BBC: Jumuia ya Afrika Mashariki mashakani, Marais wa Kenya, Uganda na Rwanda waunda umoja wao!

Unajua kwamba tuliwaambia Uganda na Rwanda waondoke Congo? That is a strategy to show case their anger I suppose.
 
Jk haongei na mbwa, anaongea na mwenye mbwa!! Kesho kutwa hapa obama atakuwa magogoni tegeta,mbagala na gongolamboto, hamjiulizi kwann haendi kwao kenya anakuja kinondoni?

Kwa mawazo kama haya hatuwezi kufika we unadhani Marekani wana Rafiki? Fuatilia urafiki wao na Osama,Sadam Hussein,Gadafi,Mubarak,Mobutu na wengineo uliishia wapi, Marekani wanakutumia wakimaliza wanakutema usifikiri Obama haendi Kenya kisa hawapendi hataki tu kuwaibia walichonacho,Marekani wanakimbizana na spidi ya China kuwekeza Afrika kwahyo sio fahari sana mkuu.
 
Kweli hili jambo kufanyika wakati huu litaibua hisia mbali2 zitazopelekea mpasuko na hivyo jumuia hiyo kuelekea kifo kama ilivyokuwa 1977.
 
Tanzania hakuna uongozi thabiti na viongozi waliopo longolongo tuu hakuna utekelezaji,huku KKK ni kuchapa kazi kwa kwenda mbele.Hembu tujiulize ni miaka mingapi tangu tuseme reli ya dar-rwanda,burundi itajengwa?tanga-mwanza kupitia serengeti ku save uganda?
 
wanajf!kwa aliyebahatika kusikiliza bbc jioni ya leo atakubaliana nami kuwa jk amechokwa au anatengwa na wenzake,, kitendo cha kagame,museveni na uhuru kenyata kukutana kikao cha faragha leo entebe-uganda bila kumshirikisha jk,imeniweka pabaya!!hawa marais wanamuonaje rais wetu! naomba kuwasilisha
Hili jambo limenishangaza hata mimi. We are the big brother. How on earth could they do this? I was shocked. Uganda inataka kujenga bomba la mafuta kutoka Mombasa. Aidha, inasemekana wanataka kumkingia kifua Kenyatta kwenye kesi ya the Hague. Hii ni kali lakini haileweshi.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wiki hii Marais wa Kenya, Uganda, na Rwanda wamekutana nchini Uganda katika mazungumzo maalumu ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji. Ukiangalia hizi ni nchi zilizopo kwenye umoja wa kibiashara. Je, tuseme ndani ya Afrika Mashariki tunao umoja mwingine mpya? Ila kubwa zaidi kwanini wameitenga Tanzania kwenye mazungumzo haya?

Je, Umoja wa Afrika Mashariki bado una uhai kwa siku za usoni?

Nafikiri Watanzania tutafute washirika wengine wa kibiashara tutakaoweza kushirikiana nao maana kwa vyovyote vile kuwa mshirika/ mbia na mtu ambaye anakuangalia kwa jicho la chuki lazima atakufanyia vitimbi tu pale atakapo ona unataka kufanikiwa.
 
Sijui kama mradi wetu wa reli na Rwanda utasalimika, maana moja ya maamuzi ni Rwanda kujiunga katika reli ya Kenya na Uganda!
 
Tanzania mtawala ( usiseme kiongozi) wetu wa nchi anawaza namna ya kuidhibiti CHADEMA. Shame on you JK
 
Jamani Rais kikwete hana shida tatizo niwatendaji wake na kuhusu kwenda kwenye kikao jamani tambueni kuwa Rais naye anapangiwa ratiba huwa hajiendei tu kama ww unavyotoka nyumbani kwako ok na anaongozwa na sheria pia kuna gharama kulingana huwa haendi peke yake.
Inawezekana kweli. Mauaji ya CCM polisi usikute anayeyasimamia ni mgomea mtarajiwa wa CCM (kama Membe n.k.) anakuwa na mikakati ya kuhakikisha anawamaliza nguvu CDM. Kumbukeni JK alisema wagombea mjipange sasa wajipangeje??
 
Aisee hii mbona si habari kama unafuatilia news za dunia. Uhuru kabla ajatangaza kungombea alikuja kumuiona JK na baada ya uchaguzi alikutana na makamu wake serengeti. Nadhani JK kamtuma uhuru akawaambie washikaji wazingatie ushauri wake aliowapa.
 
Tanzania hakuna uongozi thabiti na viongozi waliopo longolongo tuu hakuna utekelezaji,huku KKK ni kuchapa kazi kwa kwenda mbele.Hembu tujiulize ni miaka mingapi tangu tuseme reli ya dar-rwanda,burundi itajengwa?tanga-mwanza kupitia serengeti ku save uganda?

Naunga mkono hoja. Sisi tumejaa maneno wakati wenzetu wamejaa vitendo.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Hata mimi ningekuwa wao singemuita.......kwa lipi sasa.......?
 
Back
Top Bottom