Barua za Dada..Nafikiri kumtimua

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
IMG00277-20110618-0903.jpg IMG00276-20110618-0902.jpg IMG00247-20110618-0844.jpg IMG00269-20110618-0901.jpg mail.google.com.jpg IMG00265-20110618-0900.jpg IMG00266-20110618-0900.jpg IMG00279-20110618-0903.jpg

Haya mambo ya Dada (House Girl) kutoka kusini mwa nchi yetu. Alianza ajira shwari kabisa, baada ya muda mwenendo wake ukabadilika, pengine akienda sokoni kurejea lazima achelewe. Siku chache zilizopita, mamsapu alijaribu kuchukua simu anayoitumia kwa mawasiliano hapa nyumbani tulimnunulia kwa hilo tui, mara simu ikalia, baada ya kupiokea, sauti ya jamaa ikasikika ikikoroma "vipi we mtoto mbona huonekani buchani sasa mimi nimeweka nyama kibao uje ule??...njoo bwana tiufanye kama siku ile leo nitakupa na hela ya mtoko.." Mamsapu akashtuka na kuuliza, vipi ??? Jamaa likakata simu..badaa ya kumuuliiza dada akakataa..lakini baada ya muda akakiri anasumbuliwa na jamaa fulani ..akaahidi kuacha haya mambo. Tukamnyang'anya simu.

Aidha, katika harakati ya kujaribu kumsaidia..tuliendelea kumwonya tu ili azingatie kile ambacho kimemleta mjini asije ishia kwenye matatizo ikiwemo maradhi...lakini inaonerkana kabinti kamezoea..leo naletewa kesi hii,...eti dada anatumia daftari, karamu na rangi za watoto kuandikia barua wanaume...khaaa.

Nafikiri kutimua mtu this evening!! Naona hakuna kitu hapa!!
 
yaah kumsaidia ni kumtimua unajua barehe ni kitu kibaya sana ......na pindi inapomfikia kijana inategemea inamwangukia wapi sasa huyu imeangukia kwenye ngono naomba ujivue kwani mwisho wa siku utapata matatizo ya kuhudumia yeye na kiumbe bora jiondoe mapema,,,,,,,,,,,kwa sababu yeye anaona kama unamnyanyasa kwa sasa
 
Du! Usimtimua kwanza, ni stage ya maisha ambayo hata mtoto wako atakuja kupitia/ashapitia. Jaribu kumchukulia kama mwanao, na 'umlee' katika hilo ili litakapokuja kuwa kwa mwanao, uwe na experience.

Mkuu, ni ngumu kukaa na binti wa mtu ambaye ulimchukua kwa malengo (tumemwajiri kufanya kazi za ndani). Hapa tunaishi na watoto wadogo ambayo anapaswa pengine awe nao karibu, sasa kama anawashwa tena mkuu pengine unaweza kukuta nyumba nyeupe wakati yeye yupo kwenye "heat" nje na mijamaa..awali tulidhani tutamdhibiti tukimnyang'anya simu kumbe hatukujua bado kuna maunjanja yale ya zama zetu ya kuandikiana barua zenye mijipicha ya mioyo na mikuki.

Hata kama ni balehe, bado anahitaji kuwa mwangalifu na msikivu kwa kuwa hana uwezo wowote zaidi ya nguvu zake za kufanya kazi. Tulimchukua tuishi nae kama mtoto wetu lakni inakuwa ngumu kummudu katika mambo kama haya, mtaishia kula uchafu kila siku au kuonekana mnamtesa binti bila sababu pindi mtakapo mkalipia.
 
Ukionya, ukikaripia, ukifundisha, ukishauri halafu hakuna matokeo mazuri, basi nawa mikono kama Pilato. Na aondoke kwa amani, atakuja kuyakumbuka siku yakimkuta hayo anayokatazwa. Ndipo wema na ubaya wenu utakapo onekana kwake.
 
Sijajua sababu ya wewe kutaka kumtimua,sijui ni kwa sababu ni HG wako au ni mdogo kiumri au vipi sijui,lakini hata kama ni hg wako na ana umri mkubwa ana haki ya kuwa na mahusiano cha msingi asiharibu kazi na heshima iwepo!Otherwise uwe na sababu za msingi kumzuia!
 
Kaka mtimue. Mfanyakazi ni mfanyakazi ndugu, hukumleta kwako ili umlee. Na nakwambia huyo dada akipata mimba wazazi wake watakususia kwa kuwa umeshindwa "kumlea". Next time tafute msichana mkubwa kuajiri vibinti vidogo ni headache ndugu yangu.

Wanaosema angekuwa mwanao sijuhi nini; siyo mwanao sasa kwa nini kichwa kikuume. Na nakwambia akawii kuwa analeta mabwana ndani mkiwa kazini huku watoto wakipata movie ya bure.
 
huyo msichana anaitwa nani? maana si tumemtimua msichana fulani kwa sababu ya muuza nyama na amemuambukiza HIV wasichana hawa mmh!! kumsaidia hapo timua yeye!!
 
Du! Usimtimua kwanza, ni stage ya maisha ambayo hata mtoto wako atakuja kupitia/ashapitia. Jaribu kumchukulia kama mwanao, na 'umlee' katika hilo ili litakapokuja kuwa kwa mwanao, uwe na experience.

Aisee, nimeipenda sana busara yako.
Nice one.
 
Ukionya, ukikaripia, ukifundisha, ukishauri halafu hakuna matokeo mazuri, basi nawa mikono kama Pilato. Na aondoke kwa amani, atakuja kuyakumbuka siku yakimkuta hayo anayokatazwa. Ndipo wema na ubaya wenu utakapo onekana kwake.
wewe unafaa kuwa mshauri wa jamii do it forever
 
Pole sana,
kumfukuza utakuwa hujamsaidia lolote lamsingi ni kumuita ukamshauri ukamuonya ukiona hajabadilika kama ulimtoa nyumbani kwao unaweza kuongea na ndugu zake na kuwaelezea jins mtoto wao alivyobadilika na wao wakamuonya, usifikie maamuzi ya kumfukuza chukulia kama ni mwanao na je mwanao akiwa na tabia za hivyo utamfukuza?Ikishindikana hapo mrudishe nyumbani kwao umkabidhi
 
Kwanini umfukuze? Au na wewe ulikuwa unapita siku moja moja sasa umeona muuza bucha kakuzidi?
 
Pole sana.
Unajua maisha ni kitu cha ajabu. Tujaribu kuwachukulia hawa kama wenetu wa kuwazaa hasa pale ambapo anakuja akiwa bado mdogo. Mama mfanye awe rafiki yako kama vile mwanao wa kike kwani mkishakuwa karibu ni rahisi kummonitor mara kwa mara, kumtania tania huku ujumbe ukifika moja kwa moja ni rahisi kumjengea confidence kuwa anajaaliwa na 'wazazi' wake. Mara nyingi hawa wanaowarubuni hufanikiwa kwa kuwa huwafanya wale wasichana wajisikie kuwa anajaliwa sana.

Lakini ukimchukulia eti ni mtu mzima kwa kuwa tu anakufanyia kazi na ukategemea kuwa Life skillls anazijua, matokeio yake huwa mabaya.

Usimfukuze, mkalishe chini, ongea naye taratibu, mweleze madhara yote yanayowezampata kama ataendelea (tena usimkanye kama unamsomea risala) kisha mwulize wamefika wapi, akacheck then maisha yaendelee.......kumbuka kumwonya mwenye bucha.
 
uyo ameshaonja asali na atataka kuchonga mzinga hapo hapo kwako na akipata matatizo jua kuwa unalo hilo,
siku izi mahg wana matatizo sana ukimpata mzur ushukuru mungu, sisi tulimpata mmoja huyo anapandisha mashetan
anapiga watu hovyo tulimtimua
 
Pole sana,kumfukuza utakuwa hujamsaidia lolote lamsingi ni kumuita ukamshauri ukamuonya ukiona hajabadilika kama ulimtoa nyumbani kwao unaweza kuongea na ndugu zake na kuwaelezea jins mtoto wao alivyobadilika na wao wakamuonya, usifikie maamuzi ya kumfukuza chukulia kama ni mwanao na je mwanao akiwa na tabia za hivyo utamfukuza?Ikishindikana hapo mrudishe nyumbani kwao umkabidhi
usiwe mgumu wa kuelewa jaman!si amesema kaishaptia hatua zote.
 
Mkuu pole sana kwa yanayokukabili, inshoti kuwa makini sana na huyo binti ni kweli yupo ktk wakati mgumu kwake muhimu ni kumrejesha tu kwao, kuna mwingine alikuwa anampa mtoto piritoni then anaenda kwa jamaa yake kupata dozi, la sivyo utaletewa mimba hapo mda sio mrefu
View attachment 32181View attachment 32182View attachment 32183View attachment 32184View attachment 32185View attachment 32186View attachment 32187View attachment 32188Haya mambo ya Dada (House Girl) kutoka kusini mwa nchi yetu. Alianza ajira shwari kabisa, baada ya muda mwenendo wake ukabadilika, pengine akienda sokoni kurejea lazima achelewe. Siku chache zilizopita, mamsapu alijaribu kuchukua simu anayoitumia kwa mawasiliano hapa nyumbani tulimnunulia kwa hilo tui, mara simu ikalia, baada ya kupiokea, sauti ya jamaa ikasikika ikikoroma "vipi we mtoto mbona huonekani buchani sasa mimi nimeweka nyama kibao uje ule??...njoo bwana tiufanye kama siku ile leo nitakupa na hela ya mtoko.." Mamsapu akashtuka na kuuliza, vipi ??? Jamaa likakata simu..badaa ya kumuuliiza dada akakataa..lakini baada ya muda akakiri anasumbuliwa na jamaa fulani ..akaahidi kuacha haya mambo. Tukamnyang'anya simu. Aidha, katika harakati ya kujaribu kumsaidia..tuliendelea kumwonya tu ili azingatie kile ambacho kimemleta mjini asije ishia kwenye matatizo ikiwemo maradhi...lakini inaonerkana kabinti kamezoea..leo naletewa kesi hii,...eti dada anatumia daftari, karamu na rangi za watoto kuandikia barua wanaume...khaaa. Nafikiri kutimua mtu this evening!! Naona hakuna kitu hapa!!
 
Ukionya, ukikaripia, ukifundisha, ukishauri halafu hakuna matokeo mazuri, basi nawa mikono kama Pilato. Na aondoke kwa amani, atakuja kuyakumbuka siku yakimkuta hayo anayokatazwa. Ndipo wema na ubaya wenu utakapo onekana kwake.
chukua tano!
 
Pole sana.
Unajua maisha ni kitu cha ajabu. Tujaribu kuwachukulia hawa kama wenetu wa kuwazaa hasa pale ambapo anakuja akiwa bado mdogo. Mama mfanye awe rafiki yako kama vile mwanao wa kike kwani mkishakuwa karibu ni rahisi kummonitor mara kwa mara, kumtania tania huku ujumbe ukifika moja kwa moja ni rahisi kumjengea confidence kuwa anajaaliwa na 'wazazi' wake. Mara nyingi hawa wanaowarubuni hufanikiwa kwa kuwa huwafanya wale wasichana wajisikie kuwa anajaliwa sana.

Lakini ukimchukulia eti ni mtu mzima kwa kuwa tu anakufanyia kazi na ukategemea kuwa Life skillls anazijua, matokeio yake huwa mabaya.

Usimfukuze, mkalishe chini, ongea naye taratibu, mweleze madhara yote yanayowezampata kama ataendelea (tena usimkanye kama unamsomea risala) kisha mwulize wamefika wapi, akacheck then maisha yaendelee.......kumbuka kumwonya mwenye bucha.

Sijui umri wa huyo binti?
Kama umri unaruhusu wa yeye kuwa na mpenzi sio mbaya akawa naye, ni binadamu na yeye anahitaji kupendwa.

Point ni kwamba, wewe kama bosi wake, sio mbaya ukimwelekeza ni jinsi gani ya kufanya majukumu yake na mapenzi. Pia kama inawezekana na huyo mpenzi wake umjue kwa maana ya kujitambulisha kwenu.

Tumejenga tabia kwamba kwa sababu ni mtumishi wa ndani (House girl) basi tunamfanya kama vile ni mtumwa. Kumbuka kwa vile anaishi kwako, huyo ni sehemu ya maisha yako, hivyo ni jukumu lako kama bosi wake kumfundisha tabia zile ambazo ungependa hata watoto wako wawe nazo.
Ningeshauri ukae naye chini, mpe abcd za mapenzi, mweke huru aweke mambo yake ya mapenzi hadharani..muimsaidie kutimiza ndoto zake kama ni kuolewa. Mkimshindwa au akishindwa kuwaelewa basi ni bora mchukue hatua za kumuachisha kazi.
 
View attachment 32181View attachment 32182View attachment 32183View attachment 32184View attachment 32185View attachment 32186View attachment 32187View attachment 32188

Haya mambo ya Dada (House Girl) kutoka kusini mwa nchi yetu. Alianza ajira shwari kabisa, baada ya muda mwenendo wake ukabadilika, pengine akienda sokoni kurejea lazima achelewe. Siku chache zilizopita, mamsapu alijaribu kuchukua simu anayoitumia kwa mawasiliano hapa nyumbani tulimnunulia kwa hilo tui, mara simu ikalia, baada ya kupiokea, sauti ya jamaa ikasikika ikikoroma "vipi we mtoto mbona huonekani buchani sasa mimi nimeweka nyama kibao uje ule??...njoo bwana tiufanye kama siku ile leo nitakupa na hela ya mtoko.." Mamsapu akashtuka na kuuliza, vipi ??? Jamaa likakata simu..badaa ya kumuuliiza dada akakataa..lakini baada ya muda akakiri anasumbuliwa na jamaa fulani ..akaahidi kuacha haya mambo. Tukamnyang'anya simu.

Aidha, katika harakati ya kujaribu kumsaidia..tuliendelea kumwonya tu ili azingatie kile ambacho kimemleta mjini asije ishia kwenye matatizo ikiwemo maradhi...lakini inaonerkana kabinti kamezoea..leo naletewa kesi hii,...eti dada anatumia daftari, karamu na rangi za watoto kuandikia barua wanaume...khaaa.

Nafikiri kutimua mtu this evening!! Naona hakuna kitu hapa!!

Pia naona kubandika hizi barua ni kumdhalilisha! sio vizuri kabisa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom