Barua ya wazi kwa Mkuu wa Mkoa Mara kutoka CHADEMA mkoa Mara

USTAADHI

JF-Expert Member
May 10, 2011
1,516
136
Hali si shwari kwa viongozi wa CHADEMA mkoani hapa kufuatia mlolongo wa matukio ya kinyama yanayowakuta viongozi wa CHADEMA ngazi mbalimbali wakiwemo wawakilishi wa wananchi kwa tiketi ya CHADEMA

Leo tarehe 20 -11-2014 amechinjwa katibu wa CHADEMA tawi la ROSANA ndugu MATIKO MAKENGE akiwa nyumbani kwake kata ya nyarero baada ya kutoka katika majukumu ya kuwasaidia wagombea kujaza fomu za serikali

Tarehe 18-11-2014 alivamiwa kijana Mwita Isack Kegora Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la mawasiliano na pia mfadhili wa CHADEMA kata ya bomani na mtu anayesadikiwa kuwa ni jambazi wa kukodiwa na kumuuwa kwa kumchoma kisu (MPAKA SASA HATUNA IMANI na kitendo hicho kama sio cha kisiasa )

3 Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Nyarero mzee ABDI MASWI naye amepokea ujumbe wa kuuwawa mara kadhaa kutoka kwa watu wanaosadikiwa kuwa ni wapinzani wa kisiasa wa CHADEMA wakimtaka ajitoe la sivyo roho yake ni halali yao

SERENGETI
Diwani wa kata ya nyansurura ndg JACKSON CHACHA MWITA ameshikiliwa na Mahakamana kunyimwa dhamana kwa amri ya mkuu wa Wilaya ndg JOHN HENJEWELE anayekaimu mkuu wa Wilaya Serengeti katika kwa madai ya kugomesha michango ya maabara katika kata yake ...huku undani wa sababu ukionesha dhahiri kuwa ni kudhoofisha nguvu ya chama na kukoswa leadership command figure katika eneo hilo
mgombea wa serikali ya kijiji cha mara somoche ametumiwa ujumbe mara kadhaa wa kumtaka kutochukua fomu la sivyo atakumbana na kesi ya meno ya tembo. Hali kadhalika mtendaji wa Kata ya Nyansurura amezuia utoaji fomu kwa wagombea wa CHADEMA katika nyakati mbalimbali.

MWIBARA
Mgombea wa serikali ya kijiji cha IGUNDU ndg MTESIGWA MSASE mpaka sasa amekamatwa na na kuzuiliwa polisi kujaza fomu ya Serikali aliyopaswa kujaza leo kwa tuhuma za uchochezi alizofanya kwenye mikutano ya Serikali ya Kijji mwaka uliopita.

RORYA
mwenyekiti wa kijiji cha kiariko anayemaliza muda wake naye amehukumiwa miezi 6 ama faini ya tsh 300000 ili kumtengenezea mazingira asigombee tena mbali na manyanyaso na mauaji na mlolongo wa huu UWAZI UMEKOSEKANA MAENEO MBALIMBALI

1watendaji wengi wameandaliwa kuhujumu fomu za wagombea wa chadema pindi zinaporudishwa kwa kujaza namba na kuharibu uhalisia wa fomu
2 kufunga ofisi siku ya jumamosi ili wasipatikane
3 halmashauri kuu za ccm wamekubaliana kuiba fomu kwa kuvamia wagombea wa chadema wakati wowote kwa kutumia vibaka na majambaz
4 mpango wa ccm kupita kila kaya kuorodhesha majina ya wakazi kinyume na sheria kwa kutumia mabalozi hapa mkoani pia inaaminika nyuma yake unaratibiwa na wakuu wa wilaya kwa ajili ya kuweka orodha fake za wapiga kura ili kuihakikishia ushindi ccm kwa vipengele hivi vya vielelezo tunashawishika kama chama mkoa kuwa serikali ama haiko tayari kuona uchaguzi wa amani unafanyika ama kuna maandalizi ya kuvuruga wito wetu kwa wanachama wa CHADEMA mkoa wa mara ni kuwa watulivu ila wasikubali unyanyasi kuvuka kiwango.

RAI KWA SERIKALI
ijitathmini kupitia serikali za mkoa na wilaya kama mienendo hii inaleta utulivu wanaoimba wao ama inachochea watu kukataa kwa nguvu haya maonevu na sisi kama chama mkoa hatuko tayari tena kuona hali hii inaendelea labda tujitoe

kwa mantiki hii tumia nafasi yako kama mkuu wa mkoa kurejesha amani ya watu bila kujali itikadi japo tunatambua upo kwa maslahi ya serikali ya ccm zaidi.

MWL CHACHA HECHE
KATIBU WA CHADEMA MKOA

Nakala kwa mratibu wa CHADEMA Kanda
Nakala kwa Katibu Mkuu
 
Hii issue mbona inatisha sana! Je CDM HQ au KANDA wanajua na kama wanajua wamechukua hatua gani? Hapa ninaona basi uchaguzi wa serikali umeishaingiwa na dosari!
 
Haya tuliyatazamia na bado. Mwaka huu CCM wameshikwa pabaya na hawana pa kutokea. Wakumbuke jitihada aiondoi kudura. Mwisho wao umefika.
 
Mara ninavyowafahamu wakianza kulipiza visasi hakutakalika. Kama serikali inaona hayo na inanyamaza isubiri visasi vianze maana muosha uoshwa.
 
jamani malalamiko hayana msaada kesi ya nyani upeleke kwa ngedere chukeuni hatua kama moto ni moto..mwisho wa siku wagombea wenu hawatapitishwa mtaanza kulalamika hii ni vita huyo mnaempelekea kesi ndo ametoa maagizo hayo mnategemea nini ...wakimwaga mboga niyie mwageni ugali.......ni piga nikupige hapooo msiwe watu wa kulalamika mda wa vitendo umefika naona kama chadema ya kipindi kile ya mkoani MARA inaanza kuwa ya uoga uoga jamani tunawategemea sana watu wa mkoa wa mara mkianza kulalamika huko sijui chadema ya mikoa kama tanga wafanyeje
 
Kama ccm awataki vyama vingi basi wavifute, kuliko kutesa raiya wasioyokuwa na makosa
 
Siasa za Ccm ndo kawaida yake, musoma mjini 2010 aliyekuwa mgombea wa ccm aliunda timu ya mauaji ikiongozwa na mjumbe wa Nec Rukwa anaitwa Maganga Kampala waliumiza sana watu
 
Uchaguzi wa serikali za mitaa tu visa vyote hivyo?Uchaguzi mkuu 2015 ccm
itasababisha machafuko makubwa sana katika nchi hii!
 
Inaskitisha sana, lkn wakati mwingi ukichunguza vizuri kwa makini utakuta pesa za escrow acc zinausika kwenye haya mauwaji
 
Mara ninavyowafahamu wakianza kulipiza visasi hakutakalika. Kama serikali inaona hayo na inanyamaza isubiri visasi vianze maana muosha uoshwa.

Ndugu yangu hiyo nimipango yao yakuhakikisha wanashinda unafikil nani atatoa kauli yakalipio wakat nihaohao,wafanye hvyo nao upande wapili waone kitachowatokea.
 
jamani malalamiko hayana msaada kesi ya nyani upeleke kwa ngedere chukeuni hatua kama moto ni moto..mwisho wa siku wagombea wenu hawatapitishwa mtaanza kulalamika hii ni vita huyo mnaempelekea kesi ndo ametoa maagizo hayo mnategemea nini ...wakimwaga mboga niyie mwageni ugali.......ni piga nikupige hapooo msiwe watu wa kulalamika mda wa vitendo umefika naona kama chadema ya kipindi kile ya mkoani MARA inaanza kuwa ya uoga uoga jamani tunawategemea sana watu wa mkoa wa mara mkianza kulalamika huko sijui chadema ya mikoa kama tanga wafanyeje

huyu dogo anawamudu inaonekana ila akaze buti na chama wampe support
 
Huzuni kubwa wanaua raia wenzao sababu tu ya madaraka, hiki chama twawala kimeoza .
 
Back
Top Bottom