BAVICHA - Waziri Kawambwa na wasaidizi wajiuzuru matokeo kidato cha nne

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884

images
images



  • huo ni muendelezo wa siasa na mzaha kwa Watanzania kunakofanywa na serikali ya CCM kwenye masuala nyeti.
Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA), limemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa na wasaidizi wake kujiuzulu mara moja ili kupisha wenye uwezo wa kusimamia sekta hiyo. Katibu Mkuu wa BAVICHA, Deogratias Munishi, alisema hayo katika tamko alilolitoa jana baada ya Tume ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kutoa ripoti ya awali kuhusu sakata la kufeli vibaya kwa wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana. Akinukuu moja ya sababu za kushindwa kwa wanafunzi hao, Munishi alisema ni kutumika kwa alama mpya tofauti na miaka ya nyuma bila taarifa kwa walengwa.

Alisema kuwa huo ni muendelezo wa siasa na mzaha kwa Watanzania kunakofanywa na serikali ya CCM kwenye masuala nyeti. “BAVICHA inasisitiza Waziri Kawambwa na wasaidizi wake wajiuzulu nyadhifa zao ili kupisha watu wenye uwezo wa kusimamia sekta hii na taasisi zilizo chini yake,” alisema Munishi.

Aliongeza kuwa viwango hivyo vipya vilivyowekwa na Baraza la Mitihani bila kushirikisha wadau ni kiashiria cha uzembe uliokithiri. “Kama Baraza lilifanya maamuzi hayo bila waziri kujua nako kunaashiria uzembe uliobobea wa waziri huyu wa kushindwa kujua kinachofanyika na taasisi zilizo chini yake na kwa maana hiyo ni mzigo kwa taifa,” alisema. Kwa mujibu wa Munishi, suala hilo limeleta athari kwa wanafunzi, kwani baadhi yao wamepoteza maisha kwa kujinyonga.



images
images



mbatia AMSHANGAA WAZIRI KAWAMBWA KUTOJIUZULU
SIKU moja baada ya serikali kufuta matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na kuamuru yaandaliwe upya, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia, ametaka wazazi wa wanafunzi waliojinyonga kwa matokeo hayo walipwe fidia. Wakati akitaka wanafunzi hao walipwe fidia, pia Mbatia alimshangaa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, akihoji anasubiri nini kung’atuka wakati kuna wanafunzi wamepoteza maisha kwa uzembe wao. Alisema Kawambwa anapaswa kujiuzulu kwani Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani nchini, Joyce Ndalichako, hawezi kufanya mabadiliko makubwa ya aina hiyo bila kuishirikisha wizara.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa, Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa alisema serikali imekuja na majibu rahisi kwenye jambo gumu, kwani uamuzi wa kufuta na kuandaa upya matokeo hayo kwa utaratibu wa mwaka 2011, hauleti ufumbuzi wa mfumo wa elimu.
“Tume imekuja na majibu mepesi sana kwenye tatizo kubwa. Wanafunzi wamejiua kwa msongo wa mawazo, wengine wamekata tamaa na kuamua kuolewa, wengine kupata ujauzito, leo kwa uzembe wao wanataka kuwafaulisha wanafunzi ili kupata sifa kisiasa, haiwezekani,” alisema.

Akichambua maoni ya tume hiyo, alisema imeibua hoja ambazo yeye aliziwasilisha bungeni kupitia hoja yake binafsi ambayo ilizimwa na wabunge wa CCM kwa sababu za kulinda masilahi ya chama chao.
Alilishambulia Bunge kuwa limekuwa chanzo cha matatizo mengi kutokana na ubinafsi wa vyama bila kujali masilahi ya taifa. “Bunge linaangamiza taifa kwa sababu ya itikadi. Hizi itikadi za vyama zinaliangamiza taifa. Kuna umimi, ubinafsi kwenye mambo ya masilahi ya taifa. Nawataka wabunge watoke usingizini,” alisema Mbatia.

Juzi serikali ilitangaza kufuta matokeo ya kidato cha nne ya mwaka 2012 na kuagiza yaandaliwe upya.
Uamuzi huo mgumu ulitangazwa bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi. Akisoma tamko hilo kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Lukuvi alisema uamuzi huo wa serikali umetokana na mapendekezo ya tume ya waziri mkuu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha matokeo ya kidato cha nne mwaka jana kuporomoka kwa kiwango cha kutisha.

Matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012 yalionesha kuwa kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miaka ya hivi karibuni.
Matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni, yalionesha kwamba kati ya wanafunzi 367,756 waliofanya mtihani huo, watahiniwa 126,847 ndio waliofaulu. Katika idadi hii, wanafunzi waliofaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ni 23,520, sawa na asilimia 6.4 na daraja la nne ni 103,327, sawa na asilimia 28.1. Watahiniwa 240,909, sawa na asilimia 65.5 ya wanafunzi wote, waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012, walipata daraja sifuri.
 
Kweli hili nalo ni janga maana ukitafakari kwa makini utaona huu ni mzaha maana mtu anahesabiwa amefaulu endapo atapata only D mbili kati ya masomo 7 lakini wanafunzi wengi wameshindwa kupata hizo point na kufeli. Ukiangalia kwa mtazamo wa kawaida usio wa kitaalamu utaona kwamba tatizo si NECTA wala wanafunzi bali ni mfumo mzima wa elimu yetu ndio umefanya hivyo na si masuala ya GRADING wala nini maana kama kweli umemfundisha mwanafunzi vizuri hata kama issue kama ni grading basi tungepata idadi kubwa ya wanafunzi ambao wamefaulu katika kiwango cha kawaida tu kwa kuwa katika masomo 7 lazima kuna ambayo angekuwa amefaulu kwa kiwango juu ya wastani maana haiwezekani mtu akawa kilaza masomo yote unless kama wanafunzi waliandaliwa kupata minimum division / division four hapo sawa lakini kama mitaala yetu iliwaandaa wanafunzi wafaulu katika kiwango cha juu sidhani kama hii issue ya grading ingeleta division zero nyingi kiasi hicho wakati ukipata D mbili tu unahesabiwa umefaulu (kama ingekuwa ukipata D saba ndio umefeli hapo kidogo ingekuwa issue.

Tusiogope matatizo kwani hata kama darasa zima limefeli tumekosa watu wa kwenda form 5 kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kurekebisha tatizo ili siku zingine lisitokee pia kuangalia namna gani ya kuleta crash programme ili hawa watoto ambao ni wengi kuangalia namna ya kuwaandalia maisha yao mapya ya kitaaluma.

Kama ingekuwa ni watu makini wangetunga tu mtihani mfupi wa general knowledge kuwapima hawa wanafunzi kuona tatizo nini kabla ya kuamua kufuta matokeo
 
Kinachoshangaza wanafuata ushauri huu wakati tume ya awali iikwisha pendekeza mambo muhimu ambayo yangezuia matokeo haya mabaya. Ina maana hawakusoma au Waizri alipuuzia? Cha kushangaza zaidi hata Dibaji ya ripoti ya hiyo tume ya awali iliandikwa na Waziri mhusika.

Hizi ni sehemu chache tu nilizookota kwenye repoti yenyewe.

Waziri anaandkika hivi kwenye dibaji ya ripoti yenyewe
No wonder kwanini wadau wanasisitiza ajiuzulu lakini hata Waziri Mkuu pia

"Ninawaomba wadau wa elimu nchini kuyafanyia kazi matokeo ya utafiti huu ili kuweza
kupiga hatua katika utekelezaji wa utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi. Serikali inayo
nia ya dhati ya kutekeleza mapendekezo haya ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu
ya sekondari nchini".
Mh. Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB)



Utafiti umedhihirisha kuwa matatizo yanayohusu usimamizi na uendeshaji
yameathiri ufanisi katika utoaji wa elimu bora nchini. Baadhi ya viongozi wa
elimu huteuliwa bila kuzingatia utaalamu, taaluma, uwajibikaji, uwezo na
uadilifu. Aidha, maamuzi ya kitaalamu kuhusu uendeshaji wa elimu hufanyika
kisiasa bila kuzingatia utaalamu na tafiti


Utafiti umebaini kuwa, mmomonyoko wa maadili kama vile matumizi ya lugha
mbaya; matumizi mabaya ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA),
kutozingatia mafundisho ya dini, matumizi ya dawa za kulevya na kujiingiza
katika masuala ya mapenzi ni masuala yaliyobainishwa kuchangia kumeathiri
maendeleo ya taaluma shuleni

Utafiti umeonesha kuwepo kwa changamoto za utayarishaji na utekelezaji wa
mtaala kwa miaka mitano iliyopita. Mtaala ulioboreshwa wa mwaka 2005
umetekelezwa bila kufanyiwa majaribio (piloting). Aidha, utafiti umebaini kuwa
kwa miaka mitatu iliyopita (2008 hadi 2010), jumla ya walimu 588 (1.5%)
walipata mafunzo kabilishi. Taarifa hii inaonesha kuwa walimu wengi hawana
maarifa na stadi za kufundisha mtaala wa sekondari uliboreshwa.


Pia utafiti umebaini kuwa, katika shule 132 zilizotembelewa, shule 18 (13.53%)
zilikaguliwa mara 3 hadi 4 kwa kipindi cha mwaka 2006 hadi 2010. Hali kadhalika
shule 6 (51.88%) zilikaguliwa mara moja au mbili, na shule 46 (34.59%)
hazikukaguliwa kabisa. Aidha, taarifa za ukaguzi wa shule hazifanyiwi kazi
ipasavyo. Kutokaguliwa kwa shule hizo za sekondari kumepunguza ufanisi wa
usimamizi na utoaji wa elimu bora


Aidha, matokeo ya utafiti yameonesha kuna upungufu mkubwa wa walimu
kimasomo hususani katika masomo ya sayansi na Mathematics unaosababishwa
pia na upangaji usiozingatia mahitaji hususan katika sehemu zenye mazingira
magumu. Katika shule zilizofanyiwa utafiti imebainika kuwa somo la
Mathematics, lina mahitaji ya walimu 436 ambapo waliopo ni walimu 172 hivyo
kuna upungufu wa walimu 264 sawa na asilimia 60.6. Tatizo la upungufu wa
walimu ni changamoto katika utoaji wa elimu.


Sikuamini nilipoisoma hii

"Utafiti umebaini kuwa, uteuzi wa wasahihishaji katika ngazi ya shule haufanywi
kwa makini. Aidha, utaratibu wa kulipa wasahihishaji kwa idadi ya ‘scripts'
walizosahihisha badala ya posho ya kujikimu na muda mrefu wa usahihishaji
kwa siku ni baadhi ya masuala yanaweza kuchangia kupungua kwa umakini wa
usahihishaji."

Na hili ndiyo wanalifanyia kazi sasa kwa kufuta mitihani yote, sasa kulikuwa na haja gani ya kuwepo kamati ya pili??


Aidha utafiti umebaini
kuwa, gredi zinazotumika shuleni kwa uzoefu wa miaka mingi ni A (81-100), B
(61-80), C (41-60), D (21-40), F (0-20). Hata hivyo NECTA imethibitisha kuwa
alama za gredi zinazotumika kwa Mtihani wa Taifa wa K4 huamuliwa na Kamati
ya Kutunuku ambapo gredi D huwa si chini ya alama 30 na A si chini ya alama
70. Hali hii ya kutokuwepo kwa alama za gredi zenye ulinganifu baina ya shule
na NECTA kumeleta mkanganyiko wa matumizi ya alama za gredi. Vilevile, kuna
mapungufu ya kuadhibu watahiniwa kwa kuteremshwa daraja la I au la II kuwa
la III kutokana na kufeli baadhi ya masomo ya msingi na ya mchepuo.


Na hapa walionya kuwa "Athari ya matokeo mabaya katika mitihani ya kuhitimu ni kuwa na jamii ambayo haina elimu ya kiwango kilichokusudiwa kitaifa"

Niliposoma para hii ilinibidi nicheke maana inaelekea alipoondoka Lowassa hakuna aliyefutilia swala la Elimu tena nchini Serikali iliyolala usingizi haifahamu kuwa inapoongeza idadi ya wanafunzi matumizi huongezeka?

"Idadi ya shule za sekondari (za serikali na zisizo za serikali) imefikia 4,266 mwaka
2010 ukilinganisha na shule 1,745 zilizokuwepo mwaka 2005, ongezeko hili ni sawa
na asilimia 144.5. Mafanikio hayo ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya wanafunzi
(Kidato cha 1-4) walioandikishwa katika shule za sekondari za kawaida kutoka
wanafunzi 489,942 mwaka 2005 hadi kufikia 1,566,685 mwaka 2010."


Cha kushangaza hata swala la mitaala na umuhimu wake limezungumziwa sana tu
"2.7 Mtaala na Utekelezaji
Sera ya Elimu na Mafunzo (1995) inaeleza kuwa kila mfumo wa elimu ni lazima uwe
na mitaala ya shule kukidhi mahitaji ya kielimu katika taifa husika. Mtaala
umegawanyika katika maeneo manne muhimu ambayo ni malengo na madhumuni ya
mtaala; maudhui au mada; vitendo vya kufundishia na kujifunzia; na upimaji au njia
za kupima mafanikio. Aidha, Taasisi ya Elimu ya Tanzania itawajibika kwa maandalizi,
maendeleo, utoaji, ufuatiliaji na tathmini ya mitaala ya elimu ya awali, msingi,
sekondari na ualimu (Sera ya Elimu na Mafunzo 1995,

Kufika hapa nilipata kichefuchefu
"Kimsingi watungaji wote ambao wanateuliwa kutunga mitihani wanatakiwa wapatiwe
mfunzo ya msingi na mbinu za uandaji wa maswali mazuri ya mitihni. Hata hivyo
imeonekana kuwa hali hiyo haifanyiki na watungaji wa mitihani hutegemea utaalamu
kama walimu na uzoefu wao kazini"

Kuhsu uwepo wa maabara ,mashuleni
"Takwimu zinaonesha kwamba asilimia 77 ya shule za serikali hazina
maabara za sayansi"

Hiyo ni nusu tu ya ripoti yenyewe, ni haki kabisa wananchi wakimtaka ajiuzulu. Na ni aibu kwa Waziri kujiona anastahili kuendelea kuiongoza wizara ya Elimu.
 
Back
Top Bottom