Barua ya Mhe Diwani L Mbuya kwa Katibu Mkuu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Mpendwa Joseph,
> Salamu sana.
> Naharakisha kukuletea nakala ya barua ya Mhe Diwani
> L
> Mbuya kwa Katibu Mkuu. Nakala hii alipatiwa
> Mwenyekiti
> Peter Ndowo juzi.
> Barua hii naonyesha jinsi alivyo na chuki na dharau
> kwa Mwenyekiti wetu wa Kijiji. Imejaa uongo na
> matukano.
> Nimeshamtafsiria Mwenyekiti naye ataijibu wiki
> ijayo.
> Nimeona iwahi kwako mapema.
> Viambatisho diwani alivyovitaja hakumletea
> Mwenyekiti
> hivyo ana nia ya kuvipata kabla ya kuijibu barua
> hii.
> La ajabu ni kuwa Mhe Diwani hajui kuwa mimi sikuwa
> madarakani kipindi Peter akikaimu! Hii ni kwa sababu
> Diwani hujibu barua peke yake bila kuwasiliana na
> Afisa Mtendaji wa Kata! Pia sijawahi kuwa kwenye
> kamati ya maji wala ya mfereji! Huzua uongo
> apendavyo!
> Tafadhali endelea kutusaidia kwani ufumbuzi uko
> machoni kupatikana kwani wataalamu wa Mkurugenzi
> wameshaanza kazi. Walitutembelea Jumatano.
> Kwa leo sina mengi ila kukutakia afya na ufanisi
> katika shughuli zako.
> Wasalaam,
> Canute Temu,
> Mjumbe wa Halmashauri ya Kijiji cha Masaera
 
Mpendwa Joakim,
Salamu sana. Naamini uliliona jibu la Mheshimiwa
Mbunge Kimaro. Limenishangaza hasa ukizingatia
ameshakuwa madarakani kama Mbunge [kiongozi wa Taifa]
kwa miaka miwili sasa!
Bahati mbaya anapakwa matope na Diwani wa Kilema
Kusini na inaelekea hajatambua hilo! Laiti angejua
historia ya huyu diwani!! Ukweli utajulikana tu!
Hebu angalia majibu ya Mhe Diwani kwa Katibu Mkuu
Tamisemi. Inaelekea Mhe Diwani hatambui kuwa Serikali
ya Kijiji ni serikali halali kwa mujibu wa katiba ya
nchi. Anadiriki kutukana kwa maandishi na kuendeleza
uongo! Hafanyi kazi na Afisa Mtendaji wake hivyo hana
kumbukumbu rasmi! Sitachoka kusema ukweli. Aliwahi
kusema raia takriban 40 wa kijiji cha Masaera waliunda
njama za kumwua!! Akatangaza hata kwenye magazeti!!
Akapeleka ripoti polisi!! Ndani ya orodha hiyo
walikuwamo mwenyekiti wa kijiji, afisa mtendaji wa
kijiji, na hata wajumbe wa kamati ya siasa ya chama
tawala cha CCM!!!
Subira yavuta heri. Na Mungu mwona yote anaona pia!!
Wasalaam
Canute Temu.
 
Mheshimiwa Bwana Canute,

Salaam sana na pole kwa mahangaiko na misukumsuko ya huko Kilema nakubaliana na barua yako kwamba majibu ya Mh. Mbunge wetu kuhusu tuhuma dhidi ya Diwani hayakuwatosheleza na hasa ukizingatia kwamba yeye mwenyewe katika kikao cha KDDTF cha 30 alitamka wazi kuwa matatizo makubwa yaliyoko huko vijijini ni uongozi mbovu ambao umajaa ufisadi mtupu - fedha na mali za wananchi zinatafunwa wazi wazi na viongozi ambao wako madarakani. Kwa hakika nadhani ni muda mwafaka kwa wananchi kuelezwa wazi wazi juu ya maswala haya yote yanayohusu maendeleo yao hususani masuala yanoyohusu fedha na mali za vijiji hayana budi kuwekwa bayana hadharani bila ya kificho au mizengwe yoyote ile. Dhana kwamba kiongozi hawezi kukosolewa au ni makosa kumkosoa kiongozi na kwamba kufanya hivyo ni chokochoko au fitina za kugombea madaraka mawazo kama hayo hayana nafasi katika dunia ya utandawazi na maendeleo ya sasa. Kwa mantiki hiyo basi naona suala hili linageuzwa kuwa ni vita binafsi ambavyo sivyo [kulingana taarifa ambazo umeziambatanisha barua ya awali]

Kwamba fedha zilitolewa na UNDP kwa wananchi wa Masaera kwa maendeleo yao kupitia asasi au kikundi husika na kwamba je fedha hizo zimetumika kama ilivyotakikana? Kwamba wasaini katika fedha hizo ni mtoto wa Diwani na mfanyakazi wake ni jambo lisilokubalika kisheria kwa masuala yanayohusu usimamizi wa fedha za umma je uchaguzi ulifanyika na kuwachagua hao wasaini ?


Mheshimiwa Bwana Canute bila ya kuingilia kwa undani zaidi saula hili na kulingana na sheria na taratibu za nchi yetu na katiba ya nchi - uhuru wa kutoa maoni -kama ibara namba 18 inavyojieleza

18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru
kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,

kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo

chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa

mawasiliano yake kutoingiliwa kati.

(2) Kila raia anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu

matukio mbalimbali nchini na duniani kote ambayo ni muhimu

kwa maisha na shughuli za wananchi, na pia juu ya masuala

muhimu kwa jamii.



na zaidi pia kulingana na madaraka ya Umma kama ilivyooanishwa katika katiba ya nchi yetu - ibara 145



MADARAKA YA UMMA

Serikali za Mitaa

Sheria ya 1984

Na.15 ib.50

145

.-(1) Kutakuwa na vyombo vya Serikali za Mitaa katika
kila mkoa, wilaya, mji na kijiji, katika Jamhuri ya Muungano,

ambayo vitakuwa vya aina na majina yatakayowekwa na sheria

iliyotungwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi.

(2) Bunge au Baraza la Wawakilishi, kadri itakavyokuwa,

litatunga sheria itakayofafanua utaratibu wa kuanzisha vyombo

vya Serikali za Mitaa; miundo na wajumbe wake, njia za mapato

na utaratibu wa utekelezaji wa shughuli za vyombo hivyo.

Kazi za Serikali

za Mitaa Sheria

ya 1984 Na.15

ib.20

146

.-(1) Madhumuni ya kuwapo Serikali ya Mitaa ni
kupeleka madaraka kwa wananchi. Na vyombo vya Serikali za

Mitaa vitakuwa na haki na mamlaka ya kushiriki kuwashirikisha

wananchi katika mipango na shughuli za utekelezaji wa

maendeleo katika sehemu zao na nchini kote kwa jumla.

(2) Bila ya kuathiri maelezo ya jumla yaliyomo katika ibara

ndogo ya (1) ya ibara hii, hiki chombo cha Serikali za Mitaa, kwa

kuzingatia masharti ya sheria iliyokianzisha, kitahusika na

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

_________________________________________________________________

104

shughuli zifuatazo -

(a) Kutekeleza kazi za Serikali za Mitaa katika eneo

lake;

(b) Kuhakikisha utekelezaji wa sheria na ulinzi wa

wananchi; na

(c) Kuimarisha demokrasi katika eneo lake na kuitumia

demokrasi kuharakisha maendeleo ya wananchi.


Mheshimiwa ndugu Canute nadhani kulingana na taratibu hizi ikiwa kiongozi anaonekana kupingana na katiba na matendo na mwelekeo wake hauridhishi ni vema akajiuzulu wadhifa huo. Kwa kuwa ni wazi viongozi wengi katika nchi za Kiafrika hawana tabia ya uwajibikaji ni vema juhudi za kujenga mila ya uwajibikaji kwa viongozi ikaanza kushirikishwa katika mila na desturi zetu za Kitanzania.

Kwamba ukweli haufichiki na ikiwa hayo mliyoyaeleza ni kweli basi nadhani ni vema Mwenyekiti wa kijiji pamoja serikali ya kijiji, Afisa Mtendaji wa Kata ya Kilema Kusini pamoja na wananchi mkaitisha mkutano wa wazi na ikiwezekana mkashirikisha pia uongozi wa serikali katika ngazi ya wilaya ambapo mambo yote haya mtayajadili na ikiwa Mh. Diwani atakuwa na tuhuma za kujibu basi itafaa awajibike na kama atakataa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye na kuondolewa madarakani kama wananchi watamkataa. Nadhani Bwana Canute umefikia muda wa kuwaweka viongozi waliochaguliwa kuwajibika kwa wale waliowachagua kwa kuanzisha taratibu za " IMPEACHMENT" hiyo ndiyo njia inayofaa badala ya kusubiri miaka mitano ya uchaguzi. Kwa waraka huu Mh. Bwana Canute KDDTF inaamini kabisa kwamba matatizo mengi ya ufukara, uhalifu na ujambazi kwa kiasi fulani unachangiwa na uongozi dhaifu na wababaishaji katika tarafa hii ni wazi kwamba KDDTF inaamini kuwa usuluhishi wa matatizo haya yote utatatuliwa au kumalizwa na wanajamii ya Kilema wenyewe kwa kuchukua juhudi mahususi za kupambana nayo katika ngazi zote kwa uwazi, ukweli na kwa haki kwa wote.

Tumsifu Yesu Kristo!

Wako katika utumishi

Dr. Joakim Michael Kifai

Katibu Mkuu_KDDTF

Dar es Salaam 6/11/2007.
 
Back
Top Bottom