Basil Pesambili Mramba

Nipohaitena

Member
Jan 6, 2011
22
0
kuna tetesi kuwa aliyekuwa mbunge wa rombo ameteuliwa kuwa balozi nchi ya Uswisi. kama kuna mwenye taarifa yoyote. inaniwia vigumu kukubali kutokana na kesi yake inayo endelea.

nawasilisha Ps.P
 
Wewe ni mgeni na nchi hii nini!! Mbele ya sisiem hakuna uhusiano kati ya cheo na kesi mahakamani!! Inawezekana kweli mramba akaukwaa ukubwa hata kama siyo ubalozi. Ebu fikiria makongoro mahanga, pamoja na kukutwa na kithibitisho cha uwizi wa kura, bado ameteuliwa kuwa naibu waziri!!!!!!
 
Tutapeleka taarifa uswiss wamkatae kwa vile ni mtuhumiwa ana kesi nyingi tu za kujibu. Case closed. Mwambieni JK hatujalala bado asitufanye sisi wajinga.
 
Haahaaa! Sasa hapo nani ataonekana hajui analofanya? Mi sisemi maana kichwa changu najaribu kukitafutia kitabu chenye mahesabu magumu nikichangamshe kuliko kutembea mabega juu wakati kichwani niko empty na bado nalinga kuwa naongoza watu.
 
Sina taarifa ila kwa ccm sitashangaa! Kwao hakuna mwenye hatia wala kosa la jinai as long as yuko nao!
 
Mzee hilo haliwezekani, hawawezi kuwa wajinga kiasi hicho. Hata Mramba mwenyewe atakuwa mjinga akikubali kwani anatafuta nini tena?
 
labda taarifa ziende umoja wa mataifa (un) ambako tayari
mama migiro yupo kwani ubalozi uliopo geneva unahusika na
umoja wa mataifa na mshirikaa mengine ya kimataifa na sio uhusiano na serikali
ya uswiss.

Tutapeleka taarifa uswiss wamkatae kwa vile ni mtuhumiwa ana kesi nyingi tu za kujibu. Case closed. Mwambieni JK hatujalala bado asitufanye sisi wajinga.
 
Back
Top Bottom