Barua ya Sakina ya kujiuzulu hii hapa

Status
Not open for further replies.
Hii ni stori ya upande mmoja of course – hatujapata bado upande wa pili. Ukweli wa huyu mama utakuja kujulikana tu.

Lakini habari zinazotoka newsroom ya IPP-Media zinaonyesha kuwa mzee Mengi alimshtukia mama huyu Mdosi kwamba ni “pandikizi” wa wale mapapa aliyowataja – akina RA. Wanavyosema wenyewe kule IPP ni kwamba alivuta mzigo kabambe kutoka kwao ili awe anawatolea siri za IPP Media nk.

Kwa hivyo Sakina sasa akiajiriwa Habari Corporation haitashangaza – tusubiri tu.

Kuna uongo wa dhahiri katika barua yake hiyo ya kujiuzuru – na hasa katika suala la kumkumbatia balozi wa Palestina kuwa ndiyo sababu ambayo ilimwondoa pale, kwani Mengi ana mahusiano mazuri na Israel.

Hii kaiweka kwa sababu eti tu Mengi ana uhusiano na kampuni ya Coca Cola ambayo inamilikiwa na Wayahudi. Sidhani kama sababu hii ni strong – hasa ukiona bidhaa hizo za coca Cola zinavyouzwa katika nchi za Kiarabu, pamoja na sehemu za Wapalestina.

Lakini kikubwa ni kwamba Sakina katunga uongo, kwa sababu miaka kama miwili au mitatu nyuma, ITV ilitoa coverage ya tukio ambapo balozi wa zamani wa Palestina, akiandama na timu ya maripota wa ITV na Guardian walikwenda Mkuranga ku-cover tukio la kumtuza mtoto mmoja aliyezaliwa na ulemavu pale na ambaye wazazi wake walimpa jina la Arafat.

Balozi huyo alimvalisha medali yenye picha ya Arafat na pia kutoa misaada mingine ya pesa nk kwa mtoto huyo na wazazi wake. Hii coverage ilisimamiwa na Kyondo Mshana wa Guardian na ripota wengine wa ITV.

Mimi nadhani ITV itatoa hiyo footage kuonyesha jinsi balozi wa Palestina alivyokarimiwa na ITV ili ku-mprove Sakina wrong. Jee wakati huo Mengi hakuwa na uhusiano na Coca Cola?

Aidha kuna mwana JF mmoja hapo juu kasema eti Sakina amethibitisha habari kwamba Mengi anaamrisha habari zipi zitoke na zipi zisitoke kwenye magazeti. Pengine sipingi hilo, lakini ukijua jinsi RA anavyoamrisha wahariri wa magazeti yake kutoa habari anazotaka yeye, utaona ya Mengi ni “cha mtoto.”

Mnakijua kilichonfanya Atilio Tagalile aliyekuwa Mhariri Mkuu wake kujiuzulu? Mnakijua kilichomuondoa Rosemary Mwakitwange kama CEO wa New Habari Corporation? Ni hayo hayo – kulazimisha kuwekwa kwa stori zisizokuwa na maadili kabisa - za kutetea ufisadi na mafisadi – hakuna kingine. Mkiweza muulizeni Mama Mwakitwange.

RA amejaza ma-yesmen katika newsroom yake. Nani asiyejua u-spin doctor wa Muhimgo Rweyemamu, Manyerere Jackton na wengine?

Muongo mkubwa wewe,Rostam hana muda na vyombo vya habari vyake,lini uliona gazeti la Habari lina picha za Rostam? lakini Mengi kila siku ITV ina dakika 40 za habari zake na kila gazeti ni habari zake tu.

Sakina kafanya jambo zuri kuandika upuuzi wa MENGI wote humu ndani.
 
Hata mimi nakumbuka hiyo coverage ya ITV na balozi wa Palestina - nadhani yule aliyeondoka, siyo huyu, kwani muda umepita kidogo.

Lakini issue ni vipi anaandika barua ya kujiuzulu ndefu hivyo na kutoa malalamiko ya upande mmoja na kuileak (au alitaka iwe leaked) humu JF? Anataka sympathy ya nani? Kama aliyakoroga kule Guardian, basi ni ayanywe tu polepole, kama wanavyofanya wengi, akiwemo huyo mama Mwakitwange aliyetajwa hapo juu -- kimya kimya tu aliondoka New habari, bila kupayuka hovyo!

Hayo ya kumkandia Mengi bila shaka amefundishwa na hao waliomtuma kwenda huko Guardian -- wale mafisadi mapapa. Nadhani itakuwa ni hivyo tu.

Kaandika barua ndefu ili Mengi AJIFUNZE,pia SAKINA hakujipeleka Guardian bali MENGI ndiye aliyekwenda kwake na kumpa MILIONI 25 kama kishawishi aondoke Mwananchi na akamuahidi mshahara mara nne ya Mwananchi.

wako wengi walioshindwa kufanya kazi na MENGI kama Julius NYAISANGA,MIKIDADI MAHMOUD ETC jee nao walitumwa na kina Rostam?

mwacheni aandikie anavyotaka kwanza itamsaidia MENGI kuwaonesha mayahudi kuwa siri yake imetoka hivyo wamuongezee pesa na miradi.
 
duh!thank you GREAT THINKERS.....
ningesoma habari hii kwenye magazeti ningepata picha mbaya ya kipotoshaji.....nilimuamini sana Sakina LAKINI kwa resignation kama hii ni unprofessional kabisa hasa kipengele cha kumponda mwajili direct halafu unamkabidhi notice ya 1month,hii ni sawa na kusema MAREHEMU alikuwa mtu mbaya sana,mzinzi,mlevi,mgovi,pengo lake hatuhitaji kuliziba

sifa za wizi Mengi anazo kaiba NBC,ugomvi ndio kila mtu anagombana nae hata wewe mfanyakazi wake unajua hilo,Mzinzi linajuklikana sana,wizi hadi mishahara anayowapa wafanyakazi wake ni midogo na wengi hawana vyeti vya taaluma, wengine ni vibarua kwa miaka kadhaa.

kwani Mengi ni professional? Sakina kafanya kazi nzuri sana tumezidi kumjua Mengi kwa rangi yake original.ndio maana Rostam alipofanya press juu ya ufisadi wa Mengi,Mengi hakujibu akajificha na kuwatuma vibarua wake kujibu hoja za Rostam.

ghafla akaibukia kanisani HAI na kutoa milioni mia nne kwa waumini wamuunge mkono, yeye anajifanya ni mtu wa Watanzania wote kwanini awape wakristu tu na kuna wasio na dini,waislam,budhaa n.k? Mengi wachezee kina JOYCE MHAVILE tu sio Sakina mtoto wa mjini amekulia kisutu utamdanganya nini?
 
Ila Rostam sio mdini..si ndio? Na huyu Sakina na kumsingizia Mengi vs Wapalestina? Au ndio usomi wenyewe huo?

Rostam anahusika vipi hapa? hata hivyo Rostam sio mdini kwani amekuwa akiyapa pesa makanisa,Mtikila amekuwa akimsaidia zaidi ya miaka kumi na tano kwa pesa tena kwa siri.MENGI hajafanya hivyo.Sakina ni msomi sio siri huoni barua nzito hii alivyomtwanga MANGI?
 
JF kwa kuingiza udini kwenye kila kitu siku hizi mh. Hata mtu kutoa msaada kwa kanisa imekua shida? Sasa hivi mtu akitoa kitu kwa kanisa basi a match the same amount kwenye kila dhehebu la sivyo watadai ni mdini. Pesa za msaada ni mtu kujitolea. Hauwezi kumuamulia mtu atoe pesa zake wapi. Basi na nyie pia mchangia huko kwingine mnapo ona hajachangia.
 
JF kwa kuingiza udini kwenye kila kitu siku hizi mh. Hata mtu kutoa msaada kwa kanisa imekua shida? Sasa hivi mtu akitoa kitu kwa kanisa basi a match the same amount kwenye kila dhehebu la sivyo watadai ni mdini. Pesa za msaada ni mtu kujitolea. Hauwezi kumuamulia mtu atoe pesa zake wapi. Basi na nyie pia mchangia huko kwingine mnapo ona hajachangia.

Thanks MWanaFA,

NAdhani kuna haja, tena haja kubwa sana kuhakikisha masuala ya udini hayatuharibii mijadala!!!

 
Sakina kaeleza mazuri yake yote kadri alivyoona yanapaswa, thats great. Lakini bahati mbaya hatufahamu weakness zake....ambazo bila shaka zipo. Pili, hizo success zote alizotaja its okay but watu hufanya kazi kama team work, sio kweli mawazo yake tu ndio yalileta success zote hizo, bali michango ya wenzake pia. Kuhusu hiyo collision ya mwisho sababu ya kuhost balozi wa Palestina ameona ni gia tu ya kutokea kwa vile alishasema tangu mwanzo walipingana kuhusu magazeti ya udaku.... na kwa hali ilivyo sasa Mengi Vs Mafisadi sio rahisi kwa Mengi kumsikiliza Sakina juu ya hilo. So Mengi alipoona Sakina anasumbua kuhusu hizo issues then akaona amweke pembeni, lakini as usual tumezoea kupanda, so mtu akiona anashuka anaona bora ajiachie..

Mtizamo wangu, naweza kupingwa..

Kwetu ni kwetu, nakubaliana na wewe kwa % kubwa. We only have one sided story, her-story. Although, nimefurahishwa nae, she seems focused on her job, good for her, hataki kushuka, kurudi nyuma.
 
Thanks MWanaFA,

NAdhani kuna haja, tena haja kubwa sana kuhakikisha masuala ya udini hayatuharibii mijadala!!!


Unajua mkuu wanaoingiza udini ni watu wasio na hoja. Kwa maana wanajua wakisha ingiza udini mtu ataogopa kupinga hoja zake kwa nguvu kwa kuogopa kuonekana mdini. Ukiangalia jukwa la siasa sasa hivi limejaa thread za dini ambazo hazihusiani chochote na siasa. Kuna watu wanapenda kudivert attention from the real issues lakini watashindwa tu.
 
Rostam anahusika vipi hapa? hata hivyo Rostam sio mdini kwani amekuwa akiyapa pesa makanisa,Mtikila amekuwa akimsaidia zaidi ya miaka kumi na tano kwa pesa tena kwa siri.MENGI hajafanya hivyo.Sakina ni msomi sio siri huoni barua nzito hii alivyomtwanga MANGI?


Una takwimu zozote kuwa Mangi hajawahi kuwasaidia waislamu? Usomi wa barua ya Sakina ni upi? Kuandika kingereza?

Unauliza Rostam anahusika vipi? kasome post yako mwenyewe # 43. Halafu unasema Rostam alikuwa anamsaidia Mtikila kwa siri? Hujiulizi kwanini asaidie kwa siri? au udini unakupofusha hata unashindwa kuona? Hizo pesa anazogawa ulishajiuliza chanzo chake? Umeshajiuliza ni ngapi zimeshaliwa na wasilamu wenye njaa kumuharibia Mangi?
 
Nikifikiri sana, nadhani Zak yuko right -- huenda hiyo barua imekuwa leaked kimakusudi, pengine kwa agizo mahsusi la RM, ili tuone upumbavu wa huyo mama.

Unasemaje kuhusu hiyo cc ilitoelekezwa kwa Mr Mshana (ticked) au mzee ndio chuki binafsi na ushabiki??
 
Kanda2 said:
"Muongo mkubwa wewe,Rostam hana muda na vyombo vya habari vyake,lini uliona gazeti la Habari lina picha za Rostam? lakini Mengi kila siku ITV ina dakika 40 za habari zake na kila gazeti ni habari zake tu.

Sakina kafanya jambo zuri kuandika upuuzi wa MENGI wote humu ndani."

Kanda2;

Sina hakika kama ni kweli unayosema -- Rostam ameshaonekana katika magazeti yake.

Lakini kikubwa ni kwamba siyo magazeti yake, New habari Corp siyo yake -- makampuni yote yanayodaiwa ni yake siyo yake. Wizi na utapeli wa hela za wananchi ndiyo unaomsumbua hadi kujiweka katika hali hiyo ya kujifichaficha tu! Hataki aonekane ni yeye iwapo tuhuma zitamkabili.
 
tonge nyama said:
"Unasemaje kuhusu hiyo cc ilitoelekezwa kwa Mr Mshana (ticked) au mzee ndio chuki binafsi na ushabiki??"

tonge nyama:
Sikuelewi hapo mkuu. kama hiyo nakala ya barua ilikwenda kwa Mshana, basi kwani ipo ngumu gani kwa RM kumwagiza Mshana ai-leak hiyo katika JF ili watu waisome na waone ujinga wa huyo mama mdosi?
 
resignation letter= no need ya kuweka achievements zako...lol.hio sio CV unaomba kazi.Unajiuzulu basi mchezo umekwisha malalamiko mengi ya kazi gani?????
job true true!!!lol

Mauza uza, naungana na wewe Barua ya resignation haipaswi kuwa ndefu namna hii. Inawezekana ameandika CV yake kwenye hizo paragraph kadhaa. Kinachotakiwa kwenye resignation letter ni kuandika utamaliza muda wako lini na kwa nini unaacha kazi. Sio kuandika gazeti.
 
"Unasemaje kuhusu hiyo cc ilitoelekezwa kwa Mr Mshana (ticked) au mzee ndio chuki binafsi na ushabiki??"
______________________

tonge nyama:
Sikuelewi hapo mkuu. kama hiyo nakala ya barua ilikwenda kwa Mshana, basi kwani ipo ngumu gani kwa RM kumwagiza Mshana ai-leak hiyo katika JF ili watu waisome na waone ujinga wa huyo mama mdosi?

sorry jamaa nilimsoma vibaya, nilisoma RA badaya ya RM kama alivyoandika.

pamoja baba!!
 
duh!thank you GREAT THINKERS.....
ningesoma habari hii kwenye magazeti ningepata picha mbaya ya kipotoshaji.....nilimuamini sana Sakina LAKINI kwa resignation kama hii ni unprofessional kabisa hasa kipengele cha kumponda mwajili direct halafu unamkabidhi notice ya 1month,hii ni sawa na kusema MAREHEMU alikuwa mtu mbaya sana,mzinzi,mlevi,mgovi,pengo lake hatuhitaji kuliziba

Sakina si mnafiki, amejieleza vizuri kwa kuita kila kitu kwa jina lake na wala si vinginevyo.
 
whatever it takes, I am proving JF are great thinkers, it is always wise to have a look on 2 dimensions of these things!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom