Elections 2010 BBC nao ni mawakala wa CCM?

rugumye

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
561
178
Jana jioni nilishangaa kusikia mjadara juu ya uchaguzi wa Tanzania BBC wakiwapa watu mbalimbali live kutoa view zao, moja baya ambalo lilikuwa kichefuchefu ni kumweka mtu wa CCM kutamba kuilaumu CCM bila kutoa nafasi kwa mtu from Chadema.siyo sahihi. safari nyingine BBC mnapotoa mjadara hakikisheni pande zote zinakuwepo.
 
kama watu wenyewe ndio sampuli ya kina TIDO unategemea ninin !wanalamba miguu ili wakimaliza huko waje wateuliwe !
 
Kwa nini msijiulize na kupata majibu rahisi katika hili? Kenya ni nchi ya kitu kidogo na wale watangazaji wa BBC wanatoka Kenya na wamefanya kazi na Tido Mhando kwa muda mrefu. Jumlisha factor ya Salva Rweyemamu anavyo teleza kama nyoka ktk kuwatumikia mabwana zake! Kilichonishangaza sana jana na kuniumiza ni Mhe. Namwaba yule mbunge machachari wa kenya aliyekataa kuapa kiapo cha utii kwa Kibaki na badala yake kumtaja Laila Amolo Odinga!!
Yeye alisema kuwa tume ya uchaguzi ya kenya ya Kivuitu ilikuwa mbaya wakati ya tanzania ni nzuri!!! Asichokijua ni kuwa afadhali tume ya Kivuitu ilikuwa imeundwa kwa makubaliano ya vyama mwaka 1997 ingawa baadhi ya makamishina walikuwa wamechomekewa. Tume ya uchaguzi ya Tanzania haistahili hata kuitwa tume ya uchaguzi!! Hili ni genge tu la vikongwe ambalo liko pale kulinda maslahi ya waliowaweka .
hawako huru kwa maana ya aliyewateuwa, hawana uwezo kwa maana kuwa si weledi, hawana maana kwa kuwa hawawezi hata kufikiri na kukataa kutumiwa!
Hawana uwezo wa kusimamia uchaguzi wenye credibility maana hawako huru, hawana wafanya kazi wala hawana bajeti inayojitegemea zaidi ya kupewa fedha na Ikulu!!
Sasa niliposikia Mh. Nababu Namwaba akiwasifu nilishangaa sana nikajisemea kuwa Njaa haina adabu!!
 
Jana jioni nilishangaa kusikia mjadara juu ya uchaguzi wa Tanzania BBC wakiwapa watu mbalimbali live kutoa view zao, moja baya ambalo lilikuwa kichefuchefu ni kumweka mtu wa CCM kutamba kuilaumu CCM bila kutoa nafasi kwa mtu from Chadema.siyo sahihi. safari nyingine BBC mnapotoa mjadara hakikisheni pande zote zinakuwepo.

Uingereza ndio iliyowaambia Tanzania iwe na jina kama lao British Broadcasting Corporation (BBC) na Tanzania tukawa na Tanzania Broadcasting Corporation (TBC). Waliwapeleka baadhi ya wafanyakazi wa ngazi za juu kwenda UK kusoma masters. Na walisema kabisa UK itafaidika na hilo.
 
Back
Top Bottom