Barua ya wazi kwa mbunge wangu MH. HAWA GHASIA kutoka kwa mwanachi wa Mtwara Vijijini

Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,802
282
Kwako mama, mbunge wangu mpendwa,
Shikamoo.....

Kwa healshima nimeona nikutumie barua hii ili kukufikishia malalamiko na maoni ya sisi wanachi wa jimbo lako!!

ELIMU
Hali sio mzuri, hizi shule za kata hazina walimu wa kufundisha kwa kweli. Shule za MNIMA, KITAYA, MBEMBALEO, MTINIKO, MNYAWI NA ZOOTE mpya ni kichekesho. Eti shule za sekondari kuna mwalimu mkuu na walimu wawili. Nimeishi Moshi kwa miaka mitatu, hakuna jambo hili.

Mheshimiwa, hili jimbo lako unajuwa asilimia kama 65 hawajuwi kusoma wala kuandika!??? Tafadhali, jitahidi kuweka mkakati wa kukuza elimu.

Nanyamba Secondary School, tunaomba iwe high school. Najuwa haupendi watu wa eneo hili, sijuwi sio wamakonde wa malaba wa kwenu pwani??? ivi sasa wanakuogopa, waadhani ulimuua bwana CHINAVACHI, jambo ambalo si kweli, alikufa na UKIMWI tu,.loooh.

Tafadhali, ni aibu jimbo halina high school. Hii shule ni nzuri, mimi nimesoma hapa enz hizo,basi badilisha mambo. Kumbuka ni shule ya kwanza kongwe, hadi 2005 ilikuwa ni shule hii tu pekee ya sekondari, naipenda sana, fanya mkakati watoto wapate njia ya kwenda chuo kikuu. Mwenzako Chikawe yuko katika hatua ya mwisho NACHINGWEA DAY kuwa high school

MAJI
Mama hii ni hatari, juhudi za makusudi zinahitajika. Hakuna maji ya bomba jimboni kwako, unafahamu hili?? Najua ukanda wa pwani maeneo ya Kitaya umeweka ule mradi wa pump za kisima from underground water of ruvuma river!! Hali ni mbaya katika vijiji vyako, hasa vile vya karibu na Tandahimba. Mnyawi kuna mradi wa maji wenye kusaidia vijiji vingi sana, lakini nilifika.mara ya mwisho, ni vituko tupu, pump zimekufa. HIVI, una wazo la kupitisha umeme hapo kwenye chanzo cha maji ili kupump na kusambaza hayo maji?? Ulipita ukatengeneza matenki ya maji vijijin, ni miaka mitano sasa, hatuyaoni yanatoka, vipi mama??? tena una masters ya rural development..""""""

UMEME
hapa mama hauko fair hata kidogo. Vijiji vyote hata kimoja chenye umeme. Cha kushangaza, mnazi bay iko Msimbati ndani ya wilaya yako. Ni laana kufikiria kupeleka umeme Tanga wakati sisi wenyewe hatunufaiki. Ole wenu mupeleke huko kabla ya kugawa hapa Mtwara vijijini, mtaaaaniwa milele. Naongea kwanjzba kwa vile inaniudhi xana..
Mimi ni mzawa wa hpa jimboni. Plz, mh. ghasia hujachelewa, kuna vijiji vikubwa kama NANGURUWE, KITAYA, MSIMBATI, MBEMBALEO , NANYAMBA, NITEKELA, MNIMA,N.K. fanya juhudi za makusudi, andaa project, omba msaada huko ulaya, umeme uje.

KILIMO
hongera saaaana, korosho zinanunuliwa vema saana. Niko huku, watu wanafurahia. Wakati niko chuo kikuu nilifanya research ya stakabadhi ghalani, nilizunguka jimbo lote, nakupa hongera tena......... najua umeweka mkono mkubwaaa hapa!

TUNAWASILIANAJE NA WEWE MH MBUNGE???
Duuu, hapa ni ngumu!!! Nimejaribu kukutafuta kwa facebook, twitter na hata e-mail yako, bila majibu. Last month, nilimtembelea rafiki yangu anayesoma MWALIMU NYERERE ACADEMY akasema uko strictly, haupatikani kabisa. Tulikuja hapo wizarani tukuone, haaaa, mbona hao watu walitukatisha tamaaa majibu yao!! Naskia kuna baadhi ya wazee wako wa huku nyumbani wana namba za simu...... kumbuka hawa hawana elimu na exposure ya kukushauri. About 99% ya hawa hawana elimu hata ya form two.Tena madiwani wako wote haaawaaana elimu hata ya form four......... naomba usomapo, unipe njia ya kuwasiliana na ww.

UKUAJI WA UCHUMI.
Mtwara mjini mambo yamekucha...kwa sasa ni kama mtaa fulani wa CAPE TOWN.... nafurahi sana juhudi zako za kukuza huu mji. Lakin ni Mkapa aliyeweka hii mikakati under umbrela of MTWARA CORRIDOR..... kuna kila kitu, nyumba za kisasa zinajengwa, barabara za mitaani ziko na lami, majengo ya mkoa yamekarabatiwa upya, nyumba ya mkuu wa mkoa ni kama white house.......

Lakini, maisha ya vijijini bado ni magumuuuuuuuuuu, yako vile vile. Au unataka sisi wasomi vijana tujiunge na upinzani tukunyang'anye jimbo??? ni rahisi, najua tukujioganaiz tunaweza. Nimesoma hapa Nanyamba, kika kijiji najua kuna mtu nimesoma nae, wengine wana digriii na wengine wako huko...... tunaweza kuandaa vuguvugu, after all wewe najua kuna sehemu haukubaliki. LAKINI, BADO TUNAKUHESHIMU, MI NATAKA UFIKD HADI 2020 MAMA, TUMIA ELIMU YAKO SIO KUKAA HUKO DAR NA KUDEAL NA ISHU ZA KITAIFA. Yaani hata ndugu katani wa CUF pale Tandahimba haumfikii kwa anavyohamasisha maendeleo.

UVUNAJI WA RASILIMALI
hapa kila siku najiuliza, je hawa wazungu na wawekezaji wanaokuja kuvuna utajiri wa jimboni kwetu wana tija?? gas inazalishwa, mafuta yameanza kuchimbwa, kiwanda cha.sementi kinnajengwa,je mimi mzawa na wanakijiji wenzangu tulioko vijijini tunanufaikaje?? Mfano, mimi niko hapa Lipwidi kijii cha ujamaa, nauza dagaa pamoja na elimu yangu coz nna diploma ya ualim na shanhada ya uhasibu na fedha...... ctaki ajira zenu, isje wana jf muniambie niombe kaz

MWISHO
Nakutakia maisha mema mama.... niko njiani kuwaongoza wna mtwara. Nimeombwa na vijana na wazee nigombee ubunge 2015, nafikiria ombi lao. Then, mimi najuwa hunijuwi, lakn muulize HAMISI NAMALECHE NA SHARIFA MPEME...

MY TAKE,Kijana anachezea maisha, huyu mama ni mchawi.........baba ni hatari!!
 
Common song! mkuu hamasisha wananchi wa huko wakae mkao wa mabadiliko ili 2015 huu wimbo usiwepo. Japo najua siasa za huko ni ngumu kutenganisha na dini
 
Fair kabisa, Alipokosea umemuonesha na alipofaulu umempa credits.

Sasa kazi kwako Mh. Mbunge, kama korosho umeweza hayo mengine jitahidi
 
Nimewahi fanya kazi kwa muda Mtwara vijijini, hali inatisha sana hasa upande wa elimu na maji.
 
sasa mkuu unamuuliza huyu kilaza kuhusu facebook na twiter?sidhani kama anajua kutumia mouse!
 
Nimewahi fanya kazi kwa muda Mtwara vijijini, hali inatisha sana hasa upande wa elimu na maji.

tatizo ni mambo ya dini mkuu....
wananchi wa enzi zile walikataa shule eti kisa wanaogopa kura nguruwe.

mfano mzuri baba yangu..... ndio chanzo cha umaskini mtwara vijijin....
 
huyo mama ni kilaza na sijui hata jk alitumia criteria gani kumpa uwaziri
 
Mzee! Rasiliali za kitaifa kama gas, mafuta (kama yapo) nk si mali ya jimbo ni za taifa. Umeme wa mnazi bay waweza pelekwa hata huko Tanga na kwingineko even kabla ya jimbo la Mtw V. Koni watu wa Geita au Nyamongo wananufaika na nini na kuwepo madini kwenye ardhi yao kama si chemikali za sumu na kupigwa shaba. Hope will act in the same manner though not right.
 
haaaaa, sina maana hiyo!?
rudia tena kusoma uje ukomenti....
nimesema hakuna kijiji hata kimoja chenye umeme!!!!!
 
Acha uoga gombea.................. . Sasa wewe eti Mbunge mtarajiwa halafu unatoa shikamoo kwenye barua??? No wonder ana kiburi sanahuyu dada............ halafu unasema ulisoma enzi zile au ile hijab unafikiri ni mama mzee?? Ni kijana tu yule.
 
Wamakonde tatzo lenu mnaongea sana na hamfanyi mambo kwa vitendo.Frankly speaking nachelea kusema mmechelewa sana kukombolewa KIFIKRA.Wahimize nduguzo wasome kwani siku hizi Mtwara kuna influx kubwa ya wasomi Mtwara ya sasa tofauti na zamani.
 
Pasco jnr, nimeipenda hii barua yako kwa Mama Ghasia haswa ulivyobalance mazuri na udhaifu wake.

Nimebahatika kumfahamu Hawa Ghasia kwa karibu, ni mtu anayejali watu and she is down to earth. Niliwahi kutana naye kwenye mkutano wa African Civil Service mahali nje ya nchi. Wakati wa lunch break aliponiana japo ni mwandishi tuu aliniuliza kama nimeshakula, nikamwambia sisi waandishi hula nwisho!. Akaniambia maadam na wewe ni Mtanzania mwenzetu, jiunge nasi, nikajiunga na gvt delegation nikala VIP!. Huu ni ushahidi sio mtu wa kujiskia au kujiona yuko simple na down to earth!.

Ukimfikiria Hawa Ghasia na kuangalia maisha yake, hata mumewe ni mtu wa watu na ni mtu wa msaada sana!. Watanzania wanaoishi India hili wanalijua nami ni mmoja wa waliosaidiwa sana na Bw. Yahya Mhata!. Mungu awabariki sana hawa watu kwa mioyo yao mema!.

Ila pia ni kweli kwenye e-mail anapatikana kwa taabu!. Hata hii barua ya wazi kama imetumwa JF pekee, then haitamfikia!. Nenda pale Utumishi muone binti anaitwa Zama omba e-mail ya Zama, ukimtumia Zama, kwa Hawa Ghasia umemfikia!.

Kati ya yote uliyoeleza, mimi limenigusa zaidi hili la kuanzisha harakati, Mikoa ya Kusini ndio ngome kuu ya CCM. CCM ina take advantage ya umasikini na ignorance yenu kuji legitimize kuwa iliumbwa kutawala milele!. Ujio wa Mtwara Corridor na gesi na mafuta ita itransform Mtwara kuwa heaven na wakazi wa asili mtajikuta mmesukumwa deep interior na mabwana wa pesa ambao watainunua pwani yote na kuimiliki kama hali ilivyo Bagamoyo, Dar na kule Zanzibar wakazi asili wamehamishwa na sasa maeneo hayo ni ya wageni!.

Kwa taarifa za siri, mafuta tayari yapo na yanachimbwa off-shore na kupakiwa juu kwa juu!. Msingoje wageni waje ndio vuguvugu lianze, anzisheni ili wageni wakija wakute wenyeji mlitangulia!.
 
Kwa mara ya kwanza nilukutana na Hawa Ghasia ilikuwa Addis Ababa tukisubiri ndege kwenda washington....ni mtu mzuri sana tuliongea mengi sana na kunipa ushauri wa kimaisha...sikuamini kama nilikuwa naongea na kiongozi wa juu kiasi kile.....

Tumefika marekani huwezi kuamini alikuwa anapigia simu kila wakati akiniuliza kama nimeboreka...namuambia hapana mama....akaniambia niende nikae nao excetive lonji....aisee huyu mama ni mtu wa watu sana...Mungu ambariki....
 
Back
Top Bottom