Simulizi: Before I die

BEFORE I DIE
SEHEMU YA 18
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Hatimaye akawasili katika jengo zilimo ofisi za taasisi binafsi inayoendeshwa na mwanadada Latoya. Aliposhuka garini akapanda lifti ya jengo lile hadi ghorofa ya tisa ambamo ndimo zilimokuwa ofisi za taasisi hiyo.Mtu wa kwanza kumtambua Inno alikuwa ni Sabrina.
“kaka Innocent karibu sana” Sabrina akamkaribisha Inno kwa furaha huku akitabasamu
“Hii ndiyo ofisi yetu kaka Innocent karibu sana.” Sabrina akasema huku akimtambulisha Inno kwa wafanyakazi waliokuwa pale ofisini.Innocent hakuificha furaha yake.Kwa muda huu mfupi aliowasili hapa kila mmoja alionekana kuufurahia ucheshi na uchangamfu wa Innocent. Baada ya maongezi na utani wa hapa na pale kama kawaida yake ,Sabrina akamchukua Inno na kumpeleka katika ofisi ya Latoya.
“Dada huyu ndiye Innocent,amekuja kukuona kwa ajili ya lile suala nililokueleza” Sabrina akamtambulisha Innocent kwa Latoya.Kwa sekunde kadhaa walibaki wanatazamana halafu Latoya akasema
“Karibu sana Innocent,nafurahi kukufahamu” Latoya akasema huku akisimama na kumpa mkono
“Hata mimi nafurahi sana kukufahamu “ Innocent akajibu huku akihisi kama vile macho yake yalikuwa yakimdanganya kwa msichana aliyekuwa mbele yake.

ENDELEA……………………………

Alikuwa akitazamana na msichana mwenye umbo dogo,mweupe na mwenye nywele ndefu nzuri na nyeusi.Msichana huyu alikuwa na macho mazuri ya kupendeza yaliyokuwa yamefunikwa na miwani mizuri iliyozidi kumfanya awe mrembo zaidi.Siku ya leo alikuwa amevaa koti refu la rangi nyeusi lililofika hadi mapajani na chini alivaa suruali nyeusi iliyomkaa vyema na kisha akamalizia na viatu virefu vyeusi.Koti lile lililoonekana la gharama kubwa lilikuwa limeachwa wazi hadi sehemu za chini ya kifua na kuifanya fulana nyeusi aliyokuwa ameivaa ndani kuonekana ikiwa imekifunika kifua cheupe na cha kupendeza kilichokuwa kinang’aa kwa cheni nzuri ya dhahabu.
“Nilitegemea Latoya angekuwa ni mama mtu mzima ,lakini kumbe ni binti mdogo tu kama huyu.She looks so pretty.Au ndiye huyu Latoya Bilionea ambaye niwahi kumsikia kwamba ana utajiri mkubwa lakini bado ni binti mdogo?” Akawaza Innocent
“Innocent karibu sana.Mimi naitwa Latoya na ndiye mmiliki wa taasisi hii yenye kuwasaidia wanawake wasiokuwa na uwezo kupata tiba za maradhi mbali mbali yanayowasumbua.Sabrina alinieleza kwamba una mgonjwa anayehitaji msaada wa figo?” Latoya akasema kwa sauti yake laini.
“Ni kweli Latoya .Nina mgonjwa wangu anaitwa Marina yuko hospitali kwa sasa na anahitaji kubadilishiwa figo.” Inno akasema
“Pole sana Innocent.Sasa umefikia wapi kuhusu kupata figo nyingine?? Latoya akauliza
“Mpaka sasa hivi bado sijafanikiwa kupata figo.Nilikuwa naelekea kuonana na mmoja wa rafiki zangu ambaye ni daktari ili nione kama anaweza kunisadia,lakini Sabrina akanipigia simu na kuniambia kwamba ameongea na wewe na umemwambia kwamba nije kuonana nawe.Kwa hiyo mpaka sasa hivi bado hiyo figo haijapatikana”
Latoya akatoa miwani yake akamtazama Innocent na kusema
“Baada ya Sabrina kunieleza niliguswa sana na nikamwambia akutaarifu uje hapa ili tuweze kushauriana nini tufanye kwa sababu kwa bahati mbaya ni kwamba hakuna mahala tunakoweza kununua figo.Inatakiwa apatikane mtu ambaye atakuwa tayari kujitolea figo hiyo kwa ajili ya Marina.Umeshajaribu kuongea na watu mbali mbali kama marafiki,ndugu na jamaa kuhusu mmoja wao kujitolea figo?
“Latoya ,labda kwa kukupa picha halisi ya msichana huyu ni kwamba Marina ni binti mdogo ambaye nilimkuta akifanya biashara ya ukahaba katika moja ya kumbi za burudani.Nilipomuona nilijikuta nikiguswa sana ,kwanza kwa umri wake na pili kwa ile biashara aliyokuwa akiifanya.Nilifanya jitihada za kuonana naye nikijifanya ni mteja ninayehitaji huduma ya ngono .Tulipokuwa hotelini nilimweleza kuhusu lengo langu la kutaka kumsaidia ili aweze kuondokana na maisha yale yasioendana na umri wake.Alinieleza historia yake.Ni mtoto asiyekuwa na wazazi wala ndugu yeyote hapa mjini.Ndugu yake pekee anayemfahamu alikuwa ni mama yake ambaye alifariki miaka kadhaa iliyopita hivyo kumfanya Marina kujiingiza katika biashara hii ya kuuza mwili ili aweze kuyaendesha maisha yake.Nilifika hadi mahala alikokuwa akiishi na wenzake.kwa kweli wanaishi maisha mabaya sana.Mwanzoni Marina alikuwa mgumu kukubali kubadilisha aina ya maisha anayoyaishi.Alikwisha kata tamaa na maisha yake.Siku ya pili tangu nimemfahamu nilipigiwa simu na mjumbe wa eneo analoishi Marina kwamba Marina pamoja na wenzake wawili wamekamatwa kwa wizi wa simu ,nilikwenda kumtoa polisi na kulipa vifaa vyote ambavyo yeye na wenzake walikuwa wakituhumiwa kuviiba.Matatizo yalianza baada ya kutoka polisi kwani alianza kuumwa sana ikanibidi kumpeleka hospitali akapata matibabu halafu nikampeleka nyumbani kwetu.Kule nyumbani kwetu mambo hayakuwa mazuri sana ,wazazi hawakupendezwa na kitendo cha mimi kumpeleka Marina akaishi pale.Siku iliyofuata nikiwa kazini nilipigiwa simu kwamba Marina ameondoka nyumbani.Nikaenda tena kumtafuta na kumkuta kule alikokuwa akiishi na wasichana wenzake.Nilimchukua na kumpeleka tena hospitali kwani hakuwa akijisikia vizuri.Baada ya uchunguzi ikagundulika kwamba ana matatizo ya figo kwa hiyo inabidi abadilishiwe figo nyingine.Jana jioni nilirudi naye tena nyumbani lakini ukatokea mtafaruku baina yangu na mama ambaye hakuwa akitaka Marina akae pale nyumbani.Niliumia sana kwa kitendo kile na hivyo ikanilazimu kuondoka nyumbani na kwenda kuchukua chumba katika hoteli.Usiku wa manane hali ya Marina ilibadilika ikanibidi nimkimbize hospitali ambako bado amelazwa hadi sasa.Kwa maana hiyo Marina ni mtu asiye na ndugu wala mtu wa karibu ambaye anaweza akamshughulikia au kuyajali matatizo yake.kwa sasa mtu pekee ambaye anaweza kumuita ndugu ni mimi . Marina anahitaji msaada mkubwa na wa haraka.Kama kuna lolote unaloweza kufanya ili kuaokoa maisha yake tafadhali naomba unisaidie” Innocent akasema.
Maneno yale ya Innocent yalionyesha kumchoma moyo Latoya ambaye alishindwa kujizuia na kutoa chozi.
“Pole sana Innocent kwa matatizo uliyonayo.Ni watu wachache sana wenye moyo wa huruma kama wa kwako.Mimi niliposikia kuhusu mgonjwa wako nikajua labda ni ndugu yako wa karibu au dada yako,lakini kumbe ni mtu ambaye hata humfahamu.Pole sana Inno.Siwezi kuelezea ni jinsi gani nilivyoguswa kwa tatizo hili hadi nimejikuta nikitoa machozi.Innocent taasisi yangu inajihusisha na kutatua matatizo mbali mbali ya wanawake wasiokuwa na msaada.Ninafahamiana na madaktari wengi na hospitali nyingi kubwa ndani na nje ya nchi.Ninachotaka kukifanya ni kufanya mawasiliano nao ili nione namna gani wanaweza wakanisaidia…” Akasema Latoya lakini kabla hajaendelea simu ya Innocent ikaita,akasogea pembeni na kuipokea.Baada ya maongezi yaliyochukua kama dakika mbili hivi sura ya Innocent ikabadilika ghafla.Akajishika kiuno.
“Innocent mbona umebadilika hivyo? Latoya akauliza
“Hospitali wamenipigia simu kwamba hali ya Marina imebadilika na kuwa mbaya zaidi.Latoya ngoja nikimbie nikamuangalie anaendeleaje.I cant let her die…..”
“sawa Innocent ,mimi ninaendelea kuwasiliana na watu mbali mbali ili nione watatusaidia vipi.Wahi hospitali mara moja na lolote nitakalolipata nitakutaarifu mara moja.Usife moyo Innocent tuko pamoja katika suala hili.Chukua hizi namba zangu za simu kwa mawasiliano.Nipigie simu kunifahamisha kuhusu hali ya mgonjwa” Latoya akasema na kwa haraka Innocent akatoka mle ofisini kwake.
Dakika arobaini zilimfikisha Innocent hospitali na moja kwa moja akafululiza hadi katika ofisi ya daktari mkuu ambako alifahamishwa kwamba hali ya Marina ilibadilika ghafla na tayari amehamishiwa katika chumba cha wagonjwa mahututi akisubiri kubadilishiwa figo ili kuokoa uhai wake.
Innocent akainua kichwa chake akatazama juu akafikiri kwa muda kisha akashusha pumzi ndefu,na kusema
“Daktari hatuwezi kumpoteza Marina kwa ukosefu wa figo.Nitajitolea figo yangu ili Marina apone” Daktari yule akainua kichwa na kumtazama Innocent asiamini kile alichokisikia.Ikambidi amuulize tena kama alimaanisha alichokiongea.Innocent akasisistiza kwamba figo yake moja itolewe na awekewe Marina ili waweze kuokoa uhai wake.Daktari akatoka mle ofisini na kwenda kuwataarifu madaktari wenzake juu ya uamuzi ule wa Inno na kuanza maandalizi ya kuifanya operesheni ile mara moja.Innocent alikuwa amekaa katika sofa la mle ofisini kwa daktari mkuu akiomba Mungu kimoyo moyo na baada ya nusu saa daktari akarejea na kumtaka waongozane.Kabla hajatoka mle ofisini Innocent akakumbuka kitu.Akaitoa simu yake mfukoni na kubonyeza namba za simu za Latoya akampigia.
“Latoya naomba usiendelee tena kutafuta ile figo.Hali ya Marina inaendelea kuwa mbaya kwa hiyo hatutakuwa na muda mwingi wa kusubiri figo hiyo ipatikane.Nimeamua kujitolea mimi mwenyewe figo yangu ili kuokoa uhai wa Marina.Nashukuru sana kwa msaada wako na samahani kwa usumbufu niliokusababishia”
Latoya akavuta pumzi ndefu na kusema
“Innocent nashukuru kama umeamua wewe mwenyewe kujitolea figo kwa ajili ya Marina.Naomba ufute kabisa wazo kwamba umenisumbua.Hukunisumbua kitu chochote na niliamua kujitolea kwa moyo wangu wote kusaidiana nawe katika tatizo hili.Innocent nakosa maneno ya kusema kwa sababu sijawahi kukutana na kijana mwenye roho ya huruma kama ya kwako.Kutokana na umuhimu wa suala hili naahirisha shughuli zangu zote na ninakuja huko hospitali kuungana nawe.Innocent tuko pamoja katika hili.” Latoya akaongea kwa sauti ya upole yenye kuonyesha uchungu ndani yake
“Nashukuru sana Latoya kwa kunipa moyo.Tafadhali naomba umtaarifu na Sabrina ili afahamu kinachoendelea Kwa sasa.yeye na Grace ndio watu pekee ambao naweza kusema kwamba ni familia yangu iliyobaki baada ya familia yangu kunitenga.Latoya I need to go now.See you later” Innocent akakata simu na kuizima kabisa kisha akaongozana na madkatari wawili waliokuwa wakimsubiri amalize kuongea na simu akapelekwa moja kwa moja hadi katika chumba maalum akatoa mavazi yake na kuvishwa mavazi mengine ya hospitali kisha akaingizwa katika chumba kimoja chenye mitambo mingi akalazwa juu ya kitanda.Mashine moja iliyokuwa juu ikaanza kushuka taratibu huku wale madaktari wakiangalia katika luninga zilizokuwemo mle ndani.mashine ile ikashuka hadi karibu kabisa na tumbo na kisha ikawaka taa.Dakika kumi baadae mwanga ule ukazima na mashine ile ikarudi tena juu.madkatari wakajadiliana na wakaendelea kuchunguza mambo mengine kama vile damu n.k.
“Innocent tumeliangalia figo lako na kuona linafaa kuwekwa kwa Marina kwa hiyo kama bado haujabadili mawazo tunaanza kufanya maandalizi ya operesheni hii ya figo.”
“Thank you God.Nilikuwa na wasi wasi sana kama figo yangu ingeonekana haifai kuwekewa Marina.Daktari nimedhamiria kuokoa maisha ya Marina kwa hiyo tusipoteze wakati,mimi niko tayari kwa operesheni hiyo.” Innocent akasema
Madkatari wale wakaondoka katika chumba kile na kumuacha Innocent pale kitandani.Baada ya dakika kumi na tano akaingia muuguzi wa kike na kumuomba Innocent apande juu ya kitanda cha magurudumu kwa ajili ya kupelekwa katika chumba cha upasuaji.Huku akitabasamu Innocent akapanda juu ya kile kitanda cha magurudumu halafu muuguzi akaanza kukisukuma na kutoka ndani ya kile chumba.Moja kwa moja akapelekwa hadi katika mlango wa chumba cha upasuaji.Mlango ukafunguliwa na akaingizwa ndani.Katika chumba cha kwanza ambacho hakikuwa na vitu vingi akatokea daktari mmoja ambaye akamtazama na kumwambia.
“Innocent upasuaji tunaoenda kuufanya ni mkubwa na kabla hatujakuingiza katika chumba cha upasuaji ,una mtu yeyote ambaye ungependa kuwasiliana naye?
Inno akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
“Nashukuru daktari lakini watu wangu wa muhimu tayari nimekwisha wasiliana nao.Mnaweza kuendelea na taratibu za upasuaji Innocent akasema na kisha daktari akaruhusu aingizwe katika chumba cha upasuaji.


TUKUTANE SEHEMU IJAYO
 
BEFORE I DIE
SEHEMU YA 19
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Madkatari wale wakaondoka katika chumba kile na kumuacha Innocent pale kitandani.Baada ya dakika kumi na tano akaingia muuguzi wa kike na kumuomba Innocent apande juu ya kitanda cha magurudumu kwa ajili ya kupelekwa katika chumba cha upasuaji.Huku akitabasamu Innocent akapanda juu ya kile kitanda cha magurudumu halafu muuguzi akaanza kukisukuma na kutoka ndani ya kile chumba.Moja kwa moja akapelekwa hadi katika mlango wa chumba cha upasuaji.Mlango ukafunguliwa na akaingizwa ndani.Katika chumba cha kwanza ambacho hakikuwa na vitu vingi akatokea daktari mmoja ambaye akamtazama na kumwambia.
“Innocent upasuaji tunaoenda kuufanya ni mkubwa na kabla hatujakuingiza katika chumba cha upasuaji ,una mtu yeyote ambaye ungependa kuwasiliana naye?
Inno akafikiri kwa sekunde kadhaa na kusema
“Nashukuru daktari lakini watu wangu wa muhimu tayari nimekwisha wasiliana nao.Mnaweza kuendelea na taratibu za upasuaji Innocent akasema na kisha daktari akaruhusu aingizwe katika chumba cha upasuaji.

ENDELEA……………………………..

Mara tu baada ya kumaliza kuongea na Innocent Latoya akajikuta amekaa juu ya meza.Alihisi baridi ya ghafla.
“Innocent ni kijana wa ajabu sana.Yaani kwa ajili ya kuokoa uhai wa Marina ameamua kujitolea figo yake mwenyewe? Sijawahi kukutana na kijana mwenye roho ya huruma kama yake.” Latoya akawaza huku akiifungua pochi yake kubwa na ghafla akatulia na kuanza kuwaza tena.
“Mbona nimeanza kuogopa ghafla namna hii? Nahisi mwili wote kunitetemeka.Namuonea huruma Innocent.Amejitolea kitu kikubwa sana kwa ajili ya kuokoa maisha ya msichana ambaye hana undugu naye wowote .Katika operesheni lolote linaweza kutokea.No ! Nothing bad is going to happen to him.He’s going to be ok .I must be there now.Ngoja niwahi hospitali ili nipate kuongea na Innocent walau maneno machache kabla hajaingizwa katika chumba cha upasuaji” Latoya akawaza huku akiifunga pochi yake kubwa na kumpigia simu msaidizi wake kumtaarifu kwamba amepata dharura kwa hiyo hatakuwepo kwa siku hiyo.Kwa haraka Latoya akatoka na kumchukua Sabrina kisha wakaingia garini na kuelekea moja kwa moja hospitali
“Dada latoya una uhakika Innocent atakuwa mzima hata baada ya operesheni? Atakuwa katika hali yake ya kawaida baada ya kutolewa figo moja? Sabrina akauliza huu ameikunja mikono yake na kuiweka pamoja kifuani
“Sabrina usiwe na wasi wasi.Innocent atakuwa mzima.Operesheni kubwa kama hizi huwa zinafanywa na madaktari wataalamu sana kwa hiyo usiwe na wasi wasi wowote.Ninawaamini madaktari wa hospitali ile.Vile vile Innocent atakuwa katika hali yake ya kawaida hata baada ya operesheni kwa sababu mtu unaweza ukaishi ukiwa na figo moja bila matatizo.” Latoya akajibu
“Naogopa sana dada Latoya.Nina wasi wasi sana.Sitaki Innocent apate matatizo yoyote kwa sababu ni ndugu yangu pekee ninayemtambua kwa sasa.Ni yeye pekee ambaye alisimama na kunipigania hadi leo hii ninafanya kazi katika taasisi yako.” Sabrina akasema na kwa mbali machozi yakaanza kumchuruzika.Latoya akamtazama na kusema
“ Usilie Sabrina.Tunatakiwa tusimame imara kwa ajili ya Innocent.We have to be strong for him so stop crying”
Sabrina akatoa kitambaa na kujifuta kisha akachukua simu yake na kumpigia Grace.
“hallo Grace uko wapi sasa hivi?
“niko nyumbani najiandaa kwa ajili ya kuelekea chuoni” Grace akajibu
“Grace kuna tatizo limetokea”
“tatizo gani hilo” Grace akauliza kwa wasi wasi
“Ni kuhusu Innocent.”
“Innocent !! kafanya nini tena?
“Innocent ameamua kutoa figo yake moja kwa ajili ya kuokoa uhai wa Marina.Hivi tunavyoongea wanajiandaa kumuingiza katika chumba cha upasuaji.Mimi na dada Latoya tunaelekea huko kwa hiyo kama una nafasi nakuomba nawe ufike hospitali mara moja.Nadhani unafahamu ni namna gani Innocent alivyo mtu muhimu kwetu.”
Huku sauti yake ikionyesha mstuko wa dhahiri Grace akajibu.
“nakuja sasa hivi huko hospitali”
“Huyo Grace ni ndugu yako?” Latoya akamuuliza Sabrina baada ya kumaliza kuongea na Grace simuni.
“Grace ni msichana ambaye kwa pamoja tuko mahala tulipo kwa jitihada za Innocent.Sote tunaishi nyumbani kwao na ni Innocent aliyetusaidia mpaka tukafika hapa tulipo” Sabrina akasema na kumfanya Latoya azidi kuwa na mawazo mengi.
“Hivi huyu Innocent ni kijana mwenye moyo wa namna gani? Kwa mujibu wa maelezo aliyonipa Sabrina ni kwamba anamuheshimu Innocent kupita hata baba yake mzazi.Anasema mambo aliyomfanyia Innocent haoni hata ni neno gani alitumie kumshukuru.Si hawa wasichana wawili tu , anasema kwamba Innocent amekuwa akiwasaidia wau wengi pia.Innocent anaanza kunigusa sana.Sielewi ni kwa nini nimeguswa ghafla hivi wakati nimeonana naye kwa siku moja tu.Ninahitaji kumfahamu kijana huyu kwa undani wake.Kwa mbali ninaanza kuwa na mawazo kwamba labda ile ndoto yangu imeanza kutimia.May be Innocent is the one “ akawaza Latoya akastuliwa na simu yake iliyokuwa ikiita.Akaichukua akaangalia mpigaji akaamua kuizima kabisa.
“Sihitaji kuwasiliana na mtu yeyote muda kama huu.Akili yangu inawaza kitu kimoja tu Innocent atoke ndani ya chumba cha upasuaji mzima” Latoya akaongea huku sura yake ikionyesha alikuwa na mawazo mengi.Akageuka na kumtazama Sabrina
“Sabrina huyo Marina ulifanikiwa kumuona?
“Ndiyo nilimuona.Ni mimi ndiye nilikuwa nikimuhudumua Innocet alipomleta pale nyumbani.” Sabrina akajibu
“Unaweza ukamuelezeaje Marina? Latoya akauliza tena
“Ni msichana mdogo lakini aliyepitia shida nyingi kutokana na aina ya maisha anayoyaishi.Ukikaa na kuongea naye ni msichana jasiri sana lakini anaonekana kukata tamaa na kuridhika na maisha anayoyaishi sasa”
“Is she pretty” Latoya akauliza na kumfanya Sabrina atabasamu
“kwa kweli napenda nikiri kwamba Marina ni binti mzuri ingawa kutokana na maisha yake ule uzuri wake wa asili umeanza kujificha lakini ni binti mzuri.Kwa nini umeuliza hivyo?”
“Nimeuliza hivyo ili kufahamu ni kitu gani kimepelekea hadi Innocent akubali kufanya alivyofanya.Kumtolea figo mu ambaye humfahamu na huna mahusnao naye yoyote si suala rahisi sana lakini Innocent ameweza kufanya hivyo”
“dada Latoya kaka Innocent ndivyo alivyo.Katika maisha yake hapendi kuona mtu akiteseka.Yuko tayari kwa lolote ili kumsaidia mtu yeyote mwenye uhitaji”
Latoya na Sabrina wakawasili hospitali na moja kwa moja wakaulizia mapokezi kama tayari Innocent ameingizwa katika chumba cha upasuaji wakajibiwa kwamba bado alikuwa akiandaliwa.Kwa kasi ya ajabu wakaelekea katika chumba cha upasuaji.Wakafika katika mlango wa kuingilia chumba cha upasuaji na kugonga kisha ukafunguliwa na muuguzi aliyekuwa amevaa mavazi ya kijani.
“Dada tunaomba utusaidie.Kuna kaka mmoja anatarajia kufanyiwa upasuaji wa figo mchana huu sisi ni ndugu zake na tumekuja ili walau kuongea naye kabla hajaingizwa katika chumba cha upasuaji” Latoya akasema huku moyo ukimwenda mbio
“samahani dada zangu.mmechelewa kidogo sana kama dakika mbili zilizopita Innocent ameingizwa katika chumba cha upasuaji ambako si rahisi kwa mtu asiye daktari kuingia.Itawabidi mkae hapa msubiri hadi opresheni itakapokwisha” Muuguzi yule akawataarifu akina Latoya ambao walionyesha kuishiwa nguvu na majibu yale.Taratibu wakajivuta na kukaa katika sofa kubwa jeusi lililokuwa hapo nje ya chumba cha upasuaji.
Kila mmoja alionekana kuwa na mawazo mengi .Latoya alikuwa ameinama huku amekiegemeza kichwa katika mikono yake.Dakika kama kumi hivi toka wamewasili pale hospitali mara wakatokea Grace na mama yake Innocent
“Grace Innocent yuko wapi? Akauliza mama yake Innocent huku akihema
“Mama tayari amekwisha ingizwa katika chumba cha upasuaji na si rahisi kuonana naye kwa sasa.Tumeambiwa tusubiri hapa hapa nje hadi operesheni itakapomalizika baada ya masaa matatu.” Mama yake Wayne akainua mikono yake na kukishika kichwa .
“Jamani hivi huyu Wayne amepatwa na nini hadi anaamua kufanya mambo ya hatari kama haya? “ Akalalama mama yake Wayne.Latoya ambaye muda wote alikuwa amekaa kimya akamtazama kwa macho makali.Muda huo huo baba yake Wayne akatokea.
“Hebu niambieni nini kinaendelea hapa? Akahoji mzee Benard baba yake Innocent huku jasho likimtiririka.
“Innocent tayari ameingizwa katika chumba cha upasuaji.” Mke wake akasema huku kwa mbali akitokwa na machozi.Jibu lile likamfanya mzee Benard kukaa kimya na kujitenga pembeni akiwa na mawazo mengi.Wakati kila mmoja akiwa kimya akiwaza lake mara kwa kasi akapitishwa msichana mmoja na kuingizwa katika chumba kile cha upasuaji.Alikuwa ni Marina.Sabrina akamsogelea Latoya na kumnong’oneza.
“Huyo msichana aliyepitishwa hapa ndiye Marina.” Latoya hakujibu kitu zaidi ya kutikisa kichwa chake.Akiwa ameinamisha kichwa akiwaza akastuliwa na sauti iliyomuita.Akainua kichwa na kutazama mtu aliyemuita akakutanisha macho na Dr.Rajiv Patel mkurugenzi wa hospitali hii aliyekuwa akimuangalia kwa mshangao.Hakuamini macho yake kwa kumuona Latoya maeneo yale.
“Dr Rajiv “ Latoya akasema na kuinuka wakapeana mikono.Daktari Yule alikuwa akimuangalia Latoya kana kwamba ameona malaika.Hakuyaamini macho yake
“Latoya mbona uko hapa? Kuna tatizo gani? Una mgonjwa humu ndani? akauliza Dr Rajiv huku mikono ikimtetemeka.
“Ndiyo Rajiv,kuna rafiki yangu anafanyiwa upasuaji sasa hivi”
“Ni huyu kijana anayefanyanyiwa upasuaji wa figo?
“Ndiye huyo huyo”
“Latoya kwa nini hukunitaarifu kama una mgonjwa hapa hospitali? Ulipaswa kunitaarifu ili nijue kama yule ni mgonjwa wako.Karibu basi ukapumzike kule sehemu ya V.I.P. wakati ukisubiri operesheni imalizike.Operesheni hii itachukua si chini ya saa tatu” Dr Rajiv akasema
“Nashukuru sana Dr Rajiv lakini naona ni bora kama nikikaa hapa ili kusubiri operesheni hiyo imalizike.” Latoya akasema
“Naelewa Latoya lakini mtu kama wewe hutakiwi kukaa sehemu kama hii.Tuna sehemu maalum kwa ajili ya kupumzika watu kama ninyi.Sehemu nzuri na yenye usalama wa kutosha. ” Dr Rajiv akasisitiza na kumfanya Latoya atabasamu.
“Dr Rajiv ningependa sana kuelekea huko lakini naona ingekuwa vyema kama nikikaa hapa hadi operesheni itakapokamilika.Ahsante sana Dr Rajiv kwa ukarimu wako.” Akasema Latoya
“ Latoya wewe ni mtu muhimu sana kwetu unastahili huduma za kipekee kabisa.Nasikitika sana kwa kutofahamu kama ulikuwa hapa muda mrefu.Kama haujisikii kwenda kukaa kule V.I P basi ngoja niwatume wahudumu walete meza hapa waweke pale pembeni ili uendelee kupumzika wakati operesheni ikiendelea.”
“ Ahsante sana Dr Rajiv.Naomba usisumbuke mimi hapa pananitosha sana “.akasema Latoya .
Dr Rajiv alionekana kutoridhishwa kabisa na kitendo cha Latoya kukaa pale nje ya chumba cha upasuaji.Kwa shingo upande akaagana na Latoya kwa ahadi ya kuonana naye baada ya muda mfupi kwani alitakiwa kuhudhuria kikao muhimu sana.Alipopiga hatua mbili akageuka na kuuliza .
“ Walinzi wako wako wapi? Akauliza Dr Rajiv .Huku akitabasamu Latoya akajibu
“ Leo nimeamua kutembea mwenyewe bila ulinzi wowote”
Kitendo cha Latoya kunyenyekewa namna ile na mkurugenzi wa hospitali ile kiliwashangaza sana wazazi wa Innocent.Kila mmoja alikuwa akijiuliza huyu msichana ni nani? Swali hilo likawafanya wamwite Grace na kumuuliza kama anamfahamu Latoya.
“Yule anaitwa Latoya ndiye aliyempa kazi Sabrina.Ana taasisi yake ya kuwasaidia wanawake na watu wenye matatizo mbali mbali nadhani ni rafiki wa Innocent ndiyo maana yuko hapa sasa hivi”
“Kumbe Innocent ana marafiki wazuri kama huyu sasa kwa nini apoteze muda na hatimaye ahatarishe maisha yake kwa ajili ya wasichana machangudoa wasiokuwa na msaada wowote kwake? Mzee Benard akauliza huku ameikunja sura
“Huyu niliyekuwa naongea naye ndiye mkurugenzi wa hospitali hii anaitwa Dr Rajiv Patel.” Latoya akamwambia Sabrina baada ya Dr Rajiv kuondoka.
“Inaonekana anakufahamu sana” Sabrina akasema
“Tunafahamiana sana kwa sababu huwa ananisaidia pindi ninapokuwa na wagonjwa wa kuwapeleka nje ya nchi.Ni rafiki yangu sana” Latoya akasema kisha kimya kidogo kikapita halafu akauliza
“Sabrina umeishi na Innocent kwa muda sasa,unaweza ukanieleza kwa undani ni mtu mwenye tabia zipi?
“dada Latoya nashindwa hata nikuelezee vipi kuhusu Innocent kwa sababu maelezo yake ni mengi sana.Naomba tukitoka hapa unikumbushe nitakueleza mambo mengi kuhusiana naye.Naogopa kuongea hapa mbele ya wazazi wake.Mama yake hatupendi sana mimi na Grace na ni yeye ndiye aliyesababisha Innocent aamue kuondoka pale nyumbani” Sabrina akasema kwa sauti ndogo.Ni wazi alikuwa akiwaogopa wazazi wa Innocent.
Dakika arobaini zilikatika wakiwa bado wako pale nje ya chumba cha upasuaji .Kila mmoja akiwa kimya akiwaza lake,mara milango ikafunguliwa na wauguzi wakatoka wakikisukuma kitanda kilichokuwa kimefunikwa shuka.Wote walikuwa na nyuso za huzuni.Nyuma yao alikuwepo daktari mmoja ambaye alikuwa na mavazi yake ya kijani akawafuata akina Grace ambao walikuwa wamesimama kwa wasi wasi baada ya kuona kitanda kile kikitolewa mle ndani

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
BEFORE I DIE
SEHEMU YA 20
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
“Sabrina umeishi na Innocent kwa muda sasa,unaweza ukanieleza kwa undani ni mtu mwenye tabia zipi?
“dada Latoya nashindwa hata nikuelezee vipi kuhusu Innocent kwa sababu maelezo yake ni mengi sana.Naomba tukitoka hapa unikumbushe nitakueleza mambo mengi kuhusiana naye.Naogopa kuongea hapa mbele ya wazazi wake.Mama yake hatupendi sana mimi na Grace na ni yeye ndiye aliyesababisha Innocent aamue kuondoka pale nyumbani” Sabrina akasema kwa sauti ndogo.Ni wazi alikuwa akiwaogopa wazazi wa Innocent.
Dakika arobaini zilikatika wakiwa bado wako pale nje ya chumba cha upasuaji .Kila mmoja akiwa kimya akiwaza lake,mara milango ikafunguliwa na wauguzi wakatoka wakikisukuma kitanda kilichokuwa kimefunikwa shuka.Wote walikuwa na nyuso za huzuni.Nyuma yao alikuwepo daktari mmoja ambaye alikuwa na mavazi yake ya kijani akawafuata akina Grace ambao walikuwa wamesimama kwa wasi wasi baada ya kuona kitanda kile kikitolewa mle ndani

ENDELEA………………………………..

“dada ninyi ndiye ndugu zake na Innocent na Marina? Daktari yule akawauliza akina Grace .
“Ndiye sisi” wote wakajibu kwa wasi wasi.
“ Samahani sana….” Kabla hajaendelea baba yake Innocent akadakia kwa sauti kubwa.
“Daktari nini kimetokea?
Daktari yule akawatazama akapatwa na kigugumizi cha kuongea.
“Daktari naomba tafadhali utuambie nini kimetokea huko ndani? Baba yake Innocent akasisitiza.
Daktari akakohoa kidogo na kusema
“Nasikitika sana kuwataarifu kwamba operesheni imeshindwa kufanyika kwa sababu yule msichana amefariki dunia.Marina amefariki dunia.Poleni sana” Wote wakabaki kimya nyuso zimewabadilika.
“Daktari vipi kuhusu Innocent? mama yake Inno akauliza
“Innocent ni mzima wa afya .Ila tayari alikuwa ameshachomwa sindano ya usingizi tayari kwa operesheni kwa hiyo itamchukua muda wa kama saa tatu hivi kuamka.” Akasema daktari. na kuondoka zake kwenda kuendelea na shughuli nyingine.Simanzi kubwa ikatawala eneo lile.Kila daktari aliyekuwa akitoka katika kile chumba cha upasaji alikuwa akiwapa pole familia ya Innocent.Kila mmoja aliamini kwamba Marina alikuwa ni sehemu ya familia ile .
Latoya akajitenga pembeni akajificha katika mti wa maua akatoa miwani yake na kufuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.
“I’m so sorry Innocent.Juhudi zote za kuokoa maisha ya Marina zimeshindikana.Ulipigana kufa na kupona lakini hayakuwa mapenzi ya Mungu apone.Masikini Marina upumzike kwa amani huko uliko.Umefariki bado msichana mdogo sana.Najua huko uliko sasa hivi unaziona juhudi zote alizozifanya Innocent katika kuyaokoa maisha yako .” Latoya akawaza huku akiyafuta machozi.
“ Kitendo cha Innocent kupambana hadi dakika ya mwisho kupigania uhai wa Marina kimeamsha kitu kipya moyoni mwangu.Innocent ameonyesha upendo mkubwa sana kwa binti huyu masikini.Amenifundisha namna ya kujishusha na kujiweka chini ya wale walio masikini kabisa.Innocent amenifundisha ushujaa.Kuanzia sasa sipaswi kukata tamaa tena.Nitapambana hadi dakika ya mwisho.Nina kila sababu ya kuamini kwamba ile ahadi niliyoiweka kuitimiza kabla sijafa iko njiani kutimia muda si mrefu.Naziona kila dalili za kutimia kwa ahadi yangu..Innoc………”
Ghafla Latoya akastuliwa na sauti ya Sabrina.
“dada latoya mbona umejificha huku peke yako?
“Nimepatwa na uchungu sana Grace kwa kifo cha Marina.Nasikia uchungu kwa sababu juhudi zote alizozifanya Innocent hazijafanikiwa.Kinachonisikitisha zaidi ni kwamba Marina amefariki akiwa bado binti mdogo.Hakuweza kuzitimiza ndoto zake alizokuwa nazo maishani.Ningemfahamu Innocent toka mapema tungeweza kuyaokoa maisha ya binti huyu.Nimefahamiana na Innocent dakika za mwisho za uhai wa Marina na hivyo hakukuwa na njia nyingine ya kuweza kumsaidia…” Latoya akasema kwa uchungu Sabrina akamsogelea na kumshika mabegani
“dada latoya kweli inauma sana lakini yote haya ni mapenzi ya Mungu.Kila kilichokuwa kikihitajika kufanyika ili kuokoa uhai wa Marina kilifanyika lakini ikawa hivyo ilivyotokea.”
“Kweli Sabrina .Namuonea huruma sana Innocent .Atakapoamka na kusikia kwamba Marina amefariki dunia atakuwa katika wakati mgumu sana.”
“Ni kweli atakuwa katika wakati mgumu lakini atapata faraja akiamka na kukuta sisi tupo pembeni yake.”Sabrina akasema
Kimya kidogo kikapita halafu Latoya akauliza
“Sabrina naomba nikuulize kitu.”
“Uliza tu dada Latoya”
“Umekuwa ni mtu wa karibu sana na Innocent.Amewahi hata siku moja kukueleza kwamba ana mchumba? Au hata siku moja umewahi kumuoana akiwa na rafiki yake wa kike?
Pamoja na majonzi yaliyowatawala ,Sabrina akatabasamu na kusema
“dada latoya kusema ukweli hata siku moja Innocent hajawahi kunieleza kama ana mchumba na wala hajawahi kunieleza kama ana rafiki wa kike.Toka amerudi mimi nimekuwa ni rafiki yake mkubwa na mambo yake mengi huwa ananieleza bila kunificha.Kila arudipo toka kazini lazima atutafute mimi na Grace na kutujulia hali na kama ana tatizo huwa ananieleza.Kama angekuwa na rafiki wa kike angekwisha nieleza.Lakini kuna kitu nilikiona cha tofauti wakati alipokutana na Marina.Alionyesha dalili za kuvutiwa na binti yule.Nilihisi hivyo japokuwa sikupata nafasi ya kumuuliza.”
Jibu lile la Sabrina linamfanya Latoya anyamaze na afikiri kidogo
“Kwa nini umeuliza hivyo dada Latoya? Grace akauliza
“Nimetaka kufahamu kama ana mchumba ili tumtafute na kumpatia taarifa.Unajua kwa tukio kama hili mchumba wake lazima afahamu.Kama hana mchumba basi haina shida.” akasema Latoya halafu akazama katika mawazo ghafla.
“Ouh My God ! please assure me if Innocent is the one I’ve been waiting for.I need to know if I’ve met the one I asked you to give me before I die” Latoya akawaza huku akiendelea kuyafuta machozi yaliyokuwa yakiendelea kutiririka.Ghafla katika mlango wa kuingilia chumba cha upasuaji kikatoka kitanda kikisumwa .Wazazi wa Innocent pamoja na Grace wakakisogelea na hivyo kuwafanya akina Latoya waliokuwa mbali kidogo nao kusogelea pale kwa haraka.Innocent alikuwa akitolewa katika chumba cha upasuaji na kupelekwa katika chumba maalum kupumzishwa wakati wakisubiri arejewe na fahamu zake.
“Sabrina kuna jambo ambalo ningependa kukuuliza tena” Latoya akasema wakati wakitembea kuelekea katika chumba alichokuwa anapelekwa Innocent kwa mapumziko.
“Uliza dada Latoya”
“Nakumbuka ulinidokeza kwamba Innocent alikuwa amekwaruzana na wazazi wake kuhusiana na Marina na hivyo kumlazimu aondoke nyumbani kwao.Unadhani wazazi wake wanaweza wakakubali shughuli za msiba zikafanyika hapo nyumbani kwao kwa sababu kwa mujibu wa Innocent Marina hakuwa na ndugu yeyote hapa mjini?
Sabrina akainama akafikiri na kusema.
“dada Latoya sina hakika kama wazazi wa Innocent wanaweza wakakubali msiba wa Marina uwekwe pale kwao.Sidhani kama Innocent mwenyewe atakubali kuupeleka msiba wa Marina nyumbani kwao.Kibaya zaidi ni kwamba Marina hakuwa na ndugu yeyote yule hapa mjini kwa hiyo Innocent ndiye pekee mwenye mamlaka na nini kifanyike kuhusiana na msiba huu”
“Too bad” Latoya akasema kwa masikitiko
“kama hali iko hivyo mimi nashauri kitu kimoja.Msiba huu tuupeleke nyumbani kwangu.nitagharamia kila kitu kuhusiana na msiba huu.Nadhani Innocent hatakuwa na kipingamizi katika hili”
“Hilo ni wazo zuri sana dada Latoya.Utakuwa umefanya jambo kubwa sana kwa sababu Innocent bado hana nyumba yake mwenyewe ambayo shughuli za msiba zingefanyika. “
“Sabrina naomba umwite na Grace ili tulijadili suala hili kwa pamoja” Latoya akasema na Sabrina akamwita Grace ambaye alikuja kwa haraka.
“Grace kuna suala tumekuwa tukijiuliza mimi na Sabrina.Kama wote tunavyofahamu kwamba Marina hakuwa na ndugu hapa mjini,na Innocent ndiye mtu pekee ambaye alikuwa akimchukulia kama ndugu yake.Tulikuwa tukijiuliza kama wazazi wa Innocent watakubali msiba wa Marina ufanyike nymbani kwao?”
Grace akamtazama Latoya na kusema
“kwa hilo sidhani kama litawezekana kwa sababu nimewasikia wakijadiliana kwamba mara tu Innocent atakapozinduka basi awaonyeshe walipo ndugu zake Marina ili watafutwe na wakabidhiwe maiti ya mtoto wako.Suala la msiba kufanyikia pale kwenye nyumba yao litakuwa gumu sana kwa sababu toka mwanzo hawakumkubali Marina akae pale na hiyo ndiyo sababu iliyopelekea Innocent aamue kuondoka pale nyumbani.”
“Nimekuelewa Garce.Kuna jambo nimemwambia Sabrina hapa na nikaona itakuwa vizuri kama na wewe ukifahamu ili kwa pamoja tulifanyie maamuzi.Sabrina na Grace napenda niwataarifu kwamba kabla ya kuingia katika chumba cha upasuaji niliongea na Innocent.Alinipigia simu kunitaarifu kwamba nisitishe lile zoezi la kutafuta figo kwani hali ya Marina haikuwa nzuri na kwa hiyo ilihitajika operesheni ya haraka kwa hiyo akaamua kujitolea figo yake yeye mwenyewe.Mwishoni mwa maongezi yetu aliniambia kwamba niwataarifu Sabrina na Grace kilichotokea kwa sababu ninyi ndiye ndugu zake pekee anayewafahamu kwa sasa.Kauli ile inathibitisha ni jinsi gani Innocent anavyowapenda na kuwathamini kwa hiyo chochote mtakachokiamua atakikubali.Nimemweleza sabrina kwamba kama kwa akina Inno kutakuwa na kizingiti kuhusiana na shughuli za msiba wa Marina basi ninajitolea nyumba yangu itumike kwa shughuli hizo na nitagharamia shughuli zote za mazishi.”
“Wazo zuri sana hilo dada Latoya.Nina imani hata Innocent ataliunga mkono.” Grace akasema
“kama tumekubaliana wote iwe hivyo ,basi mimi nianze maandalizi mapema iwezekanavyo..Kuna kampuni ya rafiki yangu mmoja nitaikodisha ili isimamie shughuli yote ya msiba huu.”
“ahsante sana dada latoya .Utakuwa umemsaidia sana Innocent” Sabrina na Grace wakasema kwa pamoja.
“Je kuna haja ya kuwataarifu wazazi wake kuhusiana na hili? Latoya akauliza
“dadaLatoya sidhani kama litakuwa ni jambo la busara kuwashirikisha wazazi wake kwa sababu toka mwanzo hawakuwa wamemkubali Marina kwa hiyo naamni hata Innocent asingependa kuwashirikisha katika suala la msiba.” Grace akasema
Bila kupoteza muda Latoya akachukua simu yake na kuanza kuwapigia simu watu mbali mbali akiwafahamisha kuhusiana na msiba ule.Akatoa malekezo kadhaa juu ya maandalizi ya msiba ule ambao alitaka ufanyike nyumbani kwake.

TUKUTANE SEHEMU IJAYO…
 
Speed inaridhiaha Mkuu Lege, with time watu wataelewa Utamu uliojificha ndani ya Hii story, bado ni mapema sana kama ni siku ndio kwanza kumekucha, kutapopambazuka vizuri (srory ikichanganyia) wataelewa
 
Speed inaridhiaha Mkuu Lege, with time watu wataelewa Utamu uliojificha ndani ya Hii story, bado ni mapema sana kama ni siku ndio kwanza kumekucha, kutapopambazuka vizuri (srory ikichanganyia) wataelewa
kama wanakuwa wepesi wa kuikadilia story basi story za hussen TUWA hawawezi kuzisoma kabisaa .maana mwanzo wake huwa na utata sana na sintofaham nyingi sana story huwa inaanzia mwisho na kurudi mwanzo
 
kama wanakuwa wepesi wa kuikadilia story basi story za hussen TUWA hawawezi kuzisoma kabisaa .maana mwanzo wake huwa na utata sana na sintofaham nyingi sana story huwa inaanzia mwisho na kurudi mwanzo
Hakika baada ya Kizazi cha kina Elvis Musiba, napenda kukiri Hussein Tuwa amevivaa Viatu Vya kina Elvis na Vimemtosha na Pengine muda si mrefu Vitaanza Kumbana.....
 
Hakika baada ya Kizazi cha kina Elvis Musiba, napenda kukiri Hussein Tuwa amevivaa Viatu Vya kina Elvis na Vimemtosha na Pengine muda si mrefu Vitaanza Kumbana.....
hahaha ni kweli kabisa mkuu jamaa uandishi wake upo makini sana na huwa unawachezea sana akili wasomaji wake ukisoma story yake lazima ikuteke haswaa?? kuna story yake ya MTUHUMIWA usha wahi isoma?
 
hahaha ni kweli kabisa mkuu jamaa uandishi wake upo makini sana na huwa unawachezea sana akili wasomaji wake ukisoma story yake lazima ikuteke haswaa?? kuna story yake ya MTUHUMIWA usha wahi isoma?
Taabu sana kuipata Kaka, ila naomba kama kuna mahali hapa Dar naweza pata vitabu vyake unielekeze, nipate Copy zangu
 
Taabu sana kuipata Kaka, ila naomba kama kuna mahali hapa Dar naweza pata vitabu vyake unielekeze, nipate Copy zangu
namba hiyo ni ya muuzaji wa dukani kwake pale kinondoni 0655428085 vitabu vyake vyote utavipata hapo mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom