Kufutwa kwa BAWATA, NYF na Haki za Kiraia Tanzania

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Serikali iliifuta BAWATA kwa kigezo kwamba inajihusisha na siasa. Ikaifuta NYF kwa sababu ya kujihusisha na siasa, ingawa miaka michache baadaye serikali ikatoa sababu tofauti katika maelezo bungeni. Hukumu ya kesi hii inapaswa kujenga misingi ya kuzuia taasisi nyingine kufutwa baadaye zinapoonekana kwenda kinyume na matakwa ya watawala. Ni wakati sasa wa kuitaka serikali kufuta vifungu vya sheria vilivyoelezwa na mahakama.

Serikali kuilipa BAWATA milioni 20/-(Aprili 2009)

na Happiness Katabazi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeiamuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulipa fidia ya sh milioni 20 Baraza la Wanawake Tanzania (BAWATA).

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo, Amir Manento (amestaafu), Jaji Laurian Kalegeya (Mahakama ya Rufani sasa) na Jaji Justus Mlay na kusomwa kwa niada yao na Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Saul Kinemela.

Jaji Manento alisema Serikali inapaswa kuilipa BAWATA kiasi hicho cha fedha kwa sababu amri yake ya kuzuia shughuli za baraza hilo, ilivunja katiba ya nchini.

Sambamba na hilo, mahakama hiyo imesema vifungu 2(2), 6, 9(a)(b)(iii), 12 na 13(2) vya Sheria ya Asasi za Kijamii ambavyo sasa vinasomeka kifungu cha 2(2),814,17 na 19(2) kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, vinavunja ibara ya 15(1), 18 na 20 ya Katiba ya Nchi, hivyo imeitaka serikali kuvifanyia marekebisho ndani ya mwaka mmoja kuanzia jana.

Jaji Manento alisema jopo hilo limefikia uamuzi huo baada ya serikali kusimamisha shughuli za BAWATA ili taasisi hiyo isifanye shughuli zake; uamuzi uliotolewa Septemba 17 mwaka 1996 na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, F. Mushy kwamba Baraza hilo lisifanye shughuli zake. Uamuzi huo ulikuwa batili kwa sababu ulivunja Katiba ya nchini.

Walalamikaji katika kesi hiyo ya kikatiba namba 27/1997, ni BAWATA, Profesa Anna Tibaijuka, Sherbanu Kabisa, Rose Mushi, Mary Marealle na Salma Kauli, ambao walikuwa wakitetewa na Profesa Issa Shivji dhidi ya Msajili wa Asasi za Kijamii, Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Ameir Mohamed na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katiba ya nchi ni sheria mama na endapo kuna sheria yoyote nchini inakinzana na katiba, sheria hiyo ni batili, hivyo uamuzi wa serikali wa kusimamisha shughuli za BAWATA ulikuwa batili.

Kwa kuwa jopo hili limeutangaza uamuzi huo ni batili, na kwa kuwa BAWATA ilisajiliwa kwa misingi ya kufuata sheria, tunaiamuru serikali iwalipe walalamikaji sh milioni 20, ikiwa ni usumbufu na gharama za uendeshaji kesi, kwani kwa kipindi chote hicho asasi hiyo ilikuwa imesimama kufanya shughuli zake, alisema Jaji Manento.

Aidha Jaji Manento alisema mahakama hiyo imetamka kuwa vifungu 2(2), 6, 9(a)(b)(iii), 12 na 13(2) vya Sheria ya Asasi za Kijamii ambavyo sasa vinasomeka kifungu cha 2(2),814,17 na 19(2) kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, vinavunja ibara ya 13(6), 18 na 20 ya katiba ya nchi, hivyo imeitaka serikali kuvifanyia marekebisho ndani ya mwaka mmoja tangu kutolewa kwa hukumu hiyo.

Hata hivyo, alisema upande wa serikali katika kesi hiyo umeshindwa kuthibitisha madai yake kwamba BAWATA ilikuwa ikiendeshwa kama chama cha siasa.

Kwa mujibu wa hati ya madai, inaonyesha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mushy, Septemba 17 mwaka 1996, aliamuru kusimamishwa kwa shughuli za baraza hilo kwa madai kuwa lilikuwa likiendeshwa kama chama cha siasa, katiba yake haikupitishwa na mkutano wa wanawake wote/mkutano mkuu wa wanawake uliopitisha azimio la kuiunda na kwamba badala ya kuandaa na kuongoza wanawake kijamii na kiuchumi, lilikuwa linajiingiza kwenye siasa.

Mushy aliagiza BAWATA kuendelea kufungiwa hadi baada ya kuitisha mkutano mkuu na kuchagua viongozi wake, katiba ya baraza kupitishwa na wanawake wote na mfumo wake uwe umebadilishwa kutoka ule unaofanana na chama cha siasa na kuwa wa uratibu wa vikundi vya wanawake kwa ajili ya maendeleo, na kwamba mfumo usifanane na ule wa ngazi za utawala.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Tibaijuka, alieleza tayari walishachaguliwa kwa mujibu wa katika na kwamba BAWATA si chama cha siasa.

BAWATA ilisajiliwa Mei 16, mwaka 1995 na kupewa hati Na. SO 8404 chini ya Sheria ya Asasi ya Jamii ya mwaka 2002.


Serikali yatetea kufutwa kwa National Youth Forum (April 2007)
JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI


na Mwandishi Wetu


SERIKALI imesema kuwa uamuzi wa kufutwa kwa National Youth Forum ulikuwa sahihi kwa kuwa walishindwa kujidhibitisha.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Emmanuel Nchimbi, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Kabwe.

Katika swali lake la msingi Kabwe alitaka kujua sababu za serikali kuamua kuifuta asasi ya National Youth Forum na lini serikali itaacha kuzifuta asasi kama hizo na kwamba serikali haioni kuwa ufutaji wa asasi hizo ni ukiukwaji wa demokrasia.

Akijibu maswali hayo Nchimbi alisema muungano wa wadhamini wa National Youth Forum ulifutwa kwa kuwa ulishindwa kuthibitisha taswira waliyojiwasilisha nayo kwa umma kuwa wao ni taasisi ya vijana ya taifa.

Amesema msimamizi mkuu wa wadhamini baada ya kugundua kasoro hiyo inayodaiwa kuwa ni ya msingi, alitumia mamlaka yake chini ya sheria ya muungano wa wadhamini na kuifuta taasisi hiyo.

Ameongeza kuwa serikali haina nia ya kukiuka misingi ya demokrasia ya uhuru wa kujiunga, ila inasisitiza uundaji wa asasi hizo ni muhimu zikaambatana na wajibu wa asasi husika na hasa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazounda asasi husika.

Hata hivyo, amesema serikali inatambua umuhimu na mchango unaotolewa na asasi zisizo za kiserikali na hasa zinapofuata na kuzingatia sheria.
 
NYF ilifutwa kwa kuonekana kwamba inabeba kazi zinazopaswa kufanywa na Baraza la Vijana la Taifa(BAVITA) wakati yenyewe imesajiliwa kama National Youth Forum.

Wakati huo NYF ilikuwa mstari mbele kuwaunganisha vijana bila kujali itikadi kutaka kuundwa kwa baraza la vijana la taifa. Lakini hii haikusaidia taasisi hii kukwepa hukumu kama ile iliyotolewa kwa BAWATA.
 
HONGERA NA POLE BAWATA
Kwa hukumu ya Mahamakama Kuu (Tanzania) ya jana kuhusiana na shauri la Baraza la Wanawake Tanzania (BAWATA) dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Aprili 2 imekuwa siku ya kihistoria, si kwa BAWATA pekee, bali pia kwa AZAKI zote, wanawake wote, na wanaharakati wa maendeleo wote nchini Tanzania.

BAWATA tunawapongeza! Hongera kwa ushindi dhidi ya Serikali!

Lakini BAWATA tunakupeni pole, wanachama na viongozi sawia. Miaka 12 ya kusubiri uamuzi wa shauri lenu! Hakika mtakuwa mmepoteza mengi; kuonekana, marafiki, ujuzi, uzoefu, vifaa, miradi na mshikamano wa ndani. Wenye imani haba watakuwa waliiacha BAWATA siku nyingi.

Aidha wengine watakuwa tayari wameaga dunia! Hakika hili ni pigo kubwa! Hasara yake hailipiki, achiliambali kufuta machozi cha milioni 20 mlichopewa na Mahakama. Tunaamini hukumu imetolewa sasa kwa kuwa watawala walishapata walichokitaka kutosumbuliwa. Ni haki iliyocheleweshwa! AZAKI zilikuwa chache 1997, sasa uwanja umepanuka zaidi. Marafiki wameongezeka pia.

Karibu BAWATA. Karibu tujenge taifa. Karibu tupambane dhidi ya mafisadi na wala rushwa. Hongera na Pole kwa yote yaliyokukuta.
 
hivi nauliza ni nani mrithi wa ISSA SHIVJI?

Mrithi kwa maana ya kutetea wanyonge au?

Kama ni hivyo basi nadhani itabidi kutafuta sana maana hakuna mawakili pro-bono tena.Watu wanasaka noti tu siku hizi.

Issa Shivji anaamini itikadi ya kukomboa wanyonge. Msome kwenye the Silent Class Struggle na mengine utaona anatoka wapi. Miaka hiyo alikuwa na wanasheria wafuasi wake waliovutiwa na philosophy yake, lakini most of them siku hizi ni wafanyabiashara zaidi na sijaona tena wakisaidia wanyonge.
 
I thought justice delayed justice denied.

Hii kesi imechukua takriban miaka 12! Fikiria kama una kesi ambayo unategemea upate haki ili uweze kujikimu!

Ndiyo maana ukiwaza kupambana mahakamani upate haki yako, jizatiti kisawasawa. Hakikisha uko sawa.
 
Back
Top Bottom