Barua ya wazi kwa zitto kabwe

Ushauri Mzuri saaaana......Kama wewe ni mpinzani wa kweli unapaswa kuuufuata ,Ila kama ni mamluki hutakua na jipya
 
Jamani zito no cancer. na dawa ya kansa ni kuchoma sehemu iliyoathirika au kuikata. sasa zito ameshaathiri sana chama na ni kidonda cha kukata na siyo kulelewa. Hivyo vicent vya ccm anvyokula kupitia rostam azizi vitamfanya hata kukiteketeza chama. nashauri chama kichukue maamuzi magumu.
 
Zito akomae tuu. Hana sababu ya kuomba radhi. Siasa ni msimamo. Lazima ujiamini. Usiogope wala kutishwa. Tunamkubali.
(kinumasaa)
 
hana maana yoyote, hawezi kukisaliti chama chetu, mkombozi wetu watanzani, m naona atoswe wabakie watu wenye uchungu na rasilimali zetu ili tuzifaidi,
 
na ausome huu ujumbe na kuchukua maamuzi mapema kabla ya wakati kumwishia
 
Yeye ndiye atakaye fanya wote tumuamini. Nina hakika akifanya hili, sisi wapenzi wake na washabiki wa chama chake tutamuamini na sisi tutawalazimisha viongozi wenzake waanze kumuamini wapende wasipende,

Pole Mwanalugali. Ila usimpende MTU kwanza. Huyo Zitto ameshakuwa wa Rostam, hawezi kujinasua tena. Hawezi kuaminika tena.

Nashauri upenzi wako ufuate mtiririko ufuatao:

Kwanza uipende NCHI (linda rasilimali nk.),
Pili ndipo upende CHAMA (kufuatana na malengo na matumaini yako),
Na tatu ndipo umpende MTU (anayeweza kuongoza vizuri kupitia Chama makini).
 
AMAN WARID KABOURU anatoka kigoma na ndio alikuwa katibu mkuu wa CHADEMA na sio naibu katibu mkuu.
Naomba Great thinker yeyote aimalizie hii post yangu, maana natype uku nimejawa na hasila naweza nikaaribu keyboard yangu.
Pole sana ndugu kwa kupandwa na hasira! Kabouru alikimbilia CCM ambako ameenda kumezwa ambapo, leo hii siasa zake zimeshazikwa kabisa. Hata hivyo, hatumtishie Mhe. Zitto kwa yaliyompata Kabouru, bali bila shaka mchangiaji ameleta tu mfano kuonyesha jinsi CCM inavyoweza kuwalubuni wananchama mahiri wa vyama pinzani kwa leo la kuzika siasa zao. Hata hivyo, nani tena atakuamini hata kutoka jamii ya kwenu utokapo kama njia zilizopelekea kuhama kwako zilionyesha usaliti wa hali ya juu?

Kuna mazingira ambayo hata watu wakiona mtu anahama chama, basi ni rahisi kuelezea na mifano ipo (Dr. Slaa alipotoka CCM, John Magale Shibuda pia alivyotoka CCM kwa zengwe la kunyimwa haki yake ya kusimama kama mgombea). Si hili na Mhe. na kijana mwenzangu Zitto. Utarudisha vipi imani ya wananchi kama hata unashindwa kusimamia msimamo ulioamuliwa na wanachama ndani ya kikao halali?

Cha msingi ninachoweza kusema, jaribu kujipa mwanya wewe binafsi wa kujifunza "UONGOZI" maana hakuna anayezaliwa kuwa kiongozi. Chukulia yaliyotokea juzi na jana ni changamoto katika njia zako za kujifunza kuongoza jamii. Lakini pia kumbuka kwamba, kiongozi ni yule anayeweza Ku-influence watu awaongozao kwa kuwafanya waamini njia uipitayo. Kama juzi watu hao walionyesha wasiwasi na njia uliyotaka kuwapitisha, basi jiulize wapi ulikosea na kurekebisha makosa hayo ili safari iendelee. Kujifunza uongozi ni mchakato unaohitaji muda wa kutosha, na hakuna kipindi kitafika utasema umetosha kujifunza uongozi. Kila kuchapo tunajifunza kitu hiki adimu katika jamii zetu. Ukiweza kusimamia kile wengi wakiaminicho, basi wewe utakuwa kiongozi bora na uongozi wako utakuwa na changamoto chache njiani.
 
Naungana na mtoa hoja na nawakubali mamoderator wetu hapa jamvini. Tukitumia maneno au lugha ambayo si nzuri inaonekana wote hapa hatuko sawa na wala unachokijadili hakina maana. Ni kweli kila member ana mawazo yake na sidhani ki mtazamo tunaweza kuwa sawa la msingi tuwe wastaarabu na kuheshimu mawazo ya wenzetu wanayotoa na si kutoa lugha chafu. Naamini kwa mtu kama Zitto atayafanyia kazi maneno haya si lazima atuambie. Kingine tufaham kuwa hakuna asiyekosea kwa hiyo akiomba msamaha inabidi asamehewe na kama ana nia ya dhati utaona atakachofanya baada ya huo msamaha na si kumhukum kijana mwenzetu mapema hata kablya ya yeye kufanya maamuzi. Kama walivyofanya wazee wa Chadema aangalie mwenyewe je ataweza na si kumbomoa au kumfukuza. Nawapa big up wazee na viongozi wa Chadema pongezi kwa kuonesha busara na ukomavu wa mawazo katika kutatua tatizo ambalo lilikuwa mbele yao. Wananchi wanafahamu sana kama mtu amekosea au la na jinsi ya kumuadhibu pale anapoendelea kukosa adabu.
 
Mhe. Zitto, Mbunge na Katibu Mkuu Msaidizi wa CHADEMA,
rejea barua yangu ya wazi niliyokuandikia leo asubuhi nikikuomba ufikirie upya mstakabali wako kisiasa na uamue cha kufanya ukizingatia maslahi yako, maslahi ya chama chako na matarajio yetu wapenzi wako na wafuasi wa Chadema. Nadhani umeona reaction za wanajamvi wengi kuhusu barua ile na umeona kuwa watu wengi wameifurahia ile barua ingawa wengine hawakuwa na uhakika na utakavyo ichukulia!

Lililodhahiri ambalo nimeligundua katika hoja zilizotolewa ni kuwa wale wafuasi wa CCM, NCCR, na CUF wamejitokeza kwa wingi wakisema ukomae/ujitoe/usikubali/ufukuzwe/utoswe n.k . Hawa ni wazi hawakitakii CHADEMA heri, wanajitahidi kuwachochea viongozi na wanachama wengine wa chama chako wakuchukie au wasifikirie suala la kusameheana. Lakini ninayo imani kuwa CHADEMA watajifunza kutoka katika vitabu vitakatifu vya mwenyezi Mungu vinavyo zungumzia kusamehe saba mara sabini! Naamini Viongozi wetu katika Chama wanajua suala la mwana kondoo aliyepotea kwenye vitabu vitakatifu, maana Mchungaji alilazimika kuwaacha kondoo wengine na kwenda kumtafuta mwana kondoo mmoja aliyepotea! Hivyo naamini wale wanaosema kuwa wewe hustahili kusamehewa au kuomba msamaha si waumini wa kweli bali ni waharibifu wanaotumia njia zozote kuleta mikanganyiko ktk chama.

Mheshimiwa Zitto,
Wanachama wengi na wapenzi wa chama chako wanakupenda na wanakuhitaji sana! Mimi nakushauri uchukue hatua uwe shujaa wetu kwa kuhakikisha amani na utengamano unadumu katika chama chako. Hawa wanaokuita na kukuchanganya wakiombea mkono mmoja wa CHADEMA udondoke ili nao angalau waambulie mfupa, hawakutakii lolote jema. Najua wengine wanataka uende kwao wakupe uenyekiti wa chama, wengine wanakutaka tu eti kwa sababu ya dini yako, na wengine wanakutaka ujiunge nao tu ili CHADEMA ikae ikiyumba na wapate ahueni kwenye uchaguzi ujao!! Chonde chonde ndugu yangu, Mheshimiwa Zitto usiwasikilize wala usiwaamini! Watakupa chochote utakacho, lakini kwa hakika hawatakupatia amani wala furaha ya kudumu, maana najua Chadema ni chama chako cha kuchagua! Naomba upime haya yote na uchague lililo jema kwa nchi yako na kwa mstakabali wa taifa letu! La, ukiamua kufanya uchaguzi kwa kuzingatia msala upitao, basi historia ndiyo itakayokuja kutueleza lililokuwa pumba na lipi lilikuwa mchele!
Kalaghabaho mwene wachu.
 
Tatizo lake huyu dogo tamaaaaaaaaaaaaaaaaaa ndio zinazomponzaaaaaaaaaaaaa na siku zote watu wenye tamaaa ni rahisi sana kutumiwa na watu kama ROSTAM AZIZ na wengine wengi tuuuuuuuuuuuuuuuuuu.acha tamaaaaa bwana mdogo.

Acha Tamaa mwanangu alinionya mama aliyenizaa jitunze wewe alisema yeyeyeee! Wimbo ulikua mtamu huu
 
Unasema eti,
Hivi sasa najua umekuwa lulu kwa wanaCCM,

Mtizamo kama huu, ndio unatudhohofisha na kurudisha nyuma Taifa letu. Yaani kati ya Watanzania woooooooooote huyu tu ndiye awe lulu? Kwa lipi?

Anaweza kuwa ana sifa za kuwa Mwana-Siasa lakini kuanza kumpigia mtu magoti na kumnyanyua eti ni lulu wa chama chochote nasema
a big nope!
Aliyoyafanya, ni kufanya assignment yake ya kutafiti juu ya mambo mbalimbali nchini, kisha akatumia kauli zake kuyaongea Bungeni, ktk Vikao na katika hadhara, ingawa hata wakati mwingine (si wote) kauli zake zimekuwa chini ya kiwango tunachomfikiria au anachostahili.

Utendaji wa namna hii ni wa kawaida sana na kwa taarifa yako wako wengi sana Tanzania wanaweza kufanya hivi. Narudia tena kuwa ni kawaida sanaaaaaaana!

Namshauri kama mtu mwingine yeyote kuwa, apime matendo yake mwenyewe na ya Viongozi wake na afanye uamuzi anaoona unafaa kwa Taifa lake, Jimbo lake, Chama chake, familia yake na kwake mwenyewe. Narudia hakuna cha 'ululu' hapa, vinginevyo hata mimi nitaanza kujipa 'udhahabu' na mwingine 'utanzanite!' n.k.

Ni hatari sana kufikiria kuwa bila mtu fulani mmoja au kikundi fulani basi hakuna maendeleo au maisha.
 
Zitto AFUKUZWE Chadema:
-Huyu ni Fisadi
-Huyu ni haramia wa kisiasa
-Huyu ni mnafiki
-Huyu ni msaliti wa umma
-Huyu ni msaliti wa chama
-Huyu ni changudoa wa kisiasa
-Huyu ni mroho wa pesa za RA
-Huyu ni kigeugeu
-Huyu amenunuliwa na mafisadi wa chichiema
-Huyu hafai kuajiri na waTZ kwa namna yoyote
-Huyu ni kama Kabou aliye kuwa katibu mkuu wa CDM toka Kigoma
-Huyu ni toka Kigoma, Kigoma wanatoka wasaliti wa CDM
WHEREFORE CDM imfukuze mapema iwezekanavyo, ametumwa na kununuliwa ili aiue CHADEMA.
 
watanganyika mi na mashaka na huyo mwandishi wa barua hiyo na hisi huo mpango wa kumsafisha huyo zito. Ndugu zangu zito hastahili kusamehewa na kuthamaniawa na wananchi mpaka ajibu hoja za muhimu zinamkabili kama ifuatavyo...1.yeye na zoka wa usalama wa taifa wanamahusiano gani mpaka wapigiane sim zaidi ya mara 9 kwa siku?. Yeye ni nani hasa mpaka awe na urafiki na mafisadi akiwemo jk? Na pia yeye ni nani na kafanya nini ktk historia ya tanganyika mpaka aonekane kua bila yeye hatuwezi kuiangusha ccm? Kama sote wanaharakati tunaamin ccm ndio inawabeba mafisadi na kuwalika na kuturudisha iweje zito awe na urafiki na mwenyekiti wa chama hicho mkwere? Huyu kijana hafai na kammwe sinto msamehe na sinto muamini. Sio mzalendo ni mbinafsi na anapenda sifa binafsi. Hatuhitaji mtu kama zito ambae ni kigeu geu, nawasilisha.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom