Barua ya Mh. Lowaa Hasaa kwa Msabaha Gazeti la Rai ni kumsafisha Lowaa Hasaa?

saggy

Senior Member
Nov 12, 2008
153
70
Ndugu wanajamii wenzangu.
Gazeti la Rai la Tarehe 29/10/2009 katika ukurasa wake wa mbele lilichapisha sehemu ya Barua iliyoandikwa na Mh. Eduu Lowaa Hasaa aliyekuwa waziri Mkuu wa Kwanza katika serikali ya wamu ya nne akimwandikia Mh. Ibraa Msaa- baa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini wa kwanza pia wakati wa awamu hii ya nne na wote wakazama katika Meli kubwa iliyopigwa mawimbi makali na upepo mkubwa wa RICHMOND.Kwa ufupi Barua hiyo ilieleza yafuatayo:-

1.Maagizo ya Waziri mkuu kwa Waziri wa Nishati kwamba AJIRIDHISHE na uwezo wa Kampuni hiyo kuingia mkataba na shirika la umeme nchini Tanesco

2.AOMBE USHARI Kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili kuepusha matatizo yanaweza kujitokeza katika mchakato mzima


3.Waziri wa Nishati ahakikishe anampatia taarifa KILA SIKU za mchato mzima wa kuingia makubaliano ya makataba na Kampuni ya Richmond


Barua hii imeasainiwa na Mh. Eduu Lowaaa Hasaaa na Nakala moja kwa RAISI na IKULU.

Maswali ninayojiuliza ni haya:

a.Je barua hii ina maana kwamba mh hakuhusika katika sakata la Richmond na hivyo kujiuzuru kwake ni Uzalendo tu kwa Taifa lake la Tanzania?

b.Je Kamati Teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza Mkataba huu iliwahi kupewa au kupata maelezo ya Barua hii na hivyo kuyafanyia kazi kabla utoaji wa taarifa ya Kamati?

c.Je barua hii ni ushahidi tosha kwa umma wa Tanzania kwamba Mh. E Lowaa Hasaaa ALIONEWA na Kamati Teule ya Bunge na ya Kwamba Alichukua hatua stahiki kwa nafasi yake kama Mtendaji Mkuu wa shughuli za Serikali katika Kutoa MAELEKEZO na maonyo ili kusidia Taifa liondokane na Mgao wa umeme ambao uliathiri vibaya sekta za uchumi na wakati huo huo akichukua tahadhari kusaidia Taifa liisingie hasara kutokana na mkataba huo wa Richmond?

d.Kwakuwa nakala ya Barua hii Raisi anayo,je kwanini alikubali waziri wake mkuu mteule ajiuzuru akingali anajua anaonewa na ushahidi anao?

e.Ni kwa vipi GAZETI LA RAI wameweza kupata Barua hii ya Siri na ambayo nakala yake ipo pia Ikulu na Raisi anayo,je hili si hatari kwa usalama wa Taifa?

f.Barua hii inamaanisha Mwanasheria mkuu wa zamani na Waziri "Musa shabaa" ndio wanadeba dhamana ya uzembe uliopelekea Taifa kupata Hasara kubwa kiasi hiki?

MAONI YANGU: Umeme wa uhakika ndio kiu ya wanachi,Wanasiasa acheni siasa tupeni Umeme wa Uhakika.
 
kwa kuiangalia makala hiyo iliyochapwa na RAI inaonesha wazi walikuwa na nia ya kumsafisha lowassa,kwa sababu nina uhakika kuwa rai walipata pia barua ambazo zilikuwa zinatoka kwa lowassa kwenda kwa msabaha kabla ya hiyo ambayo ilimtaka msabaha ajiridhishe na uwezo wa dowans.Barua hiyo iliandikwa iliandikwa miezi mitatu baada ya mkataba kuwa umesainiwa,kwahiyo kwa makusudi kabisa RAI wameamua kuitoa hiyo tu bila kutilia maanani zile nyingine alizokuwa anamuandikia msabaha,na zile zilizokuwa zinatoka kwa msabaha kwenda kwa viongozi wa wizara[katibu mkuu]na mwenyekiti wa bodi ya wakurugezi.
 
kwa kuiangalia makala hiyo iliyochapwa na RAI inaonesha wazi walikuwa na nia ya kumsafisha lowassa,kwa sababu nina uhakika kuwa rai walipata pia barua ambazo zilikuwa zinatoka kwa lowassa kwenda kwa msabaha kabla ya hiyo ambayo ilimtaka msabaha ajiridhishe na uwezo wa dowans.Barua hiyo iliandikwa iliandikwa miezi mitatu baada ya mkataba kuwa umesainiwa,kwahiyo kwa makusudi kabisa RAI wameamua kuitoa hiyo tu bila kutilia maanani zile nyingine alizokuwa anamuandikia msabaha,na zile zilizokuwa zinatoka kwa msabaha kwenda kwa viongozi wa wizara[katibu mkuu]na mwenyekiti wa bodi ya wakurugezi.
Nipashe ndiyo wa kwanza kuandika, kama sikosei ni Jumatatu ya wiki hii. Kwanza kwenye ukurasa wa mbele.
 
Haijalishi kwamba EL alikosea au ni waziri wake Mhe. Msabaha. Swala la umeme lilikuwa ni nyeti sana kwa uchumi na ustawi wa jamii wakati huo. Jambo nyeti kama hilo hata kama kiutendaji liko chini ya wizara fulani ni wajibu wa Ofisi ya waziri mkuu kuhakikisha mambo yanafanyika vizuri.

Kwa mfano kukitokea njaa kali sana hapa nchini hata kama kiutendaji ni wizara ya Kilimo na Chakua inahusika na swala hilo, Ofisi ya waziri mkuu ndio kinara wa jukumu hili. Waziri akivurunda katika hili waziri mkuu inabidi awajibike ipasavyo. Hii ndio iliyotokea kwa Richmond.

Kwa waziri mkuu kutoa maagizo wakati mkataba umesha sainiwa ni sawa na kukumbuka shuka wakati kumeshakucha! Hii ping pong ya nani alifanya nini kati ya mawaziri na waziri mkuu haitusaidii hata kidogo. Kama ilibidi EL abebeshwe "msalaba" kama Simon Mkeremi alivyobebeshwa msalaba wa Yesu na basi iwe hivyo kwa bosi wake (JK) la sivyo ingebidi Rais atuambie alikuwa wapi wakati "taa zinazimika". Kama ni ajali ya kisiasa kama alivyosema Rais, basi makovu yake ni makubwa mno hayawezi kufutwa na vimemo vya Rai na wengine.
 
Tuwe makini na machapisho ya mafisadi. Rai ni gazeti la fisadi wa Igunga na ni mshirika mkubwa wa Lowasaaaaaa kwa hiyo hatutehemei mapya zaidi ya kumsafisha. RAI ILIKUWA ZAMANI.
 
ukisema gazeti la rai ndio limeandika unategemea nini? Ndio maana nasikia magazeti yao hayauzi mpaka wanashindwa kuwalipa wafanyakazi mishahara
 
Nipashe ndiyo wa kwanza kuandika, kama sikosei ni Jumatatu ya wiki hii. Kwanza kwenye ukurasa wa mbele.

Kilichoandikwa na Nipashe hiki hapa soma.

Hivi ndivyo Lowassa alishiriki Richmond

Na Mwandishi wetu
*Nyaraka zaonyesha kila hatua aliweka mikono yake
*Uthibitisho wa kuibeba Richmond watolewa peupe
*Kumbe ndiye aliipora Tanesco kazi ya kusaka mzabuni
*Wizara ya Nishari na Madini ilisubiri maamuzi yake.

Kilio cha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (pichani), bungeni kwamba alidhalilishwa sana kwa kuhusishwa na mkataba tata wa kampuni ya Richmond, si lolote wala chochote baada ya uchunguzi wa kina wa nyaraka uliofanywa na gazeti hili kubaini kwamba alihusika vilivyo katika mchakato mzima wa zabuni hiyo.

Nyaraka kadhaa ambazo Nipashe imeziona, zimethibitisha si tu ushiriki wa Lowassa katika mchakato huo, bali alikuwa anatoa maelekezo ya nini kifanyike kwa kila hatua.

Nyaraka hizo zinaonyesha kwamba Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Dk. Ibrahim Msabaha, alibakia kuwa kama karani tu wa kutekeleza maagizo ya Lowassa, kila hatua alikuwa anaamua Lowassa na kuifanya Wizara ya Nishati na Madini kutekeleza kile alichotaka kiongozi huyo aliyejiuzulu Februari mwaka jana huku akilalamika kwamba ameonewa kwa kuzushiwa mambo kuhusu kashfa ya Richmond.

Akitii maagizo kutoka kwa Waziri Mkuu Lowassa, Dk. Msabaha, naye alimwandikia barua Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Athur Mwakapugi, Juni 21, 2006 akimwagiza atekeleze maagizo wa Waziri Mkuu ya kusaini mkataba na Richmond.

Kwa kifupi barua hiyo inasomeka hivi…“Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni ya Richmond kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea nakala ya kibali kilichotolewa kutoka ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara.”

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, Katibu Mkuu huyo, wakati huo, Arthur Mwakapugi, baada ya kupata maelekezo toka kwa waziri wake, naye alitoa maagizo siku hiyo hiyo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Balozi Fulgence Kazaura, akimwagiza kuhakikisha shirika hilo linaingia mkataba na Richmond.

Maelezo hayo ambayo aliyaandika kwa mkono yalisomeka kwa kifupi... “Andaa barua kwa Mwenyekiti wa Tanesco kumuagiza waingie mkataba na Richmond.”

Taarifa zinaonyesha kuwa baada kampuni ya Richmond Development Company LLC kuingia mkataba na Tanesco Juni 23, 2006 na baada ya siku kusonga mbele bila kuwepo kwa dalili yoyote ya kupatikana kwa umeme wake katika kipindi cha siku 60 kama walivyosema wenyewe, maneno yalianza kuzagaa miongoni mwa wananchi, vyombo vya habari na hata baadhi ya wabunge, hivyo Lowassa akahisi kuwa kazi aliyokuwa ameisimamia kwa nguvu zote amechemsha na hivyo kutoa maelekezo mapya.

Katika maelekezo hayo, Lowassa kwa barua yake kwenda kwa Waziri Msahaba alisema: “Kama unavyofahamu yapo maneno mengi sana yanasemwa kuhusu uwezo wa kampuni tajwa (yaani Richmond) kuagiza Gas Turbines kama alivyopewa mkataba na Tanesco baada ya kushinda zabuni. Yameandikiwa pia kwenye Gazeti la Thisday la jana (20.09.06).

“Inawezekana hivi vikawa ni vita vya kibiashara. Lakini kwa sababu ya meneno hayo yanasemwa na watu wengi na tofauti ni vizuri UKAJIRIDHISHA kwamba kampuni hii itaweza kutekeleza kazi hiyo. Kama utaona shaka lolote ni vizuri kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu mapema ili tuweze kuchukua hatua zinazopasa mara moja.”

Aidha, Lowassa akijua kwamba kuna jambo linazidi kuumuka juu ya Richmond, katika barua hiyo ya Septemba 21, 2006 alijipa moyo akisema: “Kwa upande mwingine kwa kuwa malipo yake ni kwa L/C hawezi kupata nafasi ya ‘kuturusha’. Ila unachoweza kufanya ni kuweka utaratibu wa kumfuatilia kwa karibu ili kuhakikisha kwamba analeta ‘turbines’ hizo zenye kiwango na kwa wakati. Napenda kupata taarifa za ufuatiliaji wa suala hili kila siku; bila kukosa.”

Ushiriki wa Lowassa haukuishia kwenye barua hiyo aliyoandika na kuisaini mwenyewe Septemba 21, 2006 tu; bali ushiriki wake mwingine unaonekana katika waraka wa Waziri Msabaha, aliyegeuzwa karani katika mchakato mzima huo, kwenda kwa Mwenyekiti wa bodi ya Tanesco, Balozi Flugence Kazaura.

Dk. Msabaha anamtaarifu Balozi Kazaura kuwa suala la kushughulikia mashine za umeme wa kukodi limekwisha kushughulikiwa na Waziri Mkuu Lowassa.

Katika barua hiyo ambayo pia Nipashe ilifanikiwa kuiona ya Aprili 12, 2006 inasema ifuatavyo:

“Nadhani hatukuelewana vizuri. Suala la kushughulikia gas turbines za kukodisha lilishashughulikiwa na Mhe. Waziri Mkuu, ambaye aliunda Kamati ya wataalam watatu – KM- Hazina, KM Nishati na AG. Nia ni kuliondoa suala zima kwenye mikono ya Menejimenti ya Tanesco ambayo imeshindwa kulishughulikia kwa ufanisi.”

Kwa barua hiyo, si tu kwamba Dk. Msahaba aliweka wazi msimamo wa Lowassa katika suala zima la ukodishaji wa mitambo hiyo, bali pia alionyesha jinsi ilikuwa imekubalika kuwaweka pembeni Tanesco ambao walikuwa ni wataalam wa mitambo hiyo kuliko mtu mwingine yeyote kwenye masuala ya uzalishaji umeme.

“Waache Kamati iliyoteuliwa kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na BODI yako na wataalam wa Tanesco kwa kadri watakavyoona inafaa. Pasiwe tena na picha kama vile Menejimenti ya Tanesco imerejeshewa kazi hiyo, maana huko kutakuwa ni kukiuka maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu,” kwa kauli hiyo ni dhahiri Lowassa alikuwa ndiye anayejua mwelekeo wa kile alichokuwa anakitaka.

Mikono ya Lowassa katika sakata la Richmond haipo tu kwenye kumwagiza Dk. Msabaha na Kamati ya Makatibu pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, lakini pia inaonekana jinsi alivyobariki mapendekezo ya Timu ya Majadilino ya Serikali (GNT) iliyojadiliana na Richmond.

Kwa mujibu wa barua nyingine ya Waziri Msabaha ambayo pia Nipashe imefanikiwa kuiona ya Juni 17, 2006 siku sita tu kabla ya mkataba wa Richmond kusainiwa, inaonyesha alivyoelezwa hatua kwa hatua za majadiliano baina ya GNT na Richamond na jinsi utekelezaji wa mkataba utakavyokuwa.

Katika barua hiyo, Lowassa alielezwa gharama za kuleta mitambo hiyo na mpangilio mzima wa kuileta kwa awamu tatu, kwa kuonyesha alivyokuwa amelipa suala hilo kipaumbele, Juni 21, 2006 Lowassa kupitia kwa Katibu wake, aliyetambulika kama B. Olekuyan, alimtaarifu Katibu wa Waziri wa Nishati na Madini majibu ya bosi wake.

Majibu yalisema ifuatavyo: “Mheshimwa Waziri Mkuu amekubali mapandekezo na ushauri wa Mheshimiwa Waziri. Tafadhali mjulishe.”

Kwa kasi ya ajabu, siku hiyo hiyo, Dk. Msabaha akiwa anafanyia kazi majibu ya Lowassa, alimwagiza Katibu Mkuu wake, Arthur Mwakapugi, hatua za kuchukua juu mkataba wa Richmond.

“Serikali imekubali mapandekezo ya Wizara kuwa Tanesco iagizwe kuingia mkataba wa kuleta Gas Turbines za kukodisha za jumla ya MW 105.6 na kampuni ya Richmond kwa mtiririko uliopendekezwa katika makubaliano kati ya Kampuni ya Richmond ya Marekani na GNT,” ilisema barua hiyo na kuongeza kuwa:

“Iagize Tanesco iingie mkataba na kampuni hiyo kwa ajili ya umeme wa kukodisha haraka iwezekanavyo. Nakuletea kibali kilichotolewa kutoka kwa Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu kwa kumbukumbu za Wizara.”

Mwakapugi naye kwa kasi kama ya Waziri Msabaha, siku hiyo hiyo, aliagiza Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco aagize Tanesco waingie mkataba na Richmond. Mkataba ambao kwa mujibu wa kumbukumbu za Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza mchakato wa mkataba wa Richmond, ulisainiwa usiku kwa haraka hizo hizo siku mbili baadaye.

Mikono ya Lowassa pia ilionekana kwenye mkataba wa Richmond kama waraka wa ndani wa Waziri Msabaha kwenda kwa Katibu Mkuu wa Wizara akieleza kuwa Waziri Mkuu ameamrisha Richmond wapewe dili nyingine ya kuzalisha megawati 40 za umeme.

Waraka huo wa Julai 13, 2006 baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Richmond na Tanesco, unasema:

“Nimezungumza tena na Mheshimiwa Waziri Mkuu leo juu ya bei ya mitambo ya Aggreko. Msimamo ni uleule niliokueleza awali na ameagiza tuulize Richmond kama anaweza kutoa 40 MW kwa bei isiyozidi ile ile ya 4.99 cents per kwh na kama tunaweza kuipata basi achukuliwe Richmond.”

Kwa maelekezo ya Lowassa, Msabaha katika barua hiyo kwa Katibu Mkuu alisema: “Nimempigia simu Mohamed Gire wa kampuni ya Richmond juu ya upatikanaji wa hizo MW 40. Gire amekubali kuwa anaweza kutoa MW 40 za ziada ifikapo Septemba na kwa bei hiyo ya USD cents 4.99 @ kwh. Amesema hatahitaji majadiliano mapya. Inatosha kama ataandikiwa barua tu ya nyongeza MW 40.”

Kwa mtiririko mzima wa kusakwa kwa Richmond, hakuna hata hatua moja ambayo Lowassa anaweza kudai hakuhusika katika mchakato mzima, na kama vile Dk. Msabaha alikuwa anajua kitakachotokea wakati wote alionyesha kwamba alikuwa akifanyia kazi maelekezo ya bosi wake, yaani Lowassa.

Kuna habari kwamba wakati Serikali itakapowasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimo ya Bunge juu ya Richmond, hoja ya kutaka kusafishwa kwa Lowassa itaibuka ikilenga kuionyesha kwamba alionewa na Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza mchakato wa mkataba wa Richmond na Tanesco.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom