Mheshimiwa Zitto Kabwe,
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
na Katibu Mkuu Msaidizi wa CHADEMA.
Mheshimiwa,
Kwa siku za karibuni jina lako limevuma sana katika vyombo vya habari kwa masuala mbali mbali na Watanzania hasa wanachama na wapenzi wa chama chako wamegawanyika ktk mapande mawili, wengine wakikushutumu na wengine wakikuunga mkono! Mimi leo kupitia JF ambako najua wewe ni mwanachama, naomba kupita mstari wa katikati na kukushauri kitu cha kufanya katika kipindi hiki kigumu kwa chama chako na wewe binafsi.
Kama sikosei mheshimiwa, umri wako bado ni mdogo hivyo kunipa imani kwamba bado unayo miaka mingi ya kufanya kazi hizi za kisiasa kuliko viongozi wenzako wengi mlioko CHADEMA. Najua na nina amini kuwa unao uwezo mkubwa wa kufanya siasa lakini kwa hakika wale wote tunaokupenda umetuweka roho juu na hatujui your next move. Lakini Mheshimiwa, kwa jinsi hali ilivyo nakuomba usifanye move yoyote itakayo kuumiza wewe binafsi, kuumiza chama chako au kutuumiza sisi tunaokupenda na kukushabikia!
Hivi sasa najua umekuwa lulu kwa wanaCCM, wanakutaka pia wanataka kukuchanganya kwa sababu wangependa kuona chama chako kikisambaratika ili ifikapo mwaka 2015 wasipate changamoto kama walizopata ktk uchaguzi uliopita. Najua pia kuwa vyama vya NCCR MAGEUZI na CUF wanakumezea mate na wangependa ufanye chochote ili uondokane na hawa CHADEMA na ikiwezekana uungane nao bila kujali maisha yako kisiasa.
Mheshimiwa Zitto,
Usikubali kupoteza mtaji wa kura zaidi ya Milion 2.5 zilizopatikana kwenye uchaguzi mkuu kwa chama chako. Najua kuwa ulichangia moja kwa moja au inderectly kupatikana kwa kura hizo ambazo mimi naona ni mtaji kwako wewe Mheshimiwa. CHADEMA siyo ya Mbowe, Slaa, Mtei wala Kiongozi yeyote. Naamini kuwa Chadema ni yetu sisi wananchi na wanachama wote hivyo mapambano yoyote yanayoendelea kwenye chama ni kielelezo cha mstakabali wetu na lazima historia itakuja tujuza pumba na mchele.
Mheshimiwa, nakuomba uvumilie kama kuna matatizo yoyote kwenye chama, nakuomba ufanye uamuzi wa kishujaa utoke hadharani uombe msamaha kwa yote unayotuhumiwa nayo haafu uchukue hatua ya kuwaandikia barua ya kuomba msamaha viongozi wenzako. Ukifanya hivyo, utakuwa umeshinda vita zote zilizoko mbele yako na utaonekana shujaa ktk chama chako. Najua kwa kufanya hivyo, CCM watasikitika na kukusema kuwa umeisha kisiasa lakini mimi nadhani kuwa utakuwa umezikumbatia zile kura milioni 2.5 zilizopatikana kwenye uchaguzi uliopita na utakuwa umejitengenezea njia nzuri ya kuelekea 2015.
Mheshimiwa, ni vema nikasema kuwa ni heri kupiga hatua moja mbili nyuma kuliko kurudi mwanzo na kuanza upya ili uweze kusonga mbele. Wanaokwambia ujiondoe CHADEMA hawakutakii mema wewe binafsi wala chama chako na wale wanaosema ufukuzwe hawajui mtaji uliowekeza kwenye chama na wala hawakitakii chama chako prosperity. Ndugu yangu Zitto, nakuomba utumie changamoto zilizoko sasa ufanye siasa ambyo itakuimarisha wewe na chama chako ili hata wapinzani wako waanze kukuamini na kujua kuwa wewe ni kijogoo wa siasa za Chadema.
CHADEMA for Life.
Sikiliza sauti kutoka kwa mama yako Mzazi,
Heshimu viongozi wenzako na kila anayekutakia mema kwenye Chama
Uwiwanyu Agukunda