Kazi ipo. Hebu tuone usanii unaotaka kufanyika hapa. Hata hivro wengine tulishapoteza imani na Hosea na Takukuru yake muda mrefu.Tanzania Kumekucha!
Kwani Hosea aliwekwa hapo TAKOKUU bure? si ni kwa masrahi! Atashangaza kwa mengi tu, tukae tusubiri!Huu ni mziki mzito wa Chenge akiwemo mzee Mwinyi aka Ruksa. SFO lini walim-clear Chenge, ni TAKUKURU tu ambao waliwa-clear na Richmond.
Superman......
Ole wao wabunge wakimchagua 2015 si mbali, mtakutana na hukumu ya moto!
.......
Duh! Hii ndiyo kali kweli: Poleni Watanzania.
Source: Legal and Human Rights Centre Tanzania Human Rights Report 2008: Progress through Human Rights
It is Mr. Chenge's assertion that the original sources of these funds were "professional earnings" and "family savings/ inheritance." .
Sita ukiwa spika hebu anza na hili suala tukate mzizi wa fitina, kuna siku Chenge atafungwa tu. Anataka eti kuwa spika hili afunike hili? au anatusahaulisha mambo ya uchaguzi?
Ushauri: tutumie sheria za china kumuhukumu huyu mh!
Wana JF,
Kuna kitu kimoja ambacho nafikiri CCM hawataruhusu kifanyike. Ni kumpa uspika Chenge. Nafikiri kama CCM wana akili timamu na hasa mwenyekiti wa chama hiki kiovu, hawatampa Chenge nafasi ya kuwa Spika kwa kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanajifunga goli la "nne" kwa kuongeza matatu aliyoyazungumzia Jenerali Ulimwengu. Watakuwa wamejizika na kutoa grounds za kuonyesha kwamba CCM kweli ni Chama cha mafisadi. Tunajua kwamba kuna viongozi wengi ambao tayari wamehusika na kashfa nyingi za rushwa lakini bahati mbaya wengi wao bado hawajajulikana hadharani. Kumpa Uspika Chenge ambaye ananuka rushwa tupu na ambaye bila aibu aliliibia pesa taifa letu kwa njia ya rushwa na kuwabebesha mzigo waTanzania kulipa deni mpaka leo aachwe kuwa kiongozi wa bunge linalojadili na kupitisha bajeti na miswada muhimu inayowagusa waTanzania wote. Hili litakuwa ni tusi kubwa kutoka kwa CCM kwa Watanzania wote wapenda haki na maendeleo including makada wa CCM ambao ni walala hoi kama mimi.
Silali nikaota Chenge kupewa Uspika!!!
Tiba