Bashe, Kigwangalla vita kali Nzega. Bashe amsasambua Mh. Kigwangalla

wee bashe unshutumiwa sio raia hapa,sioni sababu ya kuingilia sana mambo yetu ya ndani,endelea kufanya biashara kama wasomali wenzako,ipo siku mtaondoka hapa
 
Mi ni memba wa wanabidii huyu mbunge anachonga sana, na ni mwongo sana na ukweli umejulikana.
 
Hii makala kwa kusema ukweli hii ishu ya Kingwangala kuchukua jina la mtu mwingine na kulitumia kama lake imeishasemwa sana it's a pity and shame kiukweli jambo likisemwa sana basi kwa namna moja au nyingine inawezekana lina chembe chembe ya ukweli ndani yake inawezekana Bashe naye has his own mission maana naona ameandika kwa hisia sana ila i believe 2015 jimbo la Nzega litashika moto kwa haya ambayo tunayaona yanatokea sasa hivi
 
Bashe ni Kichwa kumbe!

Hamna kitu hapo , Bashe alishinda kura za maoni za ccm kwasababu ya udhamini wa fedha mfadhili wake alizokwapua benki kuu [EPA-KAGODA]; huyu ni crony wa Rostam kwahiyo ushindi huo ni kwasababu ya RA bila ya hivyo Selelii angeshinda. Huyu Kingwangalah ameingia hapo na kushinda kwasababu ya ufisadi uliotumika through WAMA ya mama Kikwete kuiba fedha za STIMULUS package ambayo jamaa aliilamba kwa kuanzisha kampuni ya kununua Pamba.
 
Mi ni memba wa wanabidii huyu mbunge anachonga sana, na ni mwongo sana na ukweli umejulikana.
Huwa namsoma sana kule Wanabidii anachokosea ni kujitapa kwa elimu yake badala ya kujadili hoja anajitapa hadi kwa walimu wake waliomfundisha chuo hilo nililiona wiki moja iliyopita wakati anabishana na watu kule wanabidii i think Hamis Kingwangala has to change immediately otherwise ndio hivi watu wanaanza kumuanika.
 
Hamna kitu hapo , Bashe alishinda kura za maoni za ccm kwasababu ya udhamini wa fedha mfadhili wake alizokwapua benki kuu [EPA-KAGODA]; huyu ni crony wa Rostam kwahiyo ushindi huo ni kwasababu ya RA bila ya hivyo Selelii angeshinda. Huyu Kingwangalah ameingia hapo na kushinda kwasababu ya ufisadi uliotumika through WAMA ya mama Kikwete kuiba fedha za STIMULUS package ambayo jamaa aliilamba kwa kuanzisha kampuni ya kununua Pamba.
Mkuu mimi nafikiri hawa wawili wanajuana wapi walipogusana sasa naona kila mmoja anataka amvue mwenzake nguo ndiyo haya tunayoyaoona sasa hivi.
 
Whether huu 'ufunuo' umekuja baada ya Kingwangala kuuliza swali la umeme si hoja kubwa sana hapa cha muhimu je huyu bwana amefanya hayo yaliyoandikwa? Amemkosesha kijana Hamis nafasi yake ya kusoma na sasa Hamis anaishi kwa kubangaiza? Imagine maisha ya kijijini mtu akuchukue haki ya kusoma - there is no life baada ya hapo!

Well ukizowea kula nyama ya mtu utandelea siku zote, hutoacha. Kingwangala amezowea kuishi kwa mgongo wa wengine, kuanzia elimu na sasa ubunge.
FJM hayo yanayosemwa kuhusu Kingwangala kuchukua jina la mtu nimeishasikia yakisemwa sehemu nyingi sana sasa mimi mwenyewe i even doubt it kwamba inawezekana ni kweli na huo ukweli anaujua yeye mwenyewe ila jambo likisemwa sana lazima nyuma yake kuna kitu
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa kweli hata mimi nimeisoma yote. Nimehabarika vizuri kabisa kuhusu Ubunge wa Nzega na wagombeaji wake. Na najua ugomvi wa siasa huwa unamambo yake. Hata hivyo Bashe umetueleza vizuri kabisa mambo uliyokuwa umepanga na nakusifu kwa kupanga vizuri mada zako.
Pili, kuhusu dhuruma ya majina, mimi nimesoma kule vijijini ndani kabisa hukohuko kiasi kwamba kila mwaka tulikuwa hatufaulu. Lakini najua hii ilikuwa hujuma ya hawa watu wa elimu wa mkoani na wilayani. Inasikitisha sana. Kwa hiyo napendekezaa Kingwangala Fake (Mbunge) amusomeshe Kingwangala Orijino kwa kumlipia ada na mahitaji yote ya shule na kuihudumia familia yake mpaka atakapoishia. Hayo ndo yanatakiwa kuwa malipo kwa Kingwangala Orijino kwani bado naamini ni kichwa na anaweza kabisa kusoma na kufauli. La sivyo, mi naona hata elimu yake ni fake tu.
Swala la uraia linakuzwa tu panapokuwa na masilahi fulani. Sisi wote ni binadamu ambao tumeamua kuishi Tanzania either kwa kuzaliwa au kuomba. Kwa hiyo, kama mtu anaumuhimu katika nchi yetu kama wanavyofanya wamerakani kwa nini asipewe uraia. Uraia wako siyo issue. Lakini sasa Bashe wewe ni muajiriwa wa RA, hizi tuhuma unazionaje? Huoni jamaa anatuumiza watazania wezake? Kwa nini hawana huruma na watanzania walio wengi masikini?
Mwisho, Siasa ni mchezo. Kwa hiyo unatakiwa kujua jinsi ya kuucheza. Nakutakia kila la kheri katika mkakati wako wa kugombe ubunge lakini usije kuwa fisadi tu ukifika huko bungeni.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
MAKALA HII INAUKWELI MKUBWA SANA KWA BAADHI YA MAMBO, NI KWELI Dr KINGWANGALLAH ALISOMA NA BASHE, JAPO NAYE ALIKUWA ANAJULIKANA KAMA HUSSEIN MOHAMED.
JINA LA BASHE NI JIPYA PIA.
UWEZO WA BASHE SHULENI HAUKUWA MKUBWA SANA HAPO KITONGO NA HATA ALIPOKWENDA BADRI SIDHANI IWAPO ALIPATA MUUJIZA GANI HADI KUFAULU.
KINGWANGALLAH NI KICHWA HAKUFAULU LAKINI ALIKUWA NAUWEZO WA DARASANI NAKUMBUKA NIKIWA FM 4 ALIKUWA ANANIFUNDISHA BIOS NA CHEMISTRY HE KNEW THE SUBJECT VERY WELL. MUHIMBIRI NI KATI YA VYUOMakini na vigumu sana kwa mtu wa kawaida kumaliza hivyo kumalizakwake hakuna shaka japo jina aliiba.
BASHE NI MSOMALI , MGENI, WAKUJA NA SIO MWANANZEGA KWA VIGEZO VIFUATAVYO
1. UKIANGALIA KOO ZA NZEGA AMBAZO KWA KWELI ZILITOA MACHIFU NA VIONGOZI NA ZILIKANDAMIZWA NA WAZAZI WAKE BASHE. WALIKUJA KUWANYONYA WATANZANIA WAKATI WA UKOLONI HIVYO HAFAI KUWA KIONGOZI WETU.
2. BASHE AMEKUWA MTUMISHI WA MTUAMBAYE ANASIFA MBAYA TANZANIA , MAISHA YAKE YANATEGEMEA UFISADI NAHAJACHUKUA HATUA YA KUACHANA NA AMA KUMSHAURI BRO ROSTAM ABADILIKE NA KUTUONEA HURUMA AACHANE Na ufisadi YEYE ANATAKA NAFASI YA KUNYONYA ZAIDI.
NAJUA WAPO VIJANA WENGI WA NZEGA WENYE SIFA NA HAWANA HATA DOA KAMA ENG JOSEPH PIUS, JOSEPH MASSIMBA, DR REBECA SAMWEL NA WENGINE WENGI TUTAWASHAWISHI WAGOMBEE NA TUTAWAPA MCHANGO WA HALI NA MALI WASHIDE.
ASANTE BASHE KWA TAALIFA LAKINI WEWE PIA HUFAI
 
Wanajamii sikilizeni kwa makini, haya yamekuja baada ya Hamis kuuliza swali la umeme ambalo Rostam, Bashe na Lowassa ndio Prime member................

Haya yote CCM waliyajua hata kabla ya uchaguzi, alas they didnt realise kwamba Hamis was fighting from within.

Hii yote ni ile vita ya mafisadi na ccm safi

Mtasikia mengi sana, ila kama mnaipenda Tanzania mtanielewa

Hamis amegusa mslahi ya wakubwa wa mafisadi and Bashe is their korokoroni

mbado, naona na wewe umekuwa onesided: vipi Dr Hamis vs WAMA?
 
INGWANGALLAH NI KICHWA HAKUFAULU LAKINI ALIKUWA NAUWEZO WA DARASANI NAKUMBUKA NIKIWA FM 4 ALIKUWA ANANIFUNDISHA BIOS NA CHEMISTRY HE KNEW THE SUBJECT VERY WELL.

Nafikiri Orijino ndo alikuwa kichwa zaidi ndo maana alifaulu. Mengine hayo mtamalizana wananzenga wenyewe.
 
Well said!! Tunamtaka Mhe. MH HAMIS ANDREA KIGWANGALA (SAIDI NASSOR BAGAILE) AJIBU HOJA HIZI HAPA JF; vinginevyo anapaswa kujivua nyazifa zake kulinda heshima yake maana ana kesi ya kujibu hapa!!
 
wee bashe unshutumiwa sio raia hapa,sioni sababu ya kuingilia sana mambo yetu ya ndani,endelea kufanya biashara kama wasomali wenzako,ipo siku mtaondoka hapa

Ndugu kama unaweza disapprove what he is saying. Politics aside, prove that he is not a citizen.
 
kaka, bashe ni manager wa gazeti la rostam#

nakupigia ujue nini chanzo


Nipigie na mimi basi, au unitumie PM....LOL
Anyway, nakubaliana na wewe kuwa huyo Bashe inawezekana anafight back kulinda maslahi ya mafisadi, lakini hii haiondoi hizo tuhuma dhidi ya Said Kigwangwala.
 
Nipigie na mimi basi, au unitumie PM....LOL
Anyway, nakubaliana na wewe kuwa huyo Bashe inawezekana anafight back kulinda maslahi ya mafisadi, lakini hii haiondoi hizo tuhuma dhidi ya Said Kigwangwala.
Hizi tuhuma ingekuwa vizuri huyu jamaa akaja hapa kuzijibu maana naona hawa wanajuana vizuri wanavuana nguo hadharani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom