BAWACHA kuichelewesha CHADEMA kuingia IKULU?

Nimependa Uchambuzi na pia nimefurahishwa na wepesi wa Dr Slaa kuja kujibu na kuchukua hoja, amesema wameshaanza na tuone matokeo yake hapa dar, na nilivyomwelewa ni kwamba wanaanzia dar na kuenea nchi nzima, Kundi hili la wananchi (Akina mama) ni kubwa sana; ni muhuimu lisiachwe nyuma katika safari ya kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi hii.

Aksante sana mleta hoja, hii ni hoja ya kujenga Chama na nchi kwa ujumla.
 
Je ni Dar es salaam tu? mikoani je?

Mkuu Kachanchabuseta umeielewa post aliyoiweka hapo Dk.Slaa au kwa vile katumia lugha ngeni ndo maana hujamwelewa?.kasema hivi 'ushauri umechukuliwa na hatua tayari zimechukuliwa na kwa kuanzia fuatilia shughuli za BAWACHA katika jiji la dsm',au wewe mwenzetu ulitaka waanzie wapi?na hata kama angesema Lindi napo ungeuliza ni Lindi tu mikoani je?.Elewa hata hiyo Dsm pamoja na kuwa ni jiji bado pia ni mkoa.Period
 
Kwa kweli BAWACHA imelala ni vizuri Kwamba Dr Slaa anasema wameliona hilo,tunategemea matokeo tuyaone
 
Je ni Dar es salaam tu? mikoani je?
Mkuu kila kitu kinakuwa na mwanzo wake. Dr. amesema kwa kuanzia, kwa hiyo ondoa hofu

quote_icon.png
By Dr.W.Slaa

WanaJF,
Concern and advice noted. Action already taken, naomba kwa kuanzia mfuatilie matukio ya BAWACHA katika jiji la Dar-Salaam. Feedback will be appreciated.
 
WanaJF
Ni jambo la kawaida kwa sasa kukuta watu mbalimbali majumbani,vijiweni,makazini,mashuleni na sehemu mbalimbali wakijadili siasa za Taifa letu.Na kote huko ni lazima katika kujadili siasa hizo CHADEMA itajwe.Hapo ndipo tulipofika watanzania.CHADEMA inaweza kuzungumzwa kwa njia yeyote iwe ni kwa mazuri au mabaya.Lakini jibu hapa tunapata kwamba hakuna asiyeijua CHADEMA.Nikiri tu kama makala zangu mbalimbali za huko nyuma nilivyosema CHADEMA kimefikishwa hapa kutokana na viongozi madhubuti wa chama hicho,Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa.Bila kuwasahau wabunge wote machachari wa chama hicho na viongozi wengine wa Kamati kuu na Baraza kuu la uongozi.

Dhumuni la bandiko hili ninataka kuzungumzia Baraza la Wanawake la CHADEMA-BAWACHA.Kwa hakika ukiniuliza hata kiongozi mmoja wa baraza hili ni nani simjui.Niwe muwazi kabisa siridhishwi na ukimya wa BAWACHA.Tukirudi nyuma kwenye chaguzi mbalimbali katika nchi yetu ni wazi wanawake ndio wapiga kura wakuu na tuseme ndio nguzo kuu ya CCM.Wanaume wanaweza kuwa wapiganaji wazuri na wasemaji sana lakini siku ya uchaguzi hawajitokezi kupiga kura.

Kwanini nawalaumu BAWACHA?
Ni ukweli ulio wazi kwamba ngome kuu ya CHADEMA kwa sasa ni vijana chini ya baraza lao BAVICHA.Na binafsi nimefurahishwa na jitihada zinazofanywa na viongozi wa vijana chini ya Mwenyekiti wao John Heche na katibu wake Deogratius Munisi.Ni juzi tu BAVICHA wamezindua jengo lao na hakika wanastahili pongezi za dhati.Sasa nikiangalia jitihada za vijana hawa kwanini jumuiya kubwa kama Baraza la wanawake wa chama liwe kimya hivyo? Tunafahamu kupitia Baraza hili CHADEMA imeteua wabunge wa viti maalum 25.Sasa hapa najiuliza idadi hii kubwa ya wabunge wa viti maalum si ndio inapaswa kuwa chachu ya kuunganisha nguvu ya kina mama mikoani? Mbona sijawahi kusikia hata mkutano mmoja umeandaliwa na BAWACHA? Ninadhani wakati mwingine unaweza kuiga mazuri kutoka kwa mtani wako.Sasa ni wakati wa BAWACHA kuangalia jinsi UWT ya CCM ilivyo imara na jinsi ilivyo chachu ya kuipa CCM ushindi wa kishindo hasa vijijini.BAWACHA wanapaswa kujua kwamba kinamama wa vijijini hawana uhuru wa kifikra na wakati mwingine wamekuwa wakibebwa na viongozi wa jumuiya ya UWT kwenda kumpigia kura hata mtu wasiyemtaka.BAWACHA wanapaswa kujua kwamba mageuzi katika mataifa mbalimbali kama ya Afrika Magharibi na kwingineko kama Zambia na Malawi yalichochewa sana na wanawake.Ilifika mahali katika kupigania demokrasia wanawake katika mataifa haya wamekuwa hata wakivua nguo na kuandamana ili dunia isikie kilio chao.BAWACHA mpo wapi?

BAWACHA wanapaswa kufanya nini?
· Wanapaswa kuunganisha nguvu ya kinamama kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa
· Wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulaani na kukemea maovu mbalimbali kwenye jamii hasa madhila dhidi ya kinamama na watoto..mf wamtazame mama Ananilea Nkya
· Wanapaswa kujitambulisha kama nguzo kuu ya kinamama kote nchini
· Wanapaswa kuzunguka nchi nzima kufanya mikutano ya hadhara na ya ndani kuhamasisha kinamama kutokuogopa mageuzi
· Wanapaswa kujitambulisha kama nguzo kuu ya CHADEMA
· Wanapaswa kuwa na viongozi machachari wasiotishwa na wapinzani wao.
· Wanapaswa kuepuka kuwa Baraza la kufanya mkutano siku tu wanapoteua wabunge wa viti maalum.
· Wanapaswa kuandaa program ya kuwaimarisha vijana wakike walio masekondari na vyuoni ili kuwa wakakamavu na kuwaondolea hofu ya kuwa viongozi miaka ijayo
· Wanapaswa kujua kazi ya BAWACHA sio kupigania ubunge wa viti maalum tu.

Wito wangu.
Ninatoa wito kwa viongozi wakuu wa CHADEMA hasa Katibu mkuu Dr Wilbroad Slaa kwamba hakika jumuiya hii inapaswa kuangaliwa upya na ni vema ikawa na mvuto kama wa BAVICHA.Si dhambi kama viongozi wa BAWACHA wameshindwa majukumu yao wakakaa pembeni wakawapisha wengine watakaoifanya BAWACHA ionekane kweli ni moto kama chama kilivyo. Nionavyo mimi BAWACHA inaweza kuichelewesha CHADEMA kuingia madarakani

WanaJF karibuni kwa mjadala!

Truly patriotic. Siongezi neno
 
WanaJF,
Concern and advice noted. Action already taken, naomba kwa kuanzia mfuatilie matukio ya BAWACHA katika jiji la Dar-Salaam. Feedback will be appreciated.

Nakushukuru sana Dr Slaa kwa jinsi ulivyo makini na unavyojibu hoja hapa JF.Nimefurahishwa jinsi ulivyochukulia bandiko langu na jinsi ulivyo positive.Keep it up Dr.!
 
Nimekubali maoni yako, yako juu tunaitaji watu wenye mawazo chanya kama wewe ili kuing'oa ccm au kupata mageuzi ya kweli.
 
Fantastic ! This is ver very good analysis and advice,Our President has already take this into consideration,So wait and see moto wa BAWACHA sasa. fMpiganaji Hongera kwa kuliona hili na kuwakilisha hapa jamvini!
 
Fantastic ! This is ver very good analysis and advice,Our President has already take this into consideration,So wait and see moto wa BAWACHA sasa. fMpiganaji Hongera kwa kuliona hili na kuwakilisha hapa jamvini!

Thanks mkuu.Nashukuru kwani tayari Dr ameshalichukua
 
mkuu umefanya uchambuzi mzuri hata mimi huwa nashangaa kuwa chadema ina wabunge almost 25 kupitia hao bawacha but to my suprise wanazidiwa na Bavicha ambao hata hawana hata representation bungeni. nashindwa kuelewa kuwa hao wabunge wanaifanyia nini hiyo idara ya wanawake. Bawacha wakiwatumia hao wanawake wabunge nadhani itasaidia kuwafikia wanawake wengi ambao wanateseka na maisha magumu yanayosababishwa na ccm.
 
mkuu umefanya uchambuzi mzuri hata mimi huwa nashangaa kuwa chadema ina wabunge almost 25 kupitia hao bawacha but to my suprise wanazidiwa na Bavicha ambao hata hawana hata representation bungeni. nashindwa kuelewa kuwa hao wabunge wanaifanyia nini hiyo idara ya wanawake. Bawacha wakiwatumia hao wanawake wabunge nadhani itasaidia kuwafikia wanawake wengi ambao wanateseka na maisha magumu yanayosababishwa na ccm.

Ni kweli mkubwa kama ulivyosema
 
Fantastic ! This is ver very good analysis and advice,Our President has already take this into consideration,So wait and see moto wa BAWACHA sasa. fMpiganaji Hongera kwa kuliona hili na kuwakilisha hapa jamvini!

Its Extremly analysis!
 
Bawacha pia wahakikishe wanahamasisha akina mama kujiandikisha kwa wingi katika kupiga kura.
 
WanaJF,
Concern and advice noted. Action already taken, naomba kwa kuanzia mfuatilie matukio ya BAWACHA katika jiji la Dar-Salaam. Feedback will be appreciated.

WAW!! Thank you Ma President "I SALUTE YOU".
 
Ni ukweli wa wazi vyama imara vinahitaji taasisi imara na hizi ndiyo jumuia za chama, unapokuwa na jumuia zisizowajibika unaua chama kwa hiyo analysis yako ni msaada kwa chama chochote kinachozingatia ushauri UNAOTOLEWA NA WADAU WA SIASA ZA NCHI
 
Back
Top Bottom