BAVICHA kuandaa maandamano nchi nzima

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,932
32,337
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la CHADEMA (BAVICHA), John Heche amesema ataandaa mikutano itakayofanyanyika nchi nzima kulaani kitendo cha kukamatwa na kuwekwa ndani mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana kwa njia ya simu akiwa Mwanza, Heche alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lilitolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa la kuruhusu vijana wa chama hicho kuandamana nchi nzima.

"Katibu ameishatoa tamko la kuruhusu maandamano nchi nzima mimi naunga mkono tamko hilo natarajia kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mikutano hiyo kwa baadhi ya mikoa." alisema

Heche na kuongeza maandamano yanatarajia kufanyika wakati wowote.

SOURCE: MWANANCHI JUNI 8, 2011
 
Wabunge wa CDM wasipochukua hatua za kusimamia maendeleo ya majimbo yao huenda wakaongoza hayo majimbo kwa kipindi kimoja tuu. Wengi wao wamejikita katika kukitangaza chama kitaifa (ushiriki wao kwenye maandamano sehemu mbali mbali nchini) badala ya kusimamia maendeleo sehemu walizopigiwa kura.

Madhalani tuchukulie Jimbo la Arusha mjini, moja ya wafuasi wakubwa wa CDM ni Wamachinga na ahadi kubwa aliyotoa Mh. Mbunge ni kujenga Machinga Complex mbili. Leo hii, ambapo imebaki takribani miaka minne na miezi mitatu kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2015 hakuna lolote (tangible) liliofanyika.

Mvuto alioanza na Mh. Mbunge wa Arusha mjini kama hataweka mbele utekelezaji wa yale aliyoahidi, huenda mvuto wake kwa wapiga kura ukafifia kwa stahili ile ile ya Raisi wetu wa sasa.
 
Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano. Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania.

Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.

Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza.
 
Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano, Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania, Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.
Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza
Umetumwa na NAPE naona unawza kwa kutumia makamasi wewe,haya wasalimu masaki huko,na mdogo wako anayesoma Marekani
 
Haina haja ya maandamano kama Mbowe ametoka wapambane Bungeni saizi kupigania maendeleo.
 
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche amesema ataandaa mikutano itakayofanyanyika nchi nzima kulaani kitendo cha kukamatwa na kuwekwa ndani mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana kwa njia ya simu akiwa Mwanza, Heche alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lilitolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willirbrod Slaa la kuruhusu vijana wa chama hicho kuandamana nchi nzima.
"Katibu ameishatoa tamko la kuruhusu maandamano nchi nzima mimi naunga mkono tamko hilo natarajia kurejea Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza maandalizi ya mikutano hiyo kwa baadhi ya mikoa." alisema Heche na kuongeza maandamano yanatarajia kufanyika wakati wowote.
SOURCE: MWANANCHI JUNI 8, 2011

Kwa nini yawe ya kulaani kukamatwa kwa Mbowe na sio wabunge wa upinzani kwa ujumla wake? Tuondokane na fikra za mwenyekiti kwani hata kukamatwa kwa Zitto na Esterina Kilasa ni mbinu chafu za kudhoofisha upinzani.

Yakiisha hayo, yaandaliwe mengine ya kulaani uonevu wa serikali ya CCM kutumia vyombo vya serikali kwa kuwatesa wananchi (TRA na Polisi).
 
Wabunge wa CDM wasipochukua hatua za kusimamia maendeleo ya majimbo yao huenda wakaongoza hayo majimbo kwa kipindi kimoja tuu. Wengi wao wamejikita katika kukitangaza chama kitaifa (ushiriki wao kwenye maandamano sehemu mbali mbali nchini) badala ya kusimamia maendeleo sehemu walizopigiwa kura. Madhalani tuchukulie Jimbo la Arusha mjini, moja ya wafuasi wakubwa wa CDM ni Wamachinga na ahadi kubwa aliyotoa Mh. Mbunge ni kujenga Machinga Complex mbili. Leo hii, ambapo imebaki takribani miaka minne na miezi mitatu kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2015 hakuna lolote (tangible) liliofanyika. Mvuto alioanza na Mh. Mbunge wa Arusha mjini kama hataweka mbele utekelezaji wa yale aliyoahidi, huenda mvuto wake kwa wapiga kura ukafifia kwa stahili ile ile ya Raisi wetu wa sasa.

Kweli mkuu, mambo ya ajabu kabisa kila kukicha wabunge wa Chadema wao na maandamano nchi aijengwe na maandamano
 
Umetumwa na NAPE naona unawza kwa kutumia makamasi wewe,haya wasalimu masaki huko,na mdogo wako anayesoma Marekani

Angalia mimi nimejiunga lini JF na huyo Nape kachaguliwa lini, jenga hoja usilete porojo
 
Heche mwenyewe kachaguliwa kwa rushwa, zengwe, (Bavicha) leo na yeye anataka kuwaingiza watu barabarani hii kweli ni Deceit kabisa
 
Wabunge wa CDM wasipochukua hatua za kusimamia maendeleo ya majimbo yao huenda wakaongoza hayo majimbo kwa kipindi kimoja tuu. Wengi wao wamejikita katika kukitangaza chama kitaifa (ushiriki wao kwenye maandamano sehemu mbali mbali nchini) badala ya kusimamia maendeleo sehemu walizopigiwa kura.

Madhalani tuchukulie Jimbo la Arusha mjini, moja ya wafuasi wakubwa wa CDM ni Wamachinga na ahadi kubwa aliyotoa Mh. Mbunge ni kujenga Machinga Complex mbili. Leo hii, ambapo imebaki takribani miaka minne na miezi mitatu kabla ya kampeni za uchaguzi wa 2015 hakuna lolote (tangible) liliofanyika.

Mvuto alioanza na Mh. Mbunge wa Arusha mjini kama hataweka mbele utekelezaji wa yale aliyoahidi, huenda mvuto wake kwa wapiga kura ukafifia kwa stahili ile ile ya Raisi wetu wa sasa.

Hapo umenena kweli,na kwa muhutasari wabunge wengi wa CDM uchaguzi ujao hawatoweza kupita, pia viti maalum vitaondoshwa kitu ambacho kitakuwa ni pigo kubwa sana kwa chadema, kwani itakuwa imetengeneza wingi wa wabunge waliong'atuliwa na kuwafanya washinde kijiweni pale kinondoni kama slaa, na mbaya zaidi watakuwa hawewezi kulipwa kama Dr anavyokula kwa mlija.
 
wameanzisha thread halafu wanachangia wao wenyewe .... teh teh teh

napita tuu kwa kupotezea

kazi njema
 
Endeleeni na thread yenu, maana ninyi wenyewe mlioanzisha mnatosha, bado Faiza Foxy anakuja.
 
  • Thanks
Reactions: LAT
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. wajinga wameshaliwa. watu wanajifanya mabalozi wa kukijibia Chama humu, kumbe hawakijui chama wala hakiwajui wao. Unacheza wewe! Mtu ameshindwa kwenye dini ndo aje aweze kwenye siasa?
 
Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano. Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania.

Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.

Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza.

Niliwaambia kwenye nyuzi nyingine kule watumie "scientific approach" kwenye siasa. Hawajui kuwa ngoma ikivuma sana hupasuka. Hawana jipya na hao wanaoandaa maamndamo wamejipatia njia moja ya kujipatia posho kiulaini.
 
Heche mwenyewe kachaguliwa kwa rushwa, zengwe, (Bavicha) leo na yeye anataka kuwaingiza watu barabarani hii kweli ni Deceit kabisa

Halafu rushwa zenyewe walizianika humu JF mpaka za shillingi 1,500/= Wananchekeshaa!
 
Halafu rushwa zenyewe walizianika humu JF mpaka za shillingi 1,500/= Wananchekeshaa!

yatawashinda ya bavicha mmeshindwa kuzi allocate raslimali za uvccm kwa vijana wenu wamechoka kama matambala ya deki, bavicha ni zaidi ya Nape na uvccm na vitega uchumi vyenu vya kipumbafu mmeshindwa hata kuisaidia bodi ya mikopo itoe huduma bora kwa vijana tz.
 
Watanzania wenye uchungu na nchi yetu, pesa yetu walipa kodi (Ruzuku) inakwenda tena kwenye maandamano wanakwenda kugawana posho za maandamano. Chadema wamefanya maandamano kama Sekta yao ya kugawania pesa zetu Watanzania.

Takwimu zinaonyesha kila maandamano yanatumia zaidi ya milioni 40, na nchi hii ilivyokua kubwa mpaka waimalize kwa maandamano sijui watatumia kiasi gani cha pesa zetu Watanzania.

Si bora hizo pesa wangechimba visima kila jimbo walioshinda uchaguzi au wangenunua madawati watoto wetu wapate pakusomea wananchi wangewapongeza.

Kaka, Unalipa kodi wewe? in person
 
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO. wajinga wameshaliwa. watu wanajifanya mabalozi wa kukijibia Chama humu, kumbe hawakijui chama wala hakiwajui wao. Unacheza wewe! Mtu ameshindwa kwenye dini ndo aje aweze kwenye siasa?

Nape kawatuma eti, atachemka tu! Kama mvua ya masika imeshindwa umande utaweza? Dr. Slaa ni mtu makini ya mungu anayajua na hata ya dunia sasa ndie kiongozi bora na kiongoz bora ni yule anaechukia maovu na ufisadi wa viongoz wa ccm wasiomuogopa mungu.
 
Back
Top Bottom