Basi la Adventure Laungua moto (Mwanza to Kigoma)

Mwanaukweli

JF-Expert Member
May 18, 2007
4,786
1,710
Basi la Adventure toka Mwanza kwenda Kigoma lililoondoka Mwanza leo asubuhi saa 11.30 alfajiri, limepata ajali ya kuungua moto katika kijiji cha Nyantakara, karibu na Runzewe.

Hakuna mtu aliyepoteza maisha, ila kuna watu wana majeraha ya moto, na wengine wamevunjika viungo kutokana na kuruka toka kwenye basi kujisalimisha. Abiria wote wamepoteza mali zao zote walizokuwa nazo ambazo zimeteketea kwa moto.

Chanzo cha moto hakijajulikana, lakini basi lenyewe lilikuwa chakavu sana, na huenda ni hitilafu za umeme wa basi.

Kwa sasa abiria wamekwama na hawajui wataendeleaje na safari yao.
 
Mimi siko kwenye site ya ajali, ila nimejulishwa na ndugu yangu ambaye amenusurika.
 
Poleni aisee, simamisheni magari mengine
Hapo lazima walale njiani kwa kuwa kwa muda huu hawawezi kupata magari ya Kigoma. Hapo walipo ni Highway ya kwenda Rwanda, Wilaya ya Bukombe. Magari mengi yanaelekea Rusumo, Ngara na Biharamuro na si Kigoma.

Option ni kuchukua Noah mpaka Nyakanazi, toka Nyakanazi tena kutafuta Hiace mpaka Kibondo ndio wapate connection ya Kigoma.

Ingefaa kuwe na sheria ya kuwalazimisha wenye mabasi kuwakodia mabasi abiria wa namna hii.
 
kwa sasa nipo hapa eneo la tukio ,basi ni T 293 BDP. Bado moto na moshi ni mwingi. Watu wapo wanang'oa vyuma chakavu. Wengine wameungua mikono kwa kushika vyuma vya moto, hamna hata mgambo
 
kwa sasa nipo hapa eneo la tukio ,basi ni T 293 BDP. Bado moto na moshi ni mwingi. Watu wapo wanang'oa vyuma chakavu. Wengine wameungua mikono kwa kushika vyuma vya moto, hamna hata mgambo

Mkuu chitambikwa tueleze zaidi juu ya abiria walionusurika kama bado wapo hapo, na hali za majeruhi.
 
Last edited by a moderator:
Poleni aisee, simamisheni magari mengine

mimi nishahidi nanimeokoa m2 mmoja alikua amevunjika muguu nikwamba bas zilikua ta2 nazilikua zinaongoza zote zakampuni moja zikitokea mwanza kwenda kigoma ilipo pata ajari moja zingine zilisimama ikabidi zile gari 2 zigawane wale wasafiri kwahiyo wote wamesha ondoka hakuna aliye baki hapo
 
Thanks mkuu kwa update.
 
Hapo lazima walale njiani kwa kuwa kwa muda huu hawawezi kupata magari ya Kigoma. Hapo walipo ni Highway ya kwenda Rwanda, Wilaya ya Bukombe. Magari mengi yanaelekea Rusumo, Ngara na Biharamuro na si Kigoma.

Option ni kuchukua Noah mpaka Nyakanazi, toka Nyakanazi tena kutafuta Hiace mpaka Kibondo ndio wapate connection ya Kigoma.

Ingefaa kuwe na sheria ya kuwalazimisha wenye mabasi kuwakodia mabasi abiria wa namna hii.

mkuu hapo umekosea hii niwilaya yabiharamulo nasiyo yabukombe nakijiji ninyantakara nikweli niabarabara kuu inayo unanisha nchi 4 manaake burund ruwanda uganda nacongo
 
mkuu hapo umekosea hii niwilaya yabiharamulo nasiyo yabukombe nakijiji ninyantakara nikweli niabarabara kuu inayo unanisha nchi 4 manaake burund ruwanda uganda nacongo
Thanks tena mkuu.

Nilipigiwa simu toka eneo na nimeandika kama nilivyoelezwa.

Asante kwa ufafanuzi.
 
Zaidi ya abiria 10 wamejeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya Adventure lenye namba za usajiri T 294 ABD aina ya Scania walilokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto katika kijiji cha Nyantakala wilayan Biharamulo mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea jana saa 4:30 asubuhi wakati basi hilo likitokea mkoani Mwanza kwenda Kigoma.

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa kwenye hospitali Teule ya Wilaya ya Biharamulo wamejeruhiwa vibaya akiwemo wakala wa kukatisha tiketi wa basi hilo, Dotto Tryphone (30), ambaye amevunjika miguu wakati wakijinasua kutoka kwenye basi hilo.

Kwa mujibu wa wakala huyo, basi hilo lilikuwa na abiria 54 waliokuwa wamekaa kwenye viti na abiria ambao hawakuweza kutambulika idadi yao waliokuwa wamesimama kutoka mwisho wa gari hadi mlangoni kutokana na basi hilo kujaza abiria zaidi ya uwezo wake.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Paulo Alex Kalangi, alisema atatoa taarifa baadaye kwa kuwa alikuwa safarini kwa ajili ya ufuatiliaji wa ajali hiyo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo majeruhi wamesema chanzo cha ajali hiyo ni baada ya basi hilo kufika kwenye tuta la kuzuia mwendo kasi ambapo ghafra walianza kuona moshi ukitokea ndani ya basi kabla ya kushika moto na kuanza kuteketea.

Dereva wa basi hilo ambaye hakutambulika jina lake haijajulikana kama alikimbia au aliteketea kwenye basi hilo mara baada ya kutokea ajali hiyo.

Mganga Mkuu msaidizi wa hospitali hiyo, Dk. Gabriel Mashauri, alisema amepokea majeruhi tisa na kwamba saba kati yao walikuwa katika hali mbaya, lakini bado wanaendelea kupatiwa matibabu.

Aliwataja majeruhi waliolazwa kuwa ni Phinihas Elias (37), Pius John(21), Msigwa Isaya (18), Johary Chapa (23),Josephina Ngereza (46), Rashidi Mahonda (48) na Eles Ngereza(60).

Waliovunjika miguu wametambulika kwa majina ya Dotto Tryphone (30) mkazi wa Nyakanazi na Zainabu Issa, wote wamevunjika miguu ya kushoto.

Back
Top Bottom