Barua ya Wazi kwa Rais Magufuli, kutoka kwa wafanyakazi wa NIDA

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,321
11,315
Mheshimiwa rais wetu mpendwa, rais mpenda haki, rais wa wanyonge kama sisi katika hii barua, baba na mlezi wetu, barua hii iliyoandikwa kwa uchungu nasi na kilio hichi kikufikie uweze kuchukua hatua.
Asante.

================

MH: RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
IKULU,
P.O.BOX 11400
DAR ES SALAAM,
TANZANIA.

YAH: BARUA YA WAZI KWA MH.RAIS KUTOKA KWA WALIOKUWA WATUMISHI WA MUDA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA (NIDA)

Mheshimiwa Rais sisi ni Wafanyakazi tuliokuwa tukiitumikia mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA). Tumeitumikia mamlaka kwa vipindi tofauti tofauti kati ya mwaka moja hadi minne na kusitishwa mikataba yetu ya ajira mnamo tarehe 07/03/2016 baada ya masaa ya kazi kuisha kupitia Televisheni ya Taifa (TBC).

Taarifa hiyo ilitolewa na kaimu Mkurugenzi mkuu wa NIDA Dr. Modestus Kipilimba ambapo kwa mujibu wake idadi yetu tulikua wafanyakazi 597. Tulipokea kwa masikitiko makubwa sana, kwasababu taarifa hiyo ilikuwa ni ya ghafla na ya kushtukiza.Mkurugenzi alishindwa kufuata utaratibu wa kiofisi na kutumia vyombo vya habari.

Mheshimiwa Rais Tunapenda Umma wa watanzania ujue kuwa usitishwaji wetu wa ajira haukuwa wa halali, kwa sababu haukufuata sheria, kanuni na utaratibu za kazi kama inavyoelezwa chini ya kifungu cha sheria ya Ajira na mahusiano ya kazi ya mwaka 2004.

Taratibu za kusitisha ajira zinatofautiana kutegemea na sababu za kusitishwa ajira lakini zote zina kipengele cha pamoja ambacho ni haki ya mfanyakazi kusikilizwa kabla maamuzi ya kusitisha ajira hayajajadiliwa dhidi yake. Mh Rais tunakubaliana na maamuzi ya mamlaka na sababu ambazo uongozi umezitoa kwasababu za kiutawala.

Mheshimiwa Rais baada ya kupokea taarifa hiyo tulichukua hatua zifuatazo:-

1. Tuliomba muajiri wetu atupatie barua ya kuachishwa kazi kwa maandishi, ilichukua muda kidogo katika utekelezwaji wake lakini baadae mwajiri alitekeleza ombi letu, lakini barua hiyo ilikuwa na mapungufu yafuatayo:-
a. Barua haikueleza ni stahiki gani na malimbikizo gani tunayostahili kulipwa baada ya kuachishwa kazi, angali mikataba imesitishwa kabla ya wakati.

b. Barua ile haikutamka wazi kuwa lini tutalipwa stahiki zetu.

c. Pia kuna baadhi ya wenzetu hawakufanikiwa kupata barua kwa madai yakuwa Ofisi haina kumbukumbu au taarifa zao na wakaomba waandike barua za kuomba kazi upya sambamba na kupeleka wasifu wao (CV) ndipo wawaandalie barua ya kusimamishwa kazi, huu sio utaratibu, ni kukiuka sheria na kanuni za ajira.

d. Barua haikutamka kuwa tuna mafao kiasi gani katika mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo tulikuwa tukichangia kila mwezi kutokana na makato ya asilimia kumi (10%) katika mishahara yetu.

e. Haikutamka kuhusu makato yetu ya bima ya afya tuliyokuwa tunakatwa asilimia tatu (3%) kuchangia mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF),lakini hata fomu za kuomba uanachama hazikupelekwa japo tulikuwa tunakatwa kila mwezi.

2. Tuliomba taarifa fupi kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo tulikuwa tukichangia na tukabaini yafuatayo:-
a. Mifuko ya GEPF, PSPF, LAPF, na NSSF mwajiri alipeleka kwa mara ya mwisho michango yetu mwezi wa saba 2015.Hii ilionyesha kuwa mwajiri wetu hakuwa anapeleka makato yetu kama ilivyotakiwa. Tunaomba Mheshimiwa Rais ufuatilie upate kujua ni wapi hasa pesa zetu hizi halali zilipokua zikipelekwa na ni akina nani hasa walipewa fedha hizi halali zilizotokana na jasho la watumishi wako na kwa madhumuni gani, na zaid mifuko hio ya hifadhi ya jamii kwanini na wao walikua kimya kipindi chote hicho ambacho michango ya wanachama wao ilikua haipelekwi.

Mheshimiwa Rais tunatambua jitihada zako za kutumbua majipu na kuwawajibisha mafisadi wanaohujumu uchumi wa taifa, mheshimiwa Rais kuna haja ya kutumbua majipu hapa.

Mheshimiwa Rais, Tuliandika barua kwa msajili wa mifuko ya jamii SSRA, majibu tuliyoyapata ndio yaliyotusukuma kuandika barua hii kwako kwasababu hayakuridhisha.

Tunashindwa kuamini kama leo hii tumekuwa watu wakulilia haki halali inayotokana na jasho letu ndani ya nchi hii iliyokwisha pata uhuru. Tunatambua kuwa nchi hii inaendeshwa katika misingi ya sheria na kusimamia haki ya kila mwananchi kama katiba yetu ya mwaka 1977 ilivyoamuru, lakini Mh. Rais haya yanayoonekana mbele yetu ni kinyume na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Ujira ni sehemu halali tunayostahili kulipwa kutokana na jasho letu. Mtu yoyote katika meza yako akinywa kikombe hiki hatasita kupaza sauti.

Mheshimiwa Rais, sisi tunarudi mtaani kupambana na ule utaratibu wako kuwa vijana wazururaji wasio na kazi wakamatwe. Tunaomba tilipwe stahiki zetu mapema tunazodai kutokana na jasho letu halali.

Mheshimiwa Rais, sisi wengi wetu hapa ni vijana tuliohitimu baadhi ya vyuo vikuu hapa nchini, kazi hii ingetuwezesha kurejesha mikopo tunayodaiwa na bodi ya mikopo kama sera mpya ya Bodi ya mikopo zinavyoagiza, pia Mheshimiwa Rais umekua ukisikika kwenye nyumba za ibada na kwenye mikutano mbalimbali ukisema " Asiyefanya kazi na asile", lakini kwetu sisi imekua ni tofauti, tumefanya kazi bila mishahara yetu kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu tulipositishiwa mikataba yetu.

Mheshimiwa Rais maombi yetu kwako, mateso tunayoyapata kwa sasa ni makali mno, madhara na athari zimejitokeza kwa baadhi yetu wengine wamepata stroke, pia wengine wamefukuzwa kwenye nyumba walizokua wamepanga kwa kukosa kodi, athari nyingine pia zimejitokeza katika familia zetu maana wengi wetu tulikua tegemezi katika familia zetu, athari za ujauzito kutoka kutokana na jinsi jambo hili linavyoendeshwa na mengine mengi. Kilio chetu kikubwa ni malimbikizo ya mishahara yetu ya miezi 3, yaani kuanzia mwezi wa kwanza mpaka mwezi wa tatu mwaka huu ajira yetu ilipositishwa, pia stahiki zetu zote zinazotamkwa kisheria katika kifungu cha 44 cha sheria ya Ajira na Mahusiano ya kazya mwaka 2004 inayohusu taratibu za kusitisha mikataba ya Ajira.

Mheshimiwa Rais tunaomba uingilie kati swala hili tuweze kulipwa stahiki zetu na malimbikizo ya mishahara yetu mapema, ili tuweze kuendesha maisha yetu ambayo yamekuwa magumu mno, pia tukaendeleze sera yako ya kilimo kwa vijana.

Mheshimiwa Rais, tunamtaka Kaimu Mkurugenzi Mkuu Dr. Modestus Kipilimba atamke wazi ni siku gani hasa atalipa mishahara yetu na mafao yetu tunayodai na sio jambo analolifanya yeye pamoja na wasaidizi wake kueneza ahadi zisizotekelezeka kwenye vyombo vya habari ili aaminike anajali wakati ukweli halisi familia zetu zinashinda njaa na kupitia kipindi kigumu sana.

Tunakupongeza kwa kazi nzuri unayoendelea kufanya katika serikali yako tukufu, tunatumaini kilio chetu kitakufikia na kuchukua hatua.
Asante.
Imetolewa na sisi wafanyakazi wakiwa na wanyonge waliositishiwa mikataba ya ajira

MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA(NIDA).
 
Attachments

  • BARUA KWA RAISI final.docx
    11.9 KB · Views: 72

TATIZO MLIKUWA NADHARAU SANA KWA WANANCHI WENGINE KAMA VIONGOZI WALIVYONADHARAU KWA WANACHAMA WAO
 
Wengi mlishikwa mkono mkapewa kazi hapo, anyways, poleni sana ila yaliyotokea hapo hayavumiki. Ni kama mechi inapopigwa uwanjani nyasi hata kama ni za bandia lazima ziumie. When one door closes many others opens, endeleeni kupambana mh amewasikia naamini atawasaidia
 
Actions and reactions are equal but opposite!
Kumbe nanyi mnafeel pinch inapokula kwenu ?
Ndio mjue impact ya kuleta sanaa badala ya professionalism kwenye kazi.
No stone will be left unturned.
 
So sad, kazi wamewafukuza, at least waheshimu sheria wanazozisimamia... haki itendeke na ionekane imetendeka...... serikali haipaswi kunyima mtu haki kwa namna yeyote ile..
Mungu awatie nguvu mkuu.......ni kipindi tu mnapita... Mungu atawaonyesha njia.
 
Hao ambao kumbukumbu zao hazipo it means ndio wale walioshikwa mkono. Sikuwahi kusikia nafasi zikitangazwa lakini all in all wale walioshikwa mkono wawataafute wale waliowawezesha kupata haki Zao. Ila poleni sana karibuni kijiweni muone msoto tunaopigika nao. Ila inauma sana.
 
Poleni ila kipindi cha miaka minne mngetafuta kazu za kudumu mnepata maana soko LA ajira lilikua loose kidogo, ila ndo hivo jipangeni upya maana, naamini serikali haiwezi kuwanyima haki zenu , inategemeana na mikataba mliiyoingia na shirika.
 
Lowassa aliyaongea Jana haya mambo vijana wa Lumumba wakaja na povu juu.Hii ni dhuluma ya waziwazi kwanini usimlipe mtu stahiki zake kama umemwachisha kazi.Kama hukuwa na pesa ungesubiri upate ndio uwaachishe.Busara iko wapi?
 
Hili swala la mimba kutoka limenitia majonzi. Hata hvyo ni somo kwenu watumishi tuwe tayari ktk kila jambo. Maana kuna uzi humu ulikuwa unazungumzia utendaji mbovu wa hii taasisi. Ikiwemo kutiana tu mimba na kunywa chai mpaka saa nne. Naona maelezo ya barua hii kama yanareflect ukwel wa mambo
 
Back
Top Bottom