Barua kwa madaktari hovyoo T. A CHANDO ni kitu gani

mansakankanmusa

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
4,163
787
“Serikali inachotakiwa siyo kulazimisha, inapaswa kusikiliza na kutatua hoja, sisi madai yetu yamepotoshwa, hatuna vifaa vya kufanyia kazi lakini wananchi hilo hawalielewi,” alisema mmoja wa madaktari hao.


Serikali yawashtaki

Serikali imewaandikia barua za kuwashtaki madaktari wote waliofukuzwa kazi kutokana na mgomo huo kwa Baraza la Madaktari Tanzania.

Katika barua hizo ambazo inadaiwa kuwa zimeshakabidhiwa kwa madaktari waliofukuzwa kutokana na mgomo, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imelitaka Baraza hilo kuchunguza na kuchukua hatua dhidi yao.

Baraza la Madaktari Tanzania ndilo lenye dhamana ya kusajili madaktari na ndilo lenye uwezo wa kutoa adhabu kwa madaktari hao ikiwa ni pamoja na kuwafutia usajili.
Sehemu ya barua hizo inasomeka, ""Daktari mtajwa hapo juu alipelekwa katika Hospitali ya Taifa (MNH) kufanya mazoezi ya kuboresha taalamu kwa vitendo, tumepokea malalamiko kuwa kati ya Juni 23 na 29 mwaka huu alikataa kutoa huduma za kitaalamu ikiwa ni wajibu wake kama Daktari.

“Kitendo hicho siyo tu kilihatarisha usalama wa wagonjwa walioletwa katika hospitali hiyo kwa matibabu, bali pia ni kinyume na maadili ya taaluma ya udaktari,” inasomeka barua hiyo iliyosainiwa na T.A. Chando kwa niaba ya Katibu Mkuu wa wizara ya hiyo



source. mwananchi.co.tz
 
Watamhukumu vipi mtu ambaye hajasajiliwa na baraza daktari husajiliwa na baraza baada ya kumaliza internship ili upate leseni ya kupractice hivi hawa madaktari wamekuwa wajinga siku hizi hawajui utaratibu tishia nyau ha ha kwa kweli serikali imejipaka kinyesi
 
Back
Top Bottom