BAWACHA mnaiangusha CHADEMA!

Nikisikiaga kitu kinaitwa BAWACHA natamani kutofuatilia mambo ya siasa,nimeshasema mara kadhaa
BAWACHA ni janga ndani ya CDM,kuna wakati mpaka ilimlazimu DR kuja kujibu hoja hapa jamvini na
tukaambiwa sasa tutawasikia,lakini cha kusikitiasha ndio wamezidi kuwa kimya.Kama kuna eneo linalohatarisha
ushindi wa CDM ambao uko wazi 2015,ni BAWACHA."Mna bahati nyinyi wamama wa CDM kazi yangu hainiruhusu
kujihusisha na siasa,ningeanza huko chini na moto wangu mngechangamka wenyewe.Agh.......may be wanapoingia
kama akina Esther Wasira wakiingia ndani ya BAWACHA wanaweza kuleta CHANGAMOTO.

Hivi mwentekiti wa BAWACHA ni nani?, hasiki kabisa inapaswa ifumuliwe na kuundwa upya.
 
Yaani kuna mbunge huwa anakaa upande ule wa akina Zitto sijawahi kumuona akiuliza hata swali hata siku moja acha kuchangia, na mimi ni mfuatiliaji sana wa bunge , simjui
hata jina lake huwa sielewi anafanya nini pale bungeni ningekuwa na picha yake ningeiweka.
Next time tuangalie watu wanaoenda kujenga
 
Hata Shibuda ni mtoa speech mzuri sana!kuongea si kutenda usimpaishe kwa speech moja tu,kumbe ili uwe kiongoz mzuri unatakiwa uwe unajua kutoa speech?
 
presentation hiyo aliiandika kabla hata hajachukua kadi chadema na hajaiandika peke yake haya tunamsubiri kumsikia tena

Ulimwandikia wewe? Ile ukipewa hata mbele ya mumeo huwezi kuisoma sembuse mbele ya hadhara ya kisomi pale Nkrumah! Mawaziri maprofesa na madokta kibao pale mjengoni wanaandikiwa hotuba na wasaidizi wao lakini wanapozisoma ni aibu sembuse kuzichambua.

Umefuatilia Bunge la bajeti la juzi? Wale mawaziri wawili - mmoja Prof. na mwingine Dr. uliwasikia? Natumaini umepata jibu! Binti kafunika balaa hata shetani hilo analijua ni wewe tu unataka kuleta ubishi.
 
Hivi mwentekiti wa BAWACHA ni nani?, hasiki kabisa inapaswa ifumuliwe na kuundwa upya.

Hajulikani mkuu.Tutamjuaje na yeye kajifungia kwake anasubiri msimu wa viti maalum!!
 
Mkuu hujanielewa kuwezeshwa ni muhimu lakini uongozi wa BAWACHA UMEPWAYA HILO HALIHITAJ RAMLI 2ACHA USHABIKI
Hata mimi najua kabisa kwamba BAWACHA imepwaya na wala hilo si suala la kujadili. Tatizo letu wengi wetu tunapenda sana kujadili "Anguko" na siyo chanzo cha anguko lenyewe. Sioni kama nimefanya ushabiki kwenye jambo nyeti kama hili kwani mimi mwenyewe najua katika siasa wanawake ndiyo mtaji wa kura unaotegemeka kuliko wanaume.

Mabadiliko ya kisiasa bila kuungwa mkono na wanawake hayawezekani hata siku moja. Wengine tunakumbuka sana mchango wa Bibi Titi Mohamed kwenye kuijenga TANU vijijini na mjini Dar es salaam. Lakini tatizo la BAWACHA halikuanzia kwa viongozi wake bali limeanzia kwenye viongozi hao walipatikanaje.

Sote tunakumbuka vurumai ya kwenye uchaguzi wa BAWACHA ambazo zilisababisha Chiku Abwao kukata Rufani na hatimaye kwa maneno ya Barabarani "kuzawadiwa" ujumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA ili kupoza mambo. Kwa mintarafu hiyo BAWACHA na uongozi wake walianza safari yao kwa mguu mbaya na Pepo huyo mbaya ameendelea kuikalia BAWACHA hata sasa.

Kuna watu wanaamini kwamba "Decisive Votes" Zitatoka kwa vijana, kwa hiyo wanaona ni muhimu kwa CHADEMA kuwekeza kwa BAVICHA kuliko BAWACHA kwa imani kwamba kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 "Block vote" ya vijana itakuwa kubwa sana kuliko watu wengine wowote.

Kwa Mantiki hii ni vigumu sana kwa wakati mmoja BAWACHA wakiomba fedha kwa ajili ya mafunzo na BAVICHA nao wakitaka fedha kwa kazi hiyo hiyo BAWACHA wakapewa. Wabunge wa viti maalumu wanachangia kiasi fulani cha fedha kuiendesha BAWACHA lakini sidhani kama wapo wanaotilia maanani uhai wake na ufanisi wake kwenye jamii ya Watanzania kuelekea 2015.

Siasa ni zaidi ya kusemasema majukwaani, siasa ni mikakati na mikakati ni uchanganuzi wa takwimu na tarakimu zikiambatana na nadharia iliyochambuliwa kiyakinifu!!

Sina USHABIKI kwenye jambo hili.
 
Mkuu kama ni kweli uchaguz wa BAWACHA ulikua na mizengwe hili ni tatizo juu ya tatizo chama kifanye maamuz magumu kuuweka huu uliopo pembeni na masalia yke na kuweka uongozi wa muda mpka hapo uchaguz utakapofanyika ndan ya chama BAWACHA ndio kundi litakalofanya CHADEMA ichukue dola 2015 bila changmoto nyingi kama tutawapa nafas wanawake wenye uwezo wa kuwaunganisha wenzao.
 
Suala hili la BAWACHA linafahamika lakini siasa zetu zinaendeshwa kwa mtindo "usiposema neno hupatwi na neno" kwa hivo watu wanasubiri uongozi huu uliiopo upite ndipo wachague mwingine bila ya kujali athari zinazosababishwa na kuwepo kwa uongozi huu.
 
Ni kweli mkuu wanajiendesha kwa mazoea na hili tatizo ni kubwa mno BAWACHA IMELALA WATU WANAANGALIANA SURA WAKATI WA VITI MAALUMU UKIFIKA WANAANZA KUTOANA ROHO
 
ni maoni yenu,mmemuona wasira kwa vile amepata forum ya kuonekana,i think kwenye cdm we have more competent women than she is ukweli ni hawajapewa nafasi.Naungana na wachangiaji wote kwamba bawacha iko hoi nimewai kusema hata mbele ya mwenyeki wetu,Suzane Lyimo kwenye kikao chetu kimoja jimbo la segerea lakini alinishambulia as if nimemuoffende.I totaly support kufumuliwa kwa bawacha lakini i donot support Ester Wasira,na support tutoe enuogh forums kwa wanawake wa chadema ili tuweze kuwashindanisha wvinginevyo tutarudia makosa yale yale.Wristle browers kindly lishikie bango tunaweza kufika mbali
 
Unaongelea kupewa nafasi ipi tena nawakati wamekua mabubu na ndio maana nasema ESTHER ATALETA CHANGAMOTO KATIKA KIPIND CHA MPITO BAWACHA HAWANA CHA KUJITETEA KWA HILI WAMEONYESHA UTENDAJ MBOVU NDAN YA BAWACHA KUENDELEA KUNG'NG'ANIA UONGOZ KUTAKIGARIMU CDM WAPO WANAWAKE WENGI WENYE HAMASA
 
Upande huo mzee mwenzangu nakuunga mkono maana wanawake daaaahhhh! hapa bado tumekwama ebu tumtumie huyu Easter
 
Kwanza vikao vya bawacha hata zijui vinakaliwa lini?? na je chama katika program zake huwa kinawapa majukumu yeyote bawacha?? manake isije ikawa tunawalaumu bure pengine tatizo lipo juu!
 
kwanza vikao vya bawacha hata zijui vinakaliwa lini?? Na je chama katika program zake huwa kinawapa majukumu yeyote bawacha?? Manake isije ikawa tunawalaumu bure pengine tatizo lipo juu!
ni mabubu wote
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom