Elections 2010 Batilda buriani hakuwa na jipya?

Kilembwe

JF-Expert Member
Aug 19, 2009
2,056
1,598
Jana nilikuwa naangalia kipindi kimoja katika kituo cha Televisheni cha TBC1 kiitwacho MCHAKATO MAJIMBONI, na jana walikuwa jimbo la Arusha mjini, niliwaona wagombea wote wa ubunge jimbo lile, alikuwepo Lema ( Chadema) Lyimo (TLP) , Salim (CUF) na yule bwana mdogo wa Chama cha Demokrasia Makini (CDM?), lakini ajabu sikumuona Mh Batilda Buriani Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM. Nilijiuliza na napenda pia wana JF mnisaidie hili, je Buriani kutotokea pale hakuwa na taarifa, aliogopa kuulizwa maswali, alidharau au hakuwa na jipya la kuwaambia wana Arusha?
 
Ni wazi mkuu pamoja na kutkuwa na jipya ulimsikiliza Bwana Lema ? Hana mchezo . Batilda angeeishia kulia machozi jukwaani. Bora angemwachia Mrema matatizo yake. Batilda is a failure Doctor from the start.
 
Batilda Buriani ni waziri na Lema ni mtu wa kawaida,kwahiyo waziri asingevumilia mashambulizi ya mtu wa kawaida Lema
Kwasisi tunayemjua Lema si mchezo mdomoni,ni kama mtu kameza cd za habari njema kwa watanzania
.
 
Batilda aliingia mitini (period). Tunataka mdahalo wa wagombea uraisi (najua JK pia ataingia mitini kama kawaida).
 
Wanaogopa midahalo kwa kuwa hawana sera. JK hathubutu kusimama jukwaa moja na Dk. Slaa. Usishangae Batilda kusepa.
 
Soma The Citizen page 4 ya leo. Batilda na CCM (Arusha) wanasema mdahalo sio sehemu ya mkakati wao kuwafikia wapiga kura! Like father like daughter!!
 
ofcoz, hawa kijani bin manjano wote hawana jipya, mwaka huu hata wajaradie si ndo walimu hakuna cha tiki wala nini.
 
lakini nilifurahishwa zaidi na yule jamaa wa TLP Bwana Max Lyimo alionyesha uwezo mkubwa.
huyo lema alikuwa ni kujisifu tu sikuona lolote,
kulikuwa na vibaraka wa kuharibu hali ya hewa pale lakini mwongozaji Shabani Kissu alijitahidi kusawazisha mambo
 
Ukiwa unaongoza kwa mbali usiende kwenye mdahalo, huo ndio ushauri wa watu wa PR. Angalia 1995 jinsi mdahalo ulivyo mharibia Mrema na kumpandisha Mkapa.

UK mwaka 2010 mdahalo ulimharibia Cameron mpaka ikamsababaishia kushindwa kupata ushindi wa moja kwa moja mpaka kuingia kwenye coalition. Mwaka 1992 mdahalo ulimponza rais Bush pale aliposhambuliwa sana na Perot

Kama ni underdog, mdahalo ni mzuri maana huna cha kupoteza na unaweza kurusha konde likamtoa mtu knockout.

Nafikiri JK na baadhi ya wabunge wenye uhakika na nafasi zao wanalijua hilo. Hawataki kwenda kwenye matembezi yasiyo na umuhimu na wakateleza kwenye mvua na kuadhirika barabarani.
 
Mkulima said:

Mkulima,

..umepatia 100%.
 
Jana nilikuwa naangalia kipindi kimoja katika kituo cha Televisheni cha TBC1 kiitwacho MCHAKATO MAJIMBONI, na jana walikuwa jimbo la Arusha mjini, niliwaona wagombea wote wa ubunge jimbo lile, alikuwepo Lema ( Chadema) Lyimo (TLP) , Salim (CUF) na yule bwana mdogo wa Chama cha Demokrasia Makini (CDM?), lakini ajabu sikumuona Mh Batilda Buriani Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM. Nilijiuliza na napenda pia wana JF mnisaidie hili, je Buriani kutotokea pale hakuwa na taarifa, aliogopa kuulizwa maswali, alidharau au hakuwa na jipya la kuwaambia wana Arusha?

Amesema alikuwa mluteri akangoja wee kupata mume hakuna aliyejitokeza akaja usatadh akamwoa huyo akahamia uislam.....sikujua hili kuwa akina mama hungojea kanisani waolewe
 
Ukiwa unaongoza kwa mbali usiende kwenye mdahalo, huo ndio ushauri wa watu wa PR. Angalia 1995 jinsi mdahalo ulivyo mharibia Mrema na kumpandisha Mkapa.

UK mwaka 2010 mdahalo ulimharibia Cameron mpaka ikamsababaishia kushindwa kupata ushindi wa moja kwa moja mpaka kuingia kwenye coalition. Mwaka 1992 mdahalo ulimponza rais Bush pale aliposhambuliwa sana na Perot

Kama ni underdog, mdahalo ni mzuri maana huna cha kupoteza na unaweza kurusha konde likamtoa mtu knockout.

Nafikiri JK na baadhi ya wabunge wenye uhakika na nafasi zao wanalijua hilo. Hawataki kwenda kwenye matembezi yasiyo na umuhimu na wakateleza kwenye mvua na kuadhirika barabarani.

Heshima kwako Mkulima,

Mkuu nakubaliana na hoja yako 100%,Hapa ndipo ninapolipenda jamvi unakutana na vichwa haswa.
 
lakini nilifurahishwa zaidi na yule jamaa wa TLP Bwana Max Lyimo alionyesha uwezo mkubwa.
huyo lema alikuwa ni kujisifu tu sikuona lolote,
kulikuwa na vibaraka wa kuharibu hali ya hewa pale lakini mwongozaji Shabani Kissu alijitahidi kusawazisha mambo

Heshima kwako Ng'azagala,

Mkuu mgombea wa TLP nimeshamsikiliza zaidi ya mara tatu kabla ya mdahalo nilishawahi kumzunguzia hapa jamvini ni aina ya watu wanaoweza kujenga hoja za maana na kuzitetea bila kutetereka.Inasikitisha sana wakati mwingine wagombea wenye akili si lazima washinde hasa kwenye nchi zetu changa zilizogubikwa na rushwa na uhoza wote unaoufahamu.

Lema G anafaa sana kazi ya uMC harusi,mazishi na nk,ni aina ya wanasiasa wenye kukosa kipaji,uwezo na elimu ya kutosha.Ukimsikiliza vyema Lema alitamka bayana yeye ni mbunge tayari wengine ni wagombea.Maana yake haitaji kura kwakuwa tayari ni mbunge,wengine ni wagombea maana yake watahitaji kura za wapiga kura kwa kuwa wao ni wagombea.Si rahisi kugundua Lema kafanya kosa ikiwa ulikuwa ukiangalia mdahalo ukiwa na mtu unayemshabikia/unayemtaka.mwanasiasa mahiri hawezi kutamka maneno ya dharau kwa wapiga kura ilihali anajua kura zitapigwa mwezi October 2010 na anahitaji kura hizo ili awezekupata ubunge anaobwabwaja tayari keshaupata.Leo wapiga debe wa Mama Batilda Buriani na Maxmillan Lyimo wanaomba wananchi wampigie wagombea wao kwa maelezo mgombea wa CHADEMA hana haja ya kura zao kwasababu tayari ni mbunge.
 
Ukiwa unaongoza kwa mbali usiende kwenye mdahalo, huo ndio ushauri wa watu wa PR. Angalia 1995 jinsi mdahalo ulivyo mharibia Mrema na kumpandisha Mkapa.

UK mwaka 2010 mdahalo ulimharibia Cameron mpaka ikamsababaishia kushindwa kupata ushindi wa moja kwa moja mpaka kuingia kwenye coalition. Mwaka 1992 mdahalo ulimponza rais Bush pale aliposhambuliwa sana na Perot

Kama ni underdog, mdahalo ni mzuri maana huna cha kupoteza na unaweza kurusha konde likamtoa mtu knockout.

Nafikiri JK na baadhi ya wabunge wenye uhakika na nafasi zao wanalijua hilo. Hawataki kwenda kwenye matembezi yasiyo na umuhimu na wakateleza kwenye mvua na kuadhirika barabarani.

I beg to differ. It's not always entirely so. Jimmy Carter -- front runner in 1976 US Elections was not affected by mdahalo at all, in fact it destroyed Gerald Ford. This was also true with J.F. Kennedy in 1960 elections, the debate was catastrophic to Richard Nixon.
 
Ukiwa unaongoza kwa mbali usiende kwenye mdahalo, huo ndio ushauri wa watu wa PR. Angalia 1995 jinsi mdahalo ulivyo mharibia Mrema na kumpandisha Mkapa.

UK mwaka 2010 mdahalo ulimharibia Cameron mpaka ikamsababaishia kushindwa kupata ushindi wa moja kwa moja mpaka kuingia kwenye coalition. Mwaka 1992 mdahalo ulimponza rais Bush pale aliposhambuliwa sana na Perot

Kama ni underdog, mdahalo ni mzuri maana huna cha kupoteza na unaweza kurusha konde likamtoa mtu knockout.

Nafikiri JK na baadhi ya wabunge wenye uhakika na nafasi zao wanalijua hilo. Hawataki kwenda kwenye matembezi yasiyo na umuhimu na wakateleza kwenye mvua na kuadhirika barabarani.

....asante mkuu kwa observation iliyotulia.....
 
Back
Top Bottom