Bashe alivyoukwaa uenyekiti wa UVCCM kwa njia za panya

Moderator, hauko fair kabisa, mbona unafuta post zangu???? kwa nini? Mbona mimi natukanwa hapa na ninasingiziwa mambo mengi na hauyafuti?
 
Kuna wakati nchi hii huwa siielewi. Huyu mteka meli alitamkwa kwamba si raia wa nchi hii. Anaachwa vipi kupiga siasa katika nchi ya kigeni?

Mkuu weka kumbukumbu zako sawa, jamaa alirudishiwa uraia wake baada ya mchakato wa kura za maoni kumalizika na yeye kukosa kuteuliwa kugombea ubunge.

Nadhani kale kawimbo kao na kigwangala kanaelekea kufikia patamu kama huyu Bashe kapewa hako ka cheo. Kigwangala, angalia sasa mamb yanakuja, we endelea kubwata wenzio wanalamba madume ya kukumaliza.
 
Moderator, hauko fair kabisa, mbona unafuta post zangu???? kwa nini? Mbona mimi natukanwa hapa na ninasingiziwa mambo mengi na hauyafuti?

Wakati mwingine tabia ya mtu utaijua kwa namna anavyoandika au kusema mambo yake. Ataanika kila kiltu kinachomhusu ktk maisha yake, hata vile ambavyo havina umuhimu kwa jamii kuvijua!
 
Kigwangala moto huo unakuja, 2015 anza kutafuta kijiwe cha kuvutia gepu la maisha nje ya siasa. Umecheza na moto, sasa unakuja kwa kasi ya kimbunga, Bashe huyooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo! Supported by RA na EL, utauweza huo motooooooooooooooo! Anza kutafuta vijiwe 2015
 
Moderator, hauko fair kabisa, mbona unafuta post zangu???? kwa nini? Mbona mimi natukanwa hapa na ninasingiziwa mambo mengi na hauyafuti?

Mkuu wangu,

Zipi zimefutwa? Hukuangalia vyema? JF mpaka comment ifutwe elewa kuwa ina walakini mkubwa au ina matusi. Vinginevyo haitafutwa bali itakuwa edited kuweka paragraphs au kutenganisha maneno endapo yatakuwa hayasomeki au yanaleta maana mbaya.

So far kwenye hoja hii posts zako ni hizi:

Huyo muungwana ni mzaliwa wa Nzega lakini Uraia wake una 'UTATA' mkubwa mpaka pale atakaporekebisha nyaraka zake kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa...na kama asiporekebisha nyaraka zake bado atalazimika kuendelea kuwa mpiga kelele huko majukwaani na kamwe Chama chochote kile cha siasa hakitaweza kumsimamisha kama mgombea kwenye uchaguzi wowote ule wenye mamlaka ya dola...

Bashe bado hana Uraia, anatakiwa arekebishe documentations zake...

Topical,

SDina uhakika sana kama utata wa uraia wake unakuja kila akigombea Ubunge tu. Nadhani kama hajarekebisha nyaraka zake hadi leo, na kama hatozirekebisha mpaka kufikia uchaguzi Mkuu wa chama mwakani, nakuhakikishia hawezi kuruhusiwa hata kugombea ubalozi wa shina. Mwanzoni utata wa uraia wake haukuwa wazi sana kisheria, kwa sasa wapo wengi wanaofahamu utata huo uko wapi!

Mimi, wakidhani nina haja ya kumshambulia, wamekuwa wakiniletea ma-scud yanayohusu utata wa uraia wake, sema sijawahi kuamua kumlipua...
 
Huyo muungwana ni mzaliwa wa Nzega lakini Uraia wake una 'UTATA' mkubwa mpaka pale atakaporekebisha nyaraka zake kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa...na kama asiporekebisha nyaraka zake bado atalazimika kuendelea kuwa mpiga kelele huko majukwaani na kamwe Chama chochote kile cha siasa hakitaweza kumsimamisha kama mgombea kwenye uchaguzi wowote ule wenye mamlaka ya dola...

@HKingwangalla,
Kwa kumbukumbu zangu aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani ndugu Lawrence Masha (akiwa waziri) alitoa tamko rasmi kuhusu uraia wa Bashe ana alisema bila kumumunya maneno kuwa Bashe ni raia halali kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Sasa leo hii wewe mbunge unatuambia uraia wa Bashe una utata! Utata kwa vipi? Masha ambaye kwa taaluma ni mwanasheria alikosea? kati ya Masha na wewe Kingwangalla tumuamini nini?

Na tukiwa kwenye kuamini - wewe kama alibi unasifa stahiki? kwamba unaaminika kutoa ushahidi kuhusu jambo lolote likiwemo hili la uraia wa Bashe? Kwa mfani jina lako ni nani? una umri gani? unafanya kazi gani etx. Na hapa ningeomba utusaidie kwamba wewe binafsi jina lako ni Hamis Kingwangalla na muhimu zaidi (nasisitza muhimu zaidi) ulishawahi kuapa kwenye mahakama yoyote (dunia) kuhusu jina lako? kama ndio, ni wapi na kwa nini? Haya maswali ni muhimu maana yatasaidia kujua wewe kama alibi unaamika. 'Credibility is fundamentally important for any witness'
 
Kuna watu walishasema Hamis Kigwangalah anamwogopa Bashe kama ukoma, na kila comment anayoitoa Bashe au inayomhusu Kigwa lazima ajibu.
Kitu kimoja ambacho Mr Hamis Kigwa hujawahi kujibu kwa ufasaha ni ile tuhuma aliyoitoa Bashe juu ya wewe kuiba jina la mshindi std 7 kwenda Kigoma Secondary.
 
Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.

Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.
Hii ni hali halisi. So what? tamaa ndizo zinazowafikisha hapo watoto wenu wa CCM.
 
@HKingwangalla,
Kwa kumbukumbu zangu aliyekuwa Waziri wa mambo ya ndani ndugu Lawrence Masha (akiwa waziri) alitoa tamko rasmi kuhusu uraia wa Bashe ana alisema bila kumumunya maneno kuwa Bashe ni raia halali kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi. Sasa leo hii wewe mbunge unatuambia uraia wa Bashe una utata! Utata kwa vipi? Masha ambaye kwa taaluma ni mwanasheria alikosea? kati ya Masha na wewe Kingwangalla tumuamini nini?

Na tukiwa kwenye kuamini - wewe kama alibi unasifa stahiki? kwamba unaaminika kutoa ushahidi kuhusu jambo lolote likiwemo hili la uraia wa Bashe? Kwa mfani jina lako ni nani? una umri gani? unafanya kazi gani etx. Na hapa ningeomba utusaidie kwamba wewe binafsi jina lako ni Hamis Kingwangalla na muhimu zaidi (nasisitza muhimu zaidi) ulishawahi kuapa kwenye mahakama yoyote (dunia) kuhusu jina lako? kama ndio, ni wapi na kwa nini? Haya maswali ni muhimu maana yatasaidia kujua wewe kama alibi unaamika. 'Credibility is fundamentally important for any witness'
Acha ubazazi. Huyo kigeugeu na mnafiki mwezio Masha si alisema Wenye (MB) wa Nyamagana kwamba si raia ili asipate mpinzani kwenye kinyang'anyiro cha Ubunge kwa kutumia kifungu kinachompa Waziri wa Mambo hya Ndani kuthibitisha uraia wa mtu. Majibu uanayo, alibwagwa. Sasa credibility ya Masha inatoka wapi. Naye njaa tu alipewa visenti na Rostam akajivua utu wake.
 
CCM sshv wanaishi na kutawala kwa fedha na sio nguvu ya umma tena!huyu ndo Bashe
1. Alishasema ngoja CCM ishindwe 2heshimiane wakati huohuo ni mjumbe wa NEC na baraza kuu la UVCCM
2.Mkurugenzi mtendaji wa New Habari Cooperation 2006 kampun tanzu ya Rostam Aziz
3. Muumini na mfuasi muaminifu wa mapacha
4. Msomali kimuonekano mpk moyoni
 
Huu mchezo wa kuchezea uraia wa Watanzania utaleta hatari kubwa sana nchini. Nakumbuka hata Jenerali Ulimwengu walitaka kumvua uraia kwa ajili tu ya kuhoji madudu mbali mbali ndani ya Serikali.

~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

Wi
zara ya Mambo ya Ndani imemwandikia barua kada wa CCM, Hussein Bashe kuthibitisha kuwa ni raia wa Tanzania baada ya suala hilo kusababisha anyimwe nafasi ya kuwania ubunge wa Nzega kwa tiketi ya CCM. Bashe alishinda kwenye kura za maoni za CCM kwenye jimbo hilo la Nzega baada ya kupata kura zaidi ya 14,000, lakini akaenguliwa baada ya ukakasi kuibuka kwenye uraia wake.
6665792.jpg
Hussein Bashe

Baadaye katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na katibu wa idara ya itikadi na uenezi ya chama hicho, John Chiligati waliwaambia waandishi kuwa Bashe si raia na kwamba ametakiwa aanze upya taratibu za kupata uraia wa Tanzania.

Alipoulizwa kuhusu suala la Bashe jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha alisema: "Kwa mujibu wa sheria, mimi ndiye wa mwisho kuzungumzia suala hili. Jibu langu lipo pale pale na siwezi kubadili. Bashe ni raia halali wa Tanzania."

Masha, ambaye alishawahi kusema kuwa uraia wa Bashe hauna tatizo, aliongeza kusema: "Nani kasema Bashe si raia? Kama waziri mwenye dhamana nasema, Bashe ni raia halali na hakuna atakayebadilisha msimamo wangu huu.''

Taarifa ambazo Mwananchi inazo zinasema kuwa barua hiyo ya Serikali kwenda kwa Bashe imeandikwa na waziri huyo ambaye pia anasimamia Idara ya Uhamiaji, lakini alipoulizwa na Mwananchi kuhusu barua hiyo hakutaka kueleza chochote zaidi ya kusisitiza kuwa mgombea huyo wa zamani wa ubunge wa Nzega ni raia halali.

Barua ambayo Mwananchi imeiona kutoka kwa mmoja wa maofisa waandamizi wa Wizara hiyo inaonesha kuwa mbali na kumthibitishia Bashe kuwa ni raia, pia imemfafanulia tatizo lililojitokesza kwenye nyaraka za awali kuhusu kabila. Barua hiyo imeeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu Na.5 (1) au 7 (8) cha Sheria Namba 7 ya Uraia ya mwaka 1995, Bashe ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa. Barua hiyo iliyoandikwa Septemba 3 ambayo inakwenda kwa Bashe, ina kichwa cha habari kisemacho "Upotoshwaji juu ya Uraia wako" ambayo inaonekana kuwa ni majibu ya barua kutoka kwa kada huyo wa CCM akitaka ufafanuzi wa suala lake. Barua hiyo ya Masha inaeleza kuwa utata kuhusu uraia wa Bashe ulitokana na kada huyo kuwasilisha hati ya kiapo inayoonyesha kuwa ni Mnyamwezi badala ya Mtanzania mwenye asili ya Somalia.

"Utata huo haukuondolei haki yako ya kuwa Mtanzania. Hata hivyo utata huo umeondolewa kwa kiapo kingine ambacho kimerekebisha kile cha awali," anaeleza Masha katika barua hiyo.

"Kwa msingi huo, kwa barua hii ninathibitisha kuwa Hussein Mohamed Bashe Ibrahim ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Na.7 ya mwaka 1995 kifungu Na. 5(1) au 7(8)."
Barua hiyo imepelekwa kwa Bashe na kwa katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo la Bashe, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema asingeweza kulizungumzia kwa kuwa yuko mapumzikoni. "Nipo nyumbani kwa mapumziko,'' alisema na kukata simu.

Naye makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa hakutaka kuzungumzia suala hilo na badala yake alisema: "Mimi nipo Mwanza Vijijini, siyajui ya Dar es Salaam. Waulize ambao wako huko (Dar es Salaam).''

source: Hussein Bashe ni raia halali wa Tanzania - Serikali - Wavuti
 
Kazi ipo. Mimi nilishawahi kukutana na Malisa kwa bahati tu. Mara baada ya kutambulishwa nilimtupia swali moja na kugundua kuwa si mtu makini na hata Umakumu Mwenyekiti wa UVCCM ameupata kwa kubebwa.

Ukifuatilia story kati yake na Mtoto wa Mkulu, utagundua hilo. Hivyo sishangai yote yanayosemwa juu yake. Tabia yake ya kujipendekeza ni imemkaa sana kichwani hana chochote.
 
Huyo muungwana ni mzaliwa wa Nzega lakini Uraia wake una 'UTATA' mkubwa mpaka pale atakaporekebisha nyaraka zake kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa...na kama asiporekebisha nyaraka zake bado atalazimika kuendelea kuwa mpiga kelele huko majukwaani na kamwe Chama chochote kile cha siasa hakitaweza kumsimamisha kama mgombea kwenye uchaguzi wowote ule wenye mamlaka ya dola...

Kumbe aina hii ya wanasiasa ndani ya chama tawala haitabadilika....Hii ni aibu!
 
Huyo muungwana ni mzaliwa wa Nzega lakini Uraia wake una 'UTATA' mkubwa mpaka pale atakaporekebisha nyaraka zake kwa kufuata utaratibu wa kisheria uliowekwa...na kama asiporekebisha nyaraka zake bado atalazimika kuendelea kuwa mpiga kelele huko majukwaani na kamwe Chama chochote kile cha siasa hakitaweza kumsimamisha kama mgombea kwenye uchaguzi wowote ule wenye mamlaka ya dola...

Kigwangala hivi wewe ugonvi wako na Bashe hauishi? tumeshajua wewe ulifoji vyeti na kumshinda Bashe kwenye kura za maoni kimizengwe na hata Ubunge Nzega picha ilikuwa ileile kama ya Igunga, Bashe naye tunamjua kuwa ni hohehahe wa kutupwa pale Nzega nani mteule wa mafisadi, leo hii Bashe eti ana pesa za kudanganyia watu je kazipata wapi? kwanza huyu pia hana uTZ wa asili kama JK alivyowahi tangazia waTZ, sasa acheni kulumbana bali pelekeni sera zenu ndani ya CCM ili watu wakikueleweni then mtapata heshima huko huko ndani ya CCM, nyi nyi ni watu wa ajabu sana eti mkiwa kwenye vikao vyenu eti mnaelewana (kifitina tupu) mkitoka nje mmnaanza malumbano yasiyokuwa na tija kwetu...mkiweza malizaneni kabisa tumechoka na ngenga zenu,
 
kuna wakati nchi hii huwa siielewi. Huyu mteka meli alitamkwa kwamba si raia wa nchi hii. Anaachwa vipi kupiga siasa katika nchi ya kigeni?

nimecheka sana huyu mteka meli kwa kweli nimeshanga malisa alivyo badilika gafla kumbe ni mashiko, kumbe shigela yuko cheep ebu niambieni bei gani shigela kuna kazi ya ovyo nataka kumpa anifanyie.
 
Hussein Bashe alikuwa ni mgombea wa kinyang'anyiro cha uenyekiti wa UVCCM kabla ya nafasi hiyo kutengwa kwa ajili wa wagombea kutoka visiwani. Alipojaribu kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti alishindwa kutamba mbele ya Benno Malisa. Lakini kwa ustadi mkubwa muungwana huyu ameweza kutumia werevu wake na ukaribu wake na mafisadi wakwasi na kuwafanya wamteue kuwa mwenyekiti wa kukusanya maoni juu ya namna UVCCM inavyoweza kujibadili na kuwa ya kisasa. Katika kamati hii ambayo katibu wake ni katibu mkuu wa UVCCM Martine Shigela, yeye ndiye msemaji mkuu na sasa yeye ndiye msemaji mkuu wa UVCCM na hawa akina Shigela na Malisa sasa wanaripoti kwake.

Inasemekana sasa hivi yeye ndiye anayeendesha jumuiya hiyo kwa fedha anazozipata kutoka kwa wakwasi hao na hata ziara za Benno Malisa sasa hivi zimekuwa zikiandamana na Fred Lowassa, Bashe na girl friend wa Malisa Mboni Mhita. Hawa ndiyo wanaomfadhili Malisa na kumpangia nini cha kufanya na kuongea. Kimsingi Bashe na wakwasi wake wamefanikiwa kuigeuza UVCCM kuwa mdomo na chombo cha Lowassa na kwa njia hii Bashe amefanikiwa alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu, tena bila jasho. Hili limewezekana baada ya kubaini udhaifu na njaa ya Shigela na Malisa.

Ulitaka UVCCM iendeshwe na mama yako?
 
Back
Top Bottom