BAVICHA yazidi kujiimarisha

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa wito kwa wanafunzi kutoka vyuo vikuu kugombea nafasi za uongozi serikalini, kuanzia ngazi za vijiji ili kufikisha elimu ya mabadiliko kifikra maeneo hayo.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa tawi la Chadema Chuo Kikuu cha Mtakatifu John, tawi la Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Taifa (Bavicha), John Heche, alisema wananchi wengi vijijini wanakabiliwa na matatizo mengi ya umaskini yanayotokana na ukosefu wa uongozi bora.

“Tanzania ina zaidi ya vijiji 20,000 maeneo hayo yote Dk Willibrod Slaa hawezi kuyafikia na akitaka kufanya hivyo itamchukua muda mrefu, ninyi mliopata elimu ndiyo mnaostahili kwenda huko na njia pekee ya kuleta mabadiliko ni kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za vijiji,” alisema Heche.

Heche alisema kwa sababu hivi sasa chama kina mtandao kila chuo kikuu cha Tanzania, njia hiyo ndiyo itakayowezesha wananchi kunufaika na elimu ya vijana kutoka vyuo vikuu.

Source:Mwananchi Jumatano
 
Ni wito mzuri kwa wapenda mabadiliko wote popote walipo!! Kuna vyeo vingine havili muda mrefu, na uongozi ni kujitolea kwa hiyo wenye uwezo wa kugombea na wafanye hivyo.
 
Ni wito mzuri kwa wapenda mabadiliko wote popote walipo!! Kuna vyeo vingine havili muda mrefu, na uongozi ni kujitolea kwa hiyo wenye uwezo wa kugombea na wafanye hivyo.

pamoja heche.mkuu WA UKENYEGE NIMEKUMISS,ULIKUWA visiwa vya maldives nn.
 
Back
Top Bottom