BAVICHA yamkaanga spika Anne Makinda jimboni kwake

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Baraza la Vijana la Chadema BAVICHA kupitia viongozi wake wakuu John Heche na Deogratia Munishi jana lilimmwagia ***** mkali Spika Anna Makinda jimboni kwake Njombe kusini. Katika mkutano wa hadhara ulifanyika Njombe mjini na uliotanguliwa na ufunguzi wa ofisi ya Kata ya Mjimwema, Viongozi hawa waliwaeleza wananjombe jinsi ilivyo aibu kwao kutawaliwa na mama huyu kwa zaidi ya miaka 35 sasa na kuufanya ubunge kuwa wa kichifu.

Aidha, BAVICHA imesema kuwa ni fedhea kwa mbunge Anna Makinda kulitawala jimbo hilo kwa muda mrefu lakini mpaka sasa jimbo la njombe na vijiji vyake halina maji japokuwa lina mito miwili mikubwa na vyanzo vingine vya maji. Katika mkutano huo, Heche na Munishi walibainisha kuwa wananjombe wanapaswa kujilaumu kwa kulipatia taifa kiongozi dhaifu kama Anna Makinda anayeliyumbisha bunge kama spika na kwamba Makinda na udhaifu wake ni kielelezo cha watu wa Njombe na kama si hivyo basi wananchi wa Njombe japo wananchi wenyewe walipinga hilo kwa kusema wao hawakumchagua Anna Makinda kuwa mbunge wao bali alipitishwa kwa hilo kwa pesa chafu za Rostam Azizi.

Wakiwa jimbo la Njombe Kaskazini mjini Makambako, Heche na Munishi waliendelea kuisakama CCM na serikali yake. Munishi alisema kuwa rais kikwete ni muongo namba moja Tanzania kwani alidanganya vijana na watanzania kwa ujumla kwa kuahidi ajira milioni moja mwaka 2005 ambazo mpaka leo hazijapatikana. Alisema kama raisi Kikwete na serikali yake wanahesabu vijana kuokota makopo barabarani na kuyauza basi vijana wakae tayari kuitumua serikali hii madarakani kwani kuokota makopo kunawafanya vijana kutotofautishwa na machizi.

Kwa upande wake John Heche aliendelea kushikilia msimamo kuwa Rais Kikwete ni dhaifu, Waziri Mkuu Pinda ni dhaifu na Spika Anna Makinda ni dhaifu na wanalipeleka taifa shimoni. Kabla ya kuingia majimbo ya Njombe Kusini na Kaskazini hiyo jana, John Heche na Deogratias Munishi waliutubia jimbo la Iringa Mjini na kuwasulubu vikali mbunge wa viti maalumu Rita Kabati na vikundi vingine vya CCM kueneza udini jimboni Iringa
 
Nawapa hongera sana hao makamanda wetu. Ni saa ya ukombozi hii. Kila unayesoma hapa eneza ujumbe wa kupinga ufisadi, kutetea mali za uma zinazohujumiwa na viongozi wabovu wa magamba. Tujipange kwa kuichagua CDM 2015 kwa ajili ya maendeleo yetu.
 
hawaogopi kufungwa? hawajui CCM sasa haitaki masihara, wasubiri kesi sasa hivi
 
makamanda endeleeni na mapambano mpaka kieleweke,,,,,,,,,,,, Piipoooooooooooooooozzzzzzzzzzzzz
 
wamevuna wanachama wangapi wapya?
mkakati gani mnao wa kumweka mtu atakaeukubalika ili kumngoa mama?
 
Back
Top Bottom