Simulizi: Before I die

Lege usichopenda kufanyiwa usimfanyie binadam mwenzio asee,haya ni mateso bila chuki sasa
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 31


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

" Kama ndoto ile isingekuwa ya kweli nisingeamka na kujikuta na maumivu haya ninayoyasikia katika mkono ule ule ambao niliota ukiunguzwa moto.Naanza kuwa na wasi wasi mkubwa na maisha ya hapa.Nyumba hii inaonekana kuwa na mauza uza mengi .Nakumbuka Irene aliniambia kuhusu mambo yaliyowapata watu waliojaribu kutaka kuchungulia ndani ya ghorofa hii ya juu ambayo ni ya Latoya pekee.Sikuwa nikiamini mambo yale aliyonieleza Irene lakini baada ya ndoto hii niliyoota nikiunguzwa moto na kweli baada ya kuamka nakuta kweli mkono wangu ukiwa na maumivu makali sana nimeanza kuamini kwamba hapa kuna mambo mazito sana yanayoendelea.Latoya ni nani hasa? Mbona anaanza kunipa wasi wasi? Binti mzuri namna hii mwenye uzuri uliotukuka kwa nini anaishi katika maisha yaliyojaa utata mwingi namna hii? Ninaanza sasa kupata picha kwa nini mzee Curtis alikuwa akinitaka nimchunguze Latoya kwa sababu maisha yake yenye utata hata yeye kama baba yake yamemshangaza sana." akawaza Innocent kisha akainuka akaenda katika kabati la nguo na kuchukua shati lingine akavaa.Mkono wake wa kulia alihisi kama umekufa ganzi.



ENDELEA………………………


" Najaribu kutafuta maana ya ndoto ile lakini sielewi ilikuwa na maana gani.Mzee yule kwa nini alinikabidhi upanga na kusema kwamba kuanzia sasa mimi ndiye mlinzi wa Latoya? Nimlinde dhidi ya nani? Nani anayetaka kumdhuru? Kama nisingeamka na kukuta mkono wangu ukiwa na maumivu ya kuungua moto ningeamini ile ilikuwa ni ndoto tu ya kawaida lakini nimeota ninaunguzwa mkono wangu na kuamka kweli mkono ule ule nilioota unaunguzwa moto unaonekana kuungua.Nalazimika kuiamini ndoto hii na kuona kwamba haikuwa ndoto ya kawaida.Lazima kuna jambo hapa si bure.Lazima ndoto ile ina maana fulani .Nani ambaye anaweza akanipa tafsiri sahihi ya ndoto ile? Naogopa hata kumsimulia mtu yeyote yule kuhusu ndoto hii nikiogopa yasije yakanikuta mambo mengine.Mwenye kuweza kunipa majibu ya maswali ninayojiuliza ni Latoya pekee lakini nitaanzaje kumuuliza maswali kama haya kwa sababu itaonekana ni kama vile ninayachimba maisha yake kitu ambacho hakipendi Nitakaa moyoni na ndoto hii.Sintamweleza mtu yeyote yule." Akawaza Innocent akaenda kuketi katika sofa lililokuwa mle chumbani.

" Kuna wazo limenijia hapa.Nadhani suluhisho la mambo yote haya ni kuondoka hapa nyumbani kwa Latoya haraka iwezekanavyo.Naona nikiendelea kukaa hapa ninaweza kuingia katika mambo mengine ambayo yatanifanya nipoteze mwelekeo mzima wa maisha yangu na kushindwa kutimiza malengo yangu.Wazo hili ni la msingi sana na ninahisi ndilo litakuwa ni suluhisho la kuondokana na mambo ya ajabu ajabu yaliyomo ndani ya jumba hili.Hii ndoto ya leo imenistua na kuniogopesha mno.Nimeanza kumuogopa sana Latoya. Japokuwa ni mtu mwema na ana roho nzuri lakini siwezi kuendelea kukaa hapa zaidi ya siku ya leo.Itanibidi leo hii hii niondoke zangu.Nitasingizia jambo lolote lile la dharura litakalonifanya niweze kuondoka hapa.Mahala hapa si salama hata kidogo kwa mimi kuendelea kuishi.Lazima niondoke leo hii hii.Bado nina kiasi cha kutosha cha pesa katika akaunti yangu ambazo nina imani zinaweza kunisaidia kuyaanza maisha yangu.Nitatafuta nyumba ya kuishi na kuanzisha biashara yangu mwenyewe hata kama ni ndogo lakini itanisaidia kuweza kuishi kwa amani .Nitam..................." Wakati akiendelea na mawazo yake akastuliwa na mlio wa kengele ya simu.Akainuka na kwenda kuipokea.
" Hallo.." akasema Inno

" Hallo Innocent.ni mimi Irene ninaongea.Tunakuomba uje huku chini Madam Latoya amesema ana mazungumzo na watu wote wanaoishi katika nyumba hii." Innocent akawaza kidogo halafu akasema

"Ok Irene ninakuja sasa hivi" akasema Innocent.
"Innocent unaumwa? akauliza Irene

" kwa nini unauliza hivyo Irene? akauliza Innocent
"Sauti yako imebadilika sana na unasikika kama mgonjwa"

" Hapana siumwi Irene.Niko sawa kabisa.Nimeamka toka usingizini muda si mrefu.Ok nakuja huko chini sasa hivi" akasema Innocent na kukata simu.Akasimama na kuvuta pumzi ndefu

"Kuna kitu gani tena kimetokea hadi Latoya akataka kuonana na watu wote waliomo katika jumba hili? Naogopa hata kuonana naye,naogopa pengine atakuwa amekasirishwa na kitendo cha mimi kukorofishana na baba yake.Lakini sioni kama nilifanya kosa lolote kwa sababu mzee Curtis alinitaka nifanye kitu ambacho sikuwa tayari kukifanya na ndiyo maana tukapishana kauli.Ngoja niende nikasikie hilo jambo analotuitia watu wote halafu nitaitumia nafasi hiyo kumuaga kwamba nitaondoka jioni ya leo.Siwezi kulala usiku wa leo ndani ya nyumba hii" akawaza Innocent huku akivaa koti lake tayari kwa kushuka chini.Akapiga hatua mbili akasimama
" Nahisi miguu mizito sana hata kutembea.Nimekuwa muoga sana wa kuishi katika jumba hili." akawaza Innocent kisha akaanza tena kupiga hatua akafungua mlango na kutoka chumbani kwake akashuka chini.Mwili wake alihisi baridi kali na mkono wake bado ulikuwa na maumivu japo alijitahidi kujizuia ili mtu yeyote asigundue kama yuko katika maumivu makali.Alifika katika sebule kubwa na kuwakuta watumishi wote wamekusanyika pale.Wote wakamuangalia kwa mshangao ,akaanza kupatwa na wasi wasi kwa namna walivyokuwa wakimuangalia.

" Mbona wananiangalia nama hii? Wamegundua kwamba siko sawa ? Hapana..Sidhani kama wamegundua lolote kuhusu kilichonitokea.Nahisi kuna jambo linaendelea hapa." akawaza Innocent na mara Irene akamkaribisha kiti akaketi.



* * * *




Taratibu Latoya akafumbua macho na kujikuta amelala chini sakafuni.Akahisi kuishiwa nguvu akabaki amelala pale pale chini.Akakumbuka kilichotokea muda mfupi uliopita kilichompelekea apoteze fahamu.Akavuta pumzi ndefu na kuuma meno kwa uchungu.

"nahisi ninaanza kushindwa kuvumilia tena mateso na maumivu haya niyapatayo ambayo yamekuwa yakizidi kila siku.Najua siku zangu zimebaki chache sana lakini naomba kabla ile siku yangu haijafika ambayo ninajua iko karibu sana naomba niwe na nguvu ya kuweza kuyavumlia mateso haya makali ili niweze japo kwa muda mfupi kufurahi nikiwa na mwanaume ninayempenda sana katika dunia hii.Japo kwa muda mfupi tuu niitimize ahadi yangu niliyoweka kwamba kabla sijafa natakiwa niwe nimempata mwanaume ambaye nitakufa nikiwa ninampenda kwa moyo wangu wote .Tayari mtu ninayempenda amekwisha fika kwangu na yuko katika himaya yangu."akawaza Latoya na ghafla akakumbuka kitu fulani.
"Nakumbuka ni kama kuna mahala nimemuona Innocent....Yah ! it was him..sura yake na sauti ni kama yeye kabisa...nimemuona wapi? Was it in a dream? No ! it doesn’t look like it was a dream..it was so real..." akawaza Latoya na kisha akainuka pale sakafuni alikokuwa amekaa na kuikuta damu nyingi imetapakaa.Akaitazama na kuangusha machozi.Akaifuta damu ile huku akilia halafu akaenda kuoga.Wakati akioga akakumbuka tena kuhusu Innocent.

"Ni kweli nilimuona Innocent tena nakumbuka kuna mtu alimkabidhi kitu kama upanga na kumwambia maneno fulani ambayo sikuyasikia vizuri.Nakumbuka mara ya mwisho niliona kitu kama moto ukishuka katika mkono wa Innocent na kumfanya apige kelele kubwa..What kind of a dream is this? akajiuliza Latoya kisha akaendelea kuoga
" I dont have to worry about this dream..I'm used to crazy dreams like this one." akasema kwa sauti ndogo Latoya kisha akaendelea kuoga halafu akarudi chumbani kwake.Akajitazama katika kioo mwili wake mwororo wenye kila aina ya uzuri akatoa tena machozi.

" I'm so beautiful...so young...kwa nini ninateseka namna hii? Why I' going to die this young? akawaza Latoya akiendelea kujiangalia katika kioo.Akageuka ili aweze kujiangalia kwa nyuma machozi mengi yakamtoka.
"Its getting worse everyday...I'm gonna die soon.Very soon I'll die...." akawaza Latoya akaanza kuvaa.
"Ouh nimekumbuka niliwambia watumishi wote wajikusanye ninataka kuongea nao halafu ndipo nianze kushughulika na msiba wa mama yangu..Ouh mama !!..... Latoya akajikuta akianza kulia tena.
Alivaa gauni refu jeusi bila kusahau koti lake refu jeusi na kichwani aliifunga kitambaa cheusi kuonyesha kwamba alikuwa katika msiba.
Watu wote waliokuwa wamekusanyika pale sebuleni walipomuona wakasimama kwa adabu.Akawafanyia ishara wakae.Baada ya kukaa katika kiti chake akasema
"Ndugu zangu nmewaita hapa ili kuweza kufahamishana mambo machache na zaidi sana ikiwa ni maelekezo na kukumbushana mambo kadhaa.Kikubwa ambacho ninataka kuwakumbusha ni kwamba ninyi nyote ni ndugu zangu na siku zote tunaishi kama ndugu.Siwahesabu kama watumishi wangu bali ndugu zangu.Kama ndugu yenu ninasikitishwa sana pale mmoja wa ndugu zangu anapojaribu kwenda kinyume na maadili ya kazi yake wakati mwingine kwa tamaa tu ya fedha.Leo mchana kuna tukio limetokea hapa.Baba yangu mzee Curtis aliteleza akaanguka wakati akipanda ngazi na ninawashukuru watu waliokuwepo karibu kwani walimsaidia na kumkimbiza hospitali .Tukio lile lilipotokea kuna mwenzetu mmoja ambaye aliwapigia simu waandishi wa habari na kuwataarifu juu ya kilichotokea hapa.Nilifika hospitali na kukuta kundi kubwa sana la waandishi wa habari nikajiuliza wamezipataje taarifa zile mapema namna ile.Kusema ukweli sikufurahishwa na kitendo alichokifanya huyu mwenzetu.Siku zote tunakumbushana kwamba kitu chochote unachokiona hapa ndani unakiacha hapa hapa na hupaswi kumweleza mtu yeyote yule.Lakini mwenzetu huyu amekuwa akilipwa fedha na waandishi wa habari ili aweze kuwapa habari za kila kitu kinachoendelea katika jumba hili. ndugu zanguni kuna mtu yeyote yule ambaye amewahi kuja kwangu na kuniomba kiasi chochote kile cha pesa au msaada wa namna yoyote ile nikashindwa kumsaidia? Mbona watoto wenu wote ninawasomesha nje ya nchi? Nyote nimewanunulia magari ya kifahari,nimewajengea nyumba za kifahari na ninawapa kila kitu mnachokihitaji sasa kwa nini urubunike na hivi vijisenti vidogo ili uweze kutoa taarifa za hapa ndani? " akasema Latoya akionekana kukereka sana na kitendo kile kilichofanywa Stephano

"Ndugu zangu mimi ni mtu mwenye roho nzuri sana na niko tayari kumsaidia kila mtu katika jambo lolote lile analolitaka.Ninyi ni ndugu zangu na ninawapenda sana.Wapo wengi ambao wangependa kuja kuishi hapa na kufanya kazi na mimi lakini nimewachagua ninyi kwa hiyo nawaomba mjaribu kuwa waangalifu katika mambo madogo madogo kama haya.Toka ndani ya moyo wangu nimemsamehe Stephano lakini naomba suala hili lisijirudie tena katika nyumba hii.yeyote ambaye atashindwa kuishi hapa anitaarifu nami nitamruhusu aende zake .sawa jamani !!! akasema Latoya na watu wote wakaitika
"sawa madam " wakajibu wote kwa pamoja

"Vizuri ! hilo limepita na sitegemei kama litajirudia tena.Napenda niwafahamishe pia kwamba baba yangu mzee Curtis anaendelea vizuri kwa sasa lakini kuna jambo limetokea hospitali ambalo ni la kuhuzunisha sana.Mama yangu mzazi amefariki dunia."
watu wote mle sebuleni wakainamisha vichwa kwa mstuko na masikitiko.
"Niko katika kipindi kigumu sana kwa sasa.Nina msiba mkubwa wa mama yangu mzazi niliyempenda sana .Msiba utafanyika nyumbani kwake na si hapa.Taratibu za msiba zinaendelea na nyote mtafahamishwa juu ya kinachoendelea." wakati akiendelea kuzungumza na watumishi wake mara akaingia Stevie mmoja kati ya wasaidizi wa Latoya.Latoya alipomuona akasita kidogo akahisi kuna jambo haliko sawa.
" Ndugu zangu ni hayo tu niliyotaka kuwafahamisha.Nendeni mkaendelee na kazi zenu tutafahamishana juu ya kila kitu kinachoendelea kuhusiana na msiba huu mkubwa." akasema Latoya na kisha kila mtumishi akapita na kumpa mkono wa pole.Mtu wa mwisho kabisa alikuwa ni Innocent.Alimuangalia Latoya kwa makini machoni na kwa mbali aliyaona machozi yakimlenga Latoya .Akamuonea huruma sana.

" Pole sana Latoya" akasema Innocent na alipotaka kuuinua mkono wake wa kulia ili aweze kumpa Latoya mkono wa pole akashidwa kutokana na maumivu makali aliyoyasikia.

" Innocent what's wrong? akauliza Latoya

"Its nothing...Nilikuwa nimelala nadhani niliulalia huu mkono." akasema Innocent.Latoya akamuangalia kwa makini sana.Akamshika bega na kumsaidia kuketi sofani

" Pumzika hapa Innocent.Nina maongezi kidogo na Stevie" akasema Latoya kisha akaenda na Stevie katika chumba cha maongezi.

"Stevie nipe ripoti" akasema Latoya.
"Madam tayari mzee Curtis amekwisha hamishiwa katika hospitali ile uliyoelekeza.Mwili wa mama nao tayari umekwisha hamishiwa katika chumba cha maiti cha hospitali ile kama ulivyoelekeza pia.Lakini wakati nikiwa hospitali na mzee curtis kuna baadhi ya vifaa vyake aliniagiza nikamchukulie nyumbani kwake na nilipofika pale nilikuta tayari taarifa za kifo cha mama zimeshafika na watu walikuwa wamejaa wakilia.Mtu mmoja ambaye alijitambulisha kwangu kama kaka wa marehemu au mjomba wako alinipa barua hii nikuletee uisome." akasema Stevie huku akiitoa bahasha katika koti lake na kumpa Latoya.

"Madam I'll be outside" akasema Stevie wakati Latoya akiifungua barua ile .latoya akaitika kwa kichwa na kisha akaendelea kuisoma barua ile.



Kwa Latoya
Tumepokea kwa masikitiko sana kifo cha mama yako kilichotokea katika mazingira yenye utata mkubwa sana na kilichosababishwa na wewe.Tunafahamu pia kwamba hata baba yako amenusurika kifo siku ya leo.mambo haya mawili yamewapelekea wazee wa ukoo kuongea na mizimu na imewaambia ukweli kwamba matatizo haya yote yamesababishwa na wewe.Mizimu ya ukoo imekasirika sana na hawataki ufike wala ujishughulishe na kitu chochote kuhusiana na msiba huu na endapo utapuuzia onyo hili basi litakalokupata hakuna wa kulaumiwa.Pamoja na onyo hilo la mizimu wazee wa ukoo wameamua kwamba utaruhusiwa kufika msibani siku ya mazishi tu na ni siku hiyo utakapotoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu pamoja na waombolezaji wengine wote.
Kwa maelezo haya mafupi nina imani umenielewa na utayatekeleza kama ulivyoamriwa na usijaribu kwenda kinyume na maagizo ya mizimu na wazee hawa wa ukoo.
Nakupa pole nyingi za kuondokewa na mama yako.
Ni mimi mjomba wako
Ambrose.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………….



: BEFORE I DIE

SEHEMU YA 33

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
wazee akavuta pumzi ndefu na kuinama chini.

" Ouh My God...whats happening to me??...whats going to happen to me...??." akasema Innocent kwa sauti ndogo akiwa amejiinamia huku jasho jingi likimtiririka.

" innocent una matatizo gani? Nini kimekutokea? akauliza Stevie kwa mshangao

" Niambie Innocent..nini kimekutokea?

" Nothing Stevie.Nothing happened to me..Its just a dream...Let us go....." akasema Innocent huku akijifuta jasho lililokuwa likimtiririka.
"Mungu wangu mambo gani haya yananitokea mimi? Kwa nini ninaota ndoto za ajabu ajabu namna hii? Mara ya kwanza nimeota ndoto ya ajabu na nilipoamka ni kweli mkono wangu ulikuwa ni kama umeungua moto.Hivi sasa nimeota kichwa kinaungua moto na kuamka ninahisi kichwa kizito na kinauma sana.Haya ni mambo gani yanayonitokea.Latoya ni nani hasa? ..." akawaza Innocent na kuvuta pumzi ndefu



ENDELEA…………………………


"siwezi kukaa na kumuona Latoya akilia na kukaukiwa machozi.She doesnt deserve that.Nitakuwa karibu naye kwa lolote lile na nitamlinda dhidi ya kitu chochote kibaya.Ukiachilia mbali haya mambo ya ajabu ajabu ambayo bado siyaelewi elewi Latoya ni binti mzuri mwenye kila sifa ya binti mzuri na ana roho nzuri pia.Kama ni kupambana kwa ajili yake niko tayari." akawaza Innocent na mara akasikia sauti ya mtu ikisema

" Kaa tayari..." Inno akageuka akamtazama Stevie aliyekuwa ameelekeza macho yake mbele akamuuliza

" unasemaje Stevie" Stevie akashangaa.

" Sijasema kitu chochote Innocent.Kwani vipi?

" Ouh sorry......."Innocent akasema.

" Innocent leo una matatizo gani? akauliza Stevie

" usijali stevie..kichwa changu kina mambo mengi sana" akasema Innocent na kulishika paji la uso kwa kiganja cha mkono wake.Alianza kuogopa.......
Stevie alizidi kushangaa kwa hali ile aliyokuwa nayo Innocent.

" Innocent ana matatizo gani leo? Namuona kama vile hayuko sawa sawa.Something is wrong with him.sijui nitamsaidiaje" akawaza Stevie huku akimtupia jicho Inno aliyekuwa ameinama akiwaza.
" Sielewi ni mambo gani yananitokea.Ninahisi kama ninataka kuchanganyikiwa.Ninaota ndoto za ajabu ajabu zenye uhalisia.Kuna nyakati ninasikia sauti za watu lakini siwaoni.Nini kinaendelea hapa ? Latoya ni mtu wa namna gani? Ninapatwa na wasi wasi mwingi kila nikimfikiria lakini sina namna ya kufanya zaidi ya kuwa naye karibu na kumsaidia hasa katika kipindi hiki ambacho ni kigumu sana kwake .Nakumbuka katika ile ndoto ya kwanza niliyoota yule mzee alinikabidhi upanga na kusema kwamba ninatakiwa kumlinda Latoya.Najiuliza bila kupata majibu nimlinde Latoya dhidi ya nani? Nani wanaotaka kumdhuru? Muda si mrefu nimeota ndoto nyingine na mzee mwenye ndevu nyingi amenionya kwamba nimejiingiza katika mambo makubwa na mazito kwa maana hiyo ninatakiwa kuwa makini sana.Sielewi mambo haya ni kwa nini yananitokea.Sielewi ni kitu gani kinaendelea.." Innocent akazidi kuumiza kichwa kwa mawazo mengi.
Stevie akasimamisha gari katika duka la vinywaji akanunua chupa ya maji ya kunywa akarudi garini na kumpatia Innocent akanywa nusu yake.

" Unajisikiaje sasa hivi? akauliza Stevie.

" Najisikia vizuri Stevie." akasema Inno huku akitabasamu.Safari ikaendelea.
Waliwasili katika nyumba ya wazazi wa Latoya.Tayari eneo lote la mtaa ule lilikuwa limejaa watu na magari.Ndani ya muda huu mfupi tayari kulikuwa na umati mkubwa wa watu.Taarifa zilisambaa kwa haraka sana na watu wengi waliguswa na namna kifo kile kilivyotokea.Mama yake Latoya alikuwa ni mtu aliyejulikana sana.Kutokana na msururu mrefu wa magari yaliyokuwa yameegeshwa ikawalazimu Innocent na Stevie kushuka na kuanza kutembea kwa miguu.Shughuli zilikuwa zikiendelea kwa kasi.Hema zilikuwa zinajengwa na magari yalikuwa yakishusha viti vingi.Innocent moyo ulikuwa ukimuenda mbio sana .Hakujua nini kitatokea pindi atakapokutana na Ambrose mjomba wake Latoya.Hakujua angeongea naye kitu gani ili aweze kumwelewa.Watu walikuwa ni wengi kila sehemu na ilikuwa vigumu kumpata Ambrose.Hawakuwa na namba zake za simu hivyo ikawalazimu kuanza kumuulizia.Iliwachukua zaidi ya dakika arobaini kumpata Ambrose.Alikuwa ni pande la mtu ambaye alionekana kuwa na uwezo mkubwa kifedha kutokana na muonekano wake.Alikuwa akivuja jasho kwa pilika pilika za maandalizi zilizokuwa zinaendelea.yeye ndiye alikuwa msimamizi mkuu wa msiba ule..
Mtu aliyewasaidia akina Innocent kumpata Ambrose akawatambulisha kwake.

" Mzee Ambrose hawa ni wageni wako wanasema wametokea kwa Latoya" akasema yule kijana kisha akaondoka zake.Ambrose akatoa miwani yake akaifuta halafu akaivaa tena.

" Karibuni sana vijana.Ninamkumbuka huyu hapa alikuja hapa asubuhi nikampa maagizo ampelekee Latoya.Vipi ulimpatia maagizo yake? akauliza mzee Ambrose.

" Ndiyo nimempatia maagizo yake" akasema Stevie huku naye akijifuta jasho kutokana na jua kali liliokuwa likiwaka.

" Ni kutokana na maagizo hayo ndiyo maana tumekuja tena kukuona" akadakia Innocent.
" Latoya amewatuma mje kuniona mimi?

" Ndiyo tunashida na wewe mzee" akasema Innocent kwa ujasiri.
Ambrose akamuita kijana mmoja akampa maelekezo fulani ya kufuatilia shughuli zilivyokuwa zikiendelea halafu yeye akaongozana na akina Innocent kuelekea katika moja ya chumba ambacho kilionekana kana kwamba kilitumika kwa ajili ya maongezi na mikutano ya dharura.

" Ndiyo vijana karibuni sana.Amewatuma nini Latoya? akaanzisha mazungumzo mzee Ambrose.
Stevie akamuangalia Innocent na kumpa ishara kwamba aongee.Stevie yeye hakuwa muongeaji sana.

" Mzee kwanza poleni sana kwa matatizo yaliyowakuta." akasema Innocent
" Tumekwisha poa kijana wangu.Ni mambo ya kawaida na ambayo yanamkuta kila binadamu" akasema Ambrose.
" Mzee tumekuja hapa kuongea na wewe kuhusiana na barua uliyomuandikia Latoya.Nataka kufahamu sababu iliyopelekea Latoya kuzuiwa na wazee wa ukoo kuhudhuria msiba wa mama yake mzazi" akasema Innocent .Mzee Ambrose akamuangalia kwa makini na kusema
" Kijana wewe ni nani kwa Latoya?
" Mimi ni rafiki yake ninaitwa Innocent"
" Kumbe wewe ni rafiki yake.! .Sasa masuala ya familia ya Latoya yanakuhusu nini? haya ni masuala ambayo hupaswi hata kuyaingilia" akasema kwa dharau mzee Ambrose.

" Ninafahamu hayo mzee Ambrose lakini nimekuja hapa nikiwa na baraka zote za Latoya.Ninataka kufahamu sababu za kumzuia Latoya amb ye ni mtoto wa pekee kwa mama yake kutokuhudhuria msiba wa mama yake.."

" Umesema unaitwa Innocent.?? Ambrose akauliza
" Ndiyo ..ninaitwa Innocent"
" Vizuri Innocent..Natumai rafiki yako hajakueleza ni kitu gani kilichotokea.Naomba ukamuulize vizuri ni kitu gani kimetokea.Ukishaufahamu ukweli utakubaliana nami kwamba maamuzi yaliyofikiwa na wazee wa ukoo ni ya haki kabisa.Mambo yale yaliyoamriwa na mizimu na wazee hayapaswi hata kuhojiwa kwani ni mambo ya ndani sana ya kimila.Tafadhali naomba muondoke na mumfikishie ujumbe aliyewatuma kwamba maamuzi haya hayatabadilika kwani yana baraka zote za wazee wa ukoo.kama atapuuza basi jambo litakalomtokea asitulaumu sisi." akasema Ambrose huku akiinuka.
"Mzee tafadhali naomba ukae na utusikilize japo kidogo" akasisitiza Innocent

" Vijana nimewaambia ondokeni na msiendelee kunipotezea wakati wangu .Nina kazi nyingi za kufanya kwa sasa.Mwambieni Latoya tutamtaarifu siku ya mazishi.." akasema kwa ukali mzee Ambrose.
"Innocent there is nothing we can do here.Let us go back.." akasema Stevie.Innocent alichomwa sana na maneno yale ya Ambrose.Akasimama na kumuangalia kwa hasira.Pale pale akaikumbuka ile ndoto aliyoota wakati wakiwa garini .Akakumbuka yule mzee aliyemwambia iwapo atahisi anahitaji msaada sehemu yoyote ile basi ayaseme yale maneno kimoyo moyo mara tatu na atasaidiwa.

" Nafikiri ni wakati muafaka wa kuyatumia yale maneno..Nahitaji nguvu za kuongea na watu hawa.." akawaza Innocent na kisha akayatamka kimoyo moyo maneno yale na kuyarudia mara tatu.Mara ghafla akajikuta akijawa na ujasiri mkubwa sana na nguvu za ajabu zikamjia.Alijisikia kuwa na uwezo wa kuongea na mtu yeyote yule.Ambrose alikuwa akimalizikia kutoka katika mlango akasikia sauti kali ikimuita.
" Ambrose !!." Ambrose akastuka akasimama akageuka na kuwaangalia akina Innocent
" Rudi ndani Ambrose.Bado tuna mambo ya kuongea" akasema Innocent kwa sauti kali yenye amri ndani yake
Ambrose akaanza kurudi ndani na uso wake ukionyesha hasira za wazi.

" Wewe ni nani hadi uongee na mimi kwa sauti hiyo? Do you know who I am? Don't ever talk to me like that again ! ...akafoka Ambrose akimnyooshea kidole Innocent.Innocent akaushika mkono wa Ambrose akaurudisha chini.
" Sikia Ambrose.nitazame vizuri machoni na utatambua kwamba ule muda wa kukuomba kukaa na kuongea na sisi umekwisha pita.From now on you are going to listen to me and you'll do everything that I ask you to do.....Tumeelewana? akasema Innocent kwa ukali.Alikuwa amekasirika na sauti yake ilikuwa ikitetema kwa hasira.Ambrose akamtazama Innocent usoni akaogopa sana.

" Umenielewa Ambrose? ..Innocent akauliza tena kwa ukali.

" Nimekuelewa Innocent" Akajibu Ambrose.

" Good..sasa kaa pale katika kiti na usikie ninachotaka kukwambia." akaamuru Innocent.Kwa unyonge mzee Ambrose akaenda kuketi sofani.

" Kwa kuwa maamuzi haya uliyafanya wewe na wazee wa ukoo siwezi kuongea na wewe pekee.Nataka ukawalete hapa hao wazee wa ukoo ambao walimzuia Latoya kuhudhuria msiba wa mama yake mzazi.Nataka niongee nao wote." akaamuru Innocent na kwa kasi mzee Ambrose akatoka .Stevie alibaki akishangaa namna mambo yalivyobadilika ghafla.Innocent alibadilika ghafla.Hakuwa yule nnocent ambaye alikuwa naye muda mfupi uliopita.Kilichomshangaza zaidi Stevie ni namna Innocent alivyoweza kumtisha mzee Ambrose na kumfanya atekeleze kila alichomuamuru. Kutokana na uso wa Innocent kuonyesha hasira nyingi Stevie hakuthubutu hata kumsogelea au kumuuliza jambo lolote.
Katika hema moja lililokuwa pembeni kidogo ya nyumba ile walikaa wazee nane wakiendelea na majadiliano na kupanga ratiba ya msiba ule itakavyokuwa.hawa ni wazee wa ukoo wa mama yake Latoya ambao ndio waliokuwa wakiratibu kila jambo linalohusiana na mila na desturi za kabila lao.Ni wazee hawa waliomzuia Latoya kuhudhuria msiba wa mama yake.Wakati wanaendelea na majadiliano yao mara akatokea mzee Ambrose.Akaongea nao kwa kilugha na kwa kasi wakainuka wote wakaanza kutembea haraka haraka wakimfuata Ambrose.Nyuso zao wote zilionyesha kukasirika.Waliingia katika kile chumba walichokuwamo Innocent na Stevie .Ambrose akaongea nao kwa lugha ya kwao huku akimuelekezea mkono Innocent.wazee wale wakaonyesha sura za dharau baada ya maongezi mafupi wakitumia lugha ya kwao.Innocent ambaye alikuwa amesimama bado hakuwajali akawaangalia wote kisha akasema

" Ambrose natumai hawa ndio wazee wa ukoo.."

" Ni hawa lakini kuna wengine sita wameondoka wamerudi kijiini kwa ajili ya kufuatilia mambo fulani ya kijadi" akajibu Ambrose kwa adabu na kuwafanya wale wazee waangaliane.

" Shikamooni wazee wangu" akasalimu Innocent lakini hakuna hata mzee mmoja aliyeitika.Innocent hakuwajali akaendelea.

" Wazee wangu nimekuja hapa kuzungumza nanyi kuhusiana na jambo lililotokea siku ya leo.Labda kwa ufupi ningejitambulisha kwenu mimi ni nani.Mimi ninaitwa Innocent.Latoya ni rafiki yangu mkubwa.Amenituma nije hapa kuongea nanyi kuhusiana na barua mliyomuandikia kwamba asihudhurie msiba wa mama yake mkimtuhumu kumuua mama yake mzazi.Sikutegemea kama wazee wa hekima kama ninyi mnaweza mkafanya jambo la ajabu kama hilo.Haijawahi kutokea hata mara moja mtu akazuiwa kuhudhuria msiba wa mama yake.Nim......." kabla Innocet hajaendelea mzee mmoja akasimama

" Kijana mbona hatukuelewi wewe ni nani hadi unapata nguvu ya kusimama na kuongea na sisi kama vijana wenzio? Tafadhali naomba ukae chini kijana haraka sana" akasema mzee yule kwa ukali na wazee wenzake wote wakamuunga mkono

" wazee wangu nawaombeni mnisikilize .Kwa sasa mimi ndiye pekee mwenye amri hapa na hakuna mwingine ambaye anaweza akasimama na kuniamuru kitu chochote.Kwa yule ambaye anajiamini kwamba ana uwezo wa kuweza kusimama na kuniamuru jambo lolote lile basi asimame na afanye hivyo au kama kuna mtu yeyote kati yenu anayeweza kuinuka na kuondoka afanye hivyo haraka sana" akafoka Innocent na wazee wote wakajikuta wamekaa kimya.Hakuna aliyethubutu kusema jambo au hata kufungua mdomo wake.

" Hakuna mwenye uwezo huo sawa ? kwa hiyo nyote mtanisikiliza mimi ninachokwenda kuwaambia.Kuanzia sasa shughuli zote za msiba huu zitasimamiwa na Latoya pekee.Yeye ndiye atakayeamua nini kifanyike kuhusiana na msiba huu.Kama ataamua kuwaachia muendelee kushughulikia msiba huu itakuwa ni juu yake lakini kila kitu atakiamua yeye.Ninarudia tena kwamba kuanzia dakika hii shughuli zote za msiba huu zitaratibiwa na Latoya pekee.Hakuna mtu mwingine ambaye ataruhusiwa kushughulikia jambo lolote lile bila ruhusa toka kwa Latoya.Kama kuna mipango yoyote ambayo mmeipanga tafadhali naomba muipangue haraka sana.Hakuna tena suala lolote linalohusiana na mambo ya kijadi katika msiba huu. Nadhani tumeelewana na yeyote yule ambaye atakwenda kinyume na maagizo haya nitapambana naye." akasema kwa ukali Innocent halafu akamfanyia ishara Stevie waondoke.Wale wazee mle ndani walibaki kimya wakiwatazama Innocent na Stevie wakiondoka mle ndani.Moja kwa moja wakaeleka katika gari lao kimya kimya .Stevie aliogopa hata kumsemesha Innocent kwa namna alivyokuwa amekasirika.Walipoingia garini Innocent akaegemeza kichwa katika kiti cha gari akavuta pumzi ndefu halafu akachukua ile chupa ya maji akanywa maji yote yaliyobakia.Stevie bado aliendelea kumuangalia kwa uoga.
" Stevie mbona unaniangalia namna hiyo? Kulikoni? akauliza Innocent huku akitabasamu.Stevie naye akatabasamu
" Umenishangaza sana Innocent.Sikutegemea kama ungeweza kubadilika na kuwa vile"
" Kwani nilikuwaje ? akauliza Inno
" Ulikasirika ghafla,sura yako ikabadilika ukaongea kwa ujasiri mkubwa na kutoa amri na watu wote wakakaa kimya.Niliogopa sana sikuwahi kukuona ukiwa umekasirka namna ile" akasema Stevie.
" Ouh My Gosh !!..sikutegemea kama ningeweza kuwatisha wazee wale wa ukoo .Nilipoyasema kimoyo moyo yale maandisi niliyooteshwa ndotoni nilipatwa na ujasiri wa ajabu.Nilipata nguvu ya ajabu sana kiasi kwamba kila niliyeongea naye alikuwa akiniogopa.Nilikuwa na uwezo wa ajabu wa kusema lolote na likatekelezwa.Ina maana na mimi tayari nimekwisha ingia katika ulimwengu wa mambo haya ya ajabu ajabu? " akawaza Innocent
" No ! No ! After this I quit" Innocent akajikuta akitamka maneno yale kwa nguvu na kumfanya Stevie kustuka

" Innocent are you ok? akauliza Stevie
" I'm ok Stevie..usijali kuhusu mimi Kichwa changu kina mambo mengi sana kwa sasa." akasema Innocent.Safari ikaendelea kimya kimya.
Waliwasili tena katika jumba la Latoya wakapokelewa na Irene.Innocent akamuomba Irene ampigie simu Latoya kuwa tayari wamekwisha rejea.Irene akampigia simu Latoya chumbani kwake na kumtaarifu kwamba Innocent na Stevie wamerudi.Baada ya dakika tano hivi Latoya akashuka toka chumbani kwake.Alionekana amechoka na amedhoofu .Macho yake yalikuwa mekundu na yamevimba kwa kulia.Innocent akamuonea huruma sana msichana yule mdogo mwenye uzuri usioelezeka na mwenye utajiri wa kutisha lakini mwenye maisha yaliyojaa utata mkubwa.

" Ouh Mungu wangu kwa nini binti mzuri kama huyu ateseke namna hii ? Kila nikimuona Latoya najikuta nikihitaji kuwa naye karibu zaidi.Kila nikipanga kuondoka hapa nyumbani kwake najikuta mipango yote inayeyuka mara tu nikiiona sura yake.Sijui ni kwa nini hali hii lakini Latoya ni binti mzuri sana na hapaswi kuishi maisha ya namna hii.Anahitaji kuishi maisha yenye furaha daima.Ninajiona kama nina jukumu la kuyafanya maisha yake yawe na furaha kwa sababu tumetokea kuelewana sana japo tumeonana kwa muda mfupi tu" Akawaza Innocent
" Mbona mmewahi kurudi ? Sikutegema kama mngeweza kurudi mapema hivi" akasema Latoya kwa sauti yenye uchovu na majonzi ndani yake.Innocent akaumia sana moyoni kwa hali aliyokuwa nayo Latoya akamtazama kwa makini na kwa huruma.

" Mbona unanitazama hivyo Innocent" Latoya akasema na kumstua Innocent.
" Pole sana Latoya.Kila nikikuona napatwa na uchungu mwingi.Nafahamu jinsi unavyoumia kwa tukio hili la leo.Bado naendelea kusisitiza kwamba niko pamoja nawe katika wakati huu mgumu." akasema Innocent na kumfanya Latoya atoe kitambaa akajifuta machozi.
" Nipe taarifa za huko mlikokwenda" akasema Latoya

" Nimeonana na mjomba wako Ambrose na wazee wa ukoo.Nimeongea nao na kuwaambia kwamba kuanzia dakika hii shughuli zote za msiba utaziratibu wewe.Hakuna ruhusa kwa mtu mwingine yeyote yule kuratibu shughuli za msiba."
" Wakasemaje baada ya kuwaambia hivyo? akauliza Latoya

" hakuna aliyethubutu kujibu kitu.Wote walikuwa kimya kabisa" akasema Innocent na kumfanya Latoya ashangae akasindwa kujizuia machozi kumtoka.
" Innocent nakushukuru sana kwa msaada huu mkubwa.Nashukuru sana kwa kuwa nami hasa katika kipindi hiki kigumu.Sitaki kuongea mengi sasa hivi ila naomba nikukabidhi mambo machache.Utawapigia simu kampuni ile ya mazishi ya rafiki yangu Johari walioshughulikia msiba wa marina ili washughulike shughuli yote ya msiba wa mama.Pili mama yangu atazikwa hapa hapa nyumbani kwangu na yatakuwa ni mazishi yatakayohudhuriwa na familia yangu tu.Kwa sasa shughulikia kwanza taratibu zote za msiba ambao utaendelea kufanyika kule kule nyumbani kwake halafu mambo mengine yote tutaongea baadae.I need some rest..Nimekukabidhi kila kitu Innocent..please arrange everything for me.." akasema Latoya huku akiinuka na kutoka mle chumbani akaanza kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake.Innocent akamuangalia kwa huruma binti yule mwenye uzuri usioelezeka akapatwa na uchungu mkubwa.
" Pole sana Latoya." akasema kimoyomoyo Innocent.
Latoya akaingia chumbani kwake akafunga mlango na kuanza kupiga hatua kuelekea kitandani lakini kabla hajafika kitandani akasikia kizungu zungu

" Ouh My Gosh !...I'm going down again..please help me God..give me more strength" akasema Latoya akiwa amejiegemeza katika nguzo iliyokuwa kati kati ya chumba taratibu nguvu zikamuishia akaanguka na hakuweza kuona chochote tena zaidi ya giza nene.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………



BEFORE I DIE

SEHEMU YA 32

ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

Kwa Latoya
Tumepokea kwa masikitiko sana kifo cha mama yako kilichotokea katika mazingira yenye utata mkubwa sana na kilichosababishwa na wewe.Tunafahamu pia kwamba hata baba yako amenusurika kifo siku ya leo.mambo haya mawili yamewapelekea wazee wa ukoo kuongea na mizimu na imewaambia ukweli kwamba matatizo haya yote yamesababishwa na wewe.Mizimu ya ukoo imekasirika sana na hawataki ufike wala ujishughulishe na kitu chochote kuhusiana na msiba huu na endapo utapuuzia onyo hili basi litakalokupata hakuna wa kulaumiwa.Pamoja na onyo hilo la mizimu wazee wa ukoo wameamua kwamba utaruhusiwa kufika msibani siku ya mazishi tu na ni siku hiyo utakapotoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu pamoja na waombolezaji wengine wote.
Kwa maelezo haya mafupi nina imani umenielewa na utayatekeleza kama ulivyoamriwa na usijaribu kwenda kinyume na maagizo ya mizimu na wazee hawa wa ukoo.
Nakupa pole nyingi za kuondokewa na mama yako.
Ni mimi mjomba wako
Ambrose.


ENDELEA…………………

Latoya akavua miwani machozi yakaanza kumtoka.Akainama mezani na kuanza kulia kwa kwikwi.Stevie akaingia tena mle ndani baada ya kusikia Latoya analia.

"Madam Latoya......" akasema Stevie lakini Latoya akainua uso wake na kusema

"stevie leave me alone for a while..I need to cry alone.." akasema Latoya.na Stevie akatoka akaelekea sebuleni.
"Stevie Latoya yuko wapi? akauliza Innocent

"Madam Latoya yuko katika chumba cha maongezi" akasema stevie.
"Yuko peke yake?
"Yah !.amesema anahitaji kuwa peke yake .Anahitaji kulia peke yake.Innocent madam Latoya yuko katika wakati mgumu sana hivi sasa.Sijawahi kumuona akiwa katika wakati mgumu kama huu alionao hivi sasa." akasema Stevie akaketi sofani na kuinamisha kichwa akiwa na mawazo mengi.Innocent akainuka na kuanza kuelekea katika chumba ambamo alikuwemo Latoya.Akaufungua mlango na kuingia.Latoya alikuwa ameinama akilia .

" Latoya !!.." akasema Innocent
Latoya akastuka akainua kichwa na kukutanisha macho na Innocent.

" Innocent ..I need to be alone...I need to cry alone.." akasema Latoya.
"No Latoya..we'll cry together..You'll never cry alone" akasema Innocent huku akimkaribia Latoya na kutaka kumshika bega lakini ghafla akahisi kitu kama chaji za umeme zikimpitia katika mkono wake wa kulia uliokuwa na maumivu makali.Akastuka na kuruka kurudi nyuma akasimama mbali kidogo na Latoya

"dont touch me Innocent..." akasema Latoya.
Mkono ule wa Innocent ambao ulikuwa na maumivu makali sana ukarudi katika hali yake ya kawaida baada ya kupigwa na chaji zile za umeme.Hakusikia tena maumivu yoyote akabaki akishangaa.
Innocent akauinua mkono wake juu ,akauangalia kama una maumivu yoyote lakini hakuwa akisikia maumivu yoyote yale.Akabaki akimtazama Latoya kwa mshangao.Bado aliendelea kushangazwa na miujiza na mauza uza yaliyokuwa yakimtokea katika nyumba ile ya Latoya.Aliogopa sana..

"Innocent mbona unaniangalia kwa uoga namna hiyo.Kuna nini? una tataizo lolote? akauliza Latoya baada ya kumuona Innocent akimuangalia kwa uoga sana.

" hakuna tatizo lolote Latoya." akasema Innocent kwa sauti yenye kitetemeshi.

" Ok Innocent kama hakuna tatizo lolote basi naomba uniache peke yangu.I need to be alone." akasema Latoya.Macho yake yalikuwa yamejaa machozi.Innocent akamtazama akamuonea huruma sana.Akaanza kupiga hatua kutoka mle chumbani lakini alipofika mlangoni akageuka na kumtazama tena Latoya ambaye alikuwa amejiinamia mezani akilia.

"Hapana siwezi kumuacha Latoya katika hali hii.Moyo wangu unakuwa mzito sana kumuacha peke yake katika kipindi hiki.Pamoja na yote yaliyotokeza na yanayoendelea kutokea katika nyumba hii bado Latoya ni rafiki yangu na amenisaidia sana wakati nikiwa katika kipindi kigumu.I must help her.She's in a very difficult situation right now. Amempoteza mama yake mpenzi lazima awe katika wakati mgumu sana. She needs some one by her side katika wakati huu mgumu alionao.Let me forget everything for now and be by her side." akawaza Innocent halafu akarudi taratibu hadi katika meza ile ambayo Latoya alikuwa ameinama akilia.Akamtazama kwa sekunde kadhaa kisha akakohoa kidogo lakini Latoya hakustuka.

" Latoya ! nafahamu uko katika kipindi kigumu sana katika maisha yako.Umempoteza mama yako mpenzi.Nafahamu uchungu wa kumpoteza mtu unayempenda.Ni siku chache tu zimepita toka nimempoteza rafiki yangu.Nilikuwa katika wakati mgumu sana ambao sijawahi kuupitia katika maisha yangu.Kwa hiyo ninayafahamu machungu ya kupotelewa na mtu umpendaye.Katika wakati ule mgumu niliokuwa nao nilihisi dunia nzima imejitenga nami.Nilihisi kutelekezwa na dunia.Lakini sikuwa sahihi kwa sababu nilipofumbua macho ni wewe ndiye uliyekuwa pembeni yangu.Ni wewe ndiye uliyenisaidia kuyabeba machungu yangu.Ulinifariji,ukanipa moyo na matumaini katika wakati ule mgumu niliokuwa nao.Sikuwa nikikufahamu kabla na wala hatukuwa marafiki lakini hukulizingatia hilo.Kwa moyo wako uliojaa huruma na upendo ulishirikiana nami kana kwamba mimi ni ndugu yako na rafiki yako mkubwa na wa siku nyingi sana.Hata sekunde moja hukuniacha niwe peke yangu.Hukuniacha niomboleze peke yangu.Muda wote wa msiba wa Marina nimeomboleza pamoja nawe.Nimelia pamoja nawe.Latoya sina chochote ninachoweza kukulipa ambacho kitalingana na wema ulonitendea.Nina deni kubwa la kulipa kwako. Latoya naomba katika kipindi hiki kigumu ukubali niwe karibu yako,niwe mfariji wako kama ulivyokuwa kwangu.Mimi ni rafiki yako na wajibu wangu kama rafiki ni kuwa nawe katika nyakati zote za shida na raha.Latoya I'll be here by your side.I'll be the shoulder that you'll cry on.I'll be with you in every second of difficult time.Msiba huu si wako peke yako. Ni msiba wetu sote.Mama yako ni mama yangu pia. Samahani sana kwa kutofautiana mtazamo na baba yako mzee Curtis mchana wa leo.Naomba unisamehe sana kwa hilo kwa sababu yule ni sawa na baba yangu.Nitatafuta nafasi ili niweze kumuomba msamaha.Latoya siw........." Latoya akainua kichwa na kumtazama Innocent kisha akasema.

" No Innocent..usijaribu tena kwenda kuonana na baba .Please stay far away from him for now." akasema Latoya

" Innocent nashukuru sana kwa maneno yako yenye kunipa moyo.Ni kweli niko katika kipindi kigumu sana katika maisha yangu. Sijawahi kupitia kipindi kigumu kama hiki.Nimempoteza mama yangu mpenzi.Nilimpenda sana mama yangu.Ninaumia mno moyoni kila nikikumbuka kwamba mama yangu hayuko tena nami.Nilizoea kwenda kumsalimu na kumpelekea zawadi mbali mbali.Kila nilipofika nyumbani alikuwa akinipikia chakula changu nikipendacho.Alikuwa akinipenda sana.Nakumbuka toka nikiwa mdogo alikuwa akinifundisha mambo mengi .Alikuwa ni rafiki yangu mkubwa..Baada ya baba kumaliza muda wake kama balozi wa Tanzania nchini Marekani na kurudi nyumbani Tanzania mimi nilibaki Marekani nikiendelea na masmo ,kila siku mama alikuwa akinipigia simu usiku kabla sijalala na kuniuliza kama nimekula,au kama kuna jambo lolote lile ambalo limenikwaza kwa siku hiyo.Mara nyingine tulisali pamoja usiku katika simu kabla hatujalala na kisha akanibusu na kunitakia usingizi mwema.Mama yangu alinipenda sana Innocent.Siwezi kuelezea upendo wake kwangu wala kuufananisha.Bado siamini kama sintaweza kumuona tena mama yangu mpenzi" Latoya akashindwa kujizuia akaanza tena kulia.Innocent akamuangalia lakini akashindwa kumsogelea.Alikuwa akiogopa kumtokea tena jambo kama lillilomtokea muda mfupi uliopita alipohisi kama kupitiwa na chaji za umeme alipounyoosha mkono wake kutaka kumshika Latoya.Alisikia uchungu mwingi kumuona binti malaika yule akiwa katika wakati mgumu namna ile.Kwa mbali machozi yakamlenga.

" Latoya cry it all...keep on crying...cry it all....." akasema Innocent .
Latoya akaendelea kulia kisha akainua uso wake uliojaa machozi na kusema
" How long should I cry Innocent? When will all these stop? ...When will I be happy in my life? akasema kwa uchungu Latoya.
Inocent akamtazama Latoya akashindwa ampe jibu gani..

" Innocent moyo wangu unaumia sana .Ninasikia uchungu mkubwa sana.." akashindwa kuendelea akaanza tena kulia.

" Latoya I'm right here by your side.Nitakuwa nawe bega kwa bega katika wakati huu mgumu tulionao.Jipe moyo tutakipita kipindi hiki kigumu.Katika maisha yetu ya kila siku ni lazima tukutane na nyakati ngumu kama hizi.Ninaamini haya ni majaribu tu katika maisha na tunatakiwa kusimama imara kuyashinda.Jipe moyo Latoya.Haya yote yatakwisha" akasema Innocent.
" innocent nashukuru sana kwa maneno yako yenye busara na kutia moyo.Mimi ni mtu mwenye moyo wa uvumilivu sana lakini kuna nyakati ninashindwa kuvumilia.Wakati bado niko katika tafakari ya kifo cha mama yangu mpenzi,umezuka tena mgogoro mpya kati yangu na ndugu zangu wakiongozwa na mjomba wangu ambaye ni kaka yake kabisa na mama." akasema Latoya na kushindwa kuendelea.

" Nini kimetokea tena Latoya.Mjomba wako ameanza kufanya mambo gani tena? akauliza Innocent
"Nimepokea barua toka kwa mjomba akinitaka kutokusogea wala kushughulikia masuala yoyote yale ya msiba wa mama.Katika barua aliyoniandikia anasema kwamba mimi ndiye chanzo cha mama kufariki kwa hiyo wazee wa ukoo wamesema kwamba kwa vile mimi ndiye niliyesababisha kifo cha mama yangu siruhusiwi kukaribia eneo la msiba ama la sivyo nitakutana na jambo baya sana toka kwa mizimu.Innocent nashindwa kuelewa ni kwa nini wananifanyia namna hii.Kwa nini wanazidi kunipa wakati mgumu namna hii? Kwa nini wanazidi kunipa mateso? akalalamika Latoya.huku akimpa Innocent ile barua iliyotoka kwa mjomba wake.Innocent akaisoma na kujikuta akiukunja uso wake.

" This is crazy...watu hawa hawana huruma hata kidogo.Latoya tafadhali usiumize kichwa kwa jambo hili.Aliyefariki ni mama yako mzazi na wewe ndiye unayetakiwa kushughulikia kila kitu kuhusiana na msiba huu.Wewe ndiye unayetakiwa kuhakikisha kwamba mama yako anazikwa kwa heshima zote. Latoya tafadhali usiwaze kabisa kuhusu suala hili.Iet me take care of it." akasema Innocent
" Unataka kufanya nini Innocent? tayari wamekwisha toa maamuzi yao kwamba nisikanyage msibani hadi siku ya mazishi.Hivi ni haki kweli kuzuiwa kuhudhuria msiba wa mama yangu mzazi? akasema Latoya na machozi yakaanza kumtoka tena.

" Nyamaza kulia Latoya..tafadhali usilie ..I'm going to take care of this.They cant do this to you...." akasema Innocent akionekana kuguswa sana na barua ile.
Latoya akamtazama innocent akashindwa aseme nini.

" Dont say anything latoya.Nipe nafasi tafadhali ya kuweza kuliweka sawa suala hili.You need some rest.Please go get some rest and leave everything to me.I'll take care of everything." akasema Innocent.
" Innocent tafadhal.......................' Latoya akataka kusema jambo lakini Innocent akamzuia.
" Latoya please dont say anything..Mimi ni rafiki yako na niko tayari kuwa nawe bega kwa bega.machungu yako ni yangu pia.Nimekerwa sana na suala hili wanalotaka kulifanya na ninakwenda kuongea nao.Go get some rest for now.Try to get some sleep" akasema Innocent .Latoya akamtazama Innocent kwa makini usoni halafu akainuka na kuanza kutembea taratibu bila kusema lolote akapanda ngazi kulekea chumbani kwake. Innocent alitamani sana kumshika mkono na kumsaidia Latoya kuzipanda ngazi zile lakini bado aliogopa kumshika Latoya kutokana na jambo lililomtokea hapo kabla.

" Stevie twende tuondoke tunakwenda nyumbani kwa wazazi wa Latoya kuonana na huyo mjomba wake na hao wazee wa ukoo" akasema Innocent
" Kwani kumetokea nini? akauliza Stevie.

" Kuna maneno yamezuka kwamba eti Latoya ndiye chanzo cha kifo cha mama yake kwa hiyo wamemzuia asisogee kabisa katika msiba hadi katika siku ya mazishi.Hii ni sawa kweli Stevie? akauliza Innocent
" Hapana si sawa" akasema stevie huku wakiingia garini.
Mara tu alipoingia garini na safari kuanza Innocent akapitiwa na usingizi wa ghafla.Akiwa usingizini akajikuta amefika sehemu moja yenye nyumba mbili ndogo.Wazee wawili wenye ndevu nyingi nyeupe wakajitokeza .Mzee mmoja akamsogelea ,akamshika kichwa akasema

" Kijana umeingia katika matatizo makubwa.Unajiingiza katika masuala ambayo huyafahamu .Tafadhali jaribu kuwa makini sana kwa mambo unayotaka kuyafanya. Najua una nia njema ya kulipa fadhila kwa rafiki yako Latoya lakini lazima ufahamu kwamba utakumbana na mambo mengi magumu na ya hatari kwa maamuzi hayo uliyoyachukua.Unatakiwa uwe jasiri sana katika kuyatetea maamuzi yako.Tayari umekwisha pewa upanga wa moto ili kuweza kupambana na yeyote yule mwenye lengo la kumdhuru Latoya safari hii tunakupa karatasi hii uisome na uyaweke maandishi haya kichwani.Kila utakapokutana na jambo lolote gumu ambalo utahisi kwamba unahitaji msaada yasome maandishi haya unayoyaona katika karatasi hii na papo hapo msaada utapatikana .Anza kuyasoma mandishi unayoyaona katika karatasi hii taratibu" akasema mzee yule mwenye ndevu nyingi nyeupe zilizomfika kifuani..
Innocent akaanza kuyasoma maandishi yale kwa sauti na alipomaliza akaambiwa arudie tena kuyasoma kwa mara ya pili na ya tatu halafu mzee yule akasema
" maneno haya kila utakapoyatamka yatakupa nguvu kubwa na ujasiri wa kuweza kuongea au kufanya jambo lolote lile ambalo unahisi ni gumu kwako na linahitaji msaada wa ziada" akasema mzee yule kisha akamshika tena Innocent kichwani akaongea maneno fulani ambayo Innocent hakuyaelewa na kisha taratibu akaanza kuhisi kichwa cha moto sana .Akapiga kelele na kustuka akajikuta yuko ndani ya gari akitazamana naStevie.Jasho lilikuwa likimtiririka
" Innocent una matatizo gani? akauliza kwa mshangao Stevie.
" Kwani kumetokea nini ? Innocent akauliza akishangaa kwa namna Stevie alivyokuwa akimuangalia

" Ulikuwa umepitiwa na usingizi na ghafla ukaanza kuongea maneno ya ajabu ajabu kama vile uko ndotoni.Umeyarudia rudia maneno yale mara tatu halafu ukaanza kupiga ukelele mkubwa ukidai kichwa kinaungua moto .Ikanibidi nisimamishe gari ili nifahamu kitu gani kimekusibu.Innocent una matatizo gani? Hii ni ndoto ya namna gani? akauliza Stevie kwa wasi wasi
Ndoto aliyokuwa ameiota Innocent muda mfupi uliopita ikaanza kumjia tena kichwani.Akakumbuka maneno ya wale wazee akavuta pumzi ndefu na kuinama chini.

" Ouh My God...whats happening to me??...whats going to happen to me...??." akasema Innocent kwa sauti ndogo akiwa amejiinamia huku jasho jingi likimtiririka.

" innocent una matatizo gani? Nini kimekutokea? akauliza Stevie kwa mshangao

" Niambie Innocent..nini kimekutokea?

" Nothing Stevie.Nothing happened to me..Its just a dream...Let us go....." akasema Innocent huku akijifuta jasho lililokuwa likimtiririka.
"Mungu wangu mambo gani haya yananitokea mimi? Kwa nini ninaota ndoto za ajabu ajabu namna hii? Mara ya kwanza nimeota ndoto ya ajabu na nilipoamka ni kweli mkono wangu ulikuwa ni kama umeungua moto.Hivi sasa nimeota kichwa kinaungua moto na kuamka ninahisi kichwa kizito na kinauma sana.Haya ni mambo gani yanayonitokea.Latoya ni nani hasa? ..." akawaza Innocent na kuvuta pumzi ndefu.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….



BEFORE I DIE
SEHEMU YA 34
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Innocent nakushukuru sana kwa msaada huu mkubwa.Nashukuru sana kwa kuwa nami hasa katika kipindi hiki kigumu.Sitaki kuongea mengi sasa hivi ila naomba nikukabidhi mambo machache.Utawapigia simu kampuni ile ya mazishi ya rafiki yangu Johari walioshughulikia msiba wa marina ili washughulike shughuli yote ya msiba wa mama.Pili mama yangu atazikwa hapa hapa nyumbani kwangu na yatakuwa ni mazishi yatakayohudhuriwa na familia yangu tu.Kwa sasa shughulikia kwanza taratibu zote za msiba ambao utaendelea kufanyika kule kule nyumbani kwake halafu mambo mengine yote tutaongea baadae.I need some rest..Nimekukabidhi kila kitu Innocent..please arrange everything for me.." akasema Latoya huku akiinuka na kutoka mle chumbani akaanza kupanda ngazi kuelekea chumbani kwake.Innocent akamuangalia kwa huruma binti yule mwenye uzuri usioelezeka akapatwa na uchungu mkubwa.
" Pole sana Latoya." akasema kimoyomoyo Innocent.
Latoya akaingia chumbani kwake akafunga mlango na kuanza kupiga hatua kuelekea kitandani lakini kabla hajafika kitandani akasikia kizungu zungu
" Ouh My Gosh !...I'm going down again..please help me God..give me more strength" akasema Latoya akiwa amejiegemeza katika nguzo iliyokuwa kati kati ya chumba taratibu nguvu zikamuishia akaanguka na hakuweza kuona chochote tena zaidi ya giza nene.

ENDELEA………………………………

Baada ya Innocent na Stevie kuondoka wazee wa ukoo waliingia katika mjadala mkubwa kuhusiana na kitu kilichotokea.Hawakuelewa ni kwa nini walibaki wakiduwaa wakati Innocent akiongea nao na kuwazuia kutokuendelea na maandalizi ya msiba wa mama yake Latoya.
" Wazee wangu hata mimi sielewi ni kitu gani kimetokea kwa sababu wote tumejikuta tukimsikiliza yule kijana kila alichokisema .Hakuna hata mmoja kati yetu ambaye alikuwa na ujasiri wa kuinuka na kujibizana naye." akasema Ambrose.
" Nina hakika kijana yule ana nguvu ambayo si ya kawaida na ndiyo maana alikuwa na uwezo wa kutupumbaza sote na kutuamuru kitu chochote kile na sisi tukatii.":akasema mzee mwingine.
" Bado sijamuelewa vizuri yule kijana ni nani kwa Latoya lakini ninahisi anaweza akawa ni mshirika wake mkubwa na nguvu ile aliyonayo iliyotufanya sisi sote tukakaa kimya na kumsikiliza kwa kila alichokisema imetoka kwa Latoya.Nimekuwa nikiwaambia kwamba Latoya ni mchawi mkubwa sana na kama tusipoangalia anaweza akatumaliza sisi sote.Na kwa tukio hili tulilojaribu kulifanya la kumzuia kuhudhuria msiba wa mama yake litakuwa limempa hasira kubwa na nina uhakika mkubwa baada ya mazishi haya kumalizika anaweza akaanza kulipiza kisasi" akasema mzee mwingine.
" Mimi niliwaambia toka mwanzo kwamba tusiyaingilie masuala ya msiba huu mnaona sasa mambo yanayoanza kujitokeza? Tumejiingiza sisi wenyewe katika matat......." akasema mzee mwingine mfupi aliyevaa kofia lakini kabla hajamaliza mzee aliyeonekana kama ndiye kiongozi wa wazee wale akasema
" Hakuna sababu ya kujilaumu kwa maamuzi tuliyoyafanya.Latoya amefanya kosa kubwa.Ni wazi amemuua mama yake ili kuukomaza uchawi wake.Amemtoa mama yake kafara.Ina maana hamjui mambo haya yanavyokuwa?Ukiwa mchawi ni lazima itakuja siku ambayo lazima utatoa kafara ya mtu wako wa karibu na wa muhimu sana na kwa Latoya ameamua kumtoa mama yake.Ninafahamu kabisa kwamba mama yake hajafa kifo cha kawaida na kwa mida hii atakuwa amewekwa mahala akisubiri msiba umalizike ili shughuli za kumfanya msukule zianze rasmi na ndiyo maana nilitoa wazo la kumzuia Latoya asikanyage hapa msibani kwa sababu ili kukamilisha hatua hii ya kumfanya mtu msukule kuna mambo ambayo inakubidi uyafanye katika sehemu unapofanyikia msiba.Kwa kumuacha Latoya ashikilie mwenyewe taratibu zote za msiba ni kumpa urahisi wa kukamilisha uchawi wake.Na ninawaambia kwamba baada ya msiba huu mambo hayatakuwa rahisi kwa upande wetu.Lazima atalipiza kisasi .." akasema mzee yule na kuwafanya wenzake wawe na mawazo mengi.
" Sasa unatushauri tufanye nini? Tuendelee na msimamo wetu wa kumzuia Latoya kutokujihusisha na masuala yoyote ya msiba au tumuachie yeye kila kitu? akauliza mzee Ambrose
" Kwa sasa tumekwisha chelewa.Tulimuacha yule kijana akatuzidi nguvu wakati ule kwa hiyo hatuna tena namna nyingine ya kufanya zaidi ya kumuachia Latoya kila kitu kuhusiana na msiba huu wa mama yake.Kitu ninachoweza kuwashauri ni kwamba tunatakiwa kujipanga ili kupambana naye.Nina hakika kwa sasa anamtumia yule kijana kama ngao yake kwa maana hiyo sisi tutaanza na yule kijana .Baada ya kumuangusha yule kijana nina hakika Latoya ataogopa na hataweza kutufuatilia tena.Lakini tunatakiwa kujiandaa kikweli kweli.." akasema yule mzee
Wazee wale walionekana kujawa na mawazo mengi sana .Walianza kumuogopa Latoya

* * * *

Bila kupoteza wakati Innocent akawasiliana na uongozi wa kampuni ile aliyoelekezwa na Latoya na kuwaelekeza wasimamie shughuli zote za msiba ule wa mama yake.
" Irene..naomba uwaite wafanyakazi wote kuna jambo ninataka kuwafahamisha" Baada ya dakika tano wafanyakazi wote wakakusanyika
" Ndugu zangu naomba msishangae kwa kuniona nimesimama hapa ninaongea nanyi .kwa ufupi ni kwamba Latoya amenikabidhi nisimamie shughuli zote za msiba huu mkubwa uliotokea. Ninachotaka kuwataarifu kwa sasa ni kwamba mama yake Latoya atazikwa hapa hapa nyumbani kwa mwanae.Hizo ni taarifa za awali zilizotoka kwa Latoya mwenyewe lakini bado tunasubiri maelekezo yake zaidi.kwa maana hiyo kuanzia sasa tuanzeni kufanya usafi na maandalizi makubwa kwa sababu kama tunavyofahamu Latoya ana marafiki wengi na wengi wangependa kuja kuungana naye katika kipindi hiki kigumu.Shughuli za msiba zitaendelea kufanyika nyumbani kwa wazazi wake kama kawaida lakini mazishi yatafanyikia hapa.Irene atakuwepo hapa ataendelea kuwapa maelekezo mengine ya nini cha kufanya.Mimi ninaelekea nyumbani kwa wazazi wa Latoya ambako shughuli za msiba zinafanyika." akasema Innocent kisha yeye na Stevie wakaingia garini na kuondoka.
" Madam Latoya ametokea kukuamini sana Innocent hadi akakuachia usimamie kila kitu kuhusiana na msiba wa mama yake." akaanzisha mazungumzo Stevie wakiwa garini.
" Latoya ana wakati mgumu sana kwa sasa na ndiyo maana akaona atukabidhi kazi hii.Si mimi peke yangu niliyekabidhiwa kazi hii bali ametukabidhi sisi sote .sisi wote ni rafiki zake na ametokea kutuamini sana" akajibu Innocent.
" Inocent bado ninaendelea kuwafikiria wale wazee wa ukoo kwa sababu wakati unaongea nao muda ule walikuwa wanakuangalia vibaya sana.Inaonekana hawakupendezwa na jambo lile la kuwazuia kutokuendelea na maandalizi ya msiba ule wa ndugu yao."
" Usijali Stevie.Haikuwa sahihi kwa wao kumzuia Latoya asishiriki msiba wa mama yake mzazi." akajibu Innocent kwa ufupi.
Walifika msibani na kuendelea na maandalizi ya msiba.Watu walikuwa ni wengi sana . Saa moja za jioni Innocent akaomba kuonana na ndugu wa karibu ili aweze kuzungumza nao.Dakika kama kumi hivi ndugu wakakusanyika katika chumba maalum Innocent akafungua maongezi.
" Ndugu zangu naomba kwanza niwape pole sana kwa msiba huu wa ghafla uliotupata.Ninafahamu vile vile kwamba watu wengi wamekuwa na hamu ya kutaka kunifahamu mimi ni nani na ninahusika vipi na msiba huu kwa sababu toka nimekuja nimekuwa nikipita hapa na pale kufanya maandalizi ya msiba huu.Kwa jina ninaitwa Innocent.Mimi ni rafiki wa Latoya na ndiye aliyenituma nisimamie masuala yote yanayohusiana na msiba huu mzito wa mama yake. Wengi mtajiuliza ni kwa nini Latoya hajaonekana hapa msibani siku ya leo? Ukweli ni kwamba hali yake si nzuri na ameshauriwa apate mapumziko ya kutosha.Kwa hiyo amenikabidhi mimi kusimamia kila jambo linalohusiana na msiba huu.Kwa sasa shughuli zote za msiba huu zimekabidhiwa kwa kampuni maalum ambayo itahusika na kila kitu kitakachohitajika katika msiba huu .Ninaomba iundwe kamati ndogo ya wanandugu wachache ambayo itakuwa ikitoa maelekezo kwa kampuni hii juu ya nini kifanyike na nini kinahitajika.Jambo lingine ambalo ningependa kuwataarifu ni kwamba mazishi ya marehemu yafanyika nyumbani kwa mtoto wake Latoya na kwa mujibu wa maelekezo ya Latoya mwenyewe ni kwamba mazishi haya yatakuwa ni ya kifamilia na yatahudhuriwa na watu wachache sana." akasema Innocent na kuamsha minong'ono mle ndani.
" Kwa nini Latoya amefanya hivi? akauliza Ambrose mjomba wa latoya huku akiungwa mkono na ndugu wengine waliokuwa wakipaaza sauti kwa nguvu...
" Ndugu zangu haya ni maamuzi ya Latoya mwenyewe.nawaomba tuwe wavumilivu na tumsubiri atulize akili na ndipo tutakapopata maelekezo mazuri toka kwake lakini mpaka sasa hivi hayo ndiyo maelekezo yake." akasema Innocent na mara simu yake ikaita.Akaangalia mpigaji alikuwa ni Irene.
" Hallow Irene.."
" Innocent Madam Latoya ameamka na amesema kwamba anakuomba hapa nyumbani mara moja"
" Ok Irene ninakuja sasa hivi" akasema Innocent halafu akawaaga wale wana ndugu kwa ahadi ya kurejea tena asubuhi ya kesho kwa maelekezo zaidi.Innocent na Stevie wakaingia garini na kabla Stevie hajaliondoa gari kitu cha ajabu kikamtokea Innocent.Alihisi kitu kikimtambaa katika mkono wake wa kulia na mara mkono ukafa ganzi.Akajaribu kuuinua lakini haukuwa na nguvu ya kuinuka.Akabaki ameushikilia mkono ule kwa mkono wake wa kushoto huku mate yakimdondoka.Stevie akastuka baada ya kumuona Innocent katika hali ile.Akamuita lakini Innocent hakuitika wala kugeuza kichwa.Stevie akazima gari.Mwili ulikuwa ukimtetemeka kwa hali aliyokuwa nayo Innocent.
Stevie alishindwa afanye nini kwa hali aliyokuwa nayo Innocent.Alibaki ameduwaa akishangaa jinsi hali ile ilivyomtokea innocent ghafla.
" Innocent !!!.." akajaribu tena kuita lakini Innocent hakuitika.Bado alikuwa ameushikilia mkono wake wa kulia na mate yakimdondoka.
" Mungu wangu mambo gani haya yanamtokea Innocent leo? Huu ni ugonjwa wa namna gani ?Sijawahi kuona mtu mwenye ugonjwa wa namna hii" akawaza Stevie akiwa bado anashangaa.Hakuwa na wazo la kushuka garini kwenda kutafuta msaada .Akabaki ameduwaaa akimshangaa Innocent.
Baada ya kama dakika tatu hivi kupita taratibu Innocent akajinyoosha akainua kichwa na kujiegemeza kitini.Stevie akapumua kwa nguvu baada ya kuona Innocent ameinua kichwa..
" Innocent unanisikia? akauliza Stevie..lakini bado Innocent hakuweza kuongea lolote.Akiwa bado anajiuliza afanye nini kumsaidia Innocent mara Innocent akauinua mkono wake wa kulia ambao haukuwa ukifanya kazi.Akaukunja halafu akaunyoosha,akarudia zoezi lile kama mara tatu hivi halafu akachukua kitambaa na kujifuta mate yaliyokuwa yakimdomdoka.
" Innocent nini kimetokea? unajisikiaje sasa? akauliza Stevie na kwa sauti ndogo Innocent akajibu
" Najisikia vizuri"
Stevie akachukua chupa ya maji akampa anywe.
" Innocent nini kimetokea? Nimeogopa sana" akasema Stevie
" Hakuna jambo baya lililotokea" akajibu Innocent
" Innocent tafadhali hebu niambie ulipatwa na nini kwa sababu uliduwaa ghafla kwa muda halafu mate mengi yakaanza kukutoka mdomoni." akasema Stevie..Innocent akainama hakujibu kitu
" Innocent mimi ni rafiki yako,naomba uniamini na unieleze kama una tatizo lolote ili niweze kukusaidia.hali ile imenitisha sana" akasema Stevie.
" I'm ok Stevie..dont worry..endesha gari tuondoke" akasema Innocent
" No Innocent you are not ok..Nimekushuhudia kwa macho yangu mawili hali uliyokuwa nayo dakika chache zilizopita..hali ile haikuwa nzuri hata kidogo na niliogopa sana .Sijui ningemweleza nini madam Latoya kama tatizo lile lingekuwa kubwa zaidi kwa sababu hata mimi mwenyewe nilipatwa na mshangao na sikujua nini cha kufanya." akasema Stevie na kumfanya Innocent ainue kichwa na kumgeukia
" Stevie ninakuomba sana kama rafiki yako dont tell anything to anyone especially Latoya..She's going through a very hard time right now .Hali hii ni ya kawaida na huwa inanitokea kila baada ya miezi sita .Upande wa kulia wa mwili wangu huwa unapoteza mawasiliano kwa dakika kadhaa halafu hali inarejea kuwa ya kawaida tena.Please promise me that you wont tell anybody what happened " akasema Innocent.Stevie akamtazama na kusema
" .I wont tell anyone" akasema Stevie
" Good" akajibu Innocent.
Stevie akawasha gari lakini kabla hajaliondoa akamuangalia kwanza Innocent.
" Nini Stevie ? Endesha gari mimi niko sawa kabisa sasa"akasema Innocent na kisha Stevie akaliondoa gari.
Innocent akapumua kwa nguvu akakumbuka kwamba hajafunga mkanda wa gari akauvuta akafunga halafu akakiegemeza kichwa katika kiti cha gari,akafumba macho na kuzama katika mawazo mengi
" Kadiri ninavyozidi kuwa karibu na Latoya ndivyo ninavyozidi kukutana na mambo ya ajabu ajabu.Naona kama maisha yangu yamebadilika sana toka nilipokutana na Latoya.Hapo kabla maisha yangu hayakuwa hivi.Sikuwahi kukutwa na mambo ya ajabu ajabu namna hii.Nimekuwa ninaota ndoto za ajabu ajabu tu na tukio la sasa hivi ndilo limeniogopesha zaidi. Upande wangu wa kulia ulipooza kabisa kwa muda.Sijawahi kutokewa na hali kama hii hapo kabla.Nina hakika tukio hili halikuwa la kawaida.Lazima lilikuwa linahusiana na mambo yanayomzunguka Latoya.Nimeanza kuchoshwa na mambo haya yanayoyazunguka maisha ya Latoya.Kwa kweli ni mambo magumu sana ambayo yanahitaji uvumilivu.Inanibidi kuchukua hatua za haraka za kuweza kuondoka nyumbani kwa Latoya ama sivyo ninaweza nikapoteza kabisa dira na mwelekeo wangu wote wa maisha.Awali nilikuwa nikiishi maisha mazuri yenye furaha na amani ya moyo na sikutegemea hata siku moja kama ningeweza kuishi maisha ya namna hii maisha yaliyotawaliwa na miujiza kila siku." akawaza Innocent halafu akachukua kitambaa na kujifuta tena mdomo wake.
" Latoya kwa nini ameyafanya maisha yake yawe namna hii? Binti mwenye uzuri usioelezeka ni kwa nini ameingia katika ulimwengu wa namna hii? Latoya ni binti bilionea lakini maisha yake hayana furaha hata chembe.Maisha yake yametawaliwa na utata mkubwa. " akawaza Innocent akainama na kukishika kichwa chake.Sura ya Latoya akiwa na tabasamu pana ikamjia kichwani akahisi kama mstuko fulani katika moyo wake.
" Latoya ametokea kuwa rafiki yangu mkubwa na ananiamini mno.Latoya anahitaji msaada mkubwa ,anahitaji mtu wa kuwa naye karibu ,anahitaji mtu wa kumfanya atabasamu kila wakati mtu ambaye atamuondoa katika maisha haya anayoyaishi na mtu huyo nina imani ni mimi.Toka nimefika pale katika nyumba yake Latoya amekuwa ni mtu mwenye furaha kubwa.” Akawaza Inno

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 35
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Latoya kwa nini ameyafanya maisha yake yawe namna hii? Binti mwenye uzuri usioelezeka ni kwa nini ameingia katika ulimwengu wa namna hii? Latoya ni binti bilionea lakini maisha yake hayana furaha hata chembe.Maisha yake yametawaliwa na utata mkubwa. " akawaza Innocent akainama na kukishika kichwa chake.Sura ya Latoya akiwa na tabasamu pana ikamjia kichwani akahisi kama mstuko fulani katika moyo wake.
" Latoya ametokea kuwa rafiki yangu mkubwa na ananiamini mno.Latoya anahitaji msaada mkubwa ,anahitaji mtu wa kuwa naye karibu ,anahitaji mtu wa kumfanya atabasamu kila wakati mtu ambaye atamuondoa katika maisha haya anayoyaishi na mtu huyo nina imani ni mimi.Toka nimefika pale katika nyumba yake Latoya amekuwa ni mtu mwenye furaha kubwa.” Akawaza Inno

ENDELEA………………………….

Innocent na Stevie wakawasili nyumbani kwa Latoya ambaye alikuwa katika chumba cha mikutano na watu wapatao tisa .Irene akamfahamisha Latoya kuhusu kurejea kwa innocent na Stevie akaamuru waingie moja kwa moja katika chumba kile cha mikutano.
" Innocent na Stevie " akaanza utambulisho Latoya
" hawa ni wawakilishi toka katika kampuni itakayoshughulikia masuala ya mazishi ya mama yangu.Nimeona kuwe na kampuni mbili tofauti.Ile moja ambayo tayari imekwisha kabidhiwa kazi itaendelea na kazi yake kama kawaida kule nyumbani kwa wazazi na hii hapa itahusika na shughuli za hapa nyumbani pekee.Mmefika wakati mzuri kwani ndiyo kwanza tumeanza majadiliano ya maelekezo ya nini kifanyike.Innocent kwa kuwa wewe ndiye msimamizi mkuu wa msiba huu naomba uwe ndiye msemaji badala yangu.Mimi nitakusaidia pale utakapohitaji msaada" akasema Latoya huku akimkabidhi Innocent karatasi zenye michoro
" Hizo ni karatasi za michoro ya kaburi la mama namna ninavyotaka liwe.Hebu itazame vizuri halafu uone iwapo kuna kitu kinahitajika kubadilishwa au kuongezwa." akasema Latoya.Innocent akazichukua karatasi zile akazingalia na kisha wakaendelea na kuelekezana.Kilikuwa ni kikao kirefu na mara chache sana Latoya aliongea na kurekebisha baadhi ya mambo lakini Innocent ndiye aliyekuwa msemaji mkubwa.Baada ya kikao kile kumalizika watu wale wakaondoka na kwenda kuanza maandalizi ya shughuli nzima.Maandalizi yalianza usiku huo huo bila kuchelewa.Watu wote walitoka mle katika chumba cha mikutano wakabaki Latoya,Stevie na Innocent pekee.Latoya akamtuma Stevie kazi nyingine na akabaki na Innocent
" Innocent nipe taarifa za huko utokako" akasema Latoya.Innocent akakohoa kidogo na kusema
" Huko tulikotoka ni kwema kabisa.Shughuli zote zinaendelea vizuri na hakuna tatizo lolote."
" hakuna mtu aliyekuhoji ni kwa nini unasimamia masuala ya msiba wakati wewe si ndugu? akauliza Latoya na kumfanya Innocent atabasamu na kusema
" Suala kama hilo haliwezi kukosekana .wapo ndugu waliohoji mimi ni nani hadi nisimamie shughuli za msiba ule wakati ndugu wapo.Wengi hawakuonyesha kufurahishwa na mimi kusimamia msiba ule na hasa wazee wa ukoo lakini sikuwajali.Mimi nilikuwa na kazi moja tu ya kutekeleza kile ulichonituma.Naweza kusema kwamba haikuwa kazi rahisi lakini tulisimama imara na kila kitu kikaenda vizuri." akasema Innocent
" nashukuru sana Innocent kwa kuwa nami katika kipindi hiki kigumu.Kusema kweli ni kipindi kigumu mno katika maisha yangu na ninashukuru kwa kuwa nawe kwa sababu pamoja na machungu yote ninayoyasikia lakini ninafarijika kila nikikumbuka kwamba katika matatizo yote haya bado kuna mtu ambaye yuko nami kila sekunde.Yuko mtu ambaye analia na mimi.Wengi wanalia na mimi machoni kwa sababu ni marafiki zangu lakini wewe unalia na mimi toka moyoni.Uko na mimi kwa dhati ya moyo wako.Nashukuru sana Innocent kwa msaada wako mkubwa katika kipindi hiki kigumu.Sifahamu ningefanya kitu gani kama usingekuwepo .Wewe ni zaidi ya rafiki Innocet.Ukiacha baba yangu mzee Curtis wewe ndiye mtu wangu wa pekee kabisa." akasema Latoya kwa sauti ndogo.
" Ouh Latoya .nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya juu namna hiyo ya kuwa mtu muhimu katika maisha yako japokuwa hatuna muda mrefu toka tumefahamiana.Latoya nikiwa kama rafiki yako ninalazimika kusimama nawe katika shida na raha kama wewe ulivyosimama katika msiba wa Marina.Siku zote nitakuwa pambeni yako.Nitaitika muda wowote utakaponiita,nitakuja muda wowote utakaponihitaji,muda wowote utakapohitaji rafiki au mtu wa kuongea naye,kucheka naye usijiulize mara mbili ,mimi nipo hapa niite nitakuja haraka.In times like this when u need a shoulder to cry on I'll be there...Just call my name and I'll be there" akasema Innocent na kumfanya Latoya atokwe na machozi
" What a gentleman..he's so sweet..Moyo wangu haunidanganyi kwamba huyu ndiye kijana niliyekuwa nikimtafuta katika maisha yangu yote.Huyu ndiye kijana wa maisha yangu.Huyu ndiye furaha ya maisha yangu.Japokuwa sina muda mrefu wa kuishi lakini katika muda huu kidogo nilio nao lazima nijitahidi kwa kila niwezalo ili niweze kuwa na Innocent.Hata kama nikipata furaha ya kuwa naye kama mpenzi wangu kwa saa moja tu inanitosha sana.I must be with him before I die..I'll do anything..I mean anything to get him before I die." akawaza Latoya huku akimuangalia Innocent.
" Innocent do you know what you have just said? akauliza Latoya
" Yes Latoya..I know.." akajibu Innocent
" Umetamka maneno mazito mno ambayo hakuna mtu aliyewahi kunitamkia.Nashukuru sana Innocent.Thank you so much for being there." akasema Latoya halafu kikapita kimya kifupi Latoya akasema
" Innocent nafahamu kwamba kukaa karibu na mimi utakumbana na mambo mengi na mengine utayaona kama si ya kawaida.Nafahamu mambo mengine yanaweza yakakustua mno na kukufanya uogope na uniogope hata mimi.Siwezi kukuficha Innocent kwamba maisha yangu yanawachanganya watu wengi sana na wengi wamekuwa wakijaribu kutaka kunichunguza na kuyafahamu maisha yangu kiundani.Wengi wa waliotaka kufanya hivyo wamejikuta wakishindwa kuupata ukweli halisi wa maisha yangu na wakati mwingine wamejikuta wakipata matatizo.Innocent nimeamua kukueleza haya yote kwa sababu nafahamu kuna mambo ambayo yanaweza yakakutokea ambayo yatakufanya ukate tamaa hata ya kuishi katika nyumba hii.Napenda uishi hapa ,uishi na mimi hata ikiwezekana katika siku zote za maisha yako na ndiyo maana ninakuomba Innocent hata kama utakuwa na ugumu wa kuishi hapa katika nyumba yangu naomba tafadhali usifikirie kuondoka na kuniacha peke yangu.Wewe ni mtu pekee ambaye nimeweza kukuamini na umenifanya niwe na furaha ya maisha.Mimi ni billionea.Nina utajiri mkubwa mno licha ya umri wangu mdogo lakini pamoja na kuwa na kila kitu ninachokihitaji katika dunia hii bado sikuwa na rafiki ambaye ninaweza kusema ni wa kweli ambaye moyo wangu utamuamini.Hatimaye umetokea wewe Innocent mtu ambaye ninakuamini kwa kiasi kikubwa mno.Tafadhali nakuomba Innocent usiwe na mawazo ya kuondoka na kuniacha peke yangu ndani ya jumba hili.Nafahamu una ndoto nyingi na kubwa ikiwa ni kuwasaidia watu wenye matatizo mbali mbali kama ulivyofanya kwa akina Sabrina na marehemu Marina.Ouh tena umenikumbusha nilikuwa nimesahau kukwambia kwamba Sabrina ni mmoja wa wajumbe ambao wanakwenda kuiwakilisha taasisi yangu katika mkutano maalum kuhusu masuala ya jinsia huko Denmark." Innocent akatabasamu kisha Latoya akaendelea
" Innocent hata mimi nina ndoto kama zako za kusaidia watu na ninafurahi nimempata mtu ambaye ana ndoto kama zangu.Nina hakika kwa pamoja tunaweza tukafanya mambo makubwa mno.Lakini kabla ya kufanya chochote kile nimepanga kwamba mara tu baada ya msiba wa mama ninataka kwenda mapumzikoni.Mambo mengi yamenitokea kwa haraka kwa hiyo ninatakiwa kwenda kutuliza akili.Mapumziko yangu huwa ninayafanya katika kisiwa kimoja chenye utulivu wa pekee .Safari hii nitafurahi sana kama nikiwa pamoja nawe katika mapumziko haya ndani ya kisiwa..Please Innocent dont say No...." akasema Latoya .Innocent alibaki kimya hakujua ajibu nini.Maneno aliyoyaongea Latoya yalimtisha kwa kiasi kikubwa.
“ Hii ni fursa ya kipekee kabisa ya kumfahamu Latoya ni nani.Moyo wangu haunidanganyi kwamba kuna nguvu inayoniunganisha naye na tayari nimeanza kuhisi kuna kitu mioyoni mwetu zaidi ya urafiki. " akawaza Innocent akiwa ameinama .Ni sauti ya Latoya ndiyo ilimstua
" Innocent unawaza nini?
" Latoya nafikiria heshima hii kubwa uliyonipa ya kuwa nawe katika mapumziko yako.Wewe ni mtu mkubwa sana .Unaheshimika kupita hata raisi wa nchi.Kuniomba mtu kama mimi nikusindikize katika mapumziko yako ni jambo kubwa mno na kamwe siwezi kusema hapana." akasema Innocent.
" Nashukuru sana Innocent lakini kuna kitu ninataka kukuomba" akasema Latoya
" Chochote ukitakacho nitakupatia Latoya" akasema Innocent
" Naomba ukiwa na mimi nione kama Latoya msichana wa kawaida kabisa.Utajiri na vingine vyote weka pembeni." akasema Latoya na kabla Innocent hajajibu kitu simu ya Latoya ikaita akaichukua akaongea na mpigaji halafu akamgeukia Innocent na kusema
" Tayari vifaa na wataalamu wamekwisha wasili na wanataka kuanza usiku huu huu kuchimba na kutengeneza kaburi.wananihitaji nikawaonyeshe sehemu ya kuchimba kaburi.Nashukuru kwa kupata walau dakika hizi chache za kuongea nawe Innocent.Natumai baada ya msiba huu kumalizika tutapata nafasi ya kuongea zaidi..Kwa sasa twende tukawaelekeze hawa jamaa mahala pa kuchimba kaburi" akasema Latoya kisha wakainuka na kuongozana kuelekea nje.Tayari maandalizi ya mazishi ya mama yake Latoya yalikwisha anza.
" Sijui msichana huyu ana nguvu gani kwa sababu kila anachokisema ninajikuta nikimkubalia.Ouh Mungu wangu ina maana sintaweza tena kuondoka katika jumba hili?...." akawaza Innocent akiwa nyuma ya Latoya
" Latoya ni msichana mrembo mno..ameumbwa akaumbika..kila nikimuangalia ninajikuta nikizidi kuvutika kuwa naye karibu zaidi lakini mambo yake yananifanya nimuogope sana..I dont know what to do anymore...." Akawaza innocent
Mita chache toka jumba hili ambalo tunaweza kuliita ni kasri,ndiko ilipangwa azikwe mama mzazi wa Latoya. Innocent akiwa ameongozana na Latoya ambaye alikuwa akitembea kwa unyonge sana wakakutana na mkandarasi ambaye alitakiwa kulijenga kaburi lile ambalo Latoya alitaka liwe la aina yake.Alimuonyesha mkandarasi sehemu linakotakiwa kuwepo kaburi .Mkandarasi yule akaahidi kuianza kazi ile mara moja
Wakati wakiendelea kuelekezana na mkandarasi ,akatokea Irene na kumtaarifu Latoya kwamba Marcus ,mmoja kati ya wafanya biashara wakubwa nchini afrika kusini na rafiki mkubwa wa Latoya alikwisha wasili.Marcus na familia yake walikuja kuungana na Latoya katika wakati huu mgumu alionao.Latoya amekuwa rafiki mkubwa wa familia hii kwa muda mrefu na ndiyo maana waliposikia Latoya amepatwa na msiba kwa haraka wakapanda ndege yao binafsi na kuja kuungana na rafiki yao kipenzi..
Latoya na Innocent wakaachana na mkandarasi yule na kisha wakarejea ndani kuonana na Marcus.
Latoya akasalimiana na Marcus na familia yake na kisha kuwatambulisha kwa Innocent.Wakati Latoya akiongea na akina Marcus,Irene akamuita Innocent pembeni .
“ Innocent ,nina wasi wasi sana na Madam Latoya “ akasema Irene akiwa na uso wenye wasi wasi
“ Kwa nini unasema hivyo Irene? Akauliza Innocent
“ Nina wasi wasi sana kwa sababu toka asubuhi Latoya hajatia kitu tumboni.Akiendelea na hali hii hadi asubuhi afya yake itazorota sana.Hiki ni kipindi kigumu mno kwake kwa hiyo anatakiwa ale chakula na hakuna mtu anayeweza kumshawishi ili akubali kula chakula zaidi yako.” Akasema Irene
Innocent akafikiri kidogo halafu akasema
“ Latoya anapendelea chakula gani?
“ Anapenda sana nyama ya kuku.” Akajibu Irene
“ Ok .Katengeneze supu safi ya kuku ,akimaliza maongezi na rafiki zake nitajaribu kumsihi atie kitu tumboni.” Akasema Innocent na kwa kasi Irene akaelekea jikoni kuandaa supu kama alivyoelekezwa
Baada ya akina marcus kuondoka Inno akarejea sebuleni na kumkuta Latoya akiwa amekiegemeza kichwa chake sofani.Alikuwa akisinzia.Akamtazama kwa sekunde kadhaa akamuonea huruma sana.
“ binti mrembo kama huyu kwa nini anateseka kiasi hiki? Kila nikimuona Latoya najihisi kama kuna kitu kinanivuta zaidi niwe karibu naye…” akiwa bado amesimama akimkodolea macho Latoya aliyekuwa akisinzia pale sofani,simu ya Latoya ikaita na kumstua.Akafikicha macho na kuangalia mpigaji kisha akabonyeza kitufe cha kupokelea simu.Akaongea kwa dakika kama mbili hivi na baada ya kumaliza akamfanyia ishara Innocent asogee karibu yake.Bado Innocent alikuwa akiogopa kukaa karibu na Latoya kutokana na tukio lile lililompata mchana.
“ Innocent I’m feeling so weak..Kadiri muda unavyozidi kusonga mbele ndivyo ninavyozidi kujihisi mchovu sana.Ninahitaji mapumziko ya kutosha “ akasema Latoya halafu akanyoosha mkono wake na kumpatia Innocent simu yake.
“ Simu hii nakukabidhi .Nina marafiki wengi duniani na taarifa za kifo cha mama yangu zinasambaa kwa kasi ya ajabu na wengi wa marafiki zangu wanapiga simu kunipa pole.Kwa maana hiyo utapokea simu zote zitakazopigwa na utawaelekeza kila kitu kuhusiana na msiba kwa manaa kila kitu nimekukabidhi wewe .Kesho wageni mbalimbali watakuja hapa nyumbani kunipa pole,utawapokea wote na kupokea salamu za pole kwa niaba yangu.na familia yangu.Najua ni jukumu zito lakini ninaomba unisaidie kwa namna utakavyoweza kwa sababu mimi sintaweza .Siku ya kesho sintaonekana kabisa na kwa yeyote atakeyeniuliza mwambie kwamba ninapumzika ndani.”akasema Latoya huku macho yake yakionekana kuwa na machozi.
“ Latoya usihofu kitu chochote kuhusiana na maandalizi ya shughuli za mazishi.Nitasimamia kila kitu kama ulivyonikabidhi na kila kitu kitakuwa shwari.Nakuomba punguza mawazo usiwaze sana .Hii ni mitihani tu ya maisha ambayo hatuna budi kukabiliana nayo..” akasema Innocent
“ Ahsante sana Innocent.Ninafarijika sana kwa uwepo wako .Umetokea kwa wakati muafaka kabisa Umenisaidia sana Innocent na sioni neno la kukushukuru .Ila naomba upokee shukrani zangu za dhati toka moyoni mwangu ….” Akasema Latoya
“ Latoya mimi na wewe tumejuana kwa muda mfupi sana na katika muda huu mfupi tumekuwa marafiki wakubwa..Nakushukuru sana kwa kuniamini kiasi hiki.Umenipa heshima kubwa sana .Kama rafiki yako siku zote nitakuwa pamoja nawe katika shida na raha,tutacheka na kulia pamoja..Siku zote nitakushika mkono” akasema Innocent
“ Ahsante Innocent…Huwezi kutambua uzito wa maneno hayo uliyoyatamka .ahsante sana kwa kuweka ahadi ya kuwa pembeni yangu katika nyakati zote jambo ambalo wengi wameshindwa….” Akasema Latoya
“Latoya watu wanakupenda sana na wengi wako pamoja nawe hasa katika kipindi hiki kigumu…” akasema Innocent
“ Unayosema ni ya kweli Innocent,nina fahamika na watu wengi na wengi wananipenda sana lakini katika maelfu ya watu wanaonifahamu na kunipenda I trust only you…ni wewe pekee ambaye umeweza kusimama na mimi hata katika nyakati zile ngumu ambazo wengine hawawezi…Ahs...” Latoya akashindwa kuendelea akainama chini.Machozi yalikuwa yakimtoka.
“ Nyamaza kulia Latoya..Haya ni matatizo ya kawaida kwetu sisi wanadamu na yatakwisha Kaza moyo..” Inno akajaribu kumtia moyo
“ Innocent ,ninajitahidi sana kuvumilia na kujipa moyo lakini kuna nyakati ninajikuta nikikata tamaa na kupoteza kabisa matumaini…” akasema kwa uchungu Latoya huku machozi yakiendelea kumtoka.Innocent akaingiza mkono mfukoni na kutoa kitambaa cheupe akamsogelea Latoya karibu zaidi na kumpa
“ Wipe out all your tears..you don’t have to cry anymore..Kuyashinda majaribu yote ya dunia hii lazima uwe jasiri,usikate tamaa hata siku moja..Tears is the sign of defeat.You are powerfull and strong woman so don’t let the world defeat you Latoya..I’m here by your side and I’m going to help you ….” Akasema Innocent

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……
 
BEFORE I DIE
SEHEMU YA 36
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Unayosema ni ya kweli Innocent,nina fahamika na watu wengi na wengi wananipenda sana lakini katika maelfu ya watu wanaonifahamu na kunipenda I trust only you…ni wewe pekee ambaye umeweza kusimama na mimi hata katika nyakati zile ngumu ambazo wengine hawawezi…Ahs...” Latoya akashindwa kuendelea akainama chini.Machozi yalikuwa yakimtoka.
“ Nyamaza kulia Latoya..Haya ni matatizo ya kawaida kwetu sisi wanadamu na yatakwisha Kaza moyo..” Inno akajaribu kumtia moyo
“ Innocent ,ninajitahidi sana kuvumilia na kujipa moyo lakini kuna nyakati ninajikuta nikikata tamaa na kupoteza kabisa matumaini…” akasema kwa uchungu Latoya huku machozi yakiendelea kumtoka.Innocent akaingiza mkono mfukoni na kutoa kitambaa cheupe akamsogelea Latoya karibu zaidi na kumpa
“ Wipe out all your tears..you don’t have to cry anymore..Kuyashinda majaribu yote ya dunia hii lazima uwe jasiri,usikate tamaa hata siku moja..Tears is the sign of defeat.You are powerfull and strong woman so don’t let the world defeat you Latoya..I’m here by your side and I’m going to help you ….” Akasema Innocent

ENDELEA…………………………

Latoya akakipokea kitambaa kile cha Innocent na kufuta machozi halafu akasema
“ Inno nimefarijika sana kwa maneno haya machache ya faraja uliyonitamkia.Sintalia tena..Nitasimama imara .Thank you..thank you so much.Naomba sasa nikuache nikapumzike.kama kuna kitu nitakihitaji nitakupigia simu kwa sababu siku ya kesho hatutaonana kabisa.Sintaonana na mtu yeyote.I”ll need to be alone" akasema Latoya
“ Nimefarijika sana kusikia hivyo Latoya.Pamoja na hayo naomba kabla hujakwenda kupumzika ule kwanza chakula kitakachokuwezesha kuwa na nguvu” akasema Inno.
“ hapana Innocent sihitaji chakula chochote wala kitu chochote cha kutia tumboni kwa siku ya leo na kesho.This is my way of punishing myself kwa maana hiyo sihitaji chakula chochote ” akasema Latoya.Innocent akamtazama usoni halafu akamwambia.
“ Latoya you don’t have to punish yourself..You haven’t done anything wrong.Kushinda bila kula wont help us anything.Please Latoya we’re in a hard time now and we need strength .You are so weak already kwa sababu hujala kitu toka asubuhi.If you cant do that for yourself then do it for me” akasema Innocent.Latoya akafikiri kidogo na kusema
“ For the first time in my life I’ll go out of my principles just for you Innocent.Ok you win tell Irene to bring me food “ akasema Latoya huku akitabasamu.Innocent akatoka na kumfuata Irene jikoni.
“ Ouh My God please help me to win the heart of this young man.I love him.I love him so much.Kwa ajili yake nimeweza hata kwenda nje ya kanuni zangu ” akawaza Latoya akiwa ameikunja mikono na kuiweka kifuani kwake.
“ Nina hakika Innocent ndiye yule mtu niliyekuwa nikimsubiri..Sina haja ya kusubiri hadi nitumiwe malaika aniambie kwamba Innocent ndiye kijana pekee aliyeumbwa kwa ajili yangu.Ninapokuwa karibu naye najihisi kama niko ndani ya pepo..I feel complete when I’m with him…..” akawaza Latoya halafu akakumbuka kitu na kunyong’onyea ghafla
“ Inaniuma sana kwani sintaweza kukaa na Innocent kwa muda mrefu...Siku zangu zimebaki chache sana ..It hurt so much because I have to die soon…Ouh My Gosh why I have to die ? Why so soon ?..I need much time with Innocent before I die” akawaza Latoya na matone ya machozi yakaanza kumdondoka.Innocent na Irene wakaingia mle chumbani wakiwa na chakula,wakaanda meza halafu wakala pamoja na Latoya.Baada ya kula Latoya akawaaga na kwenda chumbani kwake.
“ Innocent ahsante sana kwa jambo ulilolifanya.Nilikuwa na wasi wasi sana na afya ya Latoya.Toka nimemfahamu sijawahi kumuona akiwa dhaifu namna hii.Nashukuru kwa kumshawishi mpaka akakubali kula chakula.Kuna kitu ambacho bado hujakigundua Innocent.Latoya anakuamini kupita kiasi .Tafadhali naomba ukae naye karibu na hasa katika kipindi hiki kigumu alichonacho “ akasema Irene.Innocent hakujibu kitu alikuwa akitabasamu akachukua kikombe cha kahawa na kuelekea katika sehemu iliyokuwa ikiandaliwa kwa ajili ya wageni watakaofika msibani.
“Latoya needs someone by her side.She needs me now.I have to stay with her japokuwa si kazi rahisi lakini sina namna nyingine ya kufanya.She’s so lovely,she smiles like an angel .She needs happiness.She needs someone she can trust and she has chosen to trust me”Alikuwa akiwaza Innocent akiwa bustanini akishuhudia jukwaa likijengwa .
“Sifahamu ni kwa muda gani nitaendelea kukaa hapa kwa Latoya.May be this is my destiny.May be this is where I belong..”akawaza Innocent ,akanywa kahawa kidogo halafu akapiga hatua kuelekea ufukweni akaketi juu ya gogo la mnazi.Akaendelea kunywa kahawa yake.
“ I feel like I belong to this place.Ninahisi kama kuna kitu kinanivuta nisiondoke hapa.Kuna nguvu inayoufanya moyo wangu uwe mzito sana kila linapokuja suala la kuondoka na kumuacha Latoya.Ukiacha aina ya maisha anayoishi yaliyojaa usiri mkubwa sana , Latoya ni msichana ambaye siwezi kumfananisha na msichana mwingine yeyote .Ni msichana mzuri ambaye kuna nyakati mtu unaweza ukajiuliza mara mbili mbili iwapo ni binadamu wa kawaida au ni viumbe wale wa kiroho.Uzuri wake umepitiliza.Ni msichana mwenye roho nzuri sana,anawapenda watu wote,ana roho ya huruma,anajali utu . Latoya ana kila sifa nzuri na kama ukianza kuelezea sifa zake unaweza ukatumia siku nzima kumuelezea.Pamoja na utajiri wote alionao binti huyu ambao sina haja ya kuuchunguza ameupata wapi ,kwa nini hana furaha katika maisha yake? Kwa mujibu wa Irene ambaye amemfahamu Latoya kwa muda mrefu kidogo,anasema kwamba toka ameanza kuniona nikiwa na Latoya ,ameona mabadiliko makubwa katika maisha yake.Latoya ameonekana kuwa ni mtu mwenye furaha licha ya mambo mengi ya siri yanayomzunguka.Ametokea kuniamini kwa kiwango cha juu mno kiasi cha kuniruhusu niingie hata katika baadhi ya sehemu ambazo watu wengine hawaruhusiwi kuingia.Kwa nini Latoya ameniamini ghafla namna hii? ..” akawaza Innocent akiwa bado amekaa katika gogo la mnazi.
“Ngoja niachane kwanza na mawazo kuhusiana na Latoya na maisha yake .Ninatakiwa kuelekeza akili yangu katika kazi hii kubwa aliyonikabidhi ya kuandaa msiba wa mama yake.Watu wengi maarufu watafika ikiwamo viongozi wa serikali kwa hiyo kila kitu kinatakiwa kiende kama inavyotakiwa” Inno akainuka pale katika gogo la mnazi na kuelekea mahala linakojengwa jukwaa.



* * * *


Salamu za rambi rambi ziliendelea kumiminika toka kila pembe ya dunia kwa watu waliomfahamu Latoya.Salamu zilitoka kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa ,viongozi wa dini ,wafanya biashara wakubwa na hata kwa watu wa kawaida ambao walionekana kuguswa sana na na msiba ule wa mama yake Latoya.Wengi walimuonea huruma binti huyu ambaye amekuwa msaada mkubwa hasa kwa watu masikini .Akina mama wengi amewawezesha kimitaji kwa kupitia taasisi zake mbili zinazohusiana na kuwakomboa akina mama kiuchumi.Vile vile amewasaidia vijana wengi kujiajiri kwa kuanzisha benki ya vijana inayotoa mikopo kwa vijana wengi. Kwa ujumla amekuwa ni msaada mkubwa hasa kwa jamii masikini.
Nyumbani kwa wazazi wake Latoya kulifurika maelfu ya watu waliohudhuria msiba ule.Msiba huu ulilitikisa jiji la Dar.Nyumbani kwa Latoya ambako ndiko mazishi yangefanyika waliruhusiwa watu maalum tu .Nje ya geti la kuingilia nyumbani hapo palijazwa maua na kadi za watu waliokuja kumpa pole Latoya kwa kufiwa na mama yake mzazi lakini hawakufanikiwa kuingia ndani .Msiba ule ulionekana kuwagusa watu wengi .
Latoya hakuonekana na mtu yeyote kwa siku nzima.Alikuwa amejifungia chumbani kwake na hakutaka kabisa kuonana na watu.Mtu pekee aliyekuwa akiwasiliana naye kwa simu ni Innocent ambaye alikuwa akimpa taarifa za maendeleo ya maandalizi ya mazishi ya mama yake.Wageni wote waliofika msibani walipokewa na Innocent ambaye ndiye aliyekabidhiwa jukumu zima la kuongoza kila kitu .Salamu zote za rambi rambi toka kwa watu mbali mbali ni yeye ndiye aliyekuwa akizipokea kwa niaba ya Latoya.Hakuna mtu aliyefahamu ni kwa nini Latoya aliamua kujifungia ndani bila kuonana na mtu yeyote.
Saa tatu asubuhi ya siku iliyofuata Latoya akashuka toka ghorofani.Alisalimiana na watu mbali mbali waliokuwa wamefika kumpa pole na kuungana naye katika msiba ule mzito halafu akiongozana na Innocent wakaenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa kaburi na baada ya kutoa maelekezo machache wakarejea ndani.
" Innocent umefanya kazi kubwa na nzuri .Ahsante sana.Kila kitu kimekwenda kama nilivyokuwa nataka." akasema Latoya akiwa amekaa na Innocent katika chumba kidogo cha mikutano..
" Mheshimiwa waziri mkuu pamoja na viongozi kadhaa wa kitaifa watahudhuria mazishi ya mama siku ya kesho.Kinachotakiwa ni ulinzi uwe wa uhakika kwa ajili ya viongozi wetu hawa.Ratiba ya kesho itakuwa namna hivi,tutaondoka hapa nyumbani na kwenda hospitali ambako tutamchukua baba na mwili wa marehemu kisha tutaelekea nyumbani kwake.Watu wote watatoa heshima zao za mwisho kule na baada ya hapo tutaondoka na kuja hapa kwa ajili ya mazishi ya kifamilia.Hapa kutakuwa pia na zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa wale ambao hawajafanya hivyo na baadae tutamzika mama." Akasema Latoya na kisha akaagana na Innocent akaelekea chumbani kwake akajifungia.


* * * *


Hatimaye siku ya kumzika mama yake Latoya ikawadia.Wageni walioruhusiwa kuingia nyumbani kwa Latoya walianza kuwasili kuanzia asubuhi.Viongozi mbali mbali wa kitaifa walitegemewa pia kuwasili katika mazishi hayo kwa hiyo ulinzi ulikuwa mkali sana kulizunguka kasri la Latoya. Akiwa katika pilika pilika za kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa Innocent akapigiwa simu na Latoya na kumuomba aende mara moja katika bustani yake iliyoko juu ya jumba lake.Kwa haraka Innocent akaelekea ghorofani akiwa na wasi wasi mwingi.
Latoya alikuwa ameketi bustanini akiwa katika mavazi meusi.Alionekana ni mwenye mawazo mengi.
“ Innocent kuna jambo ambalo sikuwa nimekueleza" akaanzisha mazungumzo Latoya baada ya Innocent kufika pale bustanini.
" Mazishi ya mama yatakuwa ya kifamilia na hayatahusisha watu wengi.Ninapozungumzia familia nina maana ya baba,mimi na mtu wangu wa karibu ambaye ni sehemu ya familia yangu kwa sasa yaani wewe.Tutakaoingia katika chumba kile chenye kaburi na kumzika mama yangu ni hao watu watatu tu.Mimi wewe na baba." akasema Latoya na kumfanya Innocent ashikwe na mshangao kidogo.Latoya akaendelea
" Baada ya watu kutoa heshima zao za mwisho na jeneza kuingizwa katika chumba chenye kaburi tutaingia sisi watatu pekee.Baba atakuwa wa kwanza kutupia mchanga kaburini ishara ya kumzika mama halafu atatoka nje.Nitahitaji faragha na mwili wa mama kabla hatujaushusha kaburini.Nitafanya maombi yangu ya mwisho halafu jeneza litashuka kaburini na huo utakuwa mwisho wa mama yangu.Kuna kitu ninataka kukuomba" akasema Latoya.
" Chochote unachokitaka Latoya usisite kuomba" akasema Innocent kwa wasi wasi.
" Ninaomba wakati nikiwa faragha na mwili wa mama...uwe pembeni yangu."Akasema Latoya na kumfanya Innocent astuke akakosa neno la kusema
" Innocent , I need you more than ever today..please be by my side" akasema Latoya huku akimtazama Innocent machoni.
" I'll be there Latoya.." akajibu Innocent kwa wasi wasi.
" Thank you sasa tunaweza kuondoka " akasema Latoya kisha taratibu wakashuka tayari kwa safari ya kuelekea hospitali kuuchukua mwili wa mama yake.
Huku akisindikizwa na walinzi wake sita waliokuwa wamevalia mavazi meusi Latoya akafunguliwa mlango na kuingia katika gari lake jeusi aina ya Limousine ambalo hulitumia mara chache sana.Ndani ya gari hiyo alipanda yeye na Innocent pekee. Msafara wa kuelekea hospitali kuuchukua mwili wa marehemu ulikuwa na magari kumi na mbili yote aina ya Mercedece benz rangi nyeusi isipokuwa Limousine aliyopanda Latoya na Innocent. Taratibu msafara wa magari ukaanza kuondoka pale nyumbani kuelekea hospitali.
“ Bado siamini kama ni kweli mama yangu amefariki dunia na sintamuona tena maishani.Inaniuma sana lakini sina namna nyingine ya kufanya” akasema Latoya huku machozi yakimlenga lenga.Innocent akamuangalia na kusema
“ Latoya nafahamu ni kwa namna gani unaumia kwa msiba huu.Ninayafahamu maumivu ya kufiwa hasa na yule umpendaye .Kifo hakizoeleki hata kidogo. Tunachopaswa kufanya ni kuzidi kumuombea mama apumzike kwa amani huko aliko.Japokuwa inaumiza mioyo yetu lakini hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo hata lile linaloumiza zaidi kwani mambo yote yanafanyika kwa mapenzi yake yeye .Nakuomba uwe na ujasiri hasa kwa siku hii ya leo..” akasema Innocent.Maneno yale ya faraja toka kwa Innocent ni kama yalikitonesha kidonda cha moyoni cha Latoya.Akainama na kuanza kulia.
“ Nyamaza kulia Latoya.You need to be strong today..Siku zote kazi ya Mungu haina makosa.Yeye hutoa na kutwaa katika muda anaoutaka yeye.Atwaapo kiumbe chake huwa hatoi salamu wala fursa ya kujiandaa.Nakuomba usilie tafadhali “ akasema Innocent huku akiogopa kumkaribia zaidi Latoya akikumbuka kilichomtokea alipotaka kumgusa Latoya..
“Ni bora kama yangekuwa ni mapenzi ya Mungu.Lakini….” Latoya akastuka akasita kuendelea akamtazama Innocent ambaye naye alikuwa amestuka .Wakatazamana
“ Sorry Innocent..I’m too emotional ndio maana wakati mwingine ninajikuta nikitamka mambo bila kujua ninaongea vitu gani” akasema Latoya huku akipangusa machozi.
“ Its ok Latoya usijali..Ninaelewa wakati ulionao ni mgumu sana.” Akasema Innocent lakini akionekana kuwa na wasi wasi baada ya kauli ile ya Latoya.
“ Kuna kitu alitaka kukisema Latoya halafu akasita .Alimaanisha nini aliposema ni bora kifo cha mama yake kingekuwa ni kwa mapenzi ya Mungu? Ina maana kifo cha mama yake si kifo cha kawaida?.Ni kifo ambacho kimegubikwa na mazingira yenye utata mwingi kwa mujibu wa mashuhuda wa namna kilivyotokea.Inaonekana Latoya anafahamu kwa kina sababu ya kifo cha mama yake .Mambo haya yanazidi kuniogopesha mno.Latoya ana siri kubwa moyoni.Nashindwa kumuelewa ni mtu wa namna gani huyu msichana.Kuna nyakati ninamuona kama si binadamu wa kawaida.Kuanzia muonekano wake na hata matendo yake vinanipa mashaka sana.Pamoja na mambo haya ya kutisha yanayomzunguka Latoya lakini najikuta siwezi kuondoka na kumuacha peke yake.Kuna nguvu ya ajabu inayonizuia nisimuache mrembo huyu.Ninaogopa sana lakini sina namna nyingine ya kufanya. Tayari amekwisha niamini na kunishirikisha katika baadhi ya mambo yake makubwa.Kwa sasa ananichukulia mimi kama rafiki na ndugu yake.Ninachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuizoea hali hii..Kuyazoea maajabu na mauza uza ya maisha yake.Inauma sana kwa binti mrembo kama huyu kuishi maisha ya namna hii.”akawaza Innocent huku akiwa amemkazia macho Latoya.
“ Sura yake nzuri kama wale viumbe tunaowasoma katika simulizi mbali mbali za kale.Midomo yake laini.Ana sauti nzuri na tamu kama ya mtoto mdogo.Ana macho mazuri ya kuvutia.Ukija katika kifua chake ndo hutataka kuyabandua macho yako pale.Panasisimua sana.Dah..Kwa nini Msichana mzuri kama huyu ashiriki katika mambo ya miujiza ujiza kama haya? Kuna kitu ndani ya nafsi yangu kinanituma kutaka kumchunguza Latoya na kumfahamu undani wake lakini kuna sauti inanizuia nisithubutu kufanya hivyo..Ngoja kwanza nishughulikie masuala ya msiba na yakishamalizika nitajua nini nifanye.Lazima nimsaidie msichana huyu ambaye kadiri ninavyozidi kumfahamu ndivyo ninavyozidi kuyashuhudia maajabu yake na ndivyo ninavyozidi kujikuta nikiwa karibu naye zaidi.May be this is my life.This is my dest….” Innocent akastuliwa na sauti ya Latoya.
“ Innocent unawaza nini? Mbona unaniangalia hivyo? Akauliza Latoya. Innocent akafikiri kidogo na kusema.
“ Ninaumia mno moyoni kila nikikuona ukidondosha chozi.Ninataka kukuona ukiwa na uso uliojaa furaha na tabasamu siku zote.Ninajiuliza nifanye nini ili niufanye uso wako uwe na tabasamu.Napenda nikuone ukitabasamu hata nyakati zile ngumu kama hizi..” akasema Innocent.Kwa mbali Latoya akatabasamu.
“ Innocent huna sababu ya kuumiza kichwa kutafuta ni kitu gani ufanye ili nifurahi.Toka nimekufahamu umekwisha fanya mambo makubwa sana ambayo hakuna mtu ambaye angeweza kunifanyia.Umeleta tabasamu katika maisha yangu.Usoni ninaonekana ni mwenye huzuni lakini moyo wangu umejawa na tabasamu kubwa.Moyo wangu unatabasamu kwa sababu yako Innocent.Ninachokiomba toka kwako ni kitu kidogo tu,ni kuwa karibu yangu.Moyo wangu utaendelea kutabasamu milele nikiwa karibu yako.” Akasema Latoya.
“ usijali Latoya .Mimi nitakuwa karibu yako siku zote. Nitafurahi kama nitachangia japo kidogo katika furaha ya maisha yako”
“ Nashukuru sana Innocent kwa kuwa karibu yangu hasa katika kipindi hiki kigumu” Akajibu Latoya .
TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 37
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Ninaumia mno moyoni kila nikikuona ukidondosha chozi.Ninataka kukuona ukiwa na uso uliojaa furaha na tabasamu siku zote.Ninajiuliza nifanye nini ili niufanye uso wako uwe na tabasamu.Napenda nikuone ukitabasamu hata nyakati zile ngumu kama hizi..” akasema Innocent.Kwa mbali Latoya akatabasamu.
“ Innocent huna sababu ya kuumiza kichwa kutafuta ni kitu gani ufanye ili nifurahi.Toka nimekufahamu umekwisha fanya mambo makubwa sana ambayo hakuna mtu ambaye angeweza kunifanyia.Umeleta tabasamu katika maisha yangu.Usoni ninaonekana ni mwenye huzuni lakini moyo wangu umejawa na tabasamu kubwa.Moyo wangu unatabasamu kwa sababu yako Innocent.Ninachokiomba toka kwako ni kitu kidogo tu,ni kuwa karibu yangu.Moyo wangu utaendelea kutabasamu milele nikiwa karibu yako.” Akasema Latoya.
“ usijali Latoya .Mimi nitakuwa karibu yako siku zote. Nitafurahi kama nitachangia japo kidogo katika furaha ya maisha yako”
“ Nashukuru sana Innocent kwa kuwa karibu yangu hasa katika kipindi hiki kigumu” Akajibu Latoya .

ENDELEA………………………..
Waliwasili hospitali ambako kulikuwa na idadi kubwa ya watu na waandishi wa habari.Askari polisi tayari walikuwepo pale kwa ajili ya kuhakikisha hakutokei aina yoyote ya fujo kutokana na idadi kubwa ya watu iliyojazana pale hospitali.Walinzi wa Latoya wakaufungua mlango wa gari lile la kifahari na akashuka akiwa ameongozana na Innocent .Waandishi wa habari na wapiga picha hawakuruhusiwa kumsogelea Latoya hata kidogo hivyo walichukua picha kwa kutumia kamera zenye uwezo wa kuchukua matukio toka mbali.Huku akiwa amezungukwa na walinzi wake Latoya akaongozwa moja kwa moja hadi ndani ya hospitali akapokelewa na mganga mkuu wa hospitali ambaye akawaongoza hadi katika chumba alimolazwa baba yake Latoya mzee Curtis.Latoya akawafanyia ishara walinzi wake wabaki mlangoni akaingia chumbani yeye na Innocent.Latoya akambusu baba yake halafu akaketi katika kiti kilichokuwa pembeni ya kitanda.Machozi yakamtoka.Mzee Curtis akainuka na kuketi kitandani
“Nyamaza kulia Latoya.Tafadhali usiendelee kulia.Jipe moyo hasa katika kipindi hiki kigumu kwetu sote.Yote haya ni mapenzi ya Mungu.Nakupenda sana mwanangu na hata mama yako anakupenda sana na ataendelea kukupenda hata huko aliko.Inauma sana lakini hatuna budi kumshukuru Mungu kwani ni yeye mwenye kutoa na kutwaa.” Akasema mzee Curtis ambaye kwa sasa hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.
“ Baba najitahidi sana kutokutoa machozi lakini nashindwa.Nawapenda sana wazazi wangu.Nimeumia mno kwa msiba huu wa mama..” akasema Latoya.
“ Pole sana mwanangu.Hii ni mitihani ya dunia ambayo hatuna budi kuishinda.Vipi hali yako? Watu wanaonihudumia hapa hospitali waliniambia kwamba hali yako haikuwa nzuri hata kidogo.Niliogopa sana “ akasema mzee Curtis
“ Ninaendelea vizuri baba .Ni kweli nilipata wakati mgumu sana ila namshukuru Innocent ambaye muda wote amekuwa karibu yangu na kama si yeye sijui ningefanya nini .Vipi maendeleo yako? akasema Latoya
“ Mimi ninaendelea vizuri Mungu ananisaidia.Hivi sasa najisikia ni mzima wa afya ila madaktari wamenishauri niendelee kupata mapumziko ya kutosha .”
“ Usijali baba.baada ya kumaliza shughuli za msiba utakwenda kupumzika nje ya nchi ” akasema Latoya
“ Vipi kuhusu maandalizi ya mazishi ?akauliza mzee Curtis
“ tayari kila kitu kimekamilika .Mama atazikwa nyumbani kwangu .Kaburi tayari limeandaliwa.Tutauchukua mwili wa mama na kuelekea nyumbani kwake ambako watu watatoa heshima zao za mwisho halafu tutaondoka na kuelekea nyumbani kwangu ambako zitafanyika shughuli za mazishi ambayo yatakuwa ni ya kifamilia ambayo kwa sasa ni wewe,mimi na Innocent.” Akasema Latoya.Mzee Curtis hakujibu kitu akamtazama Innocent ambaye alikuwa amesimama pembeni karibu na dirisha .
“ Innocent hujambo kijana wangu? Akasema mzee Curtis na kumstua Innocent.Akasogea taratibu na kumpa mkono mzee Curtis wakasalimiana.
“ Pole sana mzee wangu kwa matatizo” akasema Innocent
“ Nimekwisha poa kijana wangu.Matatizo tumeumbiwa binadamu,ni sehemu ya maisha yetu” akajibu
Kimya kifupi kikapita halafu mzee Curtis akamwambia Latoya
“ Latoya ,kabla hatujaondoka ninaomba niongee faragha na Innocent”
Latoya akaguna kidogo na kuuliza
“ Kuhusu nini baba?
“ Its men to men talk..Just three minutes “
Latoya akafikiri kidogo kisha akainuka
“ sawa baba nitakuwa hapo nje”
“ nashukuru sana” akajibu mzee Curtis kisha akamfanyia ishara Innocent aketi kitini
“ Innocent nimeona nichukue dakika hizi chache kuongea na wewe na kuzimaliza tofauti zetu zilizojitokeza siku chache zilizopita.Najua nilikukosea kwa kukutaka ufanye kitu ambacho hukuwa tayari kufanya.Naomba unisamehe sana kwa yote yaliyotokea.” Akasema mzee Curtis.
“ Mzee hukupaswa kuniomba mimi msamaha bali mimi ndiye niliyepaswa kukuomba msamaha .Najua nilikuudhi sana siku ile.Sikupaswa kuongea namna ile mbele yako kama mzazi.Nilikukosea heshima kama mzazi wa Latoya ambaye ni rafiki yangu mkubwa.Naomba unisamehe sana mzee wangu” akasema Innocent.
“ Nilikwisha kusamehe muda mrefu kijana wangu.Sote tumekoseana na tusameheane ili tuanze upya” akasema mzee Curtis na kumpa Innocent mkono.
“ Innocent kuna jambo lingine ambalo ninataka kukuomba.”
“ Usijali mzee Curtis sema chochote ukitakacho”
“ Kwanza ninashukuru sana kwa kuwa karibu na mwanangu Latoya.Wewe ni mtu pekee ambaye anakuamini sana kwa sasa.Tafadhali nakuomba Innocent kuwa karibu naye.Wewe ni msaada mkubwa kwake.Ni mara ya kwanza nimemuona akiwa na rafiki anayemuamini kama wewe.Narudia tena kukuomba kaa karibu naye na hasa katika kipindi hiki kigumu alichonacho.Anahitaji faraja kubwa.Nitashukuru sana kama utalikubali ombi langu” akasema mzee Curtis
“ Mzee Curtis nashukuru kwa wewe na mwanao kuniamini .Latoya ni rafiki yangu amenisaidia mambo mengi na alisimama na mimi hata katika nyakati zile ngumu nilizokuwa nazo.Mimi nitakuwa naye karibu siku zote.Usihofu kuhusu hilo”
“ Nashukuru sana Innocent .Sasa naomba nijiandae ili tuweze kuondoka.”Akasema mzee Curtis.Innocent akatoka nje na kukutana na Latoya.
“ Alikuwa anakwambia nini baba? Akauliza Latoya
“ Tulikuwa tunaombana msamaha kwa yaliyotokea .Tumesameheana” akajibu Innocent
“ Good “akajibu Latoya na kuinamisha kichwa.

Baada ya dakika saba mzee Curtis akatoka mle ndani huku akitembea taratibu.Innocent akamshika mkono na kwa pamoja wakaelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti.Tayari mwili wa mama yake Latoya ulikwisha wekwa katika sanduku zuri lenye nakshi za dhahabu .
“ Latoya uko tayari kuuona mwili wa mama? Akauliza Innocent kabla ya sanduku lile halijafunguliwa.
“ Niko tayari Innocent” akajibu latoya na taratibu sanduku likafunguliwa.Mama yake Latoya alionekana ni kana kwamba amelala usingizi.
Latoya akanyoosha mkono na kuuweka usoni pa mama yake.Baada ya dakika kama tatu akautoa mkono na sanduku likafungwa na kuingizwa katika gari maalum lililokuwa nje ya jengo.Latoya akagoma kupanda katika gari lenye maiti ya mama yake alilotakiwa kupanda yeye na baba yake. Hakutoa sababu kwa nini hakutaka kupanda gari lile .Mzee curtis akapanda katika ile mercedece benzi iliyokuwa na maiti ya mke wake akiwa na mmoja wa walinzi wa Latoya.Huku akisindikizwa na walinzi wake Latoya na Innocent wakaingia katika gari walilopanda wakati wakija hospitali na safari ya kuelekea nyumbani kwa wazazi wa Latoya ikaanza.
Ndani ya gari Latoya alikuwa anamiminikwa na machozi.
“ She’s crying..I can hear her…My mother isn’t dead..she’s not dead but I cant save her” akasema Latoya huku akilia.Innocent akastuka sana kwa kauli ile ya Latoya.
“ Latoya tafadhali usilie.kaza moyo” Innocent akajaribu kumbembeleza Latoya baada ya kumuona akidondosha machozi.
“ Innocent let me cry..nina uchungu mkubwa sana ..ninaumia sana moyoni kila nikiisikia sauti yake.She’s crying and I cant help her….”akasema Latoya huku akilia.innocent akastuka na kuuliza
“ Latoya nani analia? ..Innocent akauliza kwa mshangao.
Latoya akastuka kama mtu aliyekurupushwa usingizini…
“ What ! No body is crying..No body….”akasema Latoya na kuzidi kumchanganya Innocent.
Innocent akazidi kuingiwa na wasi wasi mwingi,akamtazama Latoya ambaye alikuwa ameinama akilia.
“ Kuna nyakati ninashindwa kumuelewa huyu Latoya hasa kutokana na matendo yake na maneno ambayo amekuwa akiyatamka .Pale mwanzo alisema kwamba kifo cha mama yake hakikuwa kifo cha kawaida.Hivi sasa amejisahau na kusema tena kwamba anaisikia sauti ya mama yake akilia.Nilipomuuliza akastuka kama mtu aliyekuwa usingizini na kuanza kuniuliza tena nani anayelia..Whats going on here? ..Innocent akazama katika lindi la mawazo.
“ Nimejiingiza katika mambo mazito sana .Nakumbuka ndoto niliyoota wazee wawili wakinionya kwamba nimeingia katika mambo mazito nisiyoyafahamu na wakanitahadharisha niwe makini .Sasa nimeanza kuamini maneno yao.Huku mahala nilikoingia ni kugumu na kuna mambo ya ajabu ajabu mno.Pamoja na yote yanayoendelea ya ajabu ajabu na ya kushangaza bado najikuta siwezi kuondoka na kumuacha Latoya peke yake.Kuna nguvu inayonizuia kufanya hivyo. Latoya ananigusa sana moyo wangu.Kila nikimuona najikuta nikijisikia tofauti na hata mawazo ya kuondoka na kumuacha yanatoweka.” Akawaza Innocent huku akimtazama Latoya ambaye bado alikuwa ameinama.
“Bado ni msichana mdogo kuingia katika mambo makubwa kama haya.Siwezi kumuacha.Lazima nimsaidie kwa kadiri nitakavyoweza.Siwezi kukubali msichana mzuri namna hii aishi maisha kama haya.lazima nitafute namna ya kumuondoa katika maisha ya namna hii na kumrudisha katika ulimwengu wa kawaida.”
“ Innocent “ akasema Latoya na kumstua Innocent katika mawazo aliyokuwa nayo.
“ Naam Latoya” akaitika Innocent
“ Unawaza nini? Akauliza Latoya
“ mambo ya kawaida tu Latoya “ akajibu Inno
“ Najua unawaza mambo mengi sana kuhusu mimi.Naomba tafadhali usiwaze lolote kuhusiana na mimi.Naomba unichukulie mimi kama Latoya msichana wa kawaida.Kwa siku hizi chache ulizokaa nami najua umekutana na mambo mengi ambayo kwako wewe si ya kawaida.I can see in your eyes you are very scared .Nafahamu umeogopa sana.Ninachokuomba ,usiogope hata kidogo.Maisha yangu ya ndani ni magumu sana na ninaomba uyavumilie.” Akasema Latoya kwa sauti ndogo.Innocent akakohoa kidogo na kusema
“ Latoya wewe ni rafiki yangu mkubwa na siwezi kukuficha kitu.Ni kweli baada ya kuingia katika jumba lako nimekutana na maisha Fulani ya tofauti kidogo na yale ambayo nimeyazoea kuishi ,kwa hiyo kwa siku za mwanzo nilipata shida sana lakini kwa sasa nimekwisha yazoea. “ akasema Innocent
“ nashukuru sana Innocent. It means a lot to me. ” akasema Latoya
“ Usinishukuru Latoya.Ni wajibu wangu kufanya hivi. Kwa hiyo kama rafiki yako nitajitahidi siku zote kuwa karibu nawe na kukufanya uwe ni mwenye furaha na tabasamu daima” maneno yakazidi kumtoka Innocent.
“ Innocent nashindwa hata niseme nini kwa maneno hayo uliyoyaongea.Ni maneno mazito sana na yameufanya moyo wangu ujawe na furaha kubwa na kunisahaulisha kwa muda machungu ya kufiwa na mama yangu .Nashukuru sana Innocent sina neno la kusema zaidi ya ahsante” akasema Latoya huku uso wake ukionyesha dhahiri furaha aliyokuwa nayo baada ya maneno yale ya Innocent.
“Nilikuwa na wasi wasi mwingi pengine Innocent angeweza kuondoka kutokana na maisha ya pale kwangu ambayo ni tofauti na maisha aliyoyazoea.This is the man I’ve been waiting to see before I die..This is my man.Sasa moyo wangu una amani kwani nina imani nimemuona mtu niliyekuwa nikimsubiri kwa hamu kwa muda mrefu.” Akawaza Latoya akiwa ameinama.
Msafara ule mkubwa wa magari ya kifahari ,uliokuwa ukiongozwa na pikipiki ya askari wa usalama barabarani ulisababisha foleni kubwa jijini wakati ukielekea nyumbani kwa wazazi wa Latoya. Watu wengi walijitokeza barabarani kuushuhudia msafara uliobeba maiti ya mama wa Latoya msichana mdogo lakini tajiri mkubwa.Wengi walikuwa wameguswa sana na msiba huu na walimuonea huruma sana Latoya ambaye alikuwa ni kipenzi cha wengi. Katika barabara walizopita wengi wa akina mama walikuwa wakipunga mikono yao ishara ya kumuaga mama mzazi wa kipenzi chao Latoya.
Hatimaye msafara ule ukafika katika mtaa waliokuwa wakiishi wazazi wa Latoya. Watu walikuwa ni wengi mno.Magari hayakuruhusiwa kuingia katika mtaa ule kutokana na uwingi wake hiyo yakatafutiwa eneo la kuegeshwa ili kuacha nafasi kwa waombolezaji waliokuwa wamekusanyika kwa maelfu. Ni gari nne tu ambazo ziliruhusiwa kuikaribia nyumba ya wazazi wa Latoya .Gari iliyobeba maiti gari ya Latoya na gari mbili za walinzi wake ndio pekee ziliruhusiwa kuegeshwa mbele ya nyumba ile. Vilio vikaanza upya baada ya gari lenye maiti kuwasili pale nyumbani.Walinzi wa Latoya wakashuka kwa haraka katika magari yao na kulizunguka gari la Latoya.Baada ya dakika kama tatu hivi mlango wa gari ile ya kifahari ukafunguliwa na Latoya akashuka akiwa ameongozana na Innocent.Baada ya Latoya kushuka garini mlango wa gari lililobeba maiti ukafunguliwa na taratibu jeneza lililokuwa limenakshiwa kwa dhahabu likaanza kushushwa na walinzi sita waliokuwa wamevalia suti nyeusi na kuliweka katika meza maalum ya magurudumu.Innocent akamshika mkono mzee Curtis baba yake Latoya na kwa pamoja wakiwa nyuma ya jeneza lililokuwa likisukumwa na walinzi ,wakaanza kutembea kuelekea ndani mahala ambako shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa marehemu zingefanyika.Eneo lote lilitawaliwa na vilio vya akina mama .Watu kadhaa walikuwa wakianguka na kupoteza fahamu baada ya kulishuhudia jeneza lenye mwili wa mama yake Latoya likiingizwa ndani.Watu wa huduma ya kwanza walikuwa wamejipanga vyema kuwahudumia watu waliopatwa na matatizo ya kuanguka na kupoteza fahamu.Hali ya mahali hapa ilikuwa ni ya simanzi kubwa sana.Mama huyu alikuwa kipenzi cha wengi.
Kwa mwendo wa taratibu sana jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa juu ya meza maalum ya magurudumu likaingizwa ndani huku Latoya ,baba yake mzee Curtis na Innocent wakifuatia nyuma.Kwaya mbali mbali zilikuwa zikitumbuiza waombelezaji kwa nyimbo za maombolezo.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 38
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Baada ya dakika kama tatu hivi mlango wa gari ile ya kifahari ukafunguliwa na Latoya akashuka akiwa ameongozana na Innocent.Baada ya Latoya kushuka garini mlango wa gari lililobeba maiti ukafunguliwa na taratibu jeneza lililokuwa limenakshiwa kwa dhahabu likaanza kushushwa na walinzi sita waliokuwa wamevalia suti nyeusi na kuliweka katika meza maalum ya magurudumu.Innocent akamshika mkono mzee Curtis baba yake Latoya na kwa pamoja wakiwa nyuma ya jeneza lililokuwa likisukumwa na walinzi ,wakaanza kutembea kuelekea ndani mahala ambako shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa marehemu zingefanyika.Eneo lote lilitawaliwa na vilio vya akina mama .Watu kadhaa walikuwa wakianguka na kupoteza fahamu baada ya kulishuhudia jeneza lenye mwili wa mama yake Latoya likiingizwa ndani.Watu wa huduma ya kwanza walikuwa wamejipanga vyema kuwahudumia watu waliopatwa na matatizo ya kuanguka na kupoteza fahamu.Hali ya mahali hapa ilikuwa ni ya simanzi kubwa sana.Mama huyu alikuwa kipenzi cha wengi.
Kwa mwendo wa taratibu sana jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa juu ya meza maalum ya magurudumu likaingizwa ndani huku Latoya ,baba yake mzee Curtis na Innocent wakifuatia nyuma.Kwaya mbali mbali zilikuwa zikitumbuiza waombelezaji kwa nyimbo za maombolezo

ENDELEA………………………..

Latoya ,baba yake na Innocent wakaenda kuketi katika jukwaa lililokuwa limeandaliwa maalum kwa ajili yao.Nyuma yao walikuwepo ndugu kadhaa wa karibu wa marehemu akiwemo mjomba wake Latoya.Hakuna ndugu yeyote aliyemsalimu Latoya.Kila aliyekuja alikuwa akimsalimu mzee Curtis pekee.Innocent aliyekuwa amekaa pembeni ya Latoya akaliona hilo na kumuomba Latoya asijali wala kuhuzunika kwa kitendo cha yeye kubaguliwa kupewa salamu za pole na ndugu zake.
Shughuli ilifunguliwa kwa ibada ya misa toka kwa askofu msaidizi wa jimbo kuu la Dar es salaam mhashamu Leonard tubarua. Katika mahubiri yake aliwakumbusha watu kujiweka tayari muda wowote kwani kifo hakipigi hodi.Vile vile aliwaasa watu kumtegemea zaidi Mungu na kuachana na imani potofu hasa sehemu kama hizi za misiba.Aliyasema haya kwa sababu alikwisha sikia minong’ono ya watu kwamba kifo cha mama yake Latoya hakikuwa cha kawaida.Kilitawaliwa na mazingara mengi.
Baada ya ibada ile ya misa kumalizika kikafuata kipindi cha watu kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu .Jeneza lenye nakshi za dhahabu likafunguliwa na watu wa kwanza kutoa heshima zao za mwisho ni mume na watoto wa marehemu.Mzee Curtis akiwa ameongozana na mwanae Latoya na Innocent wakasimama katika jeneza lile kwa muda halafu wakaondoka na kuwaachia nafasi ndugu wengine nao watoe heshima zao za mwisho.Lilikuwa ni zoezi gumu sana na akina mama wengi walianguka na kupoteza fahamu.
Pamoja na kwamba tayari alikwisha kuwa mtu mzima sana lakini mama yake Latoya bado sura yake iliendelea kung’aa na ule uzuri wake wa asili haukutoweka.Ndani ya jeneza alikuwa ametulia kana kwamba amelala usingizi.Mikono yake ilikuwa kifuani mwake na alionekana kama amepumzika.Vilio vingi vikasikika.Watu walimlilia mama huyu hadi sauti zikakauka.Vilio vile vikamchoma sana Latoya .Alisikia uchungu mkubwa na mara akaanza kusikia maumivu makali mno katika mgongo wake na kwa mbali akaanza kuhisi kama nguvu zinaanza kumuishia.Akauma meno kwa uchungu.
“ouh My Gosh..Not now…Ouh No..Its coming..Not here..Not here infront of all these people” akasema kimoyomoyo Latoya halafu akamgeukia Innocent.
“ Innocent nishike mkono nipeleke katika gari langu” akasema Latoya na bila kuuliza chochote Innocent akamshika mkono wakaondoka kwa mwendo wa haraka kuelekea katika gari la Latoya huku wakifuatiwa nyuma na walinzi wa Latoya.Innocent akawa na wasi wasi mwingi.
Latoya akawafanyia ishara walinzi wake wafungue mlango wa gari halafu akaingia ndani.
“ Innocent naomba asiingie mtu yeyote ndani ya gari.I need a privacy” Akaamuru Latoya na kuufunga mlango.Maumivu yakaongezeka na kuwa makali zaidi.Macho yake yakaanza kuona giza.
“ Ouh My Gosh.i’m going down again……”akasema Latoya na kuanguka chini .


* * * *

Msafara wa mheshimiwa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ukawasili katika kasri la Latoya.Ulinzi ulikuwa wa kutosha sana.Mheshimiwa waziri mkuu aliiwakilisha serikali katika mazishi ya mama wa Latoya binti mdogo ambaye anasemekena ndiye tajiri mkubwa nchiniTanzania na afrika Bilionea huyu mdogo amekuwa na mchango mkubwa sana katika miradi mbalimbali ya maendeleo hususani katika masuala ya afya.Amekuwa akisaidia katika ujenzi wa hospitali na zahanati nchini.Latoya amekuwa ni mfadhili mkuu wa mamia ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kila mwaka kwa matibabu baada ya kushindikana kutibiwa hapa nchini.Amekuwa mstari wa mbele katika kusaidia huduma ya afya ya mama na mtoto kwa kutoa vifaa vya kujifungulia na kuboresha wodi za wazazi katika hospitali zote za mikoa na wilaya.Katika upande wa uchumi amewasaidia maelfu ya akina mama na vijana kujiwezesha kiuchumi kwa kuwapatia mikopo yenye riba nafuu kupitia benki zake mbili. Latoya amekuwa mfadhili mkubwa wa elimu kupitia mfuko wake wa kusaidia elimu vjijini.Amesaidia katika ujenzi wa shule kubwa na nzuri zenye vifaa vya kutosha ikiwamo waalimu.Kiujumla mchango wake kwa taifa ni mkubwa sana na hivyo kuwa mmoja wa watu wanaotambuliwa na serikali kwa mchango wao mkubwa.
Mheshimiwa waziri mkuu akapokelewa na Stevie mtu maalum aliyekuwa akipokea wageni na kuongozwa hadi jukwaani.Vikundi mbali vya kwaya vilikuwa vikindelea kuimba nyimbo za maombolezo .Wageni mbali mbali waliendelea kuwasili nyumbani kwa Latoya kwa ajili ya mazishi.Wengi wa wageni waliofika hapa ni viongozi wa serikali wageni toka nje ya nchi matajiri wakubwa wa ndani na nje ya nchi pamoja na watu wake wa karibu.
Kwa mujibu wa ratiba ,ilipangwa shughuli ya mazishi ianze saa saba za mchana lakini mpaka saa nane na nusu bado shughuli haikuwa imeanza.Ikamlazimu Stevie ambaye ndiye aliyeachiwa jukumu zima la kusimamia shughuli zote za nyumbani kwa Latoya ampigie simu Innocent ili kufahamu nini kilichokuwa kinaendelea kule nyumbani kwa wazazi wa Latoya kilichosababisha wawe nje ya ratiba.
“Stevens kuna jambo limetokea hapa “ akasema Innocent baada ya kupokea simu ya Stevens.
“ Jambo gani limetokea Innocent” akauliza Steve lakini Innocent hakujibu kitu.
“ Innocent jambo gani limetokea huko ? akauliza tena Steve.
“ Steve nitakupigia baada ya muda mfupi..Kuna jambo zito hapa limetokea.” akasema Innocent kwa wasiwasi na kukata simu.Steve kijasho kikamtoka.
Steve aliingiwa na wasi wasi mwingi.Kauli ile ya Innocent kwamba kuna jambo limetokea ikampa wasi wasi mkubwa.Akatoa kitambaa na kujifuta jasho.
“ Nini kimetokea ? akajiuliza Stevie bila kupata jibu.
“ Tuko nje ya ratiba na wageni wa kitaifa wana majukumu mengine.Nitawaambia kitu gani ? akazidi kuwaza Stevie.Hali ile ilimchanganya sana kichwa chake.Akaingia ndani akatafakari kidogo na baada ya kama dakika tano hivi akaelekea moja kwa moja jukwaani akachukua kipaza sauti na kuiomba kwaya iliyokuwa ikitumbuiza isimame kwa muda.
“ Ndugu zangu waombolezaji,bado tunaendelea kuusubiri mwili wa marehemu uweze kufika hapa na shughuli za mazishi ziweze kufanyika.Kwa mujibu wa ratiba yetu inavyoonyesha ni kwamba baada ya kuuchukua mwili wa marehemu toka hospitali ,utaelekea moja kwa moja nyumbani kwa marehemu ambako itafanyika ibada na shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.Baada ya zoezi hilo kumalizika mwili utaletwa hapa kwa ajili ya watu wengine nao kutoa heshima zao za mwisho halafu yatanyika mazishi ambayo yatakuwa ni ya kifamilia. Narudia tena kwamba mazishi yatakuwa ni ya kifamilia tu kwa hiyo watakaoingia katika chumba atakamozikiwa mpendwa wetu ni familia ya marehemu tu.Tunaomba kama wewe si mwana familia usiingie katika sehemu ya kuzikia.Kwa mujibu wa taarifa nilizopokea muda si mrefu ni kwamba kumejitokeza idadi kubwa ya watu wanaotoa heshima zao za mwisho nyumbani kwa marehemu kwa hiyo tunaomba tuendelee kuwa wavumilivu .Baada ya zoezi hilo kukamilika nyumbani kwa marehemu ,mwili utaletwa hapa na sisi tutapata nafasi ya kuuaga. Tuendeleeni kuliwazika kwa nyimbo za maombolezo toka katika vikundi mbali mbali vya kwaya.” Akasema stevie halafu akashuka jukwaani.
* * * *


Bado Innocent aliendelea kuwa na wasi wasi kuhusu hali ya Latoya ilivyobadilika ghafla.
“ Latoya anasumbuliwa na nini? Mbona hali yake imebadilika ghafla? Akawaza Innocent bila kupata jibu.Bado aliendelea kusimama nje ya gari lile akiwa na walinzi wa Latoya. Japokuwa alijitahidi asiweze kuonyesha wazi wazi woga aliokuwa nao miguu yake ilikuwa ikimtetemeka.Alihisi uoga Fulani ambao hakujua ulitokana na nini.
Muda ulizidi kuyoyoma bila ya Latoya kutoka ndani ya ile gari.Taratibu idadi ya watu waliokuwa wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu ikaanza kupungua.Innocent jasho likaendelea kumtoka.
“ Itakuwaje iwapo watu watamaliza kutoa heshima zao za mwisho na latoya hajatoka ndani ya gari? Ametoa amri asiingie mtu yeyote ndani ya gari lake.Tutawezaje kumtaarifu kwamba shughuli ya kutoa heshima za mwisho imemalizika? Anafanya nini ndani ya gari? …Innocent akazidi kuumiza kichwa kwa maswali ambayo hayakuwa na majibu.
Hatimaye watu wakamaliza kutoa heshima zao za mwisho na jeneza likafungwa kuashiria kwamba shughuli ile imemalizika.Mapigo ya moyo wa Inno yakaanza kwenda mbio.Hakujua angeieleza nini hadhira ile iliyokusanyika.
Mjomba wa Latoya akamfuata Innocent .Alipomuona anakuja akahisi kuchanganyikiwa.Hakujua angempa jibu gani.
“ Kijana shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu zimemalizika.Nini kinafuata? Akauliza mjomba wa Latoya.
“Kinachofuata sasa hivi ni kuelekea nyumbani kwa Latoya ambako ndiko maziko yatafanyika.” Akajibu Innocent
“ Latoya yuko wapi ?
Inocent hakujibu kitu kitu akamfuata mlinzi mmoja wa Latoya akamnong’oneza kitu sikioni halafu akamuomba mjomba waongozane kuelekea jukwaani.
“ Wakati maandalizi ya kuelekea nyumbani kwa mtoto wa marehemu yanafanyika naomba uruhusu vikundi vya kwaya viendelee kuwaliwaza waombolezaji kwa nyimbo za faraja.” Innocent akamwambia muongoza shughuli halafu akashuka jukwaani.
“ Latoya anafanya nini ndani ya gari ? Itakuaje iwapo muda unazidi kusonga na hajatoka mle garini? Nitawaeleza nini watu iwapo watataka kufahamu mahala alipo Latoya? Innocent akazidi kuumia kichwa kwa maswali ambayo hakupata majibu yake.Ghafla simu yake ikaita.Kwa haraka akaitoa na kutazama mpigaji alikuwa ni Stevie.
“ Innocent vipi hali ya huko? Bado shughuli zinaendelea? Akauliza Stevie baada ya Inno kupokea simu
“Stevens kuna jambo limetokea hapa “ akasema Innocent
“ Jambo gani limetokea Innocent” akauliza Steve lakini Innocent hakujibu kitu.
“ Innocent jambo gani limetokea huko ? akauliza tena Steve.
“ Steve nitakupigia baada ya muda mfupi..Kuna jambo zito hapa limetokea.” akasema Innocent kwa wasiwasi na kukata simu akasimama akatafakari na mara simu yake ikaita tena.Katika kioo cha simu ,lilionekana jina la Latoya.Haraka haraka Inno akaipokea huku akihema..
“ Hallo Latoya” akasema Innocent
“ Nini kinaendelea Innocent? Akauliza Latoya kwa sauti ya chini sana.
“ Kwa sasa shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu zimemalizika na tunakusubiri wewe pekee ili tuweze kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwako kwa mazishi..” Akasema innocent
“ Innocent naomba uruhusu safari ianze kuelekea nyumbani.One more thing…” akasema Latoya halafu akanyamaza kidogo na kuendelea.
“ You will drive this car.” Latoya akatulia tena kidogo.Alikuwa akiongea kana kwamba alikuwa katika maumivu makali mno.
“ Innocent wakati ukiendesha usijaribu kutaka kuangalia nyuma.Dont do that please..” akanyamaza tena akagugumia kwa maumivu kisha akasema
“ Tukifika nyumbani ,ingiza gari moja kwa moja ndani katika maegesho yangu halafu shuka na ukanisubiri chini sebuleni.Naomba ufanye kama ninavyokuagiza Innocent” akasema Latoya.
“ Sawa Latoya nitafanya kama ulivyosema” akajibu Innocent.Alishukuru kwa kuongea na Latoya lakini kwa upande mwingine alikuwa na wasi wasi mwingi sana .
“ Nimesikia Latoya akigugumia kwa maumivu. Ana matatizo gani? Lazima kuna kitu kinamsumbua.Maisha ya Latoya yamezungukwa na fumbo gumu.Japokuwa ninajitahidi kuwa karibu naye lakini kuna nyakati ninamuogopa sana hata kumsogelea.Nakumbuka juzi niliposikia kama mkono wangu umepitiwa na umeme nilipotaka kuupeleka mgongoni mwake.Siyo siri kuishi karibu na Latoya kunataka uvumilivu mkubwa sana.Kwa nini amesema nisijaribu kuangalia nyuma ya gari? Kuna nini kinaendelea huko nyuma? Dah maisha haya yananipa wakati mgumu sana lakini sina namna nyingine ya kufanya itanibidi nifanye kama anavyotaka kwa sababu mimi ndiye mtu anayeniamini sana kwa sasa." akawaza Innocent halafu akarejea jukwaani akaongea kidogo na mzee Curtis na maandalizi ya kuelekea nyumbani kwa Latoya yakaanza.Jeneza Likapakiwa katika gari na magari yakajipanga tayari kwa kuondoka.Zoezi hili liliamsha vilio toka kwa akina mama.Baada ya kila kitu kuwa tayari,Innocent akachukua funguo za gari na kuingia akaketi katika usukani kisha akavuta pumzi ndefu.Hakuwahi kuendesha gari kama hili lakini akajipa moyo na kuliwasha.Hakuthubutu kutazama nyuma kama alivyokuwa ameamriwa na Latoya japokuwa kulikuwa na kioo cheusi ambacho dereva hawezi kuona kinachotokea nyuma. Taratibu msafara wa magari ukaanza kuondoka pale nyumbani kwa marehemu na kuacha vilio vingi.Innocent alikuwa akitiririkwa na jasho


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 39
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nakumbuka juzi niliposikia kama mkono wangu umepitiwa na umeme nilipotaka kuupeleka mgongoni mwake.Siyo siri kuishi karibu na Latoya kunataka uvumilivu mkubwa sana.Kwa nini amesema nisijaribu kuangalia nyuma ya gari? Kuna nini kinaendelea huko nyuma? Dah maisha haya yananipa wakati mgumu sana lakini sina namna nyingine ya kufanya itanibidi nifanye kama anavyotaka kwa sababu mimi ndiye mtu anayeniamini sana kwa sasa." akawaza Innocent halafu akarejea jukwaani akaongea kidogo na mzee Curtis na maandalizi ya kuelekea nyumbani kwa Latoya yakaanza.Jeneza Likapakiwa katika gari na magari yakajipanga tayari kwa kuondoka.Zoezi hili liliamsha vilio toka kwa akina mama.Baada ya kila kitu kuwa tayari,Innocent akachukua funguo za gari na kuingia akaketi katika usukani kisha akavuta pumzi ndefu.Hakuwahi kuendesha gari kama hili lakini akajipa moyo na kuliwasha.Hakuthubutu kutazama nyuma kama alivyokuwa ameamriwa na Latoya japokuwa kulikuwa na kioo cheusi ambacho dereva hawezi kuona kinachotokea nyuma. Taratibu msafara wa magari ukaanza kuondoka pale nyumbani kwa marehemu na kuacha vilio vingi.Innocent alikuwa akitiririkwa na jasho

ENDELEA…………………………….
Hatimaye msafara uliobeba mwili wa marehemu ukawasili nyumbani kwa Latoya.Gari lile la Latoya ambalo lilikuwa linaendeshwa na Innocent likaingia moja kwa moja ndani hadi katika maegesho yanayotumiwa na Latoya pekee.kama alivyokuwa ameamriwa ,Inno akazima gari na kushuka akafunga mlango na kuondoka kuelekea sebuleni .Maiti ilishushwa toka garini na kuwekwa kwanza sebuleni wakisubiri Latoya ashuke chini.Baada ya dakika kama kumi na tano hivi Latoya akashuka akiwa katika mavazi mengine kabisa tofauti na yale aliyokuwa amevaa.Bila kupoteza muda jeneza lenye mwili wa mama yake likaanza kupelekwa mahala ambao shughuli za kuuaga mwili wa mwarehemu zingefanyika.Latoya ,baba yake mzee Curtis na Innocent walikuwa wakilifuata kwa nyuma.Walipofika jukwaani wakachukua nafasi zao na shughuli zikafunguliwa kwa maombi maalum.Baada ya maombi Innocent akasoma historia ya marehemu na kisha zikafuata salamu za rambi rambi toka kwa serikali ,watu binafsi na mashirika .Mheshimiwa waziri mkuu alitoa salamu za serikali na kuelezea namna serikali na wananchi kwa ujumla walivyoguswa na msiba ule.Baada ya kumaliza kutoa salamu za serikali,zikafuata salamu toka kwa watu mbali mbali na wawakilishi wa mashirika mbali mbali.
Zoezi la salamu lilipomalizika,likafuata zoezi la kuuaga mwili wa marehemu .Kama ilivyofanyika nyumbani kwa marehemu,Latoya,baba yake mzee Curtis na Innocent walikuwa wa kwanza kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu halafu akafuata mheshimiwa waziri mkuu ,viongozi wengine wa serikali,mabalozi na watu wengine nao wakafuatia.Kila aliyekuwa akipita mbele ya jeneza na kutoa heshima zake za mwisho kwa marehemu alitakiwa kuwapa mkono wa pole wafiwa akianzia na mzee curtis,Latoya na mwisho Innocent.Wakati zoezi lile likiendelea kijana mmoja mzungu aliyekuwa amenyoa upara akatoa heshima zake kwa mwili wa marehemu lakini utoaji wake wa hesima za mwisho ukamstua kidogo Latoya .Akamuangalia yule kijana kwa makini sana mwili ukamsisimka.Alipotoa heshima zake za mwisho yule kijana akatembea taratibu hadi walipokuwa wamekaa familia ya marehemu na kuanza kutoa mkono wa pole kwa mzee Curtis. halafu akampa mkono Latoya.Mwili wake wote ukatetemeka.Macho ya Latoya yalitua katika vidole vya yule kijana.Katika kidole kimojawapo alikuwa amevaa pete ya rangi ya fedha ambayo ilikuwa na alama ya x katikati iliyokuwa ikitoa miale ya kama ya moto.Hakuna aliyekuwa akiiona miale ile mikali ya moto iliyotolewa na ile pete zaidi ya Latoya pekee.
" Huyu ndiye " Latoya akasikia sauti ikimwambia.Akahisi kuchanganyikiwa.
Kijana yule ambaye alikuwa amevaa miwani myeusi alikuwa akitabasamu.Latoya akamuagalia kijana yule kwa macho ya wasi wasi sana.Alionyesha mstuko wa dhahiri.Innocent aliyekuwa amekaa pembeni ya Latoya akagundua namna Latoya alivyokuwa amestuka baada ya kumuona yule kijana.Taratibu akautoa mkono wa Latoya toka katika mkono wa yule kijana .Latoya alionekana kuishiwa nguvu.Alionekana kama mtu aliyechanganyikiwa.
" Ouh My Gosh ! why so soon? I need more time to be with Innocent.Ninampenda kwa moyo wangu wote.I've seen the guy but I'm not ready yet..I cant do that now..." Latoya akaomba kimoyomoyo
" Nitafanya kila ninaloweza hadi nihakikishe ninakuwa na Innocent katika muda huu mfupi niliobaki nao.Yule kijana ndiye Brandon.Miaka saba iliyopita niliambiwa kwamba nitakutana na kijana aitwaye Brandon msibani.Leo imetimia.Kumuona Brandon ni ishara kwamba nimebakiwa na muda mchache sana.No I cant let that happen that fast.I must fight ."Latoya akawaza .Alikuwa amenyong'onyea sana.
Zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu liliendelea lakini Latoya alionekana kama aliyechanganyikiwa.Alikuwa amebadilika ghafla baada ya kumuona yule kijana.Ni Innocent pekee aliyeweza kuyaona mabadiliko yale ya ghafla kwa Latoya.
“ Kitu gani kimemfanya Latoya akabadilika ghafla namna hii ? Mara tu baada ya kumuona yule kijana alibadilika ghafla akawa ni kama mtu aliyepigwa na butwaa akabaki akimshangaa .Yule kijana ni nani? Halafu mbona kila alipomtazama Latoya alikuwa anatabasamu? Kuna kitu kinachoendelea hapa si bure.Yule kijana lazima atakuwa ana uhusiano fulani na Latoya.Inawezekana akawa ni mpenzi wake ? I need to find out “ akawaza Innocent huku akijaribu kuangaza angaza kama angeweza kuona mahala alikokaa yule kijana lakini hakuweza kumuona kutokana na idadi kubwa ya watu.
Zoezi la heshima za mwisho likamalizika na kilichofuata kwa mujibu wa ratiba ilikuwa ni mazishi ambayo yangefanywa na familia pekee.Muongoza shughuli akamuomba Innocent ambaye alikuwa ni kama msemaji wa familia atoe ufafanuzi wa namna mazishi yale yatakavyofanyika.
“ Ndugu waombolezaji,kwa niaba ya familia na kwa ruhusa niliyopewa na familia ya mzee Curtis ninaomba niwataarifu kwamba mazishi yatakuwa ni ya kifamilia tu ikimaanisha mume wa marehemu ,watoto na kama kuna mtu mwingine ambaye wao watapenda aungane nao katika mazishi hayo watamchagua na atajiunga nao.Tunaomba kama hujaru……..” Innocent akastuka kidogo na kunyamaza mara alipomuona yule kijana aliyemstua Latoya.Alikuwa akitabasamu kama kawaida yake.
“ Tunaomba “ akaendelea Innocent
“ Kama hujaruhusiwa na familia ya marehemu kuingia katika mahala atakakozikwa marehemu basi usisogee mahala hapo.Narudia tena watakaoingia katika chumba chenye kaburi ni familia ya marahemu na wale tu ambao watakuwa wamechagulia na familia hii .Baada ya mazishi watu wote mtaruhusiwa kuweka mashada ya maua juu ya kaburi la mpendwa wetu “ akasema Innocent .Walinzi sita wa Latoya ambao kwa siku hii walikuwa na jukumu moja tu la kukaa pembeni ya jeneza ,wakiwa wamevalia sare maalum ambazo ni suti nyeusi wakalifunga jeneza lile zuri lenye nakshi za dhahabu na kisha wakasimama pembeni yake wakisubiri amri.Latoya akasimama,akifuatiwa na mzee Curtis halafu Innocent.Walinzi wale wakaanza kulisukuma jeneza lile kulipeleka katika chumba ambacho kulikuwa na kaburi. Vilio vya chini chini vikasikika toka kwa baadhi ya wanawake waliohudhuria msiba ule.
Hatimaye wakafika katika chumba ambacho ndani yake kuna kaburi.Ni chumba ambacho kilikuwa na uzuri wa namna yake.Ilikuwa ni sehemu iliyotengenezwa kwa ustadi wa ajabu sana.Walinzi wa Latoya wakasimama mlangoni Innocent akawafanyia ishara waingize jeneza ndani.Wakaliingiza ndani ,wakalitoa juu ya kile kitanda maalum wakaliweka juu ya vyuma vilivyokuwa juu ya kaburi.Innocent akawafanyia ishara watoke nje halafu mle ndani akabaki yeye,Latoya na mzee Curtis.Kwa pamoja wakalisogelea jeneza na kisha Latoya akaanza kufanya maombi.Baada ya maombi yale,akamuomba Innocent ausogeze mchanga uliokuwa karibu.Akamuomba mzee Curtis achote kidogo na kuurushia juu ya jeneza lile kama ishara ya kumzika rasmi mke wake . Bila ubishi mzee Curtis akachota mchanga na kuutupia juu ya jeneza halafu Latoya akamuomba atoke nje.Mzee Curtis hakutaka kubishana na mwanae,akageuka na kuanza kutoka Innocent akamshika mkono na kumsaidia akatoka na kukaa nje ya kile chumba.
“ Innocent sasa ni wakati wangu wa kumzika mama na ninaomba uwe pembeni yangu.Naomba chochote utakachokiona humu kibaki kuwa siri yako.Nimekuamini na nina imani utatunza uaminifu huo” akasema Latoya.Innocent akatikisa kichwa kuonyesha kukubaliana na Latoya lakini alikuwa akitetemeka kwa ndani.
“Naomba ulifungue jeneza” akasema Latoya.Innocent huku mikono ikimtetemeka akalifungua jeneza.Latoya akaweka mikono yake yote miwili katika paji la uso la mama yake halafu akaanza kuongea maneno ambayo Innocent hakuyaelewa.Alikuwa akiongea huku amefumba macho na katika mashavu yake kulionekana michirizi ya machozi.Aliendelea kuongea yale maneno yake na mara kikatokea kitu cha ajabu ambacho nusura kimfanye Innocent atimue mbio.Uso wake uliloa jasho na mwili ukazidi kumtetemeka.
Mwili wa mama yake Latoya ulikuwa ukitetemeka mle ndani ya jeneza kadiri Latoya alivyokuwa akiongea yale meneno yake.
“ Ouh Mungu wangu haya ni maajabu gani yanatokea? Mama yake Latoya si ameshakufa sasa mbona anatingishika ndani ya jeneza? Anaonekana ni mtu aliye hai kabisa. She’s not dead..She’s alive .Ouh Mungu wangu niepushe na mauza uza haya makubwa.” Akaomba Inno
“Latoya si mtu wa kukaa naye karibu hata kidogo.Ni mtu hatari sana na ninahisi anahusika kwa namna fulani na kifo cha mama yake .Kifo chake ni kama kimezungukwa na mazingira yasiyoeleweka .Hapana kwa hali hii sintaendelea tena kuwa karibu naye. Huyu si mtu wa kuwa naye karibu hata kidogo.Mambo anayoyafanya sijawahi kuyaona na hayafai hata kuyazungumza kwa watu.Lakini nitawezaje kumuacha wakati nimekwisha muahidi kwamba nitakuwa naye siku zote? Latoya ameniamini kupita hata baba yake mzazi.Ouh Mungu wangu naomba unisaidie.Niko katika wakati mgumu sana..” akawaza Innocent
Ndani ya jeneza uso wa mama yake Latoya ulionekana kama ukiwa na jasho.Bado Latoya alikuwa akiongea katika lugha ambayo Inno hakuielewa. Inno alikuwa anatetemeka mwili mzima kwa mambo aliyoyaona.Latoya akaifungua vifungo nguo aliyokuwa amevaa mama yake halafu akatoa kitu kidogo kama kisu toka ndani ya koti lake jeusi akakata kidogo sehemu ya bega na kwa mshangao damu ikachuruzika.Inno aliona ni kama mazingaombwe fulani. Alikuwa anatetemeka mwili mzima kwa maajabu yale.
“ Help me Jesus !! ..akasema Innocent kwa sauti ndogo huku akihisi kama shati lake linaloa jasho.
Latoya akachukua damu kidogo kwa kidole chake akaipaka katika paji lauso la mama yake na kuandika herufi XXII halafu akailamba kidogo damu ile.
“ Innocent mshike mama sehemu za miguuni.Naomba ukandamize kwa nguvu “ akasema Latoya ambaye jasho jingi lilikuwa linamtoka.Innocent akakandamiza sehemu za miguu kama alivyotakiwa na Latoya halafu Latoya akaanza kuongea tena ile lugha yake isiyoeleweka.Mama yake akaanza kutikisika mle ndani ya jeneza kana kwamba anataka kutoka.Inno alizidi kutetemeka na kuogopa.Hakuwahi kuona kwa macho yake mambo kama haya.Ilikuwa ni kama anaangalia filamu lakini hii haikuwa filamu bali ni kitu cha kweli alichokuwa akikishuhudia kwa macho yake.
Ghafla chumba kikaanza kujaa moshi mweupe mithili ya wingu zito.Innocent akazidi kuogopa.Moshi ule mweupe ambao haukuwa kama ule moshi wa kawaida ambao huumiza macho ukakifunika chumba chote kiasi kwamba hakuweza kuona kitu chochote halafu akaanza kuhisi kama jeneza lile likitikisika kwa nguvu akajikuta akisukumwa na kuanguka pembeni. Baada ya dakika tatu moshi ule ukaanza kupotea na mara chumba chote kikarudi katika hali yake ya kawaida.Latoya bado alikuwa amesimama pembeni ya jeneza la mama yake akiwa amefumba macho huku midomo yake ikimtetemeka . Innocent akahisi kama miguu yake haina nguvu ya kuinuka pale alipokuwa amekaa .Bado mwili ulikuwa unamtetemeka.
“ naogopa hata kumkaribia Latoya.Huyu si binadamu wa kawaida.“ akawaza Inno akimuangalia Latoya kwa macho ya woga.Bado alikuwa amesimama akiongea maneno yake yale ya ajabu ajabu .Akageuza shingo na kumtazama Innocent aliyekuwa kimya akimuangalia kwa uoga,akamfanyia ishara ainuke pale chini na asogee katika jeneza.Inno akainuka na kulikaribia lile jeneza akakutana na kioja kingine ambacho kilimfanya atake kukimbia.Jeneza lilikuwa tupu.Maitiya mama yake Latoya haikuwemo ndani yake.Mwili ukamtetemeka akamuangalia Latoya kwa wasi wasi akashindwa aseme nini.
“ Funga jeneza” akasema Latoya na Innocent akalifunga jeneza lile.
“ Shusha jeneza chini” akasema Latoya akimuelekeza Innocent alishushe jeneza lile chini kaburini.
Inno akafyatua kidude fulani kilichokuwa pembeni ya kaburi na taratibu jeneza likaanza kushuka chini huku Latoya akiongea maneno katika ile lugha yake anayoijua mwenyewe.Jeneza liligusa sakafu ya kaburi halafu Latoya akachukua mchanga kidogo akaumwagia ndani ya kaburi lile akamuamuru na Innocent naye afanye kama alivyofanya yeye.
“ Innocent kazi imekwisha.Tayari nimemzika mama yangu.Chochote ulichokiona humu ndani itabaki siri yako.Usithubutu kumweleza mtu yeyote yule.Kwa sasa simamia mafundi waweze kulifunika kaburi hili lakini asitokee yeyote atakayethubutu kuingia ndani ya kaburi..” akasema latoya.Innoent akaitika kwa kichwa ishara kwamba amekubaliana na maagizo yale .Latoya akatoka ndani ya kile chumba akaongozana na mzee Curtis wakarejea tena katika sehemu yao ya kukaa. Kilichofuata ikawa ni chakula na vinywaji huku kwaya mbali mbali zikiendelea kuimba nyimbo za maombolezo.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 40
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“ Funga jeneza” akasema Latoya na Innocent akalifunga jeneza lile.
“ Shusha jeneza chini” akasema Latoya akimuelekeza Innocent alishushe jeneza lile chini kaburini.
Inno akafyatua kidude fulani kilichokuwa pembeni ya kaburi na taratibu jeneza likaanza kushuka chini huku Latoya akiongea maneno katika ile lugha yake anayoijua mwenyewe.Jeneza liligusa sakafu ya kaburi halafu Latoya akachukua mchanga kidogo akaumwagia ndani ya kaburi lile akamuamuru na Innocent naye afanye kama alivyofanya yeye.
“ Innocent kazi imekwisha.Tayari nimemzika mama yangu.Chochote ulichokiona humu ndani itabaki siri yako.Usithubutu kumweleza mtu yeyote yule.Kwa sasa simamia mafundi waweze kulifunika kaburi hili lakini asitokee yeyote atakayethubutu kuingia ndani ya kaburi..” akasema latoya.Innoent akaitika kwa kichwa ishara kwamba amekubaliana na maagizo yale .Latoya akatoka ndani ya kile chumba akaongozana na mzee Curtis wakarejea tena katika sehemu yao ya kukaa. Kilichofuata ikawa ni chakula na vinywaji huku kwaya mbali mbali zikiendelea kuimba nyimbo za maombolezo.

ENDELEA……………………

Wakati zoezi la chakula likiendelea Innocent alikuwa akiwasimamia mafundi kutoka kampuni ile iliyotengeneza kaburi la mama yake Latoya katika kulifunika.Alikuwa amekaa pembeni ya chumba kile kilichokuwa na nakshi za kuvutia sana akiwa na mawazo mengi mno.Alichokiona leo kilimstua sana..
“ Ndani ya kaburi hili kumuwekwa jeneza tupu.Mwili wa mama yake Latoya haupo.Umekwenda wapi? ..akajiuliza Inno bila kupata jibu.jasho jingi likaendelea kumtiririka.
“ Latoya ni mtu wa namna gani ? Nimeshindwa kumuelewa ni kiumbe wa namna gani.Naogopa hata kumsogelea . Ni mtu hatari sana na maisha yake yametawaliwa na mambo ya kutisha sana.Lazima nijitoe katika maisha haya haraka iwezekanavyo.Ili niwe salama ,lazima nikae mbali naye.Japokuwa ameniamini kupita watu wote,sina namna nyingine zaidi ya kuyaokoa maisha yangu zaidi ya kuondoka wakati bado nina nafasi.” Akawaza Innocent.
“ Tatizo nimekwisha zijua siri zake.je atakubali kuniachia niende zangu? Nadhani hiyo ndiyo itakuwa mbaya zaidi na inaweza hata kumpandisha hasira akaamua kuniua kabisa kwa sababu hataki siri zake zijulikan.Sikutegemea kama siku moja ningeingia katika maisha kama haya.” Akaendelea kuwaza Inno huku mafundi wakiendelea kulifunika kaburi.
Shughuli ya kulifunika kaburi la mama yake Latoya ilichukua kama saa moja hivi kisha watu wakaruhusiwa kuingia na kuweka mashada ya maua.Muda wa nusu saa kaburi lote lilikuwa limefunikwa na maua hata likashindwa kuonekana.Wakati zoezi lile la uwekaji wa maua likiendelea Latoya alikuwa akisalimiana na watu mbali mbali ambao walikuja kumpa pole.Wakati akisalimiana nao mara akatokea tena yule jamaa aliyemfanya astuke wakati wa kutoa heshima za mwisho. Latoya akastuka tena alipomuona akamshika mkono na kumuongoza wakaelekea ndani.
Zoezi la uwekaji wa mashada ya maua likakamilika na baadhi ya watu wakataka kuanza kuondoka akiwemo mheshimiwa waziri mkuu.Inno akamtafuta Latoya lakini hakumuona.Walinzi wake wakasema kwamba alikuwa ameelekea ndani ya nyumba akiwa ameongozana na kijana mmoja .
“ lazima atakuwa ni yule yule kijana aliyemfanya akastuka muda ule.Huyu kijana ni nani ? I must find out” akawaza Inno huku akipiga hatua kuelekea ndani. Katika chumba kidogo ambacho Latoya huwa anakitumia kwa maongezi ya faragha mlango haukuwa umefungwa Inno akajitokeza na kusikia kama watu wakibishana.Akatega sikio na kuisikia sauti ya Latoya.
“ Brandon siko tayari kwa sasa…Utalazimika kunisubiri hadi hapo nitakapokuwa tayari.Nina jambo kubwa na la msingi sana ambalo lazima nilitimize kwani ni ahadi niliyojiwekea mimi mwenywe kuitimiza kabla sijafa.Kwa namna yoyote ile lazima niitimize ahadi hiyo..” Akasema Latoya kwa sauti ya ukali
“ Nitasubiri kwa muda gani Latoya ? Sina muda zaidi wa kuendelea kusubiri. Muda wangu umefika…” akasema yule kijana
“ Brandon utanisikia na kufuata nitakavyokwambia.Lazima usubiri na hiyo ni amri na si ombi.Nasem…………..” Latoya hakumalizia sentensi yake akasikia mlango unagongwa.Alikuwa ni Innocent.wote wawili wakastuka sana.
“ Innocent ! akasema Latoya kwa mstuko.
“ How long have you been here at the door? Akauliza Latoya.
“ Ndiyo nakuja sasa hivi Latoya..kwani vipi? Akauliza Inno
“ Nothing’ akajibu Latoya.
“ So this is Innocent ? akauliza Brandon huku akimuangalia Innocent kwa macho ya mshangao.
“ Yah I’m Innocent” akasema Inno huku akimpa Brandon mkono.
“ Nimefurahi kukuona Innocent..Mimi na wewe tutakutana mara nyingi kuanzia sasa” akasema Brandon na Inno akashindwa kumuelewa akabaki anamuangalia.
“ Latoya waziri mkuu na ujumbe wake wanataka kuondoka.tunatakiwa tukawaage.” Akasema Innocent huku sauti yake ikitetemeka.
“ Brandon nadhani wewe tumekwisha malizana unaweza ukaondoka.Tutazidi kuonana” akasema Latoya akamshika mkono Innocent wakatoka mle chumbani huku Brandon akiwaangalia kwa macho makali akionekana kuwa na hasira.
“ Sharha..patakamos lahuut ba venda..Usskhoom sha lavia” akatamka maneno haya Brandon .Latoya hakumjali akamshika Inno mkono wakaondoka zao .Bado Inno alizidi kuchanganyikiwa aligeuka akamtazama tena Brandon aliyekuwa bado amesimama akiwaangalia .
" Huyu kijana ni nani na anataka nini kwa Latoya? Ni kwa nini Latoya mara tu alipomuona alistuka sana ? ..Innocent akawaza akiwa ameongozana na Latoya wakielekea sehemu ya wageni wa heshima kwenda kuagana na viongozi na wageni waliokuwa wamehudhuria mazishi yale ya mama yake.
" Brandon siko tayari kwa sasa…Utalazimika kunisubiri hadi hapo nitakapokuwa tayari.Nina jambo kubwa na la msingi sana ambalo lazima nilitimize kwani ni ahadi niliyojiwekea mimi mwenywe kuitimiza kabla sijafa.Kwa namna yoyote ile lazima niitimize ahadi hiyo..” kauli hii ya Latoya akimwambia Brandon ilizidi kujirudia kichwani kwa Innocent.
"Alikuwa na maana gani aliposema kwamba hayuko tayari kwa sasa? hayuko tayari kwa jambo gani? Ni jambo gani ambalo Latoya ameweka ahadi ya kulitimiza kabla hajafa?." Kichwa cha Innocent kikajaa mawazo mengi sana lakini hakuweza kupata majibu .
" Maisha ya Latoya ni fumbo kubwa .Kwa sasa nina hakika kabisa kwamba huyu ni mfuasi wa nguvu za giza kwa mambo niliyoyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe leo." Akawaza Innocent wakiwa tayari wamefika eneo la jukwaa kuu alikokuwapo mheshimiwa waziri mkuu pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi mbali mbali toka serikalini.Latoya akamshukuru na kuagana na mheshimiwa waziri mkuu pamoja na ujumbe wake wote wakaondoka wakifuatiwa na baadhi ya watu waliohudhuria shughuli ile ya mazishi ya mama yake Latoya.Baada ya idadi kubwa ya wageni kuondoka Latoya akamuelekeza Irene amuandalie mzee Curtis chumba cha kulala katika moja ya vyumba vya watu maalum Latoya alipatwa na mshangao pale baba yake mzazi mzee Curtis alipokataa kata kata kulala katika jumba hili la Latoya na akataka apelekwe nyumbani kwake .
" Baba kwa nini hutaki kulala hapa kwangu? akauliza Latoya
" Utanisamehe Latoya lakini kwa sasa ninahitaji kulala nyumbani kwangu katika chumba nilichokuwa nikilala na mke wangu." akasema mzee Curtis.Latoya akaumia mno moyoni kwa kauli ile ya baba yake.
" Masikini baba yangu anateseka sana kwa kifo cha mama.Ingawa hawezi kunieleza wazi wazi lakini ni wazi ameumia mno na mambo yaliyotokea.Kifo cha mama hata mimi kimenihuzunisha mno kwani sikuwa nimetarajia kama kingetokea. Kifo hiki cha mama yangu kinazidi kuniongezea maumivu na mateso makali. " akawaza Latoya huku akimuangalia baba yake kwa macho ya huruma.
"Baba nafahamu ni kwa namna gani unavyoumia kwa kifo cha mama lakini kurudi tena pale nyumbani na kulala katika chumba kile kile ulichokuwa ukikitumia na mama kutakuongezea machungu zaidi na kukufanya uzidi kuumia.Baba sitakii uendelee kuumia zaidi.Kesho nitakuhamishia nje ya nchi kwa ajili ya mapumziko jambo ambalo linaweza kukusaidia kupunguza machungu ya kifo cha mama" akasema latoya
" latoya huna haja ya kuhangaika na mimi hata kidogo.Baada ya kifo cha mke wangu niliyempenda sioni thamani yangu tena hapa duniani. Mke wangu ndiye alikuwa kila kitu kwangu.Nimeshuhudia kwa macho yangu namna alivyofariki nimeumia mno.Sitaki kwenda sehemu yoyote ile ninataka kubaki hapa hapa nyumbani kwangu Tanzania niendelee kumlilia mke wangu.Sihitaji kwenda ulaya wala sehemu nyingine yoyote ile.Nataka nikaishi nyumbani kwangu katika chumba nilichokuwa nikilala na mke wangu " akasema mzee Curtis .Latoya alishindwa kujizuia akatoa machozi.
"Sawa baba nimekuelewa.Nitakurejesha kwako lakini utakuwa chini ya uangalizi maalum wa walinzi na wahudumu wangu." akasema Latoya
" sihitaji chochote toka kwako kwa sasa Latoya.Just forget me for a while.I need a world of my own." akasema Mzee Curtis.Latoya akazidi kuumia kwa maneno yake ya baba yake.
" Baba siwezi kukuacha hata sekunde moja.wewe ndiye baba yangu na familia yangu pekee." akasema latoya.Baba yake akamuangalia kwa macho makali na kusema
" Your father and your family is your money.Utajiri wako ndiyo kila kitu kwako kwa sasa.Money is everything to you.From now on forget that you have a father" akasema mzee Curtis kwa ukali.Latoya akashindwa kujizuia kuangusha machozi.
" Innocent take my father home.Take him away from here..." akasema Latoya huku akilia.
" Latoya......" Innocent akataka kusema kitu lakini Latoya akamzuia
" Fanya ninavyokwambia Innocent..Mpeleke baba nyumbani kwake" akaamuru Latoya.Bila ubishi Innocent akamshika mkono na kumsaidia mzee Curtis kutembea hadi katika gari .Wakati anamuingiza mzee Curtis katika gari mara akageuka na kukutana na sura yenye tabasamu ya Brandon akiwa ameegemea gari lililokuwa mita chache .Wakatazamana kwa sekunde kadhaa halafu Innocent akaingia garini na kuliwasha na taratibu akaanza kundoka . Mwili wake ulikuwa umesisimka sana baada ya kumuona Brandon akiwa pale tena akiwa na tabasamu
" Who is this guy?..Innocent akajiuliza
" Anataka nini kwa Latoya? Kwa nini hataki kuondoka pale nyumbani kwa Latoya? " Bado aliendelea kuumiza kichwa .Ujio wa Brandon hata yeye ulianza kumuogopesha .
" I must find out who is that guy...Lazima niufahamu ukweli Brandon ni nani" Innocent akajikuta akitamka maneno haya kwa sauti na kumfanya mzee Curtis kustuka.
" Innocent unaongea na mimi? akauliza mzee Curtis
" Hapana mzee.. Kichwa changu kina mambo mengi sana siku ya leo" akasema Innocent
" Innocent wewe ni kijana wangu.Ni zaidi ya mwanangu kwa hiyo ninaomba nikueleze ukweli." akasema mzee Curtis
" Nimeamua kukaa mbali na maisha ya Latoya.Ni binti yangu wa pekee na ninampenda sana lakini kwa maisha yake ya sasa imenilzimu kukaa mbali naye.Kifo cha mke wangu kimeniumiza mno na hasa nikikumbuka mazingira kilivyotokea.Moyo wangu unauma kiasi ambacho siwezi kuelezea.Siwezi tena kuendelea kuwa sehemu ya maisha ya Latoya kwa sasa.Fedha mali na utajiri ndivyo vitu vyake vya thamani kwa sasa.Ninahitaji kuwa mwenyewe niendelee kumlilia mke wangu" akanyamaza kidogo halafu akaendelea
"Innocent ninakuomba kitu kimoja kijana wangu"
" Omba chochote mzee usihofu" akajibu Innocent
" Ninakuomba usimuache Latoya hata kwa sekunde moja.Wewe ndiye mtu pekee ambaye anakuamini kwa sasa na ambaye unaweza ukamfanya akatabasamu na kuwa na furaha.Nina imani hata yeye mwenyewe anaumia sana kwa kifo cha mama yake na mtu pekee wa kumfariji ni wewe. Hana mfariji mwingine kwa sasa zaidi yako." akasema mzee Curtis.Innocent hakujibu kitu.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………
 
BEFORE I DIE

SEHEMU YA 41


ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA

" Nimeamua kukaa mbali na maisha ya Latoya.Ni binti yangu wa pekee na ninampenda sana lakini kwa maisha yake ya sasa imenilzimu kukaa mbali naye.Kifo cha mke wangu kimeniumiza mno na hasa nikikumbuka mazingira kilivyotokea.Moyo wangu unauma kiasi ambacho siwezi kuelezea.Siwezi tena kuendelea kuwa sehemu ya maisha ya Latoya kwa sasa.Fedha mali na utajiri ndivyo vitu vyake vya thamani kwa sasa.Ninahitaji kuwa mwenyewe niendelee kumlilia mke wangu" akanyamaza kidogo halafu akaendelea
"Innocent ninakuomba kitu kimoja kijana wangu"

" Omba chochote mzee usihofu" akajibu Innocent

" Ninakuomba usimuache Latoya hata kwa sekunde moja.Wewe ndiye mtu pekee ambaye anakuamini kwa sasa na ambaye unaweza ukamfanya akatabasamu na kuwa na furaha.Nina imani hata yeye mwenyewe anaumia sana kwa kifo cha mama yake na mtu pekee wa kumfariji ni wewe. Hana mfariji mwingine kwa sasa zaidi yako." akasema mzee Curtis.Innocent hakujibu kitu.



ENDELEA………………………..


" Innocent naomba uniahidi kwamba hutamuacha Latoya peke yake.She needs you now more than anyone.Anahitaji mtu wa kuwa naye karibu.Anahitaji rafiki na mfariji na mtu huyo si mwingine ni wewe pekee" akasema mzee Curtis.Innocent bado aliendelea kukaa kimya akitafakari kisha akasema
" Nimekusikia mzee Curtis na nimekuelewa.Nitakuwa na Latoya na sintamuacha .Nitahakikisha anakuwa na furaha siku zote.I give you my word" akasema Innocent

" Nashukuru sana Innocent.Kwa sasa moyo wangu una amani baada ya kauli yako hii. Nina hakika kwamba kwa muda huu ambao nitakuwa nje ya maisha ya Latoya atakuwa katika mikono salama. " akasema mzee Curtis halafu ukimya ukatawala mle garini.

" Kwa muda huu mfupi nimeyashuhudia mambo mengi sana ya kutisha yanayoyazunguka maisha ya Latoya. Kubwa zaidi ni hili tukio la leo.Sijawahi kushuhudia kwa macho yangu tukio kama lile.Ni tukio ambalo litakuwepo kichwani kwangu hadi siku ninaingia kaburini.Mzee curtis ameniomba niwe karibu na mwanae na nimemkubalia na kumuhakikishia kwamba nitakuwa karibu na mwanae siku zote. akawaza Innocent .Sura ya Latoya akitoa machozi baada ya maneno makali aliyoambiwa na baba yake mzee Curtis ikamjia tena kichwani akajikuta akimuonea huruma.
" Ana wakati mgumu sana Latoya.She needs someone by her side and that some one is me..Nitaendelea kuwa naye.Lakini kama nimekubali kuendelea kuwa mtu wa karibu wa latoya inanibidi niyakubali pia maisha anayoishi pamoja na mauza uza yake.Je niko tayari kuishi na Latoya pamoja na mauza uza yake yote ? akajiuliza Innocent
" I think I'm ready.Picha ya Latoya akilia baada ya maneno ya mzee Curtis imenipa uchungu sana .Anahisi upweke wa hali ya juu kwa sasa.Kwanza mama yake amefariki ,halafu baba yake ameamua kukaa mbali naye.Kwa sasa hana mtu yeyote wa karibu. Mimi ndiye pekee mtu wake wa karibu niliyebaki.Nikisema na mimi niondoke Latoya atakuwa katika wakati mgumu sana.Ngoja niendelee kuwa karibu naye." akawaza Innocent wakati akikata kona kuingia katika mtaa anaoishi mzee curtis.Alisimimisha gari na kumshusha mzee Curtis.Watu wote waliokuwepo pale nyumbani wakiendelea na maombolezo wakapigwa na butwaa baada ya kumuona mzee Curtis akirejea.Wote hawakutarajia kama angeweza kurejea mapema namna hii.Hakutaka maongezi mengi akamuomba Innocent ampeleke hadi katika chumba chake cha kulala.Innocent akafanya hivyo halafu akamuaga lakini kabla hajaondoka mzee curtis akaomba aongee naye maneno machache
" Innocent napenda nichukue fursa hii kushukuru sana kwa kujitoa kwako kufanikisha shughuli za mazishi ya mke wangu mpendwa.Umefanya kazi kubwa sana ambayo sina hakika kama nina chochote ninachoweza kukulipa zaidi ya neno ahsante sana.Nafahamu kwamba itachukua muda mrefu kwa sisi kuonana tena kwa hiyo naomba nikupe zawadi hii ndogo.Huu ni mkufu wa dhahabu ambao nilipewa na baba mkwe wangu siku namuoa mama yake Latoya kama zawadi na mimi nikauhifadhi kwa dhumuni la kumzawadia kijana ambaye atamuoa binti yangu Latoya.Nimekupa mkufu huu wa gharama kubwa sana kwa sababu sina hakika kama nitamuona mwanaume ambaye atamuoa Latoya .Nimekupa wewe kwa sababu wewe ndiye mtu wake wa karibu sana unayemfanya awe na furaha siku zote.Natumai utautunza mkufu huu na utakuwa ukinikumbuka kila utakapokuwa unauangalia." akasema mzee Curtis huku akimkabidhi Innocent kiboksi kidogo chenye mkufu wa gharama kubwa sana.Inno akashukuru halafu akaagana na mzee Curtis akaondoka akarejea tena katika makazi ya Latoya.Bado kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi .Wakati akishuka garini mara akatokea Brandon akiwa anatabasamu.Innocent akastuka baada ya kumuona tena bado akiwa maeneo yale.

" You again !!.... akasema Innocent kwa mshangao

" Mbona umestuka innocent uliponiona? akauliza Brandon huku akitabasamu

" Mbona bado uko hapa wakati Latoya alikwisha kuomba uondoke? akasema Innocent

" Innocent hii ni sehemu ya msiba na sijawahi kushuhudia hata siku moja mtu akifukuzwa msibani.Kama ulivyo wewe ,sisi sote tulioko hapa ni watu wa karibu na Latoya na tunampenda sana .Innocent unaonekana hujafurahia hata kidogo kuniona mimi hapa" akasema Brandon huku akitabasamu .Innocent bado aliendelea kumtumbulia macho.

" Innocent usijali rafiki yangu ,bado tutaendelea kufahamiana zaidi kwa sababu nitakuwepo hapa kwa muda mrefu tu.Kwa hiyo usiwe na haraka bado ya kutaka kunifahamu na wala usinichukie kwa kuniona hapa." akasema Brandon halafu akageuka na kuondoka akaenda kuungana na waombolezaji ambao bado walikuwepo pale msibani.

" Who is this guy..? kwa mara nyingine tena Innocent akajiuliza swali hili bila kupata majibu.Alibaki amekaa ndani ya gari akitafakari kisha akashuka na kuingia ndani.

" Innocent, Madam Latoya alisema kwamba ukija uelekee moja kwa moja bustanini kwake" akasema Irene.Bila kupoteza wakati Innocent akapanda ngazi kuelekea katika bustani ya Latoya iliyoko juu kabisa ya jengo lile.Alikuwa akitembea kwa wasi wasi mkubwa hasa alipofika katika ghorofa ya mwisho ambayo ni ya latoya pekee.Mambo aliyoyashuhudia leo yalimfanya atembee kwa wasi wasi mkubwa sana.Kulikuwa na ukimya wa ajabu na wa kutisha.Innocent akaingia bustanini na kwa mbali akamuoa Latoya akiwa ameinamia meza.Akatembea taratibu akamfuata.
" Latoya " akaita Innocent baada ya kuifikia ile meza aliyokuwa ameiinamia Latoya.taratibu akainua uso wake na kumtazama Innocent

" Umerudi Innocent.." akasema Latoya kwa uchovu.
" Ndiyo Latoya nimerudi "akasema Innocent halafu Latoya akainuka pale alipokuwa amekaa.

" Follow me " akasema Latoya.Innocent akamfuata hadi katika chumba kimoja ambacho hajawahi kuingia.Hakikuwa chumba kikubwa sana na kilikuwa na sofa nzuri nyeupe" Latoya akazima taa na kuwasha mishumaa miwili.Innocent akashangaa.

" Mbona unazima taa? akauliza Inno lakini Latoya hakumjibu kitu.

" Innocent come and sit here close to me " akasema Latoya .Huku akiwa na wasi wasi mwingi Inocent akamfuata Latoya na kukaa karibu yake.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda kwa kasi na alihisi msisimko fulani mwilini mwake baada ya Latoya kumshika kiganja chake cha mkono.
" Innocent nimekuleta hapa katika chumba hiki ambacho huwa ni chumba changu cha tafakari.Ninapokuwa na jambo lolote lile lenye kuniumiza kichwa changu na kuhitaji faraja huja na kukaa humu nikatafakari kwa kina na kupata majibu.Mara nyingi nikiwa katika tafakari huwa nawasha mishumaa kwa hiyo nakuomba uwe na amani kwa kitendo hiki." akasema Latoya.

" Innocent msiba wa mama umekwisha.Ninapenda kuchukua fursa hii kukushukuru sana kwa msaada wako mkubwa wa kuweza kufanikisha msiba huu kuisha salama.Haikuwa kazi ndogo lakini hukulala hadi umehakikisha kila kitu kimekwenda sawa sawa.Sipati neno zuri la kukushukuru kwa mambo yote uliyoyafanya na siwezi kusema ahsante kwa sasa .Bado naendelea kutafakari ni kwa namna gani nitaweza kusema neno ahsante kwako." akasema Latoya halafu akauvuta zaidi mkono wa Innocent ambaye mapigo ya moyo wake yakaongezeka.

" Innocent mengi yametokea katika siku hizi chache za msiba wa mama .Umeshuhudia mengi na kama nilivyokuomba toka awali kwamba yote uliyoyaona na kuyasikia yatabaki kuwa moyoni mwako na hakuna mtu mwingine yeyote anayetakiwa kuyafahamu.Tukiachana na hayo" Latoya akanyamaza kidogo halafu akausogeza mkono wa innocent karibu kabisa titi lake lililosimama la upande wa kushoto .Innocent kijasho kikamtoka.Mwili ulizidi kumsisimka .Latoya naye mapigo wa moyo wake yalikuwa yakienda kwa kasi kubwa.Akavuta pumzi ndefu na kusema.

" Innocent nimekuita hapa kama mtu wangu wa pekee kabisa ambaye umebakia kwa sasa baada ya baba kuamua kukaa mbali nami.Simlaumu baba yangu najua ameumizwa sana na kifo cha mke wake kipenzi na kwa hiyo anahitaji muda wa kuwa peke yake. Hata mimi pia nimeumizwa sana na kifo hiki cha mama pengine kuliko mtu yeyote.Na kama alivyoamua baba kwamba anahitaji kuwa peke yake kwa sasa hata mimi ninahitaki kupata muda wa kupumzika na kutuliza akili yangu.Mambo mengi yametokea katika muda mfupi sana.I need a world of just two of us.Me and you" akasema Latoya huku akiuinua mkono wake wa kulia na kuupitisha shingoni mwa Innocent ambaye alizidi kusisimkwa mwili.
" No you cant !!!.........." Ilisema sauti ya mtu na kumfanya Latoya astuke.

" Umeisikia sauti hiyo Innocent" akauliza Latoya
" Hapana sijasikia sauti yoyote " akasema Innocent akimshangaa Latoya

" Brandon ! ..Its him " akasema latoya kwa hasira.Akaufunika uso wake kwa viganja vyake vya mikono .Innocent akazidi kushangaa.
" Innocent nenda chumbani kwako ukapumzike.Tutaongea kesho .I need to take care of something" akasema Latoya huku akiinuka.Uso wake ulionyesha hasira za wazi.Innocent akaogopa sana na moja kwa moja akaelekea chumbani kwake.

" What happened? Who is Brandon ? Anataka nini kwa Latoya? Innocent akajiuliza maswali mfululizo bila kupata jibu.
Kitendo cha Latoya kumshika mkono na kuuweka kifuani kwake kilimjia tena Innocent kichwani akasisimka sana.Hakuwahi kupata msisimko wa namna ile katika maisha yake.

" Vidole vyangu viligusa kifua cha Latoya.Niliweza kuhisi namna mapigo yake ya moyo yalivyokuwa yamebadilika na kwenda kwa kasi.Gosh ! kitendo kile kilinisisimua mno.Sijawahi kusisimkwa kama hivi katika maisha yangu." akawaza Innocent.

"Na kama alivyoamua baba kwamba anahitaji kuwa peke yake kwa sasa hata mimi ninahitaki kupata muda wa kupumzika na kutuliza akili yangu.Mambo mengi yametokea katika muda mfupi sana.I need a world of just two of us.Me and you" maneno haya ya Latoya yakamjia tena kichwani akatabasamu.

" Latoya anahitaji mapumziko katika sehemu ambayo tutakuwa wawili pekee.Aliwahi kunidokeza kuhusu suala hili kwamba anataka twende wote mapumzikoni katika kisiwa ambacho huwa anakwenda kupumzika yeye peke yake.Sifahamu nini kitakwenda kutokea huko lakini ninajikuta nikitamani kwenda huko na kupumzika pamoja naye.Licha ya maisha yake yaliyozungukwa na fumbo kubwa bado najikuta nikitamani kuwa karibu naye kila wakati " akawaza Innocent halafu akatabasamu

" Ninahisi kuna kitu kinatuvuta karibu mimi na Latoya kwa sababu kwanza tumeonana kwa muda mfupi sana na katika muda huo mfupi sana tumetokea kuwa marafiki wakubwa mno na kila mtu anashangaa hii imetokeaje.Ameniamini na kunishirikisha katika mambo yake ya siri ambayo hakuna mtu mwingine yeyote ambaye amewahi kuyashuhudia..Nikiwa karibu na latoya ninajihisi tofauti sana." akaendelea kuwaza Innocent
" Sina hakika kama hisia zangu ni za kweli lakini lazima niwe mkweli I'm in love with her.I've never felt this way before. Ouh Mungu wangu katika wanawake wote wa dunia hii kwa nini moyo wangu uangukie kwa Latoya ? Siku zote nilitaka msichana wa ndoto zangu awe ni wa kawaida asiyekuwa tajiri ,mwenye uzuri wake wa asili ,roho nzuri na anayejua kupenda lakini moyo wangu umeangukia kwa mwanamke bilionea lakini mwenye kila sifa za mwanamke ninayemuhitaji.Latoya naye hujisikia furaha sana kila anapokuwa karibu na mimi na ndiyo maana anataka kuwa nami kila dakika . Moyo wangu haunidanganyi kwamba mimi na Latoya tunapendana japokuwa hakuna aliyemweleza mwenzake na ninadhani hata baba yake mzee Curtis ameliona hilo na ndiyo maana akanikabidhi huu mkufu wa thamani kubwa ambao alikuwa amepanga kumpa zawadi mwanaume ambaye atamuoa binti yake.Je huu ni utabiri wa mzee Curtis kwamba mimi na Latoya tunaweza tukaoana ? akajiuliza Innocent.Akachukua kile kiboksi chenye mkufu aliopewa na mzee Curtis akautoa mkufu ule akautazama akatabasamu

" Nadhani mzee Curtis kuna kitu amekiona na ndiyo maana amenisisitiza mno kwamba nisimuache binti yake.Hajawahi kumuona Latoya akiwa na furaha kama katika kipindi hiki ambacho amekutana nami.Anahisi mwanae yuko salama zaidi nikiwa karibu naye.Ninakumbuka pia niliwahi kuota ndoto fulani ambayo ilikuwa ni kama kweli.Katika ndoto ile niliambiwa kwamba mimi ndiye mlinzi wa Latoya na ninatakiwa kumlinda dhidi ya watu wanaotaka kumdhuru.Nakumbuka nilichomwa na moto mkono wangu wa kulia na nilipoamka toka usingizini nilisikia mkono wangu ukiwa na maumivi makali ya kuungua .Maumivu yale yalipotea baada ya kutaka kumshika Latoya mgongoni na nikajikuta nikipigwa na kitu kama umeme.Nadhani kukutana kwangu na Latoya kuna sababu maalum na si hivi hivi ." Akainuka pale kitandani akavua koti na kulitundika kabatini.

" Usiku huu hisia za mapenzi yaliyopo kati yetu zilijidhirisha wazi wazi pale chumbani.Nilimuona Latoya akiwa katika hisia kali na za ukweli.Aliongea kwa sauti laini na ni wazi alimaanisha kile alichokisema.Nilisisimka mno alipoushika mkono wangu na kuupeleka kifuani kwake.Aliuweka mkono wangu kifuani kwake katika titi lake la kushoto nikahisi kama mwili wangu unakufa ganzi kwa msisimko nilioupata.Aliuzungusha mkono wake shingoni mwangu nilihisi kuishiwa nguvu.Sijawahi kusisimkwa namna ile.Nilianza kuhisi kama ninaona maluwe luwe vile.I felt so different like I was in a different world.Nilikuwa katika hisia kali sana japokuwa nilikuwa nikiogopa.Brandon ndiye aliyeharibu kila kitu.Yeye ndiye aliyemstua Latoya na kukatisha maongezi yetu.Damn you Brandon.!!."


TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 42
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Usiku huu hisia za mapenzi yaliyopo kati yetu zilijidhirisha wazi wazi pale chumbani.Nilimuona Latoya akiwa katika hisia kali na za ukweli.Aliongea kwa sauti laini na ni wazi alimaanisha kile alichokisema.Nilisisimka mno alipoushika mkono wangu na kuupeleka kifuani kwake.Aliuweka mkono wangu kifuani kwake katika titi lake la kushoto nikahisi kama mwili wangu unakufa ganzi kwa msisimko nilioupata.Aliuzungusha mkono wake shingoni mwangu nilihisi kuishiwa nguvu.Sijawahi kusisimkwa namna ile.Nilianza kuhisi kama ninaona maluwe luwe vile.I felt so different like I was in a different world.Nilikuwa katika hisia kali sana japokuwa nilikuwa nikiogopa.Brandon ndiye aliyeharibu kila kitu.Yeye ndiye aliyemstua Latoya na kukatisha maongezi yetu.Damn you Brandon.!!."

ENDELEA…………………………

" Huyu kijana ni nani na anataka nini kwa Latoya? Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi toka mchana lakini bado sijapata jibu.Kuna kitu gani kinachoendelea kati ya Brandon na Latoya? Kwa nini Latoya huwa ana wasi wasi kila akimuona Brandon.Jioni hii wakati nikirudi kutoka kumpeleka mzee Curtis nimekutana na Brandon na akaniambia kwamba ataendelea kuwepo hapa kwa Latoya.Bado nayakumbuka maneno yake alisema hivi:
" Innocent usijali rafiki yangu ,bado tutaendelea kufahamiana zaidi kwa sababu nitakuwepo hapa kwa muda mrefu tu.Kwa hiyo usiwe na haraka bado ya kutaka kunifahanmu na wala usinichukie kwa kuniona hapa." “Haya ni maneno aliyoniambia Brandon jioni hii tulipoonana.Lazima kuna kitu ambacho kinaendelea baina ya Latoya na Brandon.Niliwasikia wakibishana jioni ya leo na Latoya akimwambia kwamba hayuko tayari kwa sasa na Brandon itamlazimu amsubiri hadi hapo atakapokuwa tayari.Kitu gani hicho ambacho Latoya hayuko tayari kumpa Brandon kwa sasa.Kitu kingine kinachonishangaza sana Latoya ameisikiaje sauti ya Brandon wakati tumekaa kule chumbani? Mimi sikusikia sauti yoyote ya Brandon lakini Latoya aliisikia wazi na akatoka mle chumbani akiwa amekasirika sana.Inawezekana Brandon naye akawa ni mtu mwenye mauza uza kama ya Latoya? akajiuliza Innocent bado alikuwa amesimama ameliegemea kabati.
" Yawezekana akawa ni mtu mwenye mambo kama ya Latoya lakini nadhani kuna zaidi ya hapo.Ninahisi kama wanaweza wakawa na mahusiano ya kimapenzi.Kuna kila sababu ya kuamini hivyo hasa kutokana na namna Latoya anavyobadilika mara tu akimuona Brandon.Hata Brandon naye amekuwa akistuka kila anaponiona.Nadhani hata yeye amehisi kwamba Latoya ananipenda na ndiyo maana amekuwa na wasi wasi sana na mimi.Kama hisia zangu ni za kweli basi kutakuwa na kazi kubwa kati ya Latoya na Brandon na Brandon na mimi.Ukweli wa haya yote anao Latoya lakini nitawezaje kumuuliza kuhusu Brandon? Sitaki kuanza kuyachimba maisha ya Latoya kwa sababu ni kitu ambacho hakipendi.I'm confused " Innocent akaenda kuketi sofani.Alikuwa na mawazo mengi sana.


* * * *


Baada ya kuachana na Innocent Latoya akashuka chini huku uso wake ukionyasha wazi kwamba alikuwa amekasirika sana.
" Brandon kwa nini ananifanyia hivi? Nimekwisha mweleza ukweli kwamba siko tayari kwa sasa lakini kwa nini aendelee kuwa king'ang'anizi? Ameniharibia wakati wangu mzuri na mtu ninayempenda kuliko wote. Ouh Gosh ! Nilikuwa na wakati mzuri sana na Innocent.Sijawahi kuwa na wakati niliokuwa katika hisia kali za kimapenzi kama ule.Nilihisi kama siko duniani.Kwa muda ule nilisahau machungu yote ya kufiwa na mama yangu.Innocent is my man.Kwa sasa nina uhakika huo. Kwa miaka hii yote nilikuwa nikitafuta mtu ambaye angeweza kunisisimua na kunifanya hisia zangu zihame toka katika dunia hii.Mtu huyo ni Innocent pekee.Kuwa naye karibu nilijihisi kama vile niko mbingu ya saba.I love innocent and I'll do anything..I mean anything to be with him.Nothing is going to stop me from loving him . Ninafahamu kwamba nitakuwa naye kwa muda mfupi sana niliobaki nao lakini hiyo haijalishi.Nitakufa nikiwa na furaha kwa sababu ndoto yangu tayari imetimia na nimekutana na mtu ambaye nilikuwa nikimuota kwa miaka mingi.A man of my dream." akawaza Latoya akishuka ngazi kuelekea ya chini.
" Brandon anataka kuiharibu furaha yangu ambayo nimeihangaikia kwa miaka mingi.Kwa nini hataki kuniona nikiwa na furaha kwa siku hizi chache nilizobaki nazo? Ninaona hapendezwi kabisa na ukaribu wangu na Innocent.Siwezi kumruhusu kabisa akaingilia masuala yangu na Innocent.Innocent is my life.He's my everything.Nimekwisha muonya Brandon mara ya kwanza na nitamuonya asirudie tena kuyafuatilia maisha yangu binafsi.Nadhani bado hajanifahamu vizuri.Mimi ni mtu mwema sana lakini ninaweza kubadilika na kuwa mbaya mno kwa yule ambaye hataki kufuata ninavyotaka mimi. Kama akiendelea na tabia yake hii ya kutotaka kunisikia ninavyotaka mimi nitamuonyesha upande wangu wa pili namna ninavyobadilika" akawaza latoya .Moja kwa moja akaelekea katika chumba chake kidogo ambacho hukitumia kwa maongezi ya faragha.Akaufungua mlango na kumkuta Brandon akiwa amekaa kitini huku miguu ameipandisha juu ya meza.Latoya akamtazama kwa macho makali halafu akainyanyua miguu ya Brandon na kuishusha chini.
" So its you again..! akasema Latoya .Brandon hakumjibu kitu
" Kwa nini unanifanyia hivi Brandon? Kwa nini unanikosea heshima ? akasema Latoya kwa ukali.
" Sijakukosea heshima Latoya na wala sintakukosea heshima hata siku moja.Wewe ni malkia wangu na ninakupa heshima zote" akajibu Brandon.
" Kwa nini umeniharibia wakati wangu mzuri na Innocent? akauliza tena Latoya kwa ukali.Brandon akakaa kimya
" Brandon kwa sasa nina machungu ya kufiwa na mama yangu .Ni Innocent pekee ambaye amekuwa mfariji wangu katika wakati huu mgumu.Kwa nini ukaharibu wakati wangu mzuri na Innocent? akauliza tena latoya.
" Nilifanya vile kwa sababu haikuwa sahihi kwako kuwa karibu namna ile na Innocent ." akajibu Brandon.
" Wewe ni nani hadi unipangie mtu wa kuwa naye karibu?Na kwa nini unafuatilia kila ninachokifanya? akafoka Latoya.
" Innocent si mtu ambaye unapaswa kuwa naye karibu Latoya na hilo unalifahamu fika.Nilifanya vile kwa ajili ya kukulinda wewe mwenyewe kwa sababu nilikuona tayari ulikuwa umeanza kuwa na hisia za kimahaba ndiyo maana nikaona nikustue ili usije ukaenda mbali zaidi kwani kulikuwa na kila dalili za kwenda mbali zaidi kwa namna kila mmoja alivyokuwa akionyesha hisia kwa mwenzake" akasema Brandon
" Ulifanya kosa kubwa sana Brandon.Naomba unisikilize vizuri.Innocent ni mtu wangu wa karibu na ni mwanaume ambaye nimekuwa nikimuota kwa miaka mingi.Ni mtu pekee ambaye niliweka ahadi ya kumtafuta na kumpata kabla sijafa.Kwa sasa nimekwisha mpata na hakuna mtu yeyote yule ambaye anaweza akanizuia kuwa naye.Nimekwisha kuonya kwa mara ya kwanza kwamba usiyafuatilie maisha yangu na hujataka kunisikia.Mimi ni mtu mwema mno lakini huwa ni mbaya sana pale mtu mmoja anapokwenda kinyume na matakwa yangu. Ninakuonya kwa mara ya pili na ya mwisho kwamba usijaribu hata siku moja kutaka kuufahamu upande wangu wa pili.Si mzuri hata kidogo.Ninaomba hapo ulipofika pawe ndiyo mpaka wako.Usijaribu kuvuka zaidi ya hapo .Narudia tena Brandon usijaribu kutaka kuufahamu upande wangu wa pili." akasema Latoya kisha akageuka na kuanza kuondoka.Alipokishika kitasa cha mlango akageuka na kumuangalia Brandon aliyekuwa ameduwaa akimtazama Latoya.
" By the way kesho asubuhi ndege iko tayari nataka uondoke asubuhi na mapema.Ahsante sana kwa kuja kunipa pole kwa msiba wa mama yangu." akasema Latoya ambaye alikuwa amekasirika kupita kiasi
" Latoya ! kwa nini niondoke mapema namna hii? Bado nahitaji kuendelea kukaa hapa.I need to spend some more time with you.Aren't you happy that I'm here with you? akauliza Brandon.
" Brandon nimekwisha sema kwamba kesho unaondoka na sitaki kukuona tena hapa kwangu.Kauli yangu mimi ni ya mwisho na huwa sirudii maneno mara mbili.Nataka kesho saa nne asubuhi uwe umeondoka hapa Tanzania." akasema Latoya huku akimtazama Brandon kwa macho makali.
"so it's because of him ? its because of Innocent..right?
" Shut up Brandon.." akafoka Latoya
" Latoya naomba nikwambie kwamba sintakubali hata kidogo kuhusu wewe kuwa na Innocent .Utanisamehe Latoya kwa hili sintakubali hata uniambie nini." akasema Brandon
" Brandon nimekwisha kuambia kwamba sintarudia kukuonya kwa mara nyingine tena kuhusiana na suala lako la kufuatilia maisha yangu.Stay away from me.Stay away from my life..."
" Latoya sintafanya hivyo unavyonitaka kama bado una nia ya kuwa na Innocent..I'll stay away from you if Innocent is far from here and out of your life.Nitahakikisha kwa kila namna ninavyoweza kwamba unakuwa mbali naye.Its my time now " akasema Brandon.Latoya akavuta pumzi ndefu halafu akamsogelea karibu na kumuangalia kwa makini usoni kisha akamwambia kwa sauti ndogo.
" Hakuna mtu ambaye amewahi kuuona upande wangu wa pili ukoje.You'll be the first to know the second side of me...one more thing,dont you ever try to put your finger on Innocent..." akasema Latoya huku akimtazama Brandon machoni kisha akaondoka.
Brandon akaingiwa na woga mwingi.Hakuwahi kumuona Latoya akiwa amekasirika namna ile.
"Mhh ! Latoya amekasirika mno.Yote haya ni kwa sababu ya Innocent.Mimi na Latoya tumefikia hapa kwa sababu ya Innocent.Sijui huyu kijana amempa nini Latoya kiasi cha kumfanya awe namna hii.Namfahamu Latoya ni mtu hatari sana na sitaki kuufahamu upande wake wa pili kwani si mzuri lakini pamoja na hayo nitahakikisha kwamba malengo yake hayatimii.Sintakubali hata kidogo kumuona Latoya akiwa na Innocent. Ili kulitimiza hilo nitaanza kwanza kupambana na Innocent.Nitafanya kila niwezalo ili kumuondoa Innocent katika maisha ya Latoya." Akawaza Brandon .Akainuka na kusimama.Uso wake ulionekana kujaa hasira nyingi.
" Get ready Innocent .You must leave Latoya Alone " akasema Brandon kisha akatoka mle chumbani na kuelekea ufukweni mwa bahari.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 43
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Hakuna mtu ambaye amewahi kuuona upande wangu wa pili ukoje.You'll be the first to know the second side of me...one more thing,dont you ever try to put your finger on Innocent..." akasema Latoya huku akimtazama Brandon machoni kisha akaondoka.
Brandon akaingiwa na woga mwingi.Hakuwahi kumuona Latoya akiwa amekasirika namna ile.
"Mhh ! Latoya amekasirika mno.Yote haya ni kwa sababu ya Innocent.Mimi na Latoya tumefikia hapa kwa sababu ya Innocent.Sijui huyu kijana amempa nini Latoya kiasi cha kumfanya awe namna hii.Namfahamu Latoya ni mtu hatari sana na sitaki kuufahamu upande wake wa pili kwani si mzuri lakini pamoja na hayo nitahakikisha kwamba malengo yake hayatimii.Sintakubali hata kidogo kumuona Latoya akiwa na Innocent. Ili kulitimiza hilo nitaanza kwanza kupambana na Innocent.Nitafanya kila niwezalo ili kumuondoa Innocent katika maisha ya Latoya." Akawaza Brandon .Akainuka na kusimama.Uso wake ulionekana kujaa hasira nyingi.
" Get ready Innocent .You must leave Latoya Alone " akasema Brandon kisha akatoka mle chumbani na kuelekea ufukweni mwa bahari.

ENDELEA………………………..

Baada ya kuachana na brandon Latoya akapanda ghorofani huku uso wake ukiwa na hasira nyingi.
" Brandon atanilazimisha nifanye mambo ambayo sikutarajia kuyafanya kabisa katika maisha yangu.Inaonekana hapendi ukaribu wangu na Innocent na kuna hatari anaweza akamdhuru Innocent.Iwapo akithubutu kufanya hivyo basi itanilazimu kufanya yale ambayo sikutarajia kuyafanya.Ninaomba yasifike huko anakotaka yafike." akawaza Latoya huku akielekea ghorofani kwake.
" Bado nina hamu ya kutaka kukaa karibu na Innocent.Brandon aliuharibu sana wakati wangu mzuri.Sijawahi kupata wakati mzuri kama ule ambao ninaamini kwamba ulikuwa ni mwanzo mzuri wa kuelekea kule ninakotaka yaani kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Innocent. Kuna kitu nilikiona katika macho ya Innocent.I saw love feelings." akawaza Latoya halafu akasimama kwa sekunde kadhaa akatabasamu.
" Mkono wake uligusa titi langu la kushoto,nilihisi msisimko wa ajabu ambao sijawahi kuupata katika maisha haya.Ouh Gosh ! why I have to die this young? akawaza Latoya.
" Ngoja nimfuate Innocent chumbani kwake nikajaribu kukaa naye japo niisikie tena sauti yake.Sina hakika kama nitaweza kupata usingizi usiku wa leo kama sintaisikia sauti yake tena ." akawaza Latoya huku akielekea katika chumba cha Innocent.Akasimama pale mlangoni akataka kubonyeza kengele ya mlangoni lakini akasita
" Inawezekana pengine amelala.Lakini nitafanyaje wakati ninahitaji nimshike walau mkono wake? Latoya akasimama pale nje ya mlango wa innocent kwa takribani dakika tano akiwaza mwishowe akakata shauri asimsumbue Innocent.Akaelekea chumbani kwake.Alipofika chumbani moja kwa moja akavua nguo na kuingia bafuni akaoga.Alipomaliza akaelekea katika meza yake ya vipodozi iliyokuwa na vipodozi vingi.Akiwa mtupu akajiangalia katika kioo akatabasamu.
" Mungu kanijaalia uzuri wa pekee kabisa.Wanaume wengi wananitamani lakini moyo wangu umempenda mmoja tu.Sina hakika nini kitatokea siku Innocent akiutazama mwili huu mzuri nikiwa namna hii yaani mtupu kabisa.Zaidi ya Daktari wangu hakuna tena mwanaume mwingine ambaye amewahi kuushuhudia mwili wangu huu mzuri.Innocent atakuwa wa kwanza." akawaza Latoya huku akitabasamu wakati akijiangalia katika kioo.Mara akageuka ili aweze kujitazama kwa nyuma.Akastuka sana na kunyong'onyea ghafla.Akazama katika mawazo mengi.Akiwa bado amesimama pale mbele ya kioo akasikia kwa mbali sauti kama ya mvumo wa kitu..
" What's that ? akajiuliza .Akabaki amesimama ameduwaa.
" Ouh My Gosh..its here again..I'm going down again.." akawaza Latoya huku machozi yakimtoka na mwili kumtetemeka.Mara akaanza kuhisi kitu kama moto mkali ukimuunguza mgongoni
" Aaaaggghhhhhhhhhh !!!!!.....Innocent help meeeee !!!!!!!!!!!!!!!!!!......." akapiga ukelele mkubwa akaanguka chini na kupoteza fahamu kutokana na maumivu makali sana aliyokuwa akiyasikia
Innocent ambaye alikuwa ameanza kupitiwa na usingizi kutokana na uchovu mwingi akakurupuka toka usingizini baada ya kusikia sauti kama ya Latoya akilia akimuita akiomba msaada.Mwili wake ulikuwa unatokwa na jasho jingi.
" Nimeisikia sauti kama ya Latoya akilia na kuomba msaada.Inawezekana ikawa ni ndoto? akajiuliza Innocent huku jasho likiendelea kumtiririka.
" Hapana hii si ndoto hata kidogo.Nimeisikia sauti ya Latoya akiomba msaada..Something is going on.." akasema Innocent huku akiinuka pale kitandani na kuiendea simu iliyokuwapo mezani akapiga chumbani kwa Latoya lakini haikupokelewa.
“Something is wrong.Nakumbuka mara ya mwisho aliniambia kwamba anakwenda kushughulikia jambo fulani na wakati tukiwa kule chumbani nilimsikia akilitaja jina la Brandon.Kuna kitu kinachoendelea kuhusiana na huyu mtu na Latoya.I must find this guy.I'm not scared of him.Kwa ajili ya Latoya nitapambana na mtu yeyote yule." akasema Innocent huku akiufungua mlango wake na kuanza kushuka ngazi kwa kasi akielekea chini.
Innocent akashuka kwa kasi kuelekea chini.Bado jasho liliendelea kumtoka kutokana na ndoto aliyoiota
" Ile haikuwa ndoto ya kawaida.It was so real.Lazima Latoya atakuwa katika matatizo.Anahitaji msaada na ninatakiwa kumsaidia." akawaza Innocent.
" Nakumbuka katika ile ndoto ya wakati ule niliyowahi kuota niliambiwa kwamba ni lazima nimlinde Latoya dhidi ya watu wanaotaka kumdhuru.Sikujua ni watu gani ambao wana lengo la kumdhuru lakini sasa nimeanza kupata picha kwamba Brandon atakuwa ni mmoja wao.Nina uhakika huo kwa sababu kila Latoya akionana naye lazima aonyeshe mstuko fulani na kubadilika kabisa. Kuna kitu kinachoendelea baina yao.Ninahisi pengine Brandon na Latoya wamewahi kuwa wapenzi lakini wakatengana .Kama hivyo ndivyo basi hatakiwi kabisa kuendelea kumsumbua Latoya.Kwa sasa Latoya anahitaji faraja na kutuliza akili yake baada ya mambo mengi kutokea mfululizo ndani ya kipindi kifupi sana.Sintakubali kuona mtu yeyote akimtoa machozi Latoya." akawaza Innocent huku akishuka ngazi na mara katika sebule kubwa akakutana na Irene.
" Innocent mbona unaonekana una haraka namna hiyo? Kuna nini? ..akauliza Irene
" Irene umemuona wapi Brandon? akauliza Innocent.Irene akaonyesha mshangao
" Brandon !!
" Ndiyo Brandon.Umemuona wapi?
" Simfahamu huyo Bramdon" akajibu Irene
" Kuna kijana mmoja amekuja msibani ni kijana mzungu amenyoa upara na sikioni amevaa hereni .Alikuwa amevaa suti nyeusi na kuna muda alikuwa humu ndani na Latoya" akasema Innocent
" Ouh nimeshamkumbuka .Kumbe unamuongela yule kijana wa kizungu.Sikujua kama ndiye Brandon." akasema Irene.
" Unaweza ukafahamu ana mahusiano gani na Latoya? akauliza Innocent
" Sifahamu ana mahusiano gani kwa sababu sijawahi kumuona yule kijana humu ndani.Leo hii ni mara yangu ya kwanza nimemuona katika miaka hii yote niliyofanya kazi kwa Latoya." akasema Irene
" kwani vipi Innocet? Nini kimetokea? akauliza Irene.
" Hakuna chochote Irene.Nahitaji tu kufahamu yuko wapi" akasema Innocent
" Kuna wakati nilimuona akipita pale bustanini alikuwa akielekea ufukweni." akasema Irene
" Ahsante Irene" akasema Innocent na kuchomoka kuelekea ufukweni.Irene akabaki anashangaa
" Irene ni mtu ambaye amefanya kazi kwa Latoya kwa miaka mingi na anasema kwamba hajawahi kumuona Brandon pale nyumbani.Inawezekana Latoya na Brandon wakawa na mahusiano fulani lakini ya siri.Leo nataka kuufahamu ukweli." akawaza Innocent akielekea ufukweni.Sauti za mawimbi ya bahari ndizo zilikuwa zinasikika .Bustanini walikuwepo wageni wachache waliokuja msibani wakiendelea kupata vinywaji.Taa kubwa zilikuwa zinamulika eneo lote la ufukweni na kupafanya paonekane kama mchana.Innocent akamuona Brandon akiwa amekaa juu ya gogo la mnazi akivuta sigara.Akasimama akamtazama na kuvuta pumzu ndefu
" I'm not scared of him...lazima niufahamu ukweli.Mbona yuko peke yake? Latoya yuko wapi? akawaza Innocent huku akitembea taratibu kumkaribia Brandon ambaye alikuwa ametulia akivuta sigara yake huku akiyaangalia mawimbi ya bahari .Taratibu akageuza shingo yake baada ya kuhisi kama kuna mtu anakuja nyuma yake.Mara akakutanisha macho yake na Innocent.Akastuka na kuitupa chini sigara yake.
" innocent ..umenifuata huku..Una shida na mimi? akauliza Brandon.Innocent akazidi kumsogelea karibu zaidi.
" Innocent mbona huongei ? Nakuuliza una shida na mimi au umekuja kupunga upepo ? akauliza tena Brandon.Innocent akamtazama kwa macho makali halafu akavuta pumzi ndefu na kusema
" Latoya yuko wapi? akauliza Innocent huku amemkazia macho Brandon.Brandon akatabasamu na kusema
" Unapaswa kuniuliza mimi kuhusu wapi alipo Latoya au walinzi wake ? Hufahamu kwamba Latoya huongozana na walinzi wake kila sehemu anayokwenda? Kawaulize walinzi wake pengine wanajua mahala alipo bosi wao..." akasema Brandon
"Brandon I'm serious..niambie Latoya yuko wapi? akauliza tena Innocent
" Innocent I'm serious too..nenda kawaulize walinzi wake..Halafu unamuulizia Latoya namna hiyo wewe ni kama nani wake? Inocent wewe ni rafiki tu wa Latoya na ni mgeni hapa kwa hiyo lazima ufahamu nafasi yako.Fahamu mipaka yako.Hupaswi kuwa mtawala katika nyumba hii na kumuulizia Latoya kwa namna unavyotaka.Latoya si mtu wa kuuliziwa namna hiyo kama unauliza bei ya nazi sokoni.Lazima ujifunze kuwa na adabu kwa bosi wako" akasema Brandon maneno ambayo yalimuumiza Innocent.
" Huyu jamaa mbona anazungumza kwa kujiamini hivi? Pamoja na hayo siwezi kumuogopa hata kidogo." akawaza Innocent.
" Latoya ni rafiki yangu na amenipa uhuru wa kufanya lolote katika nyumba yake.Kwa hiyo naomba unieleze wapi alipo? akasema Innocent
" Innocent kama huna kitu cha maana cha kuniambia itakuwa vyema kama ukiondoka na kuniacha hapa peke yangu." akasema Brandon
" Brandon ninataka unieleze haraka Latoya yuko wapi? Umemfanya nini? akauliza Innocent
" Innocent are you crazy? Toka lini nimekuwa mlinzi wa Latoya ? wewe ndiye uliyegeuka mlinzi wake mkuu na tunapaswa kukuuliza wewe Latoya yuko wapi? akauliza Brandon.
" Sikiliza Brandon usiku huu nilikuwa nimekaa chumbani na Latoya tulikuwa tukiongea na mara akastuka na kukutaja kisha akashuka na kusema anakufuata.Niambie Latoya yuko wapi na kwa nini uliingilia maongezi yetu? Who are you ? akauliza Innocent.Brandon akatabasamu kama kawaida yake na kusema
"Nilijua tu lazima ungenitafuta.Nimefurahi sana kukutana nawe usiku huu tukiwa peke yetu.Kwanza kabisa naomba usiwe na haraka ya kutaka kunifahamu.Kama ukitaka kunifahamu utanifahamu tu lakini si sasa hivi.Ninachotaka kukwambia kwa sasa ni kitu kidogo tu kwamba Stay far away from Latoya..." akasema Brandon.
" Wewe ni nani wa kuniamuru nikae mbali na Latoya ?.Nataka kujua pia ni kwa nini ukaingilia maongezi yangu na Latoya kule chumbani na kumfanya Latoya ashuke kukufuata ? akauliza Innocent.Brandon akakunja sura yake
" Innocent ulichotaka kukifanya ni kosa kubwa sana na hujui umemsababishia matatizo gani Latoya." akasema Brandon.
" Brandon ninakuonya kwamba kama kuna jambo lolote lile umelisababisha kwa Latoya ninaapa nitakufanyia kitu kibaya sana." akasema Innocent.Brandon akatabasamu na kusema
" Hujui unalolisema Innocent .Bado naendelea kukuonya kwamba kaa mbali na Latoya na wala usifikiri lengo lako kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Latoya litafanikiwa.That wont happen ever.I'll never allow that." akasema Brandon.
" wewe ni nani Brandon wa kuweza kunizuia kuwa karibu na latoya? Hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kunizuia kuwa karibu na Latoya.Si wewe wala mtu yeyote yule anayeweza kunizuia.Latoya ni mtu wangu wa karibu na nitakuwa karibu naye siku zote na hakuna atakayenizuia." akasema Innocent kwa kujiamini.
" Why do you care about Latoya so much? Just because she's rich ?...akauliza Brandon.
" Because I love her " akasema Innocent bila kuogopa.Sura ya Brandon ikabadilika.
" You do love her ? Do you know who Latoya is? akauliza Brandon kwa ukali.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………..


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 44
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Innocent ulichotaka kukifanya ni kosa kubwa sana na hujui umemsababishia matatizo gani Latoya." akasema Brandon.
" Brandon ninakuonya kwamba kama kuna jambo lolote lile umelisababisha kwa Latoya ninaapa nitakufanyia kitu kibaya sana." akasema Innocent.Brandon akatabasamu na kusema
" Hujui unalolisema Innocent .Bado naendelea kukuonya kwamba kaa mbali na Latoya na wala usifikiri lengo lako kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Latoya litafanikiwa.That wont happen ever.I'll never allow that." akasema Brandon.
" wewe ni nani Brandon wa kuweza kunizuia kuwa karibu na latoya? Hakuna mtu au kitu chochote kinachoweza kunizuia kuwa karibu na Latoya.Si wewe wala mtu yeyote yule anayeweza kunizuia.Latoya ni mtu wangu wa karibu na nitakuwa karibu naye siku zote na hakuna atakayenizuia." akasema Innocent kwa kujiamini.
" Why do you care about Latoya so much? Just because she's rich ?...akauliza Brandon.
" Because I love her " akasema Innocent bila kuogopa.Sura ya Brandon ikabadilika.
" You do love her ? Do you know who Latoya is? akauliza Brandon kwa ukali.


ENDELEA……………………..

" Sijali kujua Latoya ni nani na anafanya nini.Kitu ninachokifahamu ni kwamba ninampenda na yeye ananipenda" akasema Innocent.Brandon akavuta pumzi ndefu na kumuangalia Innocent kwa macho ya chuki.
" Name your price Innocent and I'll pay you so that you can leave Latoya alone I know you are here because of her money" akasema Brandon.
" Kwa nini hutaki kuniona nikiwa karibu na Latoya ? akauliza Innocent
" Because that'll never happen" akasema Brandon.
"Latoya hawezi kuwa na mpenzi kama wewe." akasema tena Brandon
" Wewe ni nani Brandon na unataka nini kwa Latoya? akauliza Innocent
" Usitake kunifahamu Innocent. Utajuta ni kwa nini umenifahamu.Sipendi unifahamu lakini ukitaka kunijua mimi ni nani endelea kuwa karibu na Latoya. " akasema Brandon
" Brandon huna uwezo wa kunifanya kitu chochote na sikuogopi.Kwa sababu ya Latoya nitapambana na mtu yeyote yule anayetaka kumdhuru Latoya na kwa kuanzia nitaanza kupambana na wewe.Niambie haraka Latoya yuko wapi i? She's in pain and she needs my help" akasema Innocent huku akimsogelea Brandon.
" Innocent nakuomba tafadhali usijaribu kutaka kunifahamu.Go away.Leave Latoya alone.Kama ukihitaji kuishi kwa amani ondoka na umuache Latoya peke yake.."
" Brandon kwanini usisitize kwamba niachane na latoya na kuondoka? Huna mamlaka ya kuniamuru niondoke hapa kwa Latoya.Mwenye mamlaka hayo ni Latoya pekee ambaye hataki niondoke .She's happy with me and she needs me by her side.Look at you stupid..you are just nothing..Unaona wivu kwa sababu huna nafasi yoyote kwa Latoya.Kwake unaonekana kama taka taka .Nakuhakikishia kwamba Latoya atakuwa wangu kwa sababu ninampenda na yeye ananipenda.Huna uwezo wa kunizuia.Above all I'll never leave this place..you know why? Because its my destiny.I belong to this place " akasema Innocent na hasira za wazi zikajidhihirisha katika sura ya Brandon.Akamsogelea karibu.
" Kwa kuwa umeonyesha dharau naapa kupambana na wewe.Its just me and you now.Utapata nafasi ya kunifahamu vizuri mimi ni nani." akasema Brandon.
" Huna lolote la kunitisha Brandon na huwezi kunifanya jambo lolote lile.Na mimi ninakuapia kwamba kama umemfanya kitu chochote Latoya utanifahamu vizuri.Nitakufanyia kitu kibaya sana .." akasema Innocent.Walikuwa wamekarikbiana kiasi cha kukutanisha vifua vyao.
" What will you do to me ? akauliza Brandon.
" and you what will you do to me? Innocent naye akauliza
" I'll make your life a living hell" akasema Brandon.
" You'll be the first to go to hell" akasema innocent huku akigeuka na kuondoka.Brandon alibaki amefura kwa hasira huku akihema kwa nguvu .
" aaaaagghhhhh !!!.....akapiga ngumi gogo la mnazi kwa hasira
" stupid guy..amethubutu vipi kuongea na mimi namna ile? Innocent bado kijana mdogo sana wa kuweza kuongea na kutishana na mimi namna ile.Lazima nimfundishe adabu.Ninaapa lazima nimuondoe katika maisha ya Latoya kwa sababu inaonekana amedhamiria kabisa kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Latoya.Ninasema kwamba hilo halitawezekana hata kidogo.I will get back to you Innocent..Get ready to know me.." akasema Brandon.
Irene ambaye alikuwa sebuleni alistuka baada ya kuiona sura ya Innocent ikiwa na mabadiliko makubwa usoni .
" Innocent kumetokea nini mbona umebadiika namna hiyo? Nani kakuudhi namna hiyo? akauliza Irene.
" hakuna kitu Irene.Unaweza ukafahamu Latoya yuko wapi? akauliza Innocent
" Latoya alielekea chumbani kwake." akasema Irene
" Nilijaribu kumpigia simu chumbani kwake lakini haijapokelewa ndiyo maana nikashuka huku chini kumuangalia ." akasema Innocent
" Latoya yuko chumbani kwake na inawezekana akawa amepitiwa na usingizi kutokana na shughuli za kutwa nzima ya leo" akasema Irene.Innocent akarejea chumbani kwake.
" Brandon tayari ameniharibia siku yangu.lakini huyu kijana ni nani kwa Latoya kiasi cha kunitisha kwamba nikae mbali na latoya? Ninaanza kukubaliana na mawazo yangu kwamba wawili hawa lazima wana mahusiano fulani.Kuna wakati aliniambia kwamba kuwepo kwangu karibu na latoya kunamsababishia matatizo makubwa.Ni matatizo gani hayo ambayo Latoya anayapata nikiwa karibu naye? Kuna mambo mengi ambayo ninahitaji kuyafahamu bado na mwenye kuweza kunipa majibu ya maswali yangu ni Latoya pekee. Nini kimempata Latoya? Lazima kuna jambo ambalo limempata kwa sababu nimeisikia sauti yake ikiniita kutaka msaada.Laiti kama ningekuwa na uwezo wa kufika chumbani kwake na kufahamu ni kitu gani kimepata ningeweza kumsaidia lakini uwezo huo sina.Masikini Latoya yuko katika wakati mgumu sana.Huu ni wakati anaohitaji faraja na msaada mkubwa sana na mtu pekee wa kumsaidia ni mimi.Nitamlinda na kila baya.Nitapambana na yeyote yule ambaye anataka kumdhuru Latoya.Mtu wa kwanza kupambana naye atakuwa ni Brandon.Nataka akae mbali na Latoya." akawaza Innocent akiwa kitandani.
" Moyo unaniuma sifahamu Latoya amepatwa na jambo gani.." innocent akasimama na kuzunguka zunguka mle chumbani.
" You love her? Do you know who Latoya is? Akayakumbuka tena maneno ya Brandon
" Alikuwa na maana gani kusema maneno haya? Latoya ni nani? Ina maana Latoya si binadamu ambaye hapawi kupendwa? ..akajiuliza Innocent halafu akaendelea kukumbuka tena baadhi ya maneno ya Brandon.
" Usitake kunifahamu Innocent. Utajuta ni kwa nini umenifahamu.Sipendi unifahamu lakini ukitaka kunijua mimi ni nani endelea kuwa karibu na Latoya"
" Brandon ni nani na kwa nini ananiogopesha kwamba nisitake kumfahamu? na kwamba eti nikitaka kumfahamu niendelee kuwa karibu na Latoya? ..mambo haya yananiogopesha.Nimeingia katika ulimwengu ambao sikutegemea kama ningeufikia katika maisha yangu.Sikuwahi kuota kama maisha yangu yangefikia hapa siku moja.Nimekuwa nikikutana na mambo ya ajabu ajabu kila siku lakini kwa bahati mbaya nimejikuta nimekwama na siwezi tena kuondoka mahala hapa kwa sababu tayari nimeanza kumpenda Latoya na niko tayari kufanya lolote kwa ajili yake.I'm confused" akawaza Innocent
" Ninaanza kuhisi Latoya yuko katika wakati mgumu mno na ninatakiwa kumsaidia.I dont know how but I must help her " akawaza Innocent.








* * * *

Kengele ya simu ya chumbani ndiyo iliyomstua Innocent katika usingizi ambao aliupata mida ya alfajiri.Usiku mzima hakuweza kupata usingizi kwa mawazo mengi aliyokuwa nayo.Akafumbua macho na kutazama saa ya ukutani ilionyesha ni saa mbili za asubuhi.
" Ouh ! kumekucha " akasema Innocent huku akiinuka kitandani na kuiendea simu ya mezani ambayo bado iliendelea kuita.
" Hallo" akasema Innocent baada ya kuipokea simu
" Hallo Innocent..Irene hapa ninaongea" ikasema sauti ya upande wa pili
" Habari za asubuhi mama Irene.”
" Habari nzuri Innocent samahani kwa kukusumbua asubuhi namna hii lakini nimetumwa na yule kijana wa kizungu uliyekuwa ukimtafuta jana anasema kwamba anahitaji kukuona sasa hivi" akasema Irene.
" Kijana yupi . Brandon ? akauliza Innnocent
" Ndiye huyo huyo".
" Amesema anahitaji kuonana na mimi kwa madhumuni gani?
" Sifahamu Innocent lakini amesisitiza kwamba anahitaji kuonana na wewe sasa hivi" akasema Irene
Innocent akafikiri kwa sekunde kadhaa halafu akasema
" Ok Irene ninakuja. Latoya tayari amekwisha shuka huko chini? akauliza Inno
" Hapana Innocent bado sijamuona Latoya huku chini lakini amenipigia simu asubuhi hii na akaniambia nimtayarishie supu ya kuku" akasema Irene.
Innocent akavuta pumzi ndefu akakata simu.
" Thanx God Latoya is fine. Sikuweza kupata usingizi usiku kwa mawazo mengi juu yake.Nini kilimpata jana usiku ? Dah ! mambo haya yananichanganya sana " akawaza Innocent akiwa amekaa juu ya meza ile ndogo
"Brandon anataka nini toka kwangu asubuhi hii ? Kila nikilisikia jina lake ninapatwa na hasira sitaki awe karibu na Latoya.Simuogopi na nitapambana naye kwa kila namna nitakavyoweza " akawaza Innocent huku akivaa fulana na kutoka mle chumbani akashuka chini.Brandon alikuwa katika chumba kidogo ambacho Latoya hukitumia kwa ajili ya maongezi ya faragha na wageni wake wa muhimu.
" Karibu Innocent.Naona umestuka sana kusikia kwamba ninahitaji kukuona" akasema Brandon huku akitabasamu mara tu baada ya Innocent kuingia mle chumbani.Innocent akavuta pumzi ndefu akamtazama Brandon kwa macho makali na kusema
" Naomba uniambie ni kitu gani ulichoniitia hapa " akasema Innocent.Brandon ambaye alikuwa na kikombe cha kahawa mkononi akatabasamu na kusema
" Innocent sitaki kukupotezea muda wako mwingi lakini nimekuita hapa kwa ajili ya kukuambia mambo machache.Kwanza napenda kukutaarifu kwamba ninaondoka muda si mrefu toka sasa lakini bado tutaendelea kuonana mara nyingi tu . Pamoja na kuondoka nimeona nikukumbushe kuhusu jambo nililokwambia jana usiku kwamba kaa mbali na Latoya.Stay far away from her.Futa kabisa hisia za kimapenzi ulizonazo juu yake.Ninakiri kwamba Latoya anakupenda na anafanya kila analoweza ili aweze kuwa nawe lakini naomba nikuweke wazi kwamba hilo ni jambo lisilowezekana kama vile ardhi na mbingu zisivyoweza kukutana.Wewe na yeye mnajidanganya tu.Kwa hiyo nakuomba usiendelee kupoteza muda wako wa kuyapanga maisha yako kwa sababu ya Latoya.Hutaweza kuwa mpenzi wake hata ufanye nini.Badala yake utamzidishia matatizo makubwa sana zaidi ya haya aliyonayo kwa sasa.Ulimsikia jana usiku akilia akikuomba msaada? Basi hii ilitokana na kitendo anachotaka kukifanya cha kutaka kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na wewe.Kama kweli unampenda Latoya basi ondoka haraka na ukae naye mbali kabisa.Nimekwambia haya kwa nia nzuri ya kukusaidia wewe mwenyewe pamoja na Latoya.Ninarudia tena kukuonya kwamba hakikisha mapema iwezekanavyo unaondoka na kumuacha Latoya mwenyewe vinginevyo utaingia katika matatizo makubwa mno na mtu wa kwanza kupambana naye nitakuwa ni mimi.Kama utapuuza haya nikwambiayo jiandae kupambana na mimi na ninakwambia wazi ni bora ukakutana na mtoa roho kuliko kukutana na mimi" akaonya Brandon.Innocent alikuwa akimtazama kwa macho makali.Mara akatabasamu na kusema
" Sikiliza Brandon kama nilivyokueleza jana ninarudia tena kukueleza leo hii kwamba siwezi kuondoka hapa na mwenye mamlaka ya kunitoa hapa ni Latoya pekee.Hakuna binadamu anayeweza kunitenganisha na Latoya kamwe .Kwa taarifa yako ni kwamba hapa nimefika na siwezi kuondoka tena.This is where I belong.Ninampenda Latoya toka ndani kabisa ya moyo wangu na nitahakikisha kwamba mimi na yeye tunakuwa na mahusiano ya kimapenzi.I love her and I know she love me.We'll get married and she'll be my wife.Si wewe au mtu mwingine yeyote anayeweza kunizuia kutompenda Latoya.Nakuomba uondoke katika maisha ya Latoya na umuache aishi kwa amani.Unapoondoka hapa nakuomba usirejee tena na wala usimuwaze Latoya kwa sababu hata kama ukirudi hutamkuta .Tayari atakuwa katika maisha mengine kabisa.So dont ever think of coming back again.Kuhusu kupambana na wewe siogopi .Kwa ajili ya Latoya niko tayari kupambana na mtu yeyote yule.Nitamlinda Latoya dhidi ya mtu yeyote yule mwenye lengo baya naye na nitahakikisha Latoya anakuwa salama na anayafurahia maisha yake akiwa na mimi" akasema Innocent kwa kujiamini.Brandon akamtazama Innocent kwa hasira halafu akaweka mezani kikombe cha kahawa alichokuwa amekishika.
" Innocent narudia tena kukwambia kwamba usijidanganye etu utakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Latoya achilia mbali kumuoa.Unafahamu ni muda gani aliobaki nao Latoya kabla hajafa? akauliza Brandon kwa ukali.Innocent akastushwa sana na kauli ile .Akabaki kimya

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………….


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 45
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Sikiliza Brandon kama nilivyokueleza jana ninarudia tena kukueleza leo hii kwamba siwezi kuondoka hapa na mwenye mamlaka ya kunitoa hapa ni Latoya pekee.Hakuna binadamu anayeweza kunitenganisha na Latoya kamwe .Kwa taarifa yako ni kwamba hapa nimefika na siwezi kuondoka tena.This is where I belong.Ninampenda Latoya toka ndani kabisa ya moyo wangu na nitahakikisha kwamba mimi na yeye tunakuwa na mahusiano ya kimapenzi.I love her and I know she love me.We'll get married and she'll be my wife.Si wewe au mtu mwingine yeyote anayeweza kunizuia kutompenda Latoya.Nakuomba uondoke katika maisha ya Latoya na umuache aishi kwa amani.Unapoondoka hapa nakuomba usirejee tena na wala usimuwaze Latoya kwa sababu hata kama ukirudi hutamkuta .Tayari atakuwa katika maisha mengine kabisa.So dont ever think of coming back again.Kuhusu kupambana na wewe siogopi .Kwa ajili ya Latoya niko tayari kupambana na mtu yeyote yule.Nitamlinda Latoya dhidi ya mtu yeyote yule mwenye lengo baya naye na nitahakikisha Latoya anakuwa salama na anayafurahia maisha yake akiwa na mimi" akasema Innocent kwa kujiamini.Brandon akamtazama Innocent kwa hasira halafu akaweka mezani kikombe cha kahawa alichokuwa amekishika.
" Innocent narudia tena kukwambia kwamba usijidanganye etu utakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Latoya achilia mbali kumuoa.Unafahamu ni muda gani aliobaki nao Latoya kabla hajafa? akauliza Brandon kwa ukali.Innocent akastushwa sana na kauli ile .Akabaki kimya

ENDELEA……………………….

" You dont know..right? So please stay far away from her.Katika siku hizi chache alizobaki nazo tafadhali usiendelee kumuongezea mateso na maumivu kila kukicha kwa kujidanganya kwamba unaweza ukawa mpenzi wake. Muda wangu umekwisha na ninaondoka lakini yafanyie kazi hayo niliyokwambia.Stay far away from Latoya " akasema Brandon huku akiondoka mle chumbani akiwa na hasira .Innocent bado aliendelea kusimama akitafakari.
" Gosh ! haya maneno ameyaongea Brandon ni ya kweli? Ameniuliza kama ninafahamu muda aliobaki nao Latoya kabla hajafariki.Latoya is gong to die?
Innocent akahisi miguu yake ikiisha nguvu na kukaa kitini.
" Ukaribu wangu na Latoya unamsababishia matatizo gani? Ni nani anayempa Latoya mateso kwa sababu ya ukaribu wake na mimi ? Kwa nini Brandon anataka nikae mbali kabisa na Latoya? .." Kichwa cha Innocent kikazidi kuumia kwa mawazo.
" Mtu pekee anayeweza kunipa majibu ya mambo haya aliyoniambia Brandon ni Latoya lakini niitawezaje kumuuliza juu ya masuala haya yanayohusiana na maisha yake ya ndani ? .." akaendelea kujiuliza Inno
" Hapana siwezi kumuuliza Latoya kuhusiana na jambo hili.Hapendi kuulizwa jambo lolote linalohusiana na maisha yake.Hata hivyo nitaendelea kuwa rafiki yake na hakuna atakaye nizuia kufanya hivyo.Latoya ananihitaji na anahitaji sana msaada wangu.Siwezi kumuacha hata kwa sekunde moja.Nitakuwa karibu yake kila wakati.Nitapambana na yeyote yule ambaye ana lengo baya naye." akasema Innocent kwa sauti ndogo kisha akatoka mle chumbani na kuanza kuelekea chumbani kwake.Irene akamshangaa kwa namna alivyokuwa amebadilika..
" Kuna kitu gani kinachoendelea baina ya Innocent na yule kijana Brandon? Kila wanapokutana lazima sura ya Innocent ibadilike kabisa.Nini kinaendelea kati yao? Yule kijana ni nani kwa Latoya? akajiuliza Irene.
Innocent akaelekea chumbani kwake huku kichwa chake kikiwa kizito kwa mawazo mengi.
" Ni kweli Latoya anakaribia kufa?...akajiuliza swali hili wakati akiwa bafuni anaoga.Akasimama kwa muda akitafakari.
" Siamini kama ni kweli kwamba Latoya yuko karibu kufa kwa sababu mwenye kujua siku ya kufa kwa mtu ni Mungu peke yake.Hakuna mwanadamu anayefahamu siku yake ya kufa au hata ya mwenzake.Masuala ya kifo ni siri kubwa ya Mungu pekee.” Akawaza Innocent.
“ Lakini Brandon hakuonyesha kama ananitania aliposema kwamba Latoya hana maisha marefu.Sitakiwi kupuuzia maneno yale kwani inaonekana wazi kwamba Brandon anamfahamu vyema Latoya.Kama ni kweli Latoya amebakiwa na siku chache za kuishi kabla ya kufariki dunia basi inawezekana kabisa ikawa si kifo cha kawaida.Lazima kitakuwa ni kifo ambacho kinatokana na matakwa ya watu. Kama ni hivyo ni akina nani hao ambao wanataka kumuua? Amewakosea kitu gani? ..Kwa sasa ninaanza kupata picha kamili ya ile ndoto niliyoota nikitakiwa kumlinda Latoya. Kwa wakati ule sikuelewa ndoto ile ilikuwa na maana gani lakini sasa nimeanza kuielewa.Ni mimi pekee ambaye ninatakiwa kumlinda Latoya dhidi ya watu hawa ambao wamepanga kumuua." akawaza Innocent wakati akivaa nguo baada ya kumaliza kuoga.
" Kukutana kwangu na Latoya kulikuwa na sababu maalum. Nadhani mimi ndiye niliyechaguliwa niwe mtu wake wa karibu na nimlinde na kila baya analotaka kufanyiwa.Moyo wangu tayari umekwishampenda Latoya na nitafanya kila niwezalo ili niweze kuwa naye.Nitapambana kwa ajili yake.Nita..............................." Hakumaliza kuwaza alichokuwa akikiwaza mara kengele ya mlangoni ikalia kuashiria kwamba kuna mtu alikuwa mlangoni.Innocent akastuka .
" lazima atakuwa ni Latoya huyu,hakuna mtu mwingine ambaye anaweza akaja kunigongea mlango huku juu." akawaza halafu kwa haraka akauendea mlango akaufungua na kukutana na sura yenye tabasamu ya Latoya.Siku hii alikuwa amevaa gauni refu jeupe bila kusahau koti lake jeusi.Alikuwa amependeza vilivyo.Innocent alimtazama kana kwamba ni mara yake ya kwanza kumuona.Midomo ilikuwa inamcheza akashindwa aseme nini.
" Hallow Innocent umeamkaje? Habari za toka jana?...Latoya akauliza huku akitabasamu
" Nimeamka salama Latoya.Sijui wewe umeamka salama? Unajionaje hali ? akauliza Innocent
" Ninashukuru Innocent nimeamka salama kabisa.Hofu yangu ilikuwa kwako kama ulilala salama hasa kutokana na uchovu wa mwili uliokuwa nao kutokana na pilika pilika za siku mbili tatu zilizopita." akasema Latoya akiwa bado amesimama mlangoni.
" Niko salama Latoya wala hupaswi kuwa na hofu kuhusu mimi. Siku zote siwezi kuchoka ninapofanya kazi yoyote inayohusiana na wewe" akasema Innocent na kuifanya sura ya Latoya ichanue kwa tabasamu pana zaidi.
" Umeanza maneno yako Innocent" akasema Latoya huku akicheka.Innocent akatabasamu baada ya kuiona sura ya Latoya namna ilivyokuwa nzuri katika tabasamu lile .
" Ouh Gosh msichana mzuri kama huyu afariki dunia ! hapana haiwezekani.Lazima nipambane na wale wote wanaotaka kumuua" akawaza akiwa amemkazia macho Latoya.
" Innocent mbona leo unaniangalia namna hiyo? akauliza Latoya baada ya kugundua kwamba toka amesimama pale mlangoni Innocent alikuwa anamuangalia sana .Aligundua kitu katika macho ya Innocent
" Latoya leo umependeza sana " akasema Innocent huku akijilazimisha kutabasamu.Latoya akaanza kuwa na wasi wasi.
" Nashukuru sana" akasema Latoya
" Innocent nilipita hapa kukusalimu na kujua umeamkaje siku ya leo na vile vile kukutaka tukapate kifungua kinywa pamoja "
" Nashukuru sana Latoya.Tunaweza kwenda" akasema Innocent kisha wakaongozana kuelekea katika ukumbi wa chakula kwa ajili ya kupata kifungua kinywa.
" Innocent leo anaonekana yuko tofauti sana.Anaonekana kama ana mawazo mengi .Anawaza nini ? akajiuliza Latoya wakati wakishuka kuelekea ukumbi wa chakula.
" She's too young to die.Kama ni binadamu wamepanga kumuua Latoya basi sintawaruhusu wafanye hivyo lakini kama ni kwa mapenzi ya Mungu nitamlilia sana ampe maisha marefu binti huyu kwa sababu nimetokea kumpenda kupita ninavyoweza kueleza" akawaza Innocent akiwa nyuma ya Latoya wakielekea kupata kifungua kinywa.Tayari meza ilikwisha andaliwa na ilikuwa imesheheni vyakula vingi.
" Innocent asubuhi hii tutakwenda kulitembelea kaburi la mama baada ya hapo nataka kwenda kupunga upepo wa bahari ufukweni.Nataka kichwa changu kisahau kabisa kuhusu kifo cha mama na yote yaliyotokea..Innocent najua umenifanyia vitu vingi sana lakini bado kuna kitu kimoja ninataka kukuomba” akasema Latoya
" Latoya omba kitu chochote kile bila hofu na nitakupatia" akasema Innocent na kumfanya Latoya atabasamu
" Innocent Help me to forget everything that happened .Nisaidie kuufanya moyo wangu uwe na furaha hata kama ni kwa siku chache lakini ninataka nifurahi." akasema Latoya.Innocent akastuka kidogo.
" Latoya anamaanisha nini anaposema anahitaji kufurahi hata kama ni kwa siku chache? Ina maana maneno ya Brandon kwamba siku si nyingi aytakufa ni ya kweli? akajiuliza Innocent huku akimtazama Latoya usoni.
" Innocent unawaza nini ?
" Latoya nitakusaidia kusahau mambo yote magumu yaliyotokea ,nitakusaidia kufurahi si kwa siku chache tu bali katika siku zote za maisha yako." akasema Innocent
" Ouh Innocent hujui unachokingea.Ningefurahi sana kama ningekuwa na maisha marefu na kuendelea kufurahi pamoja nawe lakini siku zangu zimebaki chache sana.Inaniuma mno kukaa nawe kwa siku chache." akawaza Latoya na kushindwa kujizuia kudondosha chozi.
" Whats wrong Latoya? Why are you crying? akauliza Innocent
" It's nothing Innocent.Nimeshindwa kujizuia kutokwa na machozi ya furaha kwa kauli yako ya kukubali kunisaidia kusahau mambo haya magumu yaliyonitokea.Naomba nikiri kwamba katika maisha yangu sijawahi kukutana na kijana mwenye roho nzuri kama wewe Innocent ." akasema Latoya.
" Nashukuru sana Latoya" akasema Innocent halafu wakaendelea kupata kifungua kinywa kimya kimya
Walipomaliza kupata kifungua kinywa wakatoka mle ukumbini kisha wakasalimiana na watu kadhaa waliokuwepo pale nyumbani asubuhi ile pamoja na wa wafanyakazi na walinzi halafu moja kwa moja wakaelekea katika kaburi la mama yake Latoya.Bado chumba chote kilikuwa kimejazwa maua yaliyowekwa na waombolezaji.Latoya akawasha mshumaa mmoja halafu wakatoka.Wakati wakirejea ndani toka katika chumba chenye kaburi la mama yake Latoya wakakutana na Irene.
" Madam Latoya kuna wageni wamefika hapa nimewakaribisha ndani. Ni familia ya Innocent." akasema Irene.Innocent na Latoya wakatazamana.
" Usiogope Innocent nenda kawasalimu familia yako.Forget about what happened in the past.Ni wakati wa kujenga maisha mapya" akasema Latoya huku akitabasamu.
" Bado ninakumbuka mambo niliyofanyiwa wakati ule wa Marina." akasema Innocent
" Usikumbuke tafadhali.Nenda kawasalimu " akasema Latoya.
" Madam Latoya Innocent ana matatizo gani? akauliza Irene baada ya Innocent kuondoka akiwa ameinamisha kichwa chini.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………
 
BEFORE I DIE
SEHEMU YA 46
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Walipomaliza kupata kifungua kinywa wakatoka mle ukumbini kisha wakasalimiana na watu kadhaa waliokuwepo pale nyumbani asubuhi ile pamoja na wa wafanyakazi na walinzi halafu moja kwa moja wakaelekea katika kaburi la mama yake Latoya.Bado chumba chote kilikuwa kimejazwa maua yaliyowekwa na waombolezaji.Latoya akawasha mshumaa mmoja halafu wakatoka.Wakati wakirejea ndani toka katika chumba chenye kaburi la mama yake Latoya wakakutana na Irene.
" Madam Latoya kuna wageni wamefika hapa nimewakaribisha ndani. Ni familia ya Innocent." akasema Irene.Innocent na Latoya wakatazamana.
" Usiogope Innocent nenda kawasalimu familia yako.Forget about what happened in the past.Ni wakati wa kujenga maisha mapya" akasema Latoya huku akitabasamu.
" Bado ninakumbuka mambo niliyofanyiwa wakati ule wa Marina." akasema Innocent
" Usikumbuke tafadhali.Nenda kawasalimu " akasema Latoya.
" Madam Latoya Innocent ana matatizo gani? akauliza Irene baada ya Innocent kuondoka akiwa ameinamisha kichwa chini.

ENDELEA…………………………

" Hapana sifahamu ana matatizo gani .Nimejaribu kumuuliza kama ana tatizo lakini amesema hana tatizo lolote."
" ninahisi kuna kitu kinaendelea kati yake na yule kijana aliyeondoka asubuhi Brandon" akasema Irene na kumfanya Latoya astuke.
" Brandon ! .." akasema Latoya
" Ndiyo madam.Jana usiku Innocent alishuka chini na kuniuliza kama nimemuona Brandon.Nilimuelekeza mahala nilikohisi angeweza kumkuta.Sifahamu waliongea nini lakini Innocent alirudi akiwa amebadilika sana na uso wake ulikuwa na hasira nyingi." akasema Irene.
" Ouh My Gosh ! Innocent alionana na Brandon ?
" Ndiyo madam.Haikuishia hapo leo asubuhi kabla hajaondoka Brandon aliniomba nimuitie Innocent nikafanya hivyo .Baada ya maongezi ya muda mfupi Inno alitoka akiwa ni kama mtu aliyechanganyikiwa na nilimuona akipanda ngazi huku akiongea peke yake.Sifahamu kuna kitu gani ambacho walikiongea vijana hawa kwa sababu kila mmoja alitoka akiwa amekasirika mno ." akasema Irene.Latoya akavuta pumzi ndefu
" Nahisi kuna jambo Brandon alimueleza Innocent kuhusiana na maisha yangu kwani lengo lake ni kunitenganisha naye na aliapa kufanya hivyo.Ninaogopa ninaweza kumpoteza Innocent kama atakuwa ameyafahamu maisha yangu.Ndiyo maana leo nimeona kana Innocent hayuko kawaida nadhani ni kutokana na maneno aliyoambiwa na Brandon.Nitafanya nini kumtuliza kwa sababu nina hakika atakuwa ameambiwa kuhusiana na mambo ya kutisha juu yangu.Je nimweleze ukweli kuhusu maisha yangu?.
Latoya akazama katika tafakari
“No I wont tell him or anyone the truth about my life.Hii ni siri yangu ambayo nimeapa kufa nayo " akawaza Latoya.
" Lakini iwapo nitakuwa na mahusiano ya kimapenzi na Innocent sintaweza kumficha ukweli kuhusu maisha yangu kitu ambacho ni hatari kubwa kwake kwa sababu mtu yeyote atakayejua siri ya maisha yangu lazima afe.What am I going to do ? ..Latoya akaendelea kuwaza
" Madam Latoya kuna tatizo lolote ? akauliza Irene baada ya kumuona Latoya namna alivyochanganyikiwa.
" hakuna tatizo Irene.Fanya usafi katika chumba cha kaburi.Ninakwenda kuonana na familia ya Innocent." akasema Latoya na kuondoka.
" Baba Shikamoo" akasema Innocent huku akitabasamu na kumpa mkono baba yake baada ya kuingia sebuleni na kukutana naye akiwa na dada yake Sarah.Pamoja nao alikuwepo pia Grace.Innocent akatabasamu baada ya kuonana tena na Grace kwani toka alipoondoka baada ya kumalizika msiba wa Marina hawakuwahi kuonana tena.
" Ouh Innocent " akasema Sarah dada yake huku akiinuka na kumkumbatia kwa furaha kubwa.
" I'm so Happy to see you again Sarah" akasema Inno
" Karibuni sana .Nimefurahi mno kuwaona tena." akasema Innocent akiwa na tabasamu na usoni.
" Ahsante sana tumekaribia." akasema baba yake ambaye hakukaukiwa tabasamu
" Dah ! sijawahi kuona jumba kama hili katika maisha yangu.Its amazing." akasema mzee Benard .
" Kaka Innocent Sabrina yuko wapi? Toka ulipomalizika msiba wa Marina sijaonana naye tena na hata nikipiga simu yake haipatikani " akauliza Grace
" Sabrina alipata safari nje ya nchi na kwa taarifa niliyonayo ni kwamba atakuwepo huko kwa muda wa miezi zaidi ya sita.Kuna kazi anaifanya katika moja ya kampuni ya Latoya.Vipi maendeleo yako Grace?
" Ninamshukuru Mungu ninaendelea vizuri sana kwa sasa.Ninamalizia masomo yangu ya hoteli " akasema Grace.
" Nafurahi kusikia kwamba unakaribia kumaliza masomo yako.Utakapomaliza masomo yako unitaarifu mara moja ili niweze kukutafutia sehemu nzuri ya kufanya kazi" akasema Innocent
" Nitashukuru sana kaka Innocent ".
" Innocent hata mimi ninaomba unitafutie kazi nyingine nzuri ili niweze kuachana na kazi hii ya uandishi wa habari.Unaonekana ni mtu wa karibu na Latoya hivyo ukiniombea kazi katika moja ya makampuni yake hataweza kukataa" akasema Sarah
" Usijali Sarah nitalifanyia kazi suala lako." akajibu Innocent halafu kikapita kimya kifupi .Mzee Vincent Benard baba yake na Innocent akakohoa kidogo kisha akasema
" Innocent utatuwia radhi kwa ujio huu wa ghafla.Mahala kama hapa si mahala pa kuja kiholela holela kama tulivyokuja.Tunashukuru sana kwa kuja na Grace kwani ametusaidia kuweza kuingia humu ndani kirahisi kwa kuwa yeye tayari anafahamika." akasema mzee Benard
"Sikujua kama mngekuja leo .Ningetoa taarifa kwa walinzi ili wasiwasumbue pale katika geti la kuingilia.Eneo lote la kulizunguka jumba la Latoya lina ulinzi mkali sana na si rahisi kuingia mahala hapa bila ya ruhusa maalum" akasema Innocent
" Ilinilazimu kumpigia simu mama Irene na ndiye aliyetoa ruhusa turuhusiwe kupita " akasema Grace.
" karibuni sana" akasema tena Innocent
" Innocent tumekuja hapa kwanza kwa lengo la kutoa pole kwa rafiki yako Latoya.Tumesikia kuhusu msiba alioupata wa kufiwa na mama yake .Tumeguswa sana na tumeona kama familia tuje tutoe pole kwake na kwa familia yake kwa msiba huu mkubwa uliowapata.Licha ya utajiri alio nao Latoya alikuwa nasi kule hospitali siku ile uliyotakiwa kufanyiwa upasuaji wa kumtolea figo Marina.Alionyesha upendo wa ajabu kwa familia yetu na kwa maana hiyo basi tuna kila sababu ya kuungana naye katika wakati huu mgumu alionao.Vile vile tumekuja kukupa salamu zetu za pole kama familia kwa msiba wa Marina.Toka alipofariki Marina hatujaonana na hatukupata nafasi ya kukupa pole.Tunajua Marina alikuwa ni mtu muhimu sana kwako na aliondoka katika wakati ambao ulikuwa ukimuhitaji sana.Tunapenda kuchukua fursa hii kama familia kusema pole sana Innocent kwa msiba ule mkubwa uliokupata" akasema mzee Benard.Innocent
" Nashukuru sana " akasema Innocent kwa sauti ndogo.
" Jambo la pili lililotuleta hapa leo ni kukutaarifu kwamba tumekaa kama familia tumejitafakari na kugundua kwamba sisi kama wazazi ,kama familia tulikosea sana. Toka umerejea nchini mambo mengi yametokea.Kumekuwa na mikwaruzano ya mara kwa mara baina yetu na iliyopelekea ukaondoka nyumbani. Kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba ya familia yangu ninapenda kuchukua nafasi hii kukuomba samahani kwa yote yaliyotokea.Tumekosa,tumekukosea sana na tunaomba utusamehe.Tusahau yote yaliyopita na tuanze upya.Tumejitafakari na kugundua kwamba siku zote ulikuwa sahihi kuhusu mfumo mzima wa maisha yetu kama familia.Ni kweli tulikuwa tukiishi vibaya na mabinti zetu wawili Grace na Sabrina ambao walikuwa wakitusaida kazi za pale nyumbani.Napenda nikiri kwamba hatukuwatendea vizuri.Mimi na familia yangu hatukuliona hilo na ndicho hasa kilichosababisha ugomvi uliopeklekea wewe kuondoka pale nyumbani.Napenda kukiri kwamba umetufundisha jambo kubwa sana na ninapenda kwa mara nyingine tena kukuomba msamaha kwa niaba ya familia yangu katika mambo yote tuliyokufanyia yaliyotokana na mfumo wa maisha yetu.Tumegundua kosa letu na tumejirekebisha.Tumeanza maisha mapya ya upendo.Kwa hivi sasa kila siku ya jumamosi tutakuwa tukitoa misaada ya chakula na mavazi kwa wale wasiojiweza hata kama ni kwa uchache.haya ndiyo yatakuwa maisha yetu mapya.Ni kwa sababu hiyo ndiyo maana unatuona leo hii tumeongozana na Grace kitu ambacho hakikuwa cha kawaida hapo kabla. Innocent familia yetu imenituma nikwambie hayo na kubwa zaidi kukwambia kwamba bado tunakupenda na kukuhitaji na tunakuomba urejee nyumbani na kuendelea kuishi nasi kama utakuwa tayari" akasema mzee Benard.Innocent alikuwa kimya akimsikiliza baba yake.Kwa mbali macho yake yalionyesha kulengwa na machozi.Grace alikuwa ameinama ameyafunika macho kwa mkono wake alikuwa akilia.Hakuamini kama siku moja ingetokea familia ile ingemchukulia kama mtoto wao.Kimya kifupi kikapita halafu Innocent akasema
" Baba nimekosa neno la kusema .Nimepatwa na furaha isiyoelezeka.Nimefurahishwa mno na kitendo cha familia yangu na hasa wewe kama baba yangu kukiri kwamba kulikuwa na makosa katika mfumo wa maisha ya familia yetu.Baba sina cha kusema zaidi ya kumshukuru Mungu kwa kutusaidia familia yetu imebadilika na kuanza kuishi maisha mapya ya amani na upendo. IIe ndoto yangu ya muda mrefu hatimaye imetimia .Ahsante sana Mungu " akasema Innocent halafu akainuka na kwenda kumkumbatia baba yake kwa furaha.Sarah akainuka na kumshika mkono Grace na kwa pamoja wakaungana na akina Innocent.Ulikuwa ni wakati wa furaha kubwa kwa familia hii kusameheana na kuungana tena.Wakiwa bado wamekumbatiana kama familia mara akatoka Latoya aliyeingia pale sebuleni kwa kasi na kusimama ghafla akatabasamu.
" Wow ! what a wonderful moment." akawaza Latoya
" I love you my family..I love you all very much" akasema Innocent na mara akageuka na kumkuta Latoya amesimama akiwatazama huku akitabasamu.
"Samahani kama sijaingia kwa wakati muafaka " akasema Latoya
" Usijali Latoya,karibu sana kutana na familia yangu.Baba yangu mzee Vincent Benard ambaye nadhani mlikwisha kuonana wakati wa msiba wa Marina,dada yangu Sarah na dada yangu Grace ambaye si mgeni kwako." akaanza utambulisho Innocent Kwa adabu Latoya akasalimiana nao wote kisha akaenda kuketi katika kiti chake” .
“Baba,Sarah na Grace,huyu ndiye Latoya rafiki yangu mkubwa.Nadhani mmekwisha kutana lakini si katika mazingira tulivu na rasmi kama haya." akasema Innocent
" Latoya ,familia yangu ikiongozwa na baba wamekuja kutoa salamu za pole kwa msiba mkubwa uliokupata .Hata wao kama familia wameguswa mno na msiba huu na wako hapa kukupa mkono wa pole .Nadhani baba ana jambo la kusema" akasema Innocent,Mzee Benard akakohoa kidogo kisha akasema
" Latoya sisi kama familia ya Innocent tumekuja hapa ingawa bila taarifa maalum kukupa pole nyingi kwa msiba mzito uliokupata.Tumesikitishwa sana na kuondoka ghafla kwa mama yako mpenzi lakini hayo yote ni mapenzi ya Mungu.Hutoa na kutwaa katika muda ambao anautaka yeye mwenyewe.Tunachopaswa kufanya ni kuzidi kumuombea ili Mungu ampumzishe kwa amani ." akasema mzee benard.
" Kama familia tunapenda kukukabidhi salamu zetu za rambi rambi." akasema mzee Benard kisha akainuka na kumpa mkono Latoya na kumkabidhi bahasha iliyofungwa vizuri iliyoandikwa juu.MKONO WA POLE TOKA FAMILIA YA VINCENT BENARD..TSH 5,000,000/= halafu Sarah na Grace nao halikadhalika wakainuka na kumpa mkono Latoya.Ukapita ukimya mfupi kisha Latoya akasema
" Baba na dada zangu wote, kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati toka ndani kabisa mwa moyo wangu kwa kitendo chenu cha kuja kunitembelea na kunipa pole kwa msiba ulionipata.Kifo hakizoeleki na nitaendelea kulia kwa muda mrefu lakini ninawashukuru sana kwa kuja kunifariji .Ninajisikia faraja sana kwa kuja kwenu na ninajiona siko peke yangu bali niko na watu ambao wanalia na mimi.Ninasema Ahsanteni sana .Karibuni na mjisikie nyumbani.Mnakaribishwa hapa muda wowote mnapojisikia kuja kutembea.Milango iko wazi saa ishirini na nne." akasema Latoya.
" Hata sisi tunashukuru sana kwa mapokezi mazuri na makaribisho tuliyopewa.Tunashukuru sana Latoya" akasema mzee Benard kisha wakaendelea na maongezi mengine na baada ya kama saa moja ya kuwepo pale kwa Latoya wakaaga wakitaka kuondoka .
" Baba ninawashukuru sana kwa kuja kunitembelea siku ya leo.Nimefurahi sana kuonana nanyi tena.Nifikishieni salamu zangu kwa mama na mwambieni kwamba ninampenda sana na ninashukuru kama tumesameheana kwa yale yote yaliyotokea .Jambo moja ambalo ninataka kuwaeleza ni kwamba pamoja na kwamba zile tofauti zetu zote zimekwisha lakini sintaweza kurejea nyumbani.Nitaendelea kuishi hapa na Latoya.Nitakuwa nikija mara kwa mara nyumbani kuwasalimu kila pale nitakapokuwa nikipata nafasi." akasema Innocent
" Usijali Innocent.Wewe ndiye mwamuzi wa maisha yako na siku zote sisi tunataka kukuona ukiwa na furaha.Tumefurahi sana kukuona na kuhakikisha kwamba unaishi sehemu salama.Tunachokuomba usiache kuja nyumbani kututembelea.Tutafurahi sana kukuona tena nyumbani" akasema baba yake Innocent halafu wakaondoka.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO.........


BEFORE I DIE
SEHEMU YA 47
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
" Hata sisi tunashukuru sana kwa mapokezi mazuri na makaribisho tuliyopewa.Tunashukuru sana Latoya" akasema mzee Benard kisha wakaendelea na maongezi mengine na baada ya kama saa moja ya kuwepo pale kwa Latoya wakaaga wakitaka kuondoka .
" Baba ninawashukuru sana kwa kuja kunitembelea siku ya leo.Nimefurahi sana kuonana nanyi tena.Nifikishieni salamu zangu kwa mama na mwambieni kwamba ninampenda sana na ninashukuru kama tumesameheana kwa yale yote yaliyotokea .Jambo moja ambalo ninataka kuwaeleza ni kwamba pamoja na kwamba zile tofauti zetu zote zimekwisha lakini sintaweza kurejea nyumbani.Nitaendelea kuishi hapa na Latoya.Nitakuwa nikija mara kwa mara nyumbani kuwasalimu kila pale nitakapokuwa nikipata nafasi." akasema Innocent
" Usijali Innocent.Wewe ndiye mwamuzi wa maisha yako na siku zote sisi tunataka kukuona ukiwa na furaha.Tumefurahi sana kukuona na kuhakikisha kwamba unaishi sehemu salama.Tunachokuomba usiache kuja nyumbani kututembelea.Tutafurahi sana kukuona tena nyumbani" akasema baba yake Innocent halafu wakaondoka

ENDELEA…………………..

"Innocent nimeipenda familia yako.Una bahati ya kuwa na familia yenye upendo kama hii" akasema Latoya wakati wakitembea kuelekea ufukweni.
" Ningefurahi sana kama ningekuwa na familia yenye upendo kama hii.Niliingia pale sebuleni na kuwakuta mkiwa mmekumbatiana .Nilitamani sana kama na mimi ningejumuika nanyi." akasema Latoya
"Kwa nini hukujiunga nasi? akauliza Innocent huku akicheka
" Sikukaribishwa kujiunga" akasema Latoya halafu wote wakaangua kicheko.
" Pamoja na kuja kutoa salamu za rambi rambi lakini baba pia alikuja kuniomba msamaha kwa niaba ya familia kwa yale mambo yote yaliyotokea hasa wakati ule wa ugonjwa wa Marina. Kama unakumbuka tulivurugana sana na familia yangu hata ikanilazimu kuondoka nyumbani na kwa bahati nzuri ukajitokeza wewe na kunisaidia.Wamejitafakari na kugundua makosa waliyoyafanya na kwa sasa wameamua kuishi maisha mapya yenye furaha na upendo na ndiyo maana umeona leo hii wameongozana na Grace kitu ambacho hakikuwa cha kawaida huko nyuma.Kwa sababu zile tofauti zetu zote zimemalizika baba aliniomba nirejee tena kuishi nyumbani na kuniomba niendelee tena kuisimamia ile kampuni yetu ya kutengeneza maji ya kunywa ambayo imeanza kuyumba tena baada ya mimi kuondoka katika kipindi hiki cha siku chache" akasema Innocent.
" Ulimjibu nini kuhusu ombi lake hilo ? akauliza Latoya
" Nilimweleza ukweli kwamba kwa sasa siwezi tena kurejea na kuendelea kuishi nyumbani . Nimekwisha yaanza maisha mengine kabisa ." akasema Innocent.Latoya akasimama akamtazama usoni na kuuliza.
" Innocent kwa nini ulichagua kuishi na mimi hapa kuliko kwenda kuishi na familia yako?
.Innocent akatabasamu kisha akasema
" Ni kwa sababu unanihitaji zaidi ya wao wanavyonihitaji kwa sasa.One more thing,I’m here because I feel like I belong to this place" akasema Innocent .Latoya akamuangalia kwa mshangao.
" Thanx God...nakushukuru Mungu kwa kuniletea huyu kijana.Nashukuru kwa kumfanya aamini kwamba hapa ndipo sehemu anapotakiwa kuwepo" akawaza Latoya akiwa bado anamuangalia Innocent.
" Innocent sipati neno zuri la kushukuru kwa kuamua kuishi na mimi hapa.Ni kweli kwamba nakuhitaji mno.Nakuhitaji sana Innocent.Tell me one thing." akasema Latoya
" Whats that Latoya? akauliza Innocent
" Are you Happy here? akauliza Latoya.Innocent naye akamtazama Latoya usoni kwa muda kisha akasema
" I'm happy here" akasema Inno.Latoya akatabasamu
" Innocent tell me the truth..are you happy? akauliza tena Latoya
" I'm happy Latoya..very happy"
" Innocent macho yako hayaonyeshi kama una furaha.Jambo gani linakusumbua? Toka nimekuona asubuhi ya leo unaonekana ukiwa na mawazo mengi sana.Bado unayakumbuka mazishi ya mama? akauliza Latoya
" Ushofu Latoya hali hii imetokana na uchovu mwingi niliokuwa nao.Lakini naomba ufahamu kwamba nina furaha sana kuwa nawe hapa na ningependa sana kuwepo hapa kwa muda mrefu zaidi"
" Kitu gani kimekuvutia zaidi hapa kwangu? akauliza Latoya huku akitabasamu
" Kikubwa kinachonivutia zaidi ni kuwa karibu nawe.Siwezi kuielezea furaha ninayoisikia nikiwa nawe karibu lakini kinachonisikitisha na kuniumiza sana ni baada ya kusikia kwamba hautakuwa na maisha marefu.You'll have to die soon." akasema Innocent na mara Latoya akastuka sana na kumuangalia Inno kwa macho makali
"Umesema nini? akauliza Latoya.
" Latoya you are my friend.Can you tell me the truth? akauliza Innocent
" What truth Innocent? akauliza Latoya huku uso wake ukionyesha mstuko wa dhahiri na wasi wasi mwingi.
" Is it rue that you are going to die soon? akauliza tena Innocent
Latoya akavuta pumzi ndefu kisha akamtazama Innocent kwa macho makali.Alibadilika ghafla na kuanza kutokwa na jasho jingi usoni.Akakichomoa kibanio cha nywele kichwani na kukitikisa kichwa chake na nywele zake ndefu zikaruka na kuufunika uso wake. Innocent akaogopa kwa mabadiliko yale ya ghafla .Hakuwahi kumona Latoya akiwa katika hali hii.
" Help me God..Nimeharibu kila kitu kwa kumuuliza swali lile kuhusiana na jambo lile aliloniambia Brandon.Siku zote Latoya huwa hataki kuulizwa chochote kuhusiana na maisha yake.Help me God..I'm so scared..Its getting worse....." akawaza Inncent huku mwili ukimtetemeka kwa namna Latoya alivyobadilika.
" Aaaaggghhhh ..!!!!...." akasema Latoya kwa hasira huku akiigonganisha mikono yake.Innocent akazidi kuogopa.
" Bandon I hate you.I hate you so much..." akasema Latoya halafu akatoa kitambaa katika mfuko wake wa koti na kujifuta jasho jingi lililokuwa linamtiririka.Innocent alikuwa amesimama hatua kadhaa akiogopa kupita kiasi hakutaka kabisa kumkaribia Latoya kwa namna alivyokuwa amebadilika.
" Sikutegemea kama Latoya angeweza kukasirika na kubadilika namna hii...Ameniogopesha mno .Akikasirika anaonekana ni mtu hatari sana.Mungu anisaidie siku hii ya leo iweze kumalizika salama kwa sababu sijawahi kumuona Latoya akiwa katika hali hii" akawaza Innocent.Latoya bado aliendelea kusimama akijifuta jasho lililokuwa likimtoka usoni.Akazikusanya nywele zake ndefu na nzuri na kuzirudisha nyuma na kumtazama Innocent ambaye bado alikuwa amesimama akitetemeka mwili.
" Innocent mpigie simu Irene aniletee maji ya kunywa." akasema Latoya
" Usijali Latoya ngoja nikimbie mimi mwenyewe nikachukue"
Innocent akatoka mbio kufuata maji ya kunywa na kumuacha Latoya ameketi juu ya jiwe.
" Brandon ameniudhi sana .Kwa nini anifanyie hivi? Kwa nini amwambie Innocent kuhusu siri zangu? Suala hili ni siri kubwa na hakuna mtu yeyote anayefahamu kwamba nitakufa hivi karibuni.Innocent hatakiwi kujua jambo lolote lile linalohusiana na maisha yangu.Ninamuhitaji Innocent katika maisha yangu haya mafupi niliyobaki nayo na siko tayari kumuona akiondoka katika mikono yangu.Tayari Brandon amekwisha muogopesha na sijui katika mawazo yake anawaza jambo gani hivi sasa.Niliweka ahadi ya kumpata mwanaume wa maisha yangu kabla sijafa na tayari mwanaume huyo yuko mikononi mwangu.Sintakubali Innocent anipotee hata kidogo.Nitafanya kila niwezalo niendelee kuwa naye japo kwa muda huu mfupi niliobaki nao.Sijawahi kuwa na furaha katika maisha yangu licha ya kuzungukwa na utajiri wa kutisha hadi nilipokutana na Innocent.Sintakubali aondoke katika maisha yangu hata kama ikinibidi kumweleza ukweli wa maisha yangu nitafanya hivyo...." akawaza Latoya halafu akastuka ghafla
" No ! ..Innocent hapaswi kufahamu chochote kuhusu maisha yangu.Sitaki apate matatizo yoyote.I will never forgive myself if anything happens to him.The second he knows the truth about me he will die..." Latoya akainama akazama katika mawazo mengi.
" Nitafanya nini sasa? damn you Brandon !...Umeamua kupambana na mimi kupitia Innocent kwa sababu unafahamu kwamba ndiye furaha ya maisha yangu.Lakini nitapambana nawe na wala sintakupa nafasi kama hii tena ya kutaka kuuvuruga uhusiano wangu na mwanaume ninayempenda.Niko tayari kuvumilia kila aina ya mateso lakini si kumpoteza Innocent.." akawaza Latoya akiwa ameinama na mara akastuliwa na Innocent.
" Latoya maji haya hapa"
Bado sura ya Innocent ilionyesha wasi wasi mwingi.Latoya akayapokea maji yale akanywa kidogo halafu akamgeukia Innocenti.
" Ahsante sana Innocent" akasema Latoya.
" Latoya samahani sana kama nilikuudhi kwa kukuuliza swali kama lle.Sikujua kama ningekukasirisha namna ile.Naomba unisamehe sana na sintarudia tena kuuliza swali kama lile " akasema Innocent.
" Innocent njoo ukae karibu yangu" akasema Latoya.Kwa uoga Innocent akamsogelea na kuketi pembeni yake juu ya jiwe.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kwa kasi kubwa.
"Innocent ni kweli nilistuka sana na nilichukia ghafla .Sikuchukia kwa sababu umeniuliza swali lile bali kwa jambo alilolifanya Brandon.Najua ni Brandon ndiye aliyekwambia mambo haya..." akasema Latoya na kumtazama Innocent usoni.
" Ndiyo Latoya.Ni Brandon ndiye aliyeniambia mambo haya yote.Niliumia sana moyo baada ya kusikia vile ndiyo maana ikanilazimu nikuulize ili nifahamu kama ni kweli yale aliyoniambia " akasema Innocent.Latoya akainama chini kwa sekunde kadhaa halafu akainua kichwa chake.
" Ilikuaje hadi ukaonana na Brandon na akaongea maneno haya? akauliza Latoya.Innocent akakohoa kidogo na kusema
" Jana usiku nikiwa nimepitiwa na usingizi ,ghafla nikakurupuka baada ya kuota ndoto.Bado sikumbuki kama ilikuwa ni ndoto ama vipi lakini nilikusikia ukilia na kuniita ukiniomba nikusaidie.Nilikumbuka kwamba tuliachana ukisema kwamba unaenda kuonana na Brandon.Nilimkuta Brandon akiwa ufukweni akipunga upepo na nilipomuuliza kuhusu mahala ulipo tulishindwa kuelewana kabisa.Alinitolea vitisho vingi kwamba nikae mbali nawe na iwapo nitaendelea kuwa nawe karibu atanionyesha yeye ni nani.Aliniambia kwamba kamwe haitawezekana mimi na wewe kuwa ......" Innocent akastuka kisha akakaa kimya
"Haitawezekana mimi na wewe kuwa nini? akauliza Latoya
" Mimi na wewe kuendelea kuwa marafiki " akasema Innocent na kumfanya Latoya atabasamu.
" Alinieleza kwamba kwa kuwa karibu nawe ninakusababishia matatizo makubwa." akasema Innocent halafu akanyamaza kidogo na kuendelea.
" Tulishindwa kuelewana jana usiku.Leo asubuhi aliomba Irene kuonana nami tena..Aliniambia kwamba anaondoka lakini akaendelea kunisisitiza kwamba kama nikitaka kuishi maisha yenye amani na utulivu basi niondoke haraka sana katika maisha yako . Nilimueleza kwamba sintaweza kuondoka na kukuacha peke yako ndipo alipokasirika na kuniuliza kama ninafahamu ni muda gani uliobakiwa nao kabla hujafariki.Nilistuka sana na nikaanza kuogopa."
" Kwa nini uliogopa Inno? akauliza Latoya
" Kwa sababu ninafahamu kifo cha mtu ni siri ya Mungu pekee na hakuna binadamu anayefahamu siku yake ya kufa au hata siku ya kufa kwa mwenzake labda iwe ni kwa kupanga.Vile vile uhhm .. I dont want you to die" akasema Innocent
" Why you dont want me to die ?.." akauliza Latoya
" Its because....Its because......Bacause....." Innocent akababaika kujibu.
" Because of what Innocent? akauliza Latoya
" Its because you are too young to die. Nimekufahamu kwa siku chache zilizopita lakini ninafurahi sana kuwa rafiki yako.Ninahisi furaha ya ajabu sana nikiwa hapa na ndiyo maana ninathubutu kusema kwamba I belong to this place kwa sababu ni sehemu pekee ninayoweza kuhisi furaha ya moyo wangu na hasa nikiwa nawe kama hivi tulivyo" akasema Innocent
This guy..he's the one.Ninampenda Innocent zaidi ya ninavyojipenda na nitafanya kila linalowezekana niwe naye katika siku zote zilizobakia.Nitamlinda na kila anayetaka kumdhuru." akawaza Latoya.
" Innocent naomba nikuulize kitu kimoja" akasema Latoya
" Do you believe him? I mean Brandon,do you believe him? ..
Innocent akakaa kimya kwa sekunde kadhaa na kusema
"No I dont..I believe only you..tell me its not true and I’ll believe" akasema Innocent.Latoya akatabasamu
" Ahsante sana Innocent kwa kuniamini.Naomba unisamehe vile vile kwa kukasirika namna ile pale uliponiuliza swali lile.Sikutegemea hali ile kunitokea mbele yako.Sikuchukia kwa sababu eti uliniuliza lile swali lakini nilichukia kwa sababu Brandon alikudanganya.Ukweli ni kwamba mimi na Brandon ni marafiki na tumekuwa tukishirikiana kibiashara kwa muda mrefu.Matatizo baina yetu yalianza pale ambapo Brandon alianza kuingiwa na tamaa za kimwili na kunitaka niwe mpenzi wake.Kwa kuwa alikuwa ni rafiki yangu mkubwa na mshirika wangu muhimu kibiashara sikutaka kuharibu ushirikiano wetu mzuri tulionao kwa kuingiza masuala ya mapenzi.Nilimweleza ukweli kwamba sikuwa tayari kwa jambo hilo analolitaka lakini hakukata tamaa bali aliendelea kusisitiza kwamba ananipenda na atahakikisha kwamba siku moja ninakuwa mpenzi wake.Hii ni sababu iliyonifanya nikae naye mbali kwa sababu sikutaka urafiki wetu uishe kwa sababu tu ya kumkatalia ombi lake.Hadi hivi sasa bado ana mawazo kwamba siku moja mimi na yeye tutakuwa wapenzi.Ni kipindi cha muda mrefu sijaonana naye na alipopata taarifa za msiba wa mama toka kwa washirika wangu wa biashara akaja mara moja msibani na ndiyo maana kama utakumbuka nilipomuona nilistuka sana kwa sababu sikutegemea kabisa kama ningeonana naye sehemu kama ile.Brandon aligundua kwamba mimi na wewe tuna ukaribu mkubwa kitu ambacho hakukipenda kwani aliihitaji sana nafasi ya kuwa karibu na mimi kama hivi tulivyo .Nilimweleza ukweli kwamba siko tayari kumpa nafasi hiyo na akaniahidi kwamba lazima atahakikisha ananitenganisha na wewe kwa sababu anaamini kwamba wewe ndiye sababu ya mimi kumnyima nafasi katika moyo wangu.Nilimuelewesha kwamba mimi na wewe ni marafiki wa kawaida lakini hakuamini na ndiyo maana aliamua kutunga uongo wa namna hii ili kukufanya uogope na uachane nami.Innocent niko tayari kutengana na watu wote wa dunia hii lakini si kutengana na wewe.Wewe ni rafiki na mtu wa muhimu mno katika maisha yangu ambaye sijawahi kumpata.Kwa hiyo nakuomba usiuamini uongo huo aliokwambia Brandon.Lengo lake ni kunitenganisha na wewe tu"" akasema Latoya

TUKUTANE SEHEMU IJAYO………………………….

BEFORE I DIE
SEHEMU YA 48
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Ni kipindi cha muda mrefu sijaonana naye na alipopata taarifa za msiba wa mama toka kwa washirika wangu wa biashara akaja mara moja msibani na ndiyo maana kama utakumbuka nilipomuona nilistuka sana kwa sababu sikutegemea kabisa kama ningeonana naye sehemu kama ile.Brandon aligundua kwamba mimi na wewe tuna ukaribu mkubwa kitu ambacho hakukipenda kwani aliihitaji sana nafasi ya kuwa karibu na mimi kama hivi tulivyo .Nilimweleza ukweli kwamba siko tayari kumpa nafasi hiyo na akaniahidi kwamba lazima atahakikisha ananitenganisha na wewe kwa sababu anaamini kwamba wewe ndiye sababu ya mimi kumnyima nafasi katika moyo wangu.Nilimuelewesha kwamba mimi na wewe ni marafiki wa kawaida lakini hakuamini na ndiyo maana aliamua kutunga uongo wa namna hii ili kukufanya uogope na uachane nami.Innocent niko tayari kutengana na watu wote wa dunia hii lakini si kutengana na wewe.Wewe ni rafiki na mtu wa muhimu mno katika maisha yangu ambaye sijawahi kumpata.Kwa hiyo nakuomba usiuamini uongo huo aliokwambia Brandon.Lengo lake ni kunitenganisha na wewe tu"" akasema Latoya


ENDELEA………………………….

" Latoya nashukuru sana kwa kunieleza ukweli.Ninashukuru vile vile kupata nafasi ya kuwa mmoja wa watu wako wa karibu na muhimu.Ninakuahidi kwamba siku zote nitakuwa karibu nawe na sintakuacha kamwe hata kama wapo watu ambao hawapendi ukaribu wetu" akasema Innocent na mara Latoya akatabasamu
" Ahsante sana Innocent kwa maneno hayo ya faraja.Huwezi kujua ni kwa kiasi gani moyo wangu umefurahi kwa maneno hayo uliyoniambia.Ahsante sana Innocent.Nakuahidi kwamba nitakulinda na yeyote yule ambaye ana lengo baya na wewe.Nakuomba uwe na amani siku zote na kama una tatizo lolote usisite kuniambia.Niko tayari hata kutumia utajiri wangu wote nilionao kwa ajili ya kukupatia kile unachokihitaji" akasema Latoya.
" Pamoja na hayo yote Latoya naomba nikuulize swali moja dogo" akasema Innocent
" Uliza Innocent wala usihofu"
" This guy Brandon do you love him?
Latoya akainamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa.Hakuwa amelitegemea swali lile .
" Innocent sijakuelewa una maanisha nini.."
"Ninamaanisha kwamba huyu kijana Brandon una hisia zozote za kimapenzi kwake?
"Hapana.Simpendi na sijawahi kumpenda na sintampenda kamwe." akasema Latoya
“ok Good.” Akasema Innocent.Kimya kifupi kikapita halafu akauliza tena.
" Latoya una mpenzi?
" Hapana sina mpenzi .sijawahi kuwa naye lakini nategemea kuwa naye " akasema Latoya.Innocet akatabasamu na kusema
" Mwanaume atakayekupata atakuwa na bahati sana"
" Kwa nini unasema hivyo Innocent? akauliza Latoya
" Kwa sababu wewe ni mwanamke wa pekee kabisa na unafaa kuwa mke bora.Una kila kitu ambacho mwanaume anakihitaji toka kwa mwanamke.Una roho nzuri ya uvumilivu na upendo,hupendi kujikweza licha ya utajiri ulionao,na kubwa zaidi ya yote ni mzuri kama malaika" akasema Inno na kumfanya Latoya acheke kicheko kikubwa.
" Thank you Innocent for making me laugh again" akasema Latoya.
" Laiti ungejua kwamba wewe ndiye huyo mwanaume huyo mwenye bahati ya kuuteka moyo wangu.Natamani nikwambie ukweli namna gani ninakupenda lakini ninashindwa.Ninakupenda Innocent na nitafanya kila niwezalo uwe wangu" akawaza Latoya
" Latoya ni kwa nini msichana mzuri kama wewe ambaye kila mwanaume angependa awe nawe unaishi bila ya kuwa na mpenzi? akauliza Innocent.
" Ouh C'mon Innocent.Leo una maswali mengi sana.Naomba unisamehe sana kwa sababu mara nyingi huwa sipendi kuzunguzia maisha yangu binafsi.Umekuwa ukiniuliza maswali kuhusu mimi..what about you? where is your girlfriend? akauliza Latoya
" Sina rafiki wa kike kwa sasa na ninaomba usiniulize kwa nini kwa sababu hata mimi sielewi ni kwa nini. " akasema Innocent.Latoya akainuka pale katika jiwe akamshika Innocent mkono wakaanza kutembea ufukweni.
"Innocent huwezi kujua ni kwa nini huna mpenzi hadi hivi sasa,huwezi kufahamu vile vile ni kwa nini ulikutana na Marina na akafariki dunia mapema mara tu baada ya wewe kukutana naye.Kila jambo hutokea kwa sababu maalum.Huwezi kufahamu pengine kifo cha Marina kilikuwa ni daraja la kukuvusha na kukupekeleka kwa mwanamke wa maisha yako.Mapenzi ni kitu cha ajabu sana. " akasema Latoya huku wakitembea ufukweni.Baada ya ukimya mfupi Latoya akauliza
" Innocent una furaha na maisha yako ? ..
Innocent akatabasamu na kusema
" Yah..Ninajisikia furaha kubwa sana hasa baada ya kukutana nawe.What about you,are happy with your life ? Latoya akainama chini akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
" I've never been happy with my life" akasema Latoya na kukaa kimya.
" Latoya wewe ni msichana mzuri naweza kusema kuliko wote duniani,una utajiri mkubwa na unapata kila unachokihitaji katika maisha yako ,kwa nini ukose furaha? kwa nini ushindwe kuyafurahia maisha yako? akauliza Innocent.Latoya akatabasamu na kusema.
" Unaweza ukawa na kila kitu katika maisha lakini ukakosa furaha.Nina kila kitu ninachokitaka lakini sina furaha na maisha yangu ..well let’s forget about that..Let's talk about something else" akasema Latoya.Innocent akasimama akamtazama Latoya kwa makini.
" Mbona unanitazama hivyo? akauliza Latoya
" Latoya naomba niwe muwazi kwako...nimekuwa nikitafuta nafasi ya kukueleza kuhusu kile kilichomo moyoni mwangu na ninafikiri kwamba huu ni wakati muafaka wa kukueleza" akasema Innocent na kumfanya Latoya asimame akimuangalia huku moyo wake ukimuenda mbio.Hakujua Innocent anataka kumweleza kitu gani
"Nieleze Innocent. I'm listening" akasema Latoya huku akimuangalia Innocent kwa shauku ya kutaka kufahamu nini ambacho Innocent anataka kumweleza.
" Ouh C'mon Innocent Niambie tafadhali kilichomo moyoni mwako.I'm dying to know." akawaza Latoya akiwa bado anamuanglia Innocent.
“Niambie tafadhali Innocent unatachotaka kuniambia” akasema Latoya baada ya kuona Innocent yuko kimya.Innocent akakohoa kidogo na kusema
“Latoya naomba niwe wazi kwako kwamba moyo wangu unaumia sana kukuona ukiwa huna furaha.Msichana mzuri kama wewe unatakiwa uwe ni mwenye furaha wakati wote.Latoya you have everything in life but you are not happy.If there is anything that I can do to make you happy please let me know.Niko tayari kwenda hadi mwisho wa dunia kwa sababu moja tu only to make you happy” akasema Innocent.Latoya akashusha pumzi ndefu akatabasamu na kusema
“what a sweet words Innocent.Sijawahi kutamkiwa maneno mazito namna hiyo.Ni kweli unavyosema,pamoja na utajiri wangu mkubwa na kujulikana na watu wengi lakini hapajawahi tokea mtu yeyote ambaye amewahi kutambua kwamba maisha yangu hayana furaha.Kila anionaye anafikiri kwamba nina furaha kubwa na maisha yangu.You are the first person to notice that I’m not happy with my life.You are the first person also to tell me that you are ready to go to the end of the world to search for my happiness.Innocent huna haja ya kwenda hadi mwisho wa dunia kwa ajili yangu.Innocent sina haja ya kwenda mbali kuitafuta furaha ya maisha yangu wakati kila kitu kinachoweza kunifanya niwe mwenye furaha kiko nami.Innocent wewe ndiye furaha yangu.Unanifanya niwe na furaha kila dakika unapokuwa karibu yangu.Kitu pekee unachoweza kukifanya ambacho kitanipa furaha katika maisha ni kuwa karibu yangu kama ndugu yangu kama rafiki yangu kama mtu wangu wa karibu.Stay with me Innocent.Stay with me for good” akasema Latoya
Maneno yale yalimwingia Innocent akafurahi na kutamani kumkumbatia Latoya lakini akaogopa akikumbuka siku ile alipopigwa na kitu kama chaji za umeme alipojaribu kuupeleka mkono wake mgongoni kwa Latoya.
“ Kadiri siku zinavyozidi kwenda najikuta nikimpenda zaidi Latoya.Anazidi kuniingia moyoni mwangu kila sekunde.Ouh Gosh ! I don’t know what to do anymore.I cant leave this place anymore.I cant leave Latoya alone. She needs me and I’m falling in love with her” akawaza Innocent.
“ Innocent mbona uko kimya? Akauliza Latoya
“Latoya maneno yako yananifanya nikose neno la kusema.Lakini kama nilivyokwambia huko nyuma kwamba I feel connected to this place kwa maana hiyo usiwaze kuhusu mimi kuondoka na kukuacha peke yako,katu siwezi kufanya hivyo” akasema Innocent.Kimya kifupi kikapita halafu Latoya akasema
“Innocent unakumbuka nilikwambia kwamba nitakuwa na safari ya kueleka mapumzikoni?
“ Ndiyo nakumbuka” akajibu Innocent
“Basi tutakwenda sote katika hiyo safari.Kila mwaka huenda peke yangu kupumzika katika sehemu tulivu lakini safari hii naomba tuende sote.Nadhani yatakuwa ni mapumziko ya aina yake.” Akasema Latoya .Innocent akatabasamu
“Usijali Latoya nitaongozana nawe katika safari hiyo. Tutaondoka lini? Akauliza Innocent.Latoya akatabasamu na kusema
“ Nitakutaarifu.Kuna mambo ambayo nataka kuyashughulikia kabla ya kuondoka” akasema Latoya.Innocent akataka kusema kitu lakini akastushwa na sauti ya mawimbi mazito ya bahari yaliyoanza ghafla.Latoya akageuka na kutazama baharini.Mawimbi yalikuwa makubwa yakipiga kuelekea kule walikokuwa wamesimama.Upepo mkali nao ukaanza kuvuma.
“ Hali ya bahari imechafuka.Let’s go Innocent” akasema Latoya wakaondoka kurudi nyumbani ambako waliekea moja kwa moja katika ukumbi wa chakula
“ Innocent jioni ya leo kuna sehemu ambayo nataka unisindikize” akasema Latoya
“ Usijali Latoya.Nitakusindikiza” akajibu Inno halafu wakaendelea kula kimya kimya
“ Innocent do you believe in God? Akauliza Latoya.Innocent akainua kichwa chake akamtazama Latoya na kusema
“Yes I do.” akajibu Inno
“What about you? Do you believe in God” akauliza Inno.Latoya akakaa kimya,akaweka kijiko mezani akafikiri kidogo na kusema
“ I do..I believe in God”
Mara tu aliposema maneno hayo macho yake yakaanza kuwa mazito
“ Gosh !! I’m going down again..Ouh No! not here” akasema Latoya huku akiinuka
“Innocent naenda kupumzika.Tutaonana baadae” akasema Latoya .Innocent akastuka
“ Latoya mbona hujala chakula? Unajisikia vibaya?
Latoya hakujibu kitu,akatembea kwa kasi kuelekea kwenye lifti na kupanda kuelekea chumbani kwake.Mara tu alipotia mguu chumbani kwake nguvu zikamuishia akaanza kuona giza
“.I’m going down. !” akasema Latoya na kuanguka chini akapoteza fahamu
“ Latoya ana matatizo makubwa.Kuna siri gani katika maisha yake ambayo hataki watu waifahamu? Akawaza Innocent baada ya Latoya kuondoka.Sura ya Latoya ikamjia kichwani akatabasamu
“ I’m falling in love with her.I think she’s a perfect woman for me.She’s the woman of my dream” Akawaza Innocent huku akitabasamu
“Latoya hana furaha katika maisha yake na hili ndilo jambo linaloniumiza mno kichwa changu.Natamani kumjua kiundani ili niweze kumsaidia aweze kuwa na furaha kama watu wengine .”Akawaza Innocent halafu akatoka mle katika chumba cha chakula na kuelekea chumbani kwake akajitupa kitandani,
“Maisha ni kitu cha ajabu sana.Inashangaza kuona namna maisha yangu yalivyobadilika ghafla.Nilikuwa na ndoto nyingi za maisha yangu lakini kwa sasa sina hakika kama nitaweza kuzifanya ndoto hizo ziwe kweli.Ndoto yangu kubwa kwa sasa ni kumfanya Latoya awe ni mwenye furaha.Nitafanya kila ninachoweza hadi nihakikishe sura ya Latoya imekuwa ni yenye kutabasamu daima..” Akawaza Innocent halafu akainuka na kukaa kitandani

TUKUTANE SEHEMU IJAYO……………………….


: BEFORE I DIE
SEHEMU YA 49
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Latoya hakujibu kitu,akatembea kwa kasi kuelekea kwenye lifti na kupanda kuelekea chumbani kwake.Mara tu alipotia mguu chumbani kwake nguvu zikamuishia akaanza kuona giza
“.I’m going down. !” akasema Latoya na kuanguka chini akapoteza fahamu
“ Latoya ana matatizo makubwa.Kuna siri gani katika maisha yake ambayo hataki watu waifahamu? Akawaza Innocent baada ya Latoya kuondoka.Sura ya Latoya ikamjia kichwani akatabasamu
“ I’m falling in love with her.I think she’s a perfect woman for me.She’s the woman of my dream” Akawaza Innocent huku akitabasamu
“Latoya hana furaha katika maisha yake na hili ndilo jambo linaloniumiza mno kichwa changu.Natamani kumjua kiundani ili niweze kumsaidia aweze kuwa na furaha kama watu wengine .”Akawaza Innocent halafu akatoka mle katika chumba cha chakula na kuelekea chumbani kwake akajitupa kitandani,
“Maisha ni kitu cha ajabu sana.Inashangaza kuona namna maisha yangu yalivyobadilika ghafla.Nilikuwa na ndoto nyingi za maisha yangu lakini kwa sasa sina hakika kama nitaweza kuzifanya ndoto hizo ziwe kweli.Ndoto yangu kubwa kwa sasa ni kumfanya Latoya awe ni mwenye furaha.Nitafanya kila ninachoweza hadi nihakikishe sura ya Latoya imekuwa ni yenye kutabasamu daima..” Akawaza Innocent halafu akainuka na kukaa kitandani

ENDELEA………………………………...
Fahamu zilianza kumrudia Latoya.Akaanza kuhisi ubaridi ukimpenya na kwa mbali akahisi unyevu nyevu..Akafumbua macho na kujikuta amelala katika dimbwi la damu.Machozi yakamtoka
“ Ouh my God ! akasema Latoya kwa uchungu,akajitahidi kunyanyuka japokuwa mwili haukuwa na nguvu kabisa
“Ninazidi kudhoofika siku hadi siku.My death is so near.I can feel it.Ouh my God I dont want to die….I want to live..” Latoya akalia kwa uchungu.Akaitazama damu ile sakafuni akasikia uchungu mkubwa.
“ Ninapoteza damu kila siku.Nimwite daktari wangu?
Akafikiri kidogo na kusema
“ Hapana hakuna haja ya kumuita.Muda umekaribia sana na hatakuwa na msaada wowote hata kama akija.I’m going to die soon” akawaza Latoya huku akiendelea kutoa machozi.Akatembea huku akipepesuka hadi katika kabati lake kubwa akalifungua na kutoa dawa akameza halafu akaifuta damu ile iliyotapakaa pale chini
“ Nitaendelea kutumia vidonge vya kuongeza damu hadi hapo nitakapokufa.Sitaki kumuita tena daktari” akawaza Latoya huku akiendelea kuifuta damu ile.Alipomaliza akaelekea bafuni akaoga na kujilaza kitandani,sura ya Innocent ikamjia kichwani
“ I love him so much.Nataka kuitumia kila dakika ya maisha yangu yaliyobaki kuwa naye.Natakiwa niutumie vizuri muda wangu uliobaki.Kwa muda huu mchache uliobaki nataka niwe ni mwanamke mwenye furaha kama walivyo wanawake wengine.I want to be a woman.I want to be kissed,I want to make love for the first time.” Latoya akawaza halafu akastuka
“ Ouh gosh ! Sijawahi kufanya mapenzi toka nimezaliwa.Bado ni bikira mpaka leo hii.Nina hamu ya kufanya mapenzi ili nipate raha hiyo wanayoipata wanawake wenzangu.Nataka Innocent awe ni mwanaume wa pekeee ambaye ataitoa bikira yangu.Hii ni zawadi pekee kwake kabla sijafa” akawaza Latoya halafu akaanza kuhisi macho mazito akalala.
Saa kumi na mbili za jioni aliamka toka usingizini na kitu cha kwanza alichokifanya ni kumpiga simu Innocent ajiandae kuna mahala wanataka kuelekea.Bado alihisi mwili wake hauna nguvu akafungua kabati lake na kuchukua chupa ndogo yenye kinywaji fulani ndani yake ambacho huwa anakitumia kwa nyakati kama hizi anapohisi mwili wake uko dhaifu halafu akashuka na kukutana na Innocent.Hakutaka kuongozana na mlinzi yoyote.Hii ilikuwa ni safari yake na Innocent pekee.
“ Innocent endesha gari twende” akasema Latoya .Innocent akaendesha gari wakaondoka
“Unajisikiaje Latoya? Akasema Innocent baada ya kuona Latoya amekuwa kimya sana.
“ I’m ok Innocent” akajibu Latoya kwa ufupi
Walipofika katika mzunguko uliokuwa na njia tano,akamuelekeza Innocent afuate njia inayoelekea chini
Kandoni mwa barabara ile kulikuwa na maua mazuri na taa zenye rangi ya kuvutia.Baada ya mwendo wa kama dakika tano wakatokea katika jumba moja kubwa lililoonekana kama kanisa.Kulizunguka jumba hili kulikuwa na mandhari ya kuvutia mno.Maua ya kila rangi yalikuwa yamepandwa.Taa za rangi mbali mbali ziliwaka na kulifanya jumba lile kuwa la kupendeza mno.
“ what a beautiful place” akawaza Innocent halafu akaegesha gari mahala alikoelekezwa na Latoya katika kibaraza kilichokuwa na rangi nyekundu
“ Wait for me here” akasema Latoya na kushuka akalizunguka jumba lile kwa nyuma na kuingia ndani.Innocent bado eliendelea kuustaajabia uzuri wa mahala pale.Licha ya mandhari nzuri ya kuvutia,eneo lote lilikuwa na harufu nzuri ya uturi
Sehemu hii nzuri sana lakini bado sijaelewa hili ni kanisa au Jumba hili ni kwa ajili ya nini?.” akawaza Innocent halafu akastushwa na sauti ya mtu aliyemsemesha
“ Habari yako kijana? Innocent akatetemeka.Hakutegemea kumuona mtu maeneo yale yaliyokuwa na ukimya wa ajabu kiasi kwamba hakuna hata mdudu aliyekuwa akisikika akipiga kelele.Innocent akabaki amemkodolea macho mzee yule aliyekuwa amevaa suti nyeupe.Alikuwa na mvi nyingi kichwani.
“Hujambo kijana? Akarudia tena kuuliza yule mzee baada ya kuona Innocent hamjibu
“Sijambo mzee .shikamoo” akasema Inno kwa sauti ya uoga
“marahaba kijana wangu” akajibu yule mzee na kisha kimya kikapita
“Kijana unaitwa nani? Akauliza
“ naitwa Innocent” akajibu Inno
“Nafurahi kukufahamu Innocent.Mimi naitwa Ezekiah na ndiye mwangalizi wa eneo hili.Madam Sikujua kama madamLatoya alikuwa ameongozana na mtu na ndiyo maana nilipokuona nikastuka sana “ akasema mzee Ezekiah
“Jumba hili ni kwa ajili ya nini. Ni kanisa? Akauliza Innocent
“ Hapana hili si kanisa”
“ Mbona limejengwa kama kanisa?
“ kwa kweli hata mimi sifahamu jumba hili ni kwa ajili ya nini .Madamu Latoya huja hapa na kuingia ndani na sielewi huwa anafanya nini humo ndani.Sijawahi kuingia ndani na wala sijui kukoje na toka nimeanza kuliangalia eneo hili hakuna mtu yeyote ambaye amewahi kuingia ndani ya jumba hili zaidi ya madam Latoya pekee” “
“ Kwa muda gani umekuwa ukiliangalia eneo hili?
“ Huu ni mwaka wa tano sasa niko hapa.Mara tu baada ya jengo hili kukamilika mimi ndiye nilipewa kazi ya kuangalia na kutunza mazingira na kuhakikisha kwamba hakuna mtu yeyote anayekaribia eneo hili.” akasema mzee Ezekiah na kuzidi kumshangaza Innocent
“Umesema hakuna mtu anayeruhusiwa kufika eneo hili?
‘ Ndiyo Innocent.Hakuna mtu anayeruhusiwa kukanyaga eneo hili.Ni madam Latoya pekee ambaye huja hapa mara moja kila mwezi lakini nashangaa mwezi huu hii ni mara yake ya pili kufika hapa.Una uhusiano gani na Madam Latoya ? akauliza mzee Ezekiah
“ Latoya ni rafiki yangu” akasema Innocent
“ Marafiki? Mzee Ezekiah akashangaa
“ Ndiyo .Mimi na Latoya ni marafiki.Mbona umeshangaa mzee?
“ Namfahamu Latoya ana marafiki wengi lakini hata siku moja hajawahi kuongozana na mtu yeyote kuja hapa.Wewe ni mtu wa kwanza kuongozana naye kuja mahala hapa.Innocent naomba ufahamu kwamba wewe ni mtu pekee kabisa kwa Latoya.Amekuamini mno hadi akaambatana nawe sehemu hii ambayo inaonekana ni muhimu sana kwake” akasema mzee Ezekiah
“ mzee Ezekiah hebu naomba unieleze ukweli,mahala hapa kuna nini hadi asiruhusiwe mtu yeyote kupasogelea?
“ Sifahamu Innocent lakini ninachojua ni kwamba hii ni sehemu muhimu sana kwa Latoya na siku zote ajapo hapa huwa amevaa mavazi meupe na koti lake jeusi.Mimi na wewe hatuwezi kujua umuhimu wa eneo hili kwake”
“ Hujawahi kuogopa kukaa katika mazingira haya ?
“ hapo mwanzoni nilikuwa naogopa lakini kwa sasa nimekwisha zoea “ akasema Ezekiah
“ Ilikuaje hadi Latoya akakuamini na kukupa eneo hili ulitunze?
“ Kabla hajanipa kazi hii nilikuwa nafanya kazi ya kutunza bustani pale nyumbani kwake.Aliniita na kunipa masharti ambayo sitakiwi kuyavunja.Nilikubaliana na masharti yale na akanileta hapa.Madam Latoya ni mtu mzuri sana .Ana roho nzuri ya huruma.Ni msikivu na mwenye kujali watu.Hivi sasa nina maisha mazuri kuliko hata waziri.Nina jumba kubwa ,gari za kutembelea na yote hayo yametokana na wema wake.” akasema Ezekiah na ghafla eneo lote likawa na mwanga mkali.Innocent akastuka sana.
“ whats happening”?akauliza Innocent kwa woga
“ Hivi ndivyo inavyotokea kila Latoya ajapo hapa.Hutokea mwanga mkali ndani ya jumba lile na kumulika eneo hili lote” Akasema mzee Ezekiah
“ Mwanga huu mkali unatoka wapi na kulifanya eneo lote kuwa na mwangaza huu mkubwa ? “
“Innocent maswali yako ni magumu na yasiyo na majibu.Kitu pekee ambacho nataka kukushauri kijana wangu mambo yanayotokea hapa yaache kama yalivyo.Huna haja ya kutaka kufahamu chochote.Kingine kikubwa ambacho nataka kukusisitiza ni kwamba kamwe usithubutu kutaka kuyachunguza maisha ya Latoya.Ni kitu ambacho hakipendi kabisa.” Akasema mzee Ezekiah na taratibu akaondoka akamuacha Innocent peke yake akiendelea kushangaa kilichokuwa kimetokea.
“ Oh Mungu wangu ! Latoya si binadamu wa kawaida.Mambo yake ni mazito na yanaogopesha.” akawaza Innocent huku akihisi baridi mwilini
Latoya aliingia katika jumba lile ambalo lilikuwa na giza nene ndani.Akawasha taa ndogo nyekundu iliyomuwezesha kuona.Akafungua chumba kimoja akangia.Akavua mavazi yake na kuvaa gauni refu jeupe.Akatoka mle chumbani na kuelekea katika ukumbi mpana.Alikuwa akitembea taratibu hadi katika meza yenye mishumaa sita na kuiwasha halafu akapiga magoti akainama na kusujudu
“ Atha.Lut pakta du mokaja,akta pata ovakoja du mapakta” alitamka taratibu maneno haya .Akayarudia mara tatu na mara moshi ukaanza kutoka katika madhabahu ile .Latoya akaendelea kuongea maneno aliyoyafahamu yeye mwenyewe na kila alipoongea moshi mwingi ulizidi kutoka.Ulikuwa ni moshi wenye harufu nzuri ya uturi.Chumba chote kilijaa moshi na mara ghafla ukatokea mwanga mkali sana ambao ulimulika eneo lile lote.Baada ya mwanga ule mkali kutokea,Latoya akainuka na kusimama .Mbele yake toka ndani ya moshi ule wakatokea watu wawili wenye mavazi meupe na ndevu nyingi
“ Latoya unafahamu ulichokifanya leo.Kwa makusudi kabisa umelitaja jina la Mungu wao na kukiri kwamba unamuamini.Umekwenda nje ya misingi na kanuni zetu.Kwa kauli yako ile umemkana Mungu wetu ,umejikana mwenyewe na kumuabudu mungu wao.Hili ni kosa kubwa sana na unafahamu adhabu yake.Tumetumwa tukutaarifu kwamba muda wako umekaribia kuisha kwa hiyo ni wakati wako wa kufa na nafasi yako kuchukuliwa na mtu mwingine. Baada ya siku mbili unatakiwa kuanza safari na hii ndiyo safari yako ya mwisho.Hautarejea tena Tanzania.Hatakiwi mtu yeyote ajue kama ndiyo safari yako ya mwisho na kwamba hutarejea tena.Hayo ndiyo maagizo tuliyotumwa kwako na unatakiwa uyazingatie.Kwa sasa lala kifudi fudi na tukuadhibu kwa kosa la kumleta huyu kijana hapa mahala patukufu”Akasema mzee yule.Latoya alikuwa anatetemeka mwili.Taarifa ile ilimstua na kumuogopesha sana.Mzee mmoja akamfanyia ishara asogee na kupanda juu ya madhabahu.Taratibu Latoya akaisogelea madhabahu akapanda na kulala kifudi fudi juu yake.Mara akahisi kitu kama moto mkali unamuunguza mgongoni akapiga ukelele mkubwa
Innocent akiwa nje ya jumba lile aliusikia ukelele ule mkubwa alioupiga Latoya akastuka sana.
“ whats going on in there? Kwanini Latoya anapiga kelele? Akajiuliza Innocent .Ukelele ule ukazidi kuwa mkubwa
“ Latoya ana tatizo.Something is wrong in there.I have to help her.I’m going in ” akasema Innocent akashuka garini.Alipotaka kupanda ngazi ili akanyage kibaraza kile chenye rangi nyekundu alipigwa na kitu kizito usoni akaanguka na kupoteza fahamu


TUKUTANE SEHEMU IJAYO…………………………
 
Mkuu Lege tuko kwenye Foleni, ebu dondosha episodes ngingine kama Kumi hivi tupunguze Makali ya Foleni
 
I cant wait LEGE.I want to finish this story BEFORE I DIE,nimebakisha siku chache sana za kuishi jinsi unavyochelewesha huu mzigo unanisababishia maumivu makali sana aarrrrrgggggggggggh!!!!I'M GOING DOWN AGAIN!
We muite tu brandon....problem ina mauza uza sana ukisoma usiku unawezanuote
 
Dah asee inaitaji akili ya ziada kuujenga moyo wa uvumilivu kusubiria tupiamo za mkuu lege Dah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom