BAVICHA Arusha: yamuonya mkuu wa mkoa wa Arusha

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Taarifa kwa umma



Ndugu waandishi wa habari


Hivi karibuni kwa zaidi ya mwezi na nusu sasa kumejitokeza vijana wanaopita kwenye maeneo mbalimbali katika mji wa Arusha,wakitukana na kukikashifu chama chetu cha CHADEMA,matusi na kashfa hizi ni matokeo ya ripoti ambayo iliandaliwa na vijana watano wasomi wa chuo kikuu,waliotumwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana Malongo Magesa.Itakumbukwa kuwa Mkuu huyu wa mkoa wa Arusha aliletwa Arusha kwa sababu maalum na moja ya sababu hizo ni kukidhoofisha CHADEMA, hivyo aliunda kikosi kazi hicho ambacho hata hivyo miongoni mwa vijana hao watano watatu ni vijana wangu,walizunguka Arusha,na kumletea ripoti MBOVU ambayo kwa UPOFU wake naye ameifanyia kazi,moja ya ushauri waliompa ni kuwatumia wanachama wa CHADEMA kuwatukana Viongozi wao na chama,hivyo Mkuu wa mkoa pamoja na Meya Feki wa Kichina,wakawarubuni vijana wawili wanachama wa CHADEMA ambao ni Niko na Kiyeuyeu. Vijana hawa Niko Na Kiyeuyeu ambao wanalipwa na Mkuu wa Mkoa pamoja na Meya wa Kichina wamepewa pikipiki pamoja na Tshs 20,000 kila siku kwa kazi hiyo ya siasa chafu.Tunatoa Rai wa wakazi wote wa Arusha kuwapuuza Vijana hawa ambao njaa zinawasumbua hadi kufikia kujisaliti wenyewe.


BAVICHA mkoa wa Arusha tunalaani aina hii ya siasa,na tunamtaka mkuu wa Mkoa aache kutumia ofisi ya umma kwa maslahi ya ccm vinginevyo aachie ofisi ya Umma.Tunatambua kuwa mkuu wa Mkoa ana majukumu yake lakini Bwana Malongo Magesa amekuwa akiingilia utendaji wa Halimashauri ya manispaa ya Arusha,na kuwa kama Mkurugenzi,hivi karibuni alizuia Tenda ya kukusanya ushuru wa Mabango kwa kuwa mzabuni aliyeshinda sio chaguo lake na badala yake akataka kampuni ya ndugu yake ndio ipewe Tenda wakati imetender kwa hela ndogo zaidi.


Tangu ateuliwe kushika wadhifa huu huyu RC amekuwa Kituko hapa Arusha, ameunda zaidi ya Tume tatu kuchunguza ubadhirifu ulio wazi wa Halmashauri ya manispaa ya Arusha,na hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa huku tume hizo zikiwa zimetumia mamilioni ya walipa kodi maskini wa Arusha

BAVICHA tunamtaka afanye yafuatayo

1. Aache mara moja kutukana CHADEMA na Viongozi wake vinginevyo tutatangaza mgogoro naye

2. Aeleze umma wa Arusha juu ya Ripoti tatu za tume alizounda za kuchunguza ubadhirifu mkubwa katika Halimashauri ya manispaa ya Arusha, aeleze hatua gani alichukua

3.Achague kuwa Mkuu wa mkoa au Mkurugenzi




……………………..
Nanyaro Ephata
Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Arusha
14/9/2012
 
hilo nalo neno!.....mwambia ata a2mie nn kuwarubn wana arush, maisha tunaish watz yanawaumbua.
 
Pamoja kamnda yeye sio ndio aliyewashauri UVCCM pwani waseme kuwa Rais ajeye hatatokea kaskazini? ila kwa Arusha atajuta kuletwa huko
 
Huyu mkuu wa mkoa namwonea huruma sana. Akili zake ni za kizamani sana. Technic zake ni kama za Mwigulu. Hajawahi kusema ni nini kilichowaua vijana watano wa chadema huko Nduruma, mauaji ya mwenyekiti wa cdm usa na anajua yeye ndiye m/kiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa! Tukianza kuhoji, ofisi haita kalika! Atajuuuuuta.........!
 
Kwako Magesa Mulongo... Imeandikwa na wenye hekima..."Nchi hii ni mali yetu sote, hakuna mwenye hati miliki...hata chama tawala hakina hati miliki na nchi hii... Pia imeandikwa ...Wanaodhani kuwa Chama chao kitatawala mpaka atakaporudi Yesu hawajasoma historia, ni vipofu wa jazanda... Magesa Mulongo rudi shule kasome topic inayoitwa "Managing Changes".
 
Nanyaro kesho twende Usa tukayaseme haya pamoja na kamanda Nassari
 
Siasa za huyu RC hazipaswi kutushangaza. Kama ilivyobainishwa na mleta mada, ni wazi huyu alipelekwa Arusha kwa kazi maalum ya kuithibiti CHADEMA, tena kwa gharama na njia yoyote.


Kama vile ilivyo ngumu kwa CCM kuachana na rushwa/ufisadi ktk kada zake zote kadhalika ni vigumu sana kwa CCM kuacha siasa zake za maji taka.

Hivyo niwaombe makamanda hapo Arusha uongozi wa CHADEMA (M) pamoja na wadau wengine kama akina Nanyaro, Msando, Crashwise, Mungi, Liverpool na wengine mfanye yafuatayo:-

1) Keep your focus on major objectives in that particular region. Part of such workings by the puppet called RC is to create chaos, confusion and mistrusts among CHADEMA members. Always remember that UMOJA NI NGUVU, so keep it.

2) We must work on bridging the generation gap (especially the youth) regarding ethos and leadership ethics. Lazima mtambue kuwa vijana wengi hawana mafunzo/elimu wala makuzi ya kiuongozi na/au kisiasa.

3) Be the changes you want to see. I mean live the talk by walk the vision.

Nionanvyo mimi, kama mkikubali kushuka chini (degraded) mpaka ktk level yao, je nani atakayeweza kutofuatisha kati yenu na CCM? Hamuwezi na haifai kushindana na kichaa kujipaka mavi.
 
  • Thanks
Reactions: ral
Nasikia mna mkutano tarehe 15 tumieni nafasi hiyo kumlipua ila msitumie njia kama za akina mwigulu na lusinde. Pambanueni hoja zenu vizuri na msijenge chuki. Waacheni wao waendelee na matusi nyie pambaneni kwa hoja hasa na kuzinadi vizuri sera za Cdm.




Sisi sote ni ndugu tatizo ni ccm!!!!
 
Lula tu pesa za walipa kodi mtu kakaa pala hajiamini kama nini na kazi yake ni kulinda miradi ya Jakaya ni Ridhiwani haya tutaona mwisho wake
 
Muda wa ccm mahali pale haupo tena hata aje nani .Tumesema,tunasema,na tutaendelea kusema.CCM ARACHUGA NITOLEE
 
Watanunua wangapi na hadi lini? Wananchi wameshawakataa ccm hizi fedha wanazowalazimisha wafanyabiashara kuwachangia nao wanakwenda kuzitumia kuhonga na kununua wanasiasa wa upinzani zinakaribia kukata.
Hapo ndipo watakapolia na kusaga meno hasa huyo chemba na vuvuzela nape.
 
Back
Top Bottom