BBC : Wasikilizaji Afrika wawaona viongozi kinyaa

mwalimu Jr.

Member
Aug 20, 2008
51
4
WAKATI kiongozi mmoja wa Afrika anawatetea viongozi wenzake wa Afrika kwamba eti sio wezi wala mafisadi wala wala rushwa Shirika la Habari la Utangazaji likiendesha kipindi wazi cha maingiliano na wasikilizaji wake kwa kutumia batua pepe na UJumbe mfupi umeonesha maoni tofauti kabisa.

Asilimia 100 ya wote waliotuma ujumbe kuhusu nini maoni yao juu ya viongozi wao imeonesha kwamba viongozi wao ni uozo tena uoza wa kutupwa.

Pamoja na kuchukua dakika takriban 10 kutafuta ujumbe wowote uliokuwa sio 'negative' kuhusu viongozi wa Kiafrika hakuna mafanikio yoyote yaliyopatikana.

Wasikilizaji wa kipindi cha Network Africa wameonesha kuchoshwa na kukata tamaa kabisa kuhusu uwezo wa viongozi wao wa kuwaletea maisha bora wakati wa uhai wao. Baadhi yao wamesema:
. Viongozi wamekithiri kwa ubinafsi na kutanguliza nafsi zao mbele ya nchi na watu wake,
. Viongozi hao ni nuksi na wanawaletea balaa Waafrika,
. Viongozi hao ni wala rushwa, wezi na mafisadi,
. Viongozi hao wanakazana kuwapiganisha wananchi wao wenyewe kwa wenyewe ili kuficha udhaifu wao,
. Viongozi wao ni wanafaiki na waongo wakubwa,
. Baadhi ya viongozi hao wanaishi kifahari mno ukilinganisha na hali ya maisha ya watu wao,
. Viongozi hao wanawalipa watu wao mishahara ya kiutumwa,
. Viongozi hao wanachafua siasa na demokrasia kwa ujumla kwa kutumia fedha wanayokwiba toka kwa wananchi,
. Viongozi hao hawataki kubadili katiba ili waadhibiwe kutokana na madhambi yao,
. Viongozi hao wanaabudu nchi za Magharibi pamoja na ukweli kuwa hivi sasa watakuwa na wakati mgumu sana kusaidiwa na nchi hizo,
. Viongozi hao hawana vipaji vya kuona mbali wala ujasiriamali unaoweza kutoa nchi zao kutoka safu za utegemezi na uchumi wa kikoloni,
. Viongozi hao wanashindwa kugawa madaraka na kwa kuwa nchi zao ni kubwa zinawashinda kutawala,
. Viongozi hao baada ya kutaifisha sasa wanajibinafsishia kile kilichotaifishwa huku mwananchi akiumizwa mara ya pili, kwanza, kwa kukatwa kodi ili mashirika ya umma yajengwe na sasa kwa kunyimwa gawio lake baada ya mashirika kuuzwa,
. Viongozi wengi ni wababaishaji na hawana leadership skills zozote za kunusuru watu wao na nchi zao.
 
There we go, thanks for calling a spade a spade that's what they deserve.
 

NAONA upo umuhimu wa viongozi wa Afrika kukomisheni tume ya kuchunguza kwanini wananchi wao wamevunjika moyo, hawana matumaini na sasa wanawaona kinyaa.


Afrika sio masikini kiasi hicho cha kwamba watu wetu wawe na dhiki ndogondogo kama tunavyoona sasa.

Tatizo la viongozi wetu ni kwamba wanaangalia upande mmoja tu wa mahesabu nao sio mwingine ila JINSI YA WAO NA WANAOWASAIDIA wanavyoweza KUTUMIA kile kilichoko hazina. Katika hali kama hii viongozi wasio na mchango wowote wa maana katika uzalishaji mali kwenye nchi husika wanakuwa hawana faida yoyote ya kuwepo. Wakiwepo wao au wakiewepo wengine hiyo ni sawa tu.

Pili hakuna anayeangalia ni vipi PATO la TAIFA linaweza kugawanywa vyema zaidi na hivyo kuondoa umasikini wa kupindukia katika nchi. Anayehurumiwa sasa ni yule aliye nacho asiyenacho hana msamaha kama alivyosema Makamba hapa duniani na mbinguni.

Uongozi sio hotuba nzuri na ujanja wa mjini na kupakazia huyu kamuua yule au huyu kafanya kile kiasi ambacho gazeti la chama lenye waandishi wenye hadhi na heshima yao wanafikia kujidhalilisha ili tu chama kishinde pale kisipopanda chochote.

Dunia inabadilika jamani na ni vyema tuanze kubadilika na sisi pia. La sivyo tukiendelea kuwa vingunge tu basi tutakuja kukuta tumevingungetwa na kutupwa kwenye jaa la historia ya siasa za nchi hii.

TUACHANE na ya Afrika nzima tujiangalie sie wenyewe baada ya ahadi zetu tamu kuliko asali, tamu kuliko sukari, tamu kuliko aisikrimu hivi kweli wananchi tunaowaongoza wanatuonaje- si kinyaa tu. Likitoka tatizo hilo laja hili, na angalau basi yangelikuwa ni matatizo ya maendeleo lakini yote ni matatizo ya kurudishana nyuma.

Labda tuanze kukaa kama taifa na kupangia kila WIZARA, IDARA NA KILA mtu MPANGO MKAKATI [STRATEGIC PLAN] hivi kila mmoja akawa na visheni ya nchi, wizara au taasisi yake inakotakiwa kwenda na nini wafanye ili wafike huko na kisha tuwe na menejimenti ya tathmini kwa maana tuanze kufuatilia kila baada ya miezi au robo mwaka mambo yanakwenda vipi na sio kungoja miezi tele mambo yakiharibika ndio tunagundua tatizo ni wapi.

Hata akili ya kuwa na STANDBY POWER GENERATING equipment hatuna. Jeshi letu likipewa challenge kama Mwalimu Jr. anavyosema kweli watashindwa kutengeneza wakisaidiwa labda na Wachina na Wakorea kuja kufanya kazi hiyo hapa nchini?

Nenda China na Korea na Japani uone watoto wadogo wa miaka 19 wanayofanya. Na wengine hawana fursa hiyo ukiwachukua hao ukawaweka pamoja na vijana wetu hapa hata ukiwalipa vimilioni tuchache tu wataona raha ya ajabu kuifanyia nchi hii maajabu.

JIBU moja la UTANDAWAZI ni jinsi kiongozi wa nchi fulani anavyotambua umuhimu wa kuwaalika vijana na wazee wenye ufundi fulani kuja kubadili mambo muhimu katika nchi na sio kuleta makocha wa mpira wa miguu tu!!!!!

Kiongozi mzuri ataiangalia sekta ya UMEME na kusema twende tukawachukue Wakorea kusini 10 na kuwalipa milioni 10 kila mmoja kwa mwezi ili wahakikishie mitambo na vifaa vya msingi vya umeme vinazalishwa hapa hapa nyumbani.

Atakwenda India atawachukua watengenezaji kompyuta na kuhakikisha kompyuta sasa haziagizwi nje bali zinatengenezwa papa hapa na zingine kuuzwa nje.

Ataangalia sekta ya maji na kugundua tatizo ni MAFUNDI tu lakini wapo vijana wasio na kazi kuanzia Italia hadi Japani na atamtuma waziri wake kalete watu 10 waje wahakikishe maji na mitambo na mashine za maji sio tatizo tena Tanzania baada ya miaka mitatu. Uongozi si kufikiria tu yaliyotokea bali pia kuwaza na kuwazua jinsi ya kuyafanya matatizo ya watu wako kuwa historia.

KWA namana hii kweli kiongozi ataonekana kinyaa au mzigo na watu wake. Hapana. Huyu lazima awe kiongozi bora na ambaye zawadi mbalimbali za kimataifa zitamsubiri baada ya urais wake.


In collaboration with Ideas. Unlimited. [Wizi na ufisadi wa mawazo yaliyopo hapa unaruhusiwa ili mradi tu uhakikishe yanawafaa Watanzania kwa namna moja au nyingine. Shukrani sio lazima na asante ni kuyafanyia kazi-ukiweka ubinafsi nyuma na kutanguliza taifa na watu wake mbele!
 
NINA hakika maoni hayo ya SMS yasiyo rasmi yanaonesha jinsi viongozi Afrika waliyvoshindwa kazi wanavyotaka kulindana na kulazimisha kuwepo madarakani tu hata kama uwezo wa kuongoza na kuleta mabadiliko hawanao!

Mchango unaotolewa na BBC ni mkubwa kuliko unaotolewa na vyhombo vyetu vya habari vinavyomilikiwa na serikali kama vile TBC ambayo bila aibu inaiisingizia CHADEMA kumuua Wangwe wakati ukweli ni kinyume cha hayo.

SIKU za mwongo hata hivyo ni arobaini tu naam na siku ya arobaini na moja bila shaka tutauona ukweli wakati mtoto halali wa Waancholi na Wanchoka, Nyaroonyo Kicheere, atakapochaguliwa kuwa mbunge wa kuleta sio umoja tu bali pia maendeleo hapa kwetu Tarime labda Chama cha Mafisadi kiibe kura tu!
 
Back
Top Bottom