Barua Kwa Rais Magufuli

regnaldshirima

Senior Member
Aug 18, 2014
124
78
Najua sio Rahisi kukuona raisi Magufuli,Lakini Najivunia kua mtanzania.
Barua inatoka kijiji cha mbali kisicho na hadhi lakini bado tunafurahia kua Watanzania.

Barua Tumeituma na baiskeli hatujui lini utaipata,tunakusikia Kwenye redio,tunatamani kukuona rais magufuli,tukueleze yanayotusonga sisi,Mifugo yetu imekosa malisho mbunga ya wanyama imetanuliwa,Mwaka jana mvua Haijanyesha chakula cha msaada hakitufikii..

Tunatamani tukuone Rais magufuli tukueleze yanayotusibu,Mdogo angu alizaliwa njiani sababu hospitali ipo mbali kijiji cha tatu ndipo kuna barabara,Tunaomba tuje Uko tuone Lami. Najivunia Kua Mtanzania.Elimu bure mahitaji yanatushinda shuleni hatuli nyumbani Chakula hakuna chakula tunashindia maembe,Najua sio Rahisi kukuona rais.

Rais Magufuli Ukiipata Barua hii Tafadhali uje Utuone tubonge yanayotusibu,Rais vijana hatuna kazi, tunapiga mihayo lakini tunajivunia kuwa Watanzania.

Rais Magufuli Ukiipata Barua hii utufikiria nasie,maisha Magumu njoo ka nasi siku mbili tutafute kisichopatika. Rais watoto wa mjomba,shangazi na bamkubwa walimaliza darasa la saba hawanacha kufanya zaidi ya kuzurura.

Tunaomba utuokoe vijana wako,ubunifu tunao elimu hatuna,mitaji inatutatiza,tuokoe tusiwe machokora waliopendeza,tuokoe tuijenge nchi yetu.

Barua tumeituma na Baiskeli hatujui itafika Lini?
ikifika twaomba uijibu.

Kwako mh. John Pombe Magufuli.
Tunakupenda Rais wetu.
Sisi vijana Watanzania
Kijiji kisicho na hadhi.

Asante.
 
Ila atawajibu 2 maana nasikia ni mtumiaji mzur wa mitandao ya kijamii. Ila kumbuka kuwa maisha mnayoyaongelea ni maisha wanaoish watanzania zaidi ya 40% sasa sijui itakuaje kusolve tatizo la kijiji kimoja 2 pekeake wakati kunavijiji zaidi ya 10000. Na hiv uko kwani hamna mwenyekiti wa kijiji, diwani au mbunge wa kuwatatulia matatizo yenu si mliwachagua wenyewe mbona iyo baiskel imeilazimisha kwenda mwendo wa mbali wakati mngeanzia kwa ngazi ya uongozi wa kijiji chenu?
 

Ujumbe utafika sana! Kwa sababu inaonekana kuna baadhi ya hoja zilikuwa zinajibiwa pale ukumbuni, maswali yake yalizaliwa na morogogo ya kimajadiliano hapa JF
 
Back
Top Bottom