Barua kwa Lowassa

NCHI YETU, MATATIZO YETU, UPEO WETU, MAJIBU YA MATATIZO YETU ETI NI EDWARD LOWASSA. Nchi yenye umri wa miaka 50 ina watu wa ajabu sana hii, dah yaan kila kitu ni Lowassa, Lowassa, Lowassa, hebu tusaidieni kututajia uchafu wa LOWASSA na tutathmini na matatizo ya Nchi yetu ili tuone ana mchango gani yeye binafsi katika ukosefu wa ajira, mfumuko wa bei, afya,elimu ,miundombinu, nishati,ardhi, nk. Mtatusaidia kujua kuwa tatizo si CCM bali LOWASSA!
 
kwanza kabisa napenda kukwambia kuwa kuna mambo mengine hautikiwi kujihusisha ndugu yangu na mbunge wangu edward ngoyai lowassa,ivi arumeru kaka yangu ulifuata nini?AIBU ULIYOIPATA ARUMERU itakutokea tena muda si mrefu.
dhumuni la barua yangu hii mheshimiwa ni kutaka kukueleza kuwa jipange mwaka 2015 ninakuja kupambana na wewe hukoo monduli, ni kweli unajua kuhadaa na ahadi kedekede ndugu yangu, ni kweli unajua kutumia wamasai ambao walikuwa hawana elimu kukupigia kura ila mwisho ni 2015 nitatangaza nia ya kukupinga zama za kupita bila kupingwa au kupita kirais zimekwisha jiandae kaka nimekulia monduli nimesoma monduli na nitawakomboa wana monduli..... najua nitakuwa na challenge nyingi sana ila mungu ndie atakaenisaidia na wananchi wataamua siku zote naamini inawezekana

Kweli kutangaza nia sio mbaya ila unaonekana mwanasiasa muoga ambaochadema hatuwataki,mpakaleohujafungua hata tawi moja la chadema monduli halafu unataka ubunge kupitia chadema siasa sio rahisi kama unavyofikiria ,jimbo la monduli linahitaji mtu kamanda wa ukweli aliyejitolea kupambana na aina yoyote ya manyanyaso.
 
Comrade utatumia tiketi ya chama gani? ili marekebisho ya daftari la wapigakura nihamishie taarifa zangu monduli ili uipate kura yangu,ntafanya hili pale tu utakapo tumia tiketi ya CDM Nambie Comrade utaitumia tiket ya chama gani?

Kwa kupima maneno yake atakuwa anapimana nae kwenye kura za maoni ccm
 
Hakuna lisilowezekama kajaribu bahati yako ili uwe na nia ya kuwatumikia na siyo kujilimbikizia mali
 
unajua kuandika kila mtu anajua kuandika ila unapoandika bila kufikiria utakuwa una matatizo ni haki yako kuwa mwanachama wa chama chochote ila naingiwa na mashaka na uelewa wa mtu pale linapokuja suala la kuongea ukweli mtu analeta itikadi zake za ccm ivi haujui kwamba ni haki yangu kugombea uongozi wowote kama nimetimiza vigezo,tambua nyinyi wana ccm watoto wenu watakuja kupata shida kutokana na uhuni wenu mnaoufanya sasa hivi na mimi sipo tayari kwa hilo kama mwana monduli napigania haki na daima sitoacha
 
Tutakupa support ya kila aina kumtoa fisadi huyu. kitu cha maana uwe na nia safi na ya kweli kwa wana monduli na watanzania.
 
juzi kati aliita wahariri wote wanao muunga mkono nyumbani kwake wapange mbinu ingine kuna mmoja wapo alimwambia aachana na siasa za makanisani zitamuharibia sana na awezi kuwa raisi wa nchi hii hata siki moja
 
Ulichotakiwa kufanya ni kutangaza nia yako kwa wana monduli,na siyo kuandika barua kwa mhe.lowassa. Mhe lowassa hana haki miliki ya ubunge monduli, wenzio wengi wenye nia kama yako wameshaanza kutangaza nia zao mfano.sanare,mwotiko,sakita lazaro sokoine nk,cha muhimu nenda kwa wananchi ndugu yangu usitafute maneno kwenye jf.bahati mbaya 80%ya wana monduli hawana waLA hawafahamu jf ni nini. Kama unania hiyo nJOO uwanjani ndugu.

Mimi ni miongoni mwa wanamonduli sijasoma huko kama wewe nimezaliwa na ninaishi nakufanya kazi zangu hapahapa monduli.

Karibu sana
 
lowasa hana mpango wa kuwa mbunge tena anafungua kanisa lake na atakuwa baba askofu ndo maaana anazunguka kwenye makanisa
 
Back
Top Bottom