Barua kwa mpenzi enzi hizoooo

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Enzi zetu zile nakumbuka 1994 nilikuwa form II sasa leo nimekutana na hii barua niliyoaandika kwa mpenzi muone jinsi tulivyokuwa tunatongoza kwa shida sana maana hakukuwa na Simu wala mitandao.

Na enzi zile demu akikukubali anakukubali kwa mapenzi hasa sio leo hii unajua hata kutongoza sijui maana ukimtaka demu ni kama kusukuma mlevi wa gongo kwenye mteremko.

Pia enzi zile ukiaachana na demu anakurudishia kila kitu chako (picha, card, barua na zawadi zingine ulizommpa) na barua hii ni miongoni mwa nilizowahi kurudishiwa baada ya kumpiga chini demu wangu wa kwanza nikiwa form II...

attachment.php


Je wewe wakumbuka barua ya mapenzi uliyoandika au andikiwa kwa/na mahabuba wako enzi hizoooo??? Share with us here...........
 
maneno mengine ya kwenye barua mfano nikinywa maji nakuona kwenye glass hahaha enzi hizooooo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom