BAVICHA kuandaa maandamano nchi nzima

Dr. Slaa ni mtu makini ya mungu anayajua.

Na uhakika kama malaika Gabriel anasoma hii post, basi analia kwa uchungu mkubwa sana kwa kuwa sasa wanadamu wanamfananisha Mungu na shetani.
 
Hapo umenena kweli,na kwa muhutasari wabunge wengi wa CDM uchaguzi ujao hawatoweza kupita, pia viti maalum vitaondoshwa kitu ambacho kitakuwa ni pigo kubwa sana kwa chadema, kwani itakuwa imetengeneza wingi wa wabunge waliong'atuliwa na kuwafanya washinde kijiweni pale kinondoni kama slaa, na mbaya zaidi watakuwa hawewezi kulipwa kama Dr anavyokula kwa mlija.

At Least Magamba mnajipa moyo siyo mbaya!!! ila mkae mjue anguko kuu la Chama Cha Magamba(CCM) laja sooon! People's power....
 
Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano. Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania.

Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.

Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza.

Ni bora wakatumia fedha za chama kwa shughuli za chama kama hiyo ya kuwaelimisha wananchi. Ulitaka fedha za kuendesha chama wanunulie vyandarua? Serikali ndiyo inapaswa kufanya kazi ya kutumia fedha kwa ajili ya shughuli za maendeleo. Wala usifikiri kuwa si jambo la maana kufanya maandamano ili kuelimisha wananchi.
 
Niliwaambia kwenye nyuzi nyingine kule watumie "scientific approach" kwenye siasa. Hawajui kuwa ngoma ikivuma sana hupasuka. Hawana jipya na hao wanaoandaa maamndamo wamejipatia njia moja ya kujipatia posho kiulaini.

Wewe ndio Kamanda achana na hawo makamanda wa sinema za kihindi nashukuru kwa hoja zako murua
 
Kaka, Unalipa kodi wewe? in person

Kaka umenifanya niwe Sympathizer kwa kauli yako hiyo, unajua ata ukinunua vocha ya simu ya shilingi 500 unalipa kodi ambae inakwenda kwenye maandamano
 
Unalipwa posho shilingi ngapi na chama cha magamba aka mafisadi expert kulog in jf na kukomenti majibu ya kiarijojo kama ubungo wako ulivyo. Take care
niliwaambia kwenye nyuzi nyingine kule watumie "scientific approach" kwenye siasa. Hawajui kuwa ngoma ikivuma sana hupasuka. Hawana jipya na hao wanaoandaa maamndamo wamejipatia njia moja ya kujipatia posho kiulaini.
 
wabunge wa cdm wasipochukua hatua za kusimamia maendeleo ya majimbo yao huenda wakaongoza hayo majimbo kwa kipindi kimoja tuu. Wengi wao wamejikita katika kukitangaza chama kitaifa (ushiriki wao kwenye maandamano sehemu mbali mbali nchini) badala ya kusimamia maendeleo sehemu walizopigiwa kura.

Madhalani tuchukulie jimbo la arusha mjini, moja ya wafuasi wakubwa wa cdm ni wamachinga na ahadi kubwa aliyotoa mh. Mbunge ni kujenga machinga complex mbili. Leo hii, ambapo imebaki takribani miaka minne na miezi mitatu kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2015 hakuna lolote (tangible) liliofanyika.

Mvuto alioanza na mh. Mbunge wa arusha mjini kama hataweka mbele utekelezaji wa yale aliyoahidi, huenda mvuto wake kwa wapiga kura ukafifia kwa stahili ile ile ya raisi wetu wa sasa.

mkuu huoni kama upo nje ya mada,kwa kuwa unachoongelea hakiendani ya hoja iliyopo mezani!!!ingekuwa vizuri kama ungeanzisha hoja maalum ili tuichangie vizuri!!jibu lako ni zuri sana lakini si kwa sawli hili,pole sana mkuu!!
 
hapo umenena kweli,na kwa muhutasari wabunge wengi wa cdm uchaguzi ujao hawatoweza kupita, pia viti maalum vitaondoshwa kitu ambacho kitakuwa ni pigo kubwa sana kwa chadema, kwani itakuwa imetengeneza wingi wa wabunge waliong'atuliwa na kuwafanya washinde kijiweni pale kinondoni kama slaa, na mbaya zaidi watakuwa hawewezi kulipwa kama dr anavyokula kwa mlija.
dua la kuku halimpati mwewe!vipi jk ameshatekeleza ahadi zake?au kazi yake ni kwenda tu nje ya nchi?
 
Niliwaambia kwenye nyuzi nyingine kule watumie "scientific approach" kwenye siasa. Hawajui kuwa ngoma ikivuma sana hupasuka. Hawana jipya na hao wanaoandaa maamndamo wamejipatia njia moja ya kujipatia posho kiulaini.
Vipi ile ya CCM ilishapasuka?au zinapasukaga za pande hii tu?au CCM haijawahi kuvuma sasa?au imevuma sana na sasa imevimba hivyo inasubili kupasuka!!!!
 
Kuna hawa Wabunge wa Mwanza, jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje huyu Mbunge machinga wa Mwanza sehemu za makoroboi, mirongo, bugarika, na maeneo mengine awataki ata kumuona, wakati wa kampeni aliwambia mkinachugua nitahakikisha mnabaki sehemu zenu za kazi, baada ya kupata ubunge amewambia wahame, Ubunge wake umebakia kwenye maandamano tu.
Huyu Mbunge mwingine wa jimbo la Ilemela. Hayness Samson, huyu ndio hatakiwi kabisa Mwanza yeye tangu achagulie yeye anakaa Dar es Salaam, yeye kiguu na njia kwenye maandamano kila kukicha
 
Halafu rushwa zenyewe walizianika humu JF mpaka za shillingi 1,500/= Wananchekeshaa!
Kwa hiyo 1500/=siyo rushwa!!kwa hiyo rushwa inaanzia shillingi ngapi?ile rushwa inayodaiwa kutolewa na mwakalebela na iliyosababisha afikishwe mahakamani ilikuwa ni shilingi ngapi?na alikuwa amepanga kumpa kila mjumbe shilingi ngapi?
 
Kuna hawa Wabunge wa Mwanza, jimbo la Nyamagana, Ezekiel Wenje huyu Mbunge machinga wa Mwanza sehemu za makoroboi, mirongo, bugarika, na maeneo mengine awataki ata kumuona, wakati wa kampeni aliwambia mkinachugua nitahakikisha mnabaki sehemu zenu za kazi, baada ya kupata ubunge amewambia wahame, Ubunge wake umebakia kwenye maandamano tu.
Huyu Mbunge mwingine wa jimbo la Ilemela. Hayness Samson, huyu ndio hatakiwi kabisa Mwanza yeye tangu achagulie yeye anakaa Dar es Salaam, yeye kiguu na njia kwenye maandamano kila kukicha
Vipi pande ya pili wameshatekeleza ahadi walizozitoa?au ndiyo upo kazini mkuu?pole na kazi!!!
 
Vipi pande ya pili wameshatekeleza ahadi walizozitoa?au ndiyo upo kazini mkuu?pole na kazi!!!

Asante mkuu, pole na wewe na kazi, Kaka kwa hiyo upande wa pili wasipotekeleza ahadi zao nyie Chadema mnapata Excuse?
 
Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano. Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania.

Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.

Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza.

Maandamano ya CHADEMA yalifanikisha Serikali ya CCM kupunguza bei za sukari, kutoa mahindi katika magahala kwa nia ya kupunguza gharama za maisha kwa wananchi na hata bajeti ya mwaka huu kwa mara ya kwanza italenga kupunguza bei za nishati kama vile mafuta. Hii yote inatokana na jamii kupatiwa elimu kupitia mikutano na maandanmnao ya CDM. Hakuna elimu yoyote inayotolewa bure.
 
Asante mkuu, pole na wewe na kazi, Kaka kwa hiyo upande wa pili wasipotekeleza ahadi zao nyie Chadema mnapata Excuse?
Nakubaliana na wewe mkuu!lakini kinachonishangaza ni mtiririko wa hoja,kwani hoja ya msingi ilikuwa maandamano yanayotarajiwa kufanywa na BAVICHA,gafla mkaamia kwenye utekelezaji wa ahadi za wabunge wa CHADEMA,sasa hapo napata shida kuelewa!kwa nini tusijadiliane kwa hoja!na kwa nini tusijadili hoja specific iliyopo mezani?hatushindani lakini nijuavyo mimi ni kuwa tunabadilishana mawazo na hasa ukizingatia CDM na CCM ni vyama vya siasa nchi kwetu!naomba tujadiliane kwa hoja!!
 
mkuu huoni kama upo nje ya mada,kwa kuwa unachoongelea hakiendani ya hoja iliyopo mezani!!!ingekuwa vizuri kama ungeanzisha hoja maalum ili tuichangie vizuri!!jibu lako ni zuri sana lakini si kwa sawli hili,pole sana mkuu!!

Nachotaka kusema ni kuwa maandamano yanayokusudiwa hayatajibu utekeleza wa ahadi za Mbunge mmoja mmoja alizowaahidi wapiga kura wake
 
Wabunge wa CDM wasipochukua hatua za kusimamia maendeleo ya majimbo yao huenda wakaongoza hayo majimbo kwa kipindi kimoja tuu. Wengi wao wamejikita katika kukitangaza chama kitaifa (ushiriki wao kwenye maandamano sehemu mbali mbali nchini) badala ya kusimamia maendeleo sehemu walizopigiwa kura.

Madhalani tuchukulie Jimbo la Arusha mjini, moja ya wafuasi wakubwa wa CDM ni Wamachinga na ahadi kubwa aliyotoa Mh. Mbunge ni kujenga Machinga Complex mbili. Leo hii, ambapo imebaki takribani miaka minne na miezi mitatu kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2015 hakuna lolote (tangible) liliofanyika.

Mvuto alioanza na Mh. Mbunge wa Arusha mjini kama hataweka mbele utekelezaji wa yale aliyoahidi, huenda mvuto wake kwa wapiga kura ukafifia kwa stahili ile ile ya Raisi wetu wa sasa.

Nakusikitia sana kwa kutaka kuwapandikiza CDM uroho wa madaraka kama uliotalamaki CCM. Kwa maoni yangi ni sahihi kabisa kwa mbunge kuongoza kipindi kimoja kabala ajafikia hatua kuamini kuwa alizaliwa kuwa mbunge, ndio maan utawasikia wabunge wa CCM wakilalamika kuwa yupo mtu/watu wanajipitisha katika majimbo yao.

Kasome kifungu 63 b cha Katiba ya Tanzania ujielimishe kuhusu majukumu ya mbunge. Wanachohitaji watanzania ni kuchagua mtu mwenye kauli ya mwisho katika bajeti na mafungu ya fedha AMBAZO HUTUMIKA KUWALETEA MAENDELEO NA SIO UTARATIBU WA SASA WA KUCHAGUA WATU AMBAO WANAKWENDA KUWAPIGIA MAGOTI MAWAZIRI NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI.

KAZI WANAYOFANYA CDM YA KUSHINIKiZA MABADILIKO YA KATIBA KUPITIA KUWAPATIA WANANCHI ELIMU YA URAIA NDIO ITAWEZA KUFANIKISHA KUONDOA NAFASI ZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA AMBAO HAWANA TIJA YOYOTE NA kuwawezesha watanzania kuchagua wawakilisha ambao ni watendaji kama vile mameya watendaji badala ya Halamshauri kuongozwa na wakurugenzi ambao ni vibaraka wa Serikali kuu.
 
Nachotaka kusema ni kuwa maandamano yanayokusudiwa hayatajibu utekeleza wa ahadi za Mbunge mmoja mmoja alizowaahidi wapiga kura wake

Kwa mujibu wa Ibara ya 63 b ya Katiba ya Tanzania kazi za Mbunge ni kuismamia na kuishauri Serikali. Hakuna popote palipotajwa kuwa mbunge ataleta maendelo katika jimbo lake. Hiyo ni aina fulani ya ufisadi na ubinafsi kwa wananchi wa jimbo fulani kutaka mbunge alete maendelo katika jimbo lao tu na kuacha kuisimamia Serikali ipasavyo. Ndio maan madini na raslimali za Tanzania hazina wasimamizi kwa kuwa wale wanaochaguliwa kama wawakilishi wa wananchi (Wabunge) katika kuismamia Setikali yenye mamalka ya kuisimamia fedha, madini na raslimali zote za taifa wako busy kutafuta maendelo ya majimbo binafsi tena mabya zaidi kwa kuwapoigia magoti mawaziri wa Serikali waliyopaswa kuisimamia!!!
 
Back
Top Bottom