Barua ya Wazi kwa Gen. Mwamunyange: Mkikaa kisiasa, mtalaumiwa kama wanasiasa!

Good, kazi nzuri sana; nilitaka kuchangia ila umeandika yote hasa kile kipengere cha kustaafu na kuamia CCM, na lile swali la iwapo yupo tayari kusikiliza haya maoni au ana ndoa ya kufa na kupona na CCM!

Kiufupi Kaka huyu Bwana siyo msafi kwahiyo naweza kusema kuwa jibu la hili swali
Isije kuwa haya yote niliyokuandikia hayana maana kwani tayari umeshaamua kufa na CCM na kuwa una nafasi inakusubiria huko mbele ya safari na hivyo huwezi kuwa mkali sana kwani unaweza ukakosa nafasi huko mbeleni
ni ndio, hayana maana kwake.

Majibu mazuri ya hoja zako yanaweza kupatikani kupitia katiba nzuri, ambayo itaweka wazi misingi na namna ya kumpata CDF; hawa wanaochaguliwa bila kujua vigezo gani vimetumika mara zote uwa ni lobbing na makubaliano yatokea awali kuwa "mskaji tuombe mungu nikishinda wewe ndio Mkuu wa majeshi" najua kuwa wanajeshi wengi sana walishangaa kusikia jina la huyu Bwana kuwa ndio CDF, wakati tayari alikwisha kuhujumu mali nyingi sana za JKT, alikuwa amehujumu kambi ya Kuruta ilikuwa imeamishwa kutoka Kunduchi kwenda Mafinga JKT na kuisababishia serikali hasara kubwa sana kwa kuamisha kambi mara mbili, kwasababu makambi yote ya JKT yenye miradi mikubwa alikwisha kuifanya mali zake Binafsi na hivyo shughuli za Jeshi na fedha za Jeshi huko zilikuwa zake. Nadhani nimjibe hawezi, hawezi kwasababu nadhani hakuwa na CV ya kuwa CDF wapo waliokuwa zaidi yake ila hawakuwa wanaurafiki na aliyeshinda urais. Hawezi kwasababu alijua atakuwa CDF hata kabla ya uteuzi wake, kwahiyo husimtwishe mzigo ambao hauwezi. Kama anaweza basi atani-prove wrong soon kwa kuonyesha kuwa anaweza.
 
Mkuu MMKJJ pamoja na analysis yako na comparison na majeshi mengine yenye ufadhili wa serikali ya Marekani, I beg to differ with you as a matter of principle.
Jeshi letu linaongozwa na serikali ya kiraia na siyo kama ilivyo majeshi kama ya Misri na kwingineko.Si jambo la kusha ngaza kuwa hata Mubarak hakuwa na ubavu kkuliagiza jeshi kuzima maandamanano ya ya wa misri.Hii ni pamoja na jeshi letu kutawaliwa na sheria tofauti za utumishi wa umma kijeshi.
Nashangazwa vilevile kumuaddress Gen Mwamunyange kwa suala la Dr Mwinyi!
Muwajibishaji wa Dr Mwinyi ni Rais wa Jamhuri ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu,barua yako MMKJJ ingeelekezwa huko ungeeleweka.
Nawapongeza sana Jeshi kwa kutoingia katika malumbano kwa yaliyotokea ili hatimaye mchele na mpunga vijitenganishe na wananchi wajue ukweli wa mambo yaliyojiri.
Pamoja na yote kwa tatizo liliotokea kwa nini tusisubiri huo uchunguzi ili hatimaye mambo yote yajulikane.
Sifa ya Jeshi letu bado ni imara pamoja na haya yaliyotokea, you may differ, but the track recordspeaks for itself.
Milipuko katika army munitions si jambo geni duniani.Suala hili geni Tanzania? ,ndiyo, na halipendezi? , ndiyo.
Refer kwa the Halifax Explosion,December 6 , 1917.Hapa mji mzima uliteketea kwa mabomu kulipuka , na leo 2011 jeshi la Marekani bado ndilo the mightiest.
Jambo la msingi ni kujifunza kutokana na mambo haya.

Ebu soma tena hiyo thread, naamini hujailewa vizuri maudhui yake ndio maana unasema hakupaswa ku-addressed kwa CDF!! Hadhira ya hii thread ni CDF siyo Rais.
 
Hakuna paragraph wala topic sentence, kitu kilichoandikwa na mtu kakaa kama hakwenda shule huwa siwezi kukisoma.

wewe unataka tu kuonyesha kwamba umesoma writing skills, lakini wengine tuna mambo ya msingi zaidi ya kujadili. Nadhani hata wewe hujazingatia hayo unayo mkosoa mwandishi.
 
Ebu soma tena hiyo thread, naamini hujailewa vizuri maudhui yake ndio maana unasema hakupaswa ku-addressed kwa CDF!! Hadhira ya hii thread ni CDF siyo Rais.
Nimeisoma , tena vizuri sana, na ndio maana nilisema muwajibishaji wa Dr Mwinyi SI CDF wala Jeshi bali Commander in Chief.Ni lazima uelewe uhusiano uliopo kati ya Jeshi na Wizara.
Si sahihi kuwa Wizara ina mamlaka kuliwajibisha jeshi, kama paragraph za MMkjj zinavyoeleza.Miaka ya nyuma, kada wa chama, M Nnnuye alijaribu kumuwajibisha askari wa kawaida and he was reprimanded publicly na Waziri Mkuu E Sokoine.
Mkuu there is a very fine line between jeshi na wizara.
 
MM,

Sikuvunji moyo ila sijui kama hicho ulichoandika wanakielewa. Walisema jeshini hakuna uwajibikaji kwa maana ya kujiuzulu, what an interesting and sad argument.
 
Good, kazi nzuri sana; nilitaka kuc"mskaji tuombe mungu nikishinda wewe ndio Mkuu wa majeshi" najua kuwa wanajeshi wengi sana walishangaa kusikia jina la huyu Bwana kuwa ndio CDF, wakati tayari alikwisha kuhujumu mali nyingi sana za JKT, alikuwa amehujumu kambi ya Kuruta ilikuwa imeamishwa kutoka Kunduchi kwenda Mafinga JKT na kuisababishia serikali hasara kubwa sana kwa kuamisha kambi mara mbili, kwasababu makambi yote ya JKT yenye miradi mikubwa alikwisha kuifanya mali zake Binafsi na hivyo shughuli za Jeshi na fedha za Jeshi huko zilikuwa zake. Nadhani nimjibe hawezi, hawezi kwasababu nadhani hakuwa na CV ya kuwa CDF wapo waliokuwa zaidi yake ila hawakuwa wanaurafiki na aliyeshinda urais. Hawezi kwasababu alijua atakuwa CDF hata kabla ya uteuzi wake, kwahiyo husimtwishe mzigo ambao hauwezi. Kama anaweza basi atani-prove wrong soon kwa kuonyesha kuwa anaweza.

Mkuu si vizuri ku hallucinate in public, somebody said some people appear bright until you hear them talk.
Jeshi si shirika la umma kama hujui hujui tu.
 
Mwana kweli u shujaa wa kuthubutu. Vijana, wazee, watoto ama wanaume kwa wanawake ni wakati wa kukataa kuumia bila sababu za msingi.
Tuseme kwa nguvu Tumepuuzwa Kiasi cha Kutosha, Tumeaibishwa kiasi cha kutosha , tumepotoshwa kiasi cha kutoshwa, tumefukarishwa kiasi cha kutosha. Kilichobaki ni kupambana kwa kalamu na kwa vitendo, na zaidi tupeane moyo. Asante sana Mwana kwa kupasua ukweli.
 
Imetulia na wahusika wakiifanyia kazi tutarudisha imani kwa Jeshi letu na wizara kwa ujumla
 
HTML:
[[SIZE=3]Gongo la Mboto mwenye kutakiwa kuwajibika ni Waziri[/SIZE]
[SIZE=3]Nimesema hapo juu nakubaliana na uongozi wa jeshi kuwa hakuna afisa wa jeshi anayepaswa kujiuzulu na Brig. Gen. Meela alisema kweli kabisa kuwa jeshi haliongozwi kisiasa na kuwa linaongozwa na sheria ya Ulinzi ya mwaka 1966 (na mabadiliko yake ya baadaye). Matukio yote mawili (lile la Mbagala na la Gongo la Mboto) yote yanatokana kwa kiasi kikubwa na kukosekana kwa uongozi wa kisiasa wa kuweza kuangalia mahitaji ya jeshi na kuyashughulikia mapema iwezekanavyo. [/SIZE]
Lakini sheria hiyo hiyo (Section 15) inasema CDF anakuwa appointed na Rais... So CDF ni political appointee and he is serving at the pleasure of the President. My Take is that JK has got the power to fire he CDF if he does not live to the expectation of the appointing authority. CDF anaweza kujiuzulu inagwa atabakia na cheo chake cha ujenerali. Aliyewahi kuonyesha hii jeuri ya kufukuza maCDF ni M7 wa Uganda.
 
hureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee, kujiuzulu tuu ndo suluhisho!! mengine yatafata
 
Nimeisoma , tena vizuri sana, na ndio maana nilisema muwajibishaji wa Dr Mwinyi SI CDF wala Jeshi bali Commander in Chief.Ni lazima uelewe uhusiano uliopo kati ya Jeshi na Wizara.
Si sahihi kuwa Wizara ina mamlaka kuliwajibisha jeshi, kama paragraph za MMkjj zinavyoeleza.Miaka ya nyuma, kada wa chama, M Nnnuye alijaribu kumuwajibisha askari wa kawaida and he was reprimanded publicly na Waziri Mkuu E Sokoine.
Mkuu there is a very fine line between jeshi na wizara.

Mi sioni kama wewe unavyoona; kuna mmoja kati yangu mimi na wewe yupo nje ya Ukumbi wa maonyesho kwahiyo haoni vizuri Jukwaani na hivyo hajui Jukwani meza kuu amekaa nani, na pia haoni waliombele ya hadhira ya Mfasihi.

Mi naona mzungumzaji siyo MMKJJ, naona ni Watanzania, naona mambo makuu hapa siyo Dkt Mwinyi kujiuzulu, naona mambo makuu ni :-

  1. Jeshi kujiweka kwa Maslahi ya Umma kuliko ya wanasiasa hili wasionekana kama wao ni wanasiasa
  2. Jeshi kujitambua Kuwa wamepoteza heshima yako mbele ya Jamii na hivyo kufanya Jitihada za Makusudi kurejesha heshima yao kwa Umma, mtoa fasihi ametumia mifano mingi katika eneo hili na hasa la Jeshi la Misri na Jeshi letu wakati wa Mwl.
  3. Jeshi kujua kuwa wao ni Jeshi la Wananchni na siyo Jeshi la Watu wachache hasa kikundi fulani cha siasa; hapa jukwaaa limetumia mifano pia nakutoa mfano wa Jeshi kutumika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010 kinyume na matarajio ya wengi.
  4. Jeshi kuto kuwa na Maslahi na chama chochote cha Siasa, na kutambua muhimu wa mahusiano mema na vyama vyote vilivyo sajiliwa, mtoa maada kashauri kuwepo kwa mikutano pia kati ya Jeshi na Vyama vya upinzani kama ukurasa mpya wa Jeshi.
  5. Wanajeshi wenyewe kujenga heshima ya Jeshi kwa kutokuwa wakereketwa wa chama chochote, mtoa maada ametumia mifano ya askali wanaostaafu na hapo hapo kutangaza rasmi kuwa wao ni makada wa Chama Tawala na kuonyesha wazi kuwa hata walipokuwa wanatumikia Jeshi tayari walikuwa Makada wa Chama hicho.

Hata hivyo kazi yoyote iliyosimama kwa uweledi wa kijamii kama fasihi ubeba ujumbe mpana, ingawa lazima kuwepo na ujumbe mkuu katika kazi husika, unaruhusiwa kujadili kadri ya uelewa wako maana tuna-uwezotofauti katika kuchambua na kuelewa mada, kama ilivyo darasa wanafunzi wote hawapati "First Class" lakini wote upewa degree. Nakushauri husilazimishe kubadi mada kuwa kama unavyotaka wewe, wewe toa maoni yako siyo utake na maoni ya wengine yawe yako pia, unaweza kuandika barua ya kwako kuelekea wa Rais hii haikwenda huko! jaribu kuchangia na kuchambua ulichokielewa maana ndicho kinacho kuwakilisha wewe na uwezo wako.

Kucheza Muziki si lazima umuone mwiimbaji unaweza kusikiza sauti nje ya ukumbi na ukaendelea kucheza. Pole sana; siyo kosa lako.
 
Mkuu si vizuri ku hallucinate in public, somebody said some people appear bright until you hear them talk.
Jeshi si shirika la umma kama hujui hujui tu.

kama ilivyo darasa wanafunzi wote hawapati "First Class" lakini wote upewa degree. Nakushauri husilazimishe kubadi mada kuwa kama unavyotaka wewe, wewe to maoni yako siyo utake na maoni ya wengine yawe yako pia, unaweza kuandika barua ya kwako kuelekea wa Rais hii haikwenda huko! jaribu kuchangia na kuchambua ulichokielewa maana ndicho kinacho kuwakilisha wewe na uwezo wako.

Kucheza Muziki si lazima umuone mwiimbaji unaweza kusikiza sauti nje ya ukumbi na ukaendelea kucheza. Pole sana; siyo kosa lako sitaki kuongea chote chote kama kuna kitu unajua au hujui maana sioni haja Watanzania tupo wengi, hata Waziri wa Habari wa Mhe Saadam Hussein kila siku alikuwa anajipa moyo kuwa watampiga Mmarekani na kumsambaratisha hakujua jinsi ya kumshauri Mkuu wake hadi alipo kamatwa ndani ya andaki, toka ndoni amka na Pole sana.
 
kama ilivyo darasa wanafunzi wote hawapati "First Class" lakini wote upewa degree. Nakushauri husilazimishe kubadi maada kuwa kama unavyotaka wewe,

.

Maada ni kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi.
 
Back
Top Bottom