Barua ya Mama!!!!!

Ngongoseke

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
3,203
1,462
Hebu soma hii barua iliyoandikwa kwa wino wa machozi kutoka kwa mmoja wa akina mama.
Barua yenyewe hii hapa aliyoiandika Mama mmoja kwa wino wa machozi yake. Barua ameituma "Mama Makluumah" kwa kijana wake ambaye ni kama manukato ya moyo wake, maskini yule mama anasema:
"Ewe kijana wangu,
tangu miaka ishirini na tano (iliyopita) ilikuwa ni siku yenye mwanga katika maisha yangu pale aliponifahamisha Daktari wa kike kwamba mimi ni mja mzito. Na akina mama ewe mwanangu, wanajua vizuri maana ya hili neno (uja uzito) nalo linaleta maana ya kuchanganyika na furaha na ni mwanzo wa matatizo na mabadiliko ya kinafsi na ya kimwili kwa mama na baada ya ishara hii ya kuwa mja mzito ewe mwanangu-nikakubeba miezi tisa tumboni mwangu kwa furaha, (nilitaka kusimama) nasimama kwa taabu na ninalala kwa shida, na ninakula udongo, na ninapumua kwa uchungu,

lakini yote hayo hayakunipunguzia mapenzi yangu kwako na furaha yangu kwako, bali yakamea mapenzi ya kukupenda kadri siku zinavyosonga mbele.
Na ikakuwa shauku kwako. Nimekubeba ewe mwanangu juu ya uchungu, isipokuwa mimi pamoja na yote hayo nilikuwa nikifurahi na kufurahi kila ninapohisi kutingishika kwako ndani ya tumbo langu, na ninafurahi kwa kuongezeka uzito wako pamoja na kwamba ni mzigo mzito sana kwangu, hakika yalikuwa ni mateso ya muda mrefu, mara ikafika baada ya hayo yote Alfajiri ya usiku ule ambao sikulala ndani yake, na wala sikufumba jicho, na ukanikuta uchungu na shida na hofu na woga ambao kalamu haiwezi kuandika (kusifia) wala ulimi kuelezea, na nikaona kwa mboni ya jicho langu- namuapa Mwenyezi Mungu ewe mwanangu nikayaona mauti yakinijia mara nyingi, mpaka ukawa umetokea duniani! Yakachanganyika machozi ya kilio chako na machozi ya furaha yangu. Na yakaondoka machungu yangu yote na majeraha yake.
Ewe mwanangu, ikipita miaka katika umri wangu nikiwa nakubeba, moyoni mwangu na ninakuosha kwa mkono wangu, nikajaalia mapaja yangu kuwa kitanda chako. Na kifua changu kuwa ni chakula chako, nimekesha usiku wangu ili ulale, nimetaabika mchana wangu ili uwe muungwana, utukuke, matamanio yangu ni kuona tabasamu lako, na furaha yangu kila wakati ni kukuona unanitaka nikufanyie kitu chochote. Huo ndio mwisho wa utukufu wangu. Siku zikapita na mausiku yakapita nami nikawa katika hali hiyo, nikawa mtumishi bila kupunguza utumishi wangu. Na nikawa mnyonyeshaji asiyesimamisha huduma yake. Na nikawa mfanyakazi asiyechoka, mpaka ikakomaa miguu yako na kulingana sasa ujana wako, na zikaanza kuonekana kwako alama za kiume, mara nikaanza kwenda mbio kulia na kushoto ili kukutafutia mke umtakae, ukafika muda wa ndoa yako, moyo wangu ukakatika na yakatirizika machozi yangu kwa furaha kwa ajili ya maisha yako mapya yenye utukufu, na nikawa mwenye huzuni kwa kutengana na wewe. Yakapita masaa mazito, mara wewe sio yule mwanangu niliyemjua.

Hakika umenikana na umejisahaulisha haki zangu, yanapita masiku sikuoni na wala sisikii sauti yako, umeshindwa kumuelewa mtu aliyesimama kidete kwa ajili yako, umemsahau Mama yako.
Ewe mwanangu sihitaji kwako ila kitu kidogo tu. Nifanye mimi ni katika marafiki zako na machoni kwako, na wengine wasogeze hatua moja mbele yako.
Nifanye Mimi ewe mwanangu, ni moja ya vituo vya maisha yako ya mwezi ili nikuone humo japo kwa dakika chache. Ewe mwanangu, mgongo wangu umepinda, na viungo vyangu vimedhoofika, na maradhi yamenikondesha, na yamenitembelea maradhi, sisimami ila kwa taabu, na sikai ila kwa mashaka, na haukuacha moyo wangu ukizingazinga kwa mapenzi yako, kama angekukirimu mtu yeyote siku moja ungemsifu kwa kitendo chake kizuri alichokufanyia. Na ewe mwanangu Akulinde Mola wangu, mama amekufanyia wema (ihsani) ambayo huioni, na wema ambao hutaki kuulipia; hakika amekutumikia na kulisimamia jambo lako miaka na miaka, basi yako wapi malipo yake?! Umefikia upeo huu na kuwa na moyo mgumu kiasi hiki, na masiku yakakuzuia kiasi hiki kuja kuniona?!
Ewe mwanangu, kila nikifahamu kwamba wewe ni Muungwana katika maisha yako, furaha yangu huzidi, lakini naona ajabu na hali yakuwa wewe ni bidhaa iliyotengenezwa na mkono wangu, na kujiuliza ni kosa gani nimelifanya mpaka nimekuwa adui yako huwezi kuniona na kuwa mzito kwangu?!
Siwezi kupelekea mashtaka yako kwa Allaah, wala huzuni zangu kwa sababu nikiyapeleka juu ya mawingu na kuyakokota mpaka katika mlango wa mbingu, utapatwa na shari ya kugombana na wazazi, na adhabu itakuteremkia, na utashuka nyumbani kuwa kipande cha ini langu na manukato ya maisha yangu na furaha ya dunia yangu.
Zinduka ewe mwanangu, mvi zimeanza kuenea kichwani mwako, na itapita miaka kisha utakuwa baba mzee, na malipo yanategemea matendo, utakuja andika barua nyingi kwa mtoto wako, kwa wino wa machozi kama nilivyokuandikia mimi barua hii. Na kwa Allaah watakusanyika wagomvi wote ewe mwanangu, mche Mwenyezi Mungu kwa Mama yako, mfutie machozi yake, na mpungizie huzuni yake, ukitaka baada ya hapo chana barua yake, na elewa ya kwamba yeyote mwenye kutenda wema, ni kwa ajili ya manufaa ya nafsi yake na mwenye kufanya ubaya ni kwa madhara yake mwenyewe.
 
Inshallah Salam zitakua zimemfika mlengwa na wengineo wanao sahau wazee wao baada ya ndoa, wake kwa waume, mwenyezi mungu atupe fahamu na Imani juu ya wazee wetu...
 
Mkuu hii nimeipenda wapo jamaa kibao hapa dar wanajianya wako juu eti mambo safi lakini ukimtemblea mama/baba yake hali mbaya nashindwa hata kuilezea hapa jamvini.
Ujumbe umefika na ngoja niwaforwaie kwenye e-mail zao
 
Mkuu hii nimeipenda wapo jamaa kibao hapa dar wanajianya wako juu eti mambo safi lakini ukimtemblea mama/baba yake hali mbaya nashindwa hata kuilezea hapa jamvini.
Ujumbe umefika na ngoja niwaforwaie kwenye e-mail zao

Kweli mkuu wapo kibao sana hapa lakini ukiwaza kuhusu mama basi unapata jibu hakuna mwenye mapenzi ya kweli duniani anaemzidi mama
 
Back
Top Bottom