Baunsa wa night club.

Jaguar

JF-Expert Member
Mar 6, 2011
3,438
1,026
Baunsa wa night club alienda kutibiwa mgongo kwa doctor. Doctor baada ya vipimo akamuuliza baunsa ilikuwaje mpaka akapata mshtuko wa uti wa mgongo.BAUNSA;Nilipoingia ndani asubuhi nikitokea kazini,nilisikia makelele chumbani kwangu nikajua mke wangu yupo na mwanaume mwingine,nikazama chumbani lakini sikumkuta mtu,mara nikasikia mlango wa sebuleni umefunguliwa kwa fujo,nilipochungulia kupitia dirishani nikamwona mtu anakimbia huku anavaa shati,nikachukua fridge nikamrushia nikiwa ghorofa ya tatu,hapo ndipo niliposhtua uti wangu wa mgongo.{Alipomaliza tu kauli yake,akaingia mgonjwa mwingine kaharibika kama kagongwa na gari}. Doctor akamhoji;vp ndugu,nini kimekusibu?.MGONJWA;Nilisahau kuweka alarm asubuhi nikachelewa kuamka kwenda kazini,kazi yenyewe niliajiriwa jana tu baada ya kukaa jobless kwa muda mrefu,nikatoka nje huku navaa nguo,mara nikapondwa na fridge kichwani.{Mara akaingia mgonjwa wa tatu akiwa na hali mbaya kuliko waliomtangulia}.Akaanza kujieleza,'Doctor,mimi nilikuwa nimejibanza ndani ya fridge,mara ghafla lile fridge likabebwa na kutupwa kutoka ghorofa ya tatu mpaka chini'.
 
Hii nimeisikia leo kwenye Radio One, kipindi cha habari nyepesinyepesi!! kumbe kadokoa huku!!!
 
Hayaaa! Knockout hyo hapo meen.wote wamebug step kila mmoja acmame kweny nafas yake.Dr refa mm promota
 
Kama mi ndo baunsa naanza ku deal na mbaya wangu hapo hapo, huyu jamaa niliyemdondoshea frige kwa bahati mbaya nitamwomba msamaha baada ya kumaliza shughuli yangu ya kumwazibu mbaya wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom