Barua ya mwisho toka kwa mwanangu Chambondala (NIFANYEJE WADAU?)- PART I

mkulungwa

Member
Feb 20, 2011
12
1
Kwako Baba mpendwa shikamoo!!
Salamu zangu kwenu nyumbani, mimi ni mzima hofu ni kwenu mlio mbali na upeo wa macho yangu!!
Dhumuni la barua hii ni kukushukuru kwa yote ambayo umekuwa ukinifanyia katika maisha yangu, pia nataka kutoa sononeko langu kuhusu maendeleo yangu kimasomo; Baba naomba unisamehe sana kwani matokeo yangu tangu nije hapa shuleni sio mazuri. Taarifa ya muhula uliopita nimeshika nafasi ya kumi na tisa (19) kati ya wanafunzi ishirini (20). Nimepata wastani 80%, nisamehe baba nitajitahidi zaidi.
Baba, Kuna mambo ambayo yamesababisha nipate alama hizo naomba uangalia ni jinsi gani utanisaidia kuyatatua:-
i. Ukosefu wa masomo ya tuition (ziada) niwapo shule na pale niwapo likizo. Wenzangu wote hapa shuleni hulipiwa masomo ya ziada wakiwa likizo na mara warudipo shuleni huwa wameshamaliza kusoma ‘angle’ zote za mitihani. Huko huwa wanasolve papers zote na walimu wetu hutoa mitihani toka kwenye past papers.
ii. Ukosefu wa marking scheme. Baba taka usitake mfumo wetu wa mitihani siku hizi ni wakurudishia maswali ya miaka iliyopita (hakuna maswali mapya). Ukininunulia vitabu kama ufanyavyo wewe, unanipotezea muda kwani mpaka nisome nielewe concept ni muda mwingi sana!! Ukiwa na marking scheme unakariri waswali na solutions zote mpaka ushibe, baada ya hapo inabakia kucheua tu kwenye paper. Baba kama huniamini naomba waulize kina daria wanaosoma shule zinazoongoza Tanzania, hivi ndivo wanavyosoma na ndio maana wanarudia shule zile zile tu. Ukiwaleta huku hawawezi kitu.
iii. Ukosefu wa walimu wazuri wa English; unajua baba mitihani yetu tunafanya katika lugha ya English, shule yetu haina walimu wazuri wanaoongea kingereza safi, wengi wao wanagongea tu huku wakifumba macho. Wanaeleweka na kujitahidi sana baba, lakini inatufanya sisi tusiongee kwa mapozi. Please baba nipeleke shule za international nikaboreshe lugha nami personality yangu ikae juu. Kwani hutaki mwanao nionekane msomi niongeapo?
iv. Shule yetu kutokuwa katika kumi bora ; nadhani hili baba umeshuhudia kupitia matokeo ya form four. Inaniuma sana kwani inatufanya tukitembea mjini tusiheshimike. Ningesoma Maryan nahakika kwa nafasi yangu hii hii ningetesa bongo.
v. Ukosefu wa laptop baba. Hii sasa ni kitu muhimu sana, ule wakati wa kusoma vitabu vikubwa kama Nelcon, Lambart nk umepitwa na wakati. Siku hizi mambo yapo kwenye mtandao, ukibofya tu mambo kede kede unanyonya unatemea tu kwenye assignment. Wenzangu hawakeshi tena sasa. Pia twitters facebook usiseme.
Baba najua nimekuchosha kwa mahitaji yangu mengi, nakuomba uyaangalie kwa umakini wake unitatulie yale ambayo kwako yanaingia akilini kwani nakuaminia baba yangu kwa mbinu zako za kujitetea.
With love and care,
Mkamba Chambo(mtoto wa mwisho)
N.B baba elfu tano kwa siku haitoshi maisha magumu weka angalau book 10.
 
daaah umenifurahisha sana..umeiandika kwa usanifu wa hali ya juu walahi nai print nije kumpa mwanangu gaude asome jinsi kizazi hiki kilivopata shida
 
Asante kwa uandishi murua uliojaa mafunzo yenye hekima kuhusu hali halisi inayokabili watoto/wadogo zetu!
 
Hata mm nimeikubali kaka. Ubunifu umetulia na ndiyo hali halisi ya elimu yetu Tanzania
 
huyu mtoto hatari kwa mahitaji, na ww uliyetumiwa barua hiyo, mtimizi mwanao hasa hitajio la mwisho kwa haraka zaidi kabla hajaanzisha andamano juu yako. Iko poa sana.
 
Nashukuru wazee kwa comment zilizo tukuka, bado natafuta jibu la huyu kijana:mullet:
 
Mkuu safi sana kwa ujumbe wako mzito.

Umeweza kuutazama mfumo wetu wa elimu kwa mapana makubwa na kubaini mambo mengi ya ajabu ambayo yapo katika mfumo wa elimu hapa nchini kwetu.

Ni ukweli ulio wazi bila Marking scheme na ku-solve past papers sio rahisi kwa kijana kufaulu katika mfumo wetu wa sasa. Maana mfumo hauruhusu kujisomea na kuwa creative bali una-support those who are good in cramming past papers.

Athari la hili ni kuwa na wasomi ambao itakuwa vigumu kuweza ku-fit katika market ya ajira. Pia kuishia kuendeleza mawazo ya wengine na kushindwa kutumia elimu hiyo kuboresha na kuinua maisha ya Mtanzania katika mazingira yetu.

Pili, hebu tuangalie hizi shule ambazo zipo katika 20 bora, je zinafanya hivyo kwa kuwa na ufundishaji mzuri au ni kwa sababu ya kuondoa wanafunzi wote ambao wanaonekana hawawezi kukariri marking schemes? Maana utakuta shule inaanza na wanafunzi 70 na wanaomaliza ni 40 tu, tujiulize hao wengine wamepotelea wapi? Ni kweli ya kwamba uwezo wao mdogo au ni usanii tu?
 
Karbu jamvini, hiyo barua ni hali halisi ya elimu zetu hapa bongo. imetulia na ina mantiki saa bigup
 
Back
Top Bottom