Barua: Zitto akataa posho za vikao

BINAFSI NATOA PONGEZI ZANGU STAHILI.......(ANGALIZO) KAMA ALIPOELEKEZA ZIPELEKWE KWELI IKAWA NI NGO YAKE BINAFSI (hiyo ni sarkasi katuchezea) SI SAHIHI SANA.....! BALI NINGEMWELEWA ANGEPELEKA KATIKA TAASISI AMBAZO HANA MKONO WAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE!
TUHESHIMU MCHANGO WAKE NA PIA LOLOTE AMBALO AENDA KINYUME TUWE KINYUME NALO
 
Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!

Rejao think big bana hata kama zinaenda KDI real ameonyesha mfano cause hata hiyo KDI Hafaidiki nayo yy its Non-profit org zaidi ni kwa ajili ya Wananchi wake upo?
 
Hongera zito kwa kuonyesha umma watanzania uzalendo wako, naamini utakuwa umeonyesha kwenye barua yako kuwa hiyo posho itumikeje, mfano mzuri wa kuigwa
 
Yaani hata mtu akifanya jambo jema still anatiliwa shaka!!
Mbona Watanzania hatuna jema!!

Hivi Zitto huwa hachangii hiyo KDI? Huwa anachangia kutoka wapi. Si ni kutokana na mapato yake yakiwemo ya posho? Sasa kama ameamua posho ziende kwenye mfuko anaouongoza kuna jipya hapa? Hii ni sawa na kusema msinilipe cash ila niwekeeni kwenye account yangu ya bank!!!
 
Tall order for CDM MPs to follow suit! Hongera Mkuu, ila naona umewatega wenzako wakina Mbowe.....watakuwa wanakulaani chinichini!
Umepiga bao la kisigino! Tuone wafuasi wao watasema nini leo!
 
BINAFSI NATOA PONGEZI ZANGU STAHILI.......(ANGALIZO) KAMA ALIPOELEKEZA ZIPELEKWE KWELI IKAWA NI NGO YAKE BINAFSI (hiyo ni sarkasi katuchezea) SI SAHIHI SANA.....! BALI NINGEMWELEWA ANGEPELEKA KATIKA TAASISI AMBAZO HANA MKONO WAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE!
TUHESHIMU MCHANGO WAKE NA PIA LOLOTE AMBALO AENDA KINYUME TUWE KINYUME NALO

mkuu MAHESABU ... katika mfumo wa NGO hakuna kitu kama hicho kwenye red ..... hata kampuni wamiliki ni watu wawili na kuendelea

lets appreciate Hon. Zitto for his strong stance .... this is a great persuasive action
 
Mkuu Kimbunga ningependa km makamanda wote wange muunga mkono zitto, kwa mujibu wa Zitto Kabwe ile Barua ni yake binafsi, ameiandika kuelezea dhamila yake ya kutochukua posho!

Mkuu hivi huoni kama hapa kuna tatizo? Hapa inaonekana kama Zitto yupo peke yake wakati huo ni msimamo wa Chama.
 
Watu bana eti angeimarisha chama. Kwani kwa kutumia KDI CDM haiwezi kuimarika. Sometime tuweke siasa pembeni. Wana CDM wanaweza kumarisha CDM hata nje ya CDM. kuna mambo mengi ya kufanya nje ya siasa wapinzani wakifanya ni msumari kwa CCM.

Mkuu hivi huoni kama hapa kuna tatizo? Hapa inaonekana kama Zitto yupo peke yake wakati huo ni msimamo wa Chama.

Suala la posho ni suala Binafsi na hata chama bado wasingekubaliana wote. As an individual zito aana haki ya kujitolea kuonyesha njia kama wenzake wana sista sita basi yeye katangulia........... Ni kazi kwa wanaona inafaa nao wafuate njia na wakifika hata wabunge 10 utasikia hata bunge linafanya kuwa official

Zitto endelea lakini hizo pesa zi quantify zifanye nini sehemu gani .katika kila kikao cha bunge weka tangible output inayotakiwa kuonekana na uwachieved juu ya hizo pesa zako. La sivyo itakuwa ni siasa tu
 
Hivi Zitto huwa hachangii hiyo KDI? Huwa anachangia kutoka wapi. Si ni kutokana na mapato yake yakiwemo ya posho? Sasa kama ameamua posho ziende kwenye mfuko anaouongoza kuna jipya hapa? Hii ni sawa na kusema msinilipe cash ila niwekeeni kwenye account yangu ya bank!!!
Kweli kabisa!! Na hicho ndichi Zitto alichofanya. Halafu hpa ndani mijitu inampongeza tu bila hata kuthink big
 
NO SIO MSIMAMO WA CHAMA BT ILIPASWA UWE MSIMAMO WA CHAMA, Nadhani kwa Maamuzi Mazito aliyofanya chama watafuata msimamo wake na naimani wabunge wezie wataiga msimamo wao!
 
mwanzo mzuri lakini linatakiwa shinikizo kwa wabunge wengine kufanya hivyo

Mkuu shinikizo la kukataa posho litakigawa chama katika mapande mapande!! Hivi mtu ndio mara yake ya kwanza kuingia bungeni baada ya kutafuta nafasi hiyo kwa kutumia resources zake kwa miaka na mikaka leo umwambie aachane na posho!!! Hapa kuchakuwa na uchafuzi wa hali ya hewa ndani ya chama.
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi. Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.

Nilimwambia hili Zitto over a year ago, hapa hapa. What took him so long?

Mimi ningependelea wabunge hawa wachukue posho na kuzipeleka katika mipango ya maendeleo ya wananchi, kukataa kuchukua posho kunaiachia serikali tu posho hizi, ambazo zitaishia kuliwa kifisadi.
 
ni mnafiki pekee ambaye anaweza kuipinga dhamira ya safi ndg zitto kabwe ya kuipunguzia serikali gharama ya uendeshaji wa nchi ili fedha kidogo inayopatikana kwa walipa kodi kukamuliwa ielekezwe kwenye shughuli za maendeleo na huduma za jamii . kwa hili zitto amejipapanua kama kamanda wa ukweli katika kuonyesha kuwa anayaishi maneno yake. big up zitto, God bless u!
 
Kimbunga shirikisha ubongo unapoandika. KDI ni kigoma Devp Initiative na sio Zito Devp Initiative. Zito yeye ni founder member tu wa hiyo NGO kwa hiyo anakuwa ni Board members na sio mtendaji mkuu. Siku zote wanayefaidi katika NGO ni watendaji na walengwa na sio Board members na hata kama hiyo NGO ni ya Zito Kama vission na mission zake ni kuleta maendeleo kwa watu wa kigoma kwa vitendo na yakatelezeka we hv no querry abt him. Congrat Zito
 
Watu bana eti angeimarisha chama. Kwani kwa kutumia KDI CDM haiwezi kuimarika. Sometime tuweke siasa pembeni. Wana CDM wanaweza kumarisha CDM hata nje ya CDM. kuna mambo mengi ya kufanya nje ya siasa wapinzani wakifanya ni msumari kwa CCM.

Suala la posho ni suala Binafsi na hata chama bado wasingekubaliana wote. As an individual zito aana haki ya kujitolea kuonyesha njia kama wenzake wana sista sita basi yeye katangulia........... Ni kazi kwa wanaona inafaa nao wafuate njia na wakifika hata wabunge 10 utasikia hata bunge linafanya kuwa official

Zitto endelea lakini hizo pesa zi quantify zifanye nini sehemu gani .katika kila kikao cha bunge weka tangible output inayotakiwa kuonekana na uwachieved juu ya hizo pesa zako. La sivyo itakuwa ni siasa tu

Mkuu kukataa posho ni msimamo wa chama siyo msimamo wa mtu binafsi. Huo msimamo umetoka wapi kama ni mbunge mmoja tu natekeleza msimamo wa Chama? CHADEMA kama insititution inatakiwa iwe na misimamo ya ki insititution na siyo msimamo wa mtu mmoja mmoja. Kama ni msimamo wa mtu mmoja mmoja basi hakuna maana ya kuwa na msimamo wa Chama katika mambo mbalimbali.

Hapa nakumbuka msimamo wa Chama wa kutoka nje wakati JK anahutubia Bunge, ZZK akaja na msimamo wake wa kupingana na Chama. Mbona chama hakina misimamo?
 
Hongera sana Zito Kabwe, huu ni mfano mzuri wa kuigwa na mbunge yeyote yule bila kujali katoka chama gani.Big up brother, Watanzania wanamacho wanaona na wanamasikio wanasikia unayoyafanya!!!!!
 
Back
Top Bottom