoya akatabasamu baada ya kuona namna chumba kilivyokuwa kimeandaliwa na kuwekwa katika mandhari ya kimahaba kama alivyokuwa ameelekeza.Bila kupoteza muda akamtuma mmoja wa wahudumu wake akamchukue Innocent.Dakika tano baadae Innocent akawasili akiongozana na yule muhudumu
“wow ! amazing !
Akasema kwa mshangao Innocent akifurahia uzuri wa chumba kile
“Nimekipenda chumba hiki, kizuri sana” akasema Innocent na kumfanya Latoya atabasamu. Wale Wahudumu wakapewa ishara na Latoya wakaondoka na kuwaacha chumbani yeye na Innocent pekee.
“Umependeza sana usiku wa leo.Latoya you are amazing.Uzuri wako haulinganishwi na yeyote katika dunia hii“ akasema Innocent
“ Thank you Innocent’ Akajibu Latoya
“Latoya naomba niwe wazi kwako kwamba Mungu amekupendelea uzuri.Una uzuri wa kipekee kabisa.Mara ya kwanza nilipokuona nilistuka na kudhani labda wewe si binadamu wa kawaida.” Akasema Inno na kumfanya Latoya acheke kicheko kikubwa
“Thank you Innocent you always make me happy” akasema Latoya na kumkaribisha Innocent mezani
“Innocent chakula hiki cha leo ni maalum kwa ajili yetu.This is special night for me to say thank you for all that you’ve done for me” akasema Latoya
“Ouh Latoya,hakuna chochote ambacho nimekufanyia unachopaswa kushukuru.Wewe ndiye unayepaswa kushukuriwa kwa mambo ambayo umenifanyia.”
“ Innocent niruhusu nikushukuru kwa sababu pengine hufahamu thamani yako kwangu na mambo gani ambayo umenifanyia na ndiyo maana nataka kuutumia usiku huu kusema ahsante sana.Umenifanyia mambo ambayo hakuna binadamu yeyote aliyewahi kunifanyia.Umenitamkia maneno ambayo hakuna mwanadamu yeyote amewahi kunitamkia.Kwa hiyo kwa usiku wa leo nasema ahsante sana na japo kwa masaa haya machache naomba tuufanye usiku huu uwe wa aina yake.Lets forget the world for a while and make our own world” akasema Latoya halafu wakaendelea kula kwa furaha.Baada ya kumaliza kula wakaenda kuketi sofani.Latoya akamimina mvinyo katika glasi.Innocent akashangaa sana kwani toka amefahamiana naye hajawahi hata mara moja kumshuhudia akitumia mvinyo
“Latoya toka nimekufahamu sijawahi hata mara moja kukuona ukitumia mvinyo” akasema Innocent.Latoya akatabasamu halafu akanywa funda moja na kusema
“Kama nilvyokwambia awali kwamba usiku huu ni maalum kabisa kwa ajili yetu na ni usiku ambapo nina furaha ya ajabu sana na ndiyo maana nimeamua ninywe mvinyo kidogo kwa furaha niliyonayo”
“nakubaliana nawe Latoya kwamba usiku wa leo ni wa aina yake kwa sababu toka nimekufahamu sijawahi kukuona ukiwa umevaa nguo za rangi nyekundu.”
Latoya akacheka sana kusikia kauli ile ya Innoent
“Ni kweli Innocent, mimi si mpenzi sana wa rangi nyekundu, lakini leo hii imenilazimu kuvaa rangi hii kutokana na umuhimu wa usiku huu kwangu.Gauni hili nimelinunua miaka saba iliyopita na sijawahi kulivaa hata mara moja.Nilipanga nilivae gauni hili katika usiku kama huu wa leo ambao niliamini nitakutana na mtu muhimu sana katika maisha yangu.Leo ndoto yangu imetimia na ndiyo maana nimelivaa gauni hili” akasema Latoya
“.Innocent naomba ufahamu kwamba nimekwambia haya maneno toka ndani kabisa ya moyo wangu.Kwa usiku huu wa leo napenda niwe muwazi kwako kwa kila kilichopo moyoni mwangu.Vipi kuhusu wewe Innocent unaweza ukanieleza kile kilichopo moyoni mwako ambacho hujawahi kumweleza mtu yeyote? Ninamaanisha pengine kuna kitu ulipenda kunieleza lakini ulishindwa au kuogopa kutokana na mazingira? Kama unalo la kusema uwanja ni wako .Kuwa muwazi kwangu.Usiogope its just the two of us here at the middle of the ocean.” Akasema Latoya
Innocent akamtazama Latoya kwa muda halafu akataka kusema jambo lakini sauti ikakwama.Akakohoa kidogo ili kurekebisha koo lake.Latoya akamsogelea karibu akamtazama usoni na kumshika mikono,mwili wote wa Innocent ukasisimka kwa kushikwa na mikono ile laini sana.
“ Tell me Innocent,anything that you want to tell me” akasema Latoya kwa sauti laini ambayo ikampenya Innocent masikioni na kuyafanya mapigo ya moyo yaanze kwenda haraka
“Tell me Innocent” akasema tena Latoya.Mwili wa Innocent ulikuwa unatetemeka kwa hisia kalializokuwa nazo.Kitu pekee alichotaka kumweleza Latoya kwa wakati ule ni kwamba anampenda kwa moyo wake wote lakini kila alipotaka kusema ulimi ukawa mzito.Ghafla meli ikaanza kutikisika na radi kubwa ikapiga.Mvua kubwa ikaanza kunyesha.Innocent akastuka sana kwa mtikisiko ule wa meli
‘Whats that? Akauliza Innocent
“Relax Innocent.Hii ni hali ya kawaida katika safari za majini.Mara nyingi bahari huwa inachafuka” akasema Latoya
“Lakini mbona imekuwa ghafla sana? Akauliza Innocent
“ Usihofu Innocent.Meli hii ina uwezo mkubwa wa kuhimili dhoruba za baharini kama hizi.Ukiona imeyumba namna hii basi ujue kuna mawimbi makubwa sana jambo ambalo ni la kawaida baharini.Manahodha wanashughulikia suala hili na wako makini sana.” akasema Latoya kisha wakabaki wanaangaliana.Latoya akakohoa kidogo na kusema
“Innocent kama huna la kuniambia au unaogopa,mimi ninalo la kukwambia” akasema Latoya akamsogelea zaidi Innocent .Radi iliendelea kuunguruma huko nje na meli kutikisika.Latoya hakujali hilo akamsogelea zaidi Innocent na sasa nyuso zao zilikaribia kugusana.
“Innocent kuna jambo moja muhimu ambalo nataka kukwambia usiku wa leo” akanong’ona Latoya kwa sauti ndogo
“Innocent you………………” kabla hajamaliza sentensi yake ikapiga radi kubwa na meli ikatikisika kiasi kwamba vyombo vilivyokuwa mezani vikaanguka chini.Latoya akastuka na kusimama
“ Ouh gosh ! Ninafahamu sababu ya tufani hii.No ! I cant let that happen.I must do it tonight.Vyovyote itakavyokuwa usiku wa leo lazima nifanye mapenzi na Innocent.” akawaza Latoya na kisha akaenda katika meza yenye simu akawapigia manahodha wake.Aliongea nao kwa takribani dakika tatu na kisha akarejea kwa Innocent
“Nini kimetokea? Akauliza Innocent kwa wasi wasi
“relax Innocent.bahari imechafuka na sehemu hii kuna mkondo wa bahari .Usihofu tutavuka salama” akasema Latoya na kumkaribia tena Innocent
“ Innocent nataka ufahamu kwamba…….nataka ufahamu kwamba nin………….” Mara ikapiga radi kubwa na meli ikayumba .Innocent na Latoya wakajikuta wamekaribiana na midomo yao kugusana.Wote wawili walikuwa wakihema kwa kasi.
“Innocent……Inn…Innocent whatever happ…en…I..I….l..L..lo…….!!” kabla Latoya hajamaliza alichotaka kukisema ikapiga radi kubwa na kumzuia
“ Ouh gosh ! lazima nimwambie ukweli Innocent usiku huu” akawaza Latoya huku akitetemeka mwili.
“ Latoya hali inazidi kuwa mbaya..tutafanya nini? Akauliza Innocent
“Innocent naomba unisikilize.Please listen to me..” akasema Latoya huku akihema kwa kasi
“Latoya hali ni mbaya sana.Kwa nini tusiongee mambo hayo baadae wakati bahari imetulia? Akasema Innocent kwa woga huku upepo mkali sana ukiendelea kuvuma na mawimbi makubwa kuipiga na kuitikisa meli
“Innocent sikiliza kwanza.Kuna kitu unatakiwa ukifahamu.You have to know that I lo……….!!” Kabla hajamaliza sentensi yake, kishindo kikubwa cha radi kikasikika .Innocent hakuona tena kitu chochote zaidi ya giza nene.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………………


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 52
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Nini kimetokea? Akauliza Innocent kwa wasi wasi
“relax Innocent.bahari imechafuka na sehemu hii kuna mkondo wa bahari .Usihofu tutavuka salama” akasema Latoya na kumkaribia tena Innocent
“ Innocent nataka ufahamu kwamba…….nataka ufahamu kwamba nin………….” Mara ikapiga radi kubwa na meli ikayumba .Innocent na Latoya wakajikuta wamekaribiana na midomo yao kugusana.Wote wawili walikuwa wakihema kwa kasi.
“Innocent……Inn…Innocent whatever happ…en…I..I….l..L..lo…….!!” kabla Latoya hajamaliza alichotaka kukisema ikapiga radi kubwa na kumzuia
“ Ouh gosh ! lazima nimwambie ukweli Innocent usiku huu” akawaza Latoya huku akitetemeka mwili.
“ Latoya hali inazidi kuwa mbaya..tutafanya nini? Akauliza Innocent
“Innocent naomba unisikilize.Please listen to me..” akasema Latoya huku akihema kwa kasi
“Latoya hali ni mbaya sana.Kwa nini tusiongee mambo hayo baadae wakati bahari imetulia? Akasema Innocent kwa woga huku upepo mkali sana ukiendelea kuvuma na mawimbi makubwa kuipiga na kuitikisa meli
“Innocent sikiliza kwanza.Kuna kitu unatakiwa ukifahamu.You have to know that I lo……….!!” Kabla hajamaliza sentensi yake, kishindo kikubwa cha radi kikasikika .Innocent hakuona tena kitu chochote zaidi ya giza nene.


ENDELEA……………………

Moshi mkali uliomuingia puani ulimfanya apige chafya kwa nguvu mara tatu.Sauti za watu zikasikika.Walikuwa wakiongea lugha ambayo hakuifahamu.Macho yalimuuma na hakuweza kuona chochote kutokana na moshi mwingi uliokuwemo katika chumba kile.Alijaribu kufungua mdomo kutaka kuongea jambo lakini moshi mwingi ukamuingia mdomoni na kumfanya akohoe zaidi.Aliendelea kusikia watu wakiongea kwa lugha asiyoifahamu lakini hakuweza kuwaona watu hao kutokana na ,moshi mwingi.
“ Niko wapi? Ninafanya nini humu? Innocent akajiuliza huku akiendelea kukohoa na kupiga chafya mfululizo.Mwili haukuwa na nguvu na kila alipojaribu kuinua mkono alishindwa.
Mara mikono yenye nguvu ikamshika na kumnyanyua toka pale alipokuwa amelala na kumtoa ,kumpeleka sehemu nyingine yenye uwazi na upepo mzuri.Taratibu akafumbua macho na kujikuta amezungukwa na kundi la watu wanaume waliokuwa vifua wazi na viunoni mwao waljifunga ngozi za wanyama.Watu wale walikuwa wafupi wafupi na wenye miili iliyojengeka vyema.Nywele zao zilifanana na zile walizonazo watu wa bara Asia.
“ Hapa niko wapi? Hawa ni akina nani?
Akawaza Innocent akiwa amelazwa juu ya kitanda kilchosukwa kwa ngozi ya mnyama.Watu wale waliendelea kusemezana wao kwa wao huku wakimtazama .Baada ya kama dakika ishirini hivi toka awekwe pale nje, alitokea mzee mmoja mwenye ndevu nyingi nyeupe na shingoni alivaa meno mawili ya simba.Mzee yule ambaye alionekana kama ndiye mkubwa wao alimuinamia Innocent akamtazama machoni halafu akaubonyeza mkono wake.
“sukuchaa…!!!!!Kamulaping tcha..!!” akasema mzee yule na mara kikaletwa chungu ambacho ndani yake kulikuwa na vitu kama dawa.Akachota maji toka katika kile chungu akammwagia Innocent kichwani.Kilaletwa chungu cha pili kilichokuwa na kimimnika mithili ya mafuta.Mzee yule akayachota yale mafuta halafu wanaume wawili wenye nguvu wakamshika Innocent na kumpanua mdomo halafu yule mzee akayamimina mafuta yale yenye harufu mbaya mdomoni mwa Innocent ..mara tu baada ya kunywa mafuta yale Innocent akaanza kutapika huku watu wale wakishangilia.Aliendelea kutapika hatimaye nguvu zikamushia kabisa akaanza tena kuona giza akapoteza fahamu


* * * *


Alifumbua macho na kujikuta akiwa pembeni ya moto mkubwa huku idadi kubwa ya wale watu wakiwa wameuzunguka moto ule.Pembeni ya moto kulikuwa na wanyama wawili waliokuwa wakichomwa.Kiza tayari kilikuwa kimetanda lakini eneo lote lilikuwa na mwanga mkali uliotokana na ule moto mkubwa.Watu wale walikuwa wakipiga ngoma na kucheza kuuzunguka moto ule huku wakila nyama iliyokuwa inachomwa na kunywa kinywaji kilichokuwa ndani ya mitungi mikubwa.Ilikuwa ni kama sherehe kubwa
Mwili wa Innocent ulikuwa dhaifu sana na tumbo lake lilikuwa limeshinyaa kutokana na kutokuwa na kitu chochote ndani yake.Hakuwa amekula chochote.Pembeni ya pale alipokuwa amelazwa kulikuwa na watu wawili waliokuwa wamewekwa maalum kwa ajili ya kumuangalia.Walipomuona Innocent amefumbua macho wakawaita wenzao
“shukk hating ku la paochi…” akasema mzee yule.Akaushika mkono wa Innocent akauinua juu .Vijana wawili wakaleta vyungu viwili .Mzee yule akachota supu toka katika chungu kimojawapo ,Innocent akakalishwa na kunyweshwa supu ile.Baada ya supu ile akapewa uji uliochanganywa na nyama.Jasho jingi likamtiririka ,akajilaza tena kitandani akaendelea kutafakari na wale watu wakaendelea kucheza ngoma kwa furaha
“Hawa ni akina nani? Mbona wanaongea lugha ambayo siifahamu? Mimi si mtu wa maeneo haya.Sifanani kabisa watu hawa.Mimi ni nani? Nimetokea wapi? Jina langu nani? …..” akawaza Innocent
“ Ouh Mungu wangu,sikumbuki kitu chochote.Sikumbuki mimi ni nani,jina langu na nimetokea wapi.” Innocent akaogopa sana baada ya kugundua kwamba hakuwa na kumbu kumbu zozote kumhusu yeye.Alijaribu kuwaza lakini alishindwa kurejesha kumbu kumbu yoyote.
Ngoma ziliendelea kuchezwa huku nyama na vinywaji vikiendelea pia hadi walipochoka.Innocent ambaye nguvu zilianza kumrejea alikuwa amekaa akiwatazama namna walivyokuwa wanacheza .Kuna nyakati alijikuta akitabasamu baada ya kuvutiwa na uchezaji wa watu wale.Hatimaye baada ya kucheza kwa muda mrefu watu wale walipumzika na kuendelea kunywa kinywaji kile kilichokuwa katika mtungi mkubwa.Taratibu wakaanza kusinzia isipokuwa watu wale wawili waliokuwa wakimlinda.Bado aliendelea kuumiza kichwa kuhusiana na watu wale.Taratibu naye akaanza kuhisi usingzi akalala


* * * *


Sauti za watu wakizunguma karibu yake ndizo zilizomstua usingizini.Alifumbua macho na kitu cha kwanza alichokutana nacho ni anga la bluu lisilokuwa na mawingu lililong’arishwa na kijua kitamu cha asubuhi.Milio ya ndege wenye sauti mbali mbali za kuvutia ilisikika.Kwa mbali aliweza kusikia sauti za mawimbi ya bahari.Innocent alizungukwa na kundi kubwa la watu.Nyuso zao zilionyesha kuchoka kutokana na kazi kubwa ya kucheza waliyoifanya usiku uliopita.Taratibu Innocent akainuka na kukaa akaendelea kuwaangalia wale watu waliokuwa wanaongea lugha ambayo hakuifahamu.Yule mzee mkubwa wao akamsogelea na kumtazama machoni halafu akaongea maneno fulani na mara vijana wawili wakaleta chungu kilichokuwa na uji uliochanganywa na nyama Innocent akapewa akaunywa wote.Baada ya kunywa uji ule alitokwa na jasho jingi na kuanza kujisikia kupata nguvu.Watu wale waliendelea bado kumuangalia huku wakiongea kwa lugha yao.
“Nyie ni akina nani? Innocent akawauliza.Badala ya kujiibiwa watu wale wakacheka na kufurahi sana
“Hawa watu mbona wamefurahi baada ya kuisikia sauti yangu? Hawa ni akina nani? Akaendelea kujiuliza maswali ambayo hakuwa na majibu yake
Kitu kingine ambacho kiliendelea kumshangaza Innocent ni kwamba toka amejikuta katika mikono ya watu hawa hajamuona mwanamke yeyote maeneo haya
“Sijamuona mwanamke yeyote hapa.Jamii hii haina wanawake? Akajiuliza .Watu wale wakaanza kumsogelea na kumgusa ngozi yake kana kwamba walikuwa wanamshangaa.Walikuwa wanabonyeza mikono yake huku wakicheka na kufurahi.Mzee kiongozi akatamka maneno fulani halafu vijana wanne wakajitokeza na kukibeba kitanda kile alicholazwa Innocent na kuondoka huku wengine wote wakifuata kwa nyuma wakiimba na kucheza
Walitoka katika eneo lile la ufukweni na kuingia katika msitu mnene wenye kiza.Baada ya mwendo wa kama dakika ishirini hivi wakawasili katika sehemu moja iliyoonekana kama kijiji kilichokuwa na nyumba za miti.Vilikuwa ni vijumba vidogo vidogo.Innocent akawekwa ndani ya kijumba kimoja na kufungwa mikono na miguu ili asiweze kutoroka.Baada ya kama dakika kumi hivi mlango ukafunguliwa na watu wanne wakaingia ndani. Walikuwa na bakuli lililojaa nyama.Mmoja wa wale watu akamsemesha lakini Inno hakuweza kumjibu kutokana na kutoifahamu lugha yao.Watu wale wakamfungua mikono na kumsogezea bakuli la nyama akaanza kula kwa pupa.Alipomaliza kula nyama zile wale watu wakamfunga tena mikono na kuondoka zao.
“ Nimepoteza kumbu kumbu zote.Sikumbuki mimi ni nani ,nimetoka wapi na nimefikaje mikononi mwa watu hawa.Sifahamu lugha yao na siwezi kuwauliza chochote.Kwa sasa nahisi mwili wangu kuanza kupata nguvu natakiwa kufanya kitu.Lazima nifahamu hapa niko wapi na nimefikaje na ikiwezekana niweze kuondoka na kutafuta nilikotoka.” Akawaza Innocent .Watu wale waliendelea kuja mara kwa mara kumtazama na kila mara walikuwa wakimbonyeza mikono yake..Hatimaye kiza kikaingia na Innocent akalala

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 53
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Walitoka katika eneo lile la ufukweni na kuingia katika msitu mnene wenye kiza.Baada ya mwendo wa kama dakika ishirini hivi wakawasili katika sehemu moja iliyoonekana kama kijiji kilichokuwa na nyumba za miti.Vilikuwa ni vijumba vidogo vidogo.Innocent akawekwa ndani ya kijumba kimoja na kufungwa mikono na miguu ili asiweze kutoroka.Baada ya kama dakika kumi hivi mlango ukafunguliwa na watu wanne wakaingia ndani. Walikuwa na bakuli lililojaa nyama.Mmoja wa wale watu akamsemesha lakini Inno hakuweza kumjibu kutokana na kutoifahamu lugha yao.Watu wale wakamfungua mikono na kumsogezea bakuli la nyama akaanza kula kwa pupa.Alipomaliza kula nyama zile wale watu wakamfunga tena mikono na kuondoka zao.
“ Nimepoteza kumbu kumbu zote.Sikumbuki mimi ni nani ,nimetoka wapi na nimefikaje mikononi mwa watu hawa.Sifahamu lugha yao na siwezi kuwauliza chochote.Kwa sasa nahisi mwili wangu kuanza kupata nguvu natakiwa kufanya kitu.Lazima nifahamu hapa niko wapi na nimefikaje na ikiwezekana niweze kuondoka na kutafuta nilikotoka.” Akawaza Innocent .Watu wale waliendelea kuja mara kwa mara kumtazama na kila mara walikuwa wakimbonyeza mikono yake..Hatimaye kiza kikaingia na Innocent akalala

ENDELEA…………………………

Sauti za watu zikamstua Innocent toka usingizini.Akaamka na kukuta watu sita wakiwa mle kibandani.Miongoni mwao alikuwemo yule mzee kiongozi.Akamsogelea akamshika mkono akaubonyeza halafu akatabasamu na kuwageukia wenzake.Akawasemesha kwa lugha yao halafu wakaweka bakuli la nyama pembeni ya Innocent kisha wakamfungua mikono halafu wakatoka na kumuacha Innocent akiendelea kula nyama zile.Mara tu walipotoka akasikia sauti kama ya tarumbeta likipigwa na vishindo vya watu wakikimbia vikasikika halafu eneo lote likawa kimya kabisa
“Wamekwenda wapi? Tarumbeta hilo ni la nini?.Hawa jamaa wana maisha ya ajabu ajabu sana.Vitendo vyao vinanishangaza.Kila wajapo kuniangalia lazima wanibonyeze mikono yangu.Wanaangalia kitu gani katika mikono? Akawaza Innocent halafu akaanza kuzifungua kamba za miguuni baada ya kuchungulia na kuhakikisha kwamba pale hapakuwa na mtu yeyote.Kabla hajatoka mle kibandani mara mlango ukasukumwa na msichana mmoja mzuri sana mwenye nywele ndefu akaingia.Innocent akastuka asiamini macho yake.Wote wakaangaliana kwa sekunde kadhaa .Inno akataka kusema kitu lakini yule msichana akamzuia
“ shhhhhh…!!!!!!!.dont say anything.Can you speak English? Yule msichana akauliza.Innocent akatabasamu halafu akatikisa kichwa ishara ya kwamba anaweza kuzungumza kiingereza
“ Good..now follow me” akasema yule msichana huku akitoka mle kibandani.
“ where are we going? Akauliza Innocent.Msichana yule akamgeukia na kumuangalia kwa macho makali
“Stop asking question.You want to die here?
“ die here? What do you mean? Akauliza Innocent
“ C’mon guy,stop asking questions.If you want to get out of here this is the only chance you have now follow me” akasema yule msichana mzuri .Huku akiogopa Innocent akaanza kumfuata msichana yule.Walizunguka nyuma ya yale mabanda halafu wakaanza kukimbia kuelekea msitu mnene wakikimbia na kupita chini ya miti mirefu
“ Msichana huyu naye ni nani? Ananipeleka wapi? Mbona hafanani na watu hawa? Anafanya nini mahala hapa? Kwa nini ni yeye pekee anayezungmza kiingereza?
Maswali haya alijiuliza Innocent huku akiendelea kumfuata yule msichana.Mwili wake bado haukuwa na nguvu za kutosha lakini alijitahidi kwa kadiri alivyoweza kutembea kwa kasi katika msitu ule mnene.Baada ya dakika kama ishirini hivi wakajikuta wametokea ufukweni
“ Hurry up ! hurry up ! akasema yule msichana akimuongoza Innocent kuelekea sehemu kulikokuwa na boti ndogo nyeupe.waliifuata boti ile na kando yake kulikuwa na mitumbwi sita mikubwa.Wakaisukuma boti ile na kuiingiza majini
“ Hurry ..!! get in the boat” akasema yule msichana huku akimsaidia Innocent kupanda halafu akaiwasha na kuondoka kwa kasi huku Inno akishangaa.Msichana yule alionekana kuimudu vyema boti ile iliyokuwa ikienda kwa kasi kubwa.Mambo yaliyotokea Innocent aliyaona ni kama ndoto vile.Hakujua walikukokuwa wanaelekea hivyo akalazimika kumuuliza yule msichana
“ wewe ni nani na unanipeleka wapi?
“ naomba usiniulize maswali mengi tafadhali.Bado hatuko salama.Subiri hadi hapo tutakapokuwa salama na nitakujibu maswali yako yote” akasema yule msichana na kuendelea kuendesha ile boti .Bahari ilikuwa tulivu na hakukuwa na mawimbi yoyote.
Walitembea majini mwendo mrefu na hatimaye wakakiona kwa mbali kisiwa kidogo.Yule msichana akatabasamu na kusema
“ Pale ndipo tunakwenda”
“ Pale ndipo unapoishi? Akauliza Innocent lakini yule msichana hakumjibu kitu.Toka kwa mbali uzuri wa kisiwa kile ulionekana.Safari ikaendelea hadi walipofika katika kile kisiwa cha kupendeza mno.Walishuka na kuifunga boti katika kisiki cha mnazi .Kilikuwa ni kisiwa chenye uzuri wa kustaajabisha mno.Innocent akaustaajabia uzuri wa kisiwa kile kilichokuwa na miti ya kuvutia,majani mazuri na maua ya kupendeza sana.Msichana yule akamuomba Innocent amfuate na kuanza kutembea kuelekea ndani kabisa mwa kisiwa kile chenye uzuri wa kipekee.Ndege wa kila aina walikuwa wakiruka ,maua ya kila aina yalikuwa yanapatikana katika kisiwa hiki.Baada ya dakika kama kumi na tano za kutembea kwa miguu wakafika katika bustani yenye matunda mazuri yaliyoiva
“ Sijawahi kuona sehemu nzuri na ya kipekee kama hii” akasema Innocent huku akiendelea kushangaa bustani ile nzuri.
“ Ninahisi kama sipo duniani” akasema tena Innocent.
“Jina lako nani? Unatokea wapi? Yule msichana akamuuliza Innocent swali ambalo lilimbabaisha na kumfanya ashidwe kujibu
“nakuuliza jina lako nani na umetokea wapi? Akauliza tena yule msichana
“sikumbuki chochote,sina kumbukumbu zozote mimi ni nani na ninatokea wapi” akajibu Innocent
“Ulifikaje mikononi mwa wale watu? Akauliza tena yule msichana
“sina kumbu kumbu zozote nilifikaje pale.” Akajibu Innocent na kuinama chini.Yule msichana akamuangalia na kusema
“ pole sana.Usijali kumbu kumbu zitarejea taratibu.Hilo ni tatizo la kawaida katika eneo hili .Naitwa Naya” akasema yule msichana huku akimpa Innocent mkono
Kwa mra ya kanza Innocent akalishuhudia tabasamu pevu la Naya linalomfanya naye atabasamu.Uzuri wa binti huyu ulimsisimua .Akakitazama kifua chake kilichobeba titi ndogo zilizosimama akaitazama midomo laini akashusha macho yake chini na kukutana na kiuno kilichobeba miguu iliyojaa na kuzidi kumfanya binti huyu awe na uzuri wa kipekee kabisa
”nafurahi kukutana nawe Naya.U mkarimu sana” akasema Innocent
“karibu katika kisiwa hiki kijulikanacho kama black queen island.Ni kisiwa cha kipekee kabisa ulimwenguni.Upekee wake unatokana na kwamba hakimo katika ramani ya dunia” akasema Naya na kumshangaza sana Innocent
“Hakimo katika ramani ya dunia? Basi kitakuwa ni kisiwa cha kipekee kabisa.Uzuri uliomo katika kisiwa hiki haupatikani sehemu nyingine yoyote..Ukiwa ndani ya kisiwa hiki unajihis kama hauko katika dunia hii ya kawaida tuliyoizoea.Ni nani wanaishi hapa?
Naya akatabasamu na kusema
“Kisiwa hiki hakikaliwi na mtu yeyote kwa sasa.Hii ni sehemu ambayo malkia mweusi huja mara moja kila mwaka kupumzika.Majira kama haya kila mwaka huja hapa kupumzika yeye peke yake.Kuhusu wale watu kule tulikokua wanaitwa Albaque.Ni kabila dogo na wanaishi katika kisiwa kimoja kidogo mbali na hapa.Watu wale wanasifa moja kubwa tofauti na binadamu wengine. Wao wanakula binadamu wenzao”
Innocent akastuka sana na kutetemeka
“wanakula watu?! Akauliza
“Ndiyo.Wanakula watu.Huwa wanazunguka majini na katika visiwa vidogo vidogo na kuteka watu kisha huwapeleka katika kisiwa kile kuwachinja na kuwala.Ni watu makatili sana” akasema Naya
“ouh Mungu wangu..!! Nakumbuka walikuwa wakija na kunibonyeza mkono wangu lakini sikujua lengo lao lilikuwa nini”
“Hufanya vile ili kuangalia kama unafaa kuliwa.” Akasema Naya na kuzidi kumuogopesha Innocent
“Ilikuaje na wewe ukafika katika kisiwa kile? Akauliza Innocent
“ Ni hadithi ndefu kidogo lakini mimi sikutekwa.Nilifika mwenyewe katika kisiwa kile.Sikufahamu kama pale kuna watu wa aina ile .Wakati nikizunguka zunguka mle kisiwani nilijikuta nimekamatwa na wale jamaa na wakaenda kunifungia katika banda lililokuwa watu wengine wawili.Watu wale waliofungwa pamoja nami mle kibandani walianza kuliwa mmoja baada ya mwingine.Kabla ya zamu yangu kufika walikupata wewe na ukayaokoa maisha yangu.Walianza kukuandaa kwa ajili ya kuliwa .Kwa muda wa zaidi ya mwezi mmoja niliokaa nao nimewasoma vya kutosha.Kila siku asubuhi huwa wanakwenda katika sehemu yao ya kuabudu na baada ya hapo ndipo shughuli nyingine hufuata.Leo hii ndiyo ilikuwa siku yako ya kuliwa. Nilipowaona wameshuka bondeni, nilitoka haraka katika kibanda walichonifungia ambacho hakikuwa mbali na kibanda walichokufungia wewe.Ile boti tuliyoondoka nayo ni boti yangu ambayo nilifika nayo pale kisiwani.Najua hivi sasa watakuwa na hasira sana baada ya kukuta hatupo .” akasema Naya.Innocent alikuwa anaogopa na kutetemeka mwili
“Unahakika hawawezi kutufuata huku tulipo? Akauliza Innocent kwa wasiwasi.Naya akatabasamu na kusema
“Hapana.Hawawezi kufika huku.Kisiwa hiki hakuna mtu wa kawaida ambaye anaruhusiwa kuingia hapa.” Akasema Naya
“ Mbona mimi nimeingia? Akauliza Innocent
“ Unaonekana una muunganiko fulani na sehemu hii kwa sababu usingeweza kuingia katika kisiwa hiki wala hata kukiona.Kisiwa hiki huonekana kwa watu wachache tu ambao wanamuunganiko nacho.”.akasema Naya .Innocent akamtazama kwa mshangao
“ Kwani wewe ni nani Naya? Unaishi wapi? Katika kisiwa hiki kuna nini hadi mtu wa kawaida asiruhusiwe kuingia? Akauliza Innocent ..Naya hakumjibu kitu akachuma maembe mawili na kumpatia Innocent
“Twende upande wa pili wa kisiwa” akasema Naya.Wakaanza kutembea kuelekea upande wa pili wa kisiwa kile.Kila sehemu waliyopita ilikuwa na uzuri wa kipekee.
“Huyu Naya ni nani? Anaishi wapi? Mbona anaonekana kuyafahamu vyema maeneo haya? Kisiwa hiki kina siri gani kiasi kwamba hakuna mtu wa kawaida anayeweza kukiona wala kuruhusiwa kufika hapa? Nadhani kuna haja ya kukifahamu kiundani kisiwa hiki na kwa nini nina muunganiko nacho kama anavyosema Naya.Hisia zinakuja ni kama nimewahi kuwa na urafiki na msichana mmoja mrembo kama huyu Naya.” Akawaza Innocent wakati wakipanda kilima

TUKUTANE SEHEMU ILIYOPITA


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 54
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Mbona mimi nimeingia? Akauliza Innocent
“ Unaonekana una muunganiko fulani na sehemu hii kwa sababu usingeweza kuingia katika kisiwa hiki wala hata kukiona.Kisiwa hiki huonekana kwa watu wachache tu ambao wanamuunganiko nacho.”.akasema Naya .Innocent akamtazama kwa mshangao
“ Kwani wewe ni nani Naya? Unaishi wapi? Katika kisiwa hiki kuna nini hadi mtu wa kawaida asiruhusiwe kuingia? Akauliza Innocent ..Naya hakumjibu kitu akachuma maembe mawili na kumpatia Innocent
“Twende upande wa pili wa kisiwa” akasema Naya.Wakaanza kutembea kuelekea upande wa pili wa kisiwa kile.Kila sehemu waliyopita ilikuwa na uzuri wa kipekee.
“Huyu Naya ni nani? Anaishi wapi? Mbona anaonekana kuyafahamu vyema maeneo haya? Kisiwa hiki kina siri gani kiasi kwamba hakuna mtu wa kawaida anayeweza kukiona wala kuruhusiwa kufika hapa? Nadhani kuna haja ya kukifahamu kiundani kisiwa hiki na kwa nini nina muunganiko nacho kama anavyosema Naya.Hisia zinakuja ni kama nimewahi kuwa na urafiki na msichana mmoja mrembo kama huyu Naya.” Akawaza Innocent wakati wakipanda kilima

ENDELEA……………………….

“Ni kweli kumbu kumbu fulani zinakuja kwamba niliwahi kuwa na urafiki na msichana mmoja lakini simkumbuki ni nani na wapi.Ouh Mungu wangu nisaidie niweze kuzirejesha kumbu kumbu zangu.Nahitaji kukumbuka mimi ni nani,nimetoka wapi, na kwa nini niko hapa.” Akawaza Innocent.Hisia kwamba aliwahi kuwa na urafiki na msichana mrembo zikaendelea kuutesa ubongo wake
Hatimaye wakafika juu ya kilima na ghafla Innocent akapatwa na mshangao mkubwa baada ya kuushuhudia uzuri wa ajabu uliokuwa upande wa pili wa kisiwa kile.
“Haya ni maajabu.Sijawahi kuona sehemu nzuri kama hii” akasema Inno
“Jumba lile unaloliona ni la Malkia mweusi” akasema Naya
“Anatoka wapi huyo malkia mweusi? Akauliza Innocent
“Malkia mweusi hana nchi.Yeye ni malkia wa dunia nzima.Alitakiwa kuwepo hapa katika jumba lake mida hii lakini alifaya makosa makubwa katika utawala wake makosa ambayo adhabu yake ni kifo”
“Alifanya makosa gani? Kwa nini awe ni malkia wa dunia? Mbona mimi sijawahi kumsikia huyo malkia wa dunia?
“Hata kama umewahi kumsikia lakini huwezi kumkumbuka tena.Kuhusu makosa aliyoyafanya hata mimi sifahamu”
“Umewahi kuonana na malkia mweusi? Akauliza Inno
“Ndiyo.Nimewahi kuonana naye.Ni mrembo mno.Ana uzuri wa ajabu sana” akasema Naya halafu akasita kama mtu anayekumbuka kitu .Innocent akamuangalia na kuuliza
“Nani wanaishi pale katika jumba lile malkia mweusi asipokuwepo?
“Jumba lile halikaliwi na mtu yeyote .Ni malkia mweusi pekee ambaye anaruhusiwa kukaa ndani ya lile jumba”
“Kuna nini ndani ya jumba lile kiasi kwamba haruhusiwi kuingia mtu mwingine ?
“Mimi sifahamu chochote kuhusiana na kilichomo mle ndani.Hakuna mtu mwingine zaidi ya malkia mweusi anayeruhusiwa kuingia mle ndani.” akajibu Naya
Innocent akalitazama jumba lile na kusema
“Nataka kuingia ndani ya lile jumba.Nataka kuona kilichomo ndani yake.” Akasema Innocent huku akiinua mguu tayari kwa kuanza kushuka kilima.Naya akamzuia
“Hapana usithubutu kufanya hivyo.Usithubutu kuingia ndani ya jumba lile” akasema Naya
“ kama hutaniambai kuna nini ndani ya ile nyumba ,mimi naenda kuangalia mwenyewe.Nataka nifahamu siri za kisiwa hiki na kwa nini nina muunganiko nacho kama unavyosema” akasema Innocent na kuanza kupiga hatua.Naya akamkimbilia na kumshika mkono.Mara akastuka ghafla kama kwamba ameona kitu ha kutisha sana.Innocent naye akastuka wakabaki wanatazamana.Naya alikuwa anahema haraka haraka
“Naya una tatizo gani? Akauliza Innocent.Midomo ya Naya ilikuwa inatetemeka.Alishindwa kuongea.Innocent akamsogelea karibu na kumuuliza
“ Naya una tatizo gani? Mbona umebadilika ghafla?
Naya akamtazama Innocent usoni halafu akauliza kwa sauti yenye kitetemeshi
“ Hiyo pete kidoleni umeipata wapi?
Innocent akastuka na kuinua kiganja cha mkono wa kushoto .Ni kweli alikuwa na pete ya dhahabu kidoleni.Picha moja ikapita kichwani kwake ghafla lakini akashindwa kutambua picha ile.Kuna kumbu kumbu ilikuwa inakuja na kupotea
“ Sikumbuki pete hii nimeipata wapi.Kwani ina nini? Akauliza Innocent.Naya akamshika mabegani na kusema
“Tafadhali naomba ujitahidi kukumbuka pete hii umeipata wapi? Ni muhumu sana kwangu na kwako pia”
“Sikumbuki kitu chochote Naya.Sikumbuki nimeipata wapi hii pete.” akajibu Innocent halafu akakumbuka kwamba alikuwa na msalaba shingoni.Akaupeleka mkono wake na kuushika na mara kumbu kumbu fulani ikaja na kupotea.Akastuka
“ Umekumbuka kitu chochote ? akauliza Naya
“ Kuna kumbu kumbu inakuja na kupotea” akajibu Inno
“Ouh jamani.Jitahidi ukumbuke.Kumbuka chochote kuhusiana na pete hii.Kuna mtu aliwahi kukupa pete hii? Ni nani ?
“Sikumbuki chochote Naya na wala sikumbuki kama kuna mtu aliwahi kunipa hii pete ingawa kuna kumbu kumbu inanijia na kutoweka..Hii medali nakumbuka kama….kama ..k….ouh sikumbuki tena chochote” akasema Inno na kuinama chini
“ Sikumbuki chochote kuhusu hii pete wala chochote kuhusiana na maisha yangu.Kwa nini Naya amestuka baada ya kuiona pete hii ? Pete hii ina nini? Ina mahusiano yoyote na mahala hapa? Akawaza Innocent halafu akainua kichwa na kumtazama Naya
“Naya naomba uniambie pete hii ina nini?Nahitaji kufahamu tafadhali ili kama ni ya hatari basi niitoe mara moja” akasema Inno.Naya akamshika mkono na kumketisha katika majani na kusema
“Unaiona pete hii katika kidole changu? Akauliza Naya
“Ndiyo.Mbona inafanana na hii ya kwangu?
“Hicho ndicho kitu ambacho nataka kukifahamu.Pete hizi mbili zina utofauti.Hii ya kwangu ina nyota yenye rangi ya bluu na hii ya kwako ina nyota yenye rangi nyekundu.Pete hizi hazivaliwi wala kupatikana kwa mtu ambaye hahusiki.Mtu wa kawaida haruhusiwi kuwa na pete hizi” akasema Naya
“Sijakuelewa Naya.Nini maana ya pete hizi? Zinatoka wapi? Kwa nini huvaliwa na watu maalum tu? Hao watu maalum ni akina nani?Wewe ni nani Naya? Pete hii imefikaje kidoleni kwangu? Innocent akauliza maswali mfufulizo.Naya akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mpaka pete hii imefika kidoleni mwako lazima utakuwa unafahamu mambo mengi makubwa” akasema Naya na kuzidi kumchanganya Innocent
“Naya sikumbuki kama ninafahamu chochote kuhusu pete hii” akasema Inno
“Ni kwa sababu umepoteza kumbu kumbu lakini kuna mambo mazito ambayo lazima umeyashuhudia” akasema Naya na kuushika msalaba ule shingoni kwa Inno
“Huu umekusaidia .Umekuokoa” akasema Naya
“Umeniokoaje? Akauliza Inno
“Ulitakiwa ufe lakini msalaba huu umekuokoa” Naya akazidi kumchanganya Innocent
“Nilitakiwa nife? Kwanini nife? Nani alitaka kuniua? Umefahamu vipi kama nilitakiwa kufa? Akauliza Inno kwa wasi wasi.Naya akamshika mkono na kusema
“Pete hii ulipewa na malkia mweusi.”
‘Mimi ?!! Innocent akashangaa
“Sifahamiani na huyo malkia mweusi na wala sijawahi kumuona na hajawahi kunivisha pete hii”akasema Inno.Naya akamuangalia halafu akatabasamu
“Hatimaye nimefanikiwa kukuona.Ni wewe !! “ akasema Naya huku akitabasamu halafu akamkumbatia Inno kwa nguvu
“Ouh ahsante Mungu.Nimefanikiwa kuonana na mkombozi wetu” akasema Naya huku machozi yakimtoka .Inno akashangaa
“Naya sikuelewi kwa haya maneno unayoyasema.Mimi nitakuwaje mkombozi wenu? Wewe na nani?
Naya hakujibu kitu akaendelea kufuta machozi
“Naya tafadhali naomba unieleze ukweli kuhusu maneno hayo unayoyasema.” Innocent akasisitiza.Naya akainama kwa sekunde kadhaa na kusema
“Nilikuwa na umri wa miaka kumi na miwili baba yangu aliponichukua na kunipeleka katika hekalu fulani ambako alinitoa sadaka.Nakumbuka tulikuwa watu wawili siku hiyo .Mimi na malkia mweusi.Baada ya ibada ile ya kutolewa sadaka nilichukuliwa na wazazi wangu na sikuelewa maana ya kutolewa sadaka.Nilipofikisha miaka kumi na minne,nililetwa katika kisiwa kitukufu kwa ajili ya kujifunza kuhusu maisha yetu na kujiandaa kwa ajili ya kuwa mrithi wa malkia mweusi.Nimeishi kisiwani kwa miaka kumi sasa.Nimejifunza mambo mengi .Nimeiva katika imani yetu na tayari nilitegemewa kumrithi malkia mweusi lakini sikuwa tayari kwa hilo.Niliamua kutoroka na badala yake nikaishia mikononi mwa wale wala watu.Safari yangu haikuwa ya bure kwani nimefanikiwa kukutana nawe mtu muhimu sana ambaye umekuwa ukisubiriwa na watu wengi kwa muda mrefu” akasema Naya
“Naya unazidi kunichanganya.Mimi nina umuhimu gani kwenu? Sielewi chochote Naya” akasema Inno
“Huwezi kuelewa Innocent kwa sababu kumbu kumbu zako hazitarudi kamwe hadi hapo utakapokuwa umekamilisha kazi unayotakiwa kuifanya”
“Kazi ninayotakiwa kuifanya? Ni kazi gani hiyo? Akashangaa Inno
“Unatakiwa ukamuokoe malkia mweusi ambaye muda wowote atauawa.Adhabu yake imeshatolewa lakini haiwezi kutekelezwa pasipokuwapo pete hii”
“ Yuko wapi malkia mweusi? Nitamuokoa vipi ? akauliza Inno
“Iko hivi” .akasema Naya halafu akamuangalia Inno aliyekuwa kimya akisikiliza kwa makini
“Kuna kitabu ambacho unatakiwa ukipate na uichane sura ya sita kati kati.Kitabu hicho kitukufu kimehifadhiwa katika pango lenye nyoka mkubwa na katika chumba kilimo kitabu hicho kuna moto mkali sana na kati kati ya huo moto kuna jiwe kubwa ambalo juu yake ndipo kipo kitabu hicho” akasema Naya na kumuogopesha Inno
“Hilo haliwezekani Naya.Siwezi kufanya kitu kama hicho.Sehemu hiyo haiingiliki hata kidogo na hakuna uwezekano wowote wa kukichukua kitabu hicho kitukufu.Nitawezaje kupambana na huyo nyoka mkubwa? Nitawezaje kuingia katika chumba chenye moto mkali? akasema Inno
“Lazima uende.Lazima umuokoe malkia mweusi na sisi sote na huo ndio utakuwa mwisho wao.” Akasema Naya huku ameukunja uso wake.Innocent akauliza
“ Naya kwa nini mimi nikaifanye kazi hiyo ya hatari na si mtu mwingine? “
“Kwa sababu wewe ndiye uliyechaguliwa.Wewe ndiye uliyepewa nguvu za kuwamaliza hawa watu”
“Nimechaguliwa na nani? Nguvu gani nilizonazo? Ni watu gani ambao natakiwa kuwamaliza? Akauliza Inno
“Ni hadithi ndefu sana lakini nina imani haya yote yalikwisha fanyika lakini hukumbuki chochote”
“Naya bado sijakuelewa vizuri.Nani huyo aliyenichagua? Amenifahamu vipi mimi? Akauliza Inno.Naya akamtazama na kusema

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 55
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kuna kitabu ambacho unatakiwa ukipate na uichane sura ya sita kati kati.Kitabu hicho kitukufu kimehifadhiwa katika pango lenye nyoka mkubwa na katika chumba kilimo kitabu hicho kuna moto mkali sana na kati kati ya huo moto kuna jiwe kubwa ambalo juu yake ndipo kipo kitabu hicho” akasema Naya na kumuogopesha Inno
“Hilo haliwezekani Naya.Siwezi kufanya kitu kama hicho.Sehemu hiyo haiingiliki hata kidogo na hakuna uwezekano wowote wa kukichukua kitabu hicho kitukufu.Nitawezaje kupambana na huyo nyoka mkubwa? Nitawezaje kuingia katika chumba chenye moto mkali? akasema Inno
“Lazima uende.Lazima umuokoe malkia mweusi na sisi sote na huo ndio utakuwa mwisho wao.” Akasema Naya huku ameukunja uso wake.Innocent akauliza
“ Naya kwa nini mimi nikaifanye kazi hiyo ya hatari na si mtu mwingine? “
“Kwa sababu wewe ndiye uliyechaguliwa.Wewe ndiye uliyepewa nguvu za kuwamaliza hawa watu”
“Nimechaguliwa na nani? Nguvu gani nilizonazo? Ni watu gani ambao natakiwa kuwamaliza? Akauliza Inno
“Ni hadithi ndefu sana lakini nina imani haya yote yalikwisha fanyika lakini hukumbuki chochote”
“Naya bado sijakuelewa vizuri.Nani huyo aliyenichagua? Amenifahamu vipi mimi? Akauliza Inno.Naya akamtazama na kusema

ENDELEA…………………..
“Sophie alikuwa bibi mzee ambaye naye alishi maisha yake yote katika imani hii.Hakuwahi kuufurahia usichana wake hata kidogo.Nilipoletwa huku kisiwani,kwa mafunzo Sophie alinipokea na akatokea kunipenda sana .,Alinionea huruma na hakutaka niishi maisha kama aliyoishi yeye.Siku zote alinisihi kwamba nisikubaliane na chochote kile watakachoniamuru nifanye.Alikuwa ndiye mtetezi wangu.Alinikingia kifua katika kila jambo.Kwa bahati mbaya Sophie alifariki.Alifia mikononi mwangu.Kabla hajafariki aliniita chumbani kwake na kunipa siri kubwa.Aliniambia kwamba siku moja nitakutana na mtu ambaye atatukomboa.Hakuniambia kwamba mtu huyo nitakunata naye wapi lakini aliniambia kwamba mtu huyo nitakayekutana naye tayari atakuwa amejazwa nguvu za kuweza kupambana na kutukomboa.Alinipa ishara tatu ambazo zingeniwezesha kumtambua mtu huyo na ishara mojawapo ni pete hii uliyoivaa.Hii ni pete yenye nguvu sana na nina hakika lazima kuna sababu nzito sana iliyomfanya malkia mweusi akaitoa kidoleni mwake na kukupa.Inawezekana mlikuwa katika mapenzi mazito na hivyo akaona ni vyema kama atakulinda “
“mapenzi ?!! Innocent akashanga
“Sijawahi kuwa katika mapenzi na mwanamke yeyote achilia mbali huyo malkia mweusi.” Akasema Innocent ghafla kumbukumbu fulani ikamjia na kupotea
“Kuna kitu umekumbuka? Akauliza Naya
“Kuna kumbukumbu inakuja na kutoweka.Sikumbuki chochote tena lakini kuna hisia ninaanza kuzipata ni kama niliwahi kuwa mapenzini na mtu fulani” akasema Inno
“Usijali.Kumbu kumbu zote zitarejea.Kitu kikubwa ambacho tunatakiwa kukifanya sasa ni kwenda katika kituo cha kwanza alichonielekeza Sophie.Sehemu hii na zote tutakazozipitia ni za hatari lakini hatuna budi kwenda” akasema Naya.Innocent hakujibu kitu akabaki amesimama akitafakari
“Uko tayari kwenda? Unahitaji kuzirejesha kumbu kumbu zako? Akauliza Naya
“Niko tayari Naya japokuwa sielewi nitaiwezaje kazi hii ngumu “
“ahsante .Umefanya maamuzi ya busara na kwa maamuzi hayo utatukomboa sisi sote.Twende tuondoke” akasema Naya na kumshika mkono Innocent wakaanza kushuka kilima kuelekea ufukweni hadi mahala walikoiacha boti waliyokuja nayo.
“Tunaeleka wapi? Akauliza Innocent
“katika kituo cha kwanza kama alivyonielekeza Sophie”
Safari ikaanza na Naya alionekana kuyafahamu vyema mazingira yale ya bahari.Kadiri walvyozidi kusonga mbele ndivyo hali ya bahari ilivyozidi kuchafuka.Innocent akaogopa
“Naya hatuwezi kwenda zaidi ya hapa.Geuza boti turudi.bahari imechafuka na tunaweza kupoteza maisha.Twende turudi tulikotoka” akasema Inno
“Hatuwezi kurudi.Vyovyote itakavyokuwa lazima tusonge mbele.Hatuwezi kurudi nyuma.” Akasema Naya kwa ukali.Boti ile iliendelea kuchana mawimbi makubwa .Upepo mkali na ngurumo vikatawala bahari.Hali ya bahari ilikuwa mbaya sana.
“Karibu tutafika.” Akasema Naya na kumpa moyo Inno ambaye alikuwa akiogopa
Dakika kumi baadae wakasili katika kisiwa kidogo.Mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na radi ilikuwa inanyesha.Innocent alikuwa anatetemeka mwili mzima kwa baridi kali aliyoisikia.Taratibu akaanza kukata tamaa ya kuendelea mbele
“Naya siwezi kuendelea tena zaidi ya hapa.Mwili wangu hauna nguvu hata kidogo” akasema Innocent na kuanguka chini
“Jitahidi .Tumeshafika ! Tafadhali usikate tamaa” akasema Naya.Mvua kubwa ikaendelea kunyesha.Alimshika mkono Innocent aliyekuwa ameanguka pake chini kwa lengo la kumnyanyua lakini ghafla akasukumwa na kitu kama upepo mkali na kuanguka katika jiwe.Alijilaza pale juu ya jiwe huku akisikia maumivu makali .Mvua kubwa iliendea kunyesha pamoja ngurumo za kutisha za radi
“lazima nimfikishe ndani.Lazima atukomboe” akawaza Naya halafu akainuka huku akipepesuka kutoka na upepo mkali na kumfuata Innocent. Akajaribu kunyanyua lakini akashindwa.Hakukata tamaa akaanza kumvuta huku akisukumwa na upepo mkali
Hatimaye Naya akafanikiwa kumfikisha Innocent katika pango.Ndani ya pango lile kulikuwa na mwanga na joto kali tofauti na nje kulikokuwa na baridi kali mno.Mbele kabisa ya pango lile kulikuwa na jiwe mfano wa meza ndogo ambalo juu yake kulikuwa na kitu fulani chenye umbo la duara mfano wa tufe ambalo lilikuwa linatoa mwanga ule mkali.Naya akazidi kupata nguvu na kumvuta Innocent hadi katika lile jiwe mfano wa meza.Akauinua mkono wa Innocent uliokuwa na ile pete halafu akauweka katika lile tufe lenye kutoa mwanga mkali
Mara tu mkono wa Innocent ulipowekwa juu ya lile tufe,radi kubwa ikapiga na kisiwa chote kikatikisika.Pete ile ya Innocent ikaanza kutoa mwanga mwekundu na mara mwili wa Innocent ambao ulikuwa dhaifu sana ukapatwa na nguvu za ghafla.Ngurumo za radi zikaendelea kusikika na ghafla kitu cha ajabu kikamtokea.Mbele yake alisimama mzee mmoja mwenye ndevu nyingi na aliyevaa nguo ndefu nyeupe na kujifunga mshipi mwekundu kiuononi.Mkononi mwake alikuwa ameshika ubao wenye maandishi.Akamtaka Innocent ayasome maandishi yale.Mara tu alipomaliza kuyasoma maandishi yale kumbukumbu fulani ikamjia.Alikumbuka aliwahi kumuona mahala mzee yule.Wakati akijaribu kutaka kukumbuka mahala alikomuona yule mzee,lile jiwe ambalo juu yake kulikiwa na tufe alilokuwa ameliwekea mkono likaanza kutikisika halafu ,likafunguka.Naya aliogopa sana kwa mambo aliyoyaona mle pangoni
Mara mtetemeko ule ukakoma Innocent ambaye tayari alikwisha rejewa na nguvu akalitazama jiwe lile lililofunguka.Ndani yake kulikuwa na upanga wenye kumeremeta.Wakati anaendelea kuushangaa upanga ule ,mara mbele yake akasimama tena yule mzee mwenye ndevu nyingi
“Chukua huo upanga.Nenda sasa kamuokoe Latoya” akasema yule mzee na kutoweka.
“Latoya!!....? Latoya ..?!! Jina hili si geni kwangu.Nakumbuka ni jina ambalo nimezoea kulitamka.Latoya ni nani ambaye natakiwa kumuokoa? Innocent akajiuliza na kukosa majibu.Taratibu akainama na kuushika upanga ule kwa mikono yake.Mara tu alipousika ule upanga vitu kama chaji za umeme vikamuingia mwilini na kupiga ukekele mkubwa.Baada ya dakika tano akajisikia mzima .Huku akiwa na upanga wake mkononi Innocent akageuka na kumtazama Naya aliyekuwa amejikunyata kwa uoga katika pembe moja ya pango
“twende tuondoke” akasema Inocent
“Nipeleke sehemu ya pili”
Naya akamtazama Innocent akataka usema kitu lakini kabla hajatamka chochote kukatokea tetemeko kubwa.Mawe yakaanza kuporomoka
“Twende tuondoke humu haraka” akasema Innocent na kwa kasi akamshika Naya mkono wakaanza kukimbia kutoka ndani ya lile pango huku mawe yakiendelea kuporomoka nyuma yao.Walifanikiwa kutoka salama ndani ya pango lile na.Bado mvua iliendea kunyesha ikiambata na upepo mkali ngurumo na tetemeko.Miti na mawe vikaendelea kuanguka kutokana na mtikisiko ule mkubwa. Wakaingia katika boti yao na kuanza kuondoka kwa kasi
“Tazama nyuma” akasema Naya wakati wakiendelea na safari .Inno akageuza kichwa na kutazama nyuma.Kisiwa kilikuwa kinazama.
“Ouh Mungu wangu .Haya ni maajabu.Sijawahi kuona mambo ya ajabu kama haya” akasema Inno.Hakuwahi kushuhudia kitu cha namna ile katika maisha yake.Aliogopa sana
Naya aliendelea kuendesha boti ile kwa kasi kubwa.Kwa sasa hali ya bahari ilizidi kuwa mbaya na wingu zito jeusi lilitanda na kupafanya baharini kuwe na kiza.Mawimbi makubwa yalitokea na upepo mkali ukaendelea kuvuma.Ilikuwa ni hali ya kutisha sana .
“ Nashindwa kuona tunakoelekea.Hali imekuwa mbaya sana” akasema Naya.Innocent akamkumbuka yule mzee mwenye ndevu nyingi halafu kumbukumbu fulani ikamjia ghafla.Alimuona mzee yule akimuelekeza maneno fulani na kumwambia ayatamke pale anapokuwa katika matatizo.Inno akayakumbuka maneno yale na kuyatamka na mara tu alipomaliza kuyatamka pete aliyovaa ikaanza kutoa mwangaza mkubwa.Naya akatabasamu na safari ikaendelea kwani aliweza kuona walikokuwa wakielekea.
Kwa mbali waliona kitu mithili ya moto
“Pale ndipo tunalekea” akasema Naya kwa uoga
“Mbona kama kunawaka moto ? akauliza Inno
“Kisiwa kile huwa kimezungukwa na moto unaowaka masaa yote.Ni sehemu ambayo hakuna mtu wa kawaida anaweza kufika wala kupaona.Pale ndipo kinahifahiwa kitabu kitukufu” akasema Naya.Innocent akastuka sana
Kadiri walivyozidi kukikaribia kisiwa ndivyo joto lilivyozidi kuongezeka.hata maji nayo yalianza kuwa ya moto.
“ Hapa lazima tufanye kitu.Hatuwezi kuingia salama pale kisiwani” akasema Innocent.Naya hakujibu kitu akabaki anamtazama Inno.Innocent akayatamka kimya kimya maneno yale ambayo aliambiwa ayatamke mara apatapo shida na mara tu alipomaliza kuyatamka ,upepo mkali ukavuma na kusababisha mawimbi makubwa kutokea
“Ee Mungu wangu naomba utulinde na hali hii ya kutisha.Sijawahi katika maisha yangu kushuhudia mambo ya kutisha kama haya” Innocent akaomba kimya kimya akiwa ameushikilia msalaba aliouvaa shingoni.Ghafla likatokea wimbi kubwa mfano wa mlima na kuwafunika kukawa na kiza kinene .


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………….
 
BEFORE I DIE
SEHEMU YA 56
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kwa mbali waliona kitu mithili ya moto
“Pale ndipo tunalekea” akasema Naya kwa uoga
“Mbona kama kunawaka moto ? akauliza Inno
“Kisiwa kile huwa kimezungukwa na moto unaowaka masaa yote.Ni sehemu ambayo hakuna mtu wa kawaida anaweza kufika wala kupaona.Pale ndipo kinahifahiwa kitabu kitukufu” akasema Naya.Innocent akastuka sana
Kadiri walivyozidi kukikaribia kisiwa ndivyo joto lilivyozidi kuongezeka.hata maji nayo yalianza kuwa ya moto.
“ Hapa lazima tufanye kitu.Hatuwezi kuingia salama pale kisiwani” akasema Innocent.Naya hakujibu kitu akabaki anamtazama Inno.Innocent akayatamka kimya kimya maneno yale ambayo aliambiwa ayatamke mara apatapo shida na mara tu alipomaliza kuyatamka ,upepo mkali ukavuma na kusababisha mawimbi makubwa kutokea
“Ee Mungu wangu naomba utulinde na hali hii ya kutisha.Sijawahi katika maisha yangu kushuhudia mambo ya kutisha kama haya” Innocent akaomba kimya kimya akiwa ameushikilia msalaba aliouvaa shingoni.Ghafla likatokea wimbi kubwa mfano wa mlima na kuwafunika kukawa na kiza kinene .


ENDELEA………………………..

Taratibu Innocent akafumbua macho na kujikuta wakiwa walelala juu ya jiwe.Tayari walikuwa ndani ya kisiwa kile chenye kuzungukwa na moto mkali.Pembeni yakealikuwa amelala Naya
“Naya !! Naya!! “ Inno akamuamsha Naya akafumbua macho na kushangaa.
“Tuko salama? Akauliza
“Ndiyo Naya.Tuko salama.Wimbi lile kubwa limetuvusha katika moto ule mkali.Haya ni mambo ya ajabu mno.” akasema Innocent.Naya akainuka na kukaa akaangaza angaza pande zote na kusema
“Sasa unatakiwa uendelee na kazi iliyotuleta hapa” akasema Naya huku akiinuka na kuangaza huku na huko
“Ndani ya pango lile unaloliona ndimo kinamokaa kitabu kitukufu.Unatakiwa uingie humo ndani ukakichukue.Si kazi rahisi lakini unatakiwa upambane hadi ukipate kitabu hicho.Endapo utashindwa kukipata basi sisi sote na malkia mweusi tutaangamia” akasema Naya
Innocent akautazama mlango wa pango lile,mwili ukamtetemeka
“Usiogope ! nenda.Mimi niko hapa nje.Nitakusubiri hapa.Siwezi kuingia mle kwani sina kinga ya kunilinda na pango hili” akasema Naya.Inno akavuta pumzi ndefu na kumkumbatia Naya halafu akaanza kupiga hatua kuelekea mlango wa pango.Joto lilikuwa kali na ile pete iliendelea kutoa mwanga.Hali ya bahari bado ilikuwa mbaya.Naya alimuangalia Innocent na kulengwa na machozi.Inno akaufikia mlango wa pango lile akasimama na kugeuka akamtazama Naya halafu huku mwili ukimtetemeka akaanza kuingia ndani kwa tahadhari kubwa.Ilikuwa ni sehemu yenye kutisha sana.
Baada ya hatua kama kumi hivi ghafla ule mwanga uliokuwa unatoka katika pete yake na kumuwezesha kuona ukazima na kukawa na kiza kizito.Innocent akastuka na kuogopa sana.Akasimama na kuushika vizuri upanga wake.Alitamani kurudi nyuma
“Hapana siwezi kurudi nyuma.lazima nimuokoe malkia mweusi ili kumbu kumbu zangu zirudi.Nitasonga mbele na kupambana” akasema Inno na kuanza kutembea kwa tahadhari kubwa.Ghafla akajikuta amefunikwa na kitu kama
Utando wa bui bui mwili mzima.Alishindwa kwenda mbele wala kurudi nyuma.Alikuwa amenasa
“Ouh Mungu wangu hiki kitu gani? akasema Innocent
“Natakiwa nifanye jitihada za kujiokoa ama sivyo nitakufa kabla hata ya kumaliza kazi yangu ya kumuokoa malkia mweusi na wenzake” akawaza Innocent na kuanza kuukata utando ule kwa kutumia upanga wake.Wakati akiendelea kujinasua mara akasikia sauti kama ya mvumo wa kitu.
“Nasikia sauti ya kitu kinakuja upande huu” akawaza Innocent na kuendelea kuukata utando ule na ghafla kikatokea kitu cha kutisha sana.Lilitokea joka kubwa sana ambalo hakuwahi kuliona katika maisha yake.Joka lile lilikuwa na macho makubwa yenye kutoa mwangaza mithili ya taa za gari.Lilikuwa tofauti na majoka mengine ambayo amewahi kuyaona .Innocent akatetemeka sana
“Mungu wangu naomba unisaidie.Niokoe na hii hatari” akasema Innocent kwa sauti.Nusura upanga alioushika umponyoke na kuanguka kutokana na woga aliokuwa nao.Aliendelea kulitazama joka lile huku akitetemeka mwili mzima.Taratibu joka lile likaanza kujiinua upande wa kichwani.Innocent akazidi kuogopa hakuwa na sehemu ya kukimbilia.Shingo ya joka lile ikaanza kutuna.Inno akang’amua kilichokuwa kinakwenda kutokea.Joka lile lilikuwa linajiandaa kurusha mate.
Kama alivyokuwa ametegemea joka ile lililokuwa na hasira kali likatema mate mengi na kikatokea kitu cha ajabu sana.Mate yale hayakumfika Innocent yalionekana kusukumwa na kitu kama vile ncha za sumaku zinavyosukumana.Joka lile likazidi kupandwa na hasira,likatema tena mate kwa mara ya pili na ya tatu lakini bado hayakumfika Innocent na yalikuwa yakianguka mita chache toka pale alipokuwa amesimama Innocent.Mate yale hayakuonekana kama mate ya kwaida ya nyoka.Yalionekana kama gundi.Joka liliendelea kusimamisha kichwa huku likiunguruma kwa sauti ya kutisha .Innocent akapata wazo.Akauchomeka upanga wake katika mate ya lile joka na kwa kutumia upanga akayarusha mate yale yaliyokuwa yameganda kama gundi kulielekea joka na ghafla joka likabadilika baada ya mate yale kulipata.Lilianza kujigeuza huku na huko kana kwamba linaungua .Innocent akaendelea kulirushia mate yale na joka likaendelea kutoa muungurumo mkubwa huku likijigeuza
Wakati joka lile likijipundua na kuhangaika Innocent akanyata kwa lengo la kwenda kupambana nalo na mara ikatokea tafrani kubwa kati yake na joka.Katika purukushani ile ya kupambana na joka lililokuwa na ngozi ngumu mithili ya mamba Innocent akaanguka chini.Joka lile likainua kichwa chake kwa lengo la kumgonga Innocent kichwani lakini kwa kasi ya aina yake Inno akawahi kujigeuza na kupenya katika uwazi mdogo wa pembeni na kulipita joka lile.Sehemu ya nyuma ya joka lile kulikuwa na pete yenye kutoa mwangaza.Joka lile likauinua mkia wake kwa ajili ya kumchapa nao Innocent lakini akaliwahi kwa pigo moja lenye nguvu na kipande cha nyuma kabisa cha mkiani chenye ile pete yenye kutoa mwanga kikaanguka chini.Baada ya kipande kile kudondoka chini ukaanza kuwaka moto.Innocent akawahi kuuruka moto ule na kwa sasa akawa amepata upenyo wa kusonga mbele .Kwa haraka akaanza kukimbia.Kadiri alivyozidi kwenda mbele ndivyo alivyozidi kukutana na joto kali na hatimaye akakutana na moto mkali uliokuwa ukiwaka kulizunguka jiwe .
“Kwa mujibu wa maelekezo ya Naya nadhani hii ndiyo sehemu ile aliyosema kwamba kitabu hicho ninachotakiwa kukipata kinakaa.Sijui nitawezaje kuuvuka huu moto na kukiendea kitabu.Nimekwama tena” akawaza Innocent wakati akiendelea kuumiza kichwa angewezaje kuuvuka moto ule na kwenda hadi katikati ya jiwe lile na kukichukua kitabu ,mara akaisikia zauti za mvumo kama ule wa mwanzo
“Linakuja tena…Lile joka linakuja tena.Nitafanya nini? Akasema Innocent kwa wasi wasi.Hakukuwa na sehemu ya kujificha
Kufumba na kufumbua akaliona joka lile likija kwa kasi ya ajabu.Macho yake ambayo awali yalikuwa yakitoa mwanga mweupe sasa yalikuwa yanatoa mwanga mwekundu
“Munu wangu niokoe !” akasema Innocent kwa woga akilishuhudia namna joka lile lilivyokuwa linakuja likiwa na hasira zisizomithilika.
Lilipomkaribia Inno joka lile lilisimamisha kichwa huku likitoa muungurumo.Inno hakuwa na njia nyingine na kufanya zaidi ya kujiandaa kukabiliana nalo.Aliushika upanga kwa mkono wake wa kulia.Joka lile likaruka kwa dhumuni la kumvamia Innocent.Likiwa bado hewani,Inocent kwa nguvu zake zote zlizokuwa nazo akalipiga joka lile na kulikata vipande viwili.Upande wa kichwani ukaanguka katika ule moto unaowaka na kipande kingine kikamgonga Innocent na kumuangusha chini.Alihisi ni kama amepigwa na jiwe zito
Ilimchukua zaidi ya dakika tano kuweza kukisukuma kipande kile cha joka kilichokuwa kimemkandamiza pale chini.Baada ya kulisukuma pembeni joka lile ambalo bado liliendelea kujinyonga nyonga japokuwa lilikwisha katwa kichwa Innocent akasimama na kulishangaa joka lile.Lilikuwa ni joka la kutisha mno.Kichwa chake kiliangukia katika moto na kuufanya uanze kuzimika.Upanga ule wa Innocent ulikuwa umevunjika vipande viwili.Hakuamini kama alikuwa amefanikiwa kuliua joka lile kutokana na ukubwa wake.
“Ouh ahsante Mungu.” Akasema Innocent huku akivuta pumzi ndefu.Ghafla kukaanza kuwa na giza.Moto uliokuwa unawaka ilianza kuzimika.Juu ya jiwe lililokuwa likizungukwa na ule moto kulikuwa na kasha la dhahabu.Kwa kasi ya aina yake Innocent akalinyakua kasha lile.Chini ya kisanduku kile kulikuwa na ufunguo Inno akaunyakua na kuanza kuondoka akipita katika kiza totoro.Hakuweza kuona mahala alikokuwa anakwenda kitu kilichomfanya ajigonge katika majabali na kutokwa na damu nyingi .
Aliendelea kuambaa ambaa na kingo za pango lile lenye kiza huku akiendelea kusikia muungurumo wa radi na pango kutikisika.Mara kwa mbali akaanza kuona mwangaza wa radi.Akafarijika baada ya kugundua kwamba alikuwa anakaribia kutoka nje ya pango lile.Aliendelea kujikongoja kutoka nje huku mtikisiko ukizidi.Hatimaye akafanikiwa kutoka nje ya lile pango.
“ahsante Mungu” akasema Innocent huku akivuta pumzi ndefu.Ule moto uliokuwa ukiwaka kukizunguka kisiwa ulikuwa umezima.
“Naya..! Naya..!!! akaita Inno lakini hakujibiwa.Akaita tena kwa nguvu huku akielekea katika jiwe alilokuwa amemuacha Naya,akapatwa na mstuko mkubwa
“Naya hayupo..!!
Inno akaendelea kumuita Naya kwa nguvu lakini hakujibiwa.Ghafla ikawaka radi iliyotoa mwangaza mkali uliomulika kisiwa chote na mara akawaona watu wanne wenye mavazi meusi wakiwa wamemfunga kamba Naya na kumlaza juu ya jiwe na mmoja wao alikuwa na upanga mkononi akijiandaa kumkata kichwa.
“ heeeeeeyyyyyyyyyyyyyyy……….!!!!!!!!!...” akapiga ukulele mkubwa Innocent na kuwastua watu wale ambao waliruka majini.Inno akamkimbilia Naya akamfungua kamba.Naya alikuwa ameumizwa vibaya sana.Damu nyingi ilikuwa inamtoka
“Pole sana Naya.watu wale ni akina nani? Wametoka wapi na kwa nini walikufunga namna hii? Inno akamuuliza Naya.Kwa taabu Naya akajibu
“Ahsante kwa kuniokoa.Watu wale walifahamu kwamba tumekuja huku na mara moja wakafika hapa haraka kutudhibiti.Umekipata kitabu?
“ Ndiyo nimekipata.” Akasema Innocent .Naya akafurahi na kumkumbatia Innocent kwa nguvu.Radi kubwa ikapiga na kuwastua
“Kuna boti wamekuja nayo watu hawa.Tuitumie hiyo tuondoke nayo.Hatuna muda tena wa kupoteza .Ni wakati wa kuwamaliza” Akasema Naya kisha wakarukia katika boti waliyokuja nayo wale jamaa waliojirusha majini.Naya akaiwasha wakaondoka.Ule moto uliokuwa ukiwaka kukizunguka kisiwa ulikwisha zimika.
“ watu wale ni akina nani? Akauliza Innocent
“Watu wale ni walinzi wa kisiwa hiki.Hawakuwepo wakati tunafika walikuwa wamekwenda kushuhudia kifo cha malkia mweusi na kushuhudia kusimikwa kwa mfalme mpya Brandon ambaye ndiye alipangwa anioe siku ya leo.Hii ni sababu iliyonifanya nikakimbia .Sikuwa tayari kuolewa na mtu nisiyempenda na zaidi sana mfuasi wa imani hii.” Akasema Naya
“Umesema Brandon? Akauliza Innocent
“Ndiyo.Brandon.Huyu ndiye kijana atakayesimikwa kuwa mfalme siku ya leo baada ya kifo cha malkia mweusi.Mbona umestuka kusikia jina hilo?
“Jina hilo si geni kwangu Ni kama nimewahi kulisikia mahala fulani.”

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 57
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Kuna boti wamekuja nayo watu hawa.Tuitumie hiyo tuondoke nayo.Hatuna muda tena wa kupoteza .Ni wakati wa kuwamaliza” Akasema Naya kisha wakarukia katika boti waliyokuja nayo wale jamaa waliojirusha majini.Naya akaiwasha wakaondoka.Ule moto uliokuwa ukiwaka kukizunguka kisiwa ulikwisha zimika.
“ watu wale ni akina nani? Akauliza Innocent
“Watu wale ni walinzi wa kisiwa hiki.Hawakuwepo wakati tunafika walikuwa wamekwenda kushuhudia kifo cha malkia mweusi na kushuhudia kusimikwa kwa mfalme mpya Brandon ambaye ndiye alipangwa anioe siku ya leo.Hii ni sababu iliyonifanya nikakimbia .Sikuwa tayari kuolewa na mtu nisiyempenda na zaidi sana mfuasi wa imani hii.” Akasema Naya
“Umesema Brandon? Akauliza Innocent
“Ndiyo.Brandon.Huyu ndiye kijana atakayesimikwa kuwa mfalme siku ya leo baada ya kifo cha malkia mweusi.Mbona umestuka kusikia jina hilo?
“Jina hilo si geni kwangu Ni kama nimewahi kulisikia mahala fulani.”

ENDELEA……………………….

“kama ulikuwa karibu na malkia mweusi basi ni lazima utakuwa umelisikia jina hili likitajwa au hata kumuona huyo Brandon mwenyewe.” akasema Naya
Nina hamu sana ya kumuona huyo malkia mweusi ambaye unasema kwamba ninafahamiana naye.Pengine kumbu kumbu zangu zitanirudia baada ya kumuona lakini sina hakika kama ninamfahamu au nimewahi kuonana naye.” Akasema Innocent huku akiiangalia ile pete yake ambayo ilianza kutoa nuru tena
“Pete hii ina maajabu sana .Nilipokuwa kule pangoni iliacha kutoa nuru lakini ghafla imeanza tena kutoa mwanga.” Akasema Innocent.Naya akavuta pumzi ndefu na kusema
“Kuzima kwa pete hii kuna maanisha kwamba nguvu ya malkia mweusi imefika ukomo.Kwa hiyo tunatakiwa kuwahi kumuokoa” akasema Naya
“kwa hiyo malkia mweusi tayari ameuawa? Akauliza Innocent
“hapana bado hajauawa.Hawawezi kumuua bila kuipata pete hii kwanza.Kabla hajauawa ni lazima avuliwe pete hii na avishwe mtu mwingine ambaye ndiye atakaye mkata kichwa na mrithi wake anywe damu yake na kisha humpasua kifua na kuutafuna moyo wake.Haya yote atafanyiwa malkia mweusi na wale wote walioasi kama mimi.Wale jamaa waliojitosa majini walikuwa tayari kunichinja na kisha moyo na damu yangu vingeletwa huku.Nashukuru uliwahi kutokea na kuniokoa” akasema Naya
“Malkia mweusi alifanya nini hadi apewe adhabu kali namna hii? Akauliza Inno
“Alikwenda kinyume na masharti aliyopewa.” Akasema Naya na safari ikaendelea kimya kimya
“Unaona mwanga ule? Akasema Naya akionyeshea mwanga ulioonekana kwa mbali.
“Ndiyo ninaona mwanga kwa mbali sana “ akasema Inno
“Pale ndipo tunapoelekea” akasema Naya
Walizidi kukisogelea kisiwa kile na mara Innocent akaanza kuhisi kitu kama baridi kali
“Tukifika pale usifanye jambo lolote bila ya maelekezo yangu.Utafanya kile tu nitakachokuamuru ufanye.Ukienda kinyume utaharibu mambo na utatuangamiza sote” akasema Naya
“Usihofu Naya,nitafanya kama utakavyonielekeza” akajibu Inno
Walikikaribia sana kisiwa ambacho kilikuwa na mwangaza mkubwa uliotoka katika kitu mfano wa nyota kubwa iliyokuwa ikielea juu ya kisiwa kile..Umbali wa kama mita mia moja hivi Naya akazima ile boti. Kukizunguka kisiwa kile hali ya bahari ilikuwa shwari kabisa tofauti na huko walikotoka.Hakukuwa na mawimbi wala tufani.Kwa mbali waliweza kushuhudia kundi la watu wakiwa na mienge ya moto wakiwa wamejipanga ufukweni.
“Umewaona watu wale? Wanasubiri kitabu hiki kitukufu.Kazi yetu inaanzia hapo.Kichukue kitabu na kishike mkononi” akasema Naya.Innocent akafungua lile kasha akatoa kitabu ambacho kilikuwa na maandishi ya dhahabu akakishika mkononi na kumtazama Naya ambaye alikuwa ameyaelekeza macho yake ufukweni lilikosimama lile kundi la watu
“Fungua kitabu ukurasa wa pili” akasema Naya.Innocent akafungua kitabu kile ukurasa wa pili .Ulikuwa ni ukurasa wenye rangi nyeupe na maandishi ya dhahabu
“Soma aya ya kwanza kama ilivyoandikwa” akasema Naya
“Hangot mo pa kala misha bivince saga molakan hepes ka d….” ghafla ikapiga radi kubwa na kukitikisa kisiwa chote.Innocet akaogopa na kuacha kusoma.Alikuwa anatetemeka
“Endelea kusoma” akasema Naya huku akiuelekeza mkono wake wa kushoto upande ule waliokuwa wamesimama wale watu
“ Endak has mo kajiun he sinamok pa kohads”
Alipomaliza kuisoma sentensi ile kisiwa kikanza kitikisika.wale watu waliokuwa wamesimama wakiwa na mienge mikononi wakaitupa mienge yao na kuanza kukimbia.Upepo mkali ukaanza kuvuma
“Endelea kusoma” akasema Naya
‘Hengek ka mapakal ho kumulap tas en epoh lengi kamapokah ende kas kajung”
Ghafla kukatokea mwako wa radi na kumbu kumbu Fulani ikamjia Innocent.Alikumbuka akiwa amesimama na msichana mmoja katika ufukwe wa bahari alikuwa ni msichana mwenye uzuri usioelezeka.

“Latoya you have everything In life but you are not happy.If there is anything that I can do to make you happy please let me know.Niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa lengo moja tu .Only to make you happy” maneno haya alikuwa anayatamka yeye Innocent na halafu yule msichana mzuri akajibu
“what a sweet words Innocent.Sijawahi kutamkiwa maneno matamu na mazito kama haya.”

Innocent akastuka
“Naitwa Innocent.Jina langu ni Innocent.Nimekumbuka jina langu.Naitwa Innocent.Latoya..! Latoya ..! yule msichana anaitwa Latoya” Innocent akakumbuka na kutabasamu .Alipatwa na furaha ya ajabu baada ya kumbu kumbu kuanza kumrejea
“Mbona umenyamaza? Kuna kitu umekumbuka? Akauliza Naya
“Nimekumbka jina langu.Nimemuona pia msichana mmoja anaitwa Latoya.”akasema Innocent
“Endelea kusoma aya inayofuata” akasema Naya
“tes gak hang ka mapak hang de pans he dahk keshwa dis kang han la mapak…” ghafla kumbukumbu nyingine ikamjia yeye na Latoya wakiwa wameketi katika bustani yenye maua mengi mazuri.Latoya alikuwa anamvisha pete kidoleni

“Innocent nakupatia pete hii, ambayo ni muhimu sana kwangu na ninaipenda sana.Kila utakapoivaa pete hii,basi utanikumbuka na ninakuomba usiivue pete hii”

alisema Latoya.Innocent akaitazama pete ile kidoleni mwake na mara picha mbali mbali zikaanza kumjia toka mara ya kwanza alipoonana na Latoya hadi walipokuwa melini.Akakumbuka wakiwa melini yeye na Latoya na ndipo walipopigwa na dhroruba na meli ikayumba.Alikumbuka kuna kitu Latoya alitaka kumweleza lakini kila alipojaribu kusema alishidwa kutokana na dhoruba kubwa.Picha ya mwisho iliyomjia kchwani ni maneno ya mwisho aliyoyatamka Latoya

“Innocent sikiliza ,you haveto know that I lov……” hakumalizia alichotaka kukisema ikapiga radi kubwa na kumbu kumbu zikaishia hapo.
“Ouh Latoya ..!! Latoya…!!!!” I must save her” akasema Innocent
Naya akawasha boti na kuanza kuipeleka ufukweni ambako hakukuwa na mtu baada ya watu wale waliokuwa wamejipanga kukimbia na kuitupa mienge yao ya moto.Wakashuka katika boti na kuokota mienge miwili iliyotupwa na wale watu
“ Fungua ukurasa wa tano” akaamuru Naya
“ Soma aya ya tatu”
“ Hangap ka mapak ala si mu kupat alti akam mapak di ne derok…..” alipomaliza kuisoma aya ile ghafla vikaanza kuanguka vitu mithili ya vimondo vyenye kuwaka moto na kila vilipoanguka vilikuwa vinalipuka.Sauti za watu zikasikika wakipiga kelele za kuungua
“ Soma aya inayofuata” akasema Naya
“Hang akom dim as kamapak di hades hadik mangak ahn hem asak” alipomaliza kusoma aya hii ,vile vimondo vikakoma kuanguka lakini moto uliendelea kuwaka
“Katika kitabu hicho chana sura nzima ya kumi na moja na uihifadhi ” akasema Naya.Bila kupoteza muda Innocet akachana kurasa nne zilizounda aya ya kumi na moja na kuziweka mfukoni.
“Nifuate “ akaamuru Naya na kuanza kukimbia wakivuka mioto ya vimondo iliyokuwa bado inawaka.
“Niliahidi kumuokoa Latoya .lazima nimuokoe.Ouh masikini Latoya..lazima nikupate leo,lazima nikuokoe” akasema Innocent lakini ghafla Naya akaanguka chini
“ Naya ..!! Naya..!1” akaita Innocent huku akimuinamia ili kujua kilchompata lakini ghafla akasikia sauti kubwa ikimuita.Ni sauti ambayo aliwahi kuisikia mahala Fulani.Akastuka na kugeuka
“Innocent come here !!!!!!!..I ikasema tena sauti ile ambayo Innocent hakujua ilitokea wapi.Ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume.Innocent ambaye alikuwa amepiga magoti pembeni ya Naya akainuka.Umbali wa kama mia hamsini hivi akamuona mtu ambaye alimfahamu vizuri
“ Brandon !!!!!!!.. akasema Innocent kwa mshangao
Pembeni ya Brandon katika madhabahu iliyojengwa kwa mawe meupe alilala msichana mmoja ambaye alionekana kutokuwa na fahamu huku damu ikimchuruzika mdomoni.Innocent akamtambua msichana yule
“Latoya ..!!!!!! “ akasema Innocent
“Ouh Latoya !!!!!!” akasema tena Inno huku akipiga hatua kumuendea.
“Toka mwanzo nilimuonya Latoya kuhusu wewe.Nilifahamu wewe ndiye adui yetu mkubwa .Innocent wewe ndiye unayemuangamiza Latoya kwa ujinga wako.Toka awali nilikukanya uachane na Latoya kwa sababu hamuwezi kuwa wapenzi lakini ukapuuzia.Kwa sababu yako Latoya amekiuka maagizo na adhabu yake ni kifo.Ninafurahi umekuja .Haya ni makao yetu makuu na ni hapa utakaposhuhudia kifo cha Latoya.Kitu ninachokuomba kwa sasa naomba unipatie hiyo pete uliyovaa kidoleni pamoja na hicho kitabu.Ni kwa kunipa vitu hivyo viwili tu nitakuacha huru kwani vinginevyo na wewe pia lazima uuawe.Nitakuondolea adhabu ya kifo endapo utanikabidhi vitu hivyo ninavyovitaka” akasema Brandon.Mwili wa Innocent ulichemka kwa hasira.Alimtazama Latoya akiwa amelala pale juu ya madhabahu na damu ikimtoka mdomoni.Alionekana ni kama mfu
“aaaaghhhh…!!!!!!” akapiga ukelele Inno huku akikimbia na kutaka kumvamia Brandon.Huku akicheka Brandon akaunyoosha mkono wake uliokuwa umeshika kitu kama tufe dogo lenye kutoa miale na Innocent akasukumwa na miale ile yenye nguvu na kuanguka kwa kishindo.
“ Innocent huna uwezo wa kupambana na mimi.Tafadhali naomba unipatie hivyo vitu haraka.Nipe hiyo pete na hicho kitabu nakuahidi sintakuua.Nitakuacha uende zako” akasema Brandon
“Damn you Brandon !! ..I’m going to kill you.!!!!” Akasema Innocent kwa hasira huku akijiinua pale chini alipoanguka
“Innocent ninakuomba kwa mara ya mwisho nipatie hivyo vitu.Kama kweli unampenda Latoya tafadhali naomba unipatie vitu hivyo ama sivyo nitamkata kichwa Latoya” akasema Brandon .Innocent hakuwa tayari kumkabidhi Brandon ile pete na kitabu .Brandon akachukua upanga na kumsogelea Latoya.
“Huyu bazazi haonyeshi kama anatania.Atamuua kweli Latoya.Ngoja nimpe hivi vitu anavyovitaka” akawaza Innocent na mara Brandon akainua upanga juu.
“ Brandon ..! “ akaita Innocent
“Usimuue Latoya nitakupatia hivyo vitu unavyovitaka” akasema Innocent
“Nipatie haraka kitabu na hiyo pete” akasema Brandon huku akimsogelea Innocent.Inno akaanza kuivua ile pete kidoleni
“Give it to me.I promise I’ll let you go” akasema Brandon
“Innocent ..!!!!!.” sauti ya Naya ikamuita na kumfanya ageuke
“Usithubutu kumpa hivyo vitu anavyotaka.Atatuua sote” akasema Naya aliyekuwa amesimama karibu na Innocent
“Fungua ukurasa wa saba na soma aya ya tatu” akaamuru Naya .Kwa haraka Inno akaufungua ukurasa wa saba na kuanza kuisoma aya aliyoambia .wakati akiisoma aya ile Brandon naye alikuwa amelishika lile tufe mkononi huku akiongea maneno ambayo Innocent hakuyaelewa.Ghafla lile tule alilokuwa amelishika Brandon likawaka moto na Brandon akalirusha kumuelekea Innocent.Naya alikiona kitendo kile na akamuamuru Inno aendelee kuisoma aya ya saba.Inno akaisoma kwa haraka haraka lakini kabla hajamliza tufe lile lililokuwa likiwaka moto likampiga akaanguka chini.Brandon akamsogelea na kumvua pete ile kidoleni halafu akakichukua kile kitabu.Mara tu alipoivua pete ile kidoleni ilianza kutoa mwangaza mweupe na Brandon akatabasamu.Innocent ambaye alihisi maumivu makali ya kuunguzwa na moto alijihisi mwepesi mno baada ya kuvuliwa pete ile.Brandon alikuwa anamuangalia kwa ghadhabu huku upanga wake ukiwa mkononi.
“Innocent umeingia katika himaya yetu,umeharibu utukufu wetu,umeua watu wetu, umesababisha nishindwe kumuoa Naya hii leo.Kwa haya yote uliyoyafanya unastahili adhabu ya kifo.Utakufa wewe na wale wote unaoshirikiana nao.Kwanza nataka ushuhudie kifo cha Latoya halafu Naya na mwisho ni wewe.” Akasema Brandon kwa hasira na kuanza kupiga hatua kuelekea katika madhabahu alikolala Latoya
“Innocent unazo zile karatasi ulizozichana za aya ya kumi na moja?
“Ndiyo Naya ninazo mfukoni.´” akajibu Innocent akiwa katika maumivu makali
“zichome moto” akasema naya
Kwa haraka Innocent akazitoa karatasi zile na kuvuta kijinga cha moto uliokuwa unawaka pembeni yake akazichoma
“ Brandon …!!! “ akaita Innocent.Brandon akageuka na kumuona Innocent akiwa amezishika karatasi zile zikiwaka moto.Mwili ukamtetemeka
“Innocent ..Nooooooooo!!!!!!!!!!!!..” akapiga ukeleel Brandon na kuanza kupiga hatua kumwendea Innocent lakini mara akaishiwa nguvu na kuanguka chini.Mara tu karatasi ya mwisho ilipomalizika kuungua na kuwa majivu kisiwa chote kikaanza kutikisika.Radi kubwa ikapiga.Pete ile aliyokuwa ameichukua Brandon ikalipuka mithili ya bomu na moto mkubwa ukatokea.Inno akarushwa na kuanguka chini kwa nguvu ya mlipuko ule.Mwili wa Brandon ulikuwa umesambaratishwa vipande vipande.Baada ya kama dakika tano Inno akajiinua na kushuhudia kilichotokea.
“Ouh my God…!!!” hakuamini macho yake namna mwili wa Brandon ulivyosambaratishwa.Mara macho yake yakatua kwa Latoya aliyekuwa bado amelala juu ya madhabahu. Akatembea kwa kasi na kwa tahadhari kumfuata
“Latoya..!!!!! Latoya..!!!!” akasema Innocent huku akmtingisha Latoya.Latoya hakuonekana kama bado ana uhai.Damu nyingi ilikuwa inamtoka mdomoni.
“Latoya ..!!!! Latoya ..!!! “ akaita Innocent kwa uchungu huku kisiwa kikiendelea kutikisika na mawe yakianguka.
“Latoya please don’t die.I’m here to save you.Its me Innocent..” akasema Innocent huku akimfungua kamba alizokuwa amefungwa na ghafla likatokea wimbi kubwa sana mithili ya mlima mkubwa na kukifunika kisiwa chote.Kukawa na kiza totoro.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 58
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Nipatie haraka kitabu na hiyo pete” akasema Brandon huku akimsogelea Innocent.Inno akaanza kuivua ile pete kidoleni
“Give it to me.I promise I’ll let you go” akasema Brandon
“Innocent ..!!!!!.” sauti ya Naya ikamuita na kumfanya ageuke
“Usithubutu kumpa hivyo vitu anavyotaka.Atatuua sote” akasema Naya aliyekuwa amesimama karibu na Innocent
“Fungua ukurasa wa saba na soma aya ya tatu” akaamuru Naya .Kwa haraka Inno akaufungua ukurasa wa saba na kuanza kuisoma aya aliyoambia .wakati akiisoma aya ile Brandon naye alikuwa amelishika lile tufe mkononi huku akiongea maneno ambayo Innocent hakuyaelewa.Ghafla lile tule alilokuwa amelishika Brandon likawaka moto na Brandon akalirusha kumuelekea Innocent.Naya alikiona kitendo kile na akamuamuru Inno aendelee kuisoma aya ya saba.Inno akaisoma kwa haraka haraka lakini kabla hajamliza tufe lile lililokuwa likiwaka moto likampiga akaanguka chini.Brandon akamsogelea na kumvua pete ile kidoleni halafu akakichukua kile kitabu.Mara tu alipoivua pete ile kidoleni ilianza kutoa mwangaza mweupe na Brandon akatabasamu.Innocent ambaye alihisi maumivu makali ya kuunguzwa na moto alijihisi mwepesi mno baada ya kuvuliwa pete ile.Brandon alikuwa anamuangalia kwa ghadhabu huku upanga wake ukiwa mkononi.


ENDELEA…………………………

Watu waliovaa mavazi meupe waliokuwa wamemzunguka ndicho kitu cha kwanza alichokutana nacho baada ya kufumbua macho.Macho yake bado hayakuwa na nguvu ya kuona vizuri.Watu wale waliomzunguka walikuwa wakiongea lakini hakufahamu walikuwa wanaongea nini kwa sababu alisikia kwa mbali sana.Alijaribu kunyanyua kichwa chake lakini kilikuwa kizito kana kwamba kimefungiwa jiwe.Kwa mbali akahisi kitu kama chenye ncha kali kikimchoma mkononi halafu macho yakawa mazito akalala
Baada ya masaa kadhaa kupita akafumbua macho na safari hii hayakuwa mazito kama pale awali.Aliweza kuona dari zuri lenye rangi nyeupe.Akageuza macho na kukutana na chupa ya maji iliyounganishwa katika mkono wake.Mara moja akagundua kwamba alikuwa hospitali
“Nimefikaje hapa?:Ninaumwa nini? Hii ni hospitali gani? Nani kanileta hapa? Akajiuliza Innocent huku akisikia mumivu makali ya ndani ya mwili.
“kwa nini niko hapa? Nini kimenitokea . Akajiuliza Innocent mara mlango ukafunguliwa na akaingia mwanamama mmoja aliyekuwa amevaa koti jeupe.Alipomuona Innocent ameamka na kukaa kitandani akatabamu na kumsogelea Innocent
“unajisikiaje? Akauliza yule mwanamama kwa kiingereza
“najisikia vizuri sana” akajibu Innocet
“naitwa Dr Catherine stalker.Nimefurahi kwamba umeamka na unaendelea vizuri.” Akasema Dr Catherine huku akiendelea kumpima Inno na kuandika katika faili
“Jina lako nani? Akauliza Dr Catherine
“ Innocent..naitwa Innocent”
‘Umetokea wapi? Wewe ni raia wa nchi gani?
“Mimi ni raia wa Tanzania.Hapa ni wapi? Tanzania? Akauliza Innocent
“Hapana Innocent hapa si Tanzania.Hapa ni Tully hospital Queens Island Australia.
“Australia? Innocent akastuka
“Ndiyo uko Queensland Australia”
“ Nimefikaje hapa? Nani kanileta hapa? Ninaumwa nini? Akauliza Innocent huku jasho likianza kumtoka
“Tulia Innocent.Usihofu.Uko salama na hakuna tatizo lolote” akasema Dr Catherine
“Dr Catherine naomba unieleze ninaumwa nini na nimefikaje hapa?
“Innocent uliletwa hapa ukiwa umepoteza fahamu.Leo ni siku ya nne toka umefika hapa ukiwa huna fahamu.Tumekufanyia uchunguzi mkubwa na hauna tatizo lolote” akasema Dr Catherine.Innocent akashangaa
“Nini kimesababisha nikapoteza fahamu? Hapa Australia nimefikaje? Nani kanileta hapa? Akauliza Innocent
“Uliletwa hapa na wanajeshi waliokuwa wakifanya doria baharini.Wanasema waliwaokoa toka katika meli iliyokuwa inawaka moto”
“ Meli ???!! Ino akauliza kwa mshangao
“Ndiyo..waliwaokoa toka katika meli inayosemekana kuwaka moto”
“ Waliniokoa mimi na nani?
“ wewe na mwenzako ambaye naye alikuwa amepoteza fahamu na amezinduka asubuhi ya leo na anaendelea vizuri.” Akasema Dr Catherine
” Huyu mwenzangu ni wa jinsia gani?
“ Ni mwanamke “ akajibu Dr Catherine
Ghafla kumbukumbu zikaanza kumrejea Innocent,akakumbuka tukio la mwisho kutokea.Alikuwa amemuinamia Latoya halafu likatokea wimbi kubwa na kuwafunika
“ Gosh ..Latoya !!!!” akasema Innocent
“ Yuko wapi Latoya? Akauliza Inno
“ Latoya ni nani? Akauliza Dr Catherine
“Huyo mwanamke niliyeletwa naye hapa hospitali yuko wapi nahitaji kumuona sasa hivi” akasema Innocent
“Tulia Innocent .Mwenzako ni mzima na anaendelea vizuri.Utamuona usijali lakini kwanza kuna watu ambao wanahitaji kuzungumza nawe” akasema Dr Catherine na kutoka nje ya kile chumba
“Ouh ahsante Mungu Latoya yuko hai .!!!! Nilijua tayari amekisha kufa.Nimetimiza ahadi yangu.I saved her.” Akasema Innocent kwa furaha.Akaanza kukumbuka mambo yote yaliyotokea kisiwani .
“Siamini kama ni mimi ndiye niliyekuwa napambana na mambo yale ya kutisha.Sikuwahi kuota kama siku moja ningeweza kukutana na mambo ya kutisha kama yale.Dunia hii kumbe ina upande wa pili ambao si rahisi kuonekana kwa macho ya kawaida..Nimebahatika kuuona upande wa pili wa dunia.Unaogopesha sana. Ni dunia nyeusi inatisha inayotawaliwa na nguvu kubwa za giza ” akawaza Innocent huku akitetemeka mwili kila alipokumbuka mambo aliyoyashuhudia katika sakata zima la kumuokoa Latoya.
“Kwa nini Latoya alijiunga katika ulimwengu huu wa giza? Ni vigumu kuamini kwamba Latoya anamuabudu shetani. Ni kwa sababu ya kutaka utajiri? Nguvu? au ni kitu gani kilichomshawishi hadi akakubali kumuangukia shetani na kumuabudu? maisha yake yote aliyakabidhi kwa shetani na endapo nisingekuwa mimi ,tayari angekwisha uawa.Haya mambo ni mazito sana na hata mimi yananichanganya.Ni vigumu kuamini nilichokiona lakini namshukuru sana Mungu kwa kuniweka hai.Kinachonishangaza zaidi wale wazee ambao walikuwa wananitokea ndotoni na kunipa nguvu wakanitaka nimuokoe Latoya ni akina nani? Kwa kukubali kwangu kumuokoa Latoya je tayari hata mimi ni mfuasi wa ulimwengu huu wa giza? Ouh No..!Ninaapa katu sintamuabudu shetani .Ninamumini Mungu mmoja muumba wa mbingu na nchi.”
Mara mlango ukafunguliwa akaingia Dr Catherine akiwa ameongozana na maafisa watatu wa polisi ambao walijitambulisha kwa Innocent na kumuomba wamuulize maswali machache.
“Umetokea nchi gani Innocent?
“Nmetokea Tanzania” akajibu
“Mlikuwa mnaelekea wapi wewe na wenzako?
“Sikumbuki tulikuwa tunaelekea wapi lakini mimi na rafiki yangu Latoya tulikuwa katika safari yetu ya mapumziko.Nimefikaje hapa hospitali? Nini kimetutokea?
“Mliokolewa na wanajeshi waliokuwa doria baharini Wanasema kwamba meli yenu ilikuwa inawaka moto hivyo wakawaokoa na kuwaleta hapa”
“meli ?!Innocent akashangaa
“Ndiyo.Meli yenu ilikuwa inaungua moto .Kwani hukumbuki kwamba mlijitosa majini baada ya meli yenu kuanza kuungua moto?
“Inspekta Henry naomba nikusahihishe kwamba hatukuwa katika meli.Tulikuwa katika kisiwa na ndipo tulipokumbwa na masahibu haya.Kwani hamkuiona miili mingine ya watu waliokuwa wamekufa kwa kuungua moto? Akauliza Innocent
“Hapana Innocent.Hamkuwa katika kisiwa.Mlikuwa katika meli iliyoungua moto na wewe na mwenzako mkajitosa majini.Kwa muda wa siku mbili sasa kumekuwa na jitihada za kuitafuta meli hiyo lakini haionekani baharini.Tunachotaka kujua ni idadi ya watu wangapi waliokuwamo katika meli hiyo?
“Inspekta Henry naomba unielewe kwamba hatukuwa katika meli.Tulikuwa katika kisiwa.Nilikuwa na msichana mmoja aitwaye Naya .Tulizunguka katika visiwa vitatu tofauti.Nashangaa unaposema kwamba tumeokolewa toka katika meli”
Maafisa wale wakatazamana halafu mmoja wao akaufungua mkoba mdogo akatoa kitabu
“Unakifahamu hiki kitabu? Innocent akastuka baada ya kukiona kitabu kile kitukufu
“Ninakifahamu.Hiki ni kitabu kitukufu.Kilikuwa kinahifadhiwa kisiwani kinalindwa na nyoka.Nilimuua yule nyoka na kukipata kitabu hiki.Ni hiki kitabu ndicho nilikitumia kuwasambaratisha Brandon na watu wake “ akasema Innocent na kuzidi kuwachanganya wale maafisa wa polisi.
“Innocent kitabu hiki kilikutwa kinaelea majini na hakikuingia maji hata kidogo. Ni jambo ambalo hata sisi limetushangaza sana” akasema yule afisa wa polisi na kumpatia Innocent kile kitabu.
“Innocent maelezo yako yanatuchanganya sana.Hatuelewi tumuamni nani kati yako au maafisa wa jeshi waliowaokoa baharini”
Innocent akawatazama wale maafisa wa polisi na kusema
“Sikilizeni vizuri,mimi na Latoya tulikuwa tunatoka Dare es salaam Tanzania tukielekea mapumziko.Tulitumia meli binafsi ya Latoya ”
“Latoya ni nani?
“Hamumfahamu Latoya? Inno akawauliza wale maafisa wa polisi ambao walitikisa vichwa vyao ishara ya kutomfahamu Latoya
“Dunia nzima wanamfahamu Latoya.Ni msichana mdogo bilionea”
“Mlikuwa mnaelekea wapi?
“Sifahamu tulikuwa tunaeleka nchi gani ilikuwa ni siri ya Latoya.Siku ya pili tukiwa safarini bahari ilichafuka na dhoruba kubwa kutokea.Ilipiga radi kubwa na nikapoteza fahamu.Nilizinduka nikiwa katika kisiwa nimezungukwa na watu ambao baadae nilikuja kufahamu kwamba walikuwa wakila binadamu wenzao.” Maafisa wale wa polisi waliposikia taarifa hiyo ya watu kula binadamu wenzao wakastuka
“Binadamu wanaliwa? Akauliza inspekta Henry
“ndiyo inspekta Henry.”
“wewe ulinusurika vipi kuliwa na watu hao?
“Niliokolewa na Naya ambaye naye pia alikuwa amekamatwa na watu wale lakini alifanikiwa kutoroka na kuniokoa na mimi pia”
“Naya ndiye huyo msichana uliyeokolewa naye?
“hapana Msichana niliyeokolewa naye ni bilionea Latoya.Naya amepotea na nina wasi wasi atakuwa amekwisha kufa.Nakumbuka Brandon alimpiga na kitu akaanza kuvuja damu nyingi.” Akasema Innocent.Kimya kikatanda mle ndani
“Ina maana hamna taarifa zozote kama kuna watu wanakula binadamu maeneo haya? Hamuwafahamu watu hao?
“Hatuwafahamu na hakuna watu wa namna hiyo wanaoishi maeneo haya “ akasema Inspekta Henry
“Basi haya yatakuwa ni maajabu makubwa sana.Nimewaona watu hawa na hata mimi nimenusurika kuliwa.Wanaishi na wana nguvvu sana.Inawezekana labda watu wale wakawa wanaishi katika dunia ya pili” akasema Inno na kuzidi kuwachanganya wale maafisa wa polisi
“Innocent unatuchanganya na simulizi zako.Tunachohitaji kufahamu hivi sasa ni endapo mtahitaji msaada wowote wa kuwarejesha nchini kwenu au mtaelekea kule mlikokuwa mnaelekea.Baada ya hali zenu kuboreka tutawasiliana na mamlaka zinazohusika na tuone namna tutakavyoweza kuwasaidia.Tutaangalia pia kama kuna balozi wenu hapa na kumfahamisha kuhusu uwepo wenu hapa” akasema Inspekta Henry na kuagana na Innocent .
“Hii simulizi waliyokuja nayo hawa maafisa wa polisi ni yakushangaza sana.Sisi hatukuwa katika meli.Tulikuwa kisiwani.Inawezekana mambo yale yalifanyika katika ulimwengu wa pili wa giza na hayawezi kuonekana katika ulimwengu huu wa kawaida na ndiyo maana wanajeshi wale waliona kitu kama meli badala ya kisiwa. Ninahisi hata wale watu wanaokula binadamu hawaishi katika uimwengu huu na ndiyo maana hata hawa maafisa wa polisi hawajui chochote . Nimebahatika kuushuhudia ulimwengu huu wa giza namna ulivyo.Nina hakika watu hawa hawataniacha hivi hivi.Lazima wataniandama kila dakika.Lakini kwa nini mimi? Kwa nini nichaguliwe mimi kuushuhudia ulimwengu huu? Akawaza Inno na mara picha ya Latoya ikamjia mawazoni na kuanza kukumbuka toka siku ya kwanza alipokuatana naye ofisini kwake.Picha mbali mbali zikaendelea kumjia na kuufanya mwili wake usisimke.
“Nilimpenda Latoya siku ya kwanza tu nilipomuona.Nakumbuka nilipoiona sura yake tu moyo wangu ulistuka sana na kubadili mapigo.Nilihisi muunganiko Fulani kati yangu naye.Nahisi hata yeye pia alipatwa na mstuko fulani aliponiona.Baada ya kuzinduka pale hospitali nilimkuta Latoya akiwa ni mmoja wa watu waliokuwepo nilifarijika sana.Latoya alinikaribisha nyumbani kwake na kulia pamoja nami wakati wa msiba ule wa Marina.Moyo wake uliojaa upendo haukubagua masikini wala tajiri na hivyo kuufanya msiba wa Marina binti masikini kuwa wa kihistoria.Hata baada ya msiba wa Marina kumalizika nilishindwa kuondoka kwa sababu nilihitaji kuwa karibu naye kila siku.Nilihisi utofauti mkubwa ndani yangu baada ya kukutana na Latoya ambao sjawahi kuuhisi katika masha yangu.Hata pale nilipogundua kwamba maisha yake yalikuwa na siri nzito nyuma yake lakini bado sikuweza kuondoka na kumuacha only because I love her.Nampenda Latoya na kwa ajili yake niko tayari kufanya jambo lolote lile.Nguvu ya penzi langu kwake imenifanya niweze kupitia hatari nyingi na kuzishinda.” Akawaza Innocent halafu akakichukua kile kitabu na kukishika mkononi.
“Nimenusurika kupoteza uhai wangu wakati wa kukifuata kitabu hiki.Hiki ni kitabu chenye maajabu makubwa.Kinaweza kuleta maangamizi makubwa sana kwa mtu ambaye anaweza akakitumia vibaya.Naya alikitumia vyema na akaweza kuwasambaratisha akina Brandon.Bila Naya sijui ningefanya nini.Sidhani kama ningeweza kuvivuka vizingiti vile vyote.Nitamkabidhi Latoya kitabu hiki kwani nina imani yeye anafahamu matumizi yake” akawaza Innocent.Mlango ukafunguliwa akaingia Dr Catherine
“Hallow Innocent.Unaendeleaje? akauliza Dr Catherine
“Ninaendelea vizuri sana Dr Catherine.Najisikia mzima wa afya”
“Vipi kuhusu kumbu kumbu Unaweza kukumbuka kila kitu?
“Sina tatizo katika kumbu kumbu zangu Dr Catherine.Nnakumbuka kila kitu sawasawa.” Akasema Inno na Dr Catherine akamuangalia kwa muda akafikiri na kusema
“ Innocent yule mwenzako Latoya anahitaji kukuona.Mna mahusiano gani naye?
“ Ni mpenzi wangu” akajibu Inno

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 59
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Hata baada ya msiba wa Marina kumalizika nilishindwa kuondoka kwa sababu nilihitaji kuwa karibu naye kila siku.Nilihisi utofauti mkubwa ndani yangu baada ya kukutana na Latoya ambao sjawahi kuuhisi katika masha yangu.Hata pale nilipogundua kwamba maisha yake yalikuwa na siri nzito nyuma yake lakini bado sikuweza kuondoka na kumuacha only because I love her.Nampenda Latoya na kwa ajili yake niko tayari kufanya jambo lolote lile.Nguvu ya penzi langu kwake imenifanya niweze kupitia hatari nyingi na kuzishinda.” Akawaza Innocent halafu akakichukua kile kitabu na kukishika mkononi.
“Nimenusurika kupoteza uhai wangu wakati wa kukifuata kitabu hiki.Hiki ni kitabu chenye maajabu makubwa.Kinaweza kuleta maangamizi makubwa sana kwa mtu ambaye anaweza akakitumia vibaya.Naya alikitumia vyema na akaweza kuwasambaratisha akina Brandon.Bila Naya sijui ningefanya nini.Sidhani kama ningeweza kuvivuka vizingiti vile vyote.Nitamkabidhi Latoya kitabu hiki kwani nina imani yeye anafahamu matumizi yake” akawaza Innocent.Mlango ukafunguliwa akaingia Dr Catherine
“Hallow Innocent.Unaendeleaje? akauliza Dr Catherine
“Ninaendelea vizuri sana Dr Catherine.Najisikia mzima wa afya”
“Vipi kuhusu kumbu kumbu Unaweza kukumbuka kila kitu?
“Sina tatizo katika kumbu kumbu zangu Dr Catherine.Nnakumbuka kila kitu sawasawa.” Akasema Inno na Dr Catherine akamuangalia kwa muda akafikiri na kusema
“ Innocent yule mwenzako Latoya anahitaji kukuona.Mna mahusiano gani naye?
“ Ni mpenzi wangu” akajibu Inno

ENDELEA……………………..

“ Hongera sana .Mpenzi wako ni mzuri mno.Naweza kusema kwamba ni malkia wa mabinti weusi” akasema Dr Catherine na kumkubusha Inno neno alilokuwa analitumia Naya akimtaja Latoya kuwa ni malkia mweusi.
Walitoka kaitika kile chumba cha Innocent na kuelekea katika chumba cha Latoya.Sura ya Innocent ikajenga tabasamu pana sana pale alipoiona tena sura ya binti malaika Latoya aliyekuwa amelala kitandani
“ Ouh Innocent ..!! akasema Latoya kwa furaha
“ Latoya ..!! akasema Innocent kwa furaha.Latoya alikuwa anatokwa na machozi ya furaha kwa kumuona tena Innocent.Walitazamana kwa muda halafu Latoya akasema
“ Innocent thank you.Thank you for everything” akasema Latoya na kumshika Innocent mkono
“ Latoya unajisikiaje? Akauliza Innocent
“ Ninajisikia vizuri na maendeleo yangu ni mazuri.Vipi wewe unaendelaje?
“hata mimi ninaendelea vizuri sana” akajibu Innocent
“Nimefurahi sana nimekuona Innocent.Nilikuwa na wasi wasi mwingi kuhusu usalama wako.Sikuamini walivyoniambia kwamba uko hai nikaomba wakulete hapa nikushuhudie mimi mwenyewe kwa macho yangu.” Akasema Latoya huku machozi yakimtoka
“ Usilie Latoya.Mimi ni mzima na niliyekuwa nakuhofia ni wewe pekee” akasema Innocent
”Innocent nashukuru kwa yote.You saved my life” akasema Latoya
“ Shhhhhhhhhh..!!! usiseme chochote Latoya.”
“ Innocent kuna mambo mengi ambayo tunahitaji kuyaongea lakini kwa sasa nataka kufahamu kuhusu kile kitabu.Uliweza kufanikiwa kukiokoa?
Innocent akatabasamu na kusema
“Kitabu ninacho.Tumefanikiwa kuondoka nacho”
“Ahsante sana.Kihifadhi na usiruhusu mtu yeyote akakisoma.Ni kitabu ambacho kinaweza kuleta maangamizi makubwa sana duniani.” Akasema Latoya halafu akafumba macho na kuonekana kuwa katika maumivu makali
“Latoya are you ok? Akauliza Inno
“I’m ok Innocent.” Akajibu Latoya na kujilazimisha kutabasamu.Akachukua karatasi ndogo toka chini ya mto wake na kumpatia Innocent
“Piga namba hizo utaongea na mtu anaitwa Elizabeth.Mwambie kwamba nimelazwa hapa hospitali na afike mara moja” akasema Latoya
“Usijali Latoya nitaongea naye” akajibu Inno
“Innocent ahsante sana nimefurahi kukuona na moyo wangu una amani.Naomba sasa uniache nipumzike” akasema Latoya.Innocent akatoka mle chumbani kwa Latoya na nje ya chumba akakutana na Dr catherine aliyekuwa akiwasubiri wamalize maongezi.Dr Catherine akamuongoza Inno hadi chumbani kwake na kabla hajatoka Innocent akamuomba msaada wa simu alitaka kuwasiliana na mtu muhimu.Dr Catherine akatabasamu na kumpeleka katika ofisi yake na kumkabidhi Inno simu apige.
Innocent akaziandika zile namba za Elizabeth na kupiga.Simu ikapokelewa na sauti nyororo ya mwanamke
“ hallow Elizabeth” akasema Innocent
“ hallow unaongea na Trish hapa .Elizabeth yuko safari na anapatikana kwa kutumia namba nyingine kwa sasa.”
“ Unaweza ukanisaidia mawasiliano yake tafadhali? Akasema Inno
“ samahani kaka yangu ningeomba kukufahamu kwanza wewe ni nani na una tatizo gani”
“Naitwa Innocent nimepewa namba hizi za Elizabeth na Latoya ili nimpatie ujumbe muhimu”
“ Latoya !! yule msichana simuni akashangaa
“ Ndiyo” akajibu Inno
“ Sawa kaka .Naomba ukate simu ili niwasiliane na Elizabeth na atakupigia muda si mrefu” akajibu Yule dada na Innocent akakata simu
Baada ya kama dakika tano hivi simu ikaita Innocent akapokea
“ Hallow” akasema
“ hallow .Elizabeth hapa.Naongea na nani?
“ Naitwa Innocent.Nimepewa namba hizi na Latoya nikupigie.”
“ Latoya !! Elizabeth naye akashangaa
“ Ndiyo.Latoya amelazwa hapa hospitali na anakuhutaji ufike mara moja”
“ Ouh gosh.Amelazwa hospitali? Ni hospitali gani hiyo alikolazwa? Anaumwa nini? Tafadhali naomba unielekeze kwa kina kinachomsumbua Latoya” akasema Eizabeth kwa wasi wasi. Innocent akamuelekeza kila kitu isipokuwa mambo yaliyotokea kule kisiwani
“ Ok Innocent nashukuru sana kwa taarifa.Hivi sasa niko hapa Jakarta Indonesia.Nitaanza safari ya kuja huko sasa hivi.Ninatumia ndege binafsi“ akasema Elizabeth ambaye alionyesha kuchanganywa sana na taarifa zile za Latoya kulazwa hospitali. Baada ya kuongea na Elizabeth,Innocent akarejea chumbani kwake akajilaza kitandani
“Latoya alioneka kuwa na maumivu makali.Inaonekana yule shetani Brandon alimtesa sana.Msichana mrembo kama yeye hakupaswa kabisa kuongozwa na nguvu za giza.Kwa sasa baada ya kumuokoa toka kifo nadhani utakuwa ni mwanzo mzuri wa kumrudisha katka maisha ya kawaida japokuwa naelewa kutakuwa na ugumu mkubwa.Lakini pamoja na yote sintafumba jicho hadi nihakikishe Latoya amekuwa ni mwanamke mwenye furaha japokuwa nitahitaji kupata maelezo toka kwake kuhusiana na kilichotokea na nini msimamo wake na kitu gani kitafuata baada ya hapa “ akawaza Innocent


* * * *


Sauti kama ya mtu akimuita ikamstua Innocent toka usingizini.Akafumbua macho na kukutana na sura yenye tabasamu ya Dr Catherine.
“Hallow Innocent.Samahani kwa kukuamsha.Kuna mtu anataka kukuona” akasema Dr Catherine.Innocent akainuka na kukaa kitandani.Dr Catherine alikuwa ameongozana na msichana mmoja mwenye weusi wa kung’aa aliyevaa suti fupi nyeusi iliyomkaa vyema.Kifuani alikuwa amevaa mkufu wa dhahabu ulioonekana kuwa wa thamani kubwa.Alipotabasamu ,vishimo vikatokeza katika mashavu yake
“ Nitaawacha muongee” akasema Dr Catherine na kutoka mle chumbani
“ Hallo Innocent.Naitwa Elizabeth Peterson” akasema Yule msichan na kumpa mkono Innocent
“Ouh wewe ndiye Elizabeth..!!!
“ yah Ndiye mimi “
“Nafurahi kukufahamu.Pole na safari.Nilipoisikia sauti yako simuni nilijua lazima utakuwa ni mrembo sana.Nilikuwa sahihi” akasema Innocent na kumfanya Elizabeth acheke kisha akavuta kiti na kuketi
“Unaendeleaje Innocent?
“Namshukuru Mungu ninaendelea vizuri” akajibu Innocent
“Nimefurahi kukufahamu Innocent.Uliponipigia simu nilikuwa Jakarta katika shughuli zangu za kibiashara na hivyo nimelazimika kusimamisha kila kitu na kufika hapa mara moja.Ni mwendo wa kama masaa saba hivi” akasema Elizabeth
“Nashukuru umefika Elizabeth.Latoya anahitaji sana kukuona.Unaonekana ni mtu wake wa muhimu sana”
“ Latoya ni bosi wangu.kama unavyojua Latoya ana biashara nyingi katika kila pembe ya dunia .Biashara na makapuni hayo yote viko chini ya kampuni moja ambayo mkurugenzi wake ni mimi.Latoya ni zaidi ya rafiki kwangu,ni zaidi ya ndugu,ni mtu muhimu sana kwangu .Nimetoka naye mbali sana na ndiye aliyeniwezesha mimi kuwa hivi nilivyo leo.Unionavyo hivi leo sina wazazi wala ndugu.Ndugu yangu pekee ninayemfahamu ni Latoya” akasema Elizabeth
“ tayari umekwisha onana naye? Akauliza Innocent
“Tayari nimeonana naye na tumeongea.Nimemuacha anapumzika ndio maana nimekuja hapa kukujulia hali na kukufahamu.Ni mara ya kwanza kumuona Latoya akiwa amelala kitandani ndiyo maana nilistuka sana.Toka nimemfahamu sijawahi kusikia amelazwa hospitali.Hii ni mara ya kwanza inatokea.” Akasema Elizabeth na kuinamisha kichwa chini
“ Lakini madaktari wanasema kwamba Latoya anaendelea vizuri” akasema Innocent
“ Ndivyo wanavyosema lakini ukweli ni kwamba Latoya anaumwa.Mpaka kukubali kulazwa hospitali ujue anaumwa sana.Hata ukiongea naye utagundua kwamba yuko katika maumivu makali lakini hataki kuweka wazi” akasema Elizabeth
“lazima Brandon alimtesa sana Latoya na kumsababishia maumivu haya makali” akawaza Innocent .Kikapita kimya kifupi Elizabeth akamstua Innocent
“ Unawaza nini Innocent? Unamuwaza Latoya?
“Ndiyo .Ninamuwaza Latoya”
Elizabeth akamuangalia Innocent na kuuliza
“ Innocent ni kweli unampenda Latoya?
“Kwa nini unauliza hivyo Elizabeth?
“Ninauliza kwa sababu kuna kila dalili kwamba nyie wawili mko katika mapenzi.Toka nimefahamiana na Latoya sijawahi kumuona akiwa na ukaribu na mwanaume kama ilivyo kwako.Toka alipokutana nawe amekuwa akinipigia simu na kunieleza mambo mengi kuhusiana nawe jinsi ulivyomfanya akawa ni mwenye furaha.” Akasema Elizabeth
“ Elizabeth ,mimi na Latoya bado ni marafiki wa kawaida na hatuna mahusiano ya kimapenzi.Japokuwa sijamueleza bado ukweli wa moyo wangu lakini ukweli ni kwamba ninampenda sana Latoya zaidi ya ninavyojipenda mimi mwenyewe na ndiyo maana niko tayari kufanya jambo lolote lile kwa ajili yake” Akasema Innocent
“Innocent naomba nikwambie ukweli kwamba endapo unampenda Latoya nakuonya usithubutu kuuvunja moyo wake na kumfanya akalia.” Akasema Elizabeth
“Elizabeth naomba ufahamu kwamba hata siku moja siwezi kuuvunja moyo wa Latoya na ndiyo mana unaniona niko hapa kwa sababu yake.Niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa sababu ya kuitafuta furaha ya moyo wake”
“Nafurahi kusikia hivyo Innocent.Usinielewe vibaya kwa kukuuliza hivyo lakini Latoya ni bilionea na hivyo wako watu wengi wanaoitafuta nafasi ya kuwa naye kwa maslahi yao binafsi.Sitaki kumuona Latoya anaumizwa na mapenzi.Nataka kumuona ni mwenye furaha katika maisha yake ya kila siku.Hajawahi kuwa na mahusiano na mtu yeyote kwa hiyo wewe unaweza kuwa wa kwanza.” akasema Elizabeth
“ Elizabeth ni kweli kwamba Latoya hajawahi kuwa na mahusiano na mwanaume yeyote yule katka maisha yake? Akauliza Innocent
Elizabeth akamuangalia na kusema
“Nilikutana na Latoya walipokuja kutembelea kituo cha mayatima nilikokuwa nalelewa.Wakati huo Latoya alikuwa anasoma katika shule ya watoto wa mabilionea.Baba yake alikuwa balozi wa Tanzania nchini marekani.Mpaka leo hii sifahamu ilikuaje hadi Latoya akasoma katika shule hii wanayosoma watoto wa mabilionea wakati wazazi wake walionekana kuwa watu wa kawaida sana.Urafiki wetu ulianza siku hiyo.Na kila mwisho wa wiki alikuwa anakuja kunitembelea na kuniletea zawadi mbalimbali.Urafiki wetu uliendea hadi tulipomaliza chuo kikuu.Baada ya kumaliza chuo Latoya alianza kujishughulisha na biashara hapo ndipo utajiri wake ulipoanzia.Aliniweka mimi kama msimamizi mkuu wa miradi yake yote.Kwa hiyo unaweza kupata picha ni namna gani mimi na Latoya tulivyo karibu.Kulijibu swali lako ni kwamba Latoya hajawahi kuwa na mahusiano na mwanume yeyote yule hata kwa siri.Angekwisha nieleza.” Akasema Elizabeth halafu kikapita kimya kifupi
“Innocet kuna jambo ambalo nataka ulifahamu.Kesho asubuhi tunaondoka kuelekea Miami Florida.Latoya anataka akapumzike kule katika jumba lake huku akiendelea kupata matibabu katika hospitali kubwa iliyo karibu na jumba lake,hospitali aliyoijenga maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa saratani. Tutatumia ndege yake binafsi ambayo inawasili leo hii kutokea nchini China.”


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………

BEFORE I DIE
SEHEMU YA 60
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Nilikutana na Latoya walipokuja kutembelea kituo cha mayatima nilikokuwa nalelewa.Wakati huo Latoya alikuwa anasoma katika shule ya watoto wa mabilionea.Baba yake alikuwa balozi wa Tanzania nchini marekani.Mpaka leo hii sifahamu ilikuaje hadi Latoya akasoma katika shule hii wanayosoma watoto wa mabilionea wakati wazazi wake walionekana kuwa watu wa kawaida sana.Urafiki wetu ulianza siku hiyo.Na kila mwisho wa wiki alikuwa anakuja kunitembelea na kuniletea zawadi mbalimbali.Urafiki wetu uliendea hadi tulipomaliza chuo kikuu.Baada ya kumaliza chuo Latoya alianza kujishughulisha na biashara hapo ndipo utajiri wake ulipoanzia.Aliniweka mimi kama msimamizi mkuu wa miradi yake yote.Kwa hiyo unaweza kupata picha ni namna gani mimi na Latoya tulivyo karibu.Kulijibu swali lako ni kwamba Latoya hajawahi kuwa na mahusiano na mwanume yeyote yule hata kwa siri.Angekwisha nieleza.” Akasema Elizabeth halafu kikapita kimya kifupi
“Innocet kuna jambo ambalo nataka ulifahamu.Kesho asubuhi tunaondoka kuelekea Miami Florida.Latoya anataka akapumzike kule katika jumba lake huku akiendelea kupata matibabu katika hospitali kubwa iliyo karibu na jumba lake,hospitali aliyoijenga maalum kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wa saratani. Tutatumia ndege yake binafsi ambayo inawasili leo hii kutokea nchini China
ENDELEA………………..
Taratibu ndege ilipunguza mwendo na kusimama.
“ Tumefika salama “ akasema Elizabeth huku akitabasamu
“ Karibu nyumbani Innocent.Karibu Miami Florida.Pole kwa safari ndefu” akasema Latoya
“ahsanet Latoya.Ilikuwa ni safari ndefu sana.Nashukuru tumefika salama” akajibu Innocent.Mlango ukafunguliwa Latoya akaagana na marubani wake wanne pamoja na wahudumu wa ndege yake,aliwashukuru kwa kuwafikisha salama halafu akashuka akitanguliwa na Elizabeth na nyuma yake alikuwepo Innocent.Watu zaidi ya kumi walikuwa wamejipanga mstari wakisubiri kusalimiana na Latoya.Huku akitabasamu akasalimiana na watu wale na kuwatambulisha kwa Innocent
“ Innocent kutanana na walinzi na watumishi wangu hapa Miami.” Akasema Latoya .Innocent akasalimiana nao halafu yeye na Latoya wakaingia katika gari maalum aina ya Limousine lenye rangi nyeusi wakaondoka pale uwanjani
Gari lile lilienda hadi katika jumba moja kubwa lililozungukwa na taa nyingi .Wakashuka garini na kukutana na madhari ya kupendeza na kuvutia mno
“ hapa ndipo ninapoishi nikiwa huku .Karibu sana” Latoya akamwambia Innocent
“This place is amazing.Halafu nyumba hii inafanana sana na ile nyumba yako ya Dar es salaam.” akasema Inno
“Ni kweli . Nyumba zangu zote nimezijenga kwa kutumia ramani moja.Ukiwa ndani ya nyumba hii utajihisi kama uko Dar es salaam kwa sababu kila kilichomo humu ndicho kipo Dar es salaam.” akajibu Latoya halafu wakaanza kupiga hatua kuelekea ndani.Nyumba ilikuwa imepambwa kwa mapambo mazuri yenye ujumbe wa kumkaribisha Latoya nyumbani na kumfanya asiache kutabasamu
Chakula kizuri kiliandaliwa ,wakakaribishwa mezani na watumishi wenye tabasamu na baada ya kula Latoya akasema
“Innocent naona tukapumzike.Safari ilikuwa ndefu sana.Tutapata wasaa mzuri wa kuongea kuanzia kesho baada ya kupumzika.Chumba chako kiko pale pale kama katika nyumba ya Dar es salaam.” Akasema Latoya na kumfanya Elizabeth aliyekuwapo pale mezani atabasamu.Latoya akaagana na Elizabeth halafu akamshika mkono Innocent wakapanda ghorofani
Walipanda hadi ghorofa ya juu kabisa,Latoya akamuonyesha Innocent chumba chake
“Lala salama Innocent.Tutaonana kesho” akasema Latoya halafu akaelekea chumbani kwake.Alipoingia chumbani kwake akaanza kuhisi maumivu makali sana ya mwili akachukua vidonge vya kutuliza maumivu akameza.
“Siamini kama nimekiona tena chumba changu.Sikutegemea kama ningerejea katika chumba hiki nikipendacho kupita vyote.Haya yote yamewezekana kwa sababu ya Innocent.He saved me.He saved my life.Nina deni kubwa kwake na malipo peke ni kumkabidhi moyo wangu.Hilo peke ndilo litalingana na thamani yake kwangu” akawaza Latoya
“Mwili wangu nausikia mwepesi sana japokuwa una maumivu.Moyo wangu nausikia una amani tofauti na hapo kabla. Kila kitu nakiona kama kimebadilika sana.Haya ndiyo maisha yangu mapya.Maisha wanayoishi binadamu wa kawaida na ndiyo maisha ninayotaka kuishi sasa.Ninataka kuishi na mtu nimpendaye kupita wote,mtu ambaye niliweka ahadi ya kumpata kabla sijafa na ahadi hiyo ikatimia.” Akawaza Latoya halafu akavua koti lake jeusi akalitupa kitandani, akavua blauzi nyeusi aliyokuwa ameivaa ,akasogea karibu na kioo akatabasmu baada ya kukiangalia kifua chake kilichobeba titi ndogo zilizosimama wima
“I’m so sexy” akasema huku akitabasamu halafu akageuka nyuma na kujitazama mgongoni na mara sura yake ikabadilika na kupatwa na mshangao mkubwa
“Ouh Mungu wangu sikutegemea kama kingekuwa na hali mbaya namna hii.”: akasema Latoya na machozi yakamtoka.Furaha yote aliyokuwa nayo ikapotea ghafla akaenda kukaa kitandani
“How could I be so stupid and let them do sometimg like this to me? ..akajiuliza huku akilia
Siku zote nilikuwa naona kama ni kitu kidogo tu lakini kumbe kimekuwa kikubwa namna hii !! nailaumu sana nafsi yangu kwa kukubali kuwa mtumwa wa giza.”
Latoya akainuka na kurudi tena katika kioo akajitazama kwa mara nyingine na machozi yakamtoka
“Hali yake inatisha.Kwa nini siku zote hizi sikugundua kwamba hali inazidi kuwa mbaya? Walinifanya kipofu nisiweze kuona na sikuhisi chochote kutokana na nguvu walizonipa.Kwa sasa sina tena nguvu zile na ninayaona mambo katika macho ya kawaida .Ouh Mungu wangu tafadhali naomba unisamehe kwa yote niliyokukosea.Uliniumba na kunipa uzuri wa kipeke lakini ona kitu nilichokifanya katika mwili ulionipatia”
Machozi mengi yakaendelea kumtoka Latoya.Akarudi tena kitandani na kukaa
“Naamini katika uchunguzi wa afya yangu nitakaofanyiwa kesho na jopo la madaktari bingwa wataangalia namna ya kuweza kunitibu ndani ya muda mfupi ujao.Sitaki kitu chochote kile kilete kasoro katika maisha yangu mapya ninayoanza kuishi nikiwa na Innocent.” Akawaza Latoya halafu akainuka na kuzunguka zunguka mle chumbani
“Siku ya kesho nimepanga kumweleza Innocent ukweli wote wa maisha yangu.Sina haja ya kumficha tena kwa sababu tayari amekwisha shuhudia mambo mengi mno mazito.Anayafahamu maisha yangu na siri zangu nyingi.Ameyatoa maisha yake kwa ajili yangu kwa hiyo ana haki ya kuufahamu ukweli halisi.Nitamueleza kila kitu kuanzia maisha yangu ya utotoni hadi hivi leo” akasimama katika madhabahu ya mawe yenye kung’aa
“Hapa ndipo nilikuwa nawasha mishumaa nikapiga magoti na kumwabudu Mungu wa Giza.Its over now.Sintafanya tena jambo lile.Nitamuangukia na kumuabudu Mungu mmoja tu,Mungu wa kweli aliyeumba mbingu na dunia,ambaye ameniokoa toka mikono ya shetani kwa kumtumia Innocent.Kesho nitazivunja madhabahu zote za Mungu wa giza.” Akawaza na kupanda kitandani.Alihisi baridi na maumivu makali akajifunika na haikuchukua muda akapitiwa na usingizi mzito


* * * *


Mzee mmoja mnene,mweupe na mwenye ndevu nyingi zilizomfika hadi kiunoni akamshika mkono akamuinua na kumkalisha katika kiti kilichokuwa na urembo wenye kung’aa sana.Alikuwa anavuja damu mwili mzima.Alisikia maumivu makali sana ya mwili.Mzee Yule akamuangalia ,akamsogelea akamshika mikono yake akaitazama na kusikitika sana
“Haya yote umeyataka wewe mwenyewe Latoya.yasingekutokea haya endapo usingevunja maagano.Ulikwenda nje ya maagano na kuenenda katika njia unayoitaka wewe.Usidhani umeshinda Latoya.Tutakuandama usiku na mchana kwani wewe bado ni wetu na hutaweza kutuponyoka kamwe.Tumekwishakupiga muhuri wetu mgongoni kwako kwa hiyo fahamu kwamba maumivu haya unayoyapata sasa yataendelea daima na yatakuwa yakizidi kila siku lakini kuna jambo moja ambalo unaweza ukalifanya.Katika kile kitabu chetu kitukufu ambacho wewe umekisaliti fungua sura ya nne na usome aya ya sita,saba na nane na maumivu haya yote unayoyasikia yatakoma.Hautasikia tena maumivu na maisha yako yatakuwa na amani tele” akasema yule mzee na kutoweka.Ghafla Latoya akakurupuka toka usingizini.Alikuwa anaota.Kitu cha kwanza alichokihisi baada ya kustuka usingizini ni maumivu makali sana mgongoni.Alihisi pia unyevu nyevu kitandani. Akaangalia vizuri na kustuka baada ya kugundua kwamba unyevu ule ulitokana na damu .Machozi yakamtoka.Akayachukua mashuka yale na huku akikabiliwa na maumivu makali akaenda hadi katika chumba kilichokuwa na mashine ya kufulia nguo akayatupa mle na kuelekea bafuni .Alipomaliza kuoga akarejea chumbani.Kila hatua aliyopiga ndivyo maumivu yalivyozidi kuwa makali.Alipofika kati kati ya chumba akashindwa kuvumilia maumivu yale makali akahisi kizungu zungu
“ Gosh !.I’m going down again.Help me God” akasema na kuanguka sakafuni fahamu zikampotea
* * * *


Sauti za ndege waliokuwa wakilia toka katika bustani iliyoko juu ya jumba hili zilimstua Latoya ,Akafumbua macho tayari kulikwisha pambazuka.Macho yake yakatua katika saa kubwa ya ukutani ambayo ilionyesha ni saa moja za asubuhi.Alihisi uchovu na maumivu kwa mbali.Alikaa pale chini akiwaza kilichomtokea usiku pamoja na doto ile aliyoota
“Ni kweli hawataacha kuniandama hadi wahakikishe nimerejea katika mikono yao.Nimekwisha amua kuachana nao na sintarudi nyuma tena.Najua nitakutana na vikwazo vingi ,mateso mengi lakini naamini Mungu yupo na atanipigania.Naamini nitashinda vita hii” akawaza Latoya na kuinuka akaenda katika chumba cha kufulia akayafua mashuka yale yaliyokuwa yameloa damu halafu akaingia bafuni kuoga na kurejea chumbani.Akajiremba na kusimama na kuitazama madhabahu ile aliyokuwa anaitumia kwa ajili ya ibada za giza.
“Leo sitaki kuiona madhabahu hii na vyote vinavyomuhusu Mungu wa giza humu ndani mwangu.Ngoja kwanza niende hospitali nikafanya vipimo kwani madakatri watakuwa wananisubiri mida hii.” Akawaza na kutoka mle chumbani.Bado aliendelea kusikia maumivu kwa mbali ,dawa za kutuliza maumivu zilimsaidia sana
Toka chumbani kwake akaelekea moja kwa moja chumbani kwa Innocet akabonyeza kengele ya mlangoni na haukupita muda Innocent akaufungua mlango
“ Ouh Latoya..karibu “ akasema Inno
“ Ahsante sana Innocent.Unaendeleaje? Usiku wako ulikuaje?
“ Ninaendelea vizuri sana Latoya na usiku wangu ulikuwa mzuri pia.Nimelala usingizi mzito sana .Unajisikiaje hali?
“ Najisikia vizuri Innocent” akajibu Latoya
Innocent bado aliendelea kuyaelekeza macho yake katika kifua cha Latoya
“ Mbona unanitazama hivyo Innocent? Akauliza Latoya baada ya kugundua Inno alikuwa anamuangalia sana sehemu za kifua
“ You look so amazing today.Kila siku nakuona kama mpya.Latoya umebarikiwa uzuri wa kipekee ”
“ Ahsante Inno.Ahsante sana” akajibu Latoya kikapita kimya kifupi wakiangaliana
“ Innocent ninaelekea hospitali madaktari wanakwenda kunifanyia uchunguzi wa afya yangu.”
“ safi sana Latoya.Baada ya yote yaliyotokea huna budi kufanya uchunguzi wa afya.Ngoja nivae viatu tuongozane wote” akasema Inno
“ Usijali Innocent.Hospitali ninayokwenda haiko mbali ni kama mita elfu moja toka hapa.Endelea kupumzika.Sintachukua muda mrefu nitarejea Chochote utakachokihitaji usisite kusema utakipata.Wapo wahudumu wa kukuhudumia kila dakika.Halafu nitakaporudi tuna mambo muhimu ya kuongea.Make yourself at home,make yourself a king” akasema Latoya huku akicheka na kuanza kupiga hatua kushuka chini.Alisalimiana na wafanyakazi wake wote kama ilivyo kawaida yake kila asubuhi halafu akaelekea katika ukumbi wa chakula ambako tayari kifungua kinywa kilikwisha andaliwa.Alihisi njaa kali na miguu yake inakosa nguvu.Wakati akiendelea na kifungua kinywa mara akatokea Elizabeth
“ Hallo Latoya “ akasema Elizabeth
“ Ouh Elizabeth,unaendelaje?
“ Naendelea vizuri .Nimetoka kuonana na Penina Smith asubuhi hii kuna nyaraka nilitakiwa kuzisaini.Tena imekuwa vyema tumeonana kuna hizi nyaraka hapa naomba uzisaini” akasema Elizabeth.Latoya akaweka kikombe cha chai mezani akalivuta faili lenye nyaraka anazotakiwa kuzisaini ,akaziangalia na kuzisaini
“ Elizabeth,kuanzia sasa kitu chochote ambacho kitanihitaji mimi kusaini naomba usaini wewe badala yangu.Nataka nipate mapumziko .Halafu kitu kingine,mle chumbani kwangu kuna ile meza ya mawe nataka itolewe chumbani kwangu.Nitakaporejea toka hospitalini sitaki kuiona tena chumbani” akasema Latoya
“ Usijali Latoya kila kitu kitafanyika kama unavyotaka.Nimeongea na Dr Bll Drawker na amesema yuko tayari na timu yake wanakusubiri”
“ Ok ahsante sana Elizabeth.hata mimi nimeongea nao asubuhi hii ” akasema Latoya akachukua kikombe chake cha chai akanywa halafu akamtazama Elizabeth na kusema
“ Elizabeth ,kwa muda huu ambao nitakuwa hospitali tafadhali hakikisha Innocent hawi mpweke.Kama itawezekana mchukue na muonyeshe mazingira.Anapenda sana bustani na kutembea ufukweni.Please do that for me.Make him comfortable” akasema Latoya
“ Usihofu Latoya.Nitafanya hivyo.Nimefurahi kuonana na Innocent ana kwa ana.Nilitamani sana kukutana naye siku moja kutokana na maelezo uliyokuwa ukinipa.Innocent is a gentleman and you two looks good together “ akasema Elizabeth na wote wawili wakacheka
“ Hii ni mara ya kwanza kukuona ukiwa na ukaribu na mwanaume namna hii.Nimemfanyia usaili Innocent na kugundua kwamba ni kijana wa pekee sana .Hukukosea kumchagua awe mtu wako wa karibu.Ni kijana anayefaa kuaminiwa” akasema Elizabeth na kuufanya uso wa Latoya upambwe na tabasamu pana sana
“ Ahsante Elizabeth.Nilijua tu lazima ungemfanyia usaili Innocent na nilikuwa nasubiri majibu ya usaili toka kwako.Nashukuru kwa majibu yako mazuri” akasema Latoya na wote wakacheka
“ Latoya unafahamu kabisa kwamba wanaume siku hizi ni waongo na hawaaminiki na ndiyo maana siku zote nimekuwa makini sana kuhusu watu hawa kwani sitaki kukuona ukiingia katika orodha ya watu walioumizwa na wanaume .Latoya wewe ni kiumbe mwenye roho nzuri sana na hupaswi kwa namna yoyote ile kuumizwa na mtu yoyote ile” akasema Elizabeth .Latoya akatabasamu na kusema
“ Elizabeth ,tutaongea zaidi jioni .Kuna mambo meng sana ambayo nataka tuyaongee,lakini kwa sasa nawahi hospitali” akasema Latoya huku akiinuka .Elizabeth naye akainuka na kuongozana na Latoya kuelekea katika sehemu liliko gari la kifahari la Latoya.
“ Elizabeth ,jambo lingine ambalo nataka ulifanyie kazi ni kwamba kuanzia sasa sitaki kuongozana na msafara wa walinzi.Nitakuwa nikitembea na dereva na mlinzi mmoja tu kama ikihitajika.Nataka kuanza kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine” akasema Latoya
Gari lake la kifahari sana lilikuwa limezingirwa na walinzi sita waliokuwa katika suti nyeusi.Latoya akasalimiana nao .Elizabeth akawaambia kwamba hawatalazimika tena kuambatana na Latoya kila aendako labda kwa sababu maalum tu.Mlango wa gari ukafunguliwa na mlinzi na Latoya akangia,gari ikaondoka akaeleka hospitali

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………….
 
BEFORE I DIE
SEHEMU YA 61
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Latoya unafahamu kabisa kwamba wanaume siku hizi ni waongo na hawaaminiki na ndiyo maana siku zote nimekuwa makini sana kuhusu watu hawa kwani sitaki kukuona ukiingia katika orodha ya watu walioumizwa na wanaume .Latoya wewe ni kiumbe mwenye roho nzuri sana na hupaswi kwa namna yoyote ile kuumizwa na mtu yoyote ile” akasema Elizabeth .Latoya akatabasamu na kusema
“ Elizabeth ,tutaongea zaidi jioni .Kuna mambo meng sana ambayo nataka tuyaongee,lakini kwa sasa nawahi hospitali” akasema Latoya huku akiinuka .Elizabeth naye akainuka na kuongozana na Latoya kuelekea katika sehemu liliko gari la kifahari la Latoya.
“ Elizabeth ,jambo lingine ambalo nataka ulifanyie kazi ni kwamba kuanzia sasa sitaki kuongozana na msafara wa walinzi.Nitakuwa nikitembea na dereva na mlinzi mmoja tu kama ikihitajika.Nataka kuanza kuishi maisha ya kawaida kama watu wengine” akasema Latoya
Gari lake la kifahari sana lilikuwa limezingirwa na walinzi sita waliokuwa katika suti nyeusi.Latoya akasalimiana nao .Elizabeth akawaambia kwamba hawatalazimika tena kuambatana na Latoya kila aendako labda kwa sababu maalum tu.Mlango wa gari ukafunguliwa na mlinzi na Latoya akangia,gari ikaondoka akaeleka hospitali

ENDELEA………………………….
Baada ya Latoya kuondoka kuelekea hospitali,Elizabeth akapanda ghorofani hadi chumbani kwa Innocent akagonga mlango na Innocent akaufungua
“ Hallo Innocent,umeamkaje? Habari za toka jana? Akauliza Elizabeth huku akitabasamu
“ Nimeamka salama Elizabeth.Vipi wewe unaendeleaje? Habari za toka jana?
“ habari ni nzuri Innocent.Unaionaje hali ya Miami?
“ Uuhm ! Nimeipenda ni nzuri sana.Unajua hii si mara yangu ya kwanza kuja Marekani.Nimehitimu shahada yangu ya kwanza ya uchumi na fedha katika chuo kikuu cha Columbia New York kwa hiyo ninafahamu Marekani japo si kwa ukubwa wake.” Akasema Innocent
“ Ouh ! Sikujua kama umewahi kuishi na kusoma hapa.Kwa nini uliamua kurudi nyumbani Tanzania badala ya kubaki hapa na kutafuta kazi yenye maslahi manono kulingana na taaluma yako?
‘ Nilirejea nyumbani kwa sababu familia yangu walikuwa wakinihitaji.Nilitakiwa kuisimamia miradi ya familia.Pamoja na hayo nadhani ni mipango wa Mungu nirejee nyumbani kwani nisingefanya hivyo nisingekutana na Latoya na wala mimi na wewe tusingefahamiana.” Akasema Innocent na wote wakacheka
“ Innocent ,Latoya amekwenda hospitali.Sio mbali sana na hapa.Ni hospital aliyoijenga yeye mwenyewe kwa ajli yakuwahudumia watu wenye matatizo ya saratani.Ni moja kati ya hopsitali kubwa na iliyosheheni madaktari bingwa wa saratani.Naweza kusema kwamba ni moja kati ya hospitali tegemeo hapa marekani kwa kutibu Saratani.Kwa kuwa anaweza akachukua muda mrefu kidogo kule hospitali,ni jukumu langu kuhakikisha kwamba hauboreki kwa hiyo nitakuchukua na tutazunguka sehemu mbalimbali .” akasema Elizabeth
“ Hakuna shaka Elizabeth,nitafurahi sana kama ukifanya hivyo” akajibu Innocent
“ Ok Innocent wakati unaendelea kujiandaa ,ninakwenda mara moja chumbani kwa Latoya kuna kazi aliniachia ya kufanya chumbani kwake” akasema Elizabeth
“ Chumbani kwa Latoya? Innocent akashangaa
“ Kuna mtu anaruhusiwa kuingia chumbani kwa Latoya? Akauliza
“Ndiyo.Chumba cha Latoya ni ruksa kwa kila mtumishi kuingia wakati hayupo lakini wakati akiwa hapa huwa hapendi mtu yeyote aingie chumbani kwake.Kwani vipi Innocent mbona umeshangaa sana?
“ Its nothing.Utanipitia ukitoka huko” akasema Innocent .Elizabeth akamtazama na kutaka kusema kitu lakini akaghairi na kuondoka kuelekea chumbani kwa Latoya.
Kule Dares salaam hakuna mtu aliyewahi kukona chumba cha Latoya lakini hapa mtumishi yeyote anaruhusiwa kuingia katika chumba chake.Mhh ! filamu ya maisha ya Latoya bado inaendelea” akawaza Innocent
“ Innocent ni kijana mcheshi sana na amemfanya Latoya awe na furaha ya aina yake.Ingawa bado Latoya hajaniweka wazi kuhusiana na urafiki wao lakini ninaziona kila dalili za penzi zito kati yao” akawaza Elizabeth huku akikinyoga kitasa cha mlango wa chumba cha Latoya na kuingia ndani.Kitu cha kwanza alichokutana nacho ni harufu nzuri sana ya uturi ambayo hakuwahi kuisikia
“ wow ! sijawahi kuisikia harufu nzuri kama hii.” Akawaza Elizabeth na kutembea kwa haraka kuelekea katika meza ya vipodozi iliyokuwa imesheheni vipodozi vya kila namna na kuanza kuangalia chupa moja baada ya nyingine akitafuta chupa yenye harufu ile nzuri.Alizingalia chupa zote zilizokuwapo pale mezani lakini hakuipata chupa ile aliyokuwa akiitafuta.Akasimama mbele ya meza ile akajishika kiuno.
“ Nitamuuliza Latoya hii ni perfume gani yenye harufu nzuri na ya kuvutia namna hii.” Akawaza Elizabeth na kugeuka kwa dhumuni la kuelekea katika ile meza aliyoambiwa aitoe.Mara tu apogeuka nusura roho imtoke kwa kitu alichokiona.Mwili ulimtetemeka na nguvu zikamuishia .Aliuona mwisho wake .Alikuwa akitazamana na joka kubwa ambalo hajawahi kuliona katika maisha yake hata katika filamu.Lilikuwa ni joka kubwa jeusi lenye kichwa kikubwa zaidi ya kile cha binadamu.Eneo lile lilipokuwapo lile joka hakukuwa tena na ile meza ya mawe ambayo Latoya alitaka iondolewe bali joka lile kubwa.Kutokana na mstuko ule mkubwa alioupata,haja ndogo ikamtoka bila kujifahamu.Hizi zilikuwa ni sekunde chache lakini ngumu sana kuwahi kumtokea katika maisha yake sekunde ambazo alikuwa anatazama na joka lile la ajabu na la kutisha.
“Ee mungu wangu niokoe” akaomba Elizabeth na ghafla akahisi kama miguu yake inapata nguvu tena .Akajaribu kuuinua mguu wa kulia ukainuka na kitu cha kwanza alichokiona ni mlango uliokuwa wazi.kwa nguvu zake zote akatoka mbio kama mshale.Breki ya kwanza ilikuwa ni katika mlango wa chumba cha Innocent.Akauvamia kwa nguvu ukafunguka,akajitupa ndani.Innocent aliyekuwa anavaa akastuka baada ya kumuona Elizabeth ameingia mle chumbani na kuanguka chini
“ Elizabeth !! Innocent akashangaa na kumkimbilia pale chini
“ Elizabeth !! Elizabeth !! akaita Innocent kwa wasi wasi lakini Elizabeth hakuweza kuongea lolote alikuwa anaweweseka.Macho yalikuwa yamemtoka pima.Innocent akaogopa
“ Elizabeth nini imetokea? Akauliza tena lakini bado Elizabeth aliendelea kuweweseka .Innocent akahisi kuchanganyikiwa ,hakujua ni kitu gani kilichompata .Haraka haraka akachukua chupa ya maji ya kunywa akamnywesha halafu akamketisha sofani
Elizabeth akavuta pumzi ndefu .
“ Pole sana Elizabeth.” akasema Innocent.Bado Eliza aliendelea kutiririkwa na jasho jingi.Baada ya kama dakika kumi hivi Elizabeth akaanza kujisikia vizuri ingawa machozi hayakumkauka
“ Elizabeth nieleze nini kmekutokea? Unaumwa? Akauliza Inno
“ Innocent lets get out of here now.Hii ni sehemu hatari sana” akasema Elizabeth huku akitetemeka
“ Sikuelewi Elizabeth unamaanisha nini?
“ Innocent twende tuondoke haraka sana.Hii si sehemu salama hata kidogo” akasisitiza Elizabeth huku akiung’ang’ania mkono wa Innocent
“Hebu nieleze Elizabeth kimetokea nini?
Elizabeth akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Nimeona joka kubwa sana chumbani kwa Latoya.Sijawahi kuliona joka la namna ile toka kuzaliwa kwangu na hata katika filamu.Ni kitu cha kutisha sana” akasema Elizabeth na kuanza kulia tena
“Usilie Elizabeth tafadhali nyamaza kulia” Inno akambembeleza
“ Innocent ninaogopa mno.Ilibaki kidogo nipoteze maisha yangu.Innocent naomba uniondoe hapa” akasema Elizabeth
“ Hukuumia sehemu yoyote?
“ Hapana Inno .Nilipata nguvu nikawahi kukimbia.Innocent tafadhali naomba uniondoe hapa.” Elizabeth akazidi kulia
“Huyo nyoka uliyemuona alielekea wapi?
“Sifahamu.Niliwahi kukimbia.Nadhani bado yuko ndani ya chumba cha Latoya” akasema Elizabeth.Innocent akachukua kitambaa na kumfuta machozi
“ Kaa humu humu chumbani usitoke.Nakwenda kumuangalia huyo nyoka ili kama yupo tuwasiliane na vyombo vinavyohusika wafanye utaratibu wa kumuondoa” akasema Innocent
“Hapana huwezi kwenda huko.Ni joka kubwa mno halafu siwezi kuniacha humu ndani peke yangu.naogopa sana” akasema Elizabeth huku akimvuta mkono Innocent
“ Usiogope Elizabeth,hii ni sehemu salama hakuna lolote litakalokutokea Narudi sasa hivi “ akasema Innocent lakini Elizabeth hakuwa tayari kubaki peke yake
“ Tunakwenda sote.Sikubali kubaki peke yangu humu ndani” akasema Elizabeth huku akiinuka.Innocent akaamuangalia usoni halafu akamshika mkono akaufungua mlango wakatoka mle chumbani na kuelekea chumbani kwa Latoya.Elizabeth alikuwa bado anatetemeka.Walikwenda hadi katika mlango wa chumba cha Latoya ambao bado ulikuwa wazi.Innocent naye alikuwa anaogopa japokuwa hakutaka kuonyesha mbele ya Elizabeth.Inno akamfanyia ishara Elizabeth abaki pale mlangoni na yeye akaingia ndani huku akinyata.Aliangaza pande zote lakini hakuona dalili zozote za kuwepo kwa nyoka.Alifungua makabati yote hadi bafuni na chooni lakini hakukuwa na dalili zozote za hilo joka alilolisema Elizabeth.Alipohakikisha kwamba hakukuwa na nyoka yoyote mle chumbani akamfuata Elizabeth pale mlangoni aliyekuwa amesimama kwa woga huku akitetemeka
“ Umemuona” akauliza Elizabeth
“ Elizabeth hakuna dalili zozote za kuwepo nyoka humu chumbani” akasema Innocent.Elizabeth akastuka sana
“ No ! Innocent that cant be.I saw that snake.a huge snake”
“ Usihofu Elizabeth yawezekana amekimbia”
‘ Hapana Innocent.Haweze kutoroka.Ni mkubwa sana.Amepita wapi? Lazima atakuwa amejificha mahala humu chumbani.Angalia vizuri Innocent.Nina wasi wsi sana na maisha ya Latoya yako hatarini” akasema Elizabeth
“ Elizabeth nimetazama kote chooni bafuni na katika vyumba vyote vya karibu hakuna dalili zozote za kuwepo kwa huyo nyoka.”
“ Innocent believe me I saw a snake.Dont you believe me? Akasema Elizabeth huku akilia
“ I believe you Elizabeth” akasema Inno
“ If you do believe me then lets search the whole house till we find that damn snake” akasema Elizabeth.Innocent akamtazama usoni na kusema
“ Elizabeth nyoka uliyemuona ameondoka.”
Elizabeth akamuangalia Innocent kwa mshangao lakini kabla hajasema chochote Innocent akasema
“ Twende tuondoke hapa ndani”
“No Innocent.We need to find that snake” akasema Elizabeth na kuingia mwenyewe chumbani kwa Latoya.Macho yake yakatua katika meza ile ya mawe ambayo Latoya alitaka iondolewe ambayo dakika chache mahala pale aliliona joka kubwa.Akashangaa sana kwa maajabu yale
“Alikuwa katika meza hii ya mawe.Latoya aliniambia kwamba meza hii ibomolewe leo kabla hajarudi toka hospitali na nilikuja ili kuiangalia kabla ya kumleta fundi wa kuibomoa.Kitu cha ajabu ni kwamba baada tu ya kuingia humu ndani sikuiona meza bali hilo joka kubwa la kutisha.” Akasema Elizabeth huku akiendelea kulia machozi
“ Usiogope Elizabeth nitaibomoa hii meza” akasema Innocent
“ Hapana Innovent.Usiiguse hiyo meza.Nitawasiliana na walinzi ili waje waivunje.” Akasema Elizabeth halafu akachukua simu yake na kupiga akawaomba walinzi wawili chumba ni kwa Latoya .Wakati wakiwasubiri walinzi wale wafike.Innocent akaendelea kukishangaa chumba cha Latoya namna kilivyo kizuri
“ Latoya anachumba kizuri sana.Sielewei ni kwani ni kule dare s salaam hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia chumbani kwake au hata anayefahamu jinsi chumba chake kilivyo.Ninahisi Latoya hakutaka watu waingie chumbani kwake kuogopa kutokewa na mambo ya ajabu ajabu kama haya yaliyomtokea Eliuzabeth.” Akawaza Innocent na mara vijana wawili wakaingia mle chumbani wakaelekezwa kazi ya kufanya wakaianza kazi ile mara moja.
Hawakutoka mle chumbani hadi walipohakikisha kwamba madhabahu ile imeondolewa kabisa kisha wakatoka ndani ya chumba kile na kuelekea chumbani kwa Innocent
“Innocent miguu yangu yote haina nguvu hata kidogo.Sina hakika kama nitaweza kufanya kazi yoyote leo.Pengine nahitaji mapumziko kwa siku ya leo.Nilichokiona kimenistua mno na kitabaki katika kumbu kumbu zangu kwa miaka mingi sana.Nahitaji kuituliza akili yangu lakini kabla ya yote lazima nimtaarifu Latoya kuhusiana na jambo hili.Lazima nimuonye ili afanye uchunguzi juu ya joka lile na wapi limetokea.Inawezekana likawa limetoka katika msitu wa karibu” “ akasema Elizabeth
“Hapana usifanye hivyo Elizabeth.Usimwambie Latoya kuhusiana na ulichokiona chumbani kwake” Elizabeth akaonyesha mshangao wa dhahiri kwa kauli ile ya Innocent
“Innocent Kwa nini nisimuonye Latoya kuhusiana na joka lile hatari nililoliona chumbani kwake? Maisha yake yako katika hatari kubwa kama nisipomuonya mapema kuhusiana na joka lile.Lazima litafutwe na lipatikane” akasema Elizabeth
“ Elizabeth ,Latoya anakabiliwa na mambo mengi hivi sasa kwa hiyo sidhani kama kumweleza kuhusiana na joka hilo ni jambo la busara kwa wakati huu.Zaidi ya yote Latoya huwa hapendi mambo yanayohusiana na maisha yake yajulikane na ndiyo maana hata kule katika nyumba yake ya Dare s salaam hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kuingia chumbani kwake na wala hakuna anayefahamu chumba cha Latoya kikoje.Kwa hiyo naonba kila ulichokiona mle chumbani kibaki kuwa ni siri yako na usimweleze mtu mwingine yeyote”
“Innocent mbona sikuelewi unamaanisha nini? Akauliza Elizabeth
“ Kama nilivyokwambia kwamba yote uliyoyaona chumbani kwa Latoya usimweleze mtu yeyote hata Latoya mwenyewe” akasema Inno
“ Innocent naomba maelezo ya kina ni kwa nini nisimweleze Latoya kuhusiana na joka lile kubwa ambalo linayafanya maisha yake yawe hatarini?
“Hapana Elizabeth hutakiwi kufanya hivyo”
“kwa nini Innocent? Kama hutaweza kuniambia sababu lazima nitamwambia Latoya.Siwezi kukubali kuyaona maisha ya mtu wangu wa karibu yako hatarini.” akasisitiza Elizabeth
“Latoya anafahamu kila kitu” akasema Innocent .Elizabeth akamtazama kwa mshangao mkubwa
“Unamaanisha nini….??!!!!..oh gosh …!!! Latoya anajua kama kuna joka kubwa chumbani kwake?” akauliza Elizabeth huku akimuangalia Innocent kwa macho makali.Innocent akatikisa kichwa kuonyesha kukubaliana na kile alichokiuliza
“ Ouh my gosh ! Siamini.Latoya anafahamu kuhusiana na joka lile na asinieleze kitu chochote? Kwa nini basi alinituma chumbani kwake wakati akifahamu kuna vitu vya kutisha kama lile joka? Alitaka niuliwe?
“Hapana Elizabeth.Si hivyo unavyofikiria” akasema Innocent
“Kama si hivyo nini maana ya kunituma chumbani kwake wakati akifahamu kwamba kuna joka kubwa la kutisha na la hatari? Kwa nini hakunipa tahadhari bado mapema? Hapana lazima anieleze ukweli kuhusiana na suala hli” akasema Elizabeth huku akitembea kwa kasi akitaka kutoka mle chumbani Innocent akamuwahi na kumshika mkono.
“Sikiliza Elizabeth.Kuna jambo ambalo unatakiwa ulifahamu”
“ Jambo gani Innocent? Akauliza Elizabeth
“twende bustanini” akasema Innocent halafu wakaongozana hadi bustanini wakaketi juu ya kiti cha kupumzikia

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………..

BEFORE I DIE
SEHEMU YA 62
ILI[POISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Latoya anafahamu kila kitu” akasema Innocent .Elizabeth akamtazama kwa mshangao mkubwa
“Unamaanisha nini….??!!!!..oh gosh …!!! Latoya anajua kama kuna joka kubwa chumbani kwake?” akauliza Elizabeth huku akimuangalia Innocent kwa macho makali.Innocent akatikisa kichwa kuonyesha kukubaliana na kile alichokiuliza
“ Ouh my gosh ! Siamini.Latoya anafahamu kuhusiana na joka lile na asinieleze kitu chochote? Kwa nini basi alinituma chumbani kwake wakati akifahamu kuna vitu vya kutisha kama lile joka? Alitaka niuliwe?
“Hapana Elizabeth.Si hivyo unavyofikiria” akasema Innocent
“Kama si hivyo nini maana ya kunituma chumbani kwake wakati akifahamu kwamba kuna joka kubwa la kutisha na la hatari? Kwa nini hakunipa tahadhari bado mapema? Hapana lazima anieleze ukweli kuhusiana na suala hli” akasema Elizabeth huku akitembea kwa kasi akitaka kutoka mle chumbani Innocent akamuwahi na kumshika mkono.
“Sikiliza Elizabeth.Kuna jambo ambalo unatakiwa ulifahamu”
“ Jambo gani Innocent? Akauliza Elizabeth
“twende bustanini” akasema Innocent halafu wakaongozana hadi bustanini wakaketi juu ya kiti cha kupumzikia

ENDELEA……………………….

“Haya niambie Innocent ulichotaka kuniambia” akasema Elizabeth.Innocent akakohoa kidogo na kusema
“Elizabeth Latoya ni rafiki yako wa tangu utotoni lakini bado hujamfahamu vizuri na wala hajawahi kukueleza chochote kuhusiana na yeye.”
“Hapana Innocent si kweli.Ninamfahamu Latoya vizuri sana kuliko mtu yeyote yule.” akasema Eliza
“nakubaliana nawe Elizabeth ,lakini si kila kitu unachokifahamu kwake.Kuna mambo mengine yanayomuhusu yeye peke yake na ambayo ni watu wachache sana wanaoyafahamu.” Akasema Inno
“ Ni mambo gani hayo Innocent.Unayafahamu?
“Ndiyo.Ninamfahamu Latoya japo si kiundani sana kama unavyomfahamu wewe” akasema Inno halafu akaanza kumweleza Elizabeth namna anavyomfahamu Latoya.Hakumficha kitu alimweleza kila kitu hadi alivyofanikisha kumuokoa toka kifo.Mpaka anamaliza simulizi ile Elizabeth alikuwa anatetemeka mwili mzima.Aliogopa kupita kiasi.Machozi mengi yalikuwa yanamtoka
“Kwa hiyo hayo ndiyo maisha ya Latoya ambayo hakuna aliyekuwa anayafahamu na hakutaka mtu yeyote ayafahamu.Nimekwambia haya yote kwa sababu sisi ndio watu wa karibu sana naye na ndio wenye jukumu kubwa la kuhakikisha kwamba maisha ya Latoya yanabadilika na kuwa ya kawaida.Ameaniahidi baada ya kutoka hospitali leo tutakuwa na maongezi marefu pengine kuna jambo anataka kunieleza kuhusiana na kilichotokea.Tafadhali naomba usimwambie kitu chochote kuhusiana na haya niliyokueleza hadi atakapokueleza yeye mwenyewe”
“Innocent nimeogopa sana.Mwili wote unanitetemeka.Sikuwahi kuota kama simu moja Latoya anaweza kuwa namna hii.Japokuwa niliwahi kusikia tetesi kama hizo kuhusiana na utajiri wake lakini nilizipuuza.Ni vigumu sana kuamini.Innocent siku yangu imeharibika.Nahitaji mapumziko na kutuliza akili yangu” akasema Elizabeth halafu akaaga na kuondoka zake


* * * *

Takribani masaa matano yamekwisha katika toka Latoya aanze kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na jopo la madaktari bingwa.Vipimo vilionyesha hakuwa anasumbuliwa na tatizo lolote mwilini.Mifumo yote ilikuwa inafanya kazi vizuri.Kilichowaumiza vichwa madaktari ni kidonda kikubwa kilichokuwa mgongoni mwake.Vipimo vilirudiwa zaidi ya mara tatu ili kujiridhisha kwamba haikuwa ni saratani .
Hatimaye baada ya kazi ngumu iliyowachukua zaidi ya saa nane wakakamilisha kazi yao na Latoya akapelekwa katika chumba maalum cha kupumzika.Uso wake ulionyesha wasi wasi mkubwa.Hakujua angepewa majibu gani kuhusiana na afya yake kwani aliwaona namna madaktari wale walivyokuwa wakihangaika na hivyo kumpa mashaka kwamba kuna kitu hakikuwa sawa
Baada ya saa moja na dakika kama ishirini hivi,mlango ukafunguliwa na daktari mmoja kijana akaingia
“ Madam Latoya unajisikiaje? Akauliza yule daktari huku uso wake ukiwa na tabasamu
“ Najisikia vizuri sana” akasema Latoya
“madam Latoya Madaktari wako tayari na wanahitaji kukuona” akasema Dr Edwin halafu akaongozana na Latoya hadi katika chumba walichokuwamo madaktari wale bingwa waliomfanyia uchunguzi ule wa afya yake.Mara tu Latoya alipoingia mle chumbani wakasimama wote ishara ya kumpa heshima msichana huyu ambaye alikuwa mdogo sana kiumri kwao
“Poleni sana kwa kazi ngumu ya kutwa nzima ya leo” akaanzisha mazungumzo Latoya
“ Tunashukuru sana Madam.Pole sana nawe” wakasema kwa pamoja
“Madam Latoya tumekuita hapa ili tukupe matokeo ya uchunguzi wetu” akasema Dr Bill mkuu wa jopo lile la madaktari
“Mifumo yote ya mwili inaonyesha kufanya kazi vizuri kabisa.Hakuna mahala tulikogundua tatizo lolote katika upande huu wa ufanyaji kazi wa mifumo ya mwili.” Akasema Dr Bill huku akiendela kulisoma faili lililokuwa mbele yake.
“Pamoja na mifumo yote kuwa sawa lakini tumegundua tatizo kubwa katika kidonda kilichopo mgongoni.Kwa kweli hali yake si nzuri na kimetushangaza hata sisi pia.Tulidhani labda yaweza kuwa ni saratani lakini tumefanya uchunguzi na kugundua kwamba si saratani.Uchunguzi unaonyesha kwamba kidonda hiki kimetokana na virusi waitwao Sethypothes ambao wamekuwa wakiharibu tabaka la juu la ngozi na hivyo kusababisha kidonda hiki kuzidi kukua siku hadi siku.Virusi hawa huzaliana kwa wingi sana na huzalisha sumu iitwayo Altroutraczema ambayo huingia katika mfumo wa damu na kuangamiza chembe nyekundu za damu na kukusababishia upungufu mkubwa wa damu.Madam Latoya naomba nikiri kwamba ugonjwa huu ni hatari sana kwa afya yako na tunaendelea kufanya utafiti ili tuone kama unaweza kuambukiza watu wengine.Si nia yangu kukuogopesha lakini hatua iliyofikia hivi sasa ni mbaya na tunafanya kila tuwezalo kuweza kuupatia ufumbuzi ugonjwa huu.Kitu kingine kikubwa ambacho kinatuumiza sana vichwa vyetu ni kwamba mpaka hivi sasa hatujaweza kupata dawa ya kuwaangamiza virusi hawa.Virusi wa aina hii wana gamba gumu ambalo huweza kuwakinga dhidi ya sumu ya aina yoyote ile na hivyo kuwafanya wawe ni miongoni mwa virusi wasiotibika.Tumepeleka sampuli katika chuo kikuu cha Havard kwa uchunguzi zaidi. Tutashirikiana nao katika uchunguzi huu ili tuweze kupata dawa itakayoweza kuwaangamiza virusi hawa.” Akasema Dr Bill
“ Ouh Gosh ! Hili sasa ni balaa jingine.Nitafanya nini mimi? Akawaza Latoya na kuinama chini.Wote mle chumbani wakakaa kimya.Walimuonea huruma sana binti yule mdogo mwenye ugonjwa ule wa ajabu na wa kushangaza.Latoya akainua kichwa na kufuta machozi kisha akasema
“ Dr Bill naomba unifafanulie zaidi kuhusiana na ugonjwa huu.Kutokana na maelezo yako umesema kwamba virusi hawa wanazaliana kwa wingi sana je kuna uwezekano wa kidonda hiki kukua na kusambaa sehemu nyingine za mwili? Na je kama haitapatikana dawa ina maana nitakufa? Akauliza Latoya huku macho yake yakiwa yamejaa machozi.Dr Bill akavuta pumzi ndefu na kusema
“ Madam Latoya,kuna uwezekano mkubwa sana kidonda hiki kikasambaa katika sehemu kubwa ya mwili kutokana na kukua kwa kasi kwa virusi hawa na kuendelea kushambulia sehemu ya juu ya ngozi.Hata hivyo tunaendelea kuwafanyia uchunguzi ili tujue ni sehemu zipi hasa za mwili ambazo wanazipenda “
“ Dr Bill hujajibu swali langu la pili,kama hakutapatikana dawa yoyote ,ina maana ninakwenda kufa?
“Madam Latoya ,tunajitahidi kufanya kila tunaloweza ili tuweze kupata dawa ya kuwadhibiti virusi hawa hatari.Lakini endapo itashindikana kupata dawa mapema nasikitika madam hakutakuwa na njia nyingine zaidi ya kupoteza maisha kwani kadiri virusi hawa wanavyoendelea kuzaliwa kwa wingi na ndivyo wanavyozalisha sumu kwa wingi na damu kuendelea kukauka kwa haraka.Katika uchunguzi tunaoendelea kuufanya tunataka kubaini kama sumu hiyo pia inaweza kuleta madhara mengine mwilini.Usiogope madam Latoya mimi na jopo la madaktari tukishirikiana na vyuo vikuu vya sayansi hapa Marekani tunakuahidi kufanya kila linalowezekana ili kulipatia ufumbuzi wa haraka jambo hili.Wakati uchunguzi wetu ukiendelea tutaendelea kukupatia tiba ikiwa ni pamoja na kukuongezea damu mara kwa mara.” Akasema Dr Bill.Hii ilikuwa ni taarifa mbaya sana kwa Latoya.Aliumia sana.Akainama akazama katika mawazo halafu akainua kichwa na kusema
“ Dr Bill naomba uniambie ni lini nitakufa? Ni muda gani toka sasa? Akauliza Latoya kwa hali ya kukata tamaa.
“ Madam Latoya,nakuomba usifikirie suala la kufa kwa sasa.Hilo linaweza kuokea lakini ni baada ya jitihada zote za kuwadhibiti virusi hawa kushindikana.Sisi kwa upande wetu kama madaktari ,tukishirikiana na wanasayansi tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba unapona.Kwa hiyo nakuomba madam Latoya ufute kabisa kichwani kwako mawazo ya lini utakufa” akasema Dr Bill
“ Ninaweza kumuambukiza mtu mwingine? Akauliza Latoya
“Kama nilivyokwambia awali ni kwamba kwa sasa bado hatuna uhakika kama virusi hawa wanaweza kusambaa na kwenda kwa mtu mwingine.Tutalibaini hilo katika uchunguzi wetu tunaoendelea kuufanya na endapo tutagundua kwamba virusi hawa wanaweza kusambaa kwa njia yoyote ile basi tutakutaarifu mara moja.Kwa hiyo mpaka tutakapokuwa na uhakika kwamba virusi hawa wanaweza kusambaa,unaweza ukaendelea kuchangamana na watu wako kama kawaida lakini kwa ushauri tu unaweza ukapunguza idadi ya watu unaoonana nao kwa sasa” akasema Dr Bill
“ Ahsante sana Dr Bill kwa niaba ya wote.Pamoja na hayo kuna jambo nataka kuwaomba”
“ Omba lolote madam Latoya.Tuko hapa kwa ajili yako”
“ najua jambo hili linaweza kuwa kubwa na taarifa zikasambaa dunia nzima .Nawaombeni sana jambo hili libaki kuwa ni siri yetu mimi na ninyi mlio ndani ya chumba hiki.Sitaki jambo hili lijulikane kwa sasa .Mko tayari kunisaidia kwa hilo?
“ Madam Latoya kwa sasa jambo hili litabaki kuwa miongoni mwetu lakini siwezi kukuhakikishia kwamba itaendelea kuwa hivyo siku zote.Usiri wa jambo hili utategemea sana majibu ya uchunguzi tunaoendelea kuufanya tukishirikiana na vyuo vikuu vya sayansi ya tiba.Endapo itathibitika kwamba ugonjwa huu unaambukiza basi hatutakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kuliweka wazi suala hili ikiwa ni pamoja na kuwafanyia uchunguzi watu wako wote wa karibu ili kubaini kama wameambukizwa.”
Baada ya maongezi marefu na ushauri toka kwa jopo lile la madaktari bingwa Latoya akapewa dawa mbali mbali za kumsaidia wakati uchunguzi wa kubaini dawa itakayoweza kuwaangamiza virusi wale ukiendelea
“Haya tena ni mambo mapya kabisa.Nilidhani nimekwepa kifo lakini kumbe nilikuwa najidanganya.Hawataniacha kamwe .Wataendelea kuniandama hadi wahakikishe nimekufa.Nimechanganyikiwa sijui nifanye nini” akawaza Latoya.Machozi yakamtoka akachukua kitambaa na kujifuta
“ madam are you ok? Akauliza dereva wake wakati wakirejea nyumbani
“ I’m fine “ akajibu Latoya na kuinama.Ile ndoto aliyoota usiku ikamjia tena kichwani ,akayakumbuka maneno ya yule mzee
“ haya yote umeyataka mwenyewe Latoya.Yasingekukukuta haya kama ungefuata maagizo uliyopewa.Ulikwenda nje ya makubalinao na ukaenenda katika njia uliyoitaka wewe .Usidhani umeshinda ,tutakuandama usiku na mchana.Wewe ni wetu na hautaweza kutukimbia kamwe” maneno yale yakajirudia tena kichwani kwake na kumfanya atokwe na machozi
“ tumekwisha kupiga muhuri wetu mgongoni kwako kwa hiyo kaa ukijua kwamba maumivu haya unayoyasikia sasa yataendelea daima na yatakuwa yakizidi kuwa makali lakini kuna jambo moja tu ambalo unaweza kulifanya .katka kitabu chetu kitukufu ambacho wewe umekisaliti,fungua sura ya nne na usome aya ya sita,saba na nane na maumivu yote yatakwisha na utarejea katika hali yako ya kawaida tena”
“ Ouh gosh ! wameamua kuniadhibu kwa njia hii.Kama walivyoahidi kwamba hawataniacha ni kweli wanachokisema.Kamwe hawatakubali niwe na maisha ya kawaida.Ndoto yangu ya kuwa na Innocent mwanaume nimpendaye kuliko wote inaweza isifanikiwe.Lakini hapana siwezi kukubali kumpoteza Innocent.I’ve sacrificed a lot for him.Niliweka ahadi ya kumpata kabla sijafa na tayari nimempata.Nimekaribia sana kuikamilisha ndoto yangu na kuwa mwanamke mwenye furaha hapa duniani.Nitapambana na kila jaribu ,nitavumilia mateso yote kwa lengo moja tu ….. to be with Innocent before I die. Nimenusurika kuuawa na Brandon but I know I’m going to die soon kukutokana na hali ya kidonda hiki nilichowekewa mgongoni lakini kabla sijafa lazima niwe nimeutumia muda wangu uliobaki nikiwa na mwanaume wa misha yangu” akawaza Latoya na mara sura ya Innocent ikamjia,akavuta pumzi ndefu
“ Nashindwa nimwambie kitu gani Innocent ili aweze kunielewa.Anyway I have no option than to tell him the truth.All the truth about me and my life” akawaza Latoya
Toka hospitali hadi nyumbani kwa Latoya ni mwendo wa dakika tano.Baada ya kufika nyumbani ,akashuka garini na kusalimiana na watumishi wake.Alijitahidi kutabasamu na hakutaka kuonyesha sura ya huzuni.Hakutaka kuwapa wasi wasi watumishi wake aliowapenda sana.Alihisi mwili wake umechoka ,akapanda moja kwa moja ghorofani chumbani kwake.Kitu cha kwanza kukitazama mara tu alipoingia chumbani kwake ni endapo ile madhabahu imeondolewa.Akashusha pumzi baada ya kukuta tayari imeondolewa.
“ Thank you God” akasema taratibu na kukaa akitandani.Akachukua simu na kumpigia Elizabeth lakini simu yake haikupatikana.Latoya akastuka .Hata siku moja haikuwahi kutokea Elizabeth kuzima simu zake zote
“ Elizabeth ana tatizo gani? Kwa ninavyomfahamu hajawahi kuzima simu zake zote hata ile ya nyumbani.Anyway inawezekana amepatwa na dharura” akawaza Latoya halafu akainua tena simu na kupiga chumbani kwa Innocebnt
“ Hallow “ ikajibu sauti ya Innocent
“ Hallo Innocent,unaendeleaje?
“ Ouh Latoya,bado uko hospitali?
“ Hapana Innoceht ,nimerudi si muda mrefu sana.Niko chumbani kwangu”
“Vipi unaendeleaje?
“ Naendelea vizuri Inno” akajibu Latoya
“ Nashukuru kusikia hvyo.Tayari nilikiwisha ingiwa na wasi wasi baada ya kuona muda unakwenda na hurejei”
“ Usihofu Innocent,tayari nimekwiwsha rudi.Umelala?
“ hapana sijalala niko dirishani nikistaajabu mandhari nzuri na yakupendeza kulizunguka jumba lako”
“ Innocent namtuma mtumishi mmoja aje akuchukue na akulete chumbani kwangu.I cant wait to see you”
“ Latoya huna haja ya kumtuma mtumishi,nitakuja mwenyewe hata mimi nina hamu sana ya kukuona”
“ Unafahamu kilipo chumba changu? Akauliza Latoya
“ Ndiyo ninafahamu.Nakuja sasa hivi” akasema Innocent na kukata simu.Latoya akavuta pumzi ndefu
“Ninahofu sana sijui nitaanzaje kumweleza Innocent hadi anielewe.Hata hivyo lazima nimweleze kila kitu.Nitamueleza ukweli na nina amini atanielewa.Alikwisha jitolea kuwa na mimi na tayari anafahamu maisha yangu na amekutana na mambo mengi makubwa ambayo hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kuyavumilia lakini yeye amevumilia na bado yuko na mimi.Mpaka leo bado sijapata wasaa wa kuongea naye na kufahamu aliwezaje kupambana hadi akaniokoa.Najaribu kujiuliza bila kupata majibu,Inno aliupata wapi ujasiri na nguvu ya kuweza kupambana hadi akafanikiwa kuniokoa? Nadhani ni wakati muafaka wa kufahamu pia kwa upande wake nini kilitokea” akawaza Latoya na mara mlango ukagongwa

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 63
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Usihofu Innocent,tayari nimekwiwsha rudi.Umelala?
“ hapana sijalala niko dirishani nikistaajabu mandhari nzuri na yakupendeza kulizunguka jumba lako”
“ Innocent namtuma mtumishi mmoja aje akuchukue na akulete chumbani kwangu.I cant wait to see you”
“ Latoya huna haja ya kumtuma mtumishi,nitakuja mwenyewe hata mimi nina hamu sana ya kukuona”
“ Unafahamu kilipo chumba changu? Akauliza Latoya
“ Ndiyo ninafahamu.Nakuja sasa hivi” akasema Innocent na kukata simu.Latoya akavuta pumzi ndefu
“Ninahofu sana sijui nitaanzaje kumweleza Innocent hadi anielewe.Hata hivyo lazima nimweleze kila kitu.Nitamueleza ukweli na nina amini atanielewa.Alikwisha jitolea kuwa na mimi na tayari anafahamu maisha yangu na amekutana na mambo mengi makubwa ambayo hakuna binadamu wa kawaida anayeweza kuyavumilia lakini yeye amevumilia na bado yuko na mimi.Mpaka leo bado sijapata wasaa wa kuongea naye na kufahamu aliwezaje kupambana hadi akaniokoa.Najaribu kujiuliza bila kupata majibu,Inno aliupata wapi ujasiri na nguvu ya kuweza kupambana hadi akafanikiwa kuniokoa? Nadhani ni wakati muafaka wa kufahamu pia kwa upande wake nini kilitokea” akawaza Latoya na mara mlango ukagongwa

ENDELEA……………………….

“ karibu ndani Innocent” akasema Latoya baada ya kuufungua mlango na kukutana na Innocent
“ Karibu sana Inno” akasema tena Latoya huku akimuelekeza Innocent aketi katika sofa zuri jeusi.
“ Pole sana Latoya,unaendeleaje? akasema Innocent
“ Naendelea vizuri Innocent.Zoezi la kupima afya lilichukua muda mrefu tofauti na nilivyotegemea.Umeshindaje leo? I missed you so much”
“ I missed you too Latoya.Nimeshinda salama lakini mawazo yote yalikuwa kwako.Nilitamani nikufuate hosptali” akasema Inno na wote wakacheka
“ Innocent nilishangaa ulponiambia unakifahamu chumba changu”
“ Sikuwa nakifahamu hapo kabla hadi leo hii asubuhi nilikuja humu na Elizabeth”
“ Elizabeth? Akauliza Latoya
“ Ndiyo.Nilikuja kumsaidia kuifanya kazi uliyomuagiza aifanye ya kuondoa ile madhabahu ya mawe.”
“ Ouh Nashukuru sana kwa hilo.Nimekuwa nikimtafuta Elizabeth simuni lakini simu zake zote hazipatikani .Nashangaa kwa sababu hii si kawaida yake.”
“Alipoondoka hapa aliniambia kwamba anahitaji kupumzika”
“ Anaumwa?
“Hapana haumiwi”
“Kama haumwi ana tatizo gani? Namfahamu vizuri sana Elizabeth ni mtumwa katika kazi yake na ni mara chache sana kumkuta amelala nyumbani.Lazima atakuwa na tatizo” akasema Latoya halafu akaangaliana na Innocent
“ Latoya, Elizabeth ana tatizo” akasema Inno
“ tatizo gani?
“ Asubuhi ya leo alikuja huku chumbani kwako kwa dhumuni la kuangalia namna atakavyoweza kuiondoa madhabahu ile uliyomuagiza .Alipofika humu chumbani alikutana na kitu kilichomstua sana”
“ Ouh gosh ! alikutana na kitu gani?Aliona nini? Latoya akauliza kwa wasi wasi mkubwa
“ Alikutana na joka kubwa sana ambalo hajawahi kuliona katika maisha yake”
“ ouh gosh !! Latoya akastuka sana
“ nini kilitokea?
“ Alifanikiwa kukimbia na kuja kuniita lakini nilipokuja humu chumbani sikukuta joka hilo.Elizabeth alipatwa na mstuko mkubwa sana ,ameshindwa kufanya chochote leo na akaniambia kwamba anahitaji kupumzika”
Latoya akashusha pumzi.Jambo lile likamstua sana.Akainama chini akafikiri halafu akasema
“ Kwa miaka mingi nimekuwa nikijitahidi kwa kila niwezavyo kuzuia mambo kama haya kuwatokea watu kama Elizabeth na ndiyo maana chumbani kwangu huwa haruhusiwa mtu mwingine aingie zaidi yangu.Nasikitika sana kwa alichokiona Elizabeth.Hakupaswa kukiona au kujua chochote kuhusiana na mimi kwani si watu wote wenye kuwa na uvumilivu na ujasiri kama ulivyo wewe Innocent.Toka umenifahamu umekutana na mambo mengi mazito na ya kutisha zaidi ya joka aliloliona Elizabeth lakini umeweza kuvumilia yote na hadi sasa bado uko hapa pembeni yangu.Sina hakika kama kuna mtu ambaye anaweza kuvumilia mambo kama uliyokutana nayo wewe .Kuna nyakati nashindwa kuamini kama wewe ni binadamu wa kawaida.Who are you Innocent? Are you an angel sent by God to help me? Akasema Latoya.Innocent akacheka kidogo na kusema
“ Latoya mimi ni Innocent ,rafiki yako ambaye siko tayari kukuacha hata sekunde moja.Wewe ni msichana mrembo na ambaye ninaweza kusema kuliko wote dunaini.Uzuri wako si wa sura pekee bali hata moyo.Unastahili furaha.Uso wako una stahili tabasamu muda wote na hicho ndicho pekee kitu ninachotaka kukifanya na hata kama nitakumbana na vikwazo vingi au hata kama ikinilazimu kufa then I’ll die trying” akasema Inno.Maneno yale mazito yakamliza Latoya
“ Innocent sijui nikwambie nini lakini fahamu kwamba wewe ni malaika wangu.Wewe ni binadamu wa pekee kabisa ambae umeweza kuingia katika maisha yangu na kugundua kwamba hayana furaha na ukajitahidi kwa kila namna kuhakikisha kwamba ninakuwa na furaha.Hakuna mwanadamu ambaye angeweza kusimama mahala pako kuhatarisha maisha yake kwa sababu ya mtu kama mimi.Innocent umeniokoa toka katika mikono ya kifo.Haikuwa kazi rahisi.Najua ulikutana na mambo mengi sana mazito na ya kutisha na ambayo nina hakika yalikushangaza sana na kukufanya ujiulize maswali mengi kuhusiana na mimi.Huu ni wakati muafaka wa kuyajibu maswali yako ,ni wakati muafaka wa kuufahamu undani wangu mimi ni nani .Unastahili kujua kila kitu kuhusiana na mimi.Here is my story “ akasema Latoya akainuka na kuchukua chupa ya maji ya kunywa akamimina katika glasi akanywa halafu akaketi sofani,akarekebisha koo lake tayari kwa kuianza simulizi yake
“Nilikuwa na umri wa miaka sita wakati baba yangu alipochaguliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Marekani.Tulihamia jijini Washington DC na kuanza kuishi pale.Siku moja baba alitembelewa na wageni wawili ofisini kwake.Hawa walikuwa ni Bwana na bibi Martin McKelly,mabilionea wakubwa nchini Marekani.Walikuwa wanahitaji maelekezo kuhusiana na utalii nchini Tanzania kwani walitegemea kuanza ziara ya kuizunguka dunia na kutembelea sehemu mbali mbali za kitalii na kituo chao cha kwanza kilikuwa nchini Tanzania.Baba kama balozi wa Tanzania aliwasaida sana mabilionea wale na wakafika nchini Tanzania.Walifurahi mno na baada ya kumaliza ziara yao na kurejea Marekani urafiki kati ya familia yetu na yao ukaanza.Mabilionea wale hawakujaliwa kuwa na mtoto kwa hiyo wakatokea kunipenda sana na kunihesabu kama mmoja wa wanafamilia yao.Kutokana na upendo wao kwangu waliwaomba wazazi wangu ili niende nikaishi nao katika jumba lao la kifahari.Wazazi wakakubali na nikahamia katika jumba lao la kifahari.Ni katika kipindi hiki bwana na Bi Mckelly walinihamisha toka shule niliyokuwa nasoma na kunipeleka katika shule ya watoto wa mabilionea wa Marekani.Hii ni shule inayosemekana kuongoza kwa kuwa na gharama za juu kabisa nchini Marekani.Katika shule hiyo watoto wenye asili ya kiafrika tulikuwa wawili tu kati ya watoto mia mbili na hamsini .Ukiacha mimi alikuwepo pia mtoto wa mwanamuziki mmoja tajiri sana nchini Marekani.Suala la mtoto wa balozi wa Tanzania kusoma katika shule ya watoto wa mabilionea lilitengeneza vichwa vya habari hapa Marekani na Tanzania wakihoji namna balozi huyo alivyoweza kupata pesa za kunisomesha katika shule hiyo yenye gharama kubwa.Bwana na Bi McKelly walijitokeza hadharani na kukiri kwamba wao ndio wanaonisomesha katika shule hiyo kwa sababu wananipenda na familia zetu ni marafiki wakubwa.Ni katika kipndi hiki ndipo nilipokutana na Elizabeth na kujenga urafiki ambao umedumu hadi leo hii.” Latoya akanyamaza akanywa maji na kuendelea
“Maisha katika jumba lile la bwana na Bi McKelly yalikuwa mazuri sana.Sikuwa nimewahi kuishi maisha ya kifahari namna ile.Hapo ndipo niliyafahamu maisha ya mabilionea.Niliishi kama mtoto wa mfalme.Nilitembelea magari ya kifahari sana.Nilikuwa na walinzi wangu maalum na watu wangu wa kunihudumia Nilivaa mavazi ya gharama kubwa,nilifundishwa kuvaa vito vya dhahabu na mapambo ya kila aina.Niliwahi kutolewa katika jarida moja la hapa marekani nikielezwa kama mtoto ninayeongoza kwa kuvaa vito na mapambo ya thamani kubwa nchini Marekani.Ni kweli nilikuwa mrembo .Nilikuwa napendeza na kila mtu alinisifu” akatulia akanywa maji kidogo na kuendelea
“Niliyazoea maisha ya ubilionea,nikayapenda .Baba na mama ambao kwao nilikuwa mtoto wao wa pekee waliingiwa na wasi wasi kutokana na aina ya maisha niliyoyaishi .Japokuwa bwana na Bi Mckelly waliwahakikishia kwamba hawataniacha nipotee kutokana na kuishi katika maisha ya kitajiri lakini mimi mwenyewe sikuwa tayari kuachana na maisha yale ya kifahari.Tayari nilikwisha yazoea na kuyapenda.Nilipata kila kitu nilichokihitaji ,niliheshimiwa na kupendwa.Kwa hiyo maisha haya ya ubilionea niliyaanza toka nikiwa na umri mdogo.” Latoya akatabasamu halafu akaendelea
“Nakumbuka wakati fulani shule zikiwa zimefungwa ,niliondoka na Bi Mckelly tukitumia boti yao ya kifahari .Tulikuwa tunazunguka katika visiwa mbali mbali .Tulifika hadi katika kisiwa kimoja chenye majumba ya kifahari sana.Usiku wa siku hiyo Bi McKelly alinifanyia jambo moja ambalo nililiona la ajabu mno.Aliniuliza kama ningependa kuyaona maisha yangu ya mbele namna yatakavyokuwa.Nilipatwa na mshangao kidogo kwa sababu hakuna mtu anayejua maisha yake ya mbele yatakuwaje lakini nilikuwa na hamu ya kutaka kujua namna maisha yangu ya mbeleni yatakavyokuwa.Nilimjibu ndiyo ninahitaji kuyajua maisha yangu ya usoni na akanipelekea katika jumba moja kubwa akaniingiza katika chumba kimoja chenye giza akatoka na kuufunga mlango
Mara tu alipotoka chumba chote kikajaa mwanga na mara ukutani nikaanza kuitazama filamu ya maisha yangu ya mbele namna yatakavyokuwa.Nilijiona nikiwa mwanamke tajiri mwenye nguvu na sauti.Niliuona utajiri nitakaokuwa nao .Niliona namna nitakavyopendwa na watu wengi niliyaona pia maisha yangu mazuri na ya kifahari.Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka kumi na mitatu tu.Niliyafurahia maisha yale kwani ndiyo nilikuwa nayahitaji.Tayari nilikwisha onja ladha ya maisha ya kitajiri kwa hiyo sikutaka kuishi maisha mengine tofauti na maisha ya kitajiri.Niliyastaajabia sana maajabu yale makubwa na nikamuuliza Bi Mckelly inawezekanaje mtu ukayaona maisha yako ya mbeleni akaniambai kwamba muda utakapofika atanifahamisha kila kitu.Nilikuwa na hamu sana ya kutaka kujua kuhusu namna ilivyotokea .
Nikiwa na umri wa mikaka kumi na mitano Bwana na Bi Mckelly walipoteza maisha katika ajali ya ndege.Lilikuwa ni pigo kubwa sana kwangu.Japokuwa waliacha mali nyingi lakini mali hizo zilianza kupotea moja baada ya nyingine kutokana na kutokuwa na usimamizi makini.Biashara mbali mbali zikafungwa na baadhi ya mali kutaifishwa na mabenki kutokana na madeni waliyokuwa wakidaiwa.Wakati misuko suko hiyo ikitokea baba alimaliza muda wake wa ubalozi nchini Marekani hivyo ikamlazimu kurejea nchini Tanzania.Kwa kuwa bado nilikuwa nikiendelea na masomo hapa nchini Marekani walikubali nibaki na nitakapomaliza nitarejea Tanzania.” Latoya akanyamaza akameza mate na kuendelea na simulizi ya maisha yake
“Baada ya wazazi wangu kurejea Tanzania bado sakata la kupotea kwa mali za Bwana na Bi McKelly liliendelea.Siku moja alikuja mama mmoja akajitambulisha kwangu kwamba anaitwa Virginia strawberry.Alinifahamihsa kwamba alikuwa ni rafiki mkubwa wa bwana na Bi McKelly.Viriginia alinikumbusha siku Bi McKelly aliponionyesha filamu ya maisha yangu ya usoni na akaniuliza kama nilikuwa tayari kuyaishi maisha yale niliyoyaona katika filamu.Nilikubali haraka haraka kwa sababu kwa wakati ule sikuwa na mtu niliyemtegemea na tayari nilikwisha yazoea maisha ya ubilionea Sikuwa tayari kurejea kuishi maisha ya kawaida waliyoishi wazazi wangu.Siku iliyofuata niliondoka na yule mama tukaelekea katika jiji la Sao Luis Brazil.Pale nilipelekwa kwa mtu mmoja ambaye aliitwa kwa jina moja tu la Visca.Nilikuja kugundua baadae kwamba Visca ni cheo.Visca alinipokea vizuri sana na katika maongezi yetu aliniuliza endapo nilitaka kuwa mtu mwenye nguvu na sauti duniani.Kwa mara nyingine tena nilikubali na siku iliyofuata tukaelekea katika kisiwa fulani kidogo kinachosemekana kuwepo kati kati ya Amerika kusini na Bara Afrika.Na hapo ndipo mambo yote yalipoanzia.” Latoya akanyamza tena akanywa maji na kuendelea.
“Usiku nilikutanishwa na wazee watatu wenye ndevu nyingi ambao walianza kunipa maelezo ya utangulizi.Waliniambia kwamba walikuwa ni viongozi wa mtandao wa imani ya watu wenye nguvu duniani na ili kuufahamu vyema mtandao na imani hiyo nitalazimika kupitia mafunzo ya mwaka mmoja.Kwa kuwa nilihitaji sana utajiri nilikuwa tayari kwa lolote lile kwa hiyo nikakubali kuanza mafunzo yale ya mwaka mmoja ili kuufahamu mtandao ule wa imani ya watu wenye nguvu aliousema yule mzee.Kitu cha kwanza kabisa ambacho walianza kunifundisha wale wazee ni kuhusiana na Mungu.Nilifundishwa kwamba hakuna Mungu.Ilikuwa ni vigumu kwa siku za mwanzo kukubaliana nao lakini kadiri siku zilivyozidi kwenda mbele nikajikuta nikikubaliana na hoja zao na kuamini ni kweli hakuna Mungu.Nilifundishwa kwamba mtu yeyote ambaye ana nguvu na uwezo wa kutenda jambo lolote ambalo binadamu wa kawaida hawezi kulitenda basi mtu huyo ni Mungu kwa hiyo watanifanya na mimi niwe Mungu.Baada ya miezi sita nilijikuta nikiamini kabisa kwamba hakuna Mungu.I believed there is no God and I myself is a God.” Akasema Latoya halafu akainama machozi yakamtoka. Akayafuta na kuendelea.
“Niliendelea na mafunzo yake na baada ya mwaka nikamaliza na kujiunga rasmi na mtandao ule unaoongozwa na Mungu wa giza ,shetani muasi mwenye nguvu kubwa ya ushawishi na lengo kuu la mtandao huu ni kuwalaghai wanadamu na kupoteza dira na mwelekeo wao kwa mwenyezi Mungu.Kuwajaza wanadamu anasa na starehe na kuwafanya wamsahau kabisa Mungu.Kuendeleza ugunduzi wa teknolojia mpya na za kisasa ili kuzidi kumfanya mwanadamu azidishe matendo machafu.Kuwateka kifikra kwa mitindo ya mavazi na urembo , kutumia vitu kama muziki na mitandao ili kuchochea matendo ya ngono.Hayo ni baadhi tu ya malengo ya mtandao huu wa kishetani.Nilikubali kuyatekekeleza hayo yote na nikatawazwa kuwa malkia wa kwanza mweusi wa mtandao huu.Pamoja na nguvu niliyopewa nilipewa pia masharti kadhaa.Moja ya masharti hayo ni kutokujihusisha kwa namna yoyote ile na jambo lolote linalohusiana na imani.Yaani siruhusiwi kukanyaga katika sehemu yoyote ya ibada na wala kushika vitabu vitakatifu au hata kulitaja kwa namna yoyote ile jina la Mungu.Endapo nitavunja sharti hilo la kwanza adhabu yangu itakuwa ni kumtoa sadaka mmoja wa wazazi wangu na damu yake ndiyo itakuwa imenitakasa tena.Sharti la pili nililopewa ni kwamba katika maisha yangu siruhusiwi kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote yule.Endapo ningevunja sharti hilo basi adhabu yake ni kifo.Ningeuawa na nafasi yangu kuchukuliwa na mtu mwingine.Nilikubaliana na masharti hayo na nikapigwa muhuri wa moto mgongoni kama alama ya maagano kati yangu na shetani mkuu.Muhuri huo niliopigwa ulisababisha kidonda kidogo mgongoni ambacho hakikuwa kikisababisha maumivu yoyote yale lakini kila pale ambapo nitakuwa nikienda kinyume na taratibu basi ningesikia maumivu makali sana ikiwa ni pamoja na kupoteza fahamu .Baada ya muhuri ule wa maagano kugongwa , nilivishwa kidoleni pete yenye nguvu ambayo kwa kupitia kwake ningeweza kusema kitu chochote kile na kikatokea,ningeweza kusababisha majanga ,maafa na kitu chochote kile.I was powerfull,very powerfull.They named me “Female black God”

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 64
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Moja ya masharti hayo ni kutokujihusisha kwa namna yoyote ile na jambo lolote linalohusiana na imani.Yaani siruhusiwi kukanyaga katika sehemu yoyote ya ibada na wala kushika vitabu vitakatifu au hata kulitaja kwa namna yoyote ile jina la Mungu.Endapo nitavunja sharti hilo la kwanza adhabu yangu itakuwa ni kumtoa sadaka mmoja wa wazazi wangu na damu yake ndiyo itakuwa imenitakasa tena.Sharti la pili nililopewa ni kwamba katika maisha yangu siruhusiwi kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote yule.Endapo ningevunja sharti hilo basi adhabu yake ni kifo.Ningeuawa na nafasi yangu kuchukuliwa na mtu mwingine.Nilikubaliana na masharti hayo na nikapigwa muhuri wa moto mgongoni kama alama ya maagano kati yangu na shetani mkuu.Muhuri huo niliopigwa ulisababisha kidonda kidogo mgongoni ambacho hakikuwa kikisababisha maumivu yoyote yale lakini kila pale ambapo nitakuwa nikienda kinyume na taratibu basi ningesikia maumivu makali sana ikiwa ni pamoja na kupoteza fahamu .Baada ya muhuri ule wa maagano kugongwa , nilivishwa kidoleni pete yenye nguvu ambayo kwa kupitia kwake ningeweza kusema kitu chochote kile na kikatokea,ningeweza kusababisha majanga ,maafa na kitu chochote kile.I was powerfull,very powerfull.They named me “Female black God”

ENDELEA………………………..
Hapo ndipo nilipoufungua ukurasa mpya katika maisha yangu.Nilianza kujulikana duniani kote.Nilifungua miradi mingi na kila mradi niliouanzisha uliniingizia fedha nyingi sana.Nilikuwa na biashara katika kila pembe ya dunia.Miradi mingine ilifunguliwa na watu hata nisiowafahamu kwa jina langu.Akaunti zangu zilifurika pesa.Nilitekeleza maagizo niliyopewa kwa kuanzisha makampuni mbali mbali ya nguo na vifaa vya elektroniki.Nguo nyingi zilizotengenezwa katika viwanda vyangu ni zile zenye kuhamasisha matendo ya ngono.Niliwatumia watu wenye majina makubwa na ushawishi duniani ili waweze kuzitangaza bidhaa za kampuni yangu.Kwa hili nilifanikiwa kwa kiasi kikubwa.Nilipeleka pesa nyingi pia katika kusaidia uvumbuzi wa kisayansi na kukuza teknolojia.Tulianzisha mpango wa kusambaza kompyuta kwa kila mwanafunzi ulaya.Lengo likiwa kukiteka kizazi cha watoto angali bado wadogo wajifunze na wafahamu matendo mbali mbali yakiwemo ya ngono na kuwafanya wahamasike na kushiriki vitendo hivyo.Kwa kupitia watu wakubwa na maarufu duniani tulihamasisha na kuchochea matendo ya mapenzi ya jinsia moja na mpaka hivi sasa watu wameonekana kuyakubali na wanayaona ni matendo ya kawaida na kuyafurahia.Tulitaka kizazi hiki cha watoto wadogo wajifunze hayo yote na hivyo kutengeza dunia iliyojaa maasi makubwa kwa Mungu.Ilianzishwa pia mitandao ya kijamii na idadi kubwa ya watu tayari wameipenda na ina mamilioni ya wafuasi duniani kote.Kupitia mitandao hii watu wanakutana na kujenga mahusiano yanayopelekea matendo ya ngono kuongezeka.Mitandao hii vile vile hutumika kujenga chuki miongoni mwa jamii moja na nyingine na kujenga mafarakano miongoni mwa mtu mmoja mmoja.Kupitia makampuni yangu tulifadhili pia mitandao ya kigaidi duniani na hivyo kuongeza mauaji ya watu wasio na hatia.Tulijenga hospitali kubwa kubwa duniani ambazo ziliongoza kwa matendo ya utoaji mimba.Haya ni baadhi tu ya mambo machafu yanayofanywa na mtandao huu wa kishetani lengo likiwa ni kupoteza idadi kubwa ya wanadamu.Innocent naomba ufahamu kwamba hali ni mbaya na watu wengi wanapotea kila siku katika mikono ya huyu mwovu.Maelfu kwa maelfu ya watu wanaangamia na kupotea kila uchao.Shetani anawatumia wanadamu katika kufanikisha malengo yake na anafanikiwa sana.” Latoya akanyamaza akainama akayafuta machozi na kuendelea.
“Mtandao huu umewahusisha watu wengi sana na wengine ni wakubwa na wenye majina na ushawishi duniani.Wamo pia viongozi mbali mbali wa dini na serikali.Miongoni mwao alikuwepo pia kardinali Gadner Barkov wa Brazil.Huyu alikuwa ni mtu mwenye nguvu na sauti kubwa katika kanisa .Ushiriki wake katika mtandao huu ulikuwa wa siri kubwa na ni watu wachache ambao walifahamu kama alikuwa ni kiongozi wa juu wa mtandao huu wa kishetani.Gadner alitokea kuwa rafiki yangu mkubwa na alinipenda sana.Kila mara katika vikao vyetu kama kuna mahala nilikosea au sikufanya vizuri basi yeye ndiye aliyekuwa mtetezi wangu.Ilitokea siku moja Gadner alinipigia simu usiku wa manane na kuniambia kwamba kesho yake nifanye juu chini nionane naye .Siku iliyofuata nilikwenda Brazil kuonana naye.Gadner alinieleza kwamba alipata maono akiwa usingizini.Alionyeshwa namna watu wanavyoangamia ,dunia inavyoangamia na maelfu ya watu wanavyopotea kila siku kutokana na mambo tunayoyafanya.Alionyeshwa idadi kubwa ya watu ambao tumekuwa tukiwasukumia katika shimo la moto mkubwa.Alionyeshwa pia idadi kubwa ya watu walio katika mtandao wetu ambao walikuwa wakiungua katika moto wa mkubwa.” Latoya akanyamaza akavuta pumzi ndefu na kusema
“Bado nayakumbuka maneno ya Gadner akiniambia kwamba
“Latoya tunawapoteza watu wengi sana na adhabu yetu ni kubwa machoni pa Mungu.Tunatakiwa tuiokoe dunia .Tunatakiwa tuache kuyafanya haya tunayoyafanya sasa na kumrudia Mungu wetu.Mungu wa kweli ambaye hakuna zaidi yake”
“ Gadner alinifumbulia kwamba hata marafiki zangu wawili ambao nao pia walikuwa ni wafuasi wa mtandao huu Melisa na Anna wako katika moto huo wakiungua.Nilistuka na kuogopa sana.Sikujua nifanye nini lakini Gadner akaahdi kunisaida nini cha kufanya.Baada ya siku tatu nilipata taarifa kwamba Gadner yu mgonjwa mahututi..Nikaenda haraka Brazil kumjulia hali .Aliponiona aliwaomba watu wote watoke nje tukabaki wawili tu mimi na yeye .Alinishika mkono wangu na kuniambia neno moja tu “ Latoya save the world” halafu akakata roho mikononi mwangu.Sikujua nifanye nini baada ya hapo.” Latoya akanyamza akafuta machozi na kisha akanywa maji kidogo na kuendelea na simulizi yake
“Nilipata wakati mgumu sana bada ya kifo cha Gadner na sikujua ningewezaje kuuokoa ulimwengu huu wakati tayari nilikwisha weka maagano na shetani.Siku moja mmoja wa wafanyakazi wangu alifariki dunia.Alikuwa ni mfanyakazi ambaye nilimpenda sana na niliumizwa mno na kifo chake.Bila kujitambua siku hiyo nikajikuta nimeingia kanisani kwa ajili ya ibada ya kumuombea marehemu.Nikiwa kanisani nilisikia kuna kitu kinanigusa moyo wangu.Nilisikia kama kuna sauti inaniita na kusema kwa uchungu
“ Latoya kwa nini unanitesa? Kwa nini unawaangamiza watu wangu?
“Nilifahamu sauti ile haikuwa ya binadamu.Nililia machozi mengi sana siku hiyo baada ya kugundua namna nilivyomuacha Mungu wa kweli na kumuangukia Mungu wa giza. Kila aliyeniona mle kanisani alidhani kwamba ninalia kutokana na kuguswa na kifo cha mfanyakazi wangu kumbe nilikuwa nikililia mambo mengine kabisa.Baada ya hapo nikahudhuria katika harambee ya ujenzi wa kanisa na nikatoa mchango mkubwa sana na hapo ndipo matatizo katika mgongo wangu ile sehemu niliyopigwa muhuri wa moto wa maagano yalipoanza.Nilikuwa nikisikia maumivu makali kupita kiasi yaliyonipeleka mara nyingine kuanguka na kupoteza fahamu na nilipozinduka nilijikuta nikiwa nimepoteza damu nyingi sana.Nilianza kuwa na mateso na maumivu makali mno kila siku na maisha yangu yakakosa furaha. Kuna nyakati nilitamani hata kufa kuliko kuendelea na mateso na maumivu yale niliyokuwa nikiyapata kila siku.Kutoka na hali hii ilinilazimu kutafuta daktari wa kunitibu na ili kuendelea kuificha siri ya ugonjwa wangu ilinilazimu kumfanya awe bubu na aliweza kuongea na mimi tu. Pamoja na mateso na maumivu yale makali lakini sikuacha kujitolea katika kujenga nyumba za ibada na adhabu yangu ikaongezeka.Viongozi waligundua kwamba nilikuwa nimetetereka kwa hiyo wakamuandaa mrithi wangu ambaye ni Brandon. Walianza kuniogopa pengine siku moja ningekuja kuwasaliti kwa hiyo wakaanza kujiandaa mapema.Niliendelea na ujenzi wa nyumba za ibada na kuanza kuifunga baadhi ya miradi ambayo ilikuwa ikifadhili matendo ya ugaidi ,utoaji mimba na ushoga na hapo ndipo nilipohukumiwa kifo.Nilianza kuwa mtu hatari kwao na tayari nilikwisha kiuka maagano.” Latoya akasimama na kuvuta pumzi ndefu na kusema
“Niliambiwa kwamba nitakutana na mrithi wangu katika msiba lakini sikufahamu ni msiba wa nani kumbe alikuwa ni mama yangu.Baada ya kumuua mama yangu nilipatwa na hasira sana na sikushiriki katika kitendo cha kunywa damu ya mama yangu kwa ajili ya kunitakasa na kunifanya mpya tena.Nilichoshwa na maisha yale na nilitamani kuishi maisha mengine yenye furaha na amani..” Machozi mengi yakamtoka Latoya akayafuta na kuendelea
“Siku ninaapishwa kuwa malkia wa giza,moja ya masharti niliyopewa ni kutojihusisha na suala lolote la mapenzi na wala sikutakiwa kuwa na mpenzi.Hili ni jambolililoniumiza mno kwani nilijikuta nikitamani kuwa na mpenzi na mimi nifurahie maisha kama wanawake wengine na hapo ndipo nilipowekaahadi ya lazimanimpate mwanaumewa ndotozangukablasijafa.Nilijitoa mhanga lakini tatizo likawa nitampata wapi mwanaume huyo?Nafahamukatika dunia ya sasa kunaulaghai mwingina wengi wa wanadamu hawana mapenzi ya kweli.Nilijua nitakufa hivi karibuni na nilitaka niyafurahie mapenzi na si kuteswa nayo.Pamoja na mambo yote niliyomkosea Mungu lakini bado aliendelea kuwa mwema kwangu na akanipatia kile ambacho nilikuwa nakitaka na kumuomba kila siku yaani mwanaume wa maisha yangu.Innocent you are that man of my dreams.Ni wewe ambaye niliamini nitakupata kablasijafa.Ni wewe ambaye nilikupenda kabla hata ya kukuona.Ni wewe ndiye niliyekuwa nakuota usiku na mchana.Ni wewe ndiye uliyeufanya moyo wangu uteseke kila siku na kukiuka maagano na Mungu wa giza..Innocent nakupenda sana kwa moyo wangu wote.Nakupenda zaidi ya ninavyoweza kukueleza.Nakupenda zaidi ya ninavyojipenda mimi mwenyewe”
Latoya akanyamaza na machozi mengi yakaendelea yakamtoka.Innocent ambaye uso wake ulikuwa umeloa jasho kutokana na simulizi ile ya Latoya alishindwa aseme kitu gani.Kutoka moyoni mwake alimpenda sana Latoya na ndiyo maana alikuwa tayari kufanya kila jambo kwa ajili yake.Siku zote alitamani kumweleza ukweli lakini aliogopa kufanya hivyo kutokana na mazingira yaliyomzunguka.Latoya bado aliendelea kulia kwa kwikwi,Innocent akanyanyuka sofani na kumuendea akaketi karibu yake na kumshika bega
“Pole sana Latoya.Nyamaza usilie.I’m here now for you.I’m here to stay”
Maneno yale ya Innocent yakamfanya Latoya anyanyue kichwa chake na kumtazama usoni.
“ Mara ya kwanza Sabrina aliponitamkia jina lako nilihisi kustuka na kutamani kuonana nawe.Nilikupenda kabla hata sijakutia machoni na siku ile nilipokuona kwa mara ya kwanza nilihisi kama vile nimeonana na malaika.Mapigo yangu ya moyo yalibadilika na niliona kama dunia imesimama.Nilimshukuru Mungu kwa kunikutanisha nawe kwani niliamini wewe ndiye yule ambaye nilikuwa nakuota usiku na mchana.Nilifahamu matatizo ninayokwenda kukutana nayo kwa kukupenda lakini tayari nilikwisha jitoa mhanga kwa lolote lile.Nilitamani sana nikwambie ukweli kwamba wewe ndiye mwanaume wa maisha yangu lakini kila nilipojaribu kufanya hivyo kulitokea kizingiti na kunizuia nisikutamkie ukweli wa moyo wangu.Kabla ya kuanza kwa safari ile nilitokewa na watu wawili wakaniambia kwamba ile safari ni safari yangu ya mwisho na kwamba nisingerejea tena kwani nilikuwa naenda kufa.Walinionya kwamba katika safari ile nisithubutu kuambatana nawe lakini kwa kuwa ninakupenda na wewe ndiye mwanaume wa ndoto zangu sikuwa tayari kufuata matakwa yao kwa hiyo nikaambatana nawe .Nilitaka nitumie hata siku mbili nilizokuwa nimebaki nazo pamoja nawe.Tukiwa safarini nilijaribu kutaka kukueleza ukweli lakini ikapiga ile radi na wewe kupotea.Sikukuona tena hadi ulipojitokeza kule kisiwani na kuniokoa toka kifo.Innocent najua umekumbana na vikwazo vingi sana na umeshuhudia mambo mengi makubwa na mazito.Naomba unisamehe sana Innocent kwa kukufanya ukaingia katika dunia ya giza isiyoonekana kwa macho ya kawaida na yenye mambo ya kutisha mno. ” Latoya akashindwa kujizuia na kuangua kilio.
“ Nyamaza kulia Latoya.Ni kweli nimekutana na mambo ya ajabu sana yasiyosimulika lakini nimeweza kuyashinda yote .Nilifanya yale yote niliyoyafanya kwa sababu ya upendo wangu mkubwa kwako.Latoya naomba na mimi nikiri kwamba ninakupenda sana na siku zote nimekuwa nikisubiri wakati muafaka ili niweze kukueleza ukweli wa moyo wangu namna gani ninavyokupenda.Mimi na wewe hatujajuana muda mrefu lakini siku ile ya kwanza tu nilipokuona nilihisi kuna muunganiko mkubwa kati yangu nawe.Uliingia moyoni mwangu toka sekunde ya kwanza kukutia machoni.Moyo wangu haukunidanganya kwamba wewe ndiye mwanamke wa maisha yangu na kukutana kwetu haikuwa ni kwa bahati mbaya.Ulinikaribisha nyumbani kwako na baada ya msiba wa Marina nilishindwa kabisa kuondoka kwa sababu nilihitaji kuwa karibu nawe.Nilijisikia furaha na amani niwapo karibu yako na ndiyo maana nimeweza kuvumilia yote mateso na magumu na nimekuwa na nguvu ya kupambana na yeyote yule aliyetaka kukudhuru.Latoya naomba nikiri kwamba mwanzoni nilipoanza kuishi pale nyumbani kwako nilipatwa na wakati mgumu sana kutokana na mambo niliyoyaona.Kuna nyakati nilitaka niondoke lakini moyo wangu haukuwa tayari kuondoka na kukuacha peke yako.Macho yangu yalikutazama hadi ndani kabisa ya moyo wako na kugundua kwamba haukuwa na furaha katika maisha yako.Niliweka ahadi ya kufanya kila niwezalo ili kukufanya uwe na furaha tena.Nilikumbana na majaribu mengi makubwa na ya kukatisha tamaa lakini niliyavumilia yote kwa sababu ya upendo wangu mkubwa kwako.Nakumbuka siku moja nikiwa nimelala niliota ndoto yenye uhalisia mkubwa .Nilikuwa sehemu fulani nikiwa na wazee Fulani na wakaniambia kwamba nitakuwa mlinzi wako na nikulinde dhidi ya wale wote wanaotaka kukuangamiza na mwisho wa yote mimi nawe tuiokoe dunia.Sikufahamu ni nani aliyekuwa anataka kukuangamiza .Baada ya kunipa maagizo yale waliuunguza mkono wangu wa kulia kwa moto.Nilipostuka nilisikia maumivu makali katika mkono wangu wa kulia maumivu ya kuungua moto.Siku hiyo ndiyo mama yako alipopoteza maisha.Nakumbuka ulirudi nyumbani ukiwa na simanzi nikataka kupeleka mkono wangu mgongoni kwako kwa lengo la kukufariji lakini nilipigwa na kitu kama chaji za umeme na pale pale mkono wangu ukapona.Yalikuwa ni mambo ya kustaajabisha sana kwangu.Wakati tukielekea nyumbani kwa wazazi wako kuonana na mjomba wako ambaye alikuzuia usikanyage msibani,nilipitiwa na usingizi na nikamuona tena Yule mzee mwenye ndevu nyingi na kanzu nyeupe pamoja na mshipi mwekundu kiunoni akaniambia kwamba niyasome maandishi yaliyokuwa katika ubao alioushika.Niliyasoma maandishi yale na akaniambia kwamba muda wowote ninapohitaji msaada basi niyatamke yale maneno niliyoyasoma katika ule ubao.Sikuyaelewa maana yake.Maneno yale ndiyo niliyoyatumia nyumbani kwenu na watu wote akiwemo mjomba wako na wazee wa ukoo wakanisikiliza na kutii kila nilichowaambia.” Akasema Innocent halafu akanyamaza kidogo na kumtazama Latoya ambaye macho yake hayakukaukiwa machozi.Akamfuta machozi na kuendelea.
“Siku ile tulipokuwa melini ulitaka kunieleza jambo lakini kabla hujatamka jambo ikapiga radi kubwa na sikuona kitu chochote tena zaidi ya giza nene.” Innocent alipofika hapa akanyamaza na kisha akavuta pumzi ndefu halafu akamueleza Latoya kila kitu kilichotokea hadi alipofanikiwa kumuokoa.Latoya akashindwa kuvumilia akalia machozi mengi.
“ Nyamaza kulia Latoya.Mambo haya yamekwisha na kilichobaki ni sisi kuangalia mambo ya mbele.Hakuna cha kuhofia tena”
Latoya akafuta machozi na kumtazama Innocent kisha akasema
“ Innocent sipati neno la kuweza kukushukuru kwa kazi kubwa uliyoifanya.Najua haya yote yamewezekana kwa msaada mkubwa wa Gadner ambaye lengo lake kubwa ni kuusambaratisha mtandao huu wa kishetani na kuzuia watu wasiendelee kupotea.Nashukuru umeniokoa Innocent.Lakini pamoja na hayo bado kuna tatizo kubwa”
“ tatizo gani Latoya?
“ Nilifanya maagano na shetani na kuahidi kutekeleza kila atakachoniagiza na kama ishara ya kuyalinda maagano yetu nilipigwa muhuri wa moto mgongoni muhuri ambao ni kidonda kidogo ambacho hakikuwa na maumivu wala madhara yoyote hadi pale nilipokwenda kinyume na maagano yetu.Pamoja na kuniokoa lakini bado hawajakata tamaa na lengo lao ni kuhakikisha ninapata mateso makali sana na kisha kuwarudia.Baada ya kuniokoa kutoka kule kisiwani,kidonda kile kilichokuwa kidogo,kimekuwa kikiongezeka kwa kasi na kuwa kikubwa na cha kutisha.Kibaya zaidi imebainika leo katika uchunguzi kwamba kidonda kile kimesbabishwa na virusi waitwao Sethypothes ambao ni virusi hatari wanaozaana kwa wingi wa ajabu ndani ya kipindi kifupi.Virusi hawa huzalisha kemikali iitwayo Altroutraczema ambayo ni sumu na huingia katika mfumo wa damu na kuua chembe nyekundu za damu na hivyo kunisababishia upungufu mkubwa wa damu.Virusi hawa wana tabia ya kubadilika na mpaka hivi sasa bado madaktari hawajaweza kugundua dawa ya kuwaangamiza. Na kutokana na kuzaliana kwa wingi wa ajabu inamaanisha kwamba kama haitapatikana dawa ya kuwaangamiza then I’m going to die very soon.” Akasema Latoya na uso wa Innocent ukaonyesha mstuko mkubwa
“No That’s not possible.There must be a way.!! akasema Innocent
“Innocent hakuna dawa ya kuweza kuwaangamiza virusi hawa kwa sasa kwa hiyo naomba niwe wazi kwako kwamba nitakufa hivi karibuni.I’m so sorry Inn…….” Latoya akashindwa kujizuia kulia kwa sauti kubwa.Innocent akahisi kuchanganyikiwa hakuelewa afanye nini.
“Innocent nasikitika sana kufa katika umri huu mdogo.Nilitamani sana kuendelea kuishi maisha ya furaha nikiwa nawe mwanaume wa maisha yangu lakini haitawezekana tena.Simlaumu mtu yeyote kwani mambo haya yote nimeyataka mimi mwenyewe.Tamaa ya mali na utajiri vimeniponza na sasa nitaviacha vyote.Pamoja na kupata vitu vyote nilivyokuwa navitaka sikuwahi kuwa na furaha katika maisha yangu hadi pale ulipotokea lakini nimechelewa sana.Sintaweza kuipata nafasi ya kufurahi pamoja nawe.Inaniuma sana kwani siku zote nilitamani kuishi maisha marefu nikiwa nawe hadi tufike uzeeni.” Machozi mengi yaliendelea kumtoka Latoya.Innocent naye alishindwa kujizuia machozi yakamtoka

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………
[07:17, 9/27/2016] PATRIC PENIELA: BEFORE I DIE
SEHEMU YA 65
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Virusi hawa huzalisha kemikali iitwayo Altroutraczema ambayo ni sumu na huingia katika mfumo wa damu na kuua chembe nyekundu za damu na hivyo kunisababishia upungufu mkubwa wa damu.Virusi hawa wana tabia ya kubadilika na mpaka hivi sasa bado madaktari hawajaweza kugundua dawa ya kuwaangamiza. Na kutokana na kuzaliana kwa wingi wa ajabu inamaanisha kwamba kama haitapatikana dawa ya kuwaangamiza then I’m going to die very soon.” Akasema Latoya na uso wa Innocent ukaonyesha mstuko mkubwa
“No That’s not possible.There must be a way.!! akasema Innocent
“Innocent hakuna dawa ya kuweza kuwaangamiza virusi hawa kwa sasa kwa hiyo naomba niwe wazi kwako kwamba nitakufa hivi karibuni.I’m so sorry Inn…….” Latoya akashindwa kujizuia kulia kwa sauti kubwa.Innocent akahisi kuchanganyikiwa hakuelewa afanye nini.
“Innocent nasikitika sana kufa katika umri huu mdogo.Nilitamani sana kuendelea kuishi maisha ya furaha nikiwa nawe mwanaume wa maisha yangu lakini haitawezekana tena.Simlaumu mtu yeyote kwani mambo haya yote nimeyataka mimi mwenyewe.Tamaa ya mali na utajiri vimeniponza na sasa nitaviacha vyote.Pamoja na kupata vitu vyote nilivyokuwa navitaka sikuwahi kuwa na furaha katika maisha yangu hadi pale ulipotokea lakini nimechelewa sana.Sintaweza kuipata nafasi ya kufurahi pamoja nawe.Inaniuma sana kwani siku zote nilitamani kuishi maisha marefu nikiwa nawe hadi tufike uzeeni.” Machozi mengi yaliendelea kumtoka Latoya.Innocent naye alishindwa kujizuia machozi yakamtoka


ENDELEA……………………

“ Hapana Latoya,usiseme hivyo.You wont die.You wont die “
“ Innocent hakuna namna ya kuweza kufanya labda ipatikane tiba ya virusi hawa vinginevyo I must die.I’m going to die Innocent” akasema Latoya.Akasimama na kuvua koti lake jeusi pamoja na kuipandisha juu fulana aliyokuwa ameivaa akamuonyesha Innocent kidonda kilichopo mgongoni.Innocent akastuka na kuogopa kutokana na hali ya kidonda kile.
“ Ouh Mungu wangu ! akasema Innocent
“ Innocent hiyo ndiyo hali halisi niliyonayo.Hakuna namna nyingine ya kukizuia na kukitibu kidonda hiki.Madaktari wamenihakikishia hivyo.I must die “ akasema Latoya kwa huzuni
“ Hapana Latoya,huwezi kufa.Please don’t say that again.You wont die.We must find a way”
“ Innocent najua unanipenda kwa moyo wako wote na ninafahamu umeumizwa sana na jambo hili .Hata mimi pia nimeumia sana kiasi kwamba ninahisi kama moyo wangu unakatwa vipande vipande lakini hatuwezi kupingana na ukweli kwamba nitakufa muda si mrefu lakini kabla sijafa kuna mambo ambayo nataka kuyafanya”
“ hapana Latoya usiseme hivyo.Moyo wangu unaumia mno.Why you have to die Latoya? No ! you cant die.” Akasema Innocent.Macho yake yalifunikwa na machozi
“ Innnocent naomba unisikilize.Hapo kabla ndoto yangu ilikuwa ni kumpata mwanaume wa maisha yangu ,nitakayempenda kuliko kitu chochote kabla sijafa.Ndoto hiyo tayari imetimia na nimekwisha kupata.Pamoja na kukupata lakini sintaweza kuishi na kufurahi nawe kwa muda mrefu.I must die Innocent.There are things I must do before I die” akasema Latoya.Innocent akafuta machozi na kupiga magoti akamtazama Latoya
“ Latoya naomba unisikilize.I’m not Go,I don’t have any power but I wont let you die.Latoya ugonjwa huu umesababishwa na maagano uliyoyafanya na shetani kiumbe ambaye ameumbwa na Mungu.Ni Mungu pekee mwenye uwezo wa kuamua hatima ya maisha ya mtu na si mwanadamu au kiumbe mwingine yeyote yule.I believe in God.Ni yeye pekee anayeweza kusema kitu na kikawa Latoya umemkosea sana Mungu lakini siku zote yeye amekuwa anatupenda hata pale tunapomkosea kwa kiwango cha juu sana na anatupa tena nafasi nyingine ya kutubu dhambi zetu na kumrejea.Hii ni nafasi nyingine umepewa ya kutubu dhambi zako na kujiweka katika mikono mitakatifu na yenye nguvu ya Mungu. Ni wakati sasa wa kuamua kubadili maisha yako na kumrudia bwana Mungu wa majeshi.So answer me do you believe in God?.
Latoya akafuta machozi na kusema
“I do Innocent.I do believe ni God…”
“Good…Fahamu kwamba ni yeye tu ambaye ana uwezo wa kukuponya ugonjwa huu.Kuna kanisa lolote hapa karibu? Akauliza Innocent.Latoya hakujibu kitu akabaki anamtazama
“ Latoya kuna kanisa lolote hapa karibu tunakoweza kumpata mtumishi yeyote wa Mungu? Akauliza tena Innocent lakini kabla Latoya hajajibu chochote kikatokea kitu cha ajabu sana.Macho ya Latoya yakabadilika na kuwa meupe na ulimi ukamtoka.Akaanguka sofani.
“ Latoya ! Latoya ! Innocent akaita lakini Latoya alikuwa amekakamaa pale sofani na povu lilikuwa linamtoka mdomoni.Innocent akaogopa sana.
“ Ouh Mungu wangu tafadhali muokoe Latoya. Akasema Innocent .Akili yake ikafanya kazi haraka haraka akashuka chini na kuomba aelekezwe mahala lilipo kanisa.Watumishi wote wakashangaa kwa hali ile aliyokuwa nayo Innocent na kwa haraka akapanda garini pamoja na dereva wa Latoya wakaondoka kwa mwendo wa kasi kuelekea kanisani.Walitumia dakika kama kumi hivi kufika kanisani na moja kwa moja Innocent akaingia katika ofisi ya askofu.Huku akihema akamwambia askofu Pater Wirth waongozane ili akamfanyie Latoya maombi.Bila tatizo askofu Peter akakubali na wakaingia garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu kurejea katika makazi ya Latoya.Walipofika moja kwa moja wakapanda ghorofani huku wakikimbia hadi chumbani kwa Latoya.Askofu peter alipoiona hali ya Latoya alistuka
‘ Tumkimbize hospitali” akasema Askofu Peter
“ Hapana baba askofu huu si ugonjwa wa hospitali.Tunahitaji maombi yako ndiyo maana nimekufuata” akasema Innocent na askofu Peter akaomba aletewe ndoo ya maji na chumvi kisha akayabariki akachanganya na chumvi ile kuanza kufanya maombi huku akimnyunyizia maji Latoya aliyekuwa amelala sofani.Wakati akiendelea kuomba huku akimnyunyizia maji ghafla kitu cha ajabu kikatokea.Mwili wa Latoya ukaanza kutoa kitu mfano wa moshi.Innocent akaogopa sana.Askofu Peter hakustuka akaendelea kuomba kwa nguvu na kumnyunyizia maji na mara Latoya akaanza kugala gala na kuanguka sakafuni.Innocent akataka kumshika lakini askofu Peter akamzuia akaendelea kuomba Latoya akaanza kutapika damu halafu akanyoosha mikono na kulala kifudi fudi.
Askofu Peter alikuwa anatokwa na jasho jingi akamuinamia Latoya na kumuita
“ Latoya ! Latoya ! ..” Latoya hakutikisika .Askofu akamgeukia Innocent ambaye alikuwa amesimama huku akiwa na wasi wasi mkubwa
“ nahisi kuna kitu kizito mno humu ndani ambacho bado kinamfunga Latoya” akasema askofu Peter .Mara moja Innocent akakumbuka kitu
“ Kitabu..” akasema na kutoka mbio hadi chumbani kwake na kurudi na kitabu mkononi akamkabidhi askofu
“ Hiki ni kitabu chenye ibada za kishetani.” Askofu peter akakishika kitabu kile akakitazama na kukiweka chini akaanza kuomba huku akikimwagia maji yaliyobarikiwa.Taratibu chumba chote kikaanza kujaa moshi .Sauti mbali mbali za mivumo zikasikika.Zilisikika pia sauti za viumbe wa ajabu ajabu zikipiga kelele.Ilikua ni hali ya kuogofya sana lakini askofu Peter hakuogopa akaendelea na maombi .Chumba kikajaa moshi na ghafla moshi ule ukatoweka na biblia ile haikuonekana tena.Ilikuwa imetoweka na badala yake pale chini palionekana ndege mkubwa mweusi akipiga mbawa zake mara tatu na kuruka akatokea dirishani na kutokomea porini.Wakati akiruka alisababisha upepo mkali mle chumbani uliowasukuma askofu Peter na Innocent wakaanguka chini
“ Mungu wangu !!!..akasema askofu Peter akishangazwa na maajabu yale.Hakuwahi kushuhudia mambo ya ajabu na yakutisha kama yale toka alipoanza kazi hii ya utumishi wa Mungu
Baada ya dege lile kutoweka,wakainuka na kumwendea Latoya.Kitu cha kushangaza ile damu aliyokuwa akitapita Latoya iliyokuwa imetapakaa sakafuni ilikuwa imetoweka Latoya alikuwa mkavu na hakuonekana na hata chembe moja ya damu.
“ Latoya ! Latoya ..! akaita Innocent .Latoya akaitika kwa saut ya mbali sana
“ Unajisikiaje Latoya?
“ Maumivu..naumwa sana.” Akasema Latoya kwa taabu.Alionekana yuko katika maumivu makali mno.Innocent akamvua lile koti jeusi alilokuwa amevaa na ndipo askofu Peter akastushwa na kidonda kikubwa mgongoni mwa Latoya
“ Jesus Christ !! akasema askofu na kushusha pumzi.Akachukua maji na kunyunyiza juu ya kile kidonda huku akifanya maombi.Kila tone la maji lilipoanguka juu ya kidonda lilionekana kutoa moshi na Latoya akasikia maumivu makali sana akapiga kelele kwa sauti kubwa na kupoteza fahamu.Baada ya kupoteza fahamu askofu Peter akaamuru Latoya apelekwe hospitali kwani kidonda kile kilikuwa katika hali mbaya.Gari la wagonjwa likaitwa likaja kwa haraka na kumkimbiza Latoya hospitali.Wakati akikimbizwa hospitali Innocent na askofu Peter waliendelea na maombi .Baadaye askofu Peter na Innocent wakaelekea katika chumba cha maongezi na Innocent akamsimulia askofu Peter kila kitu kuhusiana na Latoya bila kumficha.Alianza kwa kumuelezea historia nzima ya Latoya.Hakuficha kitu chochote alieleza kila kitu.Alieleza namna walivyokutana na maisha yake na hadi alipofanikiwa kumuokoa kule kisiwani.Ilikuwa ni simulizi iliyomuacha kinywa wazi askofu Peter.Alitetemeka sana kwa simulizi ile.Akainua mikono juu na kumshukuru Mungu kwa yote halafu akamuomba Innocent apige magoti.Akamuombea na kumbariki kisha wakaongozana hadi hospitalini ambako aliendelea na maombi mengine kwa Latoya.Bado Latoya hakuwa na fahamu
Saa mbili za usiku Elizabeth alifika pale hospitali akihema na kuonyesha sura ya kuchanganyikiwa.Alitaka kujua hali ya Latoya.Bado Latoya hakuwa na fahamu.Innocent akamtuliza .
“Innocent nimechanganyikiwa hapa nilipo na sijui wapi pa kuanzia.Tafadhali nipe hali halisi ya Latoya” akasema Elizabeth kwa wasi wasi
“ Usiwe na hofu Elizabeth..Latoya atapona tu.Mungu atamsaidia” akasema Innocent
‘Innocent kuna jambo kubwa limetokea jioni ya leo”
“ Jambo gani hilo? Akauliza Innocent kwa wasi wasi
‘makao makuu yetu New York City yameteketea kwa moto na hakuna hata kitu kimoja kilichookolewa.Kila kitu kimeteketea”
“ Mungu wangu ..!! Innocent akasema kwa mstuko akashika kichwa chake
“ Nini kimesababisha moto huo?
“ hakuna anayefahamamu chanzo cha moto huo lakini kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba moto huo uliibuka ghafla na ulikuwa mkubwa kiasi cha kushindwa kudhibitiwa.Idadi isiyojulikana ya watu waliokuwamo ndani ya jengo hilo inasemekana wamepoteza maisha.Nilikuwa nimezima simu lakini kuna mtu alinifuata nyumbani akanieleza na nilipompigia simu Latoya kumfahamisha ndipo nilipoambiwa kwamba amekimbizwa hospitali.Innocent whats going on? Kwa nini mambo haya yanatokea sasa? What are we going to do? Nimechanganyikiwa Innocent.Nyaraka zote muhimu zimeteketea na sielewi nini tutafanya kuzipata tena.” Akasema Elizabeth huku machozi yakimtoka.Innocent akamtuliza na kumsimulia kila kitu kilichotokea nyumbani kwa Latoya na ghafla Elizabeth naye akaanguka na kupoteza fahamu

* * * *

Kuendelea kupona kwa haraka kwa kidonda cha Latoya kuliwashangaza mno madaktari na wanasayansi ambao waliokuwa wakivifanyia utafiti virusi vya Sethypothes waliokuwa wamesababisha kidonda kile virusi ambao hakukuwa na dawa yenye kuweza kuwaangamiza.Ni siku ya nane sasa Latoya akiwa bado amelazwa hospitali akiendelea na matibabu
Kupona kwa haraka kwa kidonda hiki kulichangiwa na maombi yaliyofanywa kila siku na askofu Peter ambaye kila uchao alifika hospitali akafanya maombi
Kwa sasa Latoya alikuwa anaendelea vizuri na aliweza hata kuinuka na kukaa mwenyewe kitandani.Kwa muda wa wiki nzima habari kuu iliyotawala vyombo mbali mbali vya habari duniani ni kuhusiana na kuungua moto kwa makao makuu ya kampuni ya Latoya ijulikanayo kama Latoya the world Co Ltd na kuteketeza kila kitu kilichokuwamo ndani.Bado chanzo cha moto huo uliosababisha kuungua moto kwa kampuni hii kubwa duniani yenye mamia ya makampuni ndani yake hakikujulikana .Kuungua kwa jengo hili kulisababisha mabilioni ya dola kupotea kwani kumbu kumbu nyingi muhimu zilipotea.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa Elizabeth ambaye ndiye alikuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hii kubwa
Mchana huu Latoya akiwa chumbani hospitali Innocent akawasili akiwa ameongozana na askofu Peter.Uso wa Latoya ulikuwa umepambwa kwa tabasamu pana
“ Wow ! at last the African queen is back” akasema Innocent kwa furaha.Alifurahi sana kumkuta Latoya akiwa katika hali ile ya tabasamu kubwa.
“ Ouh Innocent my king..” akasema Latoya halafu akaikunjua mikono yake na kukumbatiana kwa furaha.Askofu Peter alibaki anatabasamu
“Unaendeleaje Latoya ? akauliza askofu Peter
“Naendelea vizuri sana baba askofu.Mungu ameniokoa.Amenirejeshea tena maisha yangu” akasema Latoya huku akishindwa kuyazuia machozi kumtoka
“Mwanangu,Mungu ni mwema sana na siku zote anatupenda .Hata pale tunapomkosea lakini bado yuko tayari kutupokea pale tunapotubu na kujuta dhambi zetu”
“Baba askofu ninataka kurejea katika kundi la watoto wa Mungu.Ninataka nitubu dhambi zangu makosa yangu yote na ninataka kubadilisha maisha yangu.Nimemkosea sana Mungu na sijui nifanye nini ili aweze kunisamehe.Naomba unisaidie baba askofu nahitaji kumrudia Mungu tena” akasema Latoya Askofu Peter akamtazama kwa makini na kuiona nia ya dhati ya kutaka kutubu dhambi zake zote
“ Latoya,siku zote bwana Mungu yuko tayari kumsamehe mtu yeyote anayetubu dhambi zake na kumuweka katika kundi la watoto wake.Katika Isaya 1:18 anasema “ sasa njooni nasi tunyooshe mambo kati yetu asema Yehova.Hata dhambi zenu zikiwa nyekundu zitafanywa kuwa nyeupe kama theluji,hata zikiwa nyekundu kama kitambaa ,zitakuwa nyeupe kama sufu”
Askofu peter akamuomba Innocent atoke nje akabaki mle chumbani na Latoya ambaye aliitumia nafasi ile kujuta na kutubu dhambi zake.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 66
“Unaendeleaje Latoya ? akauliza askofu Peter
“Naendelea vizuri sana baba askofu.Mungu ameniokoa.Amenirejeshea tena maisha yangu” akasema Latoya huku akishindwa kuyazuia machozi kumtoka
“Mwanangu,Mungu ni mwema sana na siku zote anatupenda .Hata pale tunapomkosea lakini bado yuko tayari kutupokea pale tunapotubu na kujuta dhambi zetu”
“Baba askofu ninataka kurejea katika kundi la watoto wa Mungu.Ninataka nitubu dhambi zangu makosa yangu yote na ninataka kubadilisha maisha yangu.Nimemkosea sana Mungu na sijui nifanye nini ili aweze kunisamehe.Naomba unisaidie baba askofu nahitaji kumrudia Mungu tena” akasema Latoya Askofu Peter akamtazama kwa makini na kuiona nia ya dhati ya kutaka kutubu dhambi zake zote
“ Latoya,siku zote bwana Mungu yuko tayari kumsamehe mtu yeyote anayetubu dhambi zake na kumuweka katika kundi la watoto wake.Katika Isaya 1:18 anasema “ sasa njooni nasi tunyooshe mambo kati yetu asema Yehova.Hata dhambi zenu zikiwa nyekundu zitafanywa kuwa nyeupe kama theluji,hata zikiwa nyekundu kama kitambaa ,zitakuwa nyeupe kama sufu”
Askofu peter akamuomba Innocent atoke nje akabaki mle chumbani na Latoya ambaye aliitumia nafasi ile kujuta na kutubu dhambi zake.

ENDELEA……………………….

BAADA YA WIKI TATU

Ni wiki ya tatu sasa imepita toka Latoya alazwe hospitali na kidonda chake kimepona.Huu ulikuwa ni muujiza mkubwa kwani madaktari bado hawakufanikiwa kupata dawa ya kuwangamiza virusi wale hatari
Hali yake iliendelea vizuri na akaruhusiwa kutoka hospitali akarejea nyumbani.Usiku wa siku hiyo aliyoruhusiwa kurejea nyumbani kuliandaliwa chakula maalum kwa ajili ya kuwashukuru wale wote waliokuwa pamoja naye katika kipindi kigumu cha ugonjwa na matatizo.Ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwa Latoya
Baada ya chakula cha usiku alielekea katika bustani yake iliyo juu ya ghorofa akiambatana na Innocent
“Innocent sijui nianzie wapi lakini naomba nichukue nafasi hii toka ndani kabisa ya moyo wangu nikushukuru sana kwa yote uliyonifanyia.Kwangu mimi nakuona wewe kama malaika wangu uliyetumwa kuja kuniokoa.Bwana Mungu amekutumia kunitoa upotevuni na kunirejesha nuruni.Haikuwa kazi rahisi lakini umepambana bila kuchoka na hatimaye leo hii niko hai bado.Umetimiza maneno yako uliyonitamkia kwamba uko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili ya kunifanya niwe ni mwenye furaha.Ninafuraha sasa.Moyo wangu umejawa na furaha.Maisha yangu yana nuru mpya.Innocent siwezi kupata neno zuri la kuielezea furaha niliyonayo” Latoya akanyamaza kidogo na kuendelea
“ Katika kipindi hiki kifupi ,nimejifunza kitu kimoja kikubwa.Nimejifunza kwamba maisha ni zawadi ambayo tunapewa na Mungu na kwa hiyo ni hiari yake Mungu kutujalia kuiona kesho.Kwa hiyo basi hatuna budi kuishi kila siku kama siku yetu ya mwisho hapa duniani.Tuishi kadiri ya mapenzi yake Mungu.Tutende matendo mema ,tuwajali masikini na wenye mahitaji na tuenende katika njia iliyo njema.Nimenusurika kifo kwa hiyo ninayafahamu vyema haya niyasemayo.Nilichungulia kuzimu na sitaki tena kurudia maisha yale.Mungu amenipa nafasi nyingine ambayo sitaki kuipoteza hata kidogo.Sitaki tena kumkosea kwani wote wafao bila kutubu dhambi zao hupotea.Kwa maana hiyo basi kuna mambo mawili muhimu ambayo nataka kuyafanya katika maisha yangu mapya.” Latoya akanyamaza akamtazama Innocent usoni na kusema
“Jambo la kwanza ninalotaka kulifanya ni kuzifunga na kuuza biashara zangu zote na fedha nitakazozipata nitazitumia katika kuanzisha biashara ambazo hazitakuwa na machukizo mbele za Mungu.Nitaanzisha makampuni ya kusindika vyakula,dawa za binadamu na nguo.Faida itakayopatikana ,nitaipeleka katika watu watu wenye uhitaji mkubwa wa msaada kama vile nchi zenye vita za wenyewe kwa wenyewe.Katika kambi za wakimbizi,na hata katika nchi zinazokabiliwa na umasikini mkubwa.Mungu anapenda tuutumie utajiri tulionao kwa manufaa ya wengine.Tutajikita vile vile katika miradi ya kuondoa umasikini katika jamii masikini kwa kujenga mashule,mahospitali , na bila kusahau kumjengea bwana nyumba zake za ibada ili watu wengi waweze kumtukuza na kumuabudu yeye pekee.Hili si jukumu dogo lakini nina imani kwa msaada wa Mungu na kwa uwepo wako karibu yangu nitaweza kufanya hayo yote niliyokwambia.Tutazunguka na kutoa misaada sehemu mbali mbali duniani na hivi ndivyo Mungu anataka tuishi.Tuyatoe maisha yetu kwa wenzetu.Tuhubiri upendo kwa vitendo.” Akasema Latoya halafu akanyamaza na kumtazama Innocent
“ Latoya kuna jambo ambalo nadhani bado hujaelezwa.Tulisubiri muda muafaka uwadie ndipo ufahamishwe”
“ Jambo gani hilo Innocent? Kuteketea kwa ofisi yangu? Akauliza Latoya huku akitabasamu
“ Umejuaje kama ofisi yako iliteketea? Akauliza Innocent kwa mshangao
“ Nilionyeshwa ndotoni namna ofisi yangu ilivyoteketea kwa hiyo nafahamu kila kitu.Hizi zote ni hatua za shetani kutaka kuchukua mali na vitu vyake.Mapambano haya yataendelea kila siku na vitu vingi vitapotea lakini mkono wenye nguvu wa Mungu aliye hai utatukinga dhidi ya kila ovu na hila za huyu mwovu.”akasema Latoya halafu kikapita kimya klifupi
“ Innoceht utakumbuka kwamba niliweka ahadi ya kumpata mwanaume wa maisha yangu kabla sijafa ahadi hiyo ikatimia.Innocent wewe ni zawadi kubwa kwangu ambayo kwayo nitaendelea kumshukuru Mungu siku zote.Wewe ni furaha yangu,pumzi yangu,wewe ni maisha yangu wewe ni kila kitu kwangu.Siwezi kuishi bila ya wewe.Wewe ni lulu ya thamani kubwa na kamwe sintakuwa tayari Lulu hii iniponyoke mikononi mwangu.Kwa sababu hiyo basi jambo la pili ambalo nataka kulifanya mapema sana ni kufunga nawe ndoa”
Innocent akaruka kwa furaha
“ OuhLatoya I love you,I love you soo much.” Akasema Innocent wakakumbatiana huku wote wawili machozi yakiwatoka

MIEZI SITA BAADAE

Kila mtu aliyekuwamo ndani ya ufukwe huu alikuwa na furaha ya aina yake.Shangwe na ndremo vilitawala katika ufukwe huu mkubwa uliokuwa umefurika watu wa kila tabaka.Walikuwepo mabilionea wakubwa wa ndani na nje ya nchi,viongozi mbali mbali wa serikali wa ndani na nje ya nchi,wawakilishi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa na yale ya binafsi.Ni sherehe iliyowakutanisha watu wa kila tabaka kuanzia mabilionea hadi masikini wa chini kabisa.Kwa muonekano wake ilionekana ni kama sherehe ya kitaifa kutokana na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu.Hii ilikuwa ni harusi ya kihistoria ya bilionea Latoya na mchumba wake Innocent ambao walifunga ndoa katika kanisa la Mt Patrick na baadae kufuatiwa na sherehe kubwa na ya aina yake katika ufukwe mkubwa unaolizunguka jumba la Latoya ambalo lijengwa upya baada ya kuungua moto.
Ni miezi takribani sita sasa toka Latoya aliponusurika kifo na kuamua kuachana na mtandao wa kishetani na kumrudia Mungu.Baada ya kunusurika aliushangaza ulimwengu pale alipotangaza kufunga na kuuza biashara zake zote .Wengi walimlaumu kwa maamuzi haya lakini hakurudi nyuma.Aliendelea kuushikilia msimamo wake na kufanikiwa kuyauza makampuni yake yote .Kama ilivyokuwa katika mipango yake,fedha alizozipata alizitumia katika kuanzisha makampuni mapya ya kutengeneza vyakula ,madawa ya binadamu na nguo.Aliyasambaza makampuni yake sehemu mbali mbali duniani kwa lengo la kurahisisha utoaji wa misaada kwa watu masikini.Wengi wa watu masikini waliufurahia uamuzi huu wa Latoya na kumuombea maisha marefu.Huu ulikuwa ni mwanzo wa maisha mapya ya bilionea Latoya mwanamke ambaye aliwahi kutumika katika mtandao wa kishetani na kuitwa Black female God kutokana na nguvu na uwezo aliokuwa nao.
Wakati sherehe zikiendelea Innocent akapewa nafasi ya kusema machache
“Ndugu zangu ,wageni waalikwa mabibi na mabwana,nashukuru kwa nafasi hii niliyopewa ya kusema machache.Kwanza kabisa nawashukuru nyote kwa kufika kwenu.Wengi wenu mmetoka katika kila pembe ye dunia kuja kuungana nasi.Latoya na mimi tunasema ahsanteni sana na Mungu awabariki. ” akasema Innocent baada ya kupewa nafasi ya kuongea machache katika harusi yao iliyofurika watu.Makofi mengi yakapigwa halafu akaendelea
“ Jambo la pili ninalotaka kulisema leo ni kwamba ,sote tumeumbwa na Mungu ,anatupenda ,anatujali kwa hiyo hatuna budi kuishi kulingana na maagizo yake.Ametuagiza tupendane kwa hiyo tupendane kama anavyotupenda yeye.Unapompenda mwenzio ,mpende kwa moyo wako wote, na uwe tayari hata kuutoa uhai wako kwa ajili yake.Huo ndio upendo wa kweli ambao tunapaswa kuuishi.Kila moja aliyeko hapa leo hii ajiulize nafsini mwake Je yuko tayari kuyaweka rehani maisha yake kwa ajili ya yule ampendaye? Kama ndiyo basi hongera sana lakini kama bado hauwezi kufanya hivyo kwa ajili ya yule umpendaye badilika sasa na ujitoe kwa ajili ya wale uwapendao.Ahsanteni sana na Mungu awabariki”
Yalikuwa ni maneno machache sana lakini mazito toka kwa Innocent ambaye siku hii ya leo alikuwa amependeza mno.Watu walimshanghilia sana hadi aliporejea kitini kukaa.Ikafuata zamu ya Latoya naye akaombwa aseme machache
“ Ndugu wageni waalikwa ,mabibi na mabwana,kwanza kabisa napenda nimshukuru Mungu kwa kunijalia nafasi hii muhimu ya kusimama mbele yenu na kusema nanyi machace.Tayari mume wangu mpenzi amekwisha toa shukrani zetu kwa kufika kwenu.Ndugu zangu wapendwa tumekusanyika hapa leo kwa sababu Mungu amependa tuwepo hapa.Ametujalia uzima na afya tele.Wengi walitamani sana kuwa nasi siku ya leo mahala hapa lakini hawajaweza kufika siku ya leo.Kwa sisi kuendelea kuishi hadi dakika hii kwanza tunapaswa kumshukuru sana Mungu na pili tunapaswa kuishi kila siku kama siku yetu ya mwisho.Hakuna kati yetu anayejua kama ataiona kesho.Ni Mungu pekee ambaye anajua hatima ya maisha ya kila mtu kwa hiyo tusithubutu kuichezea zawadi hii ya maisha au kuitumia visivyo.Tuitumie vizuri .Umepewa zawadi hii kwa malengo maalum ambayo unatakiwa uyakamilishe kabla hujafa.Kwa hiyo basi jiulize leo What am I suppose to do before I die”What do I want to achieve before I die? Whats my dream before I die? As for me I had a dream.My dream was to find a man of my life,a man that I’ll will love deeply with all my heart.Here I am today,standing before you proudly thanking God for helping me achieve my dream before I die.I’ve married a man that I love with all my heart.A man of my dream,a man that is worth to die for.” Makofi mengi yakapigwa halafu akaendelea
“ Kwa hiyo ndugu zangu tujenge tabia ya kujikumbusha kwamba siku moja tutakufa lakini tuzoee kujikumbusha vile vile kwamba nini ni ndoto zetu za kuzitimiza kabla hatujafa.Kila siku asubuhi unapoamka na kabla ya kulala usiku hili ndilo liwe neno lako kuu la kufikiria “ BEFORE I DIE” Asanteni sana”
Makofi mengi sana yakapigwa.Shangwe kubwa ikasikika wakati Latoya akirejea kuketi.Sherehe zikaendelea hadi saa nne za usiku ambapo Innocent na Latoya wakaondoka wakaeleeka hotelini na kuwaacha bado watu wakiendelea kusherehekea
“ Latoya katika ile hotuba yako fupi,umenifundisha jambo kubwa sana.Ni hotuba iliyokuwa na msisimko mkubwa.Kwa sasa baada ya kwamba tumekwisha kuwa mwili mmoja tujiulize na sisi whats our dream before we die?
Latoya akatabasamu na kusema
“we have lots of dreams but the first one is to make love all night long.Ouh Innocent I’m dying to be in your arms..Please take me to the moon” akasema Latoya kwa sauti laini .Bila kutaka maongezi zaidi Innocent akamvuta Latoya karibu yake na kumpagawisha kwa mabusu mazito mfululizo na kumfanya aanze kuweweseka.Innocent akaendelea kumtomasa sehemu mbali mbali za mwili wake na kumfanya Latoya apandwe na uchizi kutokana na raha aliyokuwa akiisikia.Hatimaye walishindwa kuvumilia na mara wakajikuta wakiogelea katika bahari pana sana ya mapenzi yenye raha isiyoelezeka.Kilichosikika humo chumbani ni vilio na miguno ya kimahaba.Latoya akaingizwa rasmi katika ulimwengu wa mahaba.Mwanzo mpya wa maisha yake akiwa na mwanaume ambaye aliweka ahadi ya kumpata kabla ya kufa kwake na tayari amekwisha mpata.

TAMATI
 
someni haraka ili ni bwage story nyingine wakati tukimsubilia PENIELA .ni bandika banduaa.

bila kusahau kufanya kazi kwa bidii.maana ukitumbuliwa huko usije kuizingizia JF

HAPA RIWAYA TUU
Asante sana LEGE duuuh stori nzuri na yenye mafundisho mengi sanaaa....ila PENIELA namsubiri kwa hamu kubwa
 
someni haraka ili ni bwage story nyingine wakati tukimsubilia PENIELA .ni bandika banduaa.

bila kusahau kufanya kazi kwa bidii.maana ukitumbuliwa huko usije kuizingizia JF

HAPA RIWAYA TUU
We jamaa ni mkali sana,inawezekana ni Innocent mwenyewe,nimeshamaliza,shusha vitu,wengine watatukuta mbele
 
someni haraka ili ni bwage story nyingine wakati tukimsubilia PENIELA .ni bandika banduaa.

bila kusahau kufanya kazi kwa bidii.maana ukitumbuliwa huko usije kuizingizia JF

HAPA RIWAYA TUU
Oooooops done bonge la story shusha nyingine mkuu
 
Asante sana. Nimeimaliza.nzuri ila mimi bado namuwaza penny. inafundisha money can't give you happines.ila hadithi za mashetani mwisho wake ni ule ule.ku confess na kuombewa .ya penny ina twist and turn, un expected,betray.naisubiri kwa hamu.nakushukuru kwa kutufurahisha humu
 
shukrani sana mkuu na hongera kwako. tatizo ni kuwa kwa sie wengine mda huwa unatukaba sana. mbona hii story nimeiachia sana hata ya penieli nayo speed yake ilikuwa sio ndogo kwa siku lazima niachie sehem 10 .wakati ile ya dany kule kwa wiki nzima hazifiki hata sehem 5? hata ningeamua kuweka kila siku sehem 1 hiyo ya peniel ingekuwa bado sana mbichi .lkn huwa najitahidi ninapopata mda naweka sehem nyingi nikiwa na maana
Tunakuelewa LEGE wala usijari mkuu kuwa na Amani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom